KANISA LENYE MALENGO
Kanisa lenye
malengo ni kanisa lililo na umoja ndani yake.Kwa maana umoja ni nguvu na
mtengano ni udhahifu.Na maandiko matakatifu yanatuonyesha kwamba,ni vema na
tena yanapendeza kukaa pamoja kwa umoja.Zab
133:1-4,Md 4:32-35.Na kanisa likiwa na umoja lazima litashugulika na lengo au
malengo yake wala si vinginevyo.Lakini fahamu kwamba umoja unanguvu zake.
Nguvu Ya Umoja.
Umoja
una nguvu zake,na nguvu hizo ni za ushindi maana palipo na umoja ushindi
haupingiki wala hauzuiliki. kwa nini ushindi wa umoja ni lazima? Mwanzo 11:1-9)
Mst 3-4 Mst 6 Mst 7-9,Ukisoma mistari hiyo katika kitabu hicho katika sura hiyo
hapo,utaona na kufahamu kwa nini ushindi wa umoja ni lazima.Watu wa
Mwanzoni walithamini umoja na ndiyo sababu yao kufaulu katika mipango na
mikakati waliyoipanga kwa kufikia malengo waliyojiwekea.Hadi Mungu alithibitisha kwamba kitu au jambo
linalofanyika katika umoja haliweza kuzuilika.Mwanzo 11:6,Bwana
akasema,Taza,
Watu
hawa ni taifa moja,na kugha yao ni moja;na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya,wala
sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
Maana Na Matumizi Ya Nguvu.
Kama
mwandamu naamini unahitaji kujuwa na kufahamu maana ya neno nguvu na jinsi
inavyofanya,au matumizi ya nguvu.Kwa kawaida sana nguvu ni uwezo wa kufanya
jambo,ni madaraka uvumilivu wa kuweza kuendeleza jambo.ngvu ni msukumo mkali
unaotokana na nishati.Kwa kuelewa nguvu ni nini hasa,ni vema tujifuze kwa Yesu
Kristo kama yasemavyo maandiko yeye, ndiye nguvu za Mungu.Wanafunzi wa Yesu
Kristo waliogopa sana.Dhoruba ilipozuka ghafla walipokuwa wakivuka bahari ya
Galilaya kwa mashua.Hapana shaka kwamba walizoea kuona dhuruba katika bahari
hiyo,kwa sababu bahadhi yao walikuwa wavuvi hodari.Math 4:18-19,Lakini
ilikuwa dhoruba kubwa ya upepo wenye nguvu nyingi.Bahari ilichafuka kwa sababu
ya dhoruba hiyo.Wanaume hao
walijikakamua sana kuongoza mashua,lakini dhoruba ilikuwa kali sana.Yesu alikuwa amelala
usingizi katika tezi,akiwa amechoka
baada ya kuwafundisha watu siku nzima,Huku wakiogopa kufa.Wanafunzi walimwamsha
na kumsihi.Bwana tuokoe,tuna karibia kuangamia.Marko 4:35-38,Math
8:23-25.Yesu hakuogopa.Kwa ujasiri aliukemea upepo.Mara moja upepo na
bahari ikatii dhoruba ikakoma,mawimbi yakatulia,kukawa shwali.Kwa hiyo fahamu
nguvu za Mungu zimo katika Yesu Kristo.Yohana 1:1-4.
1.Umoja Ushugulisha N a Lengo.
