Monday, June 1, 2020

KITABU CHA UBORA WA LUGHA YA KANISA No 2

UBORA WA LUGHA N0 2

Kitabu hiki kiitwacho ubora wa lugha namba mbili kinahusu hasa na lugha ya kushawishi mtu au watu kumwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wao.Kitabu hiki kinakupa mbinu muhimu ambazo zitatufanya tuweze kuwashawishi watu kujiunga na makanisa yetu ili zipate kuimarika na kustawi.Ubora wa lugha namba moja kimo katika Tuvuti  hii kaisome utakifuraia sana.Itapendeza kama utasoma kwanza namba moja ili upate kuelewa namba mbili hii.Nimemnukuu Daktari Mark Goulston. Anasema mambo mengi katika lugha inayoshawishi  msome hapo chini

.Daktari Mark Goulston Anasemahivi:

1:Kila Mtu Ana Mahitaji Yake.

Kila mtu ana mahitaji yake,matamanio yake na pia ajenda zake.Na tena kila mtu ana siri yake ambayo anaificha,na hataki watu wengine waijue.Na pia kila mtu anapilika zake na msongo wa mawazo,na hana muda wa kumtosha kufanya kila anachotaka kufanya.Ili kuweza kwenda na hayo yote yanayoendelea kwenye maisha yake,mtu anajitengenezea ukuta ambao bila ya kujua hayo huwezi kumshawishi kwa jambo lolote.Fahamu kwamba ukitaka mtu afanye au akupe chochote unachotaka,anza kwanza kuvunja ukuta huu ambao kila mtu amejijengea.Kanisa ni lazima kuvunja ukuta ambao umejengeka na kila mshirika kama mahitaji binafsi,matamanio binafsi,siri zake binafsi,imani,za kigeni,mategemeo,matumaini,mila,testuri,na lugha utamaduni,ili Kuimarisha na kustawisha kanisa. Za 11:10,14,2:9,3:7,7:2,28:5,29:5,46:9,48:7.Mith 15:4, Mik 2:13,3:3,Ombolezo 2:9,3:4 Math 5:19,6:19,12      :1,20,26:61,27:40,

2:Ushawishi Na Mzuguko Wake.

Ushawishi unaenda kwa mzunguko ambao ana hatua tano muhimu.Yaani kabla mtu hajashawishika kufanya chochote unachomwambia,anapitia hatua hizi tano ambazo unatakiwa kuzijua na kujua jinsi ya kumpitisha mtu kwenye kila hatua.

a:Hatua Ya Kwanza.

Hatua ya kwanza ni kumtoa mtu kwenye kukataa mpaka kuwa tayari kusikiliza.Wakati wowote mtu yupo kwenye hali ya kukataa, unahitaji kuwa na mbinu ya kufanya akusikilize.Tumia lugha ambayo mtumishi kiongozi mshirika na asiyeamini ashawishike kukusikiliza sio lugha ya kumweka mbali nawewe na kanisa.Kufanya hivyo kutaimarisha na kustawisha kanisa.

b:Hatua Ya Pili.

Hatua ya pili nikumtoa mtu kwenye kusikiliza mpaka kukufikiria.Hapa mtu anakuwa amesikiliza kile ulichomwambia,na kuna mbinu bora za kumwambia na akaanza kufikiria kwamba anaweza kufanya au anaweza kuwa tayari.Ni vema kutumia lugha ambayo itamweka mtu unaye wasiliana naye kuwa tayari kulifikiria sana kanisa lako.Kwa kufanya na kutumia lugha hiyo itaimarisha na kustawisha kanisa lako.

 c:Hatua Ya Tatu.

Hatua ya tatu ni kumtoa mtu kwenye kukufikiria mpaka kuwa tayari kufanya.Baada ya mtu kufikiria kwamba anaweza kufanya anashawishika zaidi na kuwa tayari kufanya.Tumia lugha ambayo itamfanya mtu kuwa tayari kufanya kwa ajili ya kanisa na mtu mmoja mmoja katika kanisa na katika jamii yako.Hiyo ndiyo lugha bora sio bora lugha,kufanya hivyo kutaimarishana kustawisha kanisa la mahali ulipo.

d:Hatua Ya Nne.

