Thursday, August 26, 2021

JINSI YA KUANDAA MAHUBIRI NA MAFUNDISHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KUANDAA MAHUBIRI NA MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU (HOMILETICS) BISHOP RHOBINSON S.BAIYE Yaliyomo 1.Kuelewa maana ya mahubiri. 2.Kuelewa maana ya kuhubiri. 3.Kuelewa wito wa kuhubiri. 4.Kuelewa umuhumu wa kujifunza homiletics. 5.Kuelewa aina za mahubiri hotuba na mipangilio. 6.Namna ya kuhubiri ukiwa Redioni. 7.Namna ya kuhubiri ukiwa kwenye Runinga(Tv). A.Utangulizi Katika kozi hii tutashughulika na mojawapo ya kazi kuu ya kanisa.Mojawapo ya wajibu mkuu ambao umewekwa mikononi mwa kanisa ni kuhubiri ujumbe wa Mungu yaani Injili.1Kor1:21. a.Ni amri iliyo wazi kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo kwa wafuasi wake. Mark 16:15.Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.b.Kuhubiri ni mojawapo ya kazi ya thamani sana ambayo Mungu ametupa.Kuwa kuwa wasemaji wa Mungu yaani wa jumbwe wa Mungu 2Kor 5:20. c.Kuhubiri ni wajibu mkuu.Rum 10:14-15 d.Kwa njia ya mahubiri Mungu alichagua kujidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu. B.MAANA YA MAHUBIRI Neno mahubiri linatokana na maneno mawili ya kikriki ambayo ni homileo na homilia yenye maana ya pamoja na kuongea na kuwasiliana a.Homily pia humaanisha ujumbe au hutuba b.Elimu inayohusu namna ya kuhubiri huitwa Homileticts. c.Homiletics ni ustadi wa kuhutubia au kuhubiri. d.Mtaalamu wa elimu ya kuhubiri huitwa Homilist. e.Homiletics huhusisha kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri au kutunga hotuba. f.Mahubiri huhusu kujifunza kila kitu kinachohusisha na ujuzi wa kuhubiri masomo ya Biblia. g.Mahubiri ni ujuzi wa kuhubiri. h.Ni elimu au taaluma inayohusu kuhubiri Neno la Mungu. i.Ni elimu inayohusu namna ya kuhubiri somo masomo juu ya kila kitu kinachohusiana na kuhubiri. j.Kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu.Mungu hutumia watu wake aliowachagua kuhubiri ujumbe wake. k.Ujumbe unapaswa kuwa ujumbe wa Mungu.Kitu kingine chochote na ujumu si mahubiri ila ni maoni na falsafa za kibinadamu tu. Jambo la kufahamu a.Wahubiri huzaliwa na hawafanyi kamwe wala hafundishwi mtu kuwa mhubiri kama yeye si mhubiri.Lakini mhubiri wa kuzaliwa unaweza kumsaidia na kumwelekeza akawa mhubiri bora kwa njia ya mafunzo. b.Mhubiri si chanzo cha ujumbe.Mungu ndiye chanzo cha ujumbe na mhubiri ni bomba au mfereji ambao Mungu hupitisha ujumbe wakoe kwenda kwa watu aliokusudia.Ujumbe wa Mungu hutiririka kupitia utu wa mhubiri. c.Ujumbe unapaswa kutiririka kwa uhuru toka kwenye chanzo chake ambaye ni Mungu,kwenda kwa wakusudiwa yaani hadhira au wasikilizaji. d.Mahubiri na zao la mambo mawili ambayo ni Mungu na mhubiri.Mahubiri mazuri huzaliwa kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Mungu na Mhubiri.Hivyo kuna vipengele viwili vya wazi katika mahubiri.Cha kwanza ni kile cha ki-Mungu na cha pili ni kile cha kibinadamu.Kwa sababu ya wito wake mkuu mhubiri anapaswa kuwa mwaminifu na awe na ufahamu wa kutosha juu ya Neno la Mungu. C.MAANA YA KUHUBIRI. Mahubiri yana lengo mahususi katika mpango wa Mungu.Ni njia ambayo kwayo Mungu ameamua kuwafikia waliopotea dhambini na kuwaimarisha waamini.Kwa sababu mahubiri ni njia ya Mungu kuwafikia wanadamu,tutatazama maana ya kuhubiri kwa mitazamo mbalimbali kama ilivyo ainishwa na wataalamu wa masomo ya homiletics. 1.Kuhubiri ni kuielezea imani Mojawapo ya malengo ya mahubiri ni kuelezea au kutangaza kweli za maandiko matakatifu.Kila hotuba au ujumbe wapaswa kuwasilisha kweli za maandiko kwa njia itakayowezesha hadhara kupata uelewa zaidi juu ya maandiko matakatifu.Kuhubiri husababisha imani kuumbika kwa wasikilizaji wako.Hubiri kwa kukuza imani na kuielezea imani katika mwana wa Mungu. 2:Kuhubiri ni kuitetea imani. Haitoshi kuelezea ukweli wa Mungu bali tanapaswa kuutetea ukweli huo.Shetani ulimwengi na maadui wa imani huvamia na kupotosha kweli za neno la Mungu.Hivyo ni lazima kwa mhubiri ye yote kuwa tayari kuitetea imani ya kweli kwa njia ya kuhubiri kweli za ki-Biblia.Kuna wahubiri mengi wa uongo ambao kazi yao ni kupotosha kweli za maandiko matakatifu.Ni jukumu la kila mhubiri wa kweli kuhakikisha anasimama imara katika kuitetea imani ya kweli. 3:Kuhubiri Ni Kuinjilish. Wajibu mkuu wa mhubiri ni kuitangaza injili kwa watu waliopotea dhambini.Ni lazima watu wote waliopotea wapelekewe injili ili wapate kutambua hali yao ya kupote na kuongozwa kwenye wokovu. 4:Kuhubiri ni kukemea dhambi. Kama ukuchunguza hotuba za Agano jipya utagundua kwamba hakuna mhubiri hata mmoja aliyesita kukemea dhambi.Mfano Yesu,Yohana,Paulo,Petro,nk wote walikemea dhambikwa nguvu zao katika kila mahubiri.Mhubiri nilazima akemee dhambi kila mara kwani mhubiri ni kinywa cha Mungu.Kemea dhambi bila kuogopa chochote. 5:Kuhubiri ni kuhamasisha waamini. Mahubiri hutakiwa kuwasaidia wakristo kukua katika neema ya Mungu.Pamoja na kuonya na kukemea dhambi.Mahubiri hutakiwa kuwahamasisha na kuwawezesha waamini kukua kiroho na kufikia kimo cha Kristo. 6:Kuhubiri ni kufikia mahitaji ia hadhara. Mahubiri yatakuwa yamefanikiwa kama yatakuwa yamepokelewa na kukutana na mahitaji ya wasikilizaji.Mhubiri kwa uangalifu anatakiwa kujiweka katika daraja sawa na wasikilizaji. Anatakiwa kujitahidi kuhakikisha unapokelewa na makutano na kukutana na mahitaji yao. 7:Kuhubiri ni kudhihirisha uwezo wa Mungu. Bwana Yesu aliahidi kuwa na wahubiri kwa kulithibitisha neno kwa ishara na maajabu.Popote injili inapohubiriwa,ni sharti Bwana awepo akithibitisha kwa ishara.Mark 16:15-20/1kor 2:4. D.WITO WA KUHUBIRI Sehemu muhimu sana katika kuhubiri ni wito.Kimsingi wito ni wa mtu binafsi.Mungu huwaita watu katika huduma na watu hupokea hilo rohoni mwao kisha huja uthibitisho wa nje kupitia kanisa au watumishi mbalimbali na fursa mbalimbali.Mungu huwaita watu wake katika nafasi na huduma mbalimbali.Wengine kuwa wachungaji wamishenari wazee wa kanisa wainjilisti au huduma nyinginezo.Kazi ya kuhubiri sio ajire ambayo mtu anakwenda chuoni kusoma kwa lengo la kupata baada ya kuitimu masomo yake,bali ni mwito mtakatifu ambao mtu huitwa na Mungu mwenyewe kuwa mhubiri.Bali mtu huenda chuoni kupata maarifa yatakayomwezesha na kumsaidia katika kutimiza mwito wa Mungu uliondani yake.Haendi chuoni kupata mwito bali wito husababisha mtu kwenda chuoni kama sahemu ya maadiko. MBINU ZA UTAYARISHAJI WA MAHUBIRI. A.Utayarishaji wa somo. Kuna aina nyingi za utayarishaji wa somo au hotuba na kila mojawapo ina umuhimu wake.Lakini katika mada hii tutajifunza ainatatu za utayarishaji wa somo au hotuba.Kila mwanafunzi anatakiwa kuelewa aina zote tatu ili aweze kufaidika zaidi. 