Thursday, June 4, 2020

KANISA NA UWAJIBIKAJI WAKE

Uwajibikaji Na Maana Yake.

Uwajibikaji ni tendo la watu au mtu kutekeleza kutimiza jambo ambalo hana hiari nahilo katika kulifanya.Wajibika ni tendo la kukosa hiari katikakufanya jambo.Wajibisha ni tendo la kufanya mtu awajibike yaana kutimiza wajibu wake.Na katika sura hii utajifunza jinsi kanisa ,kiongozi na uongozi unavyoweza kuimarisha na kustawisha kanisa katika kutimiza wajibu wao.Gal 3:18,5:3,Wafilipi 1:7.Wakolosai 1:10) Kwa hiyo kanisa la mahali likiwajibika ipasavyo kuimarika kwa kanisa hilo ni lazima.

A.Kanisa Na Uwajibikaji

Ni vema katika sura hii kufahamu kanisa na maana yake halisi,na pia kufahamu chanzo na mwanzilishi wa kanisa na mambo mengi ambayo hatuyajua yanayohusu kanisa.Pamoja na maana nyingi hizo maana halisi ya neno kanisa ambalo ni mwili wa Kristo na bibi arusi wake,ina maanisha kanisa ni Jumuia ya watu waliotwa kuujenga mwili wa Kroto.Md 4;32-35.

Mwanzilishi Wa Kanisa.

Kwa kufahamu mwanzilishi wa kanisa,Biblia ina  majibu sahii.Math 16:18, inasema kwamba Nami nakuambia Wewe ndiwe Petro,na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu;wala milango ya kuzimu haitalishinda,Andiko hili linamaanisha kwamba mwanzilishi wa kanisa ni Yesu Kristo.

Na katika hili Yesu aliwajibika katika mambo ya roho na katika mambo ya mwili au ya kijamii na kulirithisha kanisa kuwajibika,katika mambo ya roho na katika mambo ya kijamii pia.Fahamu kwamba tunajifunza mbinu za kuimarisha na kustawisha kanisa la mahali.Na kanisa lolote lile la mahali haliwezi kuimarika na kustawi bila kuwajibika kwa kutafuta mbinu na kuimarika na kustawi kwake.kuwajibika katika mambo yake kama kanisa, na kuwajibika katika mambo ya kijamii au uma.

Mungu anaupenda ulimwengu na hakomi kuhusika nao:Dhamira hii ya ndani inamaanisha makanisa kushiriki katika sehemu za umma.Mungu aliumba dunia kwa njia ya Neno na akalipa uhai kwa njia ya Roho.Kanisa linaitaji kuwa na mafanikio maendeleo ili kumiliki kutawala fedha pesa na mali yaani kanisa kuwa na uchumi wa hali ya juu sana.Kwamaana kanisa litakapo miliki na kutawala pesa na mali na watu wengi nilazima kanisa litaimarika na kustawi sana. Na kanisa ili limiliki pesa na mali nilazima kanisa yaani watu wa wajibike katika kujitoa au kutoa pesa zao mali zao nguvu zao,michango mbalimbali katika kanisa,kwa kufikia mafanikio ya kuimarisha na kustawisha kanisa la mahali.Kama tulivyoona katika  kanisa na maono thabiti.Kwa maana kanisa lisilokuwa na maono haliwezi kuwajibika kwa kuwa halina dira ramani na mwelekeo.Kanisa laweza kuwajibika kwa kutimiza mambo kama haya na yanayofanana na haya.Mfano kanisa laweza kuimarika kama mambo haya yakifikiwa.

A.Maendeleo Ya Kiroho

Kuhubiri injili ya Kristo Yesu popote ili kufungua makanisa kwa kupanua kazi ya Mungu.

Kufundisha waamini na kukulia neno.

Kukuza na kuendeleza huduma na karama zilizomo ndani ya watumishi na viongozi na waamini.

Kuwatuma watumishi na viongozi katika makanisa ili kufanya kazi ya Mungu.

Kubariki watoto.