Hatua ya nne ni kumtoa mtu kwenye hali ya kuwa tayari kufanya  na kufanya jambo  husika.Hapa ndipo mtu anapofanya kile ambacho unataka afanye au anakupa kile ambacho ulitaka akupe.Kumbuka Yesu alivyosema kwamba mwana  hakuja kutumikiwa bali kutumika.Hata Mungu aliziumba mbingu na nchi na vyote viijazayo kwa kutumika kwa kutamka na kusema na kutumia lugha ya kuumba pamoja na kufanya kazi kwa mikono yake ili kumuumba mtu,Mungu hakutumikiwa bali alitumika.Tunapotumia kumshawishi mtu mpaka akatumika kwa ajili ya Mungu na watu wake yaani kanisa,hiyo ndiyo lugha bora wala sio bora lugha.

e: Hatua Ya Tano.

Hatua ya tano ni kumtoa mtu kwenye kufanya mpaka kwenye kufurahia kufanya na kuendelea kufanya.Kufanya siyo mwisho wa mzunguko huu,bali mtu anahitaji kufurahia kwamba amefanya na kuendelea kufanya kadri inavyohitajika.Na huu ndio mzunguko wa ushawishi ambao unatakiwa kujua na jinsi ya kutumia kwa watu mbalimbali.Yafaa sana na kutia moyo mtu anapo fanya kazi au anapo hudumu kwa lugha ya kanisa huku anafanya kwa moyo wa kufurahi,inaleta afya katika kanisa.Na tufikie ngazi hiyo ili kuimarisha na kustawisha kanisa na makanisa yetu ya mahali,na huko ndiko kunena kwa lughampya ambayo inasemwa na maandiko.

3: Fahamu Ubongo Wa Mwanadamu.

Ili uweze kuwa na ushawishi kwa wengine unahitaji kujua vizuri ubongo wa binadamu.Ubongo wa binadamu umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo zinatofautiana kwa miaka ambayo zimekuwepo.Ubongo ndio kiini cha mfumo wa neva katika wanyama wote wenye ungwemgongo na wanyama wasio na ungwemgongo.Ubongo unapatikana katika kichwa ukilindwa na mifupa ya fuvu.Kazi kubwa ya ubongo ni kuhakikisha viungo muhimu vya mwili kama vile moyo na mapafu vinafanya kazi ipasavyo.Acha tuone baadhi ya mambo muhimu ya kufahamu kuhusiana na ubongo,kabla ya kuona mgawanyo wa sehemu tatu kuu za ubongo.

1.Ubongo wa binadamu huwa hauna vipokezi vinavyohusika na maumivu hivyo ubongo hauhisi maumivu kabisa,hivyo mtu anaweza kufanyiwa upasuaji wa ubongo huku ukiwa na ufahamu wake na hauhisi maumivu yoyote.

2:Ubongo ndiyo kiungo pekee cha mwili ambacho hutumia nguvu nyingi sana zaidi ya asilimia 20% ya nguvu zote za mwili hutumiwa na ubongo japokuwa ubongo una asilimia (2) tu uzito.

3:Zaidi ya asilimia 60% ya ubongo wa binadamu huwa umeundwa kwa mafuta huku asilia 75% uzito  ubongo inabebwa na maji.

4: Sehemu ya ubongo iitwayo  Neocortex.Ambayo ina husika na lugha pamoja na ufahamu ndiyo sehemu kubwa zaidi kuliko sehemu zote zinazounda na ubongo, huchukua zaidi ya asilimia 76% ya ubongo wa binadamu kumfanya binadamu awe tofauti na wanyama wengine katika kuwaza kunena na kutenda.

5:Kila sehemu ya ubongo hufanya kazi,Jambo hili hufanya binadamu asiweze kutumia ubongo wake kikamilifu,inasadikika kuwa binadamu hutumia chini ya asilimia 10% tu ya ubongo wake.

