Monday, June 1, 2020

KITABU CHA UBORA WA LUGHA YA KANISA No 2

UBORA WA LUGHA N0 2

Kitabu hiki kiitwacho ubora wa lugha namba mbili kinahusu hasa na lugha ya kushawishi mtu au watu kumwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wao.Kitabu hiki kinakupa mbinu muhimu ambazo zitatufanya tuweze kuwashawishi watu kujiunga na makanisa yetu ili zipate kuimarika na kustawi.Ubora wa lugha namba moja kimo katika Tuvuti  hii kaisome utakifuraia sana.Itapendeza kama utasoma kwanza namba moja ili upate kuelewa namba mbili hii.Nimemnukuu Daktari Mark Goulston. Anasema mambo mengi katika lugha inayoshawishi  msome hapo chini

.Daktari Mark Goulston Anasemahivi:

1:Kila Mtu Ana Mahitaji Yake.

Kila mtu ana mahitaji yake,matamanio yake na pia ajenda zake.Na tena kila mtu ana siri yake ambayo anaificha,na hataki watu wengine waijue.Na pia kila mtu anapilika zake na msongo wa mawazo,na hana muda wa kumtosha kufanya kila anachotaka kufanya.Ili kuweza kwenda na hayo yote yanayoendelea kwenye maisha yake,mtu anajitengenezea ukuta ambao bila ya kujua hayo huwezi kumshawishi kwa jambo lolote.Fahamu kwamba ukitaka mtu afanye au akupe chochote unachotaka,anza kwanza kuvunja ukuta huu ambao kila mtu amejijengea.Kanisa ni lazima kuvunja ukuta ambao umejengeka na kila mshirika kama mahitaji binafsi,matamanio binafsi,siri zake binafsi,imani,za kigeni,mategemeo,matumaini,mila,testuri,na lugha utamaduni,ili Kuimarisha na kustawisha kanisa. Za 11:10,14,2:9,3:7,7:2,28:5,29:5,46:9,48:7.Mith 15:4, Mik 2:13,3:3,Ombolezo 2:9,3:4 Math 5:19,6:19,12      :1,20,26:61,27:40,

2:Ushawishi Na Mzuguko Wake.

Ushawishi unaenda kwa mzunguko ambao ana hatua tano muhimu.Yaani kabla mtu hajashawishika kufanya chochote unachomwambia,anapitia hatua hizi tano ambazo unatakiwa kuzijua na kujua jinsi ya kumpitisha mtu kwenye kila hatua.

a:Hatua Ya Kwanza.

Hatua ya kwanza ni kumtoa mtu kwenye kukataa mpaka kuwa tayari kusikiliza.Wakati wowote mtu yupo kwenye hali ya kukataa, unahitaji kuwa na mbinu ya kufanya akusikilize.Tumia lugha ambayo mtumishi kiongozi mshirika na asiyeamini ashawishike kukusikiliza sio lugha ya kumweka mbali nawewe na kanisa.Kufanya hivyo kutaimarisha na kustawisha kanisa.

b:Hatua Ya Pili.

Hatua ya pili nikumtoa mtu kwenye kusikiliza mpaka kukufikiria.Hapa mtu anakuwa amesikiliza kile ulichomwambia,na kuna mbinu bora za kumwambia na akaanza kufikiria kwamba anaweza kufanya au anaweza kuwa tayari.Ni vema kutumia lugha ambayo itamweka mtu unaye wasiliana naye kuwa tayari kulifikiria sana kanisa lako.Kwa kufanya na kutumia lugha hiyo itaimarisha na kustawisha kanisa lako.

 c:Hatua Ya Tatu.

Hatua ya tatu ni kumtoa mtu kwenye kukufikiria mpaka kuwa tayari kufanya.Baada ya mtu kufikiria kwamba anaweza kufanya anashawishika zaidi na kuwa tayari kufanya.Tumia lugha ambayo itamfanya mtu kuwa tayari kufanya kwa ajili ya kanisa na mtu mmoja mmoja katika kanisa na katika jamii yako.Hiyo ndiyo lugha bora sio bora lugha,kufanya hivyo kutaimarishana kustawisha kanisa la mahali ulipo.

d:Hatua Ya Nne.

Hatua ya nne ni kumtoa mtu kwenye hali ya kuwa tayari kufanya  na kufanya jambo  husika.Hapa ndipo mtu anapofanya kile ambacho unataka afanye au anakupa kile ambacho ulitaka akupe.Kumbuka Yesu alivyosema kwamba mwana  hakuja kutumikiwa bali kutumika.Hata Mungu aliziumba mbingu na nchi na vyote viijazayo kwa kutumika kwa kutamka na kusema na kutumia lugha ya kuumba pamoja na kufanya kazi kwa mikono yake ili kumuumba mtu,Mungu hakutumikiwa bali alitumika.Tunapotumia kumshawishi mtu mpaka akatumika kwa ajili ya Mungu na watu wake yaani kanisa,hiyo ndiyo lugha bora wala sio bora lugha.

e: Hatua Ya Tano.

Hatua ya tano ni kumtoa mtu kwenye kufanya mpaka kwenye kufurahia kufanya na kuendelea kufanya.Kufanya siyo mwisho wa mzunguko huu,bali mtu anahitaji kufurahia kwamba amefanya na kuendelea kufanya kadri inavyohitajika.Na huu ndio mzunguko wa ushawishi ambao unatakiwa kujua na jinsi ya kutumia kwa watu mbalimbali.Yafaa sana na kutia moyo mtu anapo fanya kazi au anapo hudumu kwa lugha ya kanisa huku anafanya kwa moyo wa kufurahi,inaleta afya katika kanisa.Na tufikie ngazi hiyo ili kuimarisha na kustawisha kanisa na makanisa yetu ya mahali,na huko ndiko kunena kwa lughampya ambayo inasemwa na maandiko.

3: Fahamu Ubongo Wa Mwanadamu.

Ili uweze kuwa na ushawishi kwa wengine unahitaji kujua vizuri ubongo wa binadamu.Ubongo wa binadamu umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo zinatofautiana kwa miaka ambayo zimekuwepo.Ubongo ndio kiini cha mfumo wa neva katika wanyama wote wenye ungwemgongo na wanyama wasio na ungwemgongo.Ubongo unapatikana katika kichwa ukilindwa na mifupa ya fuvu.Kazi kubwa ya ubongo ni kuhakikisha viungo muhimu vya mwili kama vile moyo na mapafu vinafanya kazi ipasavyo.Acha tuone baadhi ya mambo muhimu ya kufahamu kuhusiana na ubongo,kabla ya kuona mgawanyo wa sehemu tatu kuu za ubongo.

1.Ubongo wa binadamu huwa hauna vipokezi vinavyohusika na maumivu hivyo ubongo hauhisi maumivu kabisa,hivyo mtu anaweza kufanyiwa upasuaji wa ubongo huku ukiwa na ufahamu wake na hauhisi maumivu yoyote.

2:Ubongo ndiyo kiungo pekee cha mwili ambacho hutumia nguvu nyingi sana zaidi ya asilimia 20% ya nguvu zote za mwili hutumiwa na ubongo japokuwa ubongo una asilimia (2) tu uzito.

3:Zaidi ya asilimia 60% ya ubongo wa binadamu huwa umeundwa kwa mafuta huku asilia 75% uzito  ubongo inabebwa na maji.

4: Sehemu ya ubongo iitwayo  Neocortex.Ambayo ina husika na lugha pamoja na ufahamu ndiyo sehemu kubwa zaidi kuliko sehemu zote zinazounda na ubongo, huchukua zaidi ya asilimia 76% ya ubongo wa binadamu kumfanya binadamu awe tofauti na wanyama wengine katika kuwaza kunena na kutenda.