1:SOMO LILILOANDIKWA Katika aina hii mhubiri hutakiwa kuandika kila kitu anachokusudia kuhubiri.Wakati mwingine somo lote huandikwa.Kila eneo la somo huchambuliwa kwa undani na kuwekwa katika maandishi.Ujumbe au somo lote huandikwa kikamilifu kabla ya kuhubiriwa.Mhubiri huelezea kwa undani somo lake anapohubiri likiwa katika maandishi.Mhubiri anapohubiri mara nyingi hupitia kila kitu alichoweka katika maandishi. Faida za mbinu hii. a.Ujumbe wote huandaliwa kwa uangalifu mkubwa. b.Ujumbe huwasilishwa kwa umakini na uhalisia. c.Ujumbe huwa ni wa kitaalamu. d.Mhubiri hujikita katika somo husika. Hasara za mbinu hii. 1.Somo huwa haliwavutii wasikilizaji usipo kuwa makini, 2.Utoajim wa ujumbe wa namna hii unaweza kuwa wa kuchosha usipofanywa kwa uangalifu. 3.Utayarishaji wake huhitaji muda nwingi. 2:SOMO LISILOANDIKWA. Huu ni mbinu ya utayarishaji wa somo bila kuliandika.Mhubiri husoma vifungu vya maandiko na kufitafakari kwa kina kasha hukariri vitu vya msingi vilivyom katika ujumbe wake na maandiko yanayohusika.Aina hii mara nyingi hutumika katika kutyarisha na kuhubiri ujumbe wenye uvuvio zaidi.Ujumbe hutiririka kutoka rihoni na huwa wa kuvutia mmo. Faida za mbinu hii. a.Ni raisi kutumia. b.Hauhitaji muda mwingi wa matayarisho. c.Mhubiri huwa huru kutoa kila anachokijua ndani yake maadam kimeendana na ujumbe wa somo. d.Huwasisimua wasikilizaji na kuwavutia. Udhaifu wa mbinu hii. 1.Mhubiri hutoka nje ya ujumbe wake hasa ukifanywa na mhubiri asiye na uzoefu. 2.Wasikilizaji waweza kulielewa somo vibaya. 3.Somo kutowajenga wasikilizaji na kuishia kusisimua tu wasikilizaji. 3: MBINU YA SKELETONI. Njia hii huhusisha kuandika maelezo ya somo au ujumbe kwa kifupi kwa lengo la kufundisha kwa utuzaji wa kumbukumbu sahihi juu ya ujumbe au somo.Kwa maana nyingine ni kwamba hutayarisha muhtasari wa ujumbe au somo.Mhutasari huo huwa kama skeleton ya somo mfano wa fuvu la binadamu.Mhubiri huhubiri kwa kutumia skeleton hiyo.Kazi yake mhubiri ni kuweka nyama katika skeleton hiyo kwa njia ya mahubiri.Hivyo hanapohubiri huweka nyama katika mahubiri yake ili yaweze kuwa kamili.Muhutasari wa somo huwa katika mifupa ya ujumbe.Mifupa ndiyo huleta sura na mategemeo kwa kile mhubiri anachotamani kusema.Kwa maana anavyosema anaweka nyama katika mwili wa somo lake.Hupanua mawazo yake ambayo maelezo yake mafupi yamekuza ujumbe. Faida ya mbinu hii. a.Bmbinu hii humpa mhubiri uhuru zaidi. b.Utoaji wa somo huwa wa kuvutia sana. c.Somo huwajenga wasikilizaji bila kuwachosha. d.mhubiri huweza kutoa somo kwa mtiririko mzuri na sahihi. MAENEO YA MAHUBIRI. Kuna maeneo makuu manne ambayo mahubiri huhusisha.Mhubiri yoyote ni lazima azingatie maeneo hayo ili aweze kufanikisha mahubiri yake. 1: Wazo Hii huhusu namna ya kupokea kichwa cha somo au ujumbe.Ni ujuzi unaohusu namna ya kupokea ujumbe kutoka kwa Mungu.Ikimaanisha kwamba huhusu namna ya kupata wazo la awali la kichwa cha somo.Mungu hupanda mbegu wazo kuhsu somo au ujumbe siku kadhaa kabla ya mahubiri.Mbegu hiyo hukua kwa njia ya kutafakari na maombi zaidi.Kutokana na ujuzi mhubiri anaweza kuubua mstari.Mhubiri hupaswa kulieleza na kulikuza wazo lililopandwa ndani yake kwa njia ya maombi na kutafakari kuchunguza zaidi juu ya wazo hilo ili aweze kutayarisha ujumbe.Pata muda wa utulivu utulie uweponi na omba zaidi ya ufunuo huo. 2:Muundo. Muundo huhusisha uchambuzi wa wazo ili kuweza kukundua kweli zilizomo katika wazo hilo.Baada ya kupokea wazo toka kwa Mungu unapaswa uanze kulichambua ili kutambua vitu ambavyi wazo hilo linavyo.Katika hatua hii inapaswa kuorodhesha kwa urahisi kila kitu kilichomo kwenye wazo hilo.Mara nyingi unapokuwa katika hatua hii unahitaji kuandikwa kwa haraka ili kupata kwa kifupi mtiririko wa uvuvio unaokuja.Hakikisha kwamba unaandika kila kitu.Ili uweze kuchambua baadaye. 3:Ujenzi Ujenzi huhusisha kukusanya na kuyaweka mawazo yako uliyoyachambua katika kipengele cha uchambuzi na mpangimzuri ktakusaidia na kukurahisishia katika utoaji wa somo lako.Yaani kuwasilisha wazo lako.Kuwasilisha mawazo yaliyiendelezwa hufanyika msaada sana kwa wasikilizaji wako katika kuelewa na kufuata mpangi wako wa kufikiri.Somo likiwa limechanganywa litawawia vigimu wasikilizaji wako katika kuelewa somo hilo.Ujenzi wa somo hulifanya somo rahisi kiasi cha kueleweka vizuri na wasikilizaji.Ni muhimu sana kwa mhubiri kuliweka somo katika namna itakayofanya lieleweke kwa urahisi. 4:Mawasiliano Hii huhusu namna mhubiri anavyowasilisha somo au ujumbe kwa hadhira.Mhubiri anatakiwa kuliwasilisha somo lake kwa njia rahisi na nyepesi kueleweka na wasikilizaji wake. a.Kuwasilisha ukweli uliowazi na wenye kueleweka. b.Kutoa ujumbe kwa njia ya kuteka akili za hadhara c.Kuendeleza mawazo yako katika mpango ambao hadhara wataweza kuufuata kwa urahisi. d.Kuhamasisha hadhara kulitendea kazi somo lako.Yak 1:22. SAHEMU KUU ZA MAHUBIRI NA HOTUBA Kwa kawaida mahuiri au hotua yoyote ile ni lazima iwe na sehemu tatu amazo kwa pamoja huuda hotua au mahuiri hayo. Na sehemu tatu hizo ni utangulizi,kiini na hitimisho.Sehemu mojawapo ikipuuzwa yaweza kuvuruga au kuharibu kabisa ujumbe au hotuba. Utangulizi Hii ni sehemu ya kwanza ya hotuba. Utangulizi hutambulisha hotbuba au somo zima na kutoa picha jinsi somo litakavyokuwa. Utangulizi ni sehemu muhimu ya ujmbe na kama hadhira hawajakusikilza kwa umakini katika kipindi hiki cha awali yawezekana kutokuuelewa ujmbe wako au kutokukusikiliza vizuri katika sehemu zinazobaki za hotuba yako. Mara nygingi utangulizi huwa kama muhtasari wa ujumbe.Katika utangulizi mhubiri huwaeleza hadhira kwa kifupi juu ya kile ulichopanga kuongelea au kuhubiri. Mambo ya msingi katika uangulizi. a)Kuteka usikivu. utangulizi wako unapaswa utawale hamu na mawazo ya wasikilizaji. b) Kujenga masikilizano. Lazima ujenge mawasiliano kati yako na wasikilizaji. c) Kuleta kukubalika. Ni lazima utangulizi kwako ukujengee kukubalika kwa wasikilizaji. a. Unapaswa