Tuesday, June 2, 2020

UPENDO WA KIMAPENZI MAHABA

UPENDO WA KIMAPENZI MAHABA.

Kumbuka kwamba kuna aina tano za upendo.Lakini katika kitabu hiki tutatafakari kuhusu upendo wa kimapenzi mahaba.

1.Upendo wa Ki-Mungu.

2.Upendo wa Kirafiki.

3.Upendo wa Kindugu.

4.Upendo wa Kimapenzi Mahaba

5.Upendo wa Kujipenda Mwanyewe. 

Maana Ya Upendo Wa Kimapenzi Mahaba.

Upendo wa kimapenzi au kimahaba unaokuwa kati ya watu fulani kusababisha watu hao kuwa na uhusiano  wa kimapenzi(mahaba)kati yao.yaani watu wawili mtu mme na mtu mke.Tunaona neno la Mungu katika kitabu chake maalumu kinachohusu mahaba ya wapenzi wa wili.kitabu cho wimbo ulio bora.Mapenzi na neno la Kiswahili linalojumlisha idadi kadhaa ya hisia,kuanzia mahaba,pendo hata upendo wa ki-Mungu.Ni kwamba kitenzi kupenda kinaweza kurejerea aina,za hisia hali za mitazamo tofautitofauti,kuanzia ridhaa ya jumla ya kitu(Napenda kula hiki)maamuzi kati ya watu wawili na kumbatio,kubalifu,zingatio,atamio la moyo na nafsi na akili.Kwa utaratibu wa Mungu na jamii  zilizo sawa sawa”Eros ni aina ya upendo unaotakiwa kuwa kati ya watu wenye uhusiano wa ki-ndoa,yaani mtu mme na mtu mke. Aina zote za upendo zinahusisha moyo nafsi na akili,lakini Eros huwa na sifa ya kuwa na hisia zenye nguvu zaidi kutoka moyoni kuliko aina zingine zote za upendo.Eros ni aina ya upendo wenye nguvu kali sana ya hisia za binadamu.Tunaona neno la Mungu katika kitabu maalumu kinachohusu mahaba ya wapenzi wawili.Kitabu kiitwacho Wimbo Ulio Bora. 8:6,Neno la Mungu linasema kwamba upendo Eros una nguvu sana kama mauti.Nguvu hiyo ya upendo huunganisha nafsi,fikra,hisia na maamuzi yao kwa sababu ni upendo uliolenga kujenga nendoa Nzuri na familia Bora kabisa.

Mifano Ya Upendo Wa Kimapezi.

1:UpendowaYakoboKwaRaeli.Mw29:10-30.

