Wednesday, June 3, 2020

FUNGAMANISHWA NA MADHABAHU YA KWELI 2

Kutii Agano Au Maagano

Ndugu msomaji ukiwa Baba yangu,Mama yangu,Kaka yangu,Dada yangu,Rafiki yangu,aidha mmojawapo katika ukoo,na katika jamii,naamini bado hujapoteza mwelekeo.Bado tunayaona mambo Au vitu ili tuyafahamu na kuyajua mambo au vitu ambavyo vya weza kutufungamanisha na kusababisha kuwa na mahusiano na madhabahu ambayo yanamahusihano na roho wakweli.Katika kipengele hiki tutaona jinsi Agano na Maagano,yanavyoweza kukufungamanisha na madhabahu yenyemahusiano  na roho wakweli.

Agano Au Maagano Ni Nini?

Neno agano linatokana na neno la kiebrania Berith,lenye maana ya mapatano,makubaliano au mkataba unaofanywa baina ya pande mbili.Mapatano ni uwingi wa neno patano likiwa na maana ya (ulinganifu wa mawazo,au mtazamo,maafikiano,agano)Neno,Makubaliano,lina maana ya (suluhu baina ya watu wenye maoni au mitazamo tofauti)Neno (Mkataba)Neno hili lina maana ya makubaliano baina ya watu au vikundi viwili au zaidi ili kufanya jambo au kazi fulani).Maneno hayo matatu pamoja na maana ya maneno hayo yote,ukiyajumlisha yanaunda neno agano.Tena neno hili Agano kwa Kiyunani ni Diatheke, lenye maana ya urithi au Wosia.Kwa hiyo tena twaweza kusema agano ni mapatano yanayounganisha watu wa pande mbili pamoja.

3.Mungu ni Mungu wa Maagano.

Fahamu Mungu wetu ni Mungu wa maagano kwakuwa anaweza kufanyaagano au maagano na mtu mmoja.Ninamaanisha kwamba agano ni moja lakini maagano nizaidi ya moja,kwa hiyo waweza kufanya Agano au maagano na mtu au na Mungu.Kumbuka kwamba tunajaribu kuona jinsi mtu mwanadamu anavyoweza kujifungamanisha na madhabahu ya kweli.Mungu kwa kuwa ni Mungu wa maagano tutaona baadhi ya watumishi wake aliyofaya maagano nao.Mungu amefanya maagano na watu wengi Tunaowasoma katika Biblia na ambao hawajatajwa katika bibla yaani watu wa siku zetu,twaamini bado Mungu anaendelea kufanya maagano na watumishi na watu wake,Ingawa wana Theolojia wanaamini Maagano makuu matano tu,na moja kati ya hayo bado hawajakubaliana kwalo kuwa ni agano,bali waliowengi wanasema hilo likuwa agizo.Lakini ningetamani ufahamu kwamba hatufu

ati wala hatuongozwi na wana theologia na hatuishï na kufundisha imani na mitazamo na misimamo ya wana theologia,bali tunaishi kwakile ambacho Mungu amekuamuru tukiishi na kukiamini na kutekeleza .Katika kipengele hiki tunaona watumishi wa Mungu watano aliyofanya nao maagano.Fuata kama walivyoorodheshwa hapo chini.

a.Agano la Mungu na Adamu.

b.Agano la Mungu na Nuhu.

c.Agano la Mungu na Abrahamu.

d.Agano la Mungu na Musa.

e.Agano la Daudi.

g.Agano la Mungu na Ulimwengu.Agano Japya.

a.Agano la Mungu na Adamu.

