MAOMBI YANAYOJIBIWA
Ndungu msomaji
naamini unashauku ya kufahamu mengi kihusu maombi.Lakini katika kitabu hiki
tutajikita katika mada hii isemayo maombi yanayojibiwa.Kwa maana watu wengi
huomba lakini hawapati majibu ya yale wanayo ya omba, na hilo huleta maswali
mengi katika ucha-Mungu wao na utumishi wao.Na walio wengi usema na kujiuliza
je,kweli Mungu anajibu maombi ya watu? Ni kweli Mungu hujibu maombi kupitia
jina la Yesu Kristo.Yohana 14:13-14. Na hivi karibuni tutatafakari kuhusu
maoombi yasiojibiwa kaa mkao wa kupokea.Lakini fahamu kwamba kuna aina nyingi
za maombi.
Maama Ya Maombi
Maombi ni mazungumzo yenyemahitaji muhimu kati ya
mtu na Mungu au kati ya Mungu na mtu.Mwanzo
1830-33,45-1-20
5.Namna Ya Mungu Kujibu maombi
Mungu
wetu na Bwana wetu Yesu Kristo wametujenga kwa hadi ya kupokea majibu chanya ya maombi
mahitaji yetu kutoka kwao,kama tuliwakilisha mahitaji yetu kulingana na
utaratibu wa ki-Mungu majibu ya maombi hujibiwa.Lakini nakuomba ufahamu kwamba
mara nyingine Mungu atakupa kitu au vitu
vizuri tofauti na ulivyotarajia.Inawezekana ukaomba Mungu kwa kitu
unachofikiria ya kuwa ni kitu kizuri ambacho kitakacho mtukuza Mungu,lakini
yeye ni Mungu ajuaye kila jambo,anafahamu kile uombacho kitaumiza kiasi gani
kazi zake na hata sisi vilevile.Mungu hupenda sisi watoto wake na anajua muda
na kitu fulani cha kutupatia kilicho kizuri kitakacho kuwa baraka kwetu na
kumtukuza Mungu.Mara nyingi hujibu maombi yetu si kwa kadri tulivyohitaji
lakini kwa njia bora kuliko yale tuliyoyaomba.Tunaweza kuona jambo hili kwa
baadhi ya watumishi wake.Paulo alikuwa na udhaifu mwilini mwake ambao ulimtesa
sana.Na alifikiri udhaifu huu ulikuwa kikwazo katika huduma yake,na aliomba
mara tatu Ili udhaifu huu umtoke.bali Bwana hakuruhusu udhaifu huu kumtoka
Paulo haijalishi aliomba.Bali Mungu alimjibu Paulo kwamba neema yake Mungu
inamtosha.Na hapo Paulo alibadilisha maombi na akaanza kushukuru Mungu kwa
udhaifu huo.2Kor 12:7.Mara nyingi Mungu hatuondoi katika taabu yetu wakati
tunapomwomba kufanya hayo.Halafu hutupa nguvu za kumtukuza hata tukiwa katika
taabu yenyewe.Na tunamshukuru katika mambo yote.
1.Kwa
ahadi.Isaya 58:9.Yer 29:12.Math 7:7
2.Mara
kwa ghafla. Dan 9:21,23.10:12
3.Kwa
baadae Luk 18:7.1Fal 18:42-44.Dan 10:12
4.Kwa
hali usiyoitegemea.2Kor 12:8-9
5.Vyema kuliko tegemeo letu au kuliko tulivyofikiria.Yer 33:3 Efe 3:20.
Ilimaombi yako yajibiwe Fanya Yafuatayo.
Kwakuwa
kanisa na mtu binafsi hupenda kupata majibu chanya ya Maombi yao waliyo
wakilisha mbele za Mungu, ni vyema maombi yaombwe katika utaratibu huu.
1.Omba
Kupitia Jina La Yesu Kristo.
2.Omba
Kwa Imani Na Matumaini
3.Omba
Kwa Kumaanisha.
4.Omba
Kwa Wakati Uliokubalika.
5.Omba
Kwa Utaratibu.
