FUNGAMANISHWA NA MADHABAHU
YA
KWELI.
Kutii Agano Au Maagano
Ndugu msomaji ukiwa Baba yangu,Mama yangu,Kaka yangu,Dada
yangu,Rafiki yangu,aidha mmojawapo katika ukoo,na katika jamii,naamini bado
hujapoteza mwelekeo.Bado tunayaona mambo Au vitu ili tuyafahamu na kuyajua
mambo au vitu ambavyo vya weza kutufungamanisha na kusababisha kuwa na
mahusiano na madhabahu ambayo yanamahusihano na roho wakweli.Katika kipengele
hiki tutaona jinsi Agano na Maagano,yanavyoweza kukufungamanisha na
madhabahu yenyemahusiano na roho
wakweli.
Agano Au Maagano Ni Nini?
Neno agano linatokana na neno la kiebrania Berith,lenye
maana ya mapatano,makubaliano au mkataba unaofanywa baina ya pande mbili.Mapatano
ni uwingi wa neno patano likiwa na maana ya (ulinganifu wa mawazo,au
mtazamo,maafikiano,agano)Neno,Makubaliano,lina maana ya (suluhu
baina ya watu wenye maoni au mitazamo tofauti)Neno (Mkataba)Neno
hili lina maana ya makubaliano baina ya watu au vikundi viwili au zaidi ili
kufanya jambo au kazi fulani).Maneno hayo matatu pamoja na maana ya maneno
hayo yote,ukiyajumlisha yanaunda neno agano.Tena neno hili Agano kwa Kiyunani
ni Diatheke, lenye maana ya urithi au Wosia.Kwa hiyo tena twaweza
kusema agano ni mapatano yanayounganisha watu wa pande mbili pamoja.
3.Mungu ni Mungu wa Maagano.
Fahamu Mungu wetu ni Mungu wa maagano kwakuwa anaweza kufanyaagano
au maagano na mtu mmoja.Ninamaanisha kwamba agano ni moja lakini maagano
nizaidi ya moja,kwa hiyo waweza kufanya Agano au maagano na mtu au na
Mungu.Kumbuka kwamba tunajaribu kuona jinsi mtu mwanadamu anavyoweza
kujifungamanisha na madhabahu ya kweli.Mungu kwa kuwa ni Mungu wa maagano
tutaona baadhi ya watumishi wake aliyofaya maagano nao.Mungu amefanya maagano
na watu wengi Tunaowasoma katika Biblia na ambao hawajatajwa katika bibla yaani
watu wa siku zetu,twaamini bado Mungu anaendelea kufanya maagano na watumishi
na watu wake,Ingawa wana Theolojia wanaamini Maagano makuu matano tu,na moja
kati ya hayo bado hawajakubaliana kwalo kuwa ni agano,bali waliowengi wanasema
hilo likuwa agizo.Lakini ningetamani ufahamu kwamba hatufu
ati wala hatuongozwi na wana theologia na hatuishï na kufundisha
imani na mitazamo na misimamo ya wana theologia,bali tunaishi kwakile ambacho
Mungu amekuamuru tukiishi na kukiamini na kutekeleza .Katika kipengele hiki tunaona
watumishi wa Mungu watano aliyofanya nao maagano.Fuata kama walivyoorodheshwa
hapo chini.
a.Agano la Mungu na Adamu.
b.Agano la Mungu na Nuhu.
c.Agano la Mungu na Abrahamu.
d.Agano la Mungu na Musa.
e.Agano la Daudi.
g.Agano la Mungu na Ulimwengu.Agano
Japya.
a.Agano la Mungu na Adamu.