Tumeona jinsi watu wabiblia walivyo thamini umoja.Walithamini umoja kwa
sababu waligundua mbambo makubwa ambayo yamo na yatokanayo na umoja.Jambo kubwa
la umoja ni nguvu za umoja,na nguvu za umajo kushugulika na lengo au malengo
ambayo watu jamii imejiwekea.Kama kanisa la mahali linahiji kuimarika na
kusitawi nilazima lishugulike Na lengo au malengo wala si vinginevyo.Kanisa
ambalo lisilo kuwa na migogoro ni kanisa ambalo linaloshugulika na lengo
malengo yao wala si migogoro.Lengo ni nini,lengo au malengo ni wazo au mawazo
makuu ya ubinadamu
F.Schiller
alizungumzia juu ya umuhimu wa kuweka malengo makubwa ni rahisi kuingia na
kamanda mkuu Alexander wa Macedon alisema juu ya malengo:Kama
haiwezekani,nilazima ifanyike.Fahamu lengo,katika maisha ya mtu linaweza
kuelezewa na maneno yafuhatayo:Picha halisi au halisiya nini suala la mtu
binafsi ni kwa kuifadhiwa katika akili ya matokeo ya mwisho
yaliyotarajiwa.Lengo lina muundo wake na huanza na ufahamu wa mtu juu ya
kufikiri kupitia njia zinazowezesha utendaji weke.Bila lengo hakuna
ukuaji,badala ya kutambua moja ya asili ya mtu.Uwezo wa mtu wakawaida ni kama
bahari kubwa,ni kama bara jipya lisilohifadhiwa.Ulimwengu wa uwezekano
unaotarijiwa kutolewa na kuelezwa uzuri.Fahamu kufanikiwa ni malengo,na mengine
ni maoni.Watu wote na makanisa yote yaliyofanikiwa walikuwa na lengo
kubwa.Walijua walichokitaka na walihitaji mkazo mmoja katika kufanikisha
hilo,kila siku.Uwezo wako wa kanisa kuweka malengo ni ustadi wa
mafanikio.Malengo ya kufungua akili yako chanya na mawazo chanya ya kufikiri
malengo.Ukiwa na malengo wewe ni wakuteleza tu,na utapita kwenye mikondo ya
maisha.Na ukiwa na malengo wewe ni wakuruka kama mshale moja kwa moja kwa kuwa
msababishaji ni wewe.Ukweli ni kwamba unao uwezo mkubwa zaidi na kama kanisa la
mahali linaweza kudumu hadi kuja kwa Kristo,Fahamu kwamba chochote ambacho
umekamilisha hadi sasa ni sehemu ndogo tu ya kile kinacho wezekana kwaka na kwa
kanisa pia.Moja ya sheria za kanisa kufaulu ni hili hapa,Haijalishi limeanza
kwa mazingira gani au linaongozwa na nani,limwetokao wapi,ni maamuzim ya mtu
peke yake na kanisa lenyewe pasipo kutengemea maamuzi ya mtu au watu
aharufu.Fahamu malengo yako nyenu yawe wazi.Malengo yaliyo wazi,yanaongeza
ujasiri wako na wakanisa pia.Na unakuza uwezo wako na kuongeza viwango vyako
vya motisha.
Malengo Uhunda Ulimwengu Wako
Mwenyewe.
Lengo
malengo katika ugunduzi mkubwa zaidi katika historia ya mwanadamu na nguvu ya
akili yako kuunda mambo ya maisha yako.Kila mtu anachokiona katika ulimwengu huu ni wazo la mtu na liliweka malengo yake
hadi hapo yalipofikia.Kwa maana lilianza
wazo,hamu,tumaini na ndoto,iwe katika akili ya mtu mmoja au katika akili ya
watu wengi.Wazo mawazo yako ya kanisa ni ubunifu.Mawzo malengo yako aidha ya
kanisa yanaunda ulumwengu wako ulimwengu
wa kanisa na kila kitu kinachotokea kwako na kwa kanisa pia.Kauli kuu ya
muhtasari wa dini zote,falsafa Metaphysiki,saikolojia hii.Inasema kwamba
uko hivyo ulivyo ni kwa sababu ndivyo unavyofikiri wewe kuwa.Maranyi kanisa
linaishi katika mazingira na tabia ya kiwango cha fikira za mtumishi kiongozi
mkuu.Ulimwengu wako wan je mwishowe unakuwa
onyesho lako la ulimwengu wako wa ndani na vioo hukurudia kwa
unavyofikiria.Chochote unacho fikiria juu ya hilo huibuka katika ulimwengu wa
ukweli wako.Fahamu kwamba maelfu ya watu waliofanikiwa wameulizwa,mnda wao
mwingi wanafikiria ni nini? Jibu la kawaida linalotolewa na watu waliofanikiwa
ni kwamba wanafikiria juu ya kile wanachotaka,na jinsi ya kukifanikisha.