Yakobo alipomkimbia kaka yake Esau,alikimbilia nchi ya mbali,nchi ya mama yake kwa mjomba wake Labani.Labani alikuwa na binti wawili,mkubwa aliitwa Lea na mdogo aliitwa Raheli.Neno la Mungu Biblia inasema Lea alikuwa na macho mazito,yaani ukimwangalia,utadhani amelala,kumbe ndio anakuona.Na Raheli alikuwa na umbo zuri la mwili na sura nzuri ya usoni.Biblia inasema Kwamba,Yakobo alimpenda Raheli.  Mw 29:16-20. Labani alimwambia Yakobo akachunge wanyama wake kwa mnda tena wa miaka saba nyingine kama mahari,ndipo atampa Raheli kuwa mke wake.Yakobo alipendezwa na hilo,na alikubali kutumika na kuchapa kazi kama kawaida yake ya uchapaji kazi.Kwa jinsi Yakobo alivyompenda Rahali kwa upendo wa Eros,Yakobo alikamatwa kimapenzi kuwa mke wake alichapa kazi Sana Na kwa bidii kiasi kwamba,ile miaka saba ilionekana michache sana.Hiyo ni nguvu ya upendo Eros.Yakobo alimtwaa katika upendo Eros kwa Raheli na ilikuwa kali sana.Upendo Eros ina uwezo wa kufanya mtu asione ugumu wa kazi,asione machungu,asione umbali wa mwendo,asione ukali wa jua,asione aibu wala woga mbele za watu wengine.Eros ina nguvu sana juu ya mtu mwenyewe hata kutawala utu wake wote.Eros ina nguvu ya fikra,hata kutawala mawazo ya mtu,Eros ina nguvu ya hisia,hata kutawala kuhisi kujisikia kwa mtu,Eros ina nguvu ya Maamuzi,hata kutawala matendo ya mtu kabisa.Unaweza ukamkuta kijana siku hizi ni msafi sana kuliko unavyomfahamu,kumbe amekwisha kamatwa na binti mwanamwali kama Yakobo alivyokamatwa na Raheli.Yakobo alijaa Raheli katika mawazo yake,kila saa alikwa akimuwaza Raheli kwa mnda mrefu.Yakobo alijaa Raheli katika hisia zake kiasi cha kutosikia machungu ya ile kazi na hata kuona miaka saba kuwa si kitu kikubwa,Yakobo alijaa Raheli kataka Maamuzi yake,hata kumfanya afanye kazi kwa nguvu kama roboti ili tu kumpata Raheli.Raheli ndiyekuwa nguvu na hamasa ya Yakobo kudamka alfajiri na mapema kwenda kulisha mifugo ya mjomba wake Labani.Upendo Eros una nguvu kama mauti.Upendo wa kimapenzi huwa kati ya watu wawili wanaoelekea katika uhusiano wa kudumu wa kuwa mme na mke.Hahukuw mpango wa Mungu kwamba upendo huo wa kimapenzi kuwa wa kujiribu na kuacha,kwa sababu eros ni upendo wenye nguvu sana ya hisia,hivyo huathiri sana moyo, ufahamu, hisia za mtu pengine hata afya ya mwili wa mtu kabisa kama hatajua kuutawala ipasavyo.Hivyo eros si upendo wa kuingia na kutoka utakavyo,kama mtu abadilishaye nguo.

2: Upendo wa Isaka kwa mkewe Rebeka.Mw 26:1-12.

Isaka alikuwa akiishi kataka nchi ya Wafilisti.Watu wale wakamwona Rebeka,wakavutiwa na uzuri wake,hata wakamtamani.Wakamuuliza Isaka,ee bwana huyu msichana tunayemwona katika boma lako na wakati mwingine unaambatana naye,ni nani kwako?.Isaka aliogopa kusema ni mke wake,kwa maana wange muua Isaka ili wamchukue Rebeka,kwa ajili alivyokuwa mzuri  wa kuvutia.Isaka aliwaambia kwamba ni dada yake nao waka mwacha.Lakini kumbe wale watu walitumwa na mfalme wa Wafilisti,ili kumpeleleza na kujua uhusiano wao, kwasababu mfalme alivutiwa sana na uzuri wa Rebeka,akataka kumuoa.Na hata siku moja mfalme Abimeleki alipokuwa akipita mtaani,akakatiza mtaa ambao nyumba ya Isaka ilikuwepo.Mfalme Abimeleki akachungulia dirishani,akamwona Isaka akichezacbeza na Rebeka mkewe”kimahaba,mfalme Abimeleki akamwita Isaka,akamwambia,kwa jinsi nilivyowaona mkichezeana vile lazima huyu ni mkeo,huwezi kucheza-cheza vile na dada yako,mbona uliniambia kwamba huyu ni ndugu yako?.Isaka akajibu niliogopa nisije nikauwawa kwa ajili yake.Basi Abimeleki akamlaumu Isaka,kwa kusema,mtu mmoja wetu angelala na Rebeka bila kufiliri ni mkeo kwasababu ulisema mwenyewe ni dada yako.Ndipo mfalme akaamuru watu wote wasimguse Isaka wala mkewe,akasema amgusaye mtu huyu au mkewe lazima atauawa.