Mungu
wetu niwautaratibu,kwahiyo mambo yote yatendeka kwa uzuri na kwa utaratibu
ukiwemo utaratibu wa kuomba.
1.Omba Katika Jina Langu
Yatupasa
kuomba katika jina la Yesu Kristo.Hilo nitakwa la Yesu Kristo mwenyewe.Yohana
11:13.14:13-16.15:7,16.16:24-26.Tukiomba
katika jina la Yesu Kristo
tutampendeza Mungu na Kristo pia.Unaweza kujiuliza kuomba katika jina la
Yesu humaanisha nini?.Kuomba katika jina la Yesu Kristo lina maana ya kuomba
kwa kutamka maneno yanayopatana na mapenzi yake.Ukitamka au ukisema neno au
maneno kupitia kwa jina lingine maombi hayo hayawezi kumfikia Mungu kwa kuwa
Yesu Kristo ndiye njia ya kweli na uzima.Ifahamike kwamba tunayemwomba
atutimizie mahitaji yetu ni Mungu lakini yatupasa maombi yetu yapitie katika
jina la Yesu Kristo wala si vinginevyo.Kuna baadhi ya Madhehebu ya ki-kristo
yamebuni majina mengine na kuyapa heshima ambayo hayastahili kupewa heshima
hiyo,kwa maana hata majina hayo hayajatajwa na Biblia kwa heshima hiyo wana
jifariji na kudanganya nafsi zao wenyewe. Kwa mfano heshima ya kupindukia kwa
Bikira Mariamu,pamoja na watakatifu ambao wana watakasa wao hayo yote ni
kujidanganya na kujifariji.Atambuae na kumtakasa mtu ni mtu mwenyewe na Mungu
tu.
2.Omba Kwa Imani Na Matumaini.
Walio
wenye haki wataishi kwa imani na matumaini.Mark 9:23.Math 17:20.Ebr 11:1,6.1Kor
2:4-7,8-16.2Kor 5:7.Ebr 12:2.Rum 1:17.Habakuki
2:4.Efe 2:8-9.Rum 10:17.Yak 1:22-25.Inatupasa kuomba kwa imani na
matumaini makubwa ya kupokea kile tulicho kiomba kwa Baba.Baadhi ya wacha Mungu
wanaomba lakini wana imani haba na hupoteza matumaini.
1.Omba Kwa Imani
Tunaweza
kusema kwamba imani ni njia ya kupokea kutoka kwake Mungu.katika waefeso tunaona kwamba tumeokolewa kwa neema,kwa njia
ya imani,Efe 2:8-9.Ebr 11:1,6.Tunaweza kueleza maana ya imani kwa
njia tofauti lakini inamaanisha kuwa njia rahisi ya kutazama imani na hata
kujichunguza kuona kama tuna imani yenye
nia na matumaini ya upokeaji.Tukitathimini mioyo yetu ni shughuli muhimu wakati
tunapoanza safari hii ya matumaini pamoja,kwa sababu kumtumainia Mungu na kuwa
na matarajio mazuri yanaleta uhusiano wa karibu sana na imani.Tunaweza kusema
kwamba kiwango chako cha matarajio ndicho ndicho kiwango chako cha
imani.Nionyeshe mtu mwenye matarajio madogo,nami nitakuonyesha mtu anayetumia
imani haba.Tena ionyeshe mtu mwenye matarajio makubwa na nitakuonyesha mtu anayetumia imani kubwa
ya kijasiri.Kumbuka tunaongea kuhusu kuwa na matarajio yetu katika Mungu.Hiyo
ni zaidi ya kuwa na mtazamo chanya;ni kumtegemea Mungu akutunze pamoja kila na kitu kinacho kuhusu.Neno la
Mungu linatwambia kwamba imani yetu matarajio yetu chanya,yenye matumaini
humpendeza Mungu.Ebr 11:6.na mara kadhaa katika Injili tunamwona
Yesu akichochewa kutenda jambo kwa sababu ya imani na matarajio ya wale
aliokutana nao.Math 9:29,Marko 5:34,Luk 7:50.Mungu yuko upande
wako na ana mpango mzuri katika maisha yako.Unapojaribiwa na kuwa mwenye
mashaka,na kukaribia kukata tama na kukaribia kufa moyo wewe amini na kuwa na
matarajio ya kupokea.Utafaulu kulingana na kiwango chako cha
matarajio.Usichukulie kuwa kule ulikotoka na hapo ulipo,kwamba hapawezi
kubadilika.Si kwamba mpango wako ni mbaya zaidi la hasha bali ni kwamba mpango
wa Mungu ni mzuri zaidi.Kwa hiyo omba kwa imani kubwa sana,utapokea.Mungu
hufanya zaidi ya kukushikilia usianguke;na kisha hukupeleka juu zaidi ya pale
ulipokuwa mwanzoni.