Faida Ya Kanisa Kuwa Na Malengo
Kunafaida
katika kanisa kuwa na malengo na hata mtu binafsi kuwa na malengo kuna hizi ambazo nitazihainisha hapa na faida za
jumla.yaana ni faida atakazozipata mtu dinafsi na kanisa lenyekwa na
malengo.Kwa kuwa kanisa yenye umoja ujishugulisha na lengo au malengo
waliojiwekea wala si vinginevyo.Sasa kabla hujakamilisha chochote maishani,na
lazima ufahamu unahitaji nini.Ni lazima ukae chini utafakari kama kile
unachokifanya kama kina samani kwako;ikiwa hakina thamani kwako,basi tenga muda
ujiwekee malengo yenye maana kwako.Kwa maana maisha ya kanisa au mtu bila
malengo ni sawa na kuanza safari bili kufahamu unakotaka kwaenda au
kufika.Kanisa kujiwekea malengo kuna umuhimu mkubwa sana kwa maana hufanya kanisa kujikita kwenye malengo
kuliko kujikita kwenye migogoro isiyonatija.Mtu Kanisa lifahamu kwamba
kujiwekea malengo ni hatua ya kwanza ya kufanya visivyoonekana vionekane
dhahiri.
1: Faida Ya Kwanza Yakuwa Na Lengo.
Mwanzo
kabisa lengo au malengo yanakupa mwongozo
yaani mwelekeo maishani.Malengo hulisababisha kanisa kubaini kitu
kinacholengwa,na kulifanya kanisa kuelekeza nguvu zake kwenye kitu
husika.Badala ya kushika hiki na kile au kuwa huyu na Yule malengo au lengo
litaliwezesha kanisa kufahamu kipi kifanyeke na nani afanye na kwa mnda wa
kufanya.Ifahamike kwamba kanisa kuwa na mwongozo nijambo muhimu sana kuliko
kuishi maisha ya kudandia mambo ni vizuri kanisa kama kanisa kuwa na mwelekeo.Na
mwelekeo huletwa na Malengo ya kanisa.Na kanisa ambalo halina malengo ni kanisa
ambale linafananishwa na chombo ambacho kina endeshwa na mawimbi ya bahari
likipelekwa huku na kuele likidandia mambo kwa kukosa mwongozo.Yakobo
1:5-8
2: Faida Ya Pili Yakuwa Na Lengo.
Lengo Huleta Uwezo Na Ngvu Za Maamuzi.
Baada ya kanisa kupata mwongozo utokanao na malengo sasa basi
litaweza kubaini ni maamuzi gani yanafaa na ni yapi ambayo hayafai kulingana na
malengo ambayo yapo.Pia kanisa litaweza
kufahamu mambo ya msingi katimaisha ya kanisa hilo.Kanisa lenye malengo huwa
makini sana kwenye maamuzi yake kwa kuwa linalinda,lisije likafanya maamuzi
yatakayoathiri lengo au malengo huka.Kwa hiyo kanisa lenye kudumu katika umoja
lina kuwa makini sana kulinda umoja huo katika maamuzi kulingana na maelengo
yatokanayo na umoja wao.Maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi,na kwa watu sahihi.
Kum 16:18-19,17:7-9,25:1.
3:Faida Ya Tatu Yakuwa Na Lengo.
Lengo
huwezesha Kutawa Baadaye.
Kanisa
limapokuwa na malengo na mipango sastahiki na kuyatimiza ni wazi moja kwa moja
limekwisha tawala baadaye pasipo watu kufahamu kwamba tayari kanisa limekwisha
tawala.Kuweka malengo ni jambo zuri ambalo litaliwezesha kanisa kutahamu aina
ya mfumo wa maisha yake ya baadaye.Lambo la muhimu ni kuhakkikisha kuwa unaweka
mpango sahihi na wakati sahihi na kwa watu sahihi.Kwa sababu unaweza kwafanya
vitu sahihi na kwa mnda sahihi lakini usiyafanye kwa watu sahihi utakuwa
umepoteza mnda.Ni muhimu kanisa kuhakikisha kila siku kuna kitu kinachofanyika
ili kukamilisha sehemu fulani ya malengo iliyojiwekea maishani.Fahaumu kwamba
malengo na ramani katika mzunguko wa kanisa hata maisha ya mtu.Bila shaka lengo
malengo hutawala katika mnda uliyopo na mnda wa baadaye bila watu kujua na
kufahamu.Mwanzo 1:26,Mathayo 20:25,Marko 10:42
Lengo Huwezesha Kujikita Kwenye Mambo Muhimu.