Kama ambavyo tumeona hapo juu yakwamba katika Biblia Mungu wa
kweli ni Mungu wa maagano ya kwelina Maagano au agano la Mungu na mtu
mwanadamu,hujulikana na kufahamika kuwa ni agano au maagano katika namna mbili.1,Mungu
hujitokeza kwa mwanadamu mtu na kutamka
kwamba imefanya nitafanya ilifanya agano au maagano na wewe au nanyi.2,Mungu
hutoa husema na kutoa maelekezo moja kwa moja kama atakavyo na moja kwa moja
yata sima kuwa agano au maagano.Katika Agano au maagano ya Mungu na Adamu kuna
utata katika wanatheologia,baadhi huamini Mungu alifanya maagano na Adamu.Na
wengine husema hayapo au halipo agano la Mungu na Adamu.Lakini mimi nami
naamini nimejaa mafunuo ya roho wa Mungu;kwamba yalikuwepo Maagano kati ya
Mungu na Adamu.Agano la Mungu na Adamu linapatikana katika Mwanzo 1:26-30 Mungu akasema,na tufanye mtu kwa mfano wetu,
kwa sura yetu,wakatawale samaki wa baharini,na ndege wa angani,na wanyama,na
nchi yote pia,na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.Mungu aka umba
mtu kwa mfano wake kwa mfano wa Mungu alimwumba,mwanamume na
mwanamke,aliwaumba.Mungu akawaambia,Mungu akawaambia,Zaeni,mkaongezeke,mkaijaze
nchi,na kuitiisha,mkatawale samaki wa baharini,na ndege wa angani,na kila
kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.Mungu akasema,tazama,nimewapa
kila mche utoao mbengu,ulio juu ya mchi yote pia,na kila mti,ambao matunda yake
yana mbengu vitakuwa ndivyo chakula chuo.
Mw 3:15-16,nami nitaweka uadui kati yako
na huyo mwanamke,na kati ya uzao wako na wake,huo utakupota kichwa,na wewe utamponda
kisigino.Hili la kuweka uadui kati ya
uzao wa nyoka na uzao wa Wa mwanamke, ni agano la msingi sana.kwa kuwa ni agano
la wokuvu katika Yesu Kristo.Ni agano ambalo liwekwa kwa misingi
ya neema ya Mungu kwa Adamu,kwa kuwa mwanamke amekosa basi ataokolewa kupitia
uzao wake ambaye ni Yesu Kristo ambaye hana sifa za kuwa na baba wa mwili.1Tim 2:14-15,Wala Adamu hakudanganywa,ila
mwananke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.Walakini ataokolewa
kwa uzazi wake,kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso,pomja na moyo wa
kiasi.
b.Agano la Mungu na Nuhuna viumbe Hai.
Agano la Mungu na Nuhu halikuwa na masharti kati ya Mungu na
Nuhu(hasa)na binadamu kwa ujumla.Baada ya gharika,Mungu aliahidi mwanadamu kwamba hawezi kuihiribu tena dunia
kwa mafuriko Mungu alitoa upinde wa mvua kama ishara ya agano,ahadi ya kwamba
dunia nzima hakutakuwa tena mafuriko na ukumbusho kwamba Mungu anaweza na atahukumu
dhambi.Mw 9:8-17,Mungu akamwambia
Nuhu,na wanawe pamoja naye,akasema,Mimi,tazama,nathibitisha agano langu
nanyi,tena na uzao wenu baada yenu.tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja
nanyi,ndege na Mnyama wa kufugwa,na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja
nanyi,wote wanaotoka katika safina,hata kila kilicho hai katika mchi.Na agano
langu nitalithibitisha nanyi,wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji
ya gharika,wala hakutakuwa tena gharika,baada ya hayo,kuiharibu nchi.Mungu
akasema,Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yagngu nanyi,na kila kiumbe
hai kilichoko pamoja nanyi,kwa vizazi vyote hata milele,Mini nauweka
upinde wangu winguni,nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.Hata
itakuwa ikitanda mawingu juu ya nchi,upinde utaonekana winguni,nami nitalikumbuka
agano langu,lililoko kati yangu nanyi,na kila kiumbe hai katika wote wenye
mwili,wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye wili.Basi huo
upinde utakuwa winguni,nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano langu la
milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili
kichoko katika nchi.Mungu akamwambia Nuhu,Hii ndiyo ishara ya agano
nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi. 2Pet 2:5
c.Maagano ya Mungu na Abrahamu.
Maagano ya Mungu na Abrahamu,Mwa 12:1-3,6-7)13:14-17,)17:1-14)22:15-18.Katika agano
hili,Mungu aliahidi mambo mengi.Mw
12:2,kwamba Ibrahimu angekuwa na wazao wengi wa kimwili.( Mw 13:16)Kwamba Ibrahimu angekuwa
baba wa mataifa mengi.(Mw 17:4-5)Mungu
pia alifanya ahadi kuhusu taifa liliitwa Israeli.Kwa kweli,mipaka ya
kijiografia ya agano la Ibrahimu imewekwa zaidi ya mara moja katika kitabu cha
Mwanzo.(Mw 22:7,13:14-15.15:18-21)Mpango
na agano lingine ni kwamba kwa kupitia Ibrahimu mataifa yote yatabarikiwa.