6: Homoni inayoitwa Oxytocin ambayo hujulikana kama homoni ya mapenzi huzalishwa kwa wingi kwenye ubongo,na hupatikana kwa wingi katika matukio ya mapenzi ambayo homoni hii ndiyo huamua umpende nani, umpende vipi mapenzi yenu,na hii homoni ndio huamua umpende nani kwa wingi,lakini pia homoni hii huzalishwa wakati wa kukutana kimwili mwanamme na mwanamke,lakini pia wakati wa uchungu wa kuzaa,na lamwisho homoni huongoza na Kulinda  mfumo mzima wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama

7:Tukiwa kwenye ufahamu wetu,ubongo huzalisha kati ya watts 10 hadi 23 za umeme ambao unatosha kabisa kuwasha taa moja ya umeme.

8:Kupiga miayo hutokea mara nyingi baada ya kumuona mtu mwingine kafanya hivyo hii ni kwa sababu ubongo huwa na seli zinazoitwa seli koo mirror celle.Sehemu hii  ya ubongo huingiza kitendo hiki kutoka kwa mwingine na kikitokea basi hufanya mtu awe na matatizo makubwa.

9:Ubongo huwa na mishipa ya fahamu zaidi  ya bilioni 100 hii ni mara 15 zaidi ya idadi ya watu wote tuliopo duniani.

10:Mziki husisimua sehemu ileile ya ubongo ambao hutoa kemikali za raha Dopamine wakati wa kujamiana na kula?

Mgawanyo Wa Ubongo Katika Sehemu Tatu Kuu.

1.Sehemu Ya Kwanza:Ubongo  Wa Nyuma)

Sehemu ya kwanza ya ubongo ni sehemu ya ubongo wa chini,ambao ni ubongo wa nyuma una tabia za mjusi.Hii ni ile sehemu ya ubongo ambao kazi yake kubwa ni kuhakikisha unaishi kwa Ubongo huu kazi yake ni kuakikisha umepata chakula na unaweza kujikinga na hatari.Ubongo huu huwa unachukua hatua haraka bila hata ya kufikiri kwa kina.Kwa mfano kama umewahi kuwa kwenye hatari mara kukimbizwa na mnyama kama mbwa hapo utapata nguvu nyingi za haraka hata kuruka utakuta ambao kwa kawaida usingeweza kuukuta,hii ndiyo kazi ya ubongo huu.Kama kanisa na kama viongozi na watumishi kuchukua hatua za haraka unapokuwa uhitaji wa kufanya hivyo.Mungu aliweka ubongo huo wa chini ili kuchukua hatua za haraka kwa Kuimarisha na kustawisha kanisa lako.

2.Sehemu Ya Pili: Ubongo Wa Kati.

Sehemu ya pili ni ubongo wa kati,ambao una tabia za mnyama.Hii ni sehemu ya ubongo ambayo imebeba hisia zote za mtu.Hisia za upendo,wivu,hata rahaa zipo kwenye sehemu hii ya ubongo.Sehemu hii ya ubongo ndiyo inatusukuma kufanya vitu vinavyotupa hisia nzuri na kutuepusha na vitu vinavyoleta hisia mbaya.Fahamu kwamba unapotumia lugha ambayo hajaeleweka vizuri sehemu hii hufanya kazi kwa kuhisi kama kuna kitu ambacho kimefichwa watu hawakifahamu mahali hapa.Na hapo ndipo mwanzo wa mtu kuwa na maswali yasio kuwa na majibu na kukatisha tamaa,na kulichukulia kanisa,na mwanzo wa kanisa kutokuimarika na kustawi.Lugha nzuri huusika katika sehemu hii.

