DUMISHA UMOJA WAKO KATIKA KUTUBU
NA KUSAMEHE. Math 6:14-15
Tabia Ya Kutubu Na Kusamehe.
Kukiri kosa na kuomba msamaha kunawashinda wengi.au kusamehe baada ya kuombwa msamaha ni kazi ngumu kwa wengi.Tabia ya kutubu na kusamehe hujenga mahusiano kwa upya.Ukijizoeza kutubu na kusamehe kutakufanya urekebishe makosa uliyoyafanya.Kutubu na kusamehe kunahitaji unyenyekevu wa hali ya juu sana.Lakini katika kitabu hiki tutajikita hasa katika kusamehe na kusamehewa au kuombwa samahani na kuomba samahani.
Dumisha Umoja Wako Na Mungu Katika Kutubu
Na Kusamehe.
Kutubu
hurejesha uhusiano wako na Mungu kwa
upya.kuwasamehe wengine na kuomba msamaha
huimarisha umoja wako na Mungu na kuondoa kila kunyanzi moyoni.Mungu
yuko tayari na anasubiri kumsamehe mtu anaye omba msamaha. Imeandikwa katika Zab
86:5Kama wewe Bwana u mwema,umekuwa tayari kusamehe,na mwingi wa fadhili kwa
watu wote wakuitao.
Daudi Aliweka Wapi Tumaini Lake La Kusamehewa?
Daudi
alihitaji kuweka sawa umoja ukaribu wake na Mungu ilibidi Daudi aweke tumaini
lake la kusamehewa kwa Mungu.Imeandikwa katika Zab 51:1,Ee Mungu unirehemu
sawasawa na rehema zako kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu.Fanya hivyo kati yako na Mungu na watu pia.
Rehema Ya Mungu I Kiasi Gani?
Kwa
kufahamu kuasi cha rehema ya Mungu,imeandikwa katika Zab 103:11-12,Maana
mbingu zilivyo inuka juu ya nchi kadiri ili ile rehema zake ni kuu kwa wamchao kama mashariki ilivyo
mbali na magaribi,ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
Kuna Ahadi Kwa Wanao Omba Kusamehewa
Kumbuka
kwamba kuna ahadi kwa ye yote anayeomba kusamehewa na Mungu.Imeandikwa katika 1Yoh
1:9Tukiziungama dhambi zetu,yeye nimwaminifu na wahaki hata atuondolee dhambi
zetu na kutusafisha na udhalimuwote.
Mungu Atakusamehe Kama Unawasamehe Wengine.
Biblia inadhibitisha kuwa Mungu atakusamehe ikiwa wewe unawasamehe watu wengingine.Imeandikwa katika Math 6:14-15,Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.
Wale Waliyosamehewa Husamehe.
Nakuomba
msomaji wa kitabu hiki ufahamu kwamba wale wanaosamehewa husamehe wengine.Pia
imeandikwa katika Efe 4:31,Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi kasamehane
kama Mungu katika Kristo aliwasamehe ninyi,.
Kusamehe kwa kweli hakuhesabu makosa
Fahamu
ndugu yangu kusamehe kwa kweli hakuhesabu wingi wa makosa.Imeandikwa
katika Math 18:21-22.Kisha Petro
akamwendea akamwambia Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi name ni msamehe?
Hata mara saba? Yesu akamwambia sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini.Yesu
alimaanisha kusamehe hakuna ukomo au kikomo.Wewe inakubidi kusamehe ili
kutimiza sababu za kusamehe tutakazoziona hapo chini.Endelea kusoma sababu za kusamehe.
Je Tunapo Samehewa Ni lazima Tuwe Na Hofu?
Hakuna
haja ya kuwa na hofu wakati tunapo samehewa.Imeandikwa katika . Nilikujulisha
dhambi yangu wala sikukuficha upotovu wangu Nalisema nitakiri maasi yangu kwa
Bwana nawe utanisamehe upotovu wa dhambi yangu.Katika kusamehe Yesu
ametukomboa katika sheria ya dhambi na
mauti kama mshahara wa dhambi.Rum
8:1-11.Wakolasai 2:13-14
Tunapo Hitaji Msamaha Tunahitaji Nini?
Fahamu
kwamba wakati unapo hitaji kusamehewa na Mungu unahitaji kuoshwa kutakaswa kuwa
mweupe pe.Imeandika katika Zab 51:2-4,Unioshe kabisa na uovu wangu maana
nimejaa makosa yangu na dhambi yangu I mbele yangu daima Nimekutenda dhambi
wewe peke yako na kufanya maovu mbele za macho yako wewe ujulikanaye kuwa
unahaki unenapo,na kuwa safi utoapo hukumu.