Kubatiza.

Kumega mkate (Meza ya Bwana)

Kubariki watumishi na viongozi.

Kudumu katika upendo.

Kudumu katika umoja

Kudumu katika mshikamano

Kudumu katika maombi

Kudumu katika imani thabiti.

B.Maendeleo Ya Kijamii (Kimwili)

Kanisa ni vema kuwajibika katika maswala ya kijamii yaani katika mambo ya kimwili pia.Kwa maana biblia inasema kwamba mwili pasipo roho umekufa na roho pasipo mwili imekufa.Katika mambo yanayoleta afya ya kanisa ni kama haya. Kutengeneza miradi mikubwa ya kanisa.

 

Kujenga majengo (mahekalu)

Kujenga shule za chekechea,shule za msingi,shule za sekondari,na vyuo.

Kujenga zahanati

Kujenga vituo vya kulelea watoto yatima.

Kusaidia wasio jiweza’

Kusaidia wafungwa.

Kusaidia wajane

Kumiliki vyombo vya mziki.

Vyombo vya usafiri.Magari,Ndege,nk

Kuwawezesha watumishi na viongozi katika kanisa.

Internent Café

Stationeries

Computer training Centers

Yumba za kupangisha

Nyumba za kulala wageni

Vyobo vya habari kama Radio,Tv,Stations

Mifugo mbalimbali.

Mashamba

Zana za uvuvi.

Maduka nk.

Hiyo ndiyo dira yaana mwelekeo wa kuliimarisha na kulistawisha kanisa ya mahali.

 Kiongozi Na Uwajibikaji.

Ni neno la kuaminiwa mtu akitaka kazi ya askofu atamani kazi njema.1Tim 3:1.Je! Umejitafutia mambo makuu? Usiyapate;kwa maana tazama,nitaleta mabaya juu ya wote wenye mwili,asema Bwana;lakini roho yako nitakupa iwe nyara,katika mahali pote utakapokwenda. Yer 45:5.Wakristo wengi husita katika habari ya kutazamia au kutaka kazi ya kuwa kiongozi.Hawana uhakika kama ni vizuri kwa mtu kutafuta huduma ya kuwa kiongizi.Hufikiri ni afadhali kazi ya uongozi imtafute mtu kuliko mtu kuitafuta kazi.Je,siyo hatari kumpa mtu aliye na tabia ya kunai makuu? Je, hakuna ukweli fulani katika usemi usemao kwamba,kunai makuu ni udhaifu unaowaaribu watu wenye akili nyingi?. Ni kweli si vema mtu mkristo kunai makuu kwa faida yake mwenyewe.Lakini fahamu kwamba Biblia inaturuhusu kuzitaka karama zilizo kuu yaani karama zile tuzipendazo kila mmoja wetu.Hata hivyo hakuna karama ambayo ni nzuri au kuu kuliko nyingine,bali karama na huduma itakuwa kuu kwa Yule aitakayo zaidi.Yoh 4:10,Md 8:20,11:17,Rum 1:11,5:15,6:23,11:29,12:6,1Ko

1:7,12:1,4,9,28,31,14:1,12,2Kor 1:15,8:20,9:5.

Tunaposema kwamba kiongozi na kuwajibika kwake tunamaanisha kuzingatia na kutekeleza yanayomuhusu yeye kama yeye.Fahamu kwamba kuna uongozi na kiongozi wa uongozi.Kiongozi ndiye anayeitwa mtumishi kiongozi,ikimaanisha mtumishi kiongozi wa uongozi,katika shirika na katika kanisa pia.Uwajibikaji wamwanzoni kabisa wa kiongozi ni .

Kuona kabla ya anaowaongoza hawajaona.

Kusikia kabla anaowaongoza hawajasikia.

Kufika kabla ya anaowaongoza hawajafika.

Kufanya kutenda kabla ya anaowaongoza hawajatenda.

Kushiriki kabla ya anaowaongoza hawajashiriki.

Kushika na kukusa kabla ya anaowaongoza hawajashika na kukusa.