3.Sehemu Ya Tatu: Ubongo  Wa Mbele)

Sehemu ya tatu ni ubongo wa juu ambao una tabia za utu.Huu ndio ubongo ambao unatutofautisha sisi binadamu na viumbe wengine wote.Huu ndio ubongo ambao unafikiri kwa kina kwenye kila jambo tunalofanya au linalotokea.Huu ndio ubongo ambao unatunza kumbukumbu.Ubongo huu unakusanya taarifa kutoka kwenye sehemu nyingine za ubongo na kufanya maamuzi sahihi.

 4:Fanya Maamuzi Na Ubongo Wa Juu

Tumia lugha na kufanya maamuzi kwa kutumia ubongo wa sehemu ya juu.Kwa bahati sana watu wengi wamekuwa wakifanya maamuzi  kwa kuongozwa na ubongo wa chini na ubongo wa kati.Ni mara chache sana watu wanaweza kuutumia ubongo wa juu vizuri na kufanya maamuzi bora.Maamuzi mengi yanayofanywa na ubongo wa chini na ubongo wa kati ni maamuzi ambayo yana faida ya muda mfupi lakini kwa muda mrefu yana hasara kwao.Mfano Ni mtu ambaye anabaka,hapa anauridhisha ubongo wa kati ambao utapata raha,lakini angetumia ubongo wa juu angeona siyo kitu sahihi kwake kufanya.

5:Shawishi Mtu Akiwa Kwenye Ubongo Wa Mbele

Ili uweze kumshawishi mtu yeyote,hakikisha unaongea naye akiwa kwenye ubongo wa juu.Hakuna kitu unachoweza kumwambia akakusikia na kukuelewa.Haijalishi utatumia mbinu bora kiasi gani,kama mtu hayupo kwenye ubongo wa juu utapoteza muda wako.Hii ndiyo maana ni vigumu sana kumshauri mtu ambaye ana hasira,au hana raha na yupo katikati ya hisia kali za mapenzi.Kuweza kumshawishi mtu mtoe kwanza kwenye Ubongo wa kati na wa chini na mpeleke kwenye Ubongo wa juu ambapo anaweza kufikiri sawasawa.

6:Adui Wa Kwanza Wa kushawishi Ni Wewe

Adui wa kwanza kuwashawishi wengine ni wewe mwenyewe.Ili uweze kuwashawishi wengine ni lazima wewe kwanza kushawishika.Ni lazima wewe ukubaliane na kile anachotaka wengine wafanye au kukupatia.Ni lazima  uweze kujithibiti mwenyewe ili kuweza kuwashawishi wangine kuchukua hatua ambayo unajua ni muhimu.

7:Ondoa Chujio Tayari Unalo.

Ondoa chujio ambalo tayari unalo.Fahamu kwamba kila mmoja wetu ana chujio ambalo anatumia kuwachuja wengine kwa kadiri wanavyoonekana au alivyowazoea.Hivyo tunawapanga watu kwenye makundi kwa kufikiri tunawajua sana.Ili kuweza kuwa na ushawishi kwa wengine kwanza ondoa chujio hili na mwendee kila mtu bila ya kumhukumu,kuwa tayari kujifunza zaidi kutoka kwake.Usimweke mtu kwenye upande wowote,badala yake msikilize yeye  na utapata njia bora za kuweza kumshawishi.

8:Fahamu Kitu Kinacho Kusukuma.

Naomba fahamu kwamba kila kitu anachofanya,sababu inayomsukuma kufanya.Hakuna mtu anayefanya kitu kwa ajali au kwa bahati mbaya pekee.Hivyo unapokutana na tatizo au changamoto kutoka kwa wengine jua Kuna kitu kimewasukuma kufanya walichofanya.Ili uweze kuwashawishi watu,jua ni kitu gani kinawasukuma wafanye kile ambacho wanafanya sasa na ni jinsi gani unaweza kuwafanya kuacha wanachofanya sasa na wafanye kile ambacho unawashawishi wafanye.

9:Mfanye Mtu Ajisikie Ameeleweka.