2.Omba Kwa Matumaini
Mara
kwa mara waliowengi huhisi kuwa mtu akitarajia zaidi ya alivyo navyo basi huyo
ni mlafi na mkosaji.Ijapokuwa ni kweli kwamba wakati wote tunapaswa kuridhika
na kutosheka na vile tulivyonavyo.Hivyo haimaanishi kuwa kuhitaji kuwa na vitu
vizuri zaidi ni dhambi au makosa ilimradi tuna sababu mzuri ya kuvitamani
na kuvitumia.Tunaweza kutosheka na huku
bado tunahitaji kuwa na vingi zaidi.Mimi Bishop Rhobinson Saleh Baiye sasa hivi
ninatosheka sana na kila kitu katika maisha yangu kwa sababu ninaamini wakati wa
Mungu maishani mwangu ndiyo mzuri zaidi.Ninaweza kufurahi hata kama sina kitu
chochote cha ziada kwa sababu furaha yangu na kutosheka kwangu viko katika
Kristo.Hata hivyo,wakati huo huo ninahitaji kuwa na vingi vizuri zaidi kwa
sababu ninahitaji kuendelea katika maisha kadri Mungu atakavyoniruhusu na
nimfanyie mengi zaidi isipokuwa maisha mazuri zaidi ambayo Mungu anakata
kunipa.
Ezekieli 37:11,Isaya 57:10,32:17,20:5,29:16,1Kor
9:10
3.Omba Kwa Kumaanisha.
Walio
wengi wanaomba sala na dua ndefu pasipo kumaanisha wanachohitaji.Ni vyema
kufahamu tunapoomba kumaanisha kile tunachohitaji.kwahiyo tamka kwa ufasaha
kile unachohitaji.1Timoth 2:1-4.Luk 10:2.1The 3:1.Mark 8:22-23.10:46-52(50-52)
walio wengi huogopa kuomba baadhi ya mahitaji yao muhimu.lakini fahamu ya
kwamba Yesu alisemaje kuhusu kuomba kwetu? Yesu alikuwa akiwauliza baadhi ya
watu waliyo mwendea na kusema wataka nikutendee nini? Alikuwa akihitaji musika
amaanishe kile anachohitaji kutoka kwake Krsto.Sikiliza jinsi Yesu Kristo
alivyo tufundisha kuomba kwa kumaanisha kweli kweli.Ikiwa Yesu Kristo
alipokuwa mahali fulani akiomba,alipokwisha,kuomba mmoja katika wanafunzi wake
alimwambia,Bwana tufundishe kuomba kama vile Yohana alivyo wafundisha wanafinzi
wake.Yesu Kristo akawaambia
msalipo semeni hivi,Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe,Ufalme wako
uje,[Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni.] utupe siku kwa
siku riziki yetu.Utusamehe dhambi zetu,kwa kuwa sisi nasi tuna wasamehe
waliyotukosea.Na usitutie majaribuni lakini utuokoe na Yule mwovu kwa kuwa
ufalme na nguvu na utukufu ni wako hata milele amina.
Ukifanya
uchambuzi na kutafakari kwa
makini,utagundu
a kwamba Yesu Kristo aliwafundisha jinsi ya kuomba kwa kumaanisha , kile unachokiomba na kwa Yule unaye mwomba,na kwa muda unaohitaji.Haijalishi Mungu anajibu na kufanya kwa muda wake,cha muhimu ni wewe kumaanisha kile ukiombacho na kwa Yule umwombaye.Wewe omba kwa maana Yesu Kristo alisema kwamba tutafanyiwa kila tunacho kiomba kwa jina lake ili Baba Mungu atukuzwe na ndani ya Mwana.Yohana 14:13.