Kusema na kunena kwabla ya anaowaongoza hawajasema na kunena.

Kuyabeba maono kuliko ye yeto kati ya anaowaongoza.

Ongoza Kwa Tabia Na Sifa Za Kiongozi Wa Kiroho.

Anayetamani kuongoza na anayeongoza wengine kama Mkristo, lazima ajifunze kwa Kristo.Kristo hakuongoza kwa matakwa yake mwenyewe wala kwa vitisho bali kwa maadili.Hata hivyo Yesu Kristo alifundisha wanafunzi wake jinsi ya kuongoza kwa kufuata wema wa Mungu na maadili ya Neno la Mungu.Yesu alitumia Neno la Mungu kuwa mwongozo katika kufundisha jinsi ya kuishi kwa maadili milele. Jitieni nira yangu,mjifunze kwangu;kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo;nanyi mtapata raha nafsini mwenu.Mathayo 11:29.

Ni wajibu wetu kujifunze kwa Yesu Kristo kwa maana yeye ndiye kichwa cha kanisa na mwenye maono makubwa juu ya kanisa lake.Na pia  lazima tujifunze kwake yeye aliye mwalimu mkuu wa kanisa tena Ustadi wake kama kiongzi wa watu na kanisa ni kiongozi mtumishi.Kwa maana Kristo hakuja kutumikiwa bali kutumika.Mathayo 20:26-28 (28) Yesu Kristo aliongoza kwa kutumikia wengine.Upole wake na upendo wake na moyo wa kutumika uliwavutia wote aliowaongoza.Yesu hakupima ukuu wa mtu kwa watumishi aliokuwa nao,bali kwa wingi wa watu aliotumikia.Bilashaka Yesu alitimiza wajibu wake na kuutimiza unabii wa Isaya.Isaya 53:1-12.

Alitabiriwa atakuwa mfalme, lakini ni mfalme mtumishi.Lakini  katika wakati wetu watumishi hawataki kuwa watumishi bali  Wafalme wanao tumikiwa.Yesu alikuja kwa sababu ya utumishi utumwa.Wafilipi 2:6-7.Yesu Kristo alifanya jambo ambalo lilionyesha wazi kwamba yeye ni kiongozi mtumishi mwenye kujishusha,wakati alipowatawaza wanafunzi wake miguu yao.Yohana 13:4-5.aliwafundisha kwa mfano wake mwenyewe.Na funzo hili haliwezi kusahulika kamwe katika maisha ya mtumishi ambaye ni kiongozi mtumishi.Yesu alipiga magoti na kutawadha miguu ya wapendwa wake kwa unyenyekevu mkubwa.Ni vema kujifunza kanuni za kuishi katika utumishi utumwa kutokana na Yesu Kristo Bwaana wetu,alipotawadha miguu michafu ya wapendwa wake.

Mtumishi Kiongozi Na Maisha Ya Unyenyekevu.

Ni vema kuzama kwa kina katika maisha ya mtumishi kiongozi.Fahamu kwamba kiongozi  Ni Kiongozi wa viongozi na uongozi na watu.Kwanza tuliweke sawa na kulifafanua jina au neno Kiongozi na maana yake na matumizi kake.Hapa kila herufi ina maana yake tujaribu kuona maana ya kila herufi kwa maana neno kiongozi ni kifupi cha maneno ambayo yamebeba wajibu wa kiongozi.

KIONGOZI.( K ) Ina maanisha Kielelezo.Kielelezo ni mtu au kitu halisi mfano wake kitumiwacho kuonyeshea au kuelekeza kitu halisi; ni mchoro au picha na ni tendo la kuelekeza au kuonyesha  kitu au jambo fulani.Hapo maana hiyo inatuonyesha kwamba kiongoza hana budi kuwa kielelezo kwa wale anao waongoza inampasa kuwa kelelezo ili kutimiza wajibu wake na kuwa mwajibikaji.Kila anayetaka na kutamani kazi ya mtumishi kiongozi yampasa kujifunza kwa Yesu aliye mtumishi na kiongozi na mwalimu mkuu aliye kielelezo chetu.Yohana 13:4-5,15,1The 1:7,2The 3:7-10,1Timotheo 1:16,2Timotheo 1:13,Tito 2:7,1Petro 2:21,1Timotheo 4:12.