Mfanye mtu ajisikie ameeleweka,ni lazima umwelewe mtu kabla hujakaribia kumshawishi afanye chochote unachotaka afanye.Jaribu kuvaa viatu vyake na mwelewe wazi ya kwamba unaelewa kwa nini yupo pale alipo sasa.Na hata kama anafanya kitu ambacho anakosea, mwelewe kwamba kuna kitu ambacho kinasababisha yeye afanye hivyo.Usione kwamba yeye hayupo sahihi na kumweleza hivyo,ukienda kwa njia hiyo atakachofanya ni kujitetea na hutaweza kumshawishi kwa njia yoyote ile.Mwelewe mtu na atafunguka kwako.

10:Wafanye Watu Wakujali

Kama unataka wengine wajali kuhusu wewe,anza kujali kuhusu wao kwanza.Moja ya njia muhimu za kuweza kushawishi watu ni kuwafanya wavutiwe na wewe,na wajali kuhusu wewe,na wawe tayari kufanya kile ambacho unawaambia wafanye.Lakini hii haitakuja kuwavunja moyo wewe kukazana,watu wavutiwe na wewe na wajali kuhusu wewe.Badala yake inakuja pale unapoanza kujali kuhusu wengine,na unapovutiwa na wengine.Hivyo unapokutana na watu usitumie nafasi hiyo kujisifia zaidi wewe,badala yake tumia nafasi hiyo kutaka kuwajua zaidi.Ni vema kujua ni jambo gani wanafanya changamoto gani wanapitia yapi ambayo wameweza kukamilisha.Kadri unavyojali kuhusu wao wataanza kufunguka kwako na watakuwa tayari kufanya kile unachotaka wafanye.

11:Ona Thamani Ya Wengine.

Wafanye wengine wajione ni wa thamani kwako.Hii ni mbinu muhimu sana kila mshirika wa kanisa la mahali anatakiwa kuwanayo kama anataka kuwashawishi watu ili kuimarisha na kustawisha kanisa la mahali watu huchukua hatua fulani.Hakuna kitu ambacho mtu anapenda kama kuona amethaminiwa.Hii ndio maana watu wanapenda kuitwa mheshimiwa,bosi,mtaalamu bingwa na majina mengine mengi yenye sifa za kuheshimika.Mfanye mtu aone ana mchango mkubwa kwenye kile anachofanya na kile anachotaka afanye ataweka mchango mkubwa pia.Kufanya watu kuwa wa thamani kwako au kwenu Ni zawadi kubwa sana unayoweza kupata.Hata Mungu alituthamini sisi wanadamu, maana alituumba kwa mfano na sura yake.Mwa 1:26.

12:Epuka Kueleweka Tofauti.

Epuka kueleweka tofauti na unavyotaka ueleweke.Katika harakati za kushawishi wengine unaweza kutoa picha iliyo kinyume kabisa na kile ulichokuwa unataka kutoa wewe.Mfano unataka watu wakuone wewe ni mwenye busara lakini kwao unaonekana ni mpumbavu.Au unataka wakuone mwaminifu ila wao wanakuona ni tapeli.Matokeo hayo hutokana na mtu kutokujiandaa vizuri na kutosikiliza wale ambao anataka kuwashawishi.Unahitaji kuwafundisha kwa makini na kuona wanapokeaje kile ambacho unawapa.

13:Tambua Vitu Vitatu Muhimu.

Kuna vitu vitatu ambavyo vinawasukuma watu kuchukua hatua ,ukiweza kuvitumia vizuri vitu hivi utaweza kuwashawishi watu iwe ni kwenye kazi,biashara na hata kwenye familia.Jambo la kwanza ni mapenzi,hamu au shauku.Watu wapo tayari kufanya kile ambacho wanapenda kufanya na wana shauku kubwa kukifanya.Hivyo angalia ni kitu gani watu wanapenda na kitumie katika ushawishi wako.Hata Yesu alikuwa akitazama na kugundua kile wasikilizaji wake wanachohitaji hata kama ni kinyume na mapenzi yake,aliwafundisha na alikuwa anaeleweka vizuri sana hata kama wengine hawakuwa wafuasi wake.Jambo la pili ni hamasa watu wanakuwa tayari kuchukua hatua kwenye jambo lolote ambalo wanapenda.Wafanye watu wahamasike kwenye kile ambacho unataka wafanye.Jambo la tatu ni fahari.Watu wanaona fahari pale wanapoona wamekuwa na mchango kwenye Jambo fulani.Watu wanapoona kile walichofanya kina mchango kwa wengine wanafarijika sana.Tafadhali tumia vitu hivi vitatu kwa pamoja na utaweza kushawishi watu kuchukua hatua.

