Yafahamu Majuma Sabini Ya Danieli
Majuma Sabini Ya Danieli.Danieli 9:24-27
Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako,na juu ya mji wako mtakatifu,ili kukomesha makosa na kuishiliza dhambi,na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu,na kuleta haki ya milele,na kutia muhuri maono na unabii,na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.Basi ujue na kufahamu,ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi alie mkuu,kutakuwa na majuma saba,na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia zake na handaki,naam,katika nyakati za taabu.Na baada ya yale majuma sitini na mawili,masihi atakatiliwa mbali,naye atakuwa hana kitu,na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji,na patakatifu,na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika,na hata mwisho ule vita vitakuwepo,ukiwa umekwisha kukusudiwa.Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja,na kwa nusu juma hiyo ataikomesha sadaka na madhabahu,na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu,na hivyo hata ukomo,na ghadhabu iliyokusudiwa imwangwa juu yake mwenye kuharibu.
Katika lugha ya biblia juma moja linawakilisha miaka 7.Hivyo majuma 70,ni sawa na 7*70=490
Kwa
hiyo miaka 490, imeamriwa kwa watu wake,sasa hawa watu wake
wanaozungumziwa hapa ni Wayahudi na sio watu wa mataifa.Majuma haya sabini
yalianza kuhesabiwa baada tu Danieli kupokea hayo maono.
Majuma
7 ya kwanza ambayo ni miaka 49 Danieli aliambiwa Yerusalemu itajengwa
tena upya na njia zake kuu katika kipindi cha taabu na shida.Katika hichi
kipindi Hekalu la pili lilijengwa upya na kumalizika ndani ya hii miaka 49 ya
kwanza baada ya kutoka uamishoni.
Haya
yalianza kuhesabiwa pale tu baada ya hekalu kumalizika Kujengwa ndani ya yale
majuma 7 Ikimaanisha ndani ya miaka 49.na katika haya majuma 62.Ikimaanisha,miaka
434,ikiisha masihi Yesu Kristo,atakatiliwa mbali.Mpaka hapo
majuma 69,yatakuwa yameisha.Kwaiyo masihi atakuwa ameshazaliwa na mwisho
wa hilo juma la 69 yaani 62+7=69,atakatiliwa mbali hili lilitokea
pale alipopelekwa kalvari.Bk.
Majuma 69 yalipoisha Mungu aliacha kushughika
na wayaudi na neema ikahamia kwa mataifa kwa sababu wayaudi walimkataa Masihi
wao.Kwa hiyo kikaanza kipindi cha mataifa ambacho mpaka sasa tunaendelea nacho
takribane miaka zaidi ya mika 200sasa.Neema itakapo warudia Israeli
ndipo juma moja la mwisho litakapoanza kuhesabiwa tena yaani miaka 7 ya
mwisho,kutimiza majuma sabini.Majuma haya 70 yaliamriwa kwa watu wa
Danieli yaani Wayahudi na sio pamoja na watu wa mataifa.Na katikati ya hii juma
la mwisho yaani miaka mitatu na nusu ya kwanza injili itapelekwa Israeli.Na
katikamiaka mitatu na nusu ya mwisho mpinga
kristo atavunja agano atakaloingia na Wayaudi na kukomesha sadaka na madhabihu
na ndipo ile dhiki kuu itakapoanza
Bishpo:
Rhobinson S.Baiye
No comments:
Post a Comment