kupata usikivu wao, matumaini na heshima. d) Kujulisha. Utangulizi wako unapaswa kuwaeleza wasikilizaji kwamba somo lako lina husu nini hasa, na jinsi utakavyoliwasilisha. e) Kusadikisha. Ni lazima utangulizi uwasadikishe wasilizaji juu ya umuhimu wa ujumbe na kupata usikivu mzuri wa sehemu iliyobaki ya hotuba yako. f) Usitoe utangulizi kwa kuomba msamaha. Usiseme “Bahati mbaya sikujiandaa vizuri” a. Kufanya hivyo kutapoteza usikivu wa wasikilizaji wako na kukufanya usiaminike kwao. Sifa za utangulizi mzuri. a) Sio wa kishindo mno. Utangulizi uwe wa kiasi usiweke hatua ambayo huwezi kuifikia. b) Sio mrefu mno. Kumbuka kwamba utangulizi si ujumbe wote bali ni sehemu tu hivyo unapaswa kuwa mfupi. c) Utangulizi uendane na ujumbe. Utangulizi ni sharti ulenge kichwa cha somo. Waweza kuwa mhtasari wa somo au kisa ambacho kinaonesha ukweli wakile ulichokusudia kuongelea. d) Unapaswa kuandaliwa kwa uangalifu. Kwa sababu utangulizi wako ni kitu muhimu katika kuvuta usikivu wa hadhira unapaswa kuandaliwa kwa umakini sana. Tayarisha utangulizi wako kwa kujiuliza maswali yafuatayo a) “ Ningekuwa ni msikilizaji ujmbe huu nini kingenitvuta zaidi ili kuleta usikivu katika yote niliyokusudia kuyasema? b) “ Ni jambo gani hasa ambalo lngekaata usikivu wangu? Majibu yake unayoyapata ndiyo waweza kuyatumiak katika sehemu ya utangulizi wa ujumbe wako. Utoe nafasi ya kuptia kwenye kiini cha ujumbe.Utangulizi unapaswa kutoa njia ya kupitia kwenda kwenye kiini cha ujumbe. Kusiwe na pengo kati ya utangulizi na kiini cha ujumbe. 2.Kiini. Hiini sehemu kuu ya somo au ujmbe ambayo imebeba ukweli wote wa somo. Hatua ya kwaza kwenye kiini ni kutoa sekeletoni ya kiini na kisha hatua ya pili ni kuweka nyama katika skeletoni yako.Waweza kuweka nyama katika sekeletoni yako kwa kufanya yafuatayo: Kufafanua misamiati mbalimbali inayojitokeza kwenye kiini na kutoa maelezo ya dondoo ulizoziandaa. Tumia kamusi au itifaki ya Biblia katika kupata maana ya maneno hayo. Kutumia vielelezso.Unapaswa kutumia vielelezo mbalimbali vitakavyosaidia katika kulielezea somo lako au ujmbe wako. Waweza kutumia vielelezo vifuatavyo katika kulielezea na kufafanua ujumbe wako. Vielelezo binafsi. Wahusika mbalimbali katika Biblia wanaoweza kutumika katika kuelezea dondoo zako. Ukweli wa kitaalam mfano sayansi,historia, uvumbuzi, Tiba. n.k Hadithi zenye kufafanua somo lako.Usiwaachie hadhira kutoa fasili ya bali ifafanue mwenyewe. Unapaswa kukigawa kiini katika dondoo kwa kufuata mtiririko wa mawazo. Hubiri kwa kufuata mtiririko wa mawazo wa kimantiki. 3.Hitimisho. Hii ni sehemu ya mwisho ya hotuba au ujmbe lakini kipengele cha muhumi sana . Kipengele hiki kisipozingatiwa maana na malengo yote ya kuhubiri huvurugika na kutokuwa na maana. Hivyo ni lazima kipewe uzito unaostahili. Mambo ya kuzingatia. Tunia muda kidogo kwa kuuelezea ujmbe kwa kifupi. Kazia maeneo ya msingi unayofikiri kwamba hayakueleweka vizuri kwa hadhira wakati ukuhubiri na yale yanayotakiwa kupewa uzito maalumu. Pia waweza kurudia kuzitamka kwa sauti dondoo za ujumbe wako kila moja. Usiwachushe(bore) kwa kuanza kurudia kuhubiri ujumbe wako wote. Mwaliko. Mwaliko ni kipengele muhimu sana katika hitimisho. Kwa sababu mahubiri ni tofauti na iana nyingine za hotuba hivyo mwaliko huwa ni muhimu sana kwa kuwa mahubiri huhusu kuchukua maamuzi au hatua juu ya kile kilichohubiriwa. Mahubiri blia mwaliko huwa hayajafikia lengo la kuhubiri. Mwaliko ni lazima katika mahubiri ya aina yoyote ile. Mwaliko huwa ni wakati wa kuitikia Kile Mungu amesema kupitia mahubiri. Ni wakati wa kutendea kazi kile kilichofundishwa au kuhubiriwa. Mhubiri anapaswa kuufanya mwaliko kuwa wazi kwa wasikilizaji wote. Lengo la mwaliko si kuwaita watu madhabahuni tu bali ni kuwahamasisha watu kuweka ujumbe katika matendo. Pia Mhubiri hutakiwa kuuweka ujumbe wake katika matendo. 1. Ukihubiri uponyaji waite watu madhabahuni na waombee uponyaji. 2. Kuhubiri kutembea katika mamlaka unatakiwa udhihishe mamlaka hiyo. 3. Ukihubiri utoaji waite watu kumtolea Mungu. 4. Ukihibiri toba unapaswa kuwaongoza hadhira kwenye maombi ya toba na kuwaita madhabahuni wale wanohitaji kutengeneza kwa upya mwenendo na mahusiano na Mungu na kuomba nao. Wapeleke watu kwenye matendo na matumizi Mt 21:23. Yak 2:22. Unatakiwa kuwaongoza hadhira kuomba kwaajili ya ujumbe au somo kwa kadri ya maongozi ya Mungu na kwa kadri Mungu alivyosema na kila mmoja. Unaweza kuwaongoza watu waimbe wimbo unaoendana na ujumbe uili kuwaogeza uweponi na kuwapa hamasa. Toa mwaliko kwa watu ambao wanataka kuokoka na kama wapo omba pamoja nao. Baada ya hapo maliza na mkabiribishe anaehusika na ratiba inayofuata. Kwa kuhitimisha juu ya sehemu tatu za ujumbe au hotuba twaweza kuvifupisha vipenele vyote hivyo vitatu kwa sentensi tatu ambazo ni: 1. Waambie hadhira kile unachotaka kuhubiri.(Utangulizi.) 2. Hubiri kile ulichowaambia (Kiini), kisha: 3. Waambie kile ulichohubiri.(Hitimisho). AINA MBALIMBALI ZA MAHUBIRI. I. MAHUBIRI YA KIFUNGU. Aina hii ya mahubiri hujengwa juu ya kifungu kimoja kidogo cha maandiko tu. Huhusisha kuchagua maelezo fulani maalum ya maandiko na kuyachunguza, kuchambua na kugungua kweli zote zilizomo ndani yake na kuziwasilisha kwa waikilizaji kwa mtindo rahisi na wenye kueleweka. A. Faida za mahubiri ya Kifungu. a) Huvutia. b) Huzuia kutoka nje ya somo. c) Hufanya mahubiri kuwa ya ki- Biblia. d) Humwongezea mhubiri ujasiri. e) Husaidia wasikilizaji kulikumbuka somo. B. Jinsi ya kuandaa mahubiri ya kifungu.Kuna mambo kadha ambayo mhubiri anapaswa kuyazingatia wakati wa kuandaa mahibiri ya aya badhi ya mambo hayo yamejadiliwa hapa chini. 1.Soma Biblia mara kwa mara. Unapaswa kusoma Biblia mara kwa mara ikiwa unataka kuwa mhubiri mqwenye mafanikio katika huduma yako. -Tenga muda wa kusoma biblia kila siku. Beba Biblia ndogo kila mahali unapokwenda ili upatapo mua uweze kuisoma. 2. Jifunze Biblia. Kujifunza ni zaidi ya kusoma.Kujifunza kuna husiha kusoma Biblia kwa undani kwa kuchunguza kikamilifu kila kitu kilicha katika maandiko unayosoma na kutafakari kwa kina,.Yos1:8. Unapaswa kutafakari kwa uangalifu vitu unavyosoma. Viweke kwenye akiliyako na kuvifikiri tena na tena. Unapaswa kujizoesha kuchambua kile ulichojifunza. Baada ya kukichambua kwa umakini unapaswa kukiweka tena akilini. 