KANISA NA MAONO
THABITI
Yoeli 2:28 Ufunuo 1:9-20
Twasoma
katika unabii wa Yoeli kwamba Hata itakuwa,baada ya hayo kwamba nitamimina
roho yangu juu ya wote wenye mwili;na wana wenu,wakike na wakiume,watatabiri,wazee
wataota ndoto,na vijana wenu wataona maono.Na katika ufunuo wa Yesu kwa
Yohana,Yohana anasema alikuwa katika roho na aliona maono.Je?maono au ono
inamaana gani?
Maana
ya maono
Maono
au Ono ni picha ya mambo au vitu inayomjia mtu ubongoni mwake;ni taswira ambayo
ya weza kuonekana au kujitokeza kwa njia ya dhamira safi au katika hali ya kuwa
katika roho kama Yohana alivyoyaona maono akiwa katika roho.Kwa maana nyingine yasema kwamba maono ni hali ya
kuona mbele,ukilinganisha naya nyuma.mtu moja alisema kwamba maono ni daraja
inayounganisha yaliyopo na yajayo.Kuna tofauti wa maona na ndoto,Ndoto ni
matukio ya kale,Ni kumbukumbu ya mambo
ya kale.Lakini maono yanahusika na mambo yajayo.Ndoto inahusu mambo yalivyokuwa,hali maono yanahusika na
mambo yanavyoweza kuwa.Uzee na ujana ni maneno mawili yanayohusiana.Fahamu
kwamba kuna vijana ambao huona tu vizuizi,na mawazo yao yako katika shida
wanayoiona .Na ni wanaume wenye ndoto wanafikiri kizee,wakizingatia
yaliyopita.Mwenye maono hufikiri mambo yanavyoweza kuwa Kiongozi na
kanisa lenye maono huona nyota,na kuamini kwamba ni yenye kuwa na Mungu,na ina
nguvu za kusababisha mabadiliko.
Maono
yatokayo kwa Mungu huleta mabadiliko,na maono hayo huona mafanikio katika siku
za baadaye.
Nguvu Iliyomo Katika Maono Yatokayo Kwa Mungu.
Kanisa la mahali halipaswi kupuuza nguvu zilizomo katika maono.Washirika wanaume na wanawake na vijana wenye maono hubadilisha ,mwonekano wa kanisa.Ni vema kanisa na watumishi pamoja na viongozi katika kanisa kujiuliza maono tuliopewa na Mungu na kuyapokea ni yapi? Je tumeyaishi ya maono? Na kama kanisa la mahali halijui ono lao basi kanisa hilo na watumishi wake bado wanaishi bila kutambua wito wao.Basi kanisa hilo linaishi wasivyostahili kuishi.Katika maono mnanguvu za ajabu.Kile ambacho mtu alichokiona katika ono ndicho humpa moyo na mvuto wa kufanya au kuwajibika katika kutimiza majukumu yake ya kila siku,ili kufikia kile alicho kiona.Na kama kanisa la mahali halina maono inamaanisha kwamba kanisa hilo halina dira/ mwelekeo.Tunaweza kusema kwamba hutia nguvu katika ono lako,ikiwa utadumu katika ono hilo.Mungu hawezi kuweka ngvu katika ono lako kama haudumu katika ono lenyewe.Huduma na karama na wito wako ni kazi yake.Vivyo hivyo nguvu za kutekeleza ono zinatokana naye.
Kusudi La Ono/ Maono Katika Kanisa La Mahali. watumishi na viongozi katika kanisa la mahali,huendeleza shughuli zao za kila siku wakiwa na azimio la matarajio ya kufanikiwa.maono ya kanisa humpa kiongozi mwelekeo na majukumu katika siku zake,Kusudi la kuwa na maono ni kuweka mwelekeo dira ya Mungu katika mzunguko wa maisha ya kanisa,ili kuimarisha na kulistawisha kanisa la mahali.Fahamu kanisa ilinahitaji maono ono thabiti,na yatokayo kwa Mungu.
·
Maono
yatokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa mtu.
·
Maono
yatokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa jamii.
·
Maono
yatokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa nchi.
·
Maono
yatokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa ulimwengu.
·
Maono
yatokayo kwa Mungu hutiisha kanisa.