Mw 12:3.22:18
d.Agano la Mungu na Musa.
Agano la Mungu na Msa ,Kumb 11.agano la Mungu na
Musa
lilikuwa agano la masharti ambalo lilisababisha baraka za Mungu
kuwa laana ya Mungu kwa uasi kwa taifa la Israeli.Sehemu ya agano la Musa na
Mungu Ilikuwa Amri kum 10)Kut 20:1- Napia sheria yote,ambayo
ilikuwa na amri zaidi ya 600-karibu 300,nzuri na 300,hasi.Vitabu vya historia
ya agano la kale(Yoshua na Esta)maelezo ya jinsi Israeli Ilivyoweza
kutekeleza sheria au jinsi Israeli ilivyoshindwa kwa kusikitisha katika kutii
sheria.Mw 11:26-28.
e.Agano la Mungu na Daudi.
Agano la Mungu na Daudi 2Sam 7:8-16,Agano hilo
linaonyesha kipengele cha uzao”wa agano la Ibrahimu.Ahadi kwa Daudi katika
kifungu hiki ni muhimu,Mungu aliahidi kwamba uzao wa Daudi utaishi milele na
kwamba ufalme wakehautaondoka kabisa.Ni dhahiri,kiti cha enzi cha Daudi
hajawahi kuwa mahali wakati wote,tena haitatokea mtu kutawala isipokuwa wa
Daudi.Luk 1:32-34)
f.Agano jipya(Agano la Mungu na Ulimwengu.
Agano Jipya pamoja na mawazo ya watu na wenyeelimu wanatheologia
kuwa na mitazamo na misimamo kuhusu Agano Jipya Agano hili mimi naamini agano
hili ni agano la Mungu na ulimwengu,kwa maana ndilo agano la ukombozi wa ulimwengu
na waulimwengu.Math 1:21,Naye atazaa mwana nawe utamwita jina lake Yesu
maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao.
Yoh 3:16-18,Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata
akamtoa mwanawe pekee,ili kila mtu amwamiye asipotee,bali awe na uzima wa
milele.Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili aukumu ulimwengu bali
ulimwengu uokolewe katika yeye.Amwaminiye yeye haukumiwi,asiyeamini amekwisha
kuhukumiwa kwa sababu hakuliamini jina la mwana pekee wa Mungu.
Tunaendelea kulichunguza agano Jipya.Je! Biblia inamaanisha nini
inaposema agano jipya baina yetu na Mungu? Agano jipya ndilo jibu katika uasi
wetu.Imeandikwa na Yer 31:33, Basi
agano hili ndilonitakalofanya na nyumba ya Israeli,baada ya siku zile asema
Bwana nitatia sheria yangu ndani yao na katika mioyo yao nitaiandika,nami
nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu.
Agano Jipya laja na Yesu Kristo.Imeandikwa na Luk
22:20,Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula akasema ,kikombe hiki ni agano
jipya katika damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu.
4.Namna ya kutii agano lako na madhabahu ya kweli.
Naamini nasema na mtu watu na kanisa na kondoo wa Mungu pamoja na
watumishi wa Mungu pamja Na viongozi mbalimbali walioteuliwa,na watu waishio
madhabahuni patakatifu.Ezekieli.45:1-8.Tena aamini kila asimamaye
madhabahuni na kumwamini Mungu wa kweli na Yesu Kristo aliyetumwa na Mungu huyo
analo agano au maagano na Mungu.Na kwa sababu unalo agano na Mungu nakupa mbinu
Ya kutii agano maagano yako na Mungu na maagano ya Mungu na wewe.
a.Funga milango mitano ya fahamu.
Milango ya fahamu katika hali ya mwili.Milango yafahamu ni ogani
za mwili zinazoturuhusu kujua na kuyadumu mazingira yetu kwa usahihi.Kibailojia
inaeleza kuwa ogani yenye uwezo wa kupokea habari za nje ya mwili kama vile,Nuru,Sauti,Mwendo,Harufu,na Ladha,ili kuzibadilisha katika mfumo wa
kiumeme inachukuliwa kwa njia ya mfumo wa neva hadi kwenye ubongu.Kuna milango
mitano ya fahamu katika mwili wa mwanadamu ambayo ni Jicho/Macho(kuona)Sikio/Masikio(kusikia).Pua(kunusa)Ulimi(kuonja)Ngozi(kugusa).