KIONGOZI.Katika kufafanua na kutafsiri kirefu cha neno na jina Kiongonzi herufi ( I _) Ina beba au kuwakilisha neno Imani ikimaanisha kwamba kiongozi lazima awe na imani thabiti isioyumba na kuyumbisha bali ni mtu kiongozi aliye na imani yenye viwango kuzidi wale anao waongoza.Kwanza kumbuka,Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo,ni bayana ya mambo yasiyoonekana.Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa.Kwa imani twafahamu yakuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu,hata vitu visivyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.Waebrania 11:1-3.Katika hili mtumishi kiongozi,anatakiwa kuwa na hakika na mambo yaliyomo katika maono anayoyabeba.Haijalishi kwamba hayaonekani kwa macho ya wale anaowaongoza.Yampasa kuwaaminisha na kuwafikisha katika kiwango cha imani aliyonayo,na kuakikisha  kwamba wame kuwa na  hakika na kile kinacho aminiwa na kiongoza.Hapo kiongozi atapata njia ya kuwajibika katika kuliimarisha na kulistawisha kanisa.Kumbuka mfano ambao Yesu Kristo aliowambia wanafunzi wake akisema.Akawaambia,mfano mwingine,akisema,Ufalme wambinguni umefanana na punje ya haradali,aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake;nayo ni ndogo kuliko mbengu zote;lakini ikiisha kumea,huwa kubwa kuliko mboga zote,ikiwa mti,hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake Mathayo 13:31-32.Kiongozi inampasa awe na imani ya kuhamisha milima yaani mambo yanayoshindikana kutekelezeka.Mathayo 17:20.

KIONGOZI:Katika neno au sifa hii kiongozi,twende tukatafari herufi hii kama imebeba hapo. ( O ) Katika neno hii kiongozi limebeba (o) mbili na kila moja ina maana yake,hebu tuone maana ya (o) ya mwanzoni.O.Ina maana ya Onyesha njia likitokana na kitenzi kuonyeshi.Kwa hiyo kila kiongozi ni mtu nayewajibu wa kuonyesha wale anaowaongoza njia ya kupita au ya kuenenda.Tujifunze kutoka kwa mwalimu mkuu ambaye ni Yesu Kristo ambaye ndiye kiongozi aliyeonyesha wanafunzi wake pamoja na ulimwengu wote.Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali,nitakuja tena niwakaribishe kwangu;ili nilipo mimi,nanyi mwepo.Nami niendako mwaijua njia.Tomaso akamwambia,Bwana,sisi hatujui uendako;nasi twaijuaje njia?Yesu akawaambia,Mimi ndimi njia,na kweli,na uzima mtu haji kwa baba,ila kwa njia ya mimi.Yohana 14:3-6.Kwa sababu Yesu alifahamu kwamba niwajibu wake kuwaonyesha njia wanafunzi wake na ulimwengu kwa ujumla alifanya hivyo kama kiongozi.Inatufaa zaidi kujifunza kwake na kutimiza wajibu wetu kama viongozi watumishi wa Mungu.Yesu aliweka wazi mambo matatu Kwamba yeye ndie Njia yeye ndie Kweli yeye ndie Uzima. Akiwa na maana yakwamba kila apendaye njia iliyo sahihi ya kwenda kwa Baba yampasa kumfuata yeye aliye njia.Na yeye apendaye kufahamu kweli katika jambo lolote amwamini yeye aliye kweli.Na Yule apendaye kuona na kuishi katika uzima,hana budi kumwamini na kuishi kama alivyo Kristo kwetu yeye ndiye uzima,mtu asie kufa milele.Viongozi watumishi wa Mungu hawana budi kuonyesha wale wanaongozwa njia iwapasayo.