Kama ambavyo tumeona hapo juu yakwamba katika Biblia Mungu wa kweli ni Mungu wa maagano ya kwelina Maagano au agano la Mungu na mtu mwanadamu,hujulikana na kufahamika kuwa ni agano au maagano katika namna mbili.1,Mungu hujitokeza kwa  mwanadamu mtu na kutamka kwamba imefanya nitafanya ilifanya agano au maagano na wewe au nanyi.2,Mungu hutoa husema na kutoa maelekezo moja kwa moja kama atakavyo na moja kwa moja yata sima kuwa agano au maagano.Katika Agano au maagano ya Mungu na Adamu kuna utata katika wanatheologia,baadhi huamini Mungu alifanya maagano na Adamu.Na wengine husema hayapo au halipo agano la Mungu na Adamu.Lakini mimi nami naamini nimejaa mafunuo ya roho wa Mungu;kwamba yalikuwepo Maagano kati ya Mungu na Adamu.Agano la Mungu na Adamu linapatikana katika Mwanzo 1:26-30   Mungu akasema,na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu,wakatawale samaki wa baharini,na ndege wa angani,na wanyama,na nchi yote pia,na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.Mungu aka umba mtu kwa mfano wake kwa mfano wa Mungu alimwumba,mwanamume na mwanamke,aliwaumba.Mungu akawaambia,Mungu akawaambia,Zaeni,mkaongezeke,mkaijaze nchi,na kuitiisha,mkatawale samaki wa baharini,na ndege wa angani,na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.Mungu akasema,tazama,nimewapa kila mche utoao mbengu,ulio juu ya mchi yote pia,na kila mti,ambao matunda yake yana mbengu vitakuwa ndivyo chakula chuo.

Mw 3:15-16,nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke,na kati ya uzao wako na wake,huo utakupota kichwa,na wewe utamponda kisigino.Hili la kuweka uadui kati ya uzao wa nyoka na uzao wa Wa mwanamke, ni agano la msingi sana.kwa kuwa ni agano la wokuvu katika Yesu Kristo.Ni agano ambalo liwekwa kwa misingi ya neema ya Mungu kwa Adamu,kwa kuwa mwanamke amekosa basi ataokolewa kupitia uzao wake ambaye ni Yesu Kristo ambaye hana sifa za kuwa na baba wa mwili.1Tim 2:14-15,Wala Adamu hakudanganywa,ila mwananke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.Walakini ataokolewa kwa uzazi wake,kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso,pomja na moyo wa kiasi.

b.Agano la Mungu na Nuhuna viumbe Hai.

Agano la Mungu na Nuhu halikuwa na masharti kati ya Mungu na Nuhu(hasa)na binadamu kwa ujumla.Baada ya gharika,Mungu aliahidi  mwanadamu kwamba hawezi kuihiribu tena dunia kwa mafuriko Mungu alitoa upinde wa mvua kama ishara ya agano,ahadi ya kwamba dunia nzima hakutakuwa tena mafuriko na ukumbusho kwamba Mungu anaweza na atahukumu dhambi.Mw 9:8-17,Mungu akamwambia Nuhu,na wanawe pamoja naye,akasema,Mimi,tazama,nathibitisha agano langu nanyi,tena na uzao wenu baada yenu.tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi,ndege na Mnyama wa kufugwa,na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi,wote wanaotoka katika safina,hata kila kilicho hai katika mchi.Na agano langu nitalithibitisha nanyi,wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika,wala hakutakuwa tena gharika,baada ya hayo,kuiharibu nchi.Mungu akasema,Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yagngu nanyi,na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi,kwa vizazi vyote hata milele,Mini nauweka upinde wangu winguni,nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.Hata itakuwa ikitanda mawingu juu ya nchi,upinde utaonekana winguni,nami nitalikumbuka agano langu,lililoko kati yangu nanyi,na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili,wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye wili.Basi huo upinde utakuwa winguni,nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano langu la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kichoko katika nchi.Mungu akamwambia Nuhu,Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi. 2Pet 2:5

c.Maagano ya Mungu na Abrahamu.

Maagano ya Mungu na Abrahamu,Mwa 12:1-3,6-7)13:14-17,)17:1-14)22:15-18.Katika agano hili,Mungu aliahidi mambo mengi.Mw 12:2,kwamba Ibrahimu angekuwa na wazao wengi wa kimwili.( Mw 13:16)Kwamba Ibrahimu angekuwa baba wa mataifa mengi.(Mw 17:4-5)Mungu pia alifanya ahadi kuhusu taifa liliitwa Israeli.Kwa kweli,mipaka ya kijiografia ya agano la Ibrahimu imewekwa zaidi ya mara moja katika kitabu cha Mwanzo.(Mw 22:7,13:14-15.15:18-21)Mpango na agano lingine ni kwamba kwa kupitia Ibrahimu mataifa yote yatabarikiwa. Mw 12:3.22:18

d.Agano la Mungu na Musa.

