Monday, June 1, 2020

UPENDO WA KUJIPENDA MWENYEWE


   JIPENDE MWENYEWE KWANZA

Moyo - Wikipedia, kamusi elezo huru

 

 
 Upendo wa kujipenda mwenyewe

Naomba ufahamu kwamba kitabu hiki kimehusika na aina Ya upendo wa kujipenda mwenyewe. Kwa maana kuna aina Tano za upendo haijalishi wengi hufundisha na kuaminisha watu kwamba kuna aina nne za upendo,huku wakiacha upendo wa kujipenda wewe mwenyewe.Maandoko matakatifu yanasema mpende jirani yako kama nafsi yako.Ikimaanisha kwamba mtu hujipenda au mtu upenda nafsi yake.Mathayo 22:39.

Tano Za Upendo Aina

  • Upendo wa ki-Mungu /Agape.God love
  • Upendo wa kirafiki / Phileo. Friend love
  • Upendo wa kindugu / Storge. Familiy love
  • Upendo wa kimapenzi mahaba. Romantic love.
  • Upendo wa kujipenda mwenyewa.Personal love.

upendo wakujipenda mwenyewe.

Aina hii ya upendo wa kujipenda mwenyewe ni Upendo ambao binadamu anakua nao kwa kujijali na kujipa thamani  yeye mwenyewe, pamoja na mapungufu yote yale aliyonayo.Huwezi kukuta hata siku moja mtu anajijukia mwenyewe.Aina hii ya Upendo huzaa kitu kinachoitwa ubinafsi.Pamoja na Biblia kusema Mpende jirani yako kama nafsi yako.Biblia inaturuhu tupende nafsi zetu.Na ndio sababu mtu akijitoa uhai kwa kujinyonga au kujimaliza kwa chuma cha mcha kali au kwa sumu na kwa njia ye yote ile ni mtenda Dhambi.

Umuhimu Wa Kujipenda Mwanyewe.

Unapofanikiwa kujipenda mwenyewe unakuwa umejipa nafasi kubwa sana ya kutambua thamani yako na uwezo wako ambao umebarikiwa na Mungu kuwa nao.Na kwa maana hiyo basi hata unaweza kufanya mambo yako kwa kujiamini kabisa,bila ya kutetereshwa na mtu yeyote yule.Lakini pia utakuwa na uwezo wa kukaa peke yako na hakuna kitu ambacho  kitakacho kosekana. Hayo yote ni kwa sababu tayari umeshajipenda mwenyewe unajithamini na kujijali pia.Watu wengi huwa wanashindwa kujipenda wao wenyewe na wakati huo huo wanasema kwamba Kuna watu ambao wanaowapenda.Ukweli ni kwamba huwezi kumpenda Mtu mwingine ikiwa wewe mwenyewe umeshindwa kujipenda vile ambavyo unatakiwa kujipenda.Siku zote ukijipenda mwenyewe basi kila kitu kwako kitaenda vile ambavyo kinatakiwa kiende na lazima utafurahia maisha yako na nchi yako upewayo na Bwana Mungu wako.

Ukijipena wewe mwenyewe kuna baadhi ya vitu ambavyo vinaitajika kujifanyia mwenyewe badala ya kusubiri mtu mweingine aje akufanyie.Ukikaa na kusubiri mtu  unayempenda akufanyie, nina uhakika kabisa kuwa inawekana,ukasubiri milele na vitu hivyo visitokee.Kwa hiyo basi ukijipenda wewe mwenyewe utaweza kufanya  vitu kama unavyotaka.

Mambo Ya Kudhingatia Unapofanya Maamuzi.

Unapo jipenda mwenyewe kuna mambo ambayo unatakiwa kuyadhingatia ili maisha yako yaende sawa.

 a.Kuwa huru kufanya mambo yako mwenyewe.

 b.Jipatie vile ambavyo unavihitaji bila kusubiri kuja kupewa au kufanyiwa na mtu mwingine.

 c.Tambua udhaifu wako na nguvu zako,wakati huo huo ukitumia vizuri nguvu zako huku ukijitahidi kuweka sawa unadhifu wako.

d.Jiamini katika kufanya kazi kwa kile ambacho unakuwa unakihitaji.

 e.Jua na kufahamu kwamba wewe mwenyewe unatosha kwa jinsi ulivyo.

g.Kuwa mtu wa kujifariji na kujitia moyo pale ambapo utakuwa umekosea na kufanya mambo yako yawe rahisi.