Omba Msamaha
Jambo hili ni muhimu sana.Omba msamaha usisubiri kuombwa msamaha.Imeandikwa katika Zab 51:7-12,Unisamehe kwa hisopo nami nitakuwa safi,unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko dheluji,unifanye kusikia furaha na shangwe,mifupa ilio ponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu uzuj ifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upya roho ilio tulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho wako mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha yawokovu wako unatengeneze kwa roho ya wepesi.
Kuwa
na imani kwamba Mungu amekusamehe.Imeandikwa katika Zab 32:1-6,Heri
aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake heri Bwana asiyemhesabia
upotovu,ambaye rohoni mwake hamna hila.niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa
kuugua kwangu mchana kutwa na kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea
jasho langu linakauka hatanikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi nalikujulisha
dhambi yangu wala sikuuficha upotovu wangunalisema nitayakiri naasi yangu kwa
Bwana naweukanisamehe upotovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati
unapopatikana hakika maji makuu yafurikapo hayatamfikia yeye.
Usiombe msamaha kwa sababu wengine wanaomba msamaha,bali omba usamehewe na Mungu kwa kujutia dhambi na makosa yoko.
Dumisha Umoja Wako Na Mke,Mme Katika
Kutubu
Na Kusamehe.
Kosa
linapotendeka,msamaha huhitajika kutoka pande zote mbili.kutokukiri makosa sio
njia ya kutukuwa mkosaji, na tabia hiyo huharibu uhusiano kati ya mke na
mume.Hata kama huoni kosa,fahamu mwezako analiona.Ni vyema kuomba msamaha ili
kurejesha uhusiano mzuri uliokuwepo.Unaweza kugundua baadaye kuwa ulikuwa
ukikosea.Makosa yasiwe sababu ya kufarakana na kuharibu uhusiano wenu.
Maana Ya Msamaha Au Kusamehe
Katika
Biblia neno la kigriki linalotafsriwa kusamehe linamaanisha kihalisi
kuhachilia.Ni kama wakati ambapo mtu anaamua kutodai malipo ya teni.Yesu
alitumia ulinganisho huu alipowafundisha wanafunzi wake ambao aliwaita mitume wake alipowaambia salini hivi.Utusamehe
makosa na dhambi zetu kama vile tunavyo wasamehe wanao tukosea.Luka 11:4.
Vivyo
hivyo alipotoa mfano kuhusu yule mtumwa asiye na rehema Yesu alilinganisha
msamaha na mfano wa kufuta deni.Math 18:23-35.Tunawasamehe wengine tunapoepuka kinyongo na kutodai malipo kwa
sababuu ya uchungu au hasara tuliyopata.Biblia maandiko matakatifu
yanatufundisha kwamba upendo usio na ubinafsi ndio msingi wa msamaha wa kweli
kwa kuwa upendo,hauhesabu mabaya.1Kor 13:1-8
Kusamehe Hakumaanishi Yafuatayo
Kupuuza
Kosa:Andiko
la Isaya 5:20.linawashutumu wale wanaosema kuwa matendo mabaya au yasiyofaa
hayana madhara au yanakubalika.Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema,na kwamba
wema ni uovu.watiao giza badala ya nuru,na nuru badala ya giza.Watiao uchungu
badala ya utamu na utamu badala ya uchungu!Katika undugu na urafiki na utu
na ndoa nivema kutopuuza mambo yanayofaa kati yenu.Kwa sababu kusamehe na
kusamehewa sio kupuuza mambo bali ni kufuta mambo.Usiweke kweli badala ya uongo
na usiweke uongo badala ya kweli.Kut 23:1,Usifumishe habari za uongo,usitie
mkono wako pamoja na waovu,kuwa shahidi wa uongo.
Kuishi
au kujifanya kana kwamba haujatenda kosa au haujatendewa kosa si kwamba ina
maana kwamba dhambi imesamehea la
hasha.Mungu alimsamehe Daudi Mfalme wa Israeli dhambi zito aliyoitenda,lakini
Mungu hakumlinda Daudi kutokana na madhara ya matendo yake.Mungu alimwongoza
Daudi aandike kuhusu dhambi zake na hadi leo zinakumbukwa kwa kusomwa kwa kile
Daudi alicho kiandika.2 Sam 12:9-13.
Kuruhusu Wengine Wakutumie Vibaya
Kwa
mfano,tuseme kwamba umemkopesha mtu pesa,naye anazitumia vibaya halafu anashindwa
kukulipa kama alivyoahidi.Sasa anasikitika sana na kuomba msamaha.Je,unaweza
kumsamehe kwa kuweka kinyongo moyoni,na kutomkunbusha-kumbusha jambo hilo? Na
labda hata kufuta deni hilo.Na hata hivyo unaweza kuamua kutokumkopesha pesa
tena.Zab 37:21,Mith 14:15,22:3,Gal 6:7
Kusamehe Bila Misingi Halali.