Agano la Mungu na Msa ,Kumb 11.agano la Mungu na Musa

lilikuwa agano la masharti ambalo lilisababisha baraka za Mungu kuwa laana ya Mungu kwa uasi kwa taifa la Israeli.Sehemu ya agano la Musa na Mungu Ilikuwa Amri kum 10)Kut 20:1- Napia sheria yote,ambayo ilikuwa na amri zaidi ya 600-karibu 300,nzuri na 300,hasi.Vitabu vya historia ya agano la kale(Yoshua na Esta)maelezo ya jinsi Israeli Ilivyoweza kutekeleza sheria au jinsi Israeli ilivyoshindwa kwa kusikitisha katika kutii sheria.Mw 11:26-28.

e.Agano la Mungu na Daudi.

Agano la Mungu na Daudi 2Sam 7:8-16,Agano hilo linaonyesha kipengele cha uzao”wa agano la Ibrahimu.Ahadi kwa Daudi katika kifungu hiki ni muhimu,Mungu aliahidi kwamba uzao wa Daudi utaishi milele na kwamba ufalme wakehautaondoka kabisa.Ni dhahiri,kiti cha enzi cha Daudi hajawahi kuwa mahali wakati wote,tena haitatokea mtu kutawala isipokuwa wa Daudi.Luk 1:32-34)

f.Agano jipya(Agano la Mungu na Ulimwengu.

Agano Jipya pamoja na mawazo ya watu na wenyeelimu wanatheologia kuwa na mitazamo na misimamo kuhusu Agano Jipya Agano hili mimi naamini agano hili ni agano la Mungu na ulimwengu,kwa maana ndilo agano la ukombozi wa ulimwengu na waulimwengu.Math 1:21,Naye atazaa mwana nawe utamwita jina lake Yesu maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao.

Yoh 3:16-18,Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee,ili kila mtu amwamiye asipotee,bali awe na uzima wa milele.Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili aukumu ulimwengu bali ulimwengu uokolewe katika yeye.Amwaminiye yeye haukumiwi,asiyeamini amekwisha kuhukumiwa kwa sababu hakuliamini jina la mwana pekee wa Mungu.

Tunaendelea kulichunguza agano Jipya.Je! Biblia inamaanisha nini inaposema agano jipya baina yetu na Mungu? Agano jipya ndilo jibu katika uasi wetu.Imeandikwa na Yer 31:33, Basi agano hili ndilonitakalofanya na nyumba ya Israeli,baada ya siku zile asema Bwana nitatia sheria yangu ndani yao na katika mioyo yao nitaiandika,nami nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu.

Agano Jipya laja na Yesu Kristo.Imeandikwa na Luk 22:20,Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula akasema ,kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu.

4.Namna ya kutii agano lako na madhabahu ya kweli.

Naamini nasema na mtu watu na kanisa na kondoo wa Mungu pamoja na watumishi wa Mungu pamja Na viongozi mbalimbali walioteuliwa,na watu waishio madhabahuni patakatifu.Ezekieli.45:1-8.Tena aamini kila asimamaye madhabahuni na kumwamini Mungu wa kweli na Yesu Kristo aliyetumwa na Mungu huyo analo agano au maagano na Mungu.Na kwa sababu unalo agano na Mungu nakupa mbinu Ya kutii agano maagano yako na Mungu na maagano ya Mungu na wewe.

a.Funga milango mitano ya fahamu.

Milango ya fahamu katika hali ya mwili.Milango yafahamu ni ogani za mwili zinazoturuhusu kujua na kuyadumu mazingira yetu kwa usahihi.Kibailojia inaeleza kuwa ogani yenye uwezo wa kupokea habari za nje ya mwili kama vile,Nuru,Sauti,Mwendo,Harufu,na Ladha,ili kuzibadilisha katika mfumo wa kiumeme inachukuliwa kwa njia ya mfumo wa neva hadi kwenye ubongu.Kuna milango mitano ya fahamu katika mwili wa mwanadamu ambayo ni Jicho/Macho(kuona)Sikio/Masikio(kusikia).Pua(kunusa)Ulimi(kuonja)Ngozi(kugusa).