Bila shaka hayo mambo yaliyotajwa hapo juu ya nakupa tunaini kubwa la kuweza kujipenda mwenyewe,kwani kila kitu kitaenda katika mstari wako na hiyo ni habari njema kwa kila mtu.

Kujipenda Mwenyewe Hakuna Gharama.

Kujipenda mwenyewe hakuna gharama yoyote ile zaidi ya wewe mwenyewe kujitambua na kujua ni nini ambacho unakitaka katika maisha yako.Unaweza ukajiuliza nitawezaje kujipenda Mimi mwenyewe?.Tazama hapa chini imeandaliwa njia kadhaa ambazo zitasaidia katika safari yako ya kuanza kujipenda wewe mwenyewe na utazifurahia bila shaka kwani zitakusaidia sana katika kuyaendesha maisha yako na ya wengine.Mtu asipojipenda yeye wenyewe hawazi kumpenda mtu mwingine,nikama mtu hasipo jihurumia hawezi kumuhurumia mtu mwingine.

Mambo Ya Kufanya Unapo Jipenda Mwenyewe

1:Jiongeleshe Mwenyewe Kama Vile Unaongea na Mtu Ambaye Unampenda na kumjali.

 2:Jione Mwenyewe katika Macho Ya Yule Anayekupenda.

 3:Kama kuna Kitu hukipendi Kutoka Kwako Mwanyewe basi huna budi kukibadilisha.

 4:Jihudumie vizuri mwenyewe.

 5:Jisikilize Wewe Mwenyewe

 6:Jiulize ni vitu gani unavihitaji wewe mwenyewe.

1.Ongea Wewe Mwenyewe Kama Unaongea Na Mtu.

Mara nyingi tunapoongea na watu ambao tunawapenda na kuwajali huwa tunatunia sauti tamu yenye upole ndani yake bila kusahau maneno ya busara na yaliyojaa ustaarabu ya kutosha ili tu waweze kutuelewa na waweze kutambua kuwa tunawajali na kuwapenda.Vivyo hivyo kwako mwenyewe unatakiwa uongee ndani ya kichwa chako kwa sauti tamu yenye upole huku ukiwa na maneno ya busara hakika na kwambia utajisikia vizuri sana na utaona ni jinsi gani una upendo wako mwenyewe na ujitaidi mara njingi kuonea  maneno yenye kutia moyo na faraja moyo wako.Epuka kuongea maneno mabaya ya kukukatisha tamaa na kukifanya kujiona mnyonge katika jamii.

2.Jione Mwenyewe Katika Macho Ya Yule.

Mfikirie mtu yeyote anayekupenda anaweza kuwa mtoto wako,mchumba,mama,baba,dada,mtu yeyote anayekupenda muone kama kasimama mbele yako anakuangalia,jiulize(a)anaona nini kwako.(b)Akiambiwa akuelezee wewe ni mtu wa namna gani atakuelezaje.(c)Kwa nini anakupenda?(d)Ni kitu gani anajivunia kutoka kwako?.Ukifanya zoezi litakusaidia sana kutambua ni jinsi gani unapendwa kwa kuwa maswali hayo ukijiuliza lazima majibu yake yata kuwa mazuri ambayo moja kwa moja yatakushawishi wewe mwenyewe kujipenda badala ya kujichukia.penda nafsi yako kwanza.

3:Kama Kuna Kitu Hukipendi Kutoka Kwako.

Kama kuna kitu ambacho hukipendi kutoka kwa mtu mwingine ambaye ni wakaribu yako bila shaka,utajitahidi kadiri ya uwezo wako ili mtu yule Kibadilishe,vivyo hivyo kama kuna kitu ambacho hukipendi kutoka kwako huna budi kukibadilisha kwani kikiendelea kuwepo kinaweza kuyaharidu maisha yako.Mara nyingi vitu vingi ambavyo huwa hatuvipendi kutoka kwetu wenyewe huwa vinatokana na malezi ambayo tumekulia kwa mnda mrufu,kwa hiyo kuna vijitabia ambavyo unakuta sio vizuri na huwa hatuvipendi.Basi ukishatambua kuwa kuna kitu ambacho hukipendi kutoka kwako hanza kukibadili kitu hicho kwa maana hakuna kitu ambacho kinashindikana chini ya jua hasa ukiwa umeamua kutoka moyoni kwamba kitu fulani lazima nikiache kwani hakifai katika maisha yangu.

Jihudumie  Vizuri Wewe Mwenewe.