Kama unahitaji chakula wewe omba Mungu kwa kumaanisha Mungu baba nakuomba chakula baba yangu na ni vema kumaanisha chakula unachohitaji si kwamba tu umetamka chakula fahamu kuna aina nyingi za vyakula hapa duniani,waweze kutaja baadhi ya vyakula unavyovifahamu utaona na kujua ni aina nyingi tu.wewe maanisha kila unachohitaji kutoka kwa Mungu kupitia jina la Yesu Kristo wa nazareti.Zaburi 40:8.Math 6:33
Maanisha kuomba msamaha kwa maana tunasamehewa kwa kuwa tuna wasamehe wengine.Yesu Kristo alisema wazi kwa kumaanisha kabisa ya kwamba tutasamehewa tukiwasamehe wengine.Maanisha kuutukuza utukufu wa Mungu katika kuomba kwako.Kama unahitaji kuponywa magojwa maanisha,kama unahitaji utajiri maanisha ,kam,
Unahitaji
mifugo,magari,mashamba,kama unahitaji kuwekeza majini maanisha,maanisha
chochote unachohitaji mungu atakutimizia.Usiombe kwa kumungunya maneno tamka na
kumaanisha.
4.Omba Kwa Wakati Unao kubalika
Omba
kwa wakati unaokubalika na Mungu.sio kilamuda ni wakuomba,tafuta muda
wakuomba,hasa muda ambao dhamiri zako zinahitaji kuomba.Mara nyingi baadhi ya
wakristo hujiuliza kama ni vyema kuomba mara kwa mara? au inampasa kuomba mara
ngapi kwa siku au kwa wiki au kwa mwezi au kwa mwaka? Kwa nini umeupa moyo wako
kujiuliza swali kama hilo? Je hujiamini unapo mwendea Mungu? Je wewe umechoka
kulalama mbele za Mungu ?Biblia inasemaje kuhusu kuomba kwetu. Omba bila
kukoma.Ni kweli kwamba kuna watu huwa wanachoka haraka wakati tunapoomba au
tunapowasilisha mahitaji yetu mbele za Mungu.Na tena hujihisi kwamba wameomba
vitu vingi au wameomba mara nyingi.Si hivyo alivyo Mungu wetu,anapoona na
kusikia maombi yetu mara nyingi anafurahi sana kuona tunamtegemea na kuwa
wahitaji kwake.Kwa sababu Mungu wetu ni wautaratibu basi yatupasa kuwa na
utaratibu katika kuomba kwetu.Danieli,aliomba mara tatu kwa siku Dan
6:10.Daudi,aliomba mara tatu
Zaburi 55:17. Bwana wetu Yesu Kristo alisema ya kwamba yatupasa kuomba
siku zote.Luka 18:1Katika 1Th 5:17 Tumeagizwa kuomba bili kukoma hapo tunahimizwa
kuomba muda wowote na uombe kwa mahitaji yako mwenyewe na watu wengi
vilevile.Maandiko yanasema tudumu katika kuomba Kolosai 4:2
1.Omba
Asubui
2.Omba
Mchana.
3.Omba
Jioni. Danieli 6:10
4.Omba
Usiku Zaburi 55:17.
5.Omba Kwa Utaratibu.
Fahamu
unapoomba unamfanyia Mumgu ibada.Unapokuwa katika ibada ya maombi na maombezi
fata utaratibu wa Mungu.Kuna baadhi ya wanaojiita waombaji lakini ukiwasikia
wanavyoomba hawana mpangilio wa kuomba kwao.yanayofaa kutangulia kutamkwa
yanatamkwa mwishoni mwa mazungumzo.Yale ambayo yangetamkwa mwishoni yanatamkwa
mwanzoni mwa mazungumzo yao na Mungu.Mungu wetu aliumba kwa kuweka mambo yake
katika mpangiliyo na utaratibu uliyotukuka.Mwanzo 1:1-2:1-
1.Tamka
Maneno Ya Kumshukuru Mungu.