1.  Kusikia ni  fahamu ya Sautikupitia masikio.

2.  Kuona ni fahamu ya Nuru kupitia macho.

3.  Kuonja ni fahamu ya ladha kupitia ulimi.

4.  Kunusa ni fahamu ya kunusa kupitia pua.

5.  Mguso ni fahamu ya nyuso za vitu kupitia ngozi.

Kama milango ya fahamu imeharibika,tunasema ni kipofu,bubu au kiziwi,ana matatizo ya kuelewa mazingira yake sawa na jinsi wanavyoweza watu wengine.Milango ya fahamu ni muhimu sana kwa viumbe hai kutokana na kwamba inasaidia kiumbe hai katika shuguli zake za kila siku,hata katika kutafuta mahitaji muhimu.

b.Mtu ni roho.

Kama tulivyoona katika sura ya kwanza yakwamba mtu ni roho ya roho tukimaanisha roho za viumbe ni roho za roho.Biblia inasema wazi kwamba hapo Mungu aliamua  kumuumba mtu kwa mfano wake Mungu na kwa sura yake Mungu mwenyewe kama tunavyosoma katika maandiko matakatifu katika kitabu cha Mw 1:26-27.Nataka ufuhamu kwa uhakika ya kwamba mtu anayeongelewa hapa ni roho na Sio mwili kama vile watu wengi wanavyodhani,unaposikia wewe ni mfano ni mfano wa Mungu.Basi fahamu mtu tunayesema ni mtu wa ndani (roho)ndiye mfano wa Mungu.Yoh 4:24.

c.Fahamu za rohoni.

Kama vile ulivyo mwili,mtu ambaye ni roho anazofahamu katika hali ya roho ambazo zinamuwezesha Kuelewa,kutambua mazingira ya rohoni kama vile mwili unavyoweza kutambua mazingira yake ya mwili.Fahamu zilizopo katika ulimwengu wa roho nikama zile za ulimwengu wa mwili zinazohusiana na Kugusa na kuonja na kusikia harufu.

1.Kuona rohoni(Macho ya roho)

Ili uelewe kupata uelewa sawasawa kwanza vuta picha ya mwanadamu mwenye macho ambaye anaangalia na kuona mambo mbalimbali katika maisha ya kawaida,macho yanampa uwezo wa kutambua wa watu na vitu.Kwa kutumia macho mtu anaweza kuweka kumbukumbu ya mauukio fulani katika ufahamu wake na mambo hayo aliyoyaweka yakamsaidia kuja kufanya maamuzi sahii au kuwasaidia wengine kufanya maamuzi sahihi katika maisha ya kila siku.Ndivyo ilivyo kwa mtu wa rohoni,na kufahamu vitu vya roho ni vilevile kuweka katika ufahamu wake kumbukumbu za rohoni kwa matukio aliyoyaona ili imsaidia katika kufanya maamuzi ya kiroho.Neno la Mungu linazidi kututhibitishia Kwamba yapo macho ya rohoni na watu wenye macho hayo wamefungwa wamepofushwa,macho yao Na hata hawaoni kama tunavyosoma habari ya mtumishi wa nabii Elisha katika 2Fal 6:15-17.Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka,na kwenda nje kumbe pana jeshi la watu,na farasi na magari wameuzingira mji ule.Mtumishi wake akamwambia,Ole wetu! Bwana wangu,tufanyeje? Akamjibu,Usiogope, maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.Elisha akaomba,akasema,Ee Bwana,nakusihi,mfumbue macho yake,apate kuona.Bwana Akamfumbua macho yule mtumishi,naye akaona,na tazama,kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.”Na amini umeona na kufahamu ya kwamba mtu Anaweza kuwa na macho na wakati huo asione kinachoendelea!kwa hiyo kuona kunafaa sana,lakini ili Ufikie hatua ya kutii maagano yako na Mungu nilazima ufungue mlango wako wa fahamu ya Nuru,yaani kuona.Ona katika macho ya ndani macho ya rohoni ili kuyatambua mambo ya rohoni.Mw 48:10.Kut 23:8.Am 16:28Math 6:22-23.