Watu wengi huwa tunajua kuwapa zawadi watu tunaowajali na kuwapenda na katika orodha  ya kuwapatia zawadi huwa tunasahau kujiweka na sisi wenyewe.Tunachohitaji ni wengine kuwa na furaha huku Sisi tukiwa nyuma na wanyonge.

Yabadili maisha yako sasa kwa kuweza kujipendelea wewe mwenyewe kwenye ile orodha ya watu wanaostahili kupata zawadi kutoka kwako mwenyewe halafu ya wengine yafuate.Unapojipa zawadi mwenyewe unajipa nafasi kubwa ya kujipenda na kuona kabisa kuwa unastahili vitu vizuri katika maisha yako na usisite kujipongeza kwa zawadi uliyojipatia.

5.Jisikilize Wewe Mwenyewe.

Mara nyingi tunapenda kusikiliza mawazo ya watu wengine huku tukiwa hatujipi na fasi nzuru ya kusikiliza mawazo yetu ambayo kwa kiasi kikubwa yanaweza kutusaidia sana katika maisha yetu.Ukiwa na tabia ya kujisikiliza wewe mwenyewe,nakuakikishia kwamba kila kitu lazima kitaenda sawa.Lakini wakati ukiwa unajisikiliza wewe mwenyewe haimaanishi kuwa mawazo ya watu wengine hayana nafasi,lakini pia mawazo ya watu wengine yawe na nafasi pia.kwa hiyo jijengee mahusiano mazuri wewe mwenyewe kwa kujisikiliza  wewe mwenyewe huku ukiendelea kujipenda wewe mwenyewe.

6.Jiulize Ni Vitu Gani Unahitaji Wewe Mwenyewe.

Jiulize ni vitu gani unahitaji kwa kujiuliza mwaswali haya.

a.Je nahitaji nini kwa sasa?

b.Je nahitaji muda wa kukaa peke yangu?

c.Je nahitaji kurahisisha maisha?

d.Je nahitaji muda wa kucheza na kufurahia maisha?

e.Je nahitaji kwenda sehemu yoyote?

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo unaweza kujiuliza wewe mwenyewe katika harakati za kujipenda zaidi na zaidi wewe mwenyewe.Bila shaka au mashaka akitokea mtu akikutatulia maswali yako hayo hakuna utakachokifanya zaidi ya kumpenda sana mtu huyo.Itakuwa vyema maswali ukiyatafutia ufumbuzi wewe mwenyewe ili ujipe nafasi ya kujipenda.Kukifanikiwa kujipenda utaona maisha yako yanavyobadikika na wala hautajuta katika maamuzi yako ya kujipenda wewe mwenyewe kwanza,halafu wengine wafuate ni uamuzi mzuri utakuwa umejitendea haki.

Kuipenda Nafsi Yako Kuna Maanisha Nini?

Kumbuka kwamba tumekwisha kufahamu maana ya kupenda,mwanzoni mwakitabu hiki.Kimetuambia kwamba,watu wengi wametoa maana tofautitofauti za upendo.Sasa fahumu kwamba wanatoa maana ya upendo kutokana na aina za upendo.Jambo ambalo sio sahii.Kumbuka maana ya upendo halisi ni kumbatio,maanuzi,aminio,adhimio,kukubali,kuridhia,atamio la moyo nafsi na akili.Na ili kufahamu kuipenda nafsi yako kunamaanisha nini endelea kusoma hapo chini.

Kuipenda Nafsi Yako Kwa Afya Ya Roho.