14:Tafuta Na jitahidi Kuwa Mwaminifu.

Uaminifu ni muhimu sana katika kuwashawishi wengine.Huwezi kuwashawishi watu kama hawakuamini na watu hawawezi kukuamini kama husemi kweli na kutekeleza kile unachoahidi.Usiwe na haraka katika kushawishi kwako,badala yake jenga mahusiano yenye uaminifu,kadiri watu wanavyo kuamini,kutokana na matendo yako na siyo maneno tu, ndiyo wanavyokuwa tayari kukubaliana nawe.

Lugha yenye mvuto wa kushawishi

Kushindwa kushawishi    kumewafanya watu wayaone maisha ni adhabu.kushindwa kushawishi kumewaangusha wengi katika ulimwengu huu, ulimwengu unao kwenda kwa kasi ya ajabu.Si rahisi kushawishi mtu akubali ombi na kutoa huduma au msaada kwa mtu mwingine.Kazi hii ngumu inaweza kufanikishwa kwa kutumia mbinu tano (5) rahisi.Mbinu hizo tano ni zifuatazo.

1:Kwenda Sambamba Na Mshawishiwa.

Mshawishi anapaswa kutazama kwa makini jinsi anayeshawishiwa anavyowasiliana na mshawishi hili ni pamoja na matumizi ya lugha ya ishara ya mazungumzo na ya maandishi,ili naye afanye vivyo hivyo.Ingawaje, mshawishi anapaswa kuwa makini ili asionekane anamkebehi mshawishiwa.Ikiwa mshawishiwa atagundua kuna usanii hatotia maanani yale anayoambiwa na hatimaye kutokubali kutimiza ombi la mshawishi.

2:Kutimiza Mahitaji Ya Wakati Husika.

Watu hujipendelea na watu hupenda mahitaji yao yatimizwe kwanza ndipo ya wengine yafuate.Mshawishi atambue vipaumbele vya mshawishiwa atakavyotekeleza ili maombi yake yatimizwe kwa urahisi.Mshawishi atazame mahitaji,matakwa,vionjo nk.ili aweze kuvuta hisia za mshawishiwa.Mshawishi ajitahidi kutimiza kero au matakwa ya mshawishiwa kwa kadiri ya maadili,hali na uwezo wake kabla ya kutoa ombi.

3:Mbinu Ya Tatu: Uthibitisho.

Mshawishi atoe uthibitisho unaoonyesha ya kwamba ombi au lengo lake litatekelezeka bila ya vikwazo vingi.Mshawishi atoe uthibitisho pasipo na shaka ya kwamba bidhaa bora baada ya muda husika, baada ya ombi lake kukubaliwa na kutekelezeka.Mshawishi ashindanishe Uthibitisho wake dhidi ya washindani wengine.Mshawishi ahakikishe anayosema au kutoa ni ya kweli na yanawezekana.Mshawishi aonyeshe uhusika au nafasi yake huku akitabasamu ili kukuza imani na urafiki.Pia mshawishi aonyeshe ya kwamba yupo tayari kutoa msaada wa ziada kama ikibidi kufanya hivyo.

4:Mbinu Ya Nne:Kuwasiliana Kwa Ufasaha.