2.Tamka
Maneno Ya Kumsifu Na Kutukuza Mungu.Tamka Maneno Ya Toba Na Kuomba Msamaha Kwa
Mungu.
3.Wakilisha,Mahitaji
Omba Unalohitaji Kutendewa.
5.Msikilize
Mungu Kwa Kukaa Kimya Kusubiri Majibu.
Tamka Maneno Ya Kumshukuru Mungu
1Th
Na mewe na shukrani katika kila hali.Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika
kuungana kwenu na Kristo Yesu.Mara baada ya kutuambia katika 1Th
5:17.Tuombe bila kukoma,Mtume Paulo anatuelezea tumshukuru Mungu katika kila
jambo.Haijalishi kinachoendelea katika maisha yetu kwa maana hii andiko kusudi
la Mungu kwa ajili ya maisha yetu.
Jinsi
maombi yanavyopaswa kuwa mtindo wa maisha yetu,ndivyo shukrani zetu
zinavyopaswa kuwa sehemu ya maisha
yetu.Kumshukuru Mungu hakupaswi kuwa jambo ambalo tunafanya mara moja kwa siku
tunapoketi chini na kujaribu kufikiria mambo yote mema ambayo Mungu ametufanyia
hata katika udhaifu wetu.Katika kumwishia Mungu shukrani au kushukuru kwa
sababu tunafikiria kuwa Mungu anatuhitaji tufanye.Ni kweli shukrani uendelea
kububujika kutoka kwenye moyo ambao umejaa shukrani pamoja na sifa kwa Mungu
kwa sababu ya utukufu wake na matendo
yake.tupate kibali cha ushindi na tuhitimu kuweza kupata baraka.Aina ya
shukrani ambayo Mungu anahitaji kutoka kwetu ni ile ambayo imechochewa na roho
takatifu ndani yetu ambayo inatuvuta kumwelekea Bwana yale tunayohisi katika
roho zetu.Zaburi 136:3.
2.Tamka Maneno Ya Kumsifu
Kumtukuza Mungu.
kwa
njia yake Basi Yesu yeye,na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima,yaani tunda la
midomo iliungamayo jina la lake.Ebr 13:1-.Ufahamu kwamba sifa na ibada.Sifa
ni kutamka maneno ambayo yanayorudia mema ambayo Mungu amefanya.Ibada ni namna
jinsi na mbinu za uwasilishaji wa mtu mbele za Mungu,Sifa hutambuwa uwepo wa
Mungu na utukufu wake,Ni vema kila wakati kutambua na kukiri kwa kulitukuza
jina lake katika kuomba kwetu.
3.Tamka Maneno Ya Toba Na Kuomba Msamaha.
Wakati tunapokuwa mbele za Mungu tukiwasilisha mahitaji yetu katika ibada ya maombi,ni vema kutamka maneno ya kuomba msamaha kwa Mungu,kwa maana sisi ni wakosaji muda wowote,lakini Bwana anatufanya upya siku baada ya siku.Lakini hatuwezi kuomba kusamehewa dhambi na makosa pamoja na madhaifu yetu kama hatujafikiwa na roho ya kupata toba.Toba ni njia ya mtu kutamka maneno ya kusamehewa na Mungu.Md 5:31.Toba ni hatua muhimu ya mwanzo tunayochukua kubapa msamaha wa dhambi na makosa na madhaifu yetu.Md 2:36-38,17:30.Kujihisi na kujisikia kuwa mwenye hatia kuhusiana na dhambi huja kabla ya kutubu.Na mtu atakapotamka maneno ya kutubu na kuomba kusamehewa pasipo kupa tatoba hiyo si toba yenyewe.Hakuna mtu ambaye anayetubu isipokuwa amejisikia kwanza kuwa mwenye dhambi,lakini si wote wanaojisikia wenye hatia hufanya toba ya kweli.Md 24:25.Si hiyo tu kuhuzunishwa na dhambi zako kwa