2. Kuwa na Daftari la kuandikia. Kila usomapo Biblia yako jitahidi kuwa na kalamu na daftari la kuandika mambo muhimu un ayo jifunza.Jenga mazoea ya kuandika kwa ufupikila ufunuo unaoupata. 3. Dumisha hali ya maombi. Unapaswa kuwa katika hali ya maombi kila usomapo Biblia.Omba Mungu akufunulie upate kulielewa Neno lake.Pia unapaswa kumwomba Mungu akupe usikivu juu ya kweli anazokufunulia katika Neno lake. 4. Jenga usikivu.Unapaswa kuwa katika hali ya utulivu na usikivu katika nyanjazote yaani kimwili, kiroho na kisaikolojia. Mungu hutoa ufunuo wake kwa sauti ya kimya ndani ya roho ya mhibiri. Kama hunautulivu na usikivu wa kutosha ni vigumu kugundua maarifa hayo.. - C.Sifa za aya ya mahubiri Kifungu cha mahubiri au aya yapasa kuwa : a. Yenye mamlaka ya ki-Biblia. Mafundisho anayokusudia kuhubiri toka kifungu au aya fualni ya maandiko yapasa ikubaliane na ile biblia nzima inachofundisha. Katika mahubiri ya kifungu kuna uwezekano wa kuchukua kimakosamstari nje ya maana yake na kuutumia kufundishia kitu ambacho Biblia haikubaliani nacho. Ni Muhimu sana kwa ,uhubiri kujua jinsi mstari anaoshughulikia jinsi unavyokubaliana na kusudi la sura yote na kitabu chote. Daima mhubiri anapaswa kujitahidi kufasili aya yake katika nuru ya yale ambayo Biblia nzima inafundisha. b.Kamili. Aya yapaswa kuwa katika maandisha ya ukweli ulio kamilika. Baadhi ya wahubiri huchukua kifungu cha maneno katika mstari na kukitumia bila kujali maneno yaliyotangulia au yanayofuata. Jambo hili si zuri na huzaa mafundsho ya uongo. Na huku huitwa. “Kulichanganya neno la Mungu na uongo……..2Kor 4:2. Ni lazima uepuke jambo hili kwani litaleta kutokuaminika na maelezo yasiyo ya ki- Biblia na hatimae utawapotosha wasikilizaji wako. c. Fupi kiasi. Kifungu cha mahubiri chapaswa kitolewe kwenye maelezo ya maandiko ambayo ni mafupi nay a kulizisha. c. Ya kueleweka. Aya yapaswa kueleweka na iwe muhtasari wa kutosha wa kile unachotaka kukishirikisha. *Unapaswa ubaki katika mipaka ya kile ambacho aya yako inaelezea. D. Namna ya kuandaa mahibiri ya aya. a. Elewa maneno yake vema.Kipitie kifungu kwa kukisoma mara kadhaa, kitafakari na kujenga kumbukumbu juu yake na kiseme mwenyewe kwako. Hakikisha unakielewa vizuri. b. Elewa lugha yake.Tamabua lugha yake kama ina maana halisi au kama ni lugha ya mifanotu. Jiulize kama mwandishi alikuwa na maana hasaya kile alichokiandika au maneno yake yachukuliwe kama mfano wa mahubiri? c.Changanua ujumbe wake.Chambua uhjumbe unaoupata na kuutenga katika sehemu kadhaa zenye kulandana ili uweze kuuwasilisha kwa mtiririko mzuri. d. Chunguza maneno yake. Jitahidi kugundua kile maneno hayo yalikusudia kuwasilisha hapo awali. Ikiwa una kamusi ya kigiriki au Kiebrania unapaswa kulitazama neno hilo kwa lugha ya zamani au Kigiriki. Jaribi kubaini kama kuna maana maalumu ndani ya mneno unalolishughulikia. Kufanya hivyo kutakusaidia kugundua maaana yoyote maalumu ambayo mwandishi alikusudia kuiwasilisha. e. Tathmni mwendelezo wake. Baini kweli zile mwandishi alitaka kuzielezea. Tambua jinsi alivyo kamilisha katika kuziwasilisha kweli hizo. Jaribu kufuata mwongozo wake na kuuendeleza katika mtindo huo. f. Mkutadha wa kifungu.. i.Maneno ya mbele nay a nyuma ya kifungu. Angalia jinsi mistari iliyotangulia na inayofuata inachosema. Chunguza aya kushusiana na sura nzima ambayo umetoka. Chunguza kifungu hicho katika nuru ya kitabu kizima ambamo kinapatikana. Jifunze kiini na mazingira yote ya kitabu. ii. Hali ya mila. Je mila za wakati ule ziliathiri kile kilichoandikwa? Je watu walioandikiwa kifungu hicho awali wangekuwa na wazo la kile kilichoandikwa tofauti na ambalo tungepata katika hali yetu? Kama ndivyo nini ingekuwa maana inayolingana na sasa? ii. Hali ya kihistoria. Je jambo hili liliandikwa lini?je wakati huo ulishawishi kile kilichoandikwa? Je matukio ya kwakati ule yaliyokuwa yakijulikana wakati ule wa uandishi yalikuwa na maana maalum ju ya kile kilichosemwa? iv. Hali ya kijiografia. Mwandishi alikuwa wapi wakati anaandika maneno hayo?je Watu walioandikiwa walikuwa wapi?Je mazingira yao yana uhusiano wa chochote katika kle kilichosemwa? v. Biblia kwa ujumla. Kila sehemu ya maandiko ifasiliwe kwa uaminifu na kwa umakini ili ikubaliane na maandiko yote. Andiko lolote lisifasiliwe nje ya mkutadha wake. Maandiko ni lazima yatafsiri maandiko. E.Kupanga Maelezo. Mpanglio mzuru wa maelezo na kazi kwa ujumla ni wa faida sana kwa mhubiri. Hakikisha unapnga maelezo yako kimaantiki. Mpangilo mzuri wa kazi na mawazo humwezesha mhubiri kulielewa vizuri somo na kulishughulikia somo kikamilifu. Pia huwawezesha wasikilizaji kulielwa somo na kulikumbuka somo . 1. Ujumbe uwe katika mpangilio.Panga ujumbe wako katika mtiririko mzuri ili uweze kuufuata kwa urahisi wakati wa kuhubiri. 2. Weka ujumbe wako katika hali ya kueleweka. Jitahidi kukamilisha vipengere vyote unavyohitaji kuviongelea katika mahubiri yako.Kabla ya kupanda mimbarini. 3. Kazia katika mawazo. Unapaswa kuyaweka mawazo yakob katika sentensi fupi. Jifunze namna ya kuyaimarisha mawazo yako kwa pamoja nakuyaelezea katika sentensi fupi zinazoeleweka kwa urahisi.Jizoeze kupunguza na kulielezea wazo kwa sentensi moja. 4. Tayarisha maelezo mafupi.Kumbuka kwamba maelezo yako yako ili kusaidia kumbukumbu yako.unapaswa kuwa na vidokezo vitakavyosaidia kulikumbuka somolako au ujumbe wako. 5. Ufanye rahisi kuusoma. Ni vizuri kupiga chapa mahubiri yako ili uweze kusoma kwa urahisi wakati wa ukihubiri. Pia waweza kutoa vipeperushi navijarida kwa wasikilizaji wako ili waweze kufuatilia zaidi ujmbe au somo lako. Zoezi. 1. Eleza maana ya mahubiri ya aya. 2.Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya aya. 3.Taja mambo mengine muhuimu ya kuzingatia katika mahubiri ya aya au kifungu licha ya yaliyotajwa katika kitabu hiki. 4. Andaa hotuba ya mahubiri ya aya na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako. II. MAHUBIRI YA KUFAFANUA. Mhubiri ya kufafanua ni aina ya mahubiri ambaayo huhusisha kuchagua sehemu kubwa ya maandiko na kuicghunguza kwa undani na kuifasiri na kugungua kweli zilizomo katika sehemu hiyo ya maandiko na kushirikisha mkutano au usharika wako. Mfano unaweza kuamua kupitia Injili yote ya Luka sura baada ya sura. Kuanzia sura ya kwanza, unatafuta kufasili na kuelezea maana na umuhimu wake mstari kwa mstari sura kwa sura mpaka umeimaliza yote. Waweza kushughulikia sura moja kila wiki, na baada ya wiki kadhaa utakuwa umemaliza kitabu chote.Faida ya mahubiri ya ufafanuzi. Hufanya mahubiri kuwa ya ki-Biblia. 