Kumbuka
kwamba watu wengi na makanisa mengi hayana mawazo ya hatima yao.Wengi wanaona
tu wakati uliopo na vikwazo vyake.Fahamu kwamba katika shirika lolote,lazima
pawepo na viongozi na wasimamizi.Na hufananishwa na kundi la wavumbuzi
waliokuwa wakijaribu kutengeneza njia vichakani.Msimamizi alikusanya kundi lake
akawapa visu,misumeno,na shoka kama vitendea kazi ya kutengeneza njia kwenye
msitu mzito sana,Msimamizi alipoona mambo hayawezekani aliwambia kwamba basi
yatosha na akapaza sauti na kuwa kataza kwamba wasiendelee na kazi hiyo eti
kwamba wamepotea njia na kuelekea upande usiofaa.Huyo ndiye kiongozi ambaye
anajali na kufahamu hatima ya sika za baadaye.Mungu ametupa wanaume kwa
wanawake kuongoza kututoa katika msitu.Mfano wa Musa na Nehemia, Esta na Paulo
walikuwa viongozi wenye maono.Walitoa
mwelekeo na kuakikisha kwamba wanafuata maono waliopewa na Mungu.Ni vema
kuishi katika maono au ono ulilopewa na Mungu.
Kanisa Na Umiliki Wa Ono
Au Maono Yake.
Ni
vema kila kanisa la mahali liweze kumiliki ono lake.Kufuatana na mazingira
uzoefu,maono ya kanisa ya yaweza kuwatofauti kulinga na mambo
matatu muhimo.Mazingira ya kanisa,Uzohefu na Kiwango cha fikira na ujuzi wa
mtumishi kiongozi.Lakini kumbuka haijalishi uko katika mazingira gani,wajibu wako
ni kutimiza kile ambacho Mungu amekuitia kukifata.Kazi ya Mungu ndani ya kanisa
na ndani ya watumishi na viongozi ni ono maono ambayo Mungu anayo juu ya kanisa
na watumishi wake.Soma Malaki 2:Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi
maarifa,tena yapasa watu kuitafuta sheria ya Bwana kinywani mwake,kwa kuwa yeye
ni mjumbe wa Bwana wa majeshi.
Ni
lazima kanisa lione na kuamini na
kumiliki ono lake.Kanisa likumbatie ono
lake kama kipawa na dira muhimu kutoka kwa Mungu.Mungu yuko tayari
kushiriki na wewe katika ono la kanisa la mahali.Kanisa limiliki maono katika
pande mbili muhimu.Maono katika hali ya kiroho (ibada) na maono katika hali ya
kijamii ( kimwili ) Mambo haya utayaona kwa kina katika sura ya (10).
1.Kanisa La Mahali Kutimiza Ono Lake
Kanisa
la mahali kwa kutimiza maono yake halina budi kuimiza viongozi na watumishi
pamoja na waumini kulipenda kanisa na kulithani kanisa,katika kudumu katika
upendo.1Kor 13:1-8,Upendo husababisha na kutoa msukumo wa kujitoa na
kutoa malizake na nguvu zake kwa moyo bila kusukumwa.Kwa kutimiza maono
kanisa lazima lidumu katika umoja kwamaana umoja unanguvu na unapendeza sana Zaburi
133:1-4.Kanisa la mahali likiwa pamoja kwa umoja haliwezi kushindwa
kutimiza maono yake.Soma katika sura ya pili ili ufahamu kwa kina kuhusu
umoja.Hatuwezi kusahau mshikano katika kanisa ni jambo muhimu na lenyenguvu
sana katika kutimiza maono ya kanisa la mahali mshikamano hudhihirishwa na lugha na matendo na
mwenendo.kwa kutimiza maono lazima kanisa lidumu katika maombi,na katika imani
thabiti na kumiliki uchumi ambao
hulipa kanisa uwezo wa kifedha.Imani thabiti inahitajika katika kutimiza maono
pamoja na mfumo unaofaa hufanya mambo kuwa mepesi na rahisi kufanyika.Kutambua
na kuwa na mtazamo mzuri katika nyakati.Kwa kutimizwa kwa maono ni lazima maono
yenyewe yaeleweke kwa maana kuna maono mengine hayaeleweki.Na kutoeleweka kwa
maono huleta uzito wa kutotekelezeka kwa maono ambayo hayana mpangilio na
hayaonyeshi mwelekeo.Kanisa lenyewe halina budi kuwajibika katika kutimiza
maono yake.Watumishi na viongozi hawana budi kuwajibika kila mmoja katika
nafasi yake ili kutimiza yale ambayo Mungu anahitaji kutimizia kanisa kupitia
kwa kiongozi na mtumishi huyo.