KIONGOZI.  Katika hili herufi inayofuata ni ( N ) Herufi hii katika zile zinazokamilisha neno kiongozi linamaana ya kuwa kiongozi ni mtu ambaye aliyejaa Neno la Mungu lenye kutamanika na watu na Mungu pia.Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi,maarifa,tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake;kwa kuwa yeye ni mjumbe wa BWANA wa majeshi.Hayo ni maneno ya Mungu kutoka kwa mtumishi wake Malaki.Malaki 2:7.Jifunze kutoka kwa mwalimu na wenye kujaa maneno yenye kujenga kufariji na kutia moyo.Basi kila asikiaye hayo maneno yangu,na kuyafanya,atafananishwa na mtu mwenye akili,aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;mvua ikanyesha,mafuriko yakaja,pepo zikavuma,zikaipiga nyumba ile,isianguke;kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye,atafananishwa na mtu mpumbavu,aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;mvua ikanyesha,mafuriko ya kaja,pepo zikavuma ,zikaipiga nyumba ile,ikaanguka;nalo anguko lake likawa kubwa.Mathayo 7:24-27.

KIONGOZI: Tunaendelea na ufafanuzi wetu wa neno kiongozi kwa kila herufi jinsi inavyowakilisha na kubeba utumishi wa mtumishi kiongozi katika kuongoza kwake.Na herufi ( G ) ina maana ya  Geuza  Neno geuza ni neno litokanalo na kitenzi kugeuza kikimaanisha kubadili kitu kiwe katika hali au sura na mwonekano na Umbo jingine.Ni Kufanya umpande uliokuwa chini uwe juu au uliokuwa mbele uelekee nyuma.Hapa ina beba dhamana ya mtumishi kiongozi kubadili mambo kwa kuyaboresha zaidi.Yesu anasemaje kwa hili na anahusikaje katika hili? Mungu alimtuma mwanaye kwa makusudi ya kugeuza mambo kwa kuyaboresha na kuyaandaa ili yawe kama Mungu alivyokusudia yawe.Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu,bali ulimwengu uokolewe katika yeye.Yohana 3:17.

Ukitafakari sana torati kama ilivyoandikwa na Musa Kumb 31:9,Musa akaiandika torati hii,akawapa makuhani,wana wa lawi,waliolichukua sanduku la agano la Bwana,na wazee wote wa Israeli.Utangundua kwamba imejaa hukumu.Kutoka 21:1-36.22:1-31,23:1-9

Bilashaka utaamini kwamba pia torati ilikuwa imeruhusu kulaaniwa kwa mtu.Kumb 27:15-26.

Ni vema kujifunza kwa mwalimu mkuu Yesu Kristo hijapokuwa  kuna watumishi wengi katika Biblia wafahao sisi kujifunza kwao.Kwa nini Yesu ni muhimu sana? Kwa kuwa Yesu ndiye mwisho wa sheria na wanashia.Rumi 10:4,Gal 3:24.Yesu Kristo kiongozi wa kufuatwa na kujifunza kwake ni mfano wa kuwa kiongozi mwema aliye Geuza mambo na kuyaboresha kabisa.Yesu aligeuza mambo mengi na kuyaboresha,lakini tutaona machache ya kutuimiza zaidi.

Kuhusu hukumu,kama tulivyoona hapojuu katika Yohana 3:17.Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili aukumu ulimwengu,bali ulimwengu,uokolewe katika yeye.Yesu alisemaje kuhusu hukumu? Mathayo 7:1-5. Yesu aligeuza  ikimaanisha alileta badiliko hukumu ikabadilika ikageuka kuwa upendo na msamaha kwa aliyekosa na kustahiki hukumu.Mathayo 6:14.

 

Kuhusu kulaani Yesu alileta badiliko la kubariki kuliko kulaani,Yesu ni kiongozi wa mfano wa pekee.Luka 6:24-36.