Ifahamike kwamba tuingipo katika mahusiano ya kimapenzi ndoa tuwe tume fanya maagano na Mioyo na nafsi na akili zetu.

Dalili Na Sifa Za Upendowa Kimapenzi.

RomanticLove

1.Mvuto kwa haiba yake na kuchukuliana nayo(Mwonekano  na Tabia)

2.Kukaa mawazoni kwa mtu anayependa kujaa moyoni.

3.Shauku kubwa ya kuishi pamoja kila wakati.(Kuambatana)

4.Heshima kubwa kwa mtu anayependwa.(Kipaumbele.

5.Kumjali na kumtanguliza mtu 'apendwaye.

6.Zawadi na gharama kwa mtu apendwaye.Kujitoa.

7.Furaha na Amani kutawala moyoni.

Kumpata Mwenzi Wako Wa Ndoa.

Mith 19:14-21.

a.Mweleze Mungu Haja Zako.

b.Mwombe Mungu Akukutanishe Na Mwenzi Wako.

c.Tengeneza Marafiki.

d.Thibitishia Moyo Wako Kwamba Umependa Kweli Kweli.

e.Ishasha Za Kutambua Penzi La Kweli.

f.Omba Ushauri Kwa Watu.

g.Mwendee Na Useme Naye Kwa Hekina.

h.Thibitisha Uhusiano Wako.

a:Mweleze Mungu Vizuri Zile Haja Za Moyo Wako.

Mungu ameahidi kuwa atakupa mtu w kufanana na wewe. Mw 2:18. Kwa hiyo ni muhimu sana ujijue wewe ukoje,kisha ndipo utaweza kumweleza Mungu na kumwomba  akupe mtu wa haja ya moyo wako.Hivyo ni muhimu sana kujijua kujitambua na kujielewa kwa jinsi uluvyo na ni aina gani ya watu ambao wewe unaendana nao.Hii ni kwa sababu watu tuko tofauti.Unaweza kuishi na mtu yo yote duniani,lakini hutaweza kuishi vizuri na kila mtu.Maisha mazuri yanakuja kwa kukutana na mtu ambaye mnaelewana na mnaendana.Ndio maana Mungu alisema kuhusu Adamu kwamba,mwenzi wake wa maisha atafanana naye.Usimfiche Mungu haja za moyo wako.Kumbuka yeye ni baba yetu na sisi tu watoto wakewapenzi.Fahamu kwamba Mungu anaheshimu sana,haja za moyo wako ambazo zitakupa wewe furaha ya Maisha. Math 7:7-11,Zab 145:17-18,Isaya 45:11,1Kor 7:39.Maombi yako ya bidii yatampa Mungu kumchonga,kumwanda.Kila kitu uubwa na kuandaliwa mapema na Mungu.Maombi ya mwenye haki  yafaha sana mtu akiomba kwa bidii . Yak 4:16,Kol 4:2.

b:Mwombe Mungu Akuonyeshe  Na Akukutanishe

Na akukutanishe na mwenzi wako.

Kila mmoja wetu ambaye Mungu amempangia kuwa na mwenzi,ana mwenzi huyo mahali fulani hapa duniani.Lamsingi ni kufanya Maombi kuomba Mungu kumfinyanga na kumchonga huyo mwenzi wako popote alipo.La pili inahusu kumwomba Mungu kusababisha mazingira ambayo yatawakutanisha na kutambuana baada ya kupata ufahamu wa Mungu ya kwamba ndiye.Hiyo ndiyo maana halisi ya kufunuliwa au kuonyeshwa.Zab 32:8,Isaya 43:26,45:11,Efe 1:15-19.

c:Tengeneza Marafiki Wa Kweli.