2.Ono Maono Lazima
Yaatamiwe.
Ni
vyema kufahamu kwamba nilazima maono yaatamiwe.Mtu anapopokea maono kutoka kwa
Bwana,huwa kuna msukumo wa kuanza kufanya kitu kwa haraka.Lakini maono lazima yaatamiwe kama kuku anavyoatamia
mayai yake siku (21).Tujifunze kwa Mungu aliyetuumba alikuwa na maono na mpango
mzuri juu ya mtu na ulimwengu. Yohana 3:16-17.Lakini lakuzingatia ni
kwamba Mungu aliatamia maono yake kuhusu ulimwengu na waulimwengu.Hapo mwanzo
Mungu aliziumba mbingu na nchi.Nayo nchi ilikuwa ukiwa tena utupu,na giza
ilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji;Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa
maji.Mungu ni Roho na roho ya Mungu ilitulia juu ya maono yake.Lakini makanisa
mengi ya mahali pamoja na watumishi wake hawana utulivu katika maono,na ndio
maana makanisa hayo hayaimariki na hayastawi.Ona jinsi maono ya Mungu yalivyokuwa
makubwa na yenye uzito mkubwa sana.Tafakari jinsi ufalme wa mbinguni
ulivyo,pamoja na ufalme wa anga ulivyo na ufalme wa dunia (ulimwengu)
ulivyo.Hayo yote ndiyo maono ya Mungu.Ilibidi Mungu kuatamia maono yake ili
yakomae na kuwiva.Nilazima watumishi na viongozi pamoja na washirika kuacha
papara,wawe watulivu katika maono.Hata kama maono hayajadhihirika bado yaatamie
moyoni mwako,na usiwe mwongeaji na mwenye kusema au kuyatangaza kabla ya wakati
wake.Husi yakinahi maono yako yasiwe mzingo mzito kwako na uyapende maono
yako.Yajue,yafahamu maono uliyonayo.
3.Maono Lazima Yashirikishwe
Ni
vema watu washirikishwe maono ya kanisa ili yawe wazi na yafahamike na
yaandikwe.Yatakapoandikwa na Watu kushirikishwa,kutakuwa na watu ambao
wapotayari kujiunga na kuhudumu pamoja nanyi.kwa sababu ya kuwashirikisha
watu.Kutakuwa na kundi kubwa ambalo litazaa makundi ambayo yatafanya kazi kubwa
na kwa wepesi kuliko ambavyo ungefanya peke yako au peke yenu.Ukiwa mtu wa
kufanya kila kitu peke yako hautaweza kufanya kitu cha maana katika dunia
hii.Bali mtu anayeweza kuwaandaa wengine kutekeleza maono ya pamoja na mtu
awezaye kuunda kikundi/vikundi anaweza kufanya kazi yenye maana kwa ufalme wa
Bwana wetu Yesu Kristo.Biblia inasema kwamba,Na watu watano wa kwenu
watawafukuza watu mia,na watu mia wa kwenu watawafukuza watu elfu kumi;na adui
zenu wataangamia mbele yenu kwa upanga.Mambo ya walawi 26:8.Hayo ni kwa
sababu ya kushirikisha wengine maono tulionayo.Mmoja angefukuzaje watu
elfu,Wawili wangefukuzaje elfu kumi,kama mwamba wao asingaliwauza,kama Bwana
asingaliwatoa? Shirikisha vijana,wanaume,wanawake,maskini,matajiri,
Wenye elimu mbalimbali,wasionaelimu,wazee,watu warika zote.Rasilimali zitatokana na watu hao
kama watashirikishwa kikamilifu.Chukua
mda wa kuwaandaa na kuwaelimisha
ulichokiona unachokiona na kitakacho tokea.Wape nafasi na kuhudumu kwa
uhuru.
2Kor
9:13,1Yohana 4:13.