Ni kweli kiongozi ambaye ametokana na Mungu nilazima awe mtu wa kugeuza na kuleta mabadiliko chanya katika uongozi wake.Viongozi ambao hawawezi kugeuza mambo, Biblia inasema na kuwaita Mbwa bubu.Walinzi wakeni vipofu,wote pia hawana maarifa;wote ni mbwa walio bubu,hawawezi kulia huota ndoto,hulala hupenda usingizi.Naam,mbwa hao wana choyo sana,hawashibi kamwe;na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno;wote pia wamageuka upande,wazifuate njia zao wenyewe,kila mmoja kwa faida yake,toka pande zote.Husema, Njoni,nitaleta divai,Na tunywe sana leo,Sikukuu kupita kiasi.Isaya 56:10-12.Kiongozi hugeuza mambo kwa kuandaa viongozi wapya,na kugawa madaraka inapobidi kufanyahivyo. Luka 3:5.Kila bondo litajazwa,Na kila mlima na kilima kitashushwa;Palipopotoka patakuwa pamenyoka,Na palipoparuzwa patalainishwa.Nilazima kiongozi atendee haki herufi .O.

KIONGOZI. Herufi  ( O ) ina wakilisha au inabeba wajibu kiongozi kuongoza kwa kutangulia mbele wale anao waongoza .O,Ikimaanisha kwamba kiongozi ni lazima kuwa mbele ya kundi au kikundi cha watu anaowaongoza kwa ili kuwaelekeza pakwenda.Na neno ongoza na tendo kuongoza linamaanisha kuwa mkuu na msimamizi wakila shughuli.Tujifunze kwa mwalimu mkuu Yesu Kristo anasemaje katika hii.

Yohana 10:2-5,Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.Bawabu humfungulia huyo,na kondoo humsikia sauti yake;naye huwaita kwa kondoo wake kwa majina yao,na kuwapeleka nje.Naye awatoapo nje kondoo wake wote,huwatangulia;na walekondoo humfuhata,kwa maana waijua sauti yake.wengine hawatamfuata kabisa,bali watamkimbia;kwa maana hawajui sauti za wageni.Naamini umepata jambo la msingi na la muhimu sana katika herufi O.viongozi hawana budi kutangulia katika kila jambo. Rumi 2:17-24.

KIONGOZI.Katika herufi ( Z ) inawakilisha wajibu wakiongonzi katika kuzingatia mambo.zingatia lina maana ya kutia moyoni yote ambayo ni maagizo ya Mungu kwako na maazimio ya baraza kuu na kanisa.Wewe kiongozi unapozingatia kwa kutuyumbisha.Kumbuka wakati kiongozi anaposimamia kundi la kiroho,ni mtu mwenye kusimama mbele za Mungu kwa ajili ya watu na anasimama mbele za watu kwa ajili ya Mungu.Luka 15:17.Jifunze kwa watumishi wa Mungu kama vile Musa,na  Nehemia,Manabii,Mitum

E,walivyo zingatia yawapasayo.

KIONGOZI. Herufi ( I ) Ina wakilisha na kubeba wajibu wa kiongozi wa kuimarisha na kustawisha kundi.Ni wajibu wa kiongozi kuimarisha ikiwa na maana ya kutafutakundi liwe na nguvu ya kiuchumi,nguvu ya umoja,nguvu ya kielimu,nguvu ya neno la Mungu liwe kwa wingi ndani ya anao waongoza.Kiongozi ana wajibu wa kufanya kundi liwe madhubuti.1Fal 2:12,Zab 30:7,40:2.AYubu 4:4.Ezekieli 20:32.

Hicho ndicho kirefu cha neno kiongozi.Na ili kanisa liimarike na kustawi nilazima kanisa liwajibike na kiongozi awajibike na uwongozi uwajibike,hapo ndipo kanisa la mahali litaimarika na kustawi sana.

 Rhobinson S.Baiye.

rhobinsons.blogspot.com

rhobinsonsaleh1@gmail.com

Whatsapp.0764127531

Mwanza Tanzania.

 

 

 

 

 

 

 

 


No comments:

Post a Comment

UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...