1. Yesu alitumia aina hii ya mahubiri. Alichukua kifungu cha Agano la kale na kufasili maana yake kwa wasikilizaji wake. 2. Petro alitumia njia hii siku ya Pentekoste. 3. Stefano alitumia njia hii. Huwezesha waamini kuwa na msingi na uelewa mkubwa wa Biblia.Waamini huimalisha na huwa na ufshsmu mzuri na wa kina wa Neno la Mungu. Kwani kweli zote zilizomo katika kitabu kilichopitiwa tayari hufahamika vizuri kwa usharika wote. Huvuta kuimalishwa na Roho mtakatifu. Roho mtakatifu hulithibitisha neno lake kwa ishara na miujiza sawasawa na Kweli zote zilizofunuliwa katika kitabu husika. Humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia. Mahubiri ya kufafanua humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia kwani mhubiri huhubiri kile kilicho katika maandiko ya eneo husika. Mhubiri huwa anajikita katika mkutadha wa aya, sura na kitabu chote kwa ujumla. Hivyo kiini cha kitabu ndicho ambacho hubeba mahubiri yake yote. Mambo ya kuzingatia katika kutayarisha mahubiri ya kufafanua. I. Kwa umakini cuagua kifungu cha maandiko kinachostahili. Hakikishwa kwamba kifungu hicho kitahudumia uzima na uwezo wa wasikilizajiwao. 1. Usichague somo kwa sababu linakuvutia au kukupendeza. 2. Usichage somo ambalo litazaa machafuko, mgawanyiko na mashindano. 3. JItahidi kufanyika njia ili Mungu akupitie ili Mungu akupitie ili aweze kuongea Neno lake kwa watu wake kwa kupitia wewe. 4. HIvyo basi unawajibika kutafuta kujua mawazo ya Mungu kuhusu watu wake ambao amekupa wajibu juu yao. 5. Huduma hii ni moja ya heshima kuu uliopewa lakini pia ni wajibu mkuu unaoogopesha sana. Hivyo basi unapaswa kuifanya kwa umakini wa hali ya juu. II.Tafuta ujumbe unaolingana na hali ya watu ya wakati ule. 1. Mungu kila mara huwa na ukweli wa sasa ambao hutaka kunena na watu wake. 2. Mungu hukusudia jambo maalum kwa kila kundi la waamini 3. Jifunze kujua kile Mungu anacho kwaaji ya kusanyiko kwa kilac wakati. III. Jifunze sura ya kitabu kwa umakini. 1. Soma sura unayo shughulikia mara nyingi mpaka umeielewa vizuri. 2. Soma kwa uangalifu mstari hadi mstari. 3. Kila kunapokuwepo na uhusiano wa wazi kati ya kifungu hicho na kifungu kingine unapaswa kusoma kifungu hicho ili uweze kupata maana zaidi. Maandiko hufasiri maandiko. 4. Jenga usikivu kwa sauti ya Roho mtakatifu ili kupokea ufunuo toka kwake. Tunia vitabu vya rejea ili kupatamsaada zaidi. Mfano. Itifaki ya Biblia, Kamusi ya Biblia, Biblia ya Tafsiri nyingine.Nk IV. Kusanya taarifa muhimu. Waweza kupata vitu vingine muhimu vya kuhusisha kwenye somo lako kwa kutumia mbinu ya maswali na majibu kama ifuatavyo. 1. Nimewahi kusikia au kusoma nini juu ya somo hili? 2. Roho mtakatifu amewahi kunionesha nini juu ya somo hili? 3. Nimewahi kuona nini chenye uhusiano na somo hili ? 4. Nimewahi kuwa na mawazo gani juu ya somo hili ? Naweza kupata habari zaidi ju ya somo hili kwa nani au wapi ? kueleweka. 5. V. Tambua kiini cha somo lako. 1. Daima tafuta kugundua kiini cha sura unayoshughulikia. 2. Tafuta kujua kile Roho mtakatifu alikusudia kuwasilisha alipoivuvia sura hiyo. 3. Gundua undani wa somo hilo. 4. Baini kile Mungu anataka kusema na watu wake kupitia sura hiyo. VI.Kuwa na Lengo kamili. Lengo lako daima lapaswa kuendana kikamilifu na lengo la Mungu. 1. Hakikisha kwamba Umegundua kile Mungu anataka kutoa kupitia maadiko hayo na kisha jizamishe katika kile Mungu anataka kufanya. 2. Unapaswa kuhisi kile Mungu anachohisi Mungu humshirikisha mhubiri moyo wake na akili yake ili waweze kufanya kazi pamoja. Unapaswa kuchangamka. 3. Fanyika chombo cha Mungu cha kupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu wake. 4. Kumbuka hukuitwa kushiriki mawazo yako na watu bali kuwashirikisha watu mawazo ya Mungu. VII. Zungumza kulingana na ujuzi wako mwenyewe. 1. Usitoe nadharia toa uhai. Hubiri kile ulicho na uzoefu nacho.kile ambacho umekifanyia kazi .wapaswa kuwa mtu kwa kwanza kula matunda ya kazi yako. 2. Umeitwa kuwa barua Sio tu kwamba unataikwa kuuhubiri ukweli bali pia unatakiwa kuufanyia mazoezi na kuuonesha kwa matendo. 3. Unapaswa kuwa mfano hai wa yote unayoyahubiri. VIII. Upe maana ujumbe wako. 1. Unawajibika kwa uwezo wako wote, kuhakikisha kwamba maana ya kweli na umuhimu wa maandiko unakuwa wazi. Na wakueleweka kwa wasikilizaji. 2. Daima jitahidi kuufanya ujumbe wako kuwa rahisi. 3. Hivi ndivyo Yesu alivyofanya Hii ilisababisha huduma yake kuwa na nguvu na mafanikio. 4. Alichukua mambo yaliyokuwa mafumbo na na akayaweka rahisi sana. 5. Wahubiri wengine huyachukua masomo rahisi sana na kuyafanya mafumbo magumu sana kiasi cha kutoeleweka kwa wasikilizaji wake au kuelewa kidogo. IX.Fanya ujumbe wenye kutekelezeka. 1. Daima unapohubiri jitahidi kuonesha wazi wasikilizaji wako jinsi wanavyoweza kuutendea kazi ujumbe wako. 2. Jitahidi kutoa ushauri wa kimatendo kuhusu watu wanavyotakiwa kumwitikia Mungu kwa namna ya kufaa. 3. Husianisha mahubiri yako na maazimio yako kimatendo ambayo yaweza kuwafanya watu kuwa watendaji wa Neno na si wasikilizaji tu. Zoezi 1.Eleza maana ya mahubiri ya kufafanua. 2. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya kufafanua. 3. Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya kufafanua. 