maana watu wengi sana wanasikitika kwa sababu ya matokeo ya dhambi zao au kwa sababu wamekamatwa.Watu wengi husikitika si kwa sababu ya kile walichokikosea bali ni kwa sababu ya adhabu wanayoipokea kutokana. na kushikwa 2Kor7:10.Toba sio tu kujaribu kuwa mtu mzuri,kwa maana watu wengi wanajaribu kwa nguvu zao kuwa watu wazuri kuliko kubadilisha njia zao za maisha.Nguvu yoyote ya kibinafsi ina mizizi ya kujihesabia haki ndani yake,ambayo haikubali hitaji la toba kutoka dhambi.Isaya 64:6.Toba ya kweli haitokani na kuwa wadini sana.Mafarisayo katika Biblia walikuwa watu wa dini sana katika taifa la Israeli katika tabia na desturi na sikukuu za dini lakini bado hawakutubu kwa ajili ya ukosefu wa toba.Mathayo 3:7-10,5:20.Toba ya kweli sit u kuijua kweli.Kuwa na ufahamu wa kiadili kichwani kuhusu kweli si sharti la dhamana kwamba kweli imefanyika kitu hai halisi katika maisha ya mtu.Kuamini kwa akili na kuamini kwa moyo ni kwa tofauti sana.Rum 10:10.Yakobo 2:19-20.Toba ya kweli ni sikitiko la ndani kwanza ni sikitiko muhimu zaidi ni sikitiko la kweli ya Mungu.Zab 51:1-4,38:8,Kuwa mkweli kuhusu dhambi zako.Zab 32:5,1Yoh 1:9.Ziache dhambi zako.Mat 28:13.Zichukie dhambi,Ebr 1:9,Ezekieli 20:43-44.
Msamaha Takatifu Uliokubalika
Kuomba
msamaha ni tabia na hali ya kujikubali kwa mwenye hatia na mwenye dhambi.Lakini
la muhimu kujua na kufahamu ni kwamba kuomba msamaha na kusamehewa na kusamehe
ni neema kubwa sana katika maisha ya ki-Mungu.Kuna baadhi ya waitwao Wakristo
ni wagumu kusamehe na kuomba msamaha kwa Mungu na kwa watu pia.Ndiyo maana
nimesema kwamba kusamehe na kusamehewa ni neema ya ajabu sana.Ona jinsi Isaya
alivyojihesabia kuwa mwenye dhambi na akasamehewa aloposema ole wangu mimi
mwanye midomo michafu na nimekaa katika watu wanye midomo michafu na macho
yangu yamemwona Bwana mfalme wa majeshi.Isaya 6:1-7,Yesu mwenyewe alitusamehe
bila sisi kuomba kusamehewa.Luka 23:34.ona jinsi neema ilivyo:
Kuomba Msamaha Na Kusamehewa Na Kusamehe.
Kupata nafasi ya kuomba msamaha na kusamehewa na kusamehe ni neema ya ajabu sana.Neema maana ya kawaida inayofahamika ni upendeleo wa Mungu ambao hatukustahili”kwa maneno mengine ingawa tulikuwa wenye dhambi,wenye kustahili hukumu.Mungu alitutazama kwa upendo na akatusamehe.Hata hivyo maana hii ni nusu tu,pia neema ina maana ya nguvu ya Mungu ya kuwezesha ikiwemo kukuwezesha kupata nguvu na nafasi na moyo wa kuomba msamaha na kusamehewa na kusamehe.2Th 2:16-17.Neema ya Mungu huwezesha.Efe 1:4-6, 2Kor 5:17,2Petr3:18, Mashujaa wa imani walipewa neema na Mungu.Musa alipewa neema ya kumfikia Farao.ukichunguza maisha ya Musa utaiona neema,Kutoka 3:11-13,4:1-13.Neema katika maisha ya Gideoni.Waamuzi 6:1-24.Neema katika maisha ya Paulo.Md 15:40.2Kor 11:22-33,12:9
Wakilisha Mahitaji Omba Unalohitaji Kutendwa.