5:Kila sehemu ya ubongo hufanya kazi,Jambo hili hufanya binadamu asiweze kutumia ubongo wake kikamilifu,inasadikika kuwa binadamu hutumia chini ya asilimia 10% tu ya ubongo wake.

6: Homoni inayoitwa Oxytocin ambayo hujulikana kama homoni ya mapenzi huzalishwa kwa wingi kwenye ubongo,na hupatikana kwa wingi katika matukio ya mapenzi ambayo homoni hii ndiyo huamua umpende nani, umpende vipi mapenzi yenu,na hii homoni ndio huamua umpende nani kwa wingi,lakini pia homoni hii huzalishwa wakati wa kukutana kimwili mwanamme na mwanamke,lakini pia wakati wa uchungu wa kuzaa,na lamwisho homoni huongoza na Kulinda  mfumo mzima wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama

7:Tukiwa kwenye ufahamu wetu,ubongo huzalisha kati ya watts 10 hadi 23 za umeme ambao unatosha kabisa kuwasha taa moja ya umeme.

8:Kupiga miayo hutokea mara nyingi baada ya kumuona mtu mwingine kafanya hivyo hii ni kwa sababu ubongo huwa na seli zinazoitwa seli koo mirror celle.Sehemu hii  ya ubongo huingiza kitendo hiki kutoka kwa mwingine na kikitokea basi hufanya mtu awe na matatizo makubwa.

9:Ubongo huwa na mishipa ya fahamu zaidi  ya bilioni 100 hii ni mara 15 zaidi ya idadi ya watu wote tuliopo duniani.

10:Mziki husisimua sehemu ileile ya ubongo ambao hutoa kemikali za raha Dopamine wakati wa kujamiana na kula?

Mgawanyo Wa Ubongo Katika Sehemu Tatu Kuu.

1.Sehemu Ya Kwanza:Ubongo  Wa Nyuma)

Sehemu ya kwanza ya ubongo ni sehemu ya ubongo wa chini,ambao ni ubongo wa nyuma una tabia za mjusi.Hii ni ile sehemu ya ubongo ambao kazi yake kubwa ni kuhakikisha unaishi kwa Ubongo huu kazi yake ni kuakikisha umepata chakula na unaweza kujikinga na hatari.Ubongo huu huwa unachukua hatua haraka bila hata ya kufikiri kwa kina.Kwa mfano kama umewahi kuwa kwenye hatari mara kukimbizwa na mnyama kama mbwa hapo utapata nguvu nyingi za haraka hata kuruka utakuta ambao kwa kawaida usingeweza kuukuta,hii ndiyo kazi ya ubongo huu.Kama kanisa na kama viongozi na watumishi kuchukua hatua za haraka unapokuwa uhitaji wa kufanya hivyo.Mungu aliweka ubongo huo wa chini ili kuchukua hatua za haraka kwa Kuimarisha na kustawisha kanisa lako.

2.Sehemu Ya Pili: Ubongo Wa Kati.

Sehemu ya pili ni ubongo wa kati,ambao una tabia za mnyama.Hii ni sehemu ya ubongo ambayo imebeba hisia zote za mtu.Hisia za upendo,wivu,hata rahaa zipo kwenye sehemu hii ya ubongo.Sehemu hii ya ubongo ndiyo inatusukuma kufanya vitu vinavyotupa hisia nzuri na kutuepusha na vitu vinavyoleta hisia mbaya.Fahamu kwamba unapotumia lugha ambayo hajaeleweka vizuri sehemu hii hufanya kazi kwa kuhisi kama kuna kitu ambacho kimefichwa watu hawakifahamu mahali hapa.Na hapo ndipo mwanzo wa mtu kuwa na maswali yasio kuwa na majibu na kukatisha tamaa,na kulichukulia kanisa,na mwanzo wa kanisa kutokuimarika na kustawi.Lugha nzuri huusika katika sehemu hii.

3.Sehemu Ya Tatu: Ubongo  Wa Mbele)

Sehemu ya tatu ni ubongo wa juu ambao una tabia za utu.Huu ndio ubongo ambao unatutofautisha sisi binadamu na viumbe wengine wote.Huu ndio ubongo ambao unafikiri kwa kina kwenye kila jambo tunalofanya au linalotokea.Huu ndio ubongo ambao unatunza kumbukumbu.Ubongo huu unakusanya taarifa kutoka kwenye sehemu nyingine za ubongo na kufanya maamuzi sahihi.

 4:Fanya Maamuzi Na Ubongo Wa Juu

Tumia lugha na kufanya maamuzi kwa kutumia ubongo wa sehemu ya juu.Kwa bahati sana watu wengi wamekuwa wakifanya maamuzi  kwa kuongozwa na ubongo wa chini na ubongo wa kati.Ni mara chache sana watu wanaweza kuutumia ubongo wa juu vizuri na kufanya maamuzi bora.Maamuzi mengi yanayofanywa na ubongo wa chini na ubongo wa kati ni maamuzi ambayo yana faida ya muda mfupi lakini kwa muda mrefu yana hasara kwao.Mfano Ni mtu ambaye anabaka,hapa anauridhisha ubongo wa kati ambao utapata raha,lakini angetumia ubongo wa juu angeona siyo kitu sahihi kwake kufanya.

5:Shawishi Mtu Akiwa Kwenye Ubongo Wa Mbele

Ili uweze kumshawishi mtu yeyote,hakikisha unaongea naye akiwa kwenye ubongo wa juu.Hakuna kitu unachoweza kumwambia akakusikia na kukuelewa.Haijalishi utatumia mbinu bora kiasi gani,kama mtu hayupo kwenye ubongo wa juu utapoteza muda wako.Hii ndiyo maana ni vigumu sana kumshauri mtu ambaye ana hasira,au hana raha na yupo katikati ya hisia kali za mapenzi.Kuweza kumshawishi mtu mtoe kwanza kwenye Ubongo wa kati na wa chini na mpeleke kwenye Ubongo wa juu ambapo anaweza kufikiri sawasawa.

6:Adui Wa Kwanza Wa kushawishi Ni Wewe

Adui wa kwanza kuwashawishi wengine ni wewe mwenyewe.Ili uweze kuwashawishi wengine ni lazima wewe kwanza kushawishika.Ni lazima wewe ukubaliane na kile anachotaka wengine wafanye au kukupatia.Ni lazima  uweze kujithibiti mwenyewe ili kuweza kuwashawishi wangine kuchukua hatua ambayo unajua ni muhimu.

7:Ondoa Chujio Tayari Unalo.

Ondoa chujio ambalo tayari unalo.Fahamu kwamba kila mmoja wetu ana chujio ambalo anatumia kuwachuja wengine kwa kadiri wanavyoonekana au alivyowazoea.Hivyo tunawapanga watu kwenye makundi kwa kufikiri tunawajua sana.Ili kuweza kuwa na ushawishi kwa wengine kwanza ondoa chujio hili na mwendee kila mtu bila ya kumhukumu,kuwa tayari kujifunza zaidi kutoka kwake.Usimweke mtu kwenye upande wowote,badala yake msikilize yeye  na utapata njia bora za kuweza kumshawishi.

8:Fahamu Kitu Kinacho Kusukuma.

Naomba fahamu kwamba kila kitu anachofanya,sababu inayomsukuma kufanya.Hakuna mtu anayefanya kitu kwa ajali au kwa bahati mbaya pekee.Hivyo unapokutana na tatizo au changamoto kutoka kwa wengine jua Kuna kitu kimewasukuma kufanya walichofanya.Ili uweze kuwashawishi watu,jua ni kitu gani kinawasukuma wafanye kile ambacho wanafanya sasa na ni jinsi gani unaweza kuwafanya kuacha wanachofanya sasa na wafanye kile ambacho unawashawishi wafanye.

9:Mfanye Mtu Ajisikie Ameeleweka.