Takribani watu wote wanapenda wakubalike na kueleweka kadiri wanavyohisi ni rahisi,kwa kadiri ya hisia zao bila kujali jinsi wanavyowasiliana.Mshawishi anapaswa kujiuliza,je niwasilisheje ombi langu bila ya kumkwaza mshawishiwa?.Ili kufanya hivyo, mshawishi anapaswa kutumia mbinu za mawasiliano bora.Mshawishi atambue na kukwepa maneno ambayo huathiri utu wa mtu au jamii husika kama yasipotumika kwa kuzingatia mazingira na aina ya mazungumzo.

5:Mbinu Ya Tano:Kukubaliana Na Mshawishiwa.

Takribani watu wote hupenda uridhika kwa kuambiwa “nimekuelewa”.Katika hili mshawishi ahakikishe anasikiliza kwa makini mawazo yanayofanikisha ombi lake likubalike.Mshawishi akubaliane pia na mawazo kinzani kabla ya kukosoa au kutoa ufafanuzi.Kwa mfano,unaweza kuwa sahihi lakini ni bora kama ingekuwa hivi,kwa maana natambua hali halisi lakini naomba tufanye hivi.Mshawishi ahakikishe ya kwamba pindi ombi lake litakapokubaliwa na kutekelezeka pande zote mbili zitafanikiwa ili mshawishiwa akubali kutoa msaada.Mshawishiwa atatoa msaada na ushirikiano pale atakapohisi anafanya uamuzi sahihi.

Neno La Mungu Mbinu Ya Ushawishi:

Moyo wa mwenye hekima husababisha kinywa chake kuonyesha ufahamu wenye kina,na kwa midomo yake huongeza ushawishi. Mith 16:23. Mradi wetu tukiwa waalimu wa neno la Mungu ni kuelimisha,si akili tu za Kuwafundisha watu au wanafunzi wetu,bali pia mioyo yao.Efe 1:18. Kwa hiyo, kufundisha kunahusisha mengi kuliko tu kuwasilisha habari.Mith 16:23.Moyo wa mwenye hekima husababisha kinywa chake kuonyesha ufahamu wenye kina,na kwa midomo yake huongeza ushawishi.kwa hakika,mtume Paulo alitumia kanuni hiyo katika kazi yake ya kufundisha.Alipokuwa korinto,yeye alikuwa akitoa hotuba katika sinagogi kila sabato na alikuwa akiwashawishi Wayaudi na Wagriki. Mdo 18:4.Kulingana na chanzo kimoja chenye mamlaka,neno la kigriki linalotafsiriwa hapa kushawishi lamaanisha kusababisha badiliko la moyoni kupitia uvutano wa ufikirio wa maadili.Kwa njia ya majadiliano yenye kusadikisha, Paulo aliweza kufanya watu wabadilishe hasa njia yao ya kufikiri.Uwezo wake wa kushawishi ulikuwa wa ajabu sana,maadui wake walimwogopa. Mdo 19:24-27. Hata hivyo ufundishaji wa Paulo haukuwawonyesho wa uwezo wa mwanadamu.Aliwaambia Wakorinto maneno yangu na kuhubiri kwangu haikuwa kwa maneno ya yenye ushawishi wa hekima bali kwa wonyesho wa roho na nguvu ili Imani yenu ipate kuwa si katika hekima ya wanadamu,bali katika nguvu ya Mungu. 1Kor 2:4-5. Kwa kuwa Wakristo wote wana msaada wa roho ya Mungu wote wanaweza kuwa walimu wenye kushawishi.Mifano hiyo na mafunsho ambayo Yesu alitoa na kuunganisha yaliwashawishi watu kwa kuwa alifahamu na kutambua mahitaji na mambo au vitu alivyohitaji.Alitumia lugha yenye mvuto na kutia moyo,kufariji,kujenga,kushauri,kukaripia,kukemea,ku'oa,kuteketeza,kupanda.Tujifunze njia za kushawishi kwa kumwiga Yesu Kristo.Ametuambia kwamba twende kwake na tujifunze kwake kwa kuwa yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo.Yesu alionyesha kuwathamini wote.

Watu Katika Makundi Manne.