4. Chagua sura mojawapo ya injili ya Yohana na kisha andaa mahubiri ya kufafanua kutokana na sura hiyo na kisha hubiri kwa dakika kumi. III. MAHUBIRI JUU YA MAISHA YA WATU. A.Utangulizi Hii huhusu hadithi ya maisha ya watu.Kwa hiyo njia hii huhusisha mafunzo juu ya maisha ya watu mbalimbali tunaosoma habari zao katika Biblia. Kila hadithi ya mtu iliyoandikwa katika Biblia ina umuhimu kwetu. Maisha ya kila mhusika aliye kwenye Biblia yana mafunzo kadhaa ambayo twaweza kujifunza. Kila habari iliyoandikwa kwenye Biblia ipo kutufundisha kitu fulani ambacho ni cha thamani sana. 1Kor 10:1-11. Mhubiri huchagua mhusika mmojawapo wa wahusika walio katika Biblia na kujifunza kwa kina kila kitu kilichotoke katika masiha ya mhusika huyo, tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Pia mhubiri hutakiwa kujifunza kuhusu nasaba na mbari ya mhusika huyo ili aweze kufahamu vizuri vitu vilivyomjenga na kumkuza mhusika, kisha hutayarisha mahubiri juu ya mhusika huyo na kuhubrikatika kusanyiko lake. Mafundisho ya wahusika wa Biblia ni ya kushangaza na ya kuvutia. Katkia aina hii ya mahubiri, mhubiri hupaswa kuchaqgua mhusika mmoja na kusoma habari zake zote zilizo kwenye Biblia na kisha huandikia kila wazo analolipata. Hapa mhubiri anapaswa kusoma kumbukumbuzote za mhusika katika Biblia. Baada ya kusoma kumbukumbumbu hizo unapaswa kuanza kuweka pamoja mawazo yote unayoyapata katika utaratibu wa miaka yaani jinsi matukio yalivyotokea ya mhusika huyo. B. Faida za mahubiri juu ya maisha ya watu. I.Hufunua ukweli wa maisha. Biblia imeelze wazi maisha ya wahusika kama yalivyokuwa pale kuficha chochote. Imeeleza mafanikio yao na madhaifu yao. Ukweli wa maisha ya wahusika umewekwa wazi na kwa uhalisia. Wengi wa mashujaa wa biblia wanahitilafu zao za kibinadamu.Twajua kuwa walikuwa wanadamu kama sisi na walikutana na majaribu kama sisi. Katika visa vyote vya historia kuna mtu mmoja mkamirifu ambae ni Yesu kristo pekee. Hata mashujaa wakubwa wa imani walikuwa na hitilafu zao. Hii inatupa kujua kwamba wao si tofauti na sisi. Ni mifano ya kujifunzia. Ni mifano na msada kwetu. Tunaweza kujifunza kutokananayo kuliko ujuzi wetu wa uchungu. C. Mambo ya kuzingatia a) Jifunze kuzaliwa kwa huyo mtu. b) Tafakali hali na mazingira aliyolelewa. c) Angalia uhusiano wake na Mungu katika maisha yake. d) Angalia jinsi alivyo wajibika kuhusu uhusiano wake na Mungu. e) Baini vitu alivyojifunza kutokana na mahusiano yake na Mungu. f) Tathimini mafanikio yake. Jifunze vitu vilivyomfanya afanikiwe. g) Tazama maeneo aliyokosea kama yapo. Na jifunze vitu vilivyomfanya akosee. h) Toa hitimisho kile tunachoweza kujifunza kutokana na maisha ya mtu huyo. Mambo hayo yote yanavutia na ni yenye vitu vingi vya Kutufundisha ambayo twaweza kujifunza kutokana na watu hao. Tunaosoma habari za maisha yao katika Biblia. D. Hatua za kufuata katika kuandaa mahubiri juu ya maisha ya watu. I. Chagua mtu au msusika toka kwenye Biblia. Unapaswa kuanza na watu mashuhuli katika biblia ambao habari zao ziko wazi kabisa.kama vile Ibrahimu,Musa,Samweli, Daudi, Yusufu, Debora, Miriamu, Mariamu, Dorkasi, Paulo, Petro. N.k. Hawa ni baadhi ya watu ambao matendo yao yameyanyika kuwa nuru katika historia ya dushusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Kuna mambo mengi sana ambayo twaweza kujifunza kutokana na maisha yao. Aina hii ya mahubiri ni nzuri sana, kujifunza toka kwa wacha Mungu wenzetu waliotutangulia katiki wito na huduma hii ni jambo la msingi sana. 1Kor 10.1-11. II. Chunguza maisha yake. Anza kwa kusoma hadithi inayoelezea kuzaliwa kwa mtu huyo. Tafuta maana ya jina lake. Kwani jina lina maana sana ki-Biblia. Angslia kwa umakini kusudi la Mungu katka maisha yake. Ili uweze kuvumbua vitu vingi unapaswa kujiulza mawsali fafuatayo: 1. Mungu alitaka kutekeleza nini kupitia mtu huyu ? 2. Je Mungu alifanya nini ili kusudi lake lijulikane kwa mtu huyu? 3. Mtu huyu aliitikia vipi Mungu alipomjulisha kusudi lake? 4. Tunaweza kujifunza nini kutokana na Mungu kuhusika katika maisha yake ? 5. Kuna tahadhari zozote ambazo tunapaswa kuzichukua ? 6. Je siri ya mafanikio yake ilikuwa nini ? 7. Je mwisho wa maisha yake ulikuwaje ? III. Chambua somo na kisha hubiri. Baada ya kujiuliza maswali hayo na kupata majibu utakuwa umepata vitu vingi ambavyo waweza kuvichambua kwa umakini na kuandaa somo kisha na kulihubiri somo hilo katika mpanglio na mtiririko Mzuri wwa mawazo. Mwombe Roho mtakatifu akupe ufunuo zaidi unapokuwaukihubiri somo lako na lifanye somo lako kuwa na uhalisia katika maisha ya sasa ya wasikilizaji. IV. MAHUBIRI YA MIFANO HALISI NA VIVULI. Huu ni ujuzi unaohusu kuweka wazi au kuchimbua na kuwasilisha kweli uliojificha wa mifano mbalimbali katika Biblia. Mfano ni kitu, mtu au tukio ambalo kinabii ni ishara ya kitu au mtu fulani.atakaetokea baadae. Inafanana au ni mfano wa Yule mtu au tukio. Katika matumizi ya biblia ina maana ya mtu wa bibliaau tukio litakaloonesha kitu fulani kitakachotokea. Mfsno mwanakondoo katika kitabu cha Kutoka ni mfano wa Bwana Yesu.Kila kitu kuhusu kondoo wa pasaka kiunabii kilkuwa na maana ya ukombozi ya wajibu ambao Bwana yesu Kristo angetimiza.Yn 1:29. Mifano ya biblia mara nyingi inaonekana kama kivuli(type) cha mambo yanayokuja baadae. Ebr 8:5,10:1. Siku takatifu pia katika agano la kale zilikuwa vivuli ju ya mambo ambayo yalikuwa yanakuja. Kol 2:17. Hizo siku takatifu hazikukamilika zenyewe sehemu ya kusudi la kutimizwa kwake ilikuwa ni kutanguliza sura ya kinabii ya vitu ambavyo vilikuwa bado vinakuja. Kanuni za kutumia. a. Unapojaribu kwa mara ya kwanza kufundisha kwa kutumia mifano ya kwenye Biblia, zingatia misingi ifuatayo. I. Tumia mifano rahisi zaidi. Anza na mifano rahisi mabayo maana yake iko wazi. II.Endelea na tafsiri ya wazi. Usijaribu kutafsiri kila kitu.Elezea ukweli wote kama ulivyo na wala si kutafuta kila kipengele chake na kukielezea kwa undani. III. Usitumie maneno makavu. Usitumie mifano ya kufundishia kama kanuni. IV.Sisitiza ukweli wa msingi..Usitumie nafai uliyonayo kwa kutoa mifano ya kufundishia. Mifano itumike kusisitiza mafundisho na si kutumia kama chanzo cha ukweli. V. Uwe tayari kusahihishwa. Uwe tayari kusahihishwa na kukosolewa na wale waliokomaa kuliko wewe ili uweze kujifunza zaidi. 4. Kuelezea kusudi. Ni njia ambayo kwayo mhubiri hupanua maana ya ukweli ulio katika kifungu maalum cha maandiko. Unatafuta naman ya kuuweka wazi ukweli ambao umejificha ndani ya kifungu. Hii njia nzuri sana ya kufundishia kusudi lote la ki-Mungu. Mdo 20:27. Hapa mhubiri aweza kuchukua kitabu cha Biblia na kuelezea maana yake sura baada ya sura. V. MAHUBIRI YA MADA. Aina hii ya mahubiri hukusudiakutoa kiini maalum kwa hadhira.Mhubiri huchagua somo fulani kisha huchunguza kila kitu ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo. Baada ya kuchunguza na kuchambua kweli hizo huandikwa katika mapngilo wa somo.Mhubiri hupitia vifungu mbalimbali vya maandiko vinavyohusu somo hilo. Aina hii ya amhubiri huhitaji maandalizi ya muda mrefu na utulivu mwingi. Pia huwasilishwa katika mfululizo wa vipindi kadhaa na si kimoja, kwa sababu ni vigumu kupitia kweli zote zilizo katika somo kwa kipindi kimoja tu. Mfano wa mada za kuhubiri. 