1. Kusikia ni fahamu ya Sautikupitia masikio.
2. Kuona ni fahamu ya Nuru kupitia
macho.
3. Kuonja ni fahamu ya ladha
kupitia ulimi.
4. Kunusa ni fahamu ya kunusa kupitia pua.
5. Mguso ni fahamu ya nyuso za vitu kupitia ngozi.
Kama milango ya fahamu imeharibika,tunasema ni kipofu,bubu au
kiziwi,ana matatizo ya kuelewa mazingira yake sawa na jinsi wanavyoweza watu
wengine.Milango ya fahamu ni muhimu sana kwa viumbe hai kutokana na kwamba
inasaidia kiumbe hai katika shuguli zake za kila siku,hata katika kutafuta mahitaji
muhimu.
b.Mtu ni roho.
Kama tulivyoona katika sura ya kwanza yakwamba mtu ni roho ya roho
tukimaanisha roho za viumbe ni roho za roho.Biblia inasema wazi kwamba hapo
Mungu aliamua kumuumba mtu kwa mfano wake
Mungu na kwa sura yake Mungu mwenyewe kama tunavyosoma katika maandiko
matakatifu katika kitabu cha Mw
1:26-27.Nataka ufuhamu kwa uhakika ya kwamba mtu anayeongelewa hapa
ni roho na Sio mwili kama vile watu wengi wanavyodhani,unaposikia wewe ni mfano
ni mfano wa Mungu.Basi fahamu mtu tunayesema ni mtu wa ndani (roho)ndiye mfano
wa Mungu.Yoh 4:24.
c.Fahamu za rohoni.
Kama vile ulivyo mwili,mtu ambaye ni roho anazofahamu katika hali
ya roho ambazo zinamuwezesha Kuelewa,kutambua mazingira ya rohoni kama vile
mwili unavyoweza kutambua mazingira yake ya mwili.Fahamu zilizopo katika
ulimwengu wa roho nikama zile za ulimwengu wa mwili zinazohusiana na Kugusa na
kuonja na kusikia harufu.
1.Kuona rohoni(Macho ya roho)
Ili uelewe kupata uelewa sawasawa kwanza vuta picha ya mwanadamu
mwenye macho ambaye anaangalia na kuona mambo mbalimbali katika maisha ya
kawaida,macho yanampa uwezo wa kutambua wa watu na vitu.Kwa kutumia macho mtu anaweza
kuweka kumbukumbu ya mauukio fulani katika ufahamu wake na mambo hayo aliyoyaweka
yakamsaidia kuja kufanya maamuzi sahii au kuwasaidia wengine kufanya maamuzi
sahihi katika maisha ya kila siku.Ndivyo ilivyo kwa mtu wa rohoni,na kufahamu
vitu vya roho ni vilevile kuweka katika ufahamu wake kumbukumbu za rohoni kwa
matukio aliyoyaona ili imsaidia katika kufanya maamuzi ya kiroho.Neno la Mungu
linazidi kututhibitishia Kwamba yapo macho ya rohoni na watu wenye macho hayo
wamefungwa wamepofushwa,macho yao Na hata hawaoni kama tunavyosoma habari ya
mtumishi wa nabii Elisha katika 2Fal 6:15-17.Hata asubuhi na mapema
mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka,na kwenda nje kumbe pana jeshi la
watu,na farasi na magari wameuzingira mji ule.Mtumishi wake akamwambia,Ole
wetu! Bwana wangu,tufanyeje? Akamjibu,Usiogope, maana walio pamoja nasi ni
wengi kuliko wale walio pamoja nao.Elisha akaomba,akasema,Ee
Bwana,nakusihi,mfumbue macho yake,apate kuona.Bwana Akamfumbua macho yule
mtumishi,naye akaona,na tazama,kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya
moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.”Na amini umeona na kufahamu ya
kwamba mtu Anaweza kuwa na macho na wakati huo asione kinachoendelea!kwa hiyo
kuona kunafaa sana,lakini ili Ufikie hatua ya kutii maagano yako na Mungu
nilazima ufungue mlango wako wa fahamu ya Nuru,yaani kuona.Ona katika
macho ya ndani macho ya rohoni ili kuyatambua mambo ya rohoni.Mw
48:10.Kut 23:8.Am 16:28Math 6:22-23.