2.Kusikia rohoni (Masikio ya roho)

Katika hali ya kawaida,hali ya mwili wa damu na nyama,mwanadamu anakuwa na masikio ambayo yanaweza kuwa na uwezo wa kusikia au yasiwe na uwezo wa kusikia,kama masikio yakiweza kusikia hiyo Ndio sahihi lakini kama hatuwezi kusikia basi hapo kuna shida.Yaani inawezekana mtu huyu ni kiziwi au anayomatatizo yanayomzuia kusikia sawasawa.Katika ulimwengu wa roho yapo masikio ya rohoni yanayomwezesha mtu wa rohoni kusikia sauti za rohoni.Kama mtu hana masikio ya rohoni basi huyo ni Mlemavu wa rohoni na anahitaji kuponywa mlango huo wa fahamu ya sauti,ili aondoke katika ulemavu Huo.Ufu 1:9-11,1Sam 3:1-10,Isay 14:12-15. Tumeona jinsi masikio yalivyo muhimu katika hali ya mwili Na masikio ya ndani.Mimi kakuambia kwa funga mlango wa sauti ili upate kutii agano maagano yako na Mungu.Uwe kiziwi katika mambo ya ulimwengu wa mwili,na ulimwengu roho pia uwe kiziwi usizisikie roho za upotevu.

3.Kuonja rohoni(Ulimi rohoni)

Kuna watu wamekuwa wakiota ndoto ama wanakula wenyewe au wanalishwa katika ndoto vitu vya aina Mbalimbili,mwingine atakuambia nilipewa maji machungu kwenye ndoto au chakula kibaya sana kwe ndoto Au nilikula chakula kitamu kwenye ndoto.Kumbuka ndoto ni ulimwengu wa  roho.Kama inavyokuwa Katika hali ya mwili huu wa nyama na  kwamba unaweza kujua ladha mbalimbali za vyakula au vinywaji au chochote kinachoingia kinywani,ndivyo ilivyo na kwa ulimwengu wa roho.Unapokuwa rohoni Unaweza kutambua ladha ya vitu,kwani Biblia inatufundisha kwamba upo ulimi wa rohoni kama tunavyosoma katika Luk 16:22-24.Ikawa yule maskini aliďunga,akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu.Yule tajiri naye akafa,akazikwa.Basi kule kuzimu aliyainua macho yake,alipokuwa katika mateso,alisema, Ee baba Ibrahimu,nihurumie,umtume Lazaro achovye mcha Ya kidole chake maji,auburudishe ulimi wangu,kwa sababu ninateseka katika moto huu.Kumbuka Mfano huu aliutoa Yesu alikuwa anazungumzia habari za roho ya masikini.Lazaro na roho ya Yule tajiri Baada ya kufakwao,sasa tuna kumbe tajiri alihitaji kuburudishwa ulimi wake kwa tone la maji katika Ulimwengu wa roho

Mtu wa Mungu ukizidi kusoma neno la Mungu utafahamu kwamba mtu akiwa rohoni kwa kutumia mlango wa fahamu wa kuonja(Ulimi)anaweza kujua ladha ya vitu katika ulimwengu wa roho kama tunavyosoma katika Ezekieli 3:1-3,Akaniambia,Mwanadamu,kula uonacho,kula gombo hili,kisha enenda kusema usema ukaseme na wana wa Israeli.Bas nikafunua kinywa changu,naye akanilisha like gombo akaniambia,Mwanadamu,lisha tumbo lako,ulijaze tumbu lako kwa hili gombo nikupalo.Ndipo nikalila,nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu,kama utamu wa asali.

Kumbe nabii wa Mungu Ezekieli aliweza kula na kutambua ladha ya gombo kuwa lilikuwa na utamu wa Asali.Kwa hiyo nikushauri kwamba funga mlango wako wa fahamu ya ladha kupitia ulimi kwa kutuonja ladha ya roho ya upotevu.

4.Harufu ya rohoni( Kunusa rohoni)(Pua)

Ukiwa katika hali ya mwili na kama hauna kasoro zozote katika pua zako,unaweza kufahamu,kutambua Harufu za aina fulani na ukaziweka katika kumbukumbu zako na zikakusaidia katika kufanya maamuzi katika siku za mbeleni,na siku ukinusa hata pasipo kuona utatambua kwamba kuna kitu kinaungua,hivyo Ndivyo ilivyo kwa jinsi ya rohoni.Kama pua zako za kiroho zinafanya kazi sawasawa unaweza kugundua mambo ya rohoni hata kabla ya kuyaona.2Kor 2:14-16,Ila Mungu ashukuriwe,anayetushagaza daima katika Kristo,na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yenu.Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo,Mbele za Mungu,katika wao wanaokolewa,na katika wao wanaopotea,katika hao wa pili harufu ya mauti iltayo mauti,katika hao watkwanza harufu ya uzima iletayo uzima.Naye Ni nani atoshaye kwa mambo hayo.