1. Upendo wa ki-Mungu 2. Ubatizo wa Roho mtakatifu 3. Maombi ya kufunga. 4. Nguvu ya usaidizi. 5. Vita vya kiroho. 6. Kutambua Ulimwengu wa roho. 7. Kutembea katika mamlaka. 8. Nguvu ya madhabahu. 9. Kushughulikia majira na nyakati. 10. Kutii mamlaka. Mambo ya kuzingatia katika mahubiri ya mada. 1. Uwe na ufahamu kwa kutosha juu ya somo husika. 2. Fanya maandalizi ya mudamrefu nay a kina 3. Unapaswa kuwa na lengo mahususi la mahubiri yako. 4. Gawa somo katika vipengele vidogovidogo. 5. Kila kipengele laima kiwe na maandiko yanayokithibitisha na kukielezea 6. Andiko liendane na dondoo unayoitoa. VI.MAHUBIRI YA MATUKIO. Mahubiri ya matukio ni kipengele katika mahubiri ya maada, lakini kutokana na umhuhimu wake tumekitenga na kukielezea peke yake. Mahubiri haya ni mahubiri ambayo huandaliwa kutokana na tukio lilipoau ambalo litafanyika katika kipndi fulani. Kiini cha mahubiri haya huwa ni tukio ambalo linafanyika katika ibada hiyo.Mfano wa matukio hayo ni Tukio la, 1. Kusimikwa kwa uongozi wa kanisa. 2. Ndoa au kumuaga bibi arusi. 3. Kubariki watoto. 4. Ushirika mtakatifu 5. Kuweka wakfu vitu mbalimbali. 6. Kuhitimu mafunzo.(graduation) 7. Msiba na mazishi. 8. Sikukuu mfano Pasaka, mwaka mpya, N.k Mambo ya kuzingatia 1. Mahubiri haya yanapaswa kuendana na tukio husika. 2. Mhubiri anatakiwa kufahamu ratiba nzima ya tukio hilo au shughuli hiyo. 3. Mhubiri ahubiri kulingana na tukio husika. 4. Mhubiri aepuke kutumia muda mwingi katika mahubiri. 5. Mhubiri ahubiri kwa lugha itakayoeleweka na kusanyiko lote na lugha yapaswa kuwa rahisi. 6. Mahubiri yapaswa kugusa kusanyiko lote. 7. Mhubiri anapaswa kubiri kwa upendo. 8. Mhubiri azingatie ratiba ya tukio. 1. MAHITAJI YA MUHUBIRI: a. Anapaswa kuwa ameokoka yaani amezaliwa mara ya pili. a. anapaswa kuwa na wito kamili na uliowazi kwajijli ya kazi hii na sii taaluma tu. Anapaswa kuwa amejazwa Roho mtakatifu. Anapaswakuwa na wito uliowazi kwake na kwa watu wengine pia. 3. Mhubiri anapaswa kuboresha utu na wito wake kwa njia zifuatazo: I.kuwa na ushirika wa karibu na Mungu daima. a) Maombi na kutafakari Zab 1, Yosh 1:8. b) Kuishi maisha matakatifu. c) Kuwa mnyenyekevu daima. II Anatakiwa kujifunza daima. Neno la Mungu na vitabu vinginevyo vizuri. a) Panga muda wa kusoma (soma kwa bidii). b) Pata chakula kwajili yak o mwenyewe. c) Pata chakula kwaajili ya watu wengine. d) Hudhuria makongamano na semina mbalimbali. e) Jifunze toka kwa wahubiri wengine wakubwa na wazuri waliokutangulia. III.Jifunze kutokana na watu wanaokuzunguka na mazingira yao. a) Tazama na soma watu wanavyoishi, matatizo wanayokutana nayo. b) Fungua macho yako kujifunza kila mahali. IV.. Endeleza vipawa vyako vya asili. Kil;a mtu anacho kipaji cha asili. Ni muhimu kuendeleza kipaji ulichonacho kwaajili ya utukufu wa Mungu. Mfano wa viapji vya asili ni Kuimba, kupiga muziki, kushauri, n.k. Vipaji vyote vyaweza kuendelezwa kwa njia ya mafuzo na mazoezi. Hivyo hakikisha unakuza na kuendeleza kipaji chako cha asili. V..Tunza afya yako. Ni muhimu kwa muhubiri kutunza afya yake kwanibila kuwa na afya bora muhubiri hataweza kutimiza wito wake kwa ufanisi. Pai ni jambo jema kwa muhubiri kufuata ushauri wa kitaalamu yaani kuchunguza afya yake mara kwa mara ili kushugulikia mapema kama kuna dosari zozote za kiafya kiwa bado change. Pia ili muhubiri aweze kuwa na afya bora anatakiwa kufanya yafuatayo: i. kula chakula bora. ii. Kufanya mazoezi mra kwa mara. Mfano kukimbia, kuruka, kutembea, N.k iii. Kuwa na muda wa kupumzika.( Muhubiri ni lazima awe na muda wa kutulia na familia yake. Pia mhubiri anapaswa kuwa na likizo.) VI. Vipaumbele vya muhubiri. Unapaswa kutambua vipaumbele na uviheshimu ili uweze kuwa na ufanisi katika huduma na wito wako. Vpaumbele hivyo ni: a) Mungu. b) familia. c) Huduma d) Watu wengine. Kila kipaumbele kipe nafasi yake.Usipofanya hivyo utumishi wako utatyumba. VII. Ni lazima amtegemee kikamilifu Roho mtakatifu. “ Atatwa katika yaliyo yangu na kuwapa ninyi. Yn 14:26, 16:13-14. Hivyo ni lazima mhubiri ajifunze kumtegemea Mungu kiamilifu; a) Katika maisha yake ya kila siku. b) Katika masomo yake. c) . Katika maandalizi na matayarisho. - Katika kuandaa hotuba za kuhubiri. - Katika kuandaa matirio ya kutumia katika kuandaa hotuba zake. - Katika kuwasilisha hotuba zake. a) Kwa kutumia stadi na ujuzi pekee wa homiletics na akili yako pekee kusanyiko lako litabaki tupu na ukiwa. b) Ni Roho mtakatifu pekee anaewweza kumtia nguvu mhubiri kuufikia ushindi wa kiroho Mdo 1:8. c) Ni Roho mtakatifu pekee anaeweza kubadilisha na kuhuisha wasikilizaji wako. Yn 16:7-8. d) Mhibiri unapaswa daima kumtegemea kikamilifu Roho mtakatifu katika kazi na wito wako wa uhubiri. Hakikisha unashirikiana nae kikamilifu iliuweze kuwa na ufanisi katika wito na huiduma yako. *Roho mtakatifu aweza kuwa msaada kwa mhubiri lakini yeye ni kama hua…. MADA YA PILI. A. mhubiri ni mtangaza ujumbe wa Mungu. -Yeye ni msemaji wa Mungu. Husimama katika nafasi ya mungu na kuzungumza kwa niaba yake Mungu. B. Biblia ndiyo asili ya ujumbe. Ujumbe wowote uaouhubiri nilazima utokane na Biblia nje ya Biblia si mahubiri bali ni masimulizi tu. -Ikiwa kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu mhubiri anapaswa kwenda mahali Mungu alipoongea mara nyingi na waziwazi yaani “Biblia” Kwa njia nyingine kuhubiri ni kuipa Biblia sauti.ni kuacha Mungu aongee mwenye koa kwa Neno lake. Kwa nini Biblia peke yake? Kwanini si kitu kingine toka vitabu vizuri vya kikristoau toka magazeti au maelezo na masimulizi ya mtu maarufu na aliye mkuu. 1. Biblia ni maoni ya Mungu kwa kila jambololotelililotolewa. (Mhubiri aliye kuwa amekosolewa kwaajili ya hotuba yake alisema “hata mimi sikuipenda pia lakini haikuwa maneno yangu na nilikuwa sitoi mawazo yangu bali kile Mungu amesema katika Neno lake. Kwahiyo nilitoa mawazo ya Mungu na si yangu.). Kuhubiri hotuba ya ki-Biblia humpa mhubiri ujasiri mkubwa. Kutangaza kwa nguvu; • Biblia inasema …………………. • Mungu anasema………………… 2. Neno la Mungu lina nguvu. Wab 4:12. 3.Neno la Mungu ni kama mbegu.sBiblia hukutana na kila hitajila mwanadamuna matatizo yake yote yanayomkabili. 