Watu wengi humwomba Mungu kwa uaminifu sana ili wapate wenzi wa maisha.La kini wanafanya makosa makubwa ya kujifungia katika kisiwa cha upekee.Ni ngumu sana kuonekana na kujulikana tabia na utu wako wa ndani kama hutachangamana na jumuiya za fahumu kwamba Mungu ndiye chanzo cha urafiki.Hata Yesu Kristo alikuwa na marafiki wa kiume na wa like pia. Yoh 11:5.Jitaidi kufanya marafiki mbalimbali ila mwombe Mungu akupe marafiki wazuri.kwa kuelewa vizuri kuhusu marafiki soma mada na kipengele,kinachozungumzia aina ya upendo wa kirafika katika sura hii ya kwanza katika kitabu hiki.

d.Thibitasha Moyo Wako Kwamba Unampenda

kweli.

Kadri unavyoendelea na maisha ya uaminifu katika wokovu,maombi  na kujifunza neno la Mungu na kumtumikia Mungu kwa namna mbalimbali,Mungu atasababisha ukutane na mtu anayefanana sana na haja za moyo wako kuhusu mwenzi wa maisha.Utahitaji usikivu mkubwa wa rohoni kutambua aina gani ya upendo unaingia moyoni mwako kuelekea kwake kwa sababu kuana aina tano za upendo.Upendo wa ki-Mungu,upendo wa kindugu,upendo wa kirafiki,upendo wa kimapenzi, upendo wa kijipenda mwenyewe. Muh 9:8-9. Kati ya watu unaofahamiana nao,yupo mmoja ambaye atakuwa watofauti sana ndani yako.Mungu atampa kuonekana watofauti sana kuliko wengine wote wanaokuzunguka.Hivyo kabla ya kwenda kusema naye na kumshirikisha uonavyo wewe moyoni mwako,thibitisha kimaombi tena na tena kwamba ndimi yako Kuna upendo wa kweli kwa ajili yake.Marko 5:25:34(30). Inasema wangi walimgusa Yesu lakini mmoja tu ambaye atakuwa na mguso qa tofauti katika moyo wako.

 e:Ishara Za Kutambua Upendo Wa Penzi La Kweli.

1.Mtu huyo atakamata umakini wako na atakuvutia.

2.Mtu huyo atajaa katika mawazo yako kuliko kawaida na wengine.

3.Utatamani sana uwepo wake mtu huyo katika wote kuwa naye.

4.Utapenda kuwasiliana na mtu huyo mara kwa mara kuliko wote.

5.Utakuwa na moyo wa kujali,wema zaidi na kujitoa sana kwake.

6.Utakuwa na heshima ya hali ya juu sana adabu utii uaminifu kwake.

7.Tatakuwa na maneno mazuri maneno laini,maneno ya upendo kwake.

8.Utakuwa na moyo uwezo wa kumvumilia au kumchukuliana naye vile alivyo.

9.Utakuwa na hamu ya kumgusa kumshika kwa upendo wala sio tamaa.

10.Utakuwa na moyo na utayari wa kumlinda na kumhifadhi.

11.Upendo wenu utapendeza mbele ya watu wengi si lazima wote.

12.Utakuwa na amani na furaha ya hali ya juu moyoni mwako.1Kor 13:4-8.

f.Omba Ushauri Kwa Watu.

2Kor 13:1,Zab 73:24, Mith 15:22.

Ushauri kutoka kwa watu werivu walionahufu ya Mungu ndani yao,na wanao wajua na kuwafahamu vyema ninyi wawili utakuthibitishia kwamba ulichosikia  moyoni juu ya mtu huyo Ni sahihi.Wakati mwinginse si wakati wote watu wa pembeni huwa na uwezo wa kuona mbali zaidi.Wanaweza kuona vitu ambavyo ninyi mlio ndani ya urafiki hamuoni bado.Washauri wanaweza kutumiwa na Mungu kuthibitisha mawazo uliyo nayo na mipango uliyonayo.Ushauri wa watu unaweza kusaidia kufanya maamuzi magumu muhimu.Math 18:16,1Tim 5:19,Ebr 10:28. Mwombe Mungu akuongoze kwa watu wazuri wenyehofu ya Mungu ndani yao wenye hekima watakao washauri.Lakini la muhimu liko kwako wewe kuliko watu wote.Washauri watabaki kuwa washauri wala wasiwe waamuzi,wewe ndiwe uwe mwamuzi wa mwisho.Ni vizuri kupima ushauri wote unaopewa kwa maombi na kwa uongozi wa Mungu.Wakati mwingine Mungu anaweza kukuongoza kitu ambacho hakuna mtu mwingine anachokiona ukionavyo wewe.Neno la Mungu linasema kwamba amani ya Kristo itakusaidia kufanya maamuzi.Kol 3:15,Isaya 55:12.