Mtume Paulo akiwa amejaa Roho Mtakatifu anaongelea habari ya manukato katika ulimwengu wa roho,maana yake ni kwanba mlango wako wa fahamu wa kunusa (Pua) wa rohoni unafanya kazi sawasawa.Hi ndio sababu Mtume Paulo anazungumzia harufu za aina mbili yaani harufu ya mauti na harufu ya uzima.

Vilevile tunamuona Yohana akiwa rohoni anatambua kwamba maombi ya watakatifu yalikuwepo kwa Mungu kwenye mabakuli kama manukato,aliweza kujua kwamba yale maombi ni manukato kwa waana Yake mlango wa Yohana wa fahamu katika katika kunusa ulimfahamisha kwamba yale ni manukato kwa  kunusa.Ufu 5:8,Hata alipokitwaa kile kitabu,hao wenye uhai wanne na wale wazee na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo,kila mmoja wao ana kinubi,na vitasa vya dhahabu vilivyojaa Manukato,ambayo ni maombi ya watakatifu.Hii inazidi kututhihirishia kwamba ukiwa unaweza kunusa Kutambua harufu ya sadaka inayompendeza Mungu au la.

5.Kugusa,kuguswa rohoni.( Ngozi ya kiroho.

Siku moja Yesu alikuwa katika huduma ya kuhubiri injili watu wengine walimsonga huku na kule pengine wengine walimvuta na kumuita ili awaponye.Lakini kuna mwanamke mmoja ambaye aligusa Vazi la Yesu kwa imani na Yesu akatambua kuna mtu amemgusa na kuuliza kwamba ni nani huyo kama Ilivyoandikwa katika Luk 8:43-46,Na mwanamke mmja,ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi  na miwili,alikuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga asipate kuponywa na mtu ye yote,alikwenda nyuma yake,akamgusa upindo wa vazi lake,na wara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.Yesu akasema,Ni nani aliyenigusa? Basi watu wote walipokana,Petro akamwambia,Bwana mkubwa,makutano haya wanakuzunguka na kusonga.Yesu akasema,Mtu alinigusa,mama anaona ya kuwa nguvu zimenitoka.Swali la msingi sana la kujiuliza hapa ni hili Yesu aligunduje kwamba ameguswa Na nguvu zimemtoka wakati alikuwaamezongwa na watu wengi?.Iweje mtu mmoja amguse na afahamu dhahiri na kusisitiza kwamba ameguswa?.Kwa uhakika kabisa mama yule alimgusa Yesu kwa imani kutokea rohoni na kwakuwa Yesu alikuwa wa rohoni alitambua mara ile ile,alitambua kwakuwa alitumia Mlango wa fahamu wa rohoni wa kugusa na kufahamu kwamba kuna mtu amemgusa.Katika Ufu 1:17,Nami nilipomwona,nalianguka miguuni pake kama mtu aliekufa.Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu,akasema,usiogope,Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,”Yohana alitambua kwamba Yule mtu ameweka mkono juu yake kwakuwa akiwa rohoni mlango wake wa ufahamu ulikuwa ukifanya kazi.

Naamini umeelewa vizuri milango ya fahamu inavyofanya kazi na ilivyo muhimu kama yote iko imara na Ikitumiwa vizuri.Milango hiyo mitano ya fahamu ukiifunga isiwe wazi kwa mambo ya ulimwengu utakuwa mtiifu wa maagano yako na Mungu na  utafungamanishwa na madhabahu yenye mahusiano na roho wa kweli.

 

Kimeandikwa na

Bishop. Rhobinson S.Baiye.

rhobinsons.blogspot.com

rhobinsonsaleh1@gmail.com

Whatsapp.0764127531

Mwanza Tanzania.

 

 

 

 


No comments:

Post a Comment

UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...