Mungu
hawasamehi watu wanaotenda dhambi kimakusu
Di
na kwa ukatili hukataa kukubali makosa yao na kubadilika na kuomba msamaha wale
ambao wameumizwa.Mith 28:13 Md 26:20,Ebr 10:26.Watu hao wasiotubu yaani watu
wasio mgeukia Mungu huwa ni maadui wa Mungu naye Mungu hatazamii kuwasamehe
watu ambao yeye hawasamehi.Zab 139:21-22,
Kusamehe Makosa Ya Kudhaniwa
Nyakati nyingine,huenda tukahitaji kukubali kuwa hatukuwa na sababu ya kukasirika. Biblia inasema tusiwe na hasira kwa maana hasiri hukaa katika kifua cha wapumbavu.Mith 7:9.Unapodhani kwamba umekosewa na mtu halafu ukamsamehe bila kuwa na hakika kwamba umekosewa na ukasamehe,unafananishwa na kicha mwendawazimu,ambaye husema mambo mengi lakini kesho ukimuuliza anakuambia yaliyotofauti na yajana.
KOSEA
Sababu
ni kitu ambacho kinachofanya kitu kingine kitokee.kisa chanzo.Sababu ni maelezo
yanayoonyesha kwa nini hoja zilizotolewa hazikubaliki au kwa nini
zinakubalika.Sababu ni lengo au malengo au madhumuni yanayompeleka mtu kufanya
jambu fulani.Usifanye jambo lolote pasipokuwa na sababu.Ata kicha anafanya
mambo kinyume na kawaida sababu na akili zake zimechanganikiwa hazina
kumbukumbu na hazina aibu.Hapa chini nimekuorodheshea baazi za sababu za wewe
kumsamehe aliyekukosea.
Kukuweka Huru
Kutokusamehe
kunakufanya uwekama mtumwa na kujisikia vibaya kabisa kukosa amani na zaidi ni
pale utakapokutana au kumwona yule aliyekukosea anafuraha na anaendelea na
maisha yake bila tatizo lolote.Fahamu mtenda dhambi ni mtumwa wa dhambi.Yesu
akawajibu,amin amin,nawaambia,kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.Math
8:34.Isaya 61:1.Roho ya Bwana Mungu ijuu yangu;kwa sababu Bwana amenitia mafuta
niwahubiri wanyenyekeve habari njema;amenitu
Ma
ili kuwaganga waliovujika moyokuwatangazia mateka uhuru wao,na hao waliofungwa
habari za kufunguliwa kwao.Yohana 8:38.
Kukupanguvu Za Kuendelea Mbele Zaidi
Kuna
mambo mengi mazuri na muhimu zaidi katika maisha kuliko chuki na hasara.Kwa
nini ufikirie tu kuhusu mtu aliyekuumiza au kukukwaza? Usipo msamehe utabaki
kuumia tu na kushindwa kufanya mambo muhimu ya kusonga mbele na kupata
mafanikio yatakayomshawishi na kuona umuhimu wako wa kuzaliwa na Mungu kuruhusu
wewe kuishi duniani.Math 5:16,Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya
watu, wapate kuyaona matendo yenu mema,wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni
Sheria na manabii.
Kulinda Afya Yako
Uchungu
na maumivu uliyoyapata baada ya kukosewa ni dhahiri kuwa yanaweza kusababisha
matatizo ya afya kama vile msongo wa mawazo,kukonda,ugojwa wa moyo.Kumbuka
msango wa mawazo ni chanzo cha maradhi mbalimbali kama vile shinigizo la
damu,kiharusi,nak.Sasa kwa nini yakuandame kwa sababu ya kutosamehe! Ni muhimu
na busara kusamehe aliye kukosea ili afya yako iwe vizuri.Math 9:12,Marko
2:17,16:18,2Fal 4:35.
Huondoa Hasira Na Chuki
Ni
kweli chuki na hasira huingia nafsini na moyoni mwako mara tu unapokosewa.Ukiwa
na chuki na hasira kali nafsini na moyoni mwako,na ni dhahiri utapunguza tija
katika yale unayofanya katika mzuguko wako wa maisha.Unaposamehe unajiweka
katika hali nzuri zaidi kiutendaji.Fahamu kwamba hasira hukaa kifuani mwa
mpumbavu.Na chuki husababisha mauaji.Efe 4:26,Iweni na hasira ila msitende
dhambi;jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka.Efe 4:31,Uchungu wote na
ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu,pamoja na kila namna ya
ubaya.