Yapo
mambo mengi katika maisha ya kanisa la mahali ya kila siku.Lakini yawezekana
siyo yete ya muhimukatka kutimiza malengo ya kanisa.Kanisa likiwa na malengo ni
rshisi kubaini mipango au mambo ya msingi na ya muhimu kwa kutazama yale yote
yanayokinzana na malengo.Haijalishi Kanisa linalikodolea macho jamnba
fulani,kwa kiasi gani,kama linakinzana na yake halina budi kuliacha au kuachana
nalo.Ni kweli yapo mambo mengi ambayo kanisa kama kanisa linayag`ag`ania lakini
hayana umuhimu kabisa katika afya ya kanisa.Hata wapo watumishi,viongozi,na
watenda kazi wengine katika kanisa ambao si wamuhimu lakini wanag`ag`ganiwa
kuwepo katika huduma au nafasi walizonazo ao walipo.Watu kama hao wasio wa
umuhimu wana lichelewesha kanisa kufika pale ambapo wanahitaji kufika,kulingana
na malengo yaliyopo.Kumbukumb la Torati 10:11
5: Faida Ya Tano Yakuwa Na Lngo.
Kanisa
linapokuwa na malengo thabiti washirika
pamoja na watumishi na viongozi huwa na matumaini na huhamasika pakubwa.Na
hamasa huzidi pale ambapo tunaanza kuona pale tunapokamilisha malengo yetu ya
mnd mfupi,ili kutuhamasisha kufanya bidii zaidi kuyafikia yale ya mnda mrefu.Ni
kweli na wazi kwamba chanzo kizuri cha hamasa ni kujiwekea malengo na kuanza kuyatimiza.Kumbuka kwamba
utekelezaji wa malengo ni njia mojawapo muhimu ya kuhamasisha na kushawishi
washirika kuamini na kudumu kwa kile kilicho pangwa.Na zaidi sana hata wale
ambao wako nje na kanisa,watakapoona maendeleo watafahaumu na kusema hayo ndiyo
malengo,na hivyo ni vyepesi sisi kuwafikia na kuvuta kutukaribia.Mathayo
27:20,Luka 24:29,Md 6:11,
6: Faida Ya Sita Yakuwa Na Lengo.
Fahamu kwamba mtu au kanisa lenye malengo Hulinda muda haliwezi
kamwe kupoteza muda.Kanisa likiwa na
malengo ni wazi kwamba mnda wake wote utakuwa umegawanywa kwenye kuyafanyia
kanzi na kuyatimiza malengo wala sivinginevyo.Kwa njia ya kujiwekea malengo
kanisa halitoweza kwa kufanya mambo ambayo hayaliwezeshi kanisa kifikia ndoto
malengo yake.Haitarajiwi kanisa lenye malengo kulewa na au kuleweshwa na na
matokea ya mipango ya malemalengo.Haitarajiwa kanisa kutokuwajibika kwa kuwa
lina malengo.samahani mengi ambayo ungetarajia kuyavuna katika sura hii na
kipengele hiki,yanazungumzwa kwa kina katika sura ya 8,isemayo kanisa na
nyakati.Mathatayo 2:7,16,9:15,20.
7:Faida Ya Saba Yakuwa Na Lengo.
Kanisa
lenye malengo hufanya uwekezaji.Uwekezaji ni hali au tendo na njia ya fedha au
mali zako kuzaa zaidi.Kanisa likiwa na malengo
yaliyo wazi,litafahamu nini,wapi,na lini liwekeze.Kwa kuwa malengo yataliwezesha kanisa kubaini ni uwekezaji
gani unaoendana na malengo ya kanisa.Lakini kama kanisa halina malengo kama
tulivyoona tangu mwanzoni mwa mada hii,laweza kuwekeza kwa kila kitu ambacho
kinacho jitokeza mbele yake,na matokeo
yake huwa na kinyume na matarajoyo.Kwa hiyo wewe mcha Mungu katika
Kristo fahamu kila unachokifanya katika
kanisa una wekeza na siku mja vita rudi kwako ma kukusaidia na hapo utakuwa
umepata faida kwa kile ulicho wekeza madhabahuni.Wekeza katika Ibada ya
Utoaji,Wekeza katika Ibada ya Maombi,Wekeza katika Muda,Wekeza katika kusifu na
kuabudu Mungu,na hayo yote utapata faida nzuri ya uwekezaji wako.Mathayo
2:11,19-21,Fahamu kwamba wakati utakapopata au kupokea msaada kutoka
kanisa lako,hapo fahamu umepata faida ya uwekezaji wako katika kanisa.akumbuka
kwamba Mungu hutubariki kulingana na uwekezaji wetu kwake.Kanisa linapotoa
misaada kwa mayatima,walemavu, wajane na wagane,wafungwa,nk,ha
Po
kanisa litakuwa limewekeza kwa Mungu,na litapata faida katika uwekezaji huu.