g.Mwendee Na Usemenaye Kwa Hekima.

Wimbo ulio Bora 3:1-4.

Baada ya maombi ya subira,Mungu akuongoze kusema naye kwa wakati utakaoongozwa na Mungu.Uwe jasiri na muazi.Useni wako uwe wa kawaida usichague maneno magumu wala misamiati wala mafumbo.Uwe wazi na wa  kawaida sana.Usiyatumie maneno ya kiroho saaaaaana,ili kumtisha usitumie maneno kama  Mungu ameniambia au Mungu amesema Bwana wa majeshi,maneno kama haya yanamfunga mtu kusema ndiyo”kwa maana atashituswa nayo na kuogopa lakini kama ni mtu jasiri na hajakupenda hajakukubali,mtapambana.Huo sasa  si mwelekeo mzuri.Kijana mmoja alipomfikia mt u ambaye moyo wake wa tamaa ulimwishi na alimwendea akaanza kuporomsha maneno makali mfano anazungushia mlima wa moto,hutaolewa na mtu mwingine ila mimi,na ukinikataa,Bwana atakutapika.Hii si hekima ya Mungu.Mungu harumii nguvu,ikiwa kwenda mbinguni Mungu halazimishi watu je itakuwa ndoa?Wewe ukishasema maneno rahisi, mfano nimeomba kwa muda,na hivi ndivyo ninavyosikia moyoni mwangu kwamba,nakupenda sana,na ikiwa itampendeza Mungu na wewe pia,basi na uwe mwenzi wangu wa maisha.Ukisha mwambia maneno hayo rahisi  au yanayofanana na hayo,amini kwamba kama ni mpango wa Mungu muwe wote pamoja maishani,maombi yako na neema ya Mungu vitamsaidia kufanya uamuzi mzuri kwa ajili yenu wawili.Unaweza kupata jibu la ndiyo au hapana au subiri.Mtu wa Mungu huongozwa na Mungu, halazimishi ovyo kwa kitu kama hiki.Maana yangu ni kwamba,hauhitaji kutumia nguvu za mwili wala akili kuwaza sana.Baada ya kuongea na kutua mzigo wako kwake,pumzika na umwachie Mungu kumalizia kazi.

h.Thibitisha Uhusiano Wako,Wenu.

Wimbo ulio Bora 3:4.

Baada ya kuliongea na kulitafakari pamoja kwa muda mtakaoona unatosha au unafaa,ni muhimu.Sasa mpelekane mbele katika mamlaka zenu za kifamilia na kikanisa.Uhusiano mzuri usiwe wa mafichoni.Tunaona huyu mpenzi katika kitabu cha Wimbo anasema,anataka kumtafuta mpenzi wake,amshike mkono,wapelekane kwa wazazi.Huo ndio utaratibu mzuri kibiblia.Familia na kanisa watawasaidia kufuata taratibu za kiutamaduni na kiroho ili mhalalishwe kuwa mume na mke.Ndipo ndugu na marafiki mtawashirikisha mipango yote ili kuandaa arusi yenu

 

Bishop:Rhobinson S.Baiye

rhobinsons.blogspot.com

rhobinsonsaleh1@gmail.com

Whatsapp.0764127531

Mwanza Tanzania

 

 

 

 

 

 


No comments:

Post a Comment

UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...