5. Inampendeza Mungu- Neno lake lililovuviwa amri yake ilikuwa wazi “Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi na muwafundishe kuyashika yote niliyowaamuru” 6. Roho mtakatifu hulithibitisha Neno la Mungu. C. jinsi ya kupata maandiko ya Kuhubiri. Mwombe Mungu Akupe ujumbe waq kuhubiri.kissha pokea andiko toka kwa Mungu kuhusu mahubiri hayo kwanini yeye Mungu anajua mahitaji ya watuya sasa yanayotakiwa kushughulikiwa D. Namna ya kutumia maandiko kwa usahihi. Kufasili na kutumia maandiko matakatifu kwa maana yake halisi ni kazi moja muhimu na takatifuambayo mhubiri anawajibu wa kuifanya. 1. Usipindishe wala kugeuza maana ya andiko ili kulifanya andiko likubaliane na mawazo yako. 2.Usichukue sehemu ya andiko na kuifanya iseme kitu ambacho hakiendani na mkutadha wake ambao ambacho mkuadha hauoneshi kuwa ni maana yake halisi. 3. Soma andiko kwa umakni (zingatia sarufi na misemo iliyomo katika andiko) na ulitafakari katika maana yake halisi. - Baini aina ya tungo zilizotumika na aina za maneno yaliyotumika kuunda tungo hiyo. -Tazama maneno maalumu(Key word)yanayotokeza katika andiko unalotafakari.Mfano DAmu, Msalaba, Yerusalemu N.k. -Kuwa makini kutazama tamathali za semi zilizotumika au kujitokeza. Mfano. Misemo, nahau, tashibiha, tashihisi tashititi, tafsida ,methali n.k. 4. Soma andiko katika mkutadha wake wa sasa. hapa unatazama mkutadha wa msitari, aya na sura ya andiko. 5.Soma andiko katika mkutadha wake wote. Hapa unatazama mkutaqdha wa kitabu. Waweza kutumia mAswali kadha katika kutazama mkutadha wake mfano Ninin dhamira ya kitabu au waraka huu wote? Tazama historia, jografia na utamaduni wa wakati wa Biblia hii daima yaweza kuwa msaada. * Daima kumbuka kuwa mafundisho ya Biblia yanapatana na hayapingani kamwe. Hayajipingi yenyewe kwa yenyewe lakini ufuno wake ni endelevu. *Mafundisho ya agano la kale ni lazima yafasiliwe katika nuru ya Agano jipya. Kushindwa kufanya hivyo kumesababisha kuzaliwa kwa mafundisho mengi ya uongo.(Religious cults). Mfano. Kutunza sabato, kutokula baadhi ya wanyama, Kuabudu sanamu, kuoa mitala N.k D. mawazo mawili potofu kuhusu mahubiri. Kuna dhana mbili potofu ambazo zinajitokeza katika uwanja na taaluma ya mahubiri mawazo hayo ni: a. Maaandalizi si lazima. Wazo la kwanzalenye makosa ni kwamba maandalizi si lazima na huonesha kukosa imani kwa mhubiri. Watu wenye kushikilia msimamo huu hufikili kwamba imani ya kweli hutupilia mbali jitihada yoyote inayojaribu kuandaa akili na hiyvo husimama mimbarini wakiamini kwamba Mungu atawapa maneno ya kusema.husimamia maawazo haya: i. Roho mtakatifu atakupa unachohitaji kuhubiri. Unapopanda mimbarini. _- Zab 81:10 “ Fumbua sana kinywa chako name nitakijaza”(Hutumia andiko hili kutetea msimamo wao.). Pia husema kwamba Yesu alisema kwamba “Msifikirifikiri nini cha kusema maana mtapewa kinywa cha usemi saa ili ilie mnapotakiwa kusema” Unapoyachunguza kwa umakini maandiko hayo utagundua kwamba maandiko hayo wanayafasili nje na mkutadha wake na na kulazimioshwa yaseme kile ambacho hayamaanishi. *Mahubiri ni kamana jengola kiroho ambalo linatakiwa kusanifiwa na kuandaliwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Roho mtakatifu ndiye mhandisi mkuu wa mahubiri. b. Uwezo wa mtu unatosha. Kuweka mkazo katika matayarisho na kutegemea uwezo wa kibidanu tu. Wahubri wanaoshikilia msimamo huu hudai kwamba maandalizi peke yake yanatosha na huweka mkazo kwenye matayarisho pekee.Kumtegemea Roho mtakatifu huwa ni kudogo sana au hakuna kabisa, bali tumaini la mtu binafsi ambalo ni matokeo ya kujifunza na kuendeleza uwezo wa asili. Ujumbe wa namna hii waweza kuwa mzuri kabisa lakini hauwezi kuleta matokeo yatakikanayo daima. Kwani ni Roho mtakatifu pekee ndiye anaeweza kuleta badiliko katika maisha ya waikilizaji wako. Bila yeye mahubiri huwa ni maiti na haiwezi kuleta uhai kwa sababu ni uhai wenye uwezo wa kuzaa uhai. *Roho mtakatifu huuhuishaujumbe na kuletaq matokeo yaliyokusudiwa na Mbingu katika maisha ya wasikilizaji. Ili mhubiri aweze kuhubiri sawasawa anapaswa kuwa na maansdalizi ya kutosha katika kuuandaa ujumbe wake kwa kusoma, kutafakari na kuchambua kweli zote zilizomo katika ujumbe wake. Lakini hayo yotec anapaswa kuyafanya akiwa katika hali ya maombi. Mhubiri anapaswa kumsikiliza Roho mtakatifu klwa kina na kupata uongozi kwake na kutaka Roho mtakatifu amshirikishe kile anachotaka kusema na watu wake na kukifanyia uchambuziyakinifu katika hali ya maombi ili aweze kukiwasilisha kwa ufanisi. • Mhubiri anapaswa kutambua kwamba yeye hana watu wala si Chanzo cha ujumbe. Kwasababu hiyo anatakiwa kumsikiliza mwenye watu na aliye chanzo cha huo ujumbe na kusimama katikati kwa uaminifu kuwafikishia watu kwa usahihi kile mwenye watu anachotaka kiwafikie watu wake. • Mhuibiri anapaswa kutambua kwamba kazi ya kuhubiri ni takatifusana na ni kazi nyeti ambayo yapaswa kufanywa kwa umakini, uaminifu na unyeyekevu mkuu. • Mhubiri mwenye kutegemea juhudi zake na uwezo wake wa asili atakuwa ni muhubiri kilema na halikadharika mhibiri mweye kutegemea kupewa ujumbe akiwa mimbarini atakuwa ni kilema. • Vyote viwili vyapaswa kwenda pamoja, maombi na matayarisho.Kwa sababu mahubiri ni matokeo ya mawasiliano na ushirika mzuri kati ya Roho mtakatifu na mhubiri. Aina za mahubiri. Katika kipenele hiki tutaeleza aina saba za mahubiri. Ni vizuri kwa mhubiri kufahamu aina zote za mahubiri. Hii itamsaidia kuwa na uhuru waq kutumia ainayoyote katika huduma yake na kufanya huduma yake kuwa ya kuvutia kwa watu wanaomsikiliza. 2. Mahubiri ya mada. Aina hii ya mahubiri hukusudiakutoa kiini maalum kwa hadhira.Mhubiri huchagua somo fulani kisha huchunguza kila kitu ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo. Baada ya kuchunguza na kuchambua kweli hizo huandikwa katika mapngilo wa somo.Mhubiri hupitia vifungu mbalimbali vya maandiko vinavyohusu somo hilo. Aina hii ya amhubiri huhitaji maandalizi ya muda mrefu na utulivu mwingi. Pia huwasilishwa katika mfululizo wa vipindi kadhaa na si kimoja, kwa sababu ni vigumu kupitia kweli zote zilizo katika somo kwa kipindi kimoja tu. SOMO LIMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA BISHOP RHOBINSON S.BAYE MKOLANI TEXAS MWANZA TANZANIA. 15/7/2021.

No comments:

Post a Comment

UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...