Katika harakati za kuwashawishi wengine nivema ufahamu makundi manne ambayo Wataalamu wameyahainisha ili kuweza kumshawishi mtu au watu kufuatana na kundi lake.Unapoelewa na kujuwa kundi ambalo mtu unaye mshawishi alilomo hatakupashida.

 1.Kundi La Kwanza: Filing.

Hawa watu hujali sana wengine.Wanapenda kuwafurahisha wengine hata kwa mambo yasiyo muhimu,wanapenda sana hali ya maendeleo.Kwa hiyo kwanye migogoro hawafanyi kazi vema,hata maamizi yao yanazingatia mapenzi ya watu.Wanataka kusifiwa sana mara kwa mara.Hawawezi kuwaambia watu mambo magumu na yasiyofurahisha,wana huruma na wanahusiana mazuri na watu wengi.Kwa hiyo unapomshawishi mtu mwenye kupenda sifa inakubidi ujipange sawasawa.

2:Kundi La Pili: Senling.

Hawa ni watu ambao wasiyopenda masula mapya kama hakuna utaratibu wa kuyashughulikia.Wanataka utaratibu wa kudumu.Wanafanya kazi kwa mpango wakijua hatua za kufuata na lini kazi itamalizika.Watu au kundi hili hawana uvumilifu katika mambo yanapo changanyika.Siyo rahisi kuwatia moyo kwa sababu hawaamini wanayoambiwa juu yao.Wanalinda ukweli na hawakoseikosei mambo.Watu au kundi hili halishawishiki hata kama ungefanya nini,kwa hiyo watu hawa wasikupotezee muda wa kufanya mambo mengine.

3:Kundi La Tatu: Thinking.

Watu hawa au kundi hili halitawaliwi na hisia za wengine.Wanaumiza watu bila kujua,wanataka maelezo na mafafanuzi yanayooeleweka wazi.Wanaweza kufanya kazi vizuri hata kama kuna migogoro.Wanapofanya maamuzi hawajali sana mapenzi ya watu.Wanataka kutendewa haki,hawaogopi wala kusita kuonya au kufukuza watu wanakosea.Wanaelewana zaidi na watu wanaopenda hoja nao hupoteza marafiki mara kwa mara.

4:Kundi La Nne. Intuitive.

Watu hawa au kundi hili linataka kupambana na changamoto n matatizo mapya.Hawataki kurudia-rudia Mambo,wanataka kuelewa mbinu mpya hata kama hawataitumia.Hufanya kazi kwa nguvu sana jazba halafu wanapotea.Hurukia mambo ya kuamua kabla hawajajua ukweli mzima.Wanavumilia Mambo magumu,lakini hawataki Mambo yanayo rudiwa-rudiwa kila mara.Hawapendi kuchelewa kutekeleza Mambo kwa hiyo wanafanya makosa mengi.

Uwe Msikilizaji Mzuri.

Mbinu ya kufundisha kama kushawishi ina husisha kusikiliza bali si tu kusema kama tuoivyoonyeshwa kwenyeMith 16:23. Ili tuwe wenye kushawishi ni lazima tuwe na ufahamu wenye kina.Kwa hakika Yesu alikuwa na ufahamu kwa kina kuhusu watu aliofundisha.Yoh 2:25.

hutumika kama chombo cha mawasiliano kwa kupashana habari.

b.Lugha,hutumika,kujenga Umoja,Mshikamano,Ushirikiano.

c.Lugha hutumika Kukuza,Kutunza,na Kuendeleza tamaduni za jamii.

d.Lugha hutumika katika kutetea maarifa mbalimbali.Lugha ni nyenzo ya kufundishia.e.Lugha hutumika kama alama ya utambulisho wa Taifa,Kabila ya jamii fulani.e.Lugha hutumika kutoaburudani.

Kimeandikwa na

Bishop.Rhobinson S,Baiye

rhobinson.blogspot.com

rhobinsonsaleh1@gmail.com

Whatsapp.0764127531

Mwanza Tanzania

 

 

 

 


No comments:

Post a Comment

UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...