8:Faida Ya Nane Yakuwa Na Lengo,
.Kainsa au mtu
binafsi aliye na malengo hujitathmini.Kanisa linapimaje kufanikiwa au mafanikio
yake kama halina kipimo cha kupimia
kufanikiwa huko,malengo ni kipimo muhimu kitakachowezesha kanisa kutathimini
kama limefanikiwa au la.Kanisa likiwa na malengo ni rahisi kutazama kama yale
yaliyofanywa au yanayofanywa yameliwezesha kufikia lengo au malengo yake.Kama
yameliwezesha basi ni vizura na yanatia moyo sana.Lakini ikiwa hayajaliwezesha
kufikia lengo malengo,kuna mambo ya kutazama upya.
Umuhimu Wa Kanisa Kutathimini Mambo Yake.
Katika
mfumo wa kanisa na maendeleo yake,tathmini au kutathmini ni utaratibu maalumu
wa kupima mafanikio ya matokeo na malengo yaliyokusudiwa,unafanywa kulingana na
utaratibu wa kanisa husika mara ngapi kwa mwaka au kwa miaka mingapi.kanisa
litatathmini likijitahidi kuchambua
hatua zilizofikiwa kufanikisha lengo kuu la mfumo wa kanisa ambao ni mfumo wa
ukaguzi unaofanya kazi kwa ufanisa ili kutoa huduma bora kwa washirika.Kwa
kufikia malengo au lengo hili maeneo ya matokeo yafuatayo yaliwekwa ili
yafanyiwe ufatiliaji na tathmini.
Miradi Inayofadhiliwa Inafanya Kazi Kwa Ufanisi?
Tathimini
inataka kuona namna ambayo maeneo ya kutolea huduma yanayofadhiliwa katika
kanisa yanakamilika na yanafanya kazi ya kutoa huduma zinazo hitajika.Kwa
kufahamu kama miaradi hiyo inafanya kazi kwa ufanisi nimuhimu kanisa kujifanyi
tathmini kupitia kamati ya ukaguzi wa fedha na mali za kanisa,na ifanywe kwa
upole na hofu ya Mungu.2Nyakati 32:28,Wagalatia 6:1,Efe 4:2,Mathayo
9:8,2Kor 7:11.
Vipaumbele Vya Kanisa Vinazingatiwa?
Tathmini
itapima kiwango ambacho vipaumbele vya kazi au miradi ya kanisa
ilivyozingatiwa,kutekelezwa na inavyotoa huduma zilizokusudiwa.Kanisa
lenyekudumu katika umoja lazima liwe na nguvu.Na vema kutimiza maono mikakati
na kuyatathmini kama mambo yako sawa.Luka 15:17
Jidihada Za Washirika
Zinatambulika Na Kuwezesh
Wa Na Kupewa
Usaidizi?
Tathmini
itapima namna ambavyo jitihada za washirika zinavyotambuliwa na kuungwa mkono
kifedha kitaaluma.
Kanisa
ambalo linadumu katika nguvu za umoja nilazima litathamini jitihada za
washirika.
Fedha Zinazotolewa Kwa Usawa ndani Ya Kanisa?
Tathmini
itapima namna ambavyo miradi inavyotekelezwa imeleta mabadiliko chanya katika
kanisa zetu zenye hali duni kutokana na kigezo cha mgao wa fedha kwa usawa
.Msisitizo unatolewa kwenye kupunguza utofauti wa upatikanaji wa huduma kati ya
makanisa ambayo yana hali bora nay ale yenye hali duni.1Sam 15:22,Zaburi
62:12,
Usimamiza Wa Fedha Za Kanisa Unaboreshwe.
Tathmini
itapima namna idara za makanisa
zinavyozingatia taratibu za usimamizi wa fedha kama vile maandalizi sahihi ya
malipo,maandalizi na mawasilisho ya taarifa za fedha,kujibu hoja za ukaguzi kwa
wakati.mpngo mzuri wa vyanzo vya watumishi wa idara ya fedha na vitengo au
matawi yake na mikakati ya kuboresha ukusanyaji wa vyanzo vya ya ndani ya
kanisa.Zaburi 109:8,Hesabu 3:36,1Nya 9:23,24:3,19,26:
1,2:9:4,23
2,Md 1:20./
Je,Maeneo Yenye Mazingira Mangumu Yanafaidika?