Fahamu
kwamba maono hujaribiwa kwa matatizo mengi,misiba ,uasi,yatakuweka katika
migigiro na wengine kusema kwamba sio Mungu aliyekupa maono hayo bali ni
miemuko yako tu.Kila aina ya hatua itachuliwa kinyume nawe unapoingia katika
kutekeleza maono uliyopewa na Mungu.Mkeo/mmeo watoto wako wanaweza kuinuka
kinyume na maono yako.Jaribu la kukosa watu muhimu katika maono uchumi kutokuwa
sawa,jaribu la mapinduzi katika nafasi yako kama mbeba maono.La kukumbuka ni
kwamba maono hujaribiwa kulingana na ukubwa na uzito wa maono ulivyo.Maono
makubwa kujaribiwa kwa majaribu makubwa zaidi.Twaweza kuyaona na kujifunza
kupitia maono ya Nuhu katika kutengeneza
Safina ono lilikuwa Mwisho Wa
kila mwenye mwili kuangamizwa kwa Garika.
Mwanzo 6:13.Abrahamu Kumbuka Abrahamu alikuwa na maono makubwa sana,
mataifa yote kubarikiwa kutokana na uzao wake.Je wakumbuka majaribu
aliyokumbana nayo? Mwanzo 12:1-.Tafakari kuhusu Musa Kutoka 3:1-Tafakari
kuhusu Nehemia ,1:1- Tafakari kuhusu Paulo Md 9:1- Kujaribiwa kwa maono yetu
katika kila hatua kusitukatishe tamaa wala kuogopa ya kwamba hatuwazi kuyafikia
yale tuliyoyaona.
5.Maono Lazima Ya Dumishwe.
Kudumisha
ni kuendeleza jambo.Inamaana kwamba Mungu anapokupa maono nilizima kuyadumisha
maono ambayo umepewa na Mungu,Maono ni kitu muhumu sana
Na
ni lazima kushikilia au kudumisha.Tazama
ono aliliopewa Yona kwaenda kuhudumia nchi ya Ninawi,lakini yeye
alikwenda katika njia zake zingine.Matokeo yake adhabu ya Mungu ilimfikia
Yona.Mungu akiamua kukupa maono huwa hajutii kwa nini nimempa mtu huyu maono
haya kwa maana Mungu wetu ni Mungu ajuae,na anatujua sana,ndiyo maana hawezi
kujutia.Hesabu 23:19.Tunapodumisha maono tunamfuraisha Mungu.Tuwe na
mikakati ya kuwaandaa wengine ili maono yetu yapatekudumu.Na haijalishi tunapita
kwenye shida na katika mafanikio lazima tudumishe maono.Ezekieli 29:18,Ayubu
24:22,Zaburi 89:29,85:5.( Luka 1:50)
6.Maono Lazima Yaanzishwe Na Mungu.
Maono
sahihi ni maono ambayo huanzishwa na
Mungu mwenyewe.Katika wakati wetu huu,baadhi ya wajiitao watumishi wenye maono
kutoka kwa Miungu lakini sio.Maono kamili kutoka kwa Mungu yanaweza kutoka au
kukujia kwa njia tofauti na yalivyo watokea wengine.Ona Nuhu Mungu
alimwambia,Abrahamu Mungu alisema naye moja kwa moja,ona Musa aliona na
kusema na Mungu moja kwa moja.Ona Yusufu yalimtokea katika ndoto.Je! maono
uliyonayo yametokana na nani? Isaya
6:8-13,61:1-11, 41:10-18,
7.Maono Lazima Yawe Na Mipaka.
Kama
tulivyoona maono ni kitu kizuri sana katika maisha yetu.Mungu anapokupa maono
nitabia yake kukuwekea mipaka ya hayo maono.Twaweza kwenda kinyume na maono
yenyewe hii ndiyo maana halisi ya mwanadamu.Jifunze kwa Yoshua mtumishi wa
Musa,alivyoambiwa na Mungu baada ya Musa mtumishi wa Mungu kufa.Mungu
alimwambia Yushua kwamba,Yoshua 1:1-9 (7-8)2 Wafalme 9:1-13.
8.Maono Ufunguo Wa Mafanikio.