2.Kusikia rohoni (Masikio ya roho)
Katika hali ya kawaida,hali ya mwili wa damu na nyama,mwanadamu
anakuwa na masikio ambayo yanaweza kuwa na uwezo wa kusikia au yasiwe na uwezo
wa kusikia,kama masikio yakiweza kusikia hiyo Ndio sahihi lakini kama hatuwezi
kusikia basi hapo kuna shida.Yaani inawezekana mtu huyu ni kiziwi au
anayomatatizo yanayomzuia kusikia sawasawa.Katika ulimwengu wa roho yapo
masikio ya rohoni yanayomwezesha mtu wa rohoni kusikia sauti za rohoni.Kama mtu
hana masikio ya rohoni basi huyo ni Mlemavu wa rohoni na anahitaji kuponywa
mlango huo wa fahamu ya sauti,ili aondoke katika ulemavu Huo.Ufu
1:9-11,1Sam 3:1-10,Isay 14:12-15. Tumeona jinsi masikio yalivyo muhimu
katika hali ya mwili Na masikio ya ndani.Mimi kakuambia kwa funga mlango wa
sauti ili upate kutii agano maagano yako na Mungu.Uwe kiziwi katika mambo ya
ulimwengu wa mwili,na ulimwengu roho pia uwe kiziwi usizisikie roho za upotevu.
3.Kuonja rohoni(Ulimi rohoni)
Kuna watu wamekuwa wakiota ndoto ama wanakula wenyewe au
wanalishwa katika ndoto vitu vya aina Mbalimbili,mwingine atakuambia nilipewa
maji machungu kwenye ndoto au chakula kibaya sana kwe ndoto Au nilikula chakula
kitamu kwenye ndoto.Kumbuka ndoto ni ulimwengu wa roho.Kama inavyokuwa Katika hali ya mwili huu
wa nyama na kwamba unaweza kujua ladha
mbalimbali za vyakula au vinywaji au chochote kinachoingia kinywani,ndivyo
ilivyo na kwa ulimwengu wa roho.Unapokuwa rohoni Unaweza kutambua ladha ya
vitu,kwani Biblia inatufundisha kwamba upo ulimi wa rohoni kama tunavyosoma
katika Luk 16:22-24.Ikawa yule
maskini aliďunga,akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu.Yule tajiri
naye akafa,akazikwa.Basi kule kuzimu aliyainua macho yake,alipokuwa katika
mateso,alisema, Ee baba Ibrahimu,nihurumie,umtume Lazaro achovye mcha Ya kidole
chake maji,auburudishe ulimi wangu,kwa sababu ninateseka katika moto huu.Kumbuka Mfano huu
aliutoa Yesu alikuwa anazungumzia habari za roho ya masikini.Lazaro na roho ya
Yule tajiri Baada ya kufakwao,sasa tuna kumbe tajiri alihitaji kuburudishwa
ulimi wake kwa tone la maji katika Ulimwengu wa roho
Mtu wa Mungu ukizidi kusoma neno la Mungu utafahamu kwamba mtu
akiwa rohoni kwa kutumia mlango wa fahamu wa kuonja(Ulimi)anaweza
kujua ladha ya vitu katika ulimwengu wa roho kama tunavyosoma katika Ezekieli 3:1-3,Akaniambia,Mwanadamu,kula
uonacho,kula gombo hili,kisha enenda kusema usema ukaseme na wana wa Israeli.Bas
nikafunua kinywa changu,naye akanilisha like gombo akaniambia,Mwanadamu,lisha
tumbo lako,ulijaze tumbu lako kwa hili gombo nikupalo.Ndipo nikalila,nalo
kinywani mwangu lilikuwa tamu,kama utamu wa asali.
Kumbe nabii wa Mungu Ezekieli aliweza kula na kutambua ladha ya
gombo kuwa lilikuwa na utamu wa Asali.Kwa hiyo nikushauri kwamba funga mlango
wako wa fahamu ya ladha kupitia ulimi kwa kutuonja ladha ya roho ya upotevu.
4.Harufu ya rohoni( Kunusa rohoni)(Pua)
Ukiwa katika hali ya mwili na kama hauna kasoro zozote katika pua
zako,unaweza kufahamu,kutambua Harufu za aina fulani na ukaziweka katika
kumbukumbu zako na zikakusaidia katika kufanya maamuzi katika siku za mbeleni,na
siku ukinusa hata pasipo kuona utatambua kwamba kuna kitu kinaungua,hivyo Ndivyo
ilivyo kwa jinsi ya rohoni.Kama pua zako za kiroho zinafanya kazi sawasawa
unaweza kugundua mambo ya rohoni hata kabla ya kuyaona.2Kor 2:14-16,Ila Mungu
ashukuriwe,anayetushagaza daima katika Kristo,na kuidhihirisha harufu ya kumjua
yeye kila mahali kwa kazi yenu.Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo,Mbele za
Mungu,katika wao wanaokolewa,na katika wao wanaopotea,katika hao wa pili harufu
ya mauti iltayo mauti,katika hao watkwanza harufu ya uzima iletayo uzima.Naye
Ni nani atoshaye kwa mambo hayo.