Wakati
unapofanya ibada ya maombi lengo kuu ni kuwa muhitaji mbele za Mungu ili
akutimizie yale ambayo umepungukiwa au ambayo hauna kabisa.Watu wengi hawajui
jinsi ya kuwakilisha hitaji au mahitaji yao kwa Mungu.Wakati umekaa magotini
ili kumwomba Mungu itapendeza kama utaanza na kushukuru,kusifu na
kuabudu,kujiwakilisha na kukubali wewe na mwenye dhambi na mkosaji halafu tamka
maneno ya kuomba msamaha.Baada ya kujisalimisha omba sasa kile au yale ambayo
unahitaji kutendewa na Mungu.Usione aibu wala usiogope kuomba vitu vingi na vikubwa mno.wewe omba kadri ya
uhitaji wako.Fahamu kwamba Mungu mwenyewa ametuita na kusema,Haya
njooni,tusemezane asema Bwana.Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana,zitakuwa
nyeupe kama theluji,zijapokuwa nyekundu kama bendera,zitakuwa kama sufu.Isaya
1:18.Haya,leteni maneno yenu,asema Bwana;toeni hoja zenye nguvu asema mfalme wa
Yakobo.
Msikilize Mungu Kaa Kimya
Kusubiri Majibu.
Ndugu
Mkristo na mtumishi wa Mungu wetu.Nakuomba ufahamu kwamba ni vema kumsikia na
kumsikiliza Mungu watu muumba mbingu na nchi.Natamani ufahamu kwamba ni vema
ukiomba au kuwakilisha mahitaji yako muhimu kwa Mungu wetu si vema kuomba muda
wowote bila kumsikiliza Mungu kama amejibu ili usije ukaombe tena kitu au jamba
ambalo Mungu amekwisha jibu.Unapoomba chukua muda wa kukaa kimya bila kuomba
chochote wala kuimba wala kuomboleza ,wewe nyamaza kimya ili usikie sauti ya
Mungu kukuletea majibu ya mahitaji yako.Unapo chukuwa muda wa siku saba
ukiomba,unapokamilisha siku saba kama ulivyojipangia kuwa mbele za Mungu
kuwakilisha hoja zako zenye nguvu,chukuwa siku tatu au nne za kukaa kimya bila
kuomba chochote kwa Mungu kaa kimya kumsikiliza Mungu.Unapoomba kwa muda wa
siku 30,chukuwa muda wa siku 7 kukaa kimya ili kusubiri majibu yako kutoka
Mungu.Waliyo wengi hupishana na majibu yao kutoka kwa Mungu kwa sababu ya
kutokujua umuhimu wa kukaa kimya huku ukimsikiliza Mungu kutokana na yale
uliyoyawasilisha kwake kama ameyajibu.Ukigundua kwamba ameyajibu basi
hauna ya kuyaomba tena kwa maana
amekwisha tenda kama ulivyo yahitaji.kukaa kimya kunakupa nafasi ya kuona
kusikia na kutafakari kile ambacho umekiomba na kukupa muda wa kuyafahamu majibu
na njia ambayo Mungu ameitumia kukujibu.Mungu anaweza kukujibu kupitia
maandiko,anaweza kukujibu kupitia mtu au watu,anaweza kukujibu kupitia
mazingira na matukio fulani fulani,anaweza kukujibu kwa sauti yake waziwazi
ikitoka kwenye ukuta wa chumba chako,anaweza kukujibu kupitia ndoto,pia anaweza
kukujibu kwa yeye kukaa kimya bila kusema chochote.Kwa maana ukimya wa Mungu
nao ni jibu au majibu.Maandiko yanasema kwamba Ukae kimya mbele za
Bwana,Nawe umngojee kwa saburi;Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia
zake,Wala mtuafanyaye hila.Zaburi 37:7.Nalikuwa sisemi,nalinyamaa,Sina
faraja,maumivu yangu yakazidi.Zaburi 39:2.Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake
kwa kimya,Wokovu wangu hutoka kwake.Zaburi 62:1,5.76:8,94:17,115:17.Md
8:32,9:7.Ufu 8:1Kwa hiyo ukitaka
maombi yako yajibiwe yaishi hayo.
Kimeandikwa na
Bishop Rhobinson S.Baiye
rhobinsons.blogspot.com
Whatsapp.0764127531
Mwanza Tanzania
No comments:
Post a Comment