Huondoa Utawala Wa Mtu Mwingine katika Akili
Yako
Ni
dhahiri kwamba unamkumbuka mtu aliyekukosea kila wakati akilini mwako.Ni wazi
kwamba ukisikia jina lake likitajwa au hata sauti yake tu unapata maumivu
kutokana na lile alilokufanyia.Fahamu huo ni utawala wa mtu mwingine ambao
umetawala akili na fikra zako.Ni vema msamehe leo ili uendelee na maisha yako
yeye uhuru.1Kor 15:24,Soma Wakolosai 2:23,Mambo hayo yanaonekana kana kwamba
yana hekima,katika namna ya ibada mliyoitunga wenyewe,na katika kunyenyekea,na
katika kuutawala mwili kwa ukali;lakini hayafai kitu kwa kuzuia tama za mwili.
Hukuletea Utulivu Wa Akili.
Ni
dhahiri shahiri kwamba watu wengi wakikosewa wanashindwa kupata utulivu wa
akili.Jambo hili limefanya wengi hata kushindwa kutimiza majukumu yao ya kila siku.Mara kichwa
kinauma,mara sijisikii vizuri,mara sina nguvu mara sina mood.Hayo yote
hudhihirisha ukosefu wa utulivu wa akili.Math 7:24,Bali kila asikiaye hayo
maneno yangu,na kuyafanya,atafananishwa na mtu mwenye akili,aliyejenga nyumba
yake juu ya mwamba.
Ni Aina Bora Ya Kisasi
Je
unafikiri kamba kulipa kisasi ni kufanya baya au mabaya kama uliyofanyiwa? Kama
jibu ni ndiyo,unakosea kwa kiasi kikubwa sana.Fahamu ni pale mtu anapokukosea
lakini wewe unamfanyia jambo jema.Hapo umemmwagia makaa ya moto kichwani mwake.Math
5:37,Bali maneno yenu yawe Ndiyo,ndiyo,Siyo,siyo;kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka
kwa yule mwovu kuhusu kujilipiza kisasi.Linganisha na Md 7:24.
Huonyesha Upendo Mkuu
Kuna
wakati mtu aliyekukosea anaumia kutokana na kosa alilofanya lakini anashindwa
kuja kuomba msamaha.Kumbuka kumsamehe kuna dhihirisha upendo wa hali ya juu hata kama hajaja
kukuomba msamaha.1Kor 13:1-8.Kumbuka kwamba tumesoma kwa undani sana
kuhusu neno upendo katika sur ya kwanza.Tume ona upendo wa ki-Mungu,upendo wa
kirafiki,upendo wa kindugu,upendo wa kimapenzi mahaba ndoa,upendo wa kujipeda
mwenyewe.
Kiashiria Cha Ukomavu Wa Imani
Ni
kweli hakuna mtu ambaye ana uwezo wa kusamehe kama hana au sio mkomavu wa imani
kiakili na kihekima na busara za kutosha.Fahamu watu wachanga hupenda kubeba na
kutunza chuki na hasira,wao ni heri kubaki na maumivu katika maisha yao yote kuliko
kuyaachilia ili wawe huru.Math 17:20,
Dumisha Umoja Wako Na Jamii Katika Kutubu Na
Kusamehe.
Tabia
ya kusamehe na kuomba msamaha kwa watu
wote ni ya misingi katika kujenga mahusiano mazuri na watu.Kutubu na kusamehe
kunasaidia kuliweka wazi kosa na kuanzisha jitihada za kutorudia makosa, badala
ya kujenga ukuta wa kujilinda kwamba hujakosea ni bahati mbaya.Jamii ya watu
hupenda na kuthamini mtu mwenye roho na moyo wa kuomba msamaha wakati
anapokosea jamii.Baadhi ya watu katika jamii hujilkita kuchenga ukuta wa
kujilinda ili kupata nafasi ya
kuwadhihirishia jamii kwamba hawajakosea na hata kama wamekosea ni bahadi mbaya
kwa kutokea hayo yaliyo tokea.Lakini ni vema wewe mtumishi kiongozi ama mkristo
ni vema kuomba msamaha unapokosea.
Hitimisho
Ni
dhahiri kusamehe ni jambo gumu lakinki ni muhimu hasa kwako wewe
uliyekosewa.Ikiwa ni mzazi,mpenzi,ra
Fiki,ndugu,jirani,mfanyakazi
wako,mtumishi wako,mwa
Jiri
wako,mme ama mke wako amekukosea ni vema kumsamehe kutakufungulia ukurasa
mwingine mpya.Kwa njia hii utafanya maisha yako kuwa yenye tija amani na furaha
zaidi. 1Timotheo 2:1-7,Wafilipi 4:4-7
Tutaendelea kutoa mengi katika neno hii Msamaha.
Kimeandikwa na
Bishop.Rhobinson
S.baiye
Rhobinsons.blogspot.com
Whatsapp. 0764127531
Mwanza
Tanzania.Mkolani.
No comments:
Post a Comment