Ni
kweli maono ni ufunguo wa kufaulu.Kufaulu ni kupata,yaliyokusudiwa; ni
kufanikiwa ni kushinda mtihani na nikufikia malengo.Na maono ni ufunguo wa
kupata yanayokusudiwa na maono ni ufunguo wa kushinda mtihani na mitihani katika
maisha.Maono ni ufunguo wa kufikia malengo.Biblia yasemaje kuhusu maono? Biblia
inasema kwamba,Pasipo maono watu huacha kujizuia;Bali ana heri mtu Yule
aishikaye sheria.Mith 29:18.Twaweza kujifunza kupitia Taifa la Israeli
na manabii wa Mungu kwa ajili ya Taifa hilo.Na kupitia maono na kutoa unabii
hizo zililifaa Taifa la Israeli.Maono ni dira na mwelekeo wa kanisa familia
taifa.Mfano ugonjwa wa
CORONA,ulitangazwa kutoka katika taifa la watu wa China mnano Mwezi wa 12 ( )
Mwaka 2019. Ugonjwa huo ulisambaa Duniani kote,yaani katika kila Taifa
duniani.Manabii katika mataifa mbalimbali walitoa unabii kupitia maono ambayo
waliyaona kuhusu ugonjwa huo.Watawala yaani maraisi wa mataifa mbalimbali
walitoa mwelekeo dira kwa ajili ya kushinda ugonjwa wa CORONA, COVID
19,Natamani ufahamu maono ya mtawala yaani Raisi wa Jamuhuri Ya Muungano Wa
Tanzania aliyeingia madarakani mnamo mwaka wa 2015.
Wakati,wa
kisa cha kwanza cha Corona kutangazwa mnamo tarehe 16 mwenzi wa 3 mwaka 2020,
Raisi JOHN JOSEPH POMBE MAGUFURI,aliutubia taifa kwamba wamlilie Mungu yaani
Taifa la Tanzania kufunga na kuomba kwa muda wa siku tatu.Ijuma,Juma mosi na
Juma Pili.Na matokeo chanya alipotokea Raisi huyo alitangaza tena na kuwaomba
Watanzania kuomba maombi ya Shukrani kwa muda wa siku tatu.Ijuma ya tarehe
22-23-24/5/2020.Juma mosi na Juma Pili. Mataifa yalifaulu kupita maono.Fahamu
maono ni mafunuo muhimu.
Kufa Kwa Maono
Tunayo maono lakini fahamu kwamba maono uliyonayo yaweza kufa.Haijalishi
usipokuwa makini maono yako yatakufa.Miaka kadha iliyopita mtumishi wa Mungu
aitwaye BILL GOTHARD.alisema juu ya kufa kwa ono maono.Alieleza jinsi wanaume
na wanawake walioteuliwa na Mungu walivyopitia vipindi vigumu vya
giza,walipoona ugumu katika kutimiza ono la Mungu,kama vile Eliya alivyojificha
ili asionekane na malkia Yule mkatili,Yezebeli.Eliya alikuwa na woga mwingi
ingawa Mungu alimwonyesha uwezo wake akiwa katika mlima uitwao Karmeli.Eliya
alikuwa amepoteza imani Mungu hasingefanya yale aliyosema naye.Fahamu kwamba
kila kiongozi wakati mwingine hufikia hali ya kukata tamaa.Na katika kipindi
hicho mtu mwenye maono hupoteza mwelekeo na maono na asipokuwa makini maono ni
marehemu.Jua kwamba jambo hii ni muhimu sana katika maono.Ulicho nacho ni
hakikisho la ono hilo.Unaweza kujiuliza tu,je?limetoka kwa Mungu? Au nimekosea
njia?Anachotakiwa mtu wa maono anapaswa kufanya ni kumwamini Mungu na kuamini
dhamira zake.Wakati fulani mtu mwenye maono anapoona giza,na kuzingatia imani
yake kwa Mungu,basi Mungu humpa nguvu katika ono lake.Na nyakati nyingine Mungu hutujaribu ili kudhihirisha uwazi
wako,na utayari wako katika maono.Mtume Paulo alipita katika mambo kama hayo
katika Wakorintho wa pili aliposema kuwa na hukumu ya kifo.hapo alikuwa
amevujika moyo kiasi cha kutamani kufa,lakini alipata neema na utulivu ndani ya
Kristo,na kumwezesha kuendelea.Na hata wengi wetu labda itakulazimu kuruhusa
maono ulionayo kufa.Hebu mpe aliyekupa maono kipaumbele,kwa maana yalikuwa yake kabla ya kuwa ya kwako.Ukifanya hivyo basi atatia nguvu tena katika ono
lako na litakuwa
Bishop.Rhobinson S.Baiye
rhobinsons.blogspot.com
Whatsapp.0764127531
Mwanza Tanzania.
No comments:
Post a Comment