Mtume Paulo akiwa amejaa Roho Mtakatifu anaongelea habari ya
manukato katika ulimwengu wa roho,maana yake ni kwanba mlango wako wa fahamu wa
kunusa (Pua) wa rohoni unafanya kazi sawasawa.Hi ndio sababu Mtume Paulo
anazungumzia harufu za aina mbili yaani harufu ya mauti na harufu ya uzima.
Vilevile tunamuona Yohana
akiwa rohoni anatambua kwamba maombi ya watakatifu yalikuwepo kwa
Mungu kwenye mabakuli kama manukato,aliweza kujua kwamba yale maombi ni
manukato kwa waana Yake mlango wa Yohana wa fahamu katika katika kunusa
ulimfahamisha kwamba yale ni manukato kwa
kunusa.Ufu 5:8,Hata
alipokitwaa kile kitabu,hao wenye uhai wanne na wale wazee na wanne wakaanguka
mbele za Mwana-Kondoo,kila mmoja wao ana kinubi,na vitasa vya dhahabu
vilivyojaa Manukato,ambayo ni maombi ya watakatifu.Hii inazidi
kututhihirishia kwamba ukiwa unaweza kunusa Kutambua harufu ya sadaka
inayompendeza Mungu au la.
5.Kugusa,kuguswa rohoni.( Ngozi ya kiroho.
Siku moja Yesu alikuwa katika huduma ya kuhubiri injili watu
wengine walimsonga huku na kule pengine wengine walimvuta na kumuita ili
awaponye.Lakini kuna mwanamke mmoja ambaye aligusa Vazi la Yesu kwa imani na
Yesu akatambua kuna mtu amemgusa na kuuliza kwamba ni nani huyo kama
Ilivyoandikwa katika Luk 8:43-46,Na
mwanamke mmja,ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili,alikuwa amegharimiwa mali zake zote
kwa kuwapa waganga asipate kuponywa na mtu ye yote,alikwenda nyuma
yake,akamgusa upindo wa vazi lake,na wara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.Yesu
akasema,Ni nani aliyenigusa? Basi watu wote walipokana,Petro akamwambia,Bwana
mkubwa,makutano haya wanakuzunguka na kusonga.Yesu akasema,Mtu alinigusa,mama
anaona ya kuwa nguvu zimenitoka.Swali la msingi sana la
kujiuliza hapa ni hili Yesu aligunduje kwamba ameguswa Na nguvu zimemtoka
wakati alikuwaamezongwa na watu wengi?.Iweje mtu mmoja amguse na afahamu
dhahiri na kusisitiza kwamba ameguswa?.Kwa uhakika kabisa mama yule alimgusa
Yesu kwa imani kutokea rohoni na kwakuwa Yesu alikuwa wa rohoni alitambua mara
ile ile,alitambua kwakuwa alitumia Mlango wa fahamu wa rohoni wa kugusa na
kufahamu kwamba kuna mtu amemgusa.Katika Ufu 1:17,Nami nilipomwona,nalianguka miguuni pake kama mtu
aliekufa.Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu,akasema,usiogope,Mimi ni wa
kwanza na wa mwisho,”Yohana alitambua kwamba Yule mtu ameweka
mkono juu yake kwakuwa akiwa rohoni mlango wake wa ufahamu ulikuwa ukifanya
kazi.
Naamini umeelewa vizuri milango ya fahamu inavyofanya kazi na
ilivyo muhimu kama yote iko imara na Ikitumiwa vizuri.Milango hiyo mitano ya
fahamu ukiifunga isiwe wazi kwa mambo ya ulimwengu utakuwa mtiifu wa maagano
yako na Mungu na utafungamanishwa na
madhabahu yenye mahusiano na roho wa kweli.
Kimeandikwa na
Bishop.
Rhobinson S.Baiye.
rhobinsons.blogspot.com
Whatsapp.0764127531
Mwanza Tanzania.
No comments:
Post a Comment