Ili kufamu kuipenda nadsi yako,Kumbuka kwamba ni tamko la maandiko matakatifu yaani Blblia takatifu.Kumbuka Mungu aliumba mtu akiwa  nafsi hai. Mwa 2:7. Zab 66:9. Bwana wetu Yesu Kristo alisema kwamba  Luk 17:33,Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake,ataiangamiza;na ye yote atakayeiangamiza ataiponya.Math 16:25-26, kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake,ataipoteza,na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.Kwanza atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote,na kupata hasara ya nafsi yake?Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?. Katika maandiko hayo mawili kuna mambo muhimu ya kutafakari sana.Moja kuangamiza nafsi.Mbili kuiponya natsi.Tatu kuipoteza nafsi.Nne, kuiona nafsi.Kupoteza nafsi hapa linamaanisha kwamba,kukosekana na kutojulikana na kutojali mambo ya ulimengu,kwa hiyo katika mambo ya mwili tumwe wafu.Kut 20 :13-17.Usiuwe,Usizini,Usiibe,usishudie uongo,Usitamani.Gal 5:19-21.Basi matendo ya mwili nidhahiri,ndiyo haya,uasherati,uchafu,ufisadi,ibada ya sanamu,uchawi,uadui,ugomvi,wivu,hasira,fitina,faraka,uzushi,husuda,ulevi,ulafi,na Mambo yanayofanana na hayo,katika hayo aawaambia,mapema,kama nilivyokwisha kuwaambia,ya kwamba watu watendao Mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.1Yoh 2:15-17. Msipende dunia,wala mambo yaliyomo katika dunia.Mtu akiipend dunia,kumpenda baba hakumo ndani yake.Maana kila kilichomo duniani,yaani,tamaa ya mwili,na tamaa ya macho,na kiburi cha uzima,havitokani na Baba,bali na vyatokana na dunia.Na dunia inapita,pamoja na tamaa zake,bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.Gal 5:22-24.Lakini tunda la Roho ni upendo,furaha,amani,uvumilifu,utu wema,fadhili,uaminifu,upole,kiasi,juu ya Mambo kama hayo hakuna sheria.Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake

.Ukimpenda Mungu utaipenda nafsi yako ambaye ndiye chanzo cha nafsi yako.Ukimpenda Mungu utangamiza nafsi yako,na mambo ya dunia hayatakuwa tena na mvuto kwako.Imeandikwa katika 1Yoh 2:15-17,huwezi kufurahia anasa za ulimwengu na kuwa rafiki wa Mungu.Imeandikwa katika Yak 4:4. Je ni mambogani mabaya?Imeandikwa  Gal 5:19-21.Usifuate mambo yanayopendwa na dunia yasiyo mema.Imeandikwa katika  Rum 12:2. Kumjua Yesu Kristo kunakata tamaa za ulimwengu.Imeandikwa katika Gal 6:14.Epuka elimu za dunia.Imeandikwa katika Kol 2:8.Ishi kama makao yako yako mbinguni.Imeandikwa kataka 1Pet 2:11.

Ifungue Nafsi Yako Katika Kifungo Cha Nafsi.

Mwanadamu ana sehemu kuu tatu ambazo ni,mwili,nafsi na roho.Kazi ya nafsi ni kuunganisha mwili na roho.Biblia inaongelea kuhusu uumbaji uliofanywa na Mungu kama ilivyoandikwa.Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,akampulizia puani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai.Ndiyo maana kila mwanadamu alifinyangwa kutoka kwenye mavumbi ya ardhi,na kitendo cha Mungu kumpulizia pumzi huyu mwandamu,maana yake Mungu aliweka Roho.Mtu akawa nafsi hai na hivyo Biblia haisemi kwamba mtu akawa roho hai bali nafsi hai.Maana yake kama nafsi iliwekwa ndani ya mtu vivyo hivyo nafsi yaweza kuondolewa na mtu kufa.Kuna mtu wa mbinguni na kuna  mtu wa duniani.Ndivyo ilivyoandikwa,Mtu wa kwanza,Adamu,akawa nafsi iliyo hai;Adamu wa mwisho ni Roho yenye kuhuisha. 1Kor 15:45-47.   Maana yake mbinguni hakutoki udongo,bali roho.Mtu wa kwanza udongo mtu wa pili ni roho.Zab 14:7,Uitoe nafsi yangu kifungoni.Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki wata nuzunguka.Kwa kuwa wewe unanikirimu.Nafsi inaweza kuwekwa kifungoni.Fahamu kwamba ndani ya nafsi ndiko kunakowekezwa aina zote  za elimu na imani na ujuzi.Daudi alijua kwamba nafsi yake ilikuwa salama,na kama nafsi iko salama mambo yote yatakuwa salama.Na ukimwona mtu ye yote hajisikii raha akiwa ndani ya Kristo,ujue tayari nafsi yake mtu huyo ipo kifungoni.Hesabu 30:10-13,Ayubu 33:18,22,28.Zab 35:7. Mith 3:4-5:( Zab 86:13)(Mith 23:13-14( Luk 9:23-24)Yoh 12:25,Gal 2:20,Rum 12:2(1Sam 2:30-35)Moyoni mwangu nimeliweka neno lako. Zab 119:11,Kut 15:19,123:4

 

Bishpo Rhobinson S.Baiye

rhobinsons.blogspot.com

Whatsapp:0764127531

 rhobinsonsaleh1@gmail.com

Mwanza Tanzania

 

 

 


No comments:

Post a Comment

UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...