Malengo
ni kutengeneza utaratibu wa kutekeleza miradi yenye ubora kwenye makanisa yenye
mazingira magumu katika maeneo yao,licha ya changamoto zilizopo.Tathmi
Mini
itapima kuona kama zinaandaa ya kuwavutia waamini wapya.Tufahamu kwamba
mazingira ya kanisa yanahubiri kwamba
Mungu yupo na nimtendaji mzuri sana,katika watu wake.Ezra
3:6-7,14,4:1,5:15,6:5,12,8:23;
Washika Wanaendelezwa Na Kusimamiwa Ipasavyo?
Tathmini
itapima kuona kama washirika wanaendelezwa kimafunzo yenye ufanisi katika ngazi
ya juu na ya msingi za katika ngazi zote kutokana na utaratibu wa kanisa
husika,pamoja na matokeo ya mafunzo hayo katika usimamizi wa miradi ya
kanisa.Tathmini itapima pia mbinu za bora na jitihada za kanisa kuwawezesha
watumishi kuendele kubaki hazinzina ya hekima katika kanisa.Mathayo
28:16-20,11:1,Marko 4:1,6:2,Luka 3:23,20:21,Md 1:1,4:18,Zaburi
32:8,45:4,Mithali 4:11.
Je,Kanisa Na Miradi Inasimamiwa
Kwa Uwazi..?
Uwazi
na uwajibikaji ni jambo jingine muhimu kwenye tathmini katika mfumu wa
kanisa.Ni muhimiu kuthmini ili kuona kama mfumo huu umesimamiwa kwa uwazi na
kuwajibika kwa washirika na watumishi na viongozi katika kanisa.Pia tathmini
itaainisha kuona namna kanisa lilivyochangia kukuza umoja na utawala bora.
Je Fedha Za Kanisa Zinagawika Kwa Usawa?
Tathmini
itapima matokeo ya kanuni ya ugawaji wa rasilimali iwapo imezingatia usawa na
haki katika upatikanaji wa huduma za kanisa.Ukisoma kwa makini katika kitabu
cha matendo ya mitume,inasema kwamba wakati kanisa lilipoongezeka palikuwa na
manunguniko,Md 6:1-7,Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka
hesabu yao,palikuwa na manung`uniko ya Wayaudi wa Kiyunani juu Waebrania kwa
sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku.Wale Thenashara
wakawaita jamii ya wanafunzi,wakasema,Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na
kuhudumu mezani.Basi ndugu chegueni watu saba miongoni mwenu walioshuhudiwa kuwa wema,wenye kujawa
na Roho na Hekima,ili tuwaweke juu ya jambo hii;na sisi tutadumu katika kuomba
na kulihudumia lile Neno.Neno hii likapendeza machoni pa mkutano
wote;wakachagua,Stefano,mtu aliejaa imani na Roho mtakatifu,na Filipo,na
Prokoro,na Nikanori,na Timoni,na Parmena,naNikolao mwongovu wa Antiokia.
Ambao
wakawaweka mbele ya mitume,na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu
yao.Neno la Mungu likaenea;na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika
Yerusalemu;jamii kubwa ya makuhani wakatii ile imani.
Bajeti Ya Kanisa Kwa Jumla.
Ifahamike
kwamba fedha za kanisa haziwezi kutosha kukizi vipaumbele vyote vya kanisa kwa
wakati mmoja.Hata hivyo ni muhimu kuboresha hali iliopo kwa 1% ya jumla ya
vipaumbele vyote vya kanisa vinatekelezwa kwa mwaka. Inafaa tathmini angalau
mradi mmoja kwa kila kanisa la kijii wakati wa zoezi la tathmini.Hivyo tathmini
itapima namna ambavyo fedha za kanisa
zinavyoongezeka kufikia lengo.Tunapotathmini mipamgo ya maendeleo ya kijamii ni
vema pia kujitathmini katika mambo ya roho.
Kimeandaliwa
na kuandikwa na
Bishop.Rhobinson S.Baiye.
rhobinsons.blogspot.com
Whatsapp.0764127531
Mwanza
Tanzania.
No comments:
Post a Comment