Mfanye mtu ajisikie ameeleweka,ni lazima umwelewe mtu kabla hujakaribia kumshawishi afanye chochote unachotaka afanye.Jaribu kuvaa viatu vyake na mwelewe wazi ya kwamba unaelewa kwa nini yupo pale alipo sasa.Na hata kama anafanya kitu ambacho anakosea, mwelewe kwamba kuna kitu ambacho kinasababisha yeye afanye hivyo.Usione kwamba yeye hayupo sahihi na kumweleza hivyo,ukienda kwa njia hiyo atakachofanya ni kujitetea na hutaweza kumshawishi kwa njia yoyote ile.Mwelewe mtu na atafunguka kwako.

10:Wafanye Watu Wakujali

Kama unataka wengine wajali kuhusu wewe,anza kujali kuhusu wao kwanza.Moja ya njia muhimu za kuweza kushawishi watu ni kuwafanya wavutiwe na wewe,na wajali kuhusu wewe,na wawe tayari kufanya kile ambacho unawaambia wafanye.Lakini hii haitakuja kuwavunja moyo wewe kukazana,watu wavutiwe na wewe na wajali kuhusu wewe.Badala yake inakuja pale unapoanza kujali kuhusu wengine,na unapovutiwa na wengine.Hivyo unapokutana na watu usitumie nafasi hiyo kujisifia zaidi wewe,badala yake tumia nafasi hiyo kutaka kuwajua zaidi.Ni vema kujua ni jambo gani wanafanya changamoto gani wanapitia yapi ambayo wameweza kukamilisha.Kadri unavyojali kuhusu wao wataanza kufunguka kwako na watakuwa tayari kufanya kile unachotaka wafanye.

11:Ona Thamani Ya Wengine.

Wafanye wengine wajione ni wa thamani kwako.Hii ni mbinu muhimu sana kila mshirika wa kanisa la mahali anatakiwa kuwanayo kama anataka kuwashawishi watu ili kuimarisha na kustawisha kanisa la mahali watu huchukua hatua fulani.Hakuna kitu ambacho mtu anapenda kama kuona amethaminiwa.Hii ndio maana watu wanapenda kuitwa mheshimiwa,bosi,mtaalamu bingwa na majina mengine mengi yenye sifa za kuheshimika.Mfanye mtu aone ana mchango mkubwa kwenye kile anachofanya na kile anachotaka afanye ataweka mchango mkubwa pia.Kufanya watu kuwa wa thamani kwako au kwenu Ni zawadi kubwa sana unayoweza kupata.Hata Mungu alituthamini sisi wanadamu, maana alituumba kwa mfano na sura yake.Mwa 1:26.

12:Epuka Kueleweka Tofauti.

Epuka kueleweka tofauti na unavyotaka ueleweke.Katika harakati za kushawishi wengine unaweza kutoa picha iliyo kinyume kabisa na kile ulichokuwa unataka kutoa wewe.Mfano unataka watu wakuone wewe ni mwenye busara lakini kwao unaonekana ni mpumbavu.Au unataka wakuone mwaminifu ila wao wanakuona ni tapeli.Matokeo hayo hutokana na mtu kutokujiandaa vizuri na kutosikiliza wale ambao anataka kuwashawishi.Unahitaji kuwafundisha kwa makini na kuona wanapokeaje kile ambacho unawapa.

13:Tambua Vitu Vitatu Muhimu.

Kuna vitu vitatu ambavyo vinawasukuma watu kuchukua hatua ,ukiweza kuvitumia vizuri vitu hivi utaweza kuwashawishi watu iwe ni kwenye kazi,biashara na hata kwenye familia.Jambo la kwanza ni mapenzi,hamu au shauku.Watu wapo tayari kufanya kile ambacho wanapenda kufanya na wana shauku kubwa kukifanya.Hivyo angalia ni kitu gani watu wanapenda na kitumie katika ushawishi wako.Hata Yesu alikuwa akitazama na kugundua kile wasikilizaji wake wanachohitaji hata kama ni kinyume na mapenzi yake,aliwafundisha na alikuwa anaeleweka vizuri sana hata kama wengine hawakuwa wafuasi wake.Jambo la pili ni hamasa watu wanakuwa tayari kuchukua hatua kwenye jambo lolote ambalo wanapenda.Wafanye watu wahamasike kwenye kile ambacho unataka wafanye.Jambo la tatu ni fahari.Watu wanaona fahari pale wanapoona wamekuwa na mchango kwenye Jambo fulani.Watu wanapoona kile walichofanya kina mchango kwa wengine wanafarijika sana.Tafadhali tumia vitu hivi vitatu kwa pamoja na utaweza kushawishi watu kuchukua hatua.

14:Tafuta Na jitahidi Kuwa Mwaminifu.

Uaminifu ni muhimu sana katika kuwashawishi wengine.Huwezi kuwashawishi watu kama hawakuamini na watu hawawezi kukuamini kama husemi kweli na kutekeleza kile unachoahidi.Usiwe na haraka katika kushawishi kwako,badala yake jenga mahusiano yenye uaminifu,kadiri watu wanavyo kuamini,kutokana na matendo yako na siyo maneno tu, ndiyo wanavyokuwa tayari kukubaliana nawe.

Lugha yenye mvuto wa kushawishi

Kushindwa kushawishi    kumewafanya watu wayaone maisha ni adhabu.kushindwa kushawishi kumewaangusha wengi katika ulimwengu huu, ulimwengu unao kwenda kwa kasi ya ajabu.Si rahisi kushawishi mtu akubali ombi na kutoa huduma au msaada kwa mtu mwingine.Kazi hii ngumu inaweza kufanikishwa kwa kutumia mbinu tano (5) rahisi.Mbinu hizo tano ni zifuatazo.

1:Kwenda Sambamba Na Mshawishiwa.

Mshawishi anapaswa kutazama kwa makini jinsi anayeshawishiwa anavyowasiliana na mshawishi hili ni pamoja na matumizi ya lugha ya ishara ya mazungumzo na ya maandishi,ili naye afanye vivyo hivyo.Ingawaje, mshawishi anapaswa kuwa makini ili asionekane anamkebehi mshawishiwa.Ikiwa mshawishiwa atagundua kuna usanii hatotia maanani yale anayoambiwa na hatimaye kutokubali kutimiza ombi la mshawishi.

2:Kutimiza Mahitaji Ya Wakati Husika.

Watu hujipendelea na watu hupenda mahitaji yao yatimizwe kwanza ndipo ya wengine yafuate.Mshawishi atambue vipaumbele vya mshawishiwa atakavyotekeleza ili maombi yake yatimizwe kwa urahisi.Mshawishi atazame mahitaji,matakwa,vionjo nk.ili aweze kuvuta hisia za mshawishiwa.Mshawishi ajitahidi kutimiza kero au matakwa ya mshawishiwa kwa kadiri ya maadili,hali na uwezo wake kabla ya kutoa ombi.

3:Mbinu Ya Tatu: Uthibitisho.

Mshawishi atoe uthibitisho unaoonyesha ya kwamba ombi au lengo lake litatekelezeka bila ya vikwazo vingi.Mshawishi atoe uthibitisho pasipo na shaka ya kwamba bidhaa bora baada ya muda husika, baada ya ombi lake kukubaliwa na kutekelezeka.Mshawishi ashindanishe Uthibitisho wake dhidi ya washindani wengine.Mshawishi ahakikishe anayosema au kutoa ni ya kweli na yanawezekana.Mshawishi aonyeshe uhusika au nafasi yake huku akitabasamu ili kukuza imani na urafiki.Pia mshawishi aonyeshe ya kwamba yupo tayari kutoa msaada wa ziada kama ikibidi kufanya hivyo.

4:Mbinu Ya Nne:Kuwasiliana Kwa Ufasaha.

Takribani watu wote wanapenda wakubalike na kueleweka kadiri wanavyohisi ni rahisi,kwa kadiri ya hisia zao bila kujali jinsi wanavyowasiliana.Mshawishi anapaswa kujiuliza,je niwasilisheje ombi langu bila ya kumkwaza mshawishiwa?.Ili kufanya hivyo, mshawishi anapaswa kutumia mbinu za mawasiliano bora.Mshawishi atambue na kukwepa maneno ambayo huathiri utu wa mtu au jamii husika kama yasipotumika kwa kuzingatia mazingira na aina ya mazungumzo.

5:Mbinu Ya Tano:Kukubaliana Na Mshawishiwa.

Takribani watu wote hupenda uridhika kwa kuambiwa “nimekuelewa”.Katika hili mshawishi ahakikishe anasikiliza kwa makini mawazo yanayofanikisha ombi lake likubalike.Mshawishi akubaliane pia na mawazo kinzani kabla ya kukosoa au kutoa ufafanuzi.Kwa mfano,unaweza kuwa sahihi lakini ni bora kama ingekuwa hivi,kwa maana natambua hali halisi lakini naomba tufanye hivi.Mshawishi ahakikishe ya kwamba pindi ombi lake litakapokubaliwa na kutekelezeka pande zote mbili zitafanikiwa ili mshawishiwa akubali kutoa msaada.Mshawishiwa atatoa msaada na ushirikiano pale atakapohisi anafanya uamuzi sahihi.

Neno La Mungu Mbinu Ya Ushawishi:

Moyo wa mwenye hekima husababisha kinywa chake kuonyesha ufahamu wenye kina,na kwa midomo yake huongeza ushawishi. Mith 16:23. Mradi wetu tukiwa waalimu wa neno la Mungu ni kuelimisha,si akili tu za Kuwafundisha watu au wanafunzi wetu,bali pia mioyo yao.Efe 1:18. Kwa hiyo, kufundisha kunahusisha mengi kuliko tu kuwasilisha habari.Mith 16:23.Moyo wa mwenye hekima husababisha kinywa chake kuonyesha ufahamu wenye kina,na kwa midomo yake huongeza ushawishi.kwa hakika,mtume Paulo alitumia kanuni hiyo katika kazi yake ya kufundisha.Alipokuwa korinto,yeye alikuwa akitoa hotuba katika sinagogi kila sabato na alikuwa akiwashawishi Wayaudi na Wagriki. Mdo 18:4.Kulingana na chanzo kimoja chenye mamlaka,neno la kigriki linalotafsiriwa hapa kushawishi lamaanisha kusababisha badiliko la moyoni kupitia uvutano wa ufikirio wa maadili.Kwa njia ya majadiliano yenye kusadikisha, Paulo aliweza kufanya watu wabadilishe hasa njia yao ya kufikiri.Uwezo wake wa kushawishi ulikuwa wa ajabu sana,maadui wake walimwogopa. Mdo 19:24-27. Hata hivyo ufundishaji wa Paulo haukuwawonyesho wa uwezo wa mwanadamu.Aliwaambia Wakorinto maneno yangu na kuhubiri kwangu haikuwa kwa maneno ya yenye ushawishi wa hekima bali kwa wonyesho wa roho na nguvu ili Imani yenu ipate kuwa si katika hekima ya wanadamu,bali katika nguvu ya Mungu. 1Kor 2:4-5. Kwa kuwa Wakristo wote wana msaada wa roho ya Mungu wote wanaweza kuwa walimu wenye kushawishi.Mifano hiyo na mafunsho ambayo Yesu alitoa na kuunganisha yaliwashawishi watu kwa kuwa alifahamu na kutambua mahitaji na mambo au vitu alivyohitaji.Alitumia lugha yenye mvuto na kutia moyo,kufariji,kujenga,kushauri,kukaripia,kukemea,ku'oa,kuteketeza,kupanda.Tujifunze njia za kushawishi kwa kumwiga Yesu Kristo.Ametuambia kwamba twende kwake na tujifunze kwake kwa kuwa yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo.Yesu alionyesha kuwathamini wote.

Watu Katika Makundi Manne.

Katika harakati za kuwashawishi wengine nivema ufahamu makundi manne ambayo Wataalamu wameyahainisha ili kuweza kumshawishi mtu au watu kufuatana na kundi lake.Unapoelewa na kujuwa kundi ambalo mtu unaye mshawishi alilomo hatakupashida.

 1.Kundi La Kwanza: Filing.

Hawa watu hujali sana wengine.Wanapenda kuwafurahisha wengine hata kwa mambo yasiyo muhimu,wanapenda sana hali ya maendeleo.Kwa hiyo kwanye migogoro hawafanyi kazi vema,hata maamizi yao yanazingatia mapenzi ya watu.Wanataka kusifiwa sana mara kwa mara.Hawawezi kuwaambia watu mambo magumu na yasiyofurahisha,wana huruma na wanahusiana mazuri na watu wengi.Kwa hiyo unapomshawishi mtu mwenye kupenda sifa inakubidi ujipange sawasawa.

2:Kundi La Pili: Senling.

Hawa ni watu ambao wasiyopenda masula mapya kama hakuna utaratibu wa kuyashughulikia.Wanataka utaratibu wa kudumu.Wanafanya kazi kwa mpango wakijua hatua za kufuata na lini kazi itamalizika.Watu au kundi hili hawana uvumilifu katika mambo yanapo changanyika.Siyo rahisi kuwatia moyo kwa sababu hawaamini wanayoambiwa juu yao.Wanalinda ukweli na hawakoseikosei mambo.Watu au kundi hili halishawishiki hata kama ungefanya nini,kwa hiyo watu hawa wasikupotezee muda wa kufanya mambo mengine.

3:Kundi La Tatu: Thinking.

Watu hawa au kundi hili halitawaliwi na hisia za wengine.Wanaumiza watu bila kujua,wanataka maelezo na mafafanuzi yanayooeleweka wazi.Wanaweza kufanya kazi vizuri hata kama kuna migogoro.Wanapofanya maamuzi hawajali sana mapenzi ya watu.Wanataka kutendewa haki,hawaogopi wala kusita kuonya au kufukuza watu wanakosea.Wanaelewana zaidi na watu wanaopenda hoja nao hupoteza marafiki mara kwa mara.

4:Kundi La Nne. Intuitive.

Watu hawa au kundi hili linataka kupambana na changamoto n matatizo mapya.Hawataki kurudia-rudia Mambo,wanataka kuelewa mbinu mpya hata kama hawataitumia.Hufanya kazi kwa nguvu sana jazba halafu wanapotea.Hurukia mambo ya kuamua kabla hawajajua ukweli mzima.Wanavumilia Mambo magumu,lakini hawataki Mambo yanayo rudiwa-rudiwa kila mara.Hawapendi kuchelewa kutekeleza Mambo kwa hiyo wanafanya makosa mengi.

Uwe Msikilizaji Mzuri.

Mbinu ya kufundisha kama kushawishi ina husisha kusikiliza bali si tu kusema kama tuoivyoonyeshwa kwenyeMith 16:23. Ili tuwe wenye kushawishi ni lazima tuwe na ufahamu wenye kina.Kwa hakika Yesu alikuwa na ufahamu kwa kina kuhusu watu aliofundisha.Yoh 2:25.

hutumika kama chombo cha mawasiliano kwa kupashana habari.

b.Lugha,hutumika,kujenga Umoja,Mshikamano,Ushirikiano.

c.Lugha hutumika Kukuza,Kutunza,na Kuendeleza tamaduni za jamii.

d.Lugha hutumika katika kutetea maarifa mbalimbali.Lugha ni nyenzo ya kufundishia.e.Lugha hutumika kama alama ya utambulisho wa Taifa,Kabila ya jamii fulani.e.Lugha hutumika kutoaburudani.

Kimeandikwa na

Bishop.Rhobinson S,Baiye

rhobinson.blogspot.com

rhobinsonsaleh1@gmail.com

Whatsapp.0764127531

Mwanza Tanzania

 

 

 

 


MAOMBI YANAYOJIBIWA

 

MAOMBI YANAYOJIBIWA

Ndungu msomaji naamini unashauku ya kufahamu mengi kihusu maombi.Lakini katika kitabu hiki tutajikita katika mada hii isemayo maombi yanayojibiwa.Kwa maana watu wengi huomba lakini hawapati majibu ya yale wanayo ya omba, na hilo huleta maswali mengi katika ucha-Mungu wao na utumishi wao.Na walio wengi usema na kujiuliza je,kweli Mungu anajibu maombi ya watu? Ni kweli Mungu hujibu maombi kupitia jina la Yesu Kristo.Yohana 14:13-14. Na hivi karibuni tutatafakari kuhusu maoombi yasiojibiwa kaa mkao wa kupokea.Lakini fahamu kwamba kuna aina nyingi za maombi.

Maama Ya Maombi

Maombi ni mazungumzo yenyemahitaji muhimu kati ya mtu na Mungu au kati ya Mungu na mtu.Mwanzo 1830-33,45-1-20

5.Namna Ya Mungu Kujibu maombi

Mungu wetu na Bwana wetu Yesu Kristo wametujenga  kwa hadi ya kupokea majibu chanya ya maombi mahitaji yetu kutoka kwao,kama tuliwakilisha mahitaji yetu kulingana na utaratibu wa ki-Mungu majibu ya maombi hujibiwa.Lakini nakuomba ufahamu kwamba mara nyingine  Mungu atakupa kitu au vitu vizuri tofauti na ulivyotarajia.Inawezekana ukaomba Mungu kwa kitu unachofikiria ya kuwa ni kitu kizuri ambacho kitakacho mtukuza Mungu,lakini yeye ni Mungu ajuaye kila jambo,anafahamu kile uombacho kitaumiza kiasi gani kazi zake na hata sisi vilevile.Mungu hupenda sisi watoto wake na anajua muda na kitu fulani cha kutupatia kilicho kizuri kitakacho kuwa baraka kwetu na kumtukuza Mungu.Mara nyingi hujibu maombi yetu si kwa kadri tulivyohitaji lakini kwa njia bora kuliko yale tuliyoyaomba.Tunaweza kuona jambo hili kwa baadhi ya watumishi wake.Paulo alikuwa na udhaifu mwilini mwake ambao ulimtesa sana.Na alifikiri udhaifu huu ulikuwa kikwazo katika huduma yake,na aliomba mara tatu Ili udhaifu huu umtoke.bali Bwana hakuruhusu udhaifu huu kumtoka Paulo haijalishi aliomba.Bali Mungu alimjibu Paulo kwamba neema yake Mungu inamtosha.Na hapo Paulo alibadilisha maombi na akaanza kushukuru Mungu kwa udhaifu huo.2Kor 12:7.Mara nyingi Mungu hatuondoi katika taabu yetu wakati tunapomwomba kufanya hayo.Halafu hutupa nguvu za kumtukuza hata tukiwa katika taabu yenyewe.Na tunamshukuru katika mambo yote.

1.Kwa ahadi.Isaya 58:9.Yer 29:12.Math 7:7

2.Mara kwa ghafla. Dan 9:21,23.10:12

3.Kwa baadae Luk 18:7.1Fal 18:42-44.Dan 10:12

4.Kwa hali usiyoitegemea.2Kor 12:8-9

5.Vyema kuliko tegemeo letu au kuliko tulivyofikiria.Yer 33:3 Efe 3:20.

Ilimaombi yako yajibiwe Fanya Yafuatayo.

Kwakuwa kanisa na mtu binafsi hupenda kupata majibu chanya ya Maombi yao waliyo wakilisha mbele za Mungu, ni vyema maombi yaombwe katika utaratibu huu.

1.Omba Kupitia Jina La Yesu Kristo.

2.Omba Kwa Imani Na Matumaini

3.Omba Kwa Kumaanisha.

4.Omba Kwa Wakati Uliokubalika.

5.Omba Kwa Utaratibu.

Mungu wetu niwautaratibu,kwahiyo mambo yote yatendeka kwa uzuri na kwa utaratibu ukiwemo utaratibu wa kuomba.

1.Omba  Katika Jina Langu

Yatupasa kuomba katika jina la Yesu Kristo.Hilo nitakwa la Yesu Kristo mwenyewe.Yohana 11:13.14:13-16.15:7,16.16:24-26.Tukiomba  katika jina la Yesu Kristo  tutampendeza Mungu na Kristo pia.Unaweza kujiuliza kuomba katika jina la Yesu humaanisha nini?.Kuomba katika jina la Yesu Kristo lina maana ya kuomba kwa kutamka maneno yanayopatana na mapenzi yake.Ukitamka au ukisema neno au maneno kupitia kwa jina lingine maombi hayo hayawezi kumfikia Mungu kwa kuwa Yesu Kristo ndiye njia ya kweli na uzima.Ifahamike kwamba tunayemwomba atutimizie mahitaji yetu ni Mungu lakini yatupasa maombi yetu yapitie katika jina la Yesu Kristo wala si vinginevyo.Kuna baadhi ya Madhehebu ya ki-kristo yamebuni majina mengine na kuyapa heshima ambayo hayastahili kupewa heshima hiyo,kwa maana hata majina hayo hayajatajwa na Biblia kwa heshima hiyo wana jifariji na kudanganya nafsi zao wenyewe. Kwa mfano heshima ya kupindukia kwa Bikira Mariamu,pamoja na watakatifu ambao wana watakasa wao hayo yote ni kujidanganya na kujifariji.Atambuae na kumtakasa mtu ni mtu mwenyewe na Mungu tu.

2.Omba Kwa Imani Na Matumaini.

Walio wenye haki wataishi kwa imani na matumaini.Mark 9:23.Math 17:20.Ebr 11:1,6.1Kor 2:4-7,8-16.2Kor 5:7.Ebr 12:2.Rum 1:17.Habakuki  2:4.Efe 2:8-9.Rum 10:17.Yak 1:22-25.Inatupasa kuomba kwa imani na matumaini makubwa ya kupokea kile tulicho kiomba kwa Baba.Baadhi ya wacha Mungu wanaomba lakini wana imani haba na hupoteza matumaini.

1.Omba Kwa Imani

Tunaweza kusema kwamba imani ni njia ya kupokea kutoka kwake Mungu.katika waefeso  tunaona kwamba tumeokolewa kwa neema,kwa njia ya imani,Efe 2:8-9.Ebr 11:1,6.Tunaweza kueleza maana ya imani kwa njia tofauti lakini inamaanisha kuwa njia rahisi ya kutazama imani na hata kujichunguza  kuona kama tuna imani yenye nia na matumaini ya upokeaji.Tukitathimini mioyo yetu ni shughuli muhimu wakati tunapoanza safari hii ya matumaini pamoja,kwa sababu kumtumainia Mungu na kuwa na matarajio mazuri yanaleta uhusiano wa karibu sana na imani.Tunaweza kusema kwamba kiwango chako cha matarajio ndicho ndicho kiwango chako cha imani.Nionyeshe mtu mwenye matarajio madogo,nami nitakuonyesha mtu anayetumia imani haba.Tena ionyeshe mtu mwenye matarajio makubwa  na nitakuonyesha mtu anayetumia imani kubwa ya kijasiri.Kumbuka tunaongea kuhusu kuwa na matarajio yetu katika Mungu.Hiyo ni zaidi ya kuwa na mtazamo chanya;ni kumtegemea Mungu akutunze  pamoja kila na kitu kinacho kuhusu.Neno la Mungu linatwambia kwamba imani yetu matarajio yetu chanya,yenye matumaini humpendeza Mungu.Ebr 11:6.na mara kadhaa katika Injili tunamwona Yesu akichochewa kutenda jambo kwa sababu ya imani na matarajio ya wale aliokutana nao.Math 9:29,Marko 5:34,Luk 7:50.Mungu yuko upande wako na ana mpango mzuri katika maisha yako.Unapojaribiwa na kuwa mwenye mashaka,na kukaribia kukata tama na kukaribia kufa moyo wewe amini na kuwa na matarajio ya kupokea.Utafaulu kulingana na kiwango chako cha matarajio.Usichukulie kuwa kule ulikotoka na hapo ulipo,kwamba hapawezi kubadilika.Si kwamba mpango wako ni mbaya zaidi la hasha bali ni kwamba mpango wa Mungu ni mzuri zaidi.Kwa hiyo omba kwa imani kubwa sana,utapokea.Mungu hufanya zaidi ya kukushikilia usianguke;na kisha hukupeleka juu zaidi ya pale ulipokuwa mwanzoni.

2.Omba Kwa Matumaini

Mara kwa mara waliowengi huhisi kuwa mtu akitarajia zaidi ya alivyo navyo basi huyo ni mlafi na mkosaji.Ijapokuwa ni kweli kwamba wakati wote tunapaswa kuridhika na kutosheka na vile tulivyonavyo.Hivyo haimaanishi kuwa kuhitaji kuwa na vitu vizuri zaidi ni dhambi au makosa ilimradi tuna sababu mzuri ya kuvitamani na  kuvitumia.Tunaweza kutosheka na huku bado tunahitaji kuwa na vingi zaidi.Mimi Bishop Rhobinson Saleh Baiye sasa hivi ninatosheka sana na kila kitu katika maisha yangu kwa sababu ninaamini wakati wa Mungu maishani mwangu ndiyo mzuri zaidi.Ninaweza kufurahi hata kama sina kitu chochote cha ziada kwa sababu furaha yangu na kutosheka kwangu viko katika Kristo.Hata hivyo,wakati huo huo ninahitaji kuwa na vingi vizuri zaidi kwa sababu ninahitaji kuendelea katika maisha kadri Mungu atakavyoniruhusu na nimfanyie mengi zaidi isipokuwa maisha mazuri zaidi ambayo Mungu anakata kunipa.

Ezekieli 37:11,Isaya 57:10,32:17,20:5,29:16,1Kor 9:10

3.Omba Kwa Kumaanisha.

Walio wengi wanaomba sala na dua ndefu pasipo kumaanisha wanachohitaji.Ni vyema kufahamu tunapoomba kumaanisha kile tunachohitaji.kwahiyo tamka kwa ufasaha kile unachohitaji.1Timoth 2:1-4.Luk 10:2.1The 3:1.Mark 8:22-23.10:46-52(50-52) walio wengi huogopa kuomba baadhi ya mahitaji yao muhimu.lakini fahamu ya kwamba Yesu alisemaje kuhusu kuomba kwetu? Yesu alikuwa akiwauliza baadhi ya watu waliyo mwendea na kusema wataka nikutendee nini? Alikuwa akihitaji musika amaanishe kile anachohitaji kutoka kwake Krsto.Sikiliza jinsi Yesu Kristo alivyo tufundisha kuomba kwa kumaanisha kweli kweli.Ikiwa Yesu Kristo alipokuwa mahali fulani akiomba,alipokwisha,kuomba mmoja katika wanafunzi wake alimwambia,Bwana tufundishe kuomba kama vile Yohana alivyo wafundisha wanafinzi wake.Yesu Kristo akawaambia msalipo semeni hivi,Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe,Ufalme wako uje,[Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni.] utupe siku kwa siku riziki yetu.Utusamehe dhambi zetu,kwa kuwa sisi nasi tuna wasamehe waliyotukosea.Na usitutie majaribuni lakini utuokoe na Yule mwovu kwa kuwa ufalme na nguvu na utukufu ni wako hata milele amina.

Ukifanya uchambuzi  na kutafakari kwa makini,utagundu

a kwamba Yesu Kristo aliwafundisha jinsi ya kuomba kwa kumaanisha , kile unachokiomba na kwa Yule unaye mwomba,na kwa muda unaohitaji.Haijalishi Mungu anajibu na kufanya kwa muda wake,cha muhimu ni wewe kumaanisha kile ukiombacho na kwa Yule umwombaye.Wewe omba kwa maana Yesu Kristo alisema kwamba tutafanyiwa kila tunacho kiomba kwa jina lake ili Baba Mungu atukuzwe na ndani ya Mwana.Yohana 14:13.

Kama  unahitaji chakula wewe omba Mungu kwa kumaanisha Mungu baba nakuomba chakula baba yangu na ni vema kumaanisha chakula unachohitaji si kwamba tu umetamka chakula fahamu kuna aina nyingi za vyakula hapa duniani,waweze kutaja baadhi ya vyakula unavyovifahamu utaona na kujua ni aina nyingi tu.wewe maanisha kila unachohitaji kutoka kwa Mungu kupitia jina la Yesu Kristo wa nazareti.Zaburi 40:8.Math 6:33

Maanisha kuomba msamaha kwa maana tunasamehewa kwa kuwa tuna wasamehe wengine.Yesu Kristo alisema wazi kwa kumaanisha kabisa ya kwamba tutasamehewa tukiwasamehe wengine.Maanisha kuutukuza utukufu wa Mungu katika kuomba kwako.Kama unahitaji kuponywa magojwa maanisha,kama unahitaji utajiri maanisha ,kam,

Unahitaji mifugo,magari,mashamba,kama unahitaji kuwekeza majini maanisha,maanisha chochote unachohitaji mungu atakutimizia.Usiombe kwa kumungunya maneno tamka na kumaanisha.

4.Omba Kwa Wakati Unao kubalika

Omba kwa wakati unaokubalika na Mungu.sio kilamuda ni wakuomba,tafuta muda wakuomba,hasa muda ambao dhamiri zako zinahitaji kuomba.Mara nyingi baadhi ya wakristo hujiuliza kama ni vyema kuomba mara kwa mara? au inampasa kuomba mara ngapi kwa siku au kwa wiki au kwa mwezi au kwa mwaka? Kwa nini umeupa moyo wako kujiuliza swali kama hilo? Je hujiamini unapo mwendea Mungu? Je wewe umechoka kulalama mbele za Mungu ?Biblia inasemaje kuhusu kuomba kwetu. Omba bila kukoma.Ni kweli kwamba kuna watu huwa wanachoka haraka wakati tunapoomba au tunapowasilisha mahitaji yetu mbele za Mungu.Na tena hujihisi kwamba wameomba vitu vingi au wameomba mara nyingi.Si hivyo alivyo Mungu wetu,anapoona na kusikia maombi yetu mara nyingi anafurahi sana kuona tunamtegemea na kuwa wahitaji kwake.Kwa sababu Mungu wetu ni wautaratibu basi yatupasa kuwa na utaratibu katika kuomba kwetu.Danieli,aliomba mara tatu kwa siku Dan 6:10.Daudi,aliomba mara tatu  Zaburi 55:17. Bwana wetu Yesu Kristo alisema ya kwamba yatupasa kuomba siku zote.Luka 18:1Katika 1Th 5:17 Tumeagizwa kuomba bili kukoma hapo tunahimizwa kuomba muda wowote na uombe kwa mahitaji yako mwenyewe na watu wengi vilevile.Maandiko yanasema tudumu katika kuomba Kolosai 4:2

1.Omba Asubui

2.Omba Mchana.

3.Omba Jioni.          Danieli 6:10

4.Omba Usiku         Zaburi 55:17.

5.Omba Kwa Utaratibu.

Fahamu unapoomba unamfanyia Mumgu ibada.Unapokuwa katika ibada ya maombi na maombezi fata utaratibu wa Mungu.Kuna baadhi ya wanaojiita waombaji lakini ukiwasikia wanavyoomba hawana mpangilio wa kuomba kwao.yanayofaa kutangulia kutamkwa yanatamkwa mwishoni mwa mazungumzo.Yale ambayo yangetamkwa mwishoni yanatamkwa mwanzoni mwa mazungumzo yao na Mungu.Mungu wetu aliumba kwa kuweka mambo yake katika mpangiliyo na utaratibu uliyotukuka.Mwanzo 1:1-2:1-

1.Tamka Maneno Ya Kumshukuru Mungu.

2.Tamka Maneno Ya Kumsifu Na Kutukuza Mungu.Tamka Maneno Ya Toba Na Kuomba Msamaha Kwa Mungu.

3.Wakilisha,Mahitaji Omba Unalohitaji Kutendewa.

5.Msikilize Mungu Kwa Kukaa Kimya Kusubiri Majibu.

Tamka Maneno Ya Kumshukuru Mungu

1Th Na mewe na shukrani katika kila hali.Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.Mara baada ya kutuambia katika 1Th 5:17.Tuombe bila kukoma,Mtume Paulo anatuelezea tumshukuru Mungu katika kila jambo.Haijalishi kinachoendelea katika maisha yetu kwa maana hii andiko kusudi la Mungu kwa ajili ya maisha yetu.

Jinsi maombi yanavyopaswa kuwa mtindo wa maisha yetu,ndivyo shukrani zetu zinavyopaswa  kuwa sehemu ya maisha yetu.Kumshukuru Mungu hakupaswi kuwa jambo ambalo tunafanya mara moja kwa siku tunapoketi chini na kujaribu kufikiria mambo yote mema ambayo Mungu ametufanyia hata katika udhaifu wetu.Katika kumwishia Mungu shukrani au kushukuru kwa sababu tunafikiria kuwa Mungu anatuhitaji tufanye.Ni kweli shukrani uendelea kububujika kutoka kwenye moyo ambao umejaa shukrani pamoja na sifa kwa Mungu kwa sababu ya utukufu  wake na matendo yake.tupate kibali cha ushindi na tuhitimu kuweza kupata baraka.Aina ya shukrani ambayo Mungu anahitaji kutoka kwetu ni ile ambayo imechochewa na roho takatifu ndani yetu ambayo inatuvuta kumwelekea Bwana yale tunayohisi katika roho zetu.Zaburi 136:3.

2.Tamka Maneno Ya Kumsifu  Kumtukuza Mungu.

kwa njia yake Basi Yesu yeye,na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima,yaani tunda la midomo iliungamayo jina la lake.Ebr 13:1-.Ufahamu kwamba sifa na ibada.Sifa ni kutamka maneno ambayo yanayorudia mema ambayo Mungu amefanya.Ibada ni namna jinsi na mbinu za uwasilishaji wa mtu mbele za Mungu,Sifa hutambuwa uwepo wa Mungu na utukufu wake,Ni vema kila wakati kutambua na kukiri kwa kulitukuza jina lake katika kuomba kwetu.

3.Tamka Maneno Ya Toba Na Kuomba Msamaha.

Wakati tunapokuwa mbele za Mungu tukiwasilisha mahitaji yetu katika ibada ya maombi,ni vema kutamka maneno ya kuomba msamaha kwa Mungu,kwa maana sisi ni wakosaji muda wowote,lakini Bwana anatufanya upya siku baada ya siku.Lakini hatuwezi kuomba kusamehewa  dhambi na makosa pamoja na madhaifu yetu kama hatujafikiwa na roho ya kupata toba.Toba ni njia ya mtu kutamka maneno ya kusamehewa na Mungu.Md 5:31.Toba ni hatua muhimu ya mwanzo tunayochukua kubapa msamaha wa dhambi na makosa na madhaifu yetu.Md 2:36-38,17:30.Kujihisi na kujisikia kuwa mwenye hatia kuhusiana na dhambi huja kabla ya kutubu.Na mtu atakapotamka maneno ya kutubu na kuomba kusamehewa pasipo kupa tatoba hiyo si toba yenyewe.Hakuna mtu ambaye anayetubu isipokuwa amejisikia kwanza kuwa mwenye dhambi,lakini si wote wanaojisikia wenye hatia hufanya toba ya kweli.Md 24:25.Si hiyo tu kuhuzunishwa na dhambi zako kwa maana watu wengi sana wanasikitika kwa sababu ya matokeo ya dhambi zao au kwa sababu wamekamatwa.Watu wengi husikitika si kwa sababu ya kile walichokikosea bali ni kwa sababu ya adhabu wanayoipokea kutokana. na kushikwa 2Kor7:10.Toba sio tu kujaribu kuwa mtu mzuri,kwa maana watu wengi wanajaribu kwa nguvu zao kuwa watu wazuri kuliko kubadilisha njia zao za maisha.Nguvu yoyote ya kibinafsi ina mizizi ya kujihesabia haki ndani yake,ambayo haikubali hitaji la toba kutoka dhambi.Isaya 64:6.Toba ya kweli haitokani na kuwa wadini sana.Mafarisayo katika Biblia walikuwa watu wa dini sana katika taifa la Israeli katika tabia na desturi na sikukuu za dini lakini bado hawakutubu kwa ajili ya ukosefu wa toba.Mathayo 3:7-10,5:20.Toba ya kweli sit u kuijua kweli.Kuwa na ufahamu wa kiadili kichwani kuhusu kweli si sharti la dhamana kwamba kweli imefanyika kitu hai halisi katika maisha  ya mtu.Kuamini kwa akili na kuamini kwa moyo ni kwa tofauti sana.Rum 10:10.Yakobo 2:19-20.Toba ya kweli ni sikitiko la ndani kwanza ni sikitiko muhimu zaidi ni sikitiko la kweli ya Mungu.Zab 51:1-4,38:8,Kuwa mkweli kuhusu dhambi zako.Zab 32:5,1Yoh 1:9.Ziache dhambi zako.Mat 28:13.Zichukie dhambi,Ebr 1:9,Ezekieli 20:43-44.

Msamaha Takatifu Uliokubalika

Kuomba msamaha ni tabia na hali ya kujikubali kwa mwenye hatia na mwenye dhambi.Lakini la muhimu kujua na kufahamu ni kwamba kuomba msamaha na kusamehewa na kusamehe ni neema kubwa sana katika maisha ya ki-Mungu.Kuna baadhi ya waitwao Wakristo ni wagumu kusamehe na kuomba msamaha kwa Mungu na kwa watu pia.Ndiyo maana nimesema kwamba kusamehe na kusamehewa ni neema ya ajabu sana.Ona jinsi Isaya alivyojihesabia kuwa mwenye dhambi na akasamehewa aloposema ole wangu mimi mwanye midomo michafu na nimekaa katika watu wanye midomo michafu na macho yangu yamemwona Bwana mfalme wa majeshi.Isaya 6:1-7,Yesu mwenyewe alitusamehe bila sisi kuomba kusamehewa.Luka 23:34.ona jinsi neema ilivyo:

Kuomba Msamaha Na Kusamehewa Na Kusamehe.

Kupata nafasi ya kuomba msamaha na kusamehewa na kusamehe ni neema ya ajabu sana.Neema maana ya kawaida inayofahamika ni upendeleo wa Mungu ambao hatukustahili”kwa maneno mengine ingawa tulikuwa wenye dhambi,wenye kustahili hukumu.Mungu alitutazama kwa upendo na akatusamehe.Hata hivyo maana hii ni nusu  tu,pia neema ina maana ya nguvu ya Mungu ya kuwezesha ikiwemo kukuwezesha kupata nguvu na nafasi  na moyo wa kuomba msamaha na kusamehewa na kusamehe.2Th 2:16-17.Neema ya Mungu huwezesha.Efe 1:4-6, 2Kor 5:17,2Petr3:18, Mashujaa wa imani walipewa neema na Mungu.Musa alipewa neema ya kumfikia Farao.ukichunguza maisha ya Musa utaiona neema,Kutoka 3:11-13,4:1-13.Neema katika maisha ya Gideoni.Waamuzi 6:1-24.Neema  katika maisha ya Paulo.Md 15:40.2Kor 11:22-33,12:9

Wakilisha Mahitaji  Omba Unalohitaji Kutendwa.

Wakati unapofanya ibada ya maombi lengo kuu ni kuwa muhitaji mbele za Mungu ili akutimizie yale ambayo umepungukiwa au ambayo hauna kabisa.Watu wengi hawajui jinsi ya kuwakilisha hitaji au mahitaji yao kwa Mungu.Wakati umekaa magotini ili kumwomba Mungu itapendeza kama utaanza na kushukuru,kusifu na kuabudu,kujiwakilisha na kukubali wewe na mwenye dhambi na mkosaji halafu tamka maneno ya kuomba msamaha.Baada ya kujisalimisha omba sasa kile au yale ambayo unahitaji kutendewa na Mungu.Usione aibu wala usiogope kuomba  vitu vingi na vikubwa mno.wewe omba kadri ya uhitaji wako.Fahamu kwamba Mungu mwenyewa ametuita na kusema,Haya njooni,tusemezane asema Bwana.Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana,zitakuwa nyeupe kama theluji,zijapokuwa nyekundu kama bendera,zitakuwa kama sufu.Isaya 1:18.Haya,leteni maneno yenu,asema Bwana;toeni hoja zenye nguvu asema mfalme wa Yakobo.

Msikilize Mungu  Kaa Kimya Kusubiri Majibu.

Ndugu Mkristo na mtumishi wa Mungu wetu.Nakuomba ufahamu kwamba ni vema kumsikia na kumsikiliza Mungu watu muumba mbingu na nchi.Natamani ufahamu kwamba ni vema ukiomba au kuwakilisha mahitaji yako muhimu kwa Mungu wetu si vema kuomba muda wowote bila kumsikiliza Mungu kama amejibu ili usije ukaombe tena kitu au jamba ambalo Mungu amekwisha jibu.Unapoomba chukua muda wa kukaa kimya bila kuomba chochote wala kuimba wala kuomboleza ,wewe nyamaza kimya ili usikie sauti ya Mungu kukuletea majibu ya mahitaji yako.Unapo chukuwa muda wa siku saba ukiomba,unapokamilisha siku saba kama ulivyojipangia kuwa mbele za Mungu kuwakilisha hoja zako zenye nguvu,chukuwa siku tatu au nne za kukaa kimya bila kuomba chochote kwa Mungu kaa kimya kumsikiliza Mungu.Unapoomba kwa muda wa siku 30,chukuwa muda wa siku 7 kukaa kimya ili kusubiri majibu yako kutoka Mungu.Waliyo wengi hupishana na majibu yao kutoka kwa Mungu kwa sababu ya kutokujua umuhimu wa kukaa kimya huku ukimsikiliza Mungu kutokana na yale uliyoyawasilisha kwake kama ameyajibu.Ukigundua kwamba ameyajibu basi hauna  ya kuyaomba tena kwa maana amekwisha tenda kama ulivyo yahitaji.kukaa kimya kunakupa nafasi ya kuona kusikia na kutafakari kile ambacho umekiomba na kukupa muda wa kuyafahamu majibu na njia ambayo Mungu ameitumia kukujibu.Mungu anaweza kukujibu kupitia maandiko,anaweza kukujibu kupitia mtu au watu,anaweza kukujibu kupitia mazingira na matukio fulani fulani,anaweza kukujibu kwa sauti yake waziwazi ikitoka kwenye ukuta wa chumba chako,anaweza kukujibu kupitia ndoto,pia anaweza kukujibu kwa yeye kukaa kimya bila kusema chochote.Kwa maana ukimya wa Mungu nao ni jibu au majibu.Maandiko yanasema kwamba Ukae kimya mbele za Bwana,Nawe umngojee kwa saburi;Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia zake,Wala mtuafanyaye hila.Zaburi 37:7.Nalikuwa sisemi,nalinyamaa,Sina faraja,maumivu yangu yakazidi.Zaburi 39:2.Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya,Wokovu wangu hutoka kwake.Zaburi 62:1,5.76:8,94:17,115:17.Md 8:32,9:7.Ufu 8:1Kwa hiyo ukitaka maombi yako yajibiwe yaishi hayo.

 

Kimeandikwa na

Bishop Rhobinson S.Baiye

rhobinsons.blogspot.com

rhobinsonsaleh1@gmail.com

Whatsapp.0764127531

Mwanza Tanzania

 

 

 


UPENDO WA KUJIPENDA MWENYEWE


   JIPENDE MWENYEWE KWANZA

Moyo - Wikipedia, kamusi elezo huru

 

 
 Upendo wa kujipenda mwenyewe

Naomba ufahamu kwamba kitabu hiki kimehusika na aina Ya upendo wa kujipenda mwenyewe. Kwa maana kuna aina Tano za upendo haijalishi wengi hufundisha na kuaminisha watu kwamba kuna aina nne za upendo,huku wakiacha upendo wa kujipenda wewe mwenyewe.Maandoko matakatifu yanasema mpende jirani yako kama nafsi yako.Ikimaanisha kwamba mtu hujipenda au mtu upenda nafsi yake.Mathayo 22:39.

Tano Za Upendo Aina

  • Upendo wa ki-Mungu /Agape.God love
  • Upendo wa kirafiki / Phileo. Friend love
  • Upendo wa kindugu / Storge. Familiy love
  • Upendo wa kimapenzi mahaba. Romantic love.
  • Upendo wa kujipenda mwenyewa.Personal love.

upendo wakujipenda mwenyewe.

Aina hii ya upendo wa kujipenda mwenyewe ni Upendo ambao binadamu anakua nao kwa kujijali na kujipa thamani  yeye mwenyewe, pamoja na mapungufu yote yale aliyonayo.Huwezi kukuta hata siku moja mtu anajijukia mwenyewe.Aina hii ya Upendo huzaa kitu kinachoitwa ubinafsi.Pamoja na Biblia kusema Mpende jirani yako kama nafsi yako.Biblia inaturuhu tupende nafsi zetu.Na ndio sababu mtu akijitoa uhai kwa kujinyonga au kujimaliza kwa chuma cha mcha kali au kwa sumu na kwa njia ye yote ile ni mtenda Dhambi.

Umuhimu Wa Kujipenda Mwanyewe.

Unapofanikiwa kujipenda mwenyewe unakuwa umejipa nafasi kubwa sana ya kutambua thamani yako na uwezo wako ambao umebarikiwa na Mungu kuwa nao.Na kwa maana hiyo basi hata unaweza kufanya mambo yako kwa kujiamini kabisa,bila ya kutetereshwa na mtu yeyote yule.Lakini pia utakuwa na uwezo wa kukaa peke yako na hakuna kitu ambacho  kitakacho kosekana. Hayo yote ni kwa sababu tayari umeshajipenda mwenyewe unajithamini na kujijali pia.Watu wengi huwa wanashindwa kujipenda wao wenyewe na wakati huo huo wanasema kwamba Kuna watu ambao wanaowapenda.Ukweli ni kwamba huwezi kumpenda Mtu mwingine ikiwa wewe mwenyewe umeshindwa kujipenda vile ambavyo unatakiwa kujipenda.Siku zote ukijipenda mwenyewe basi kila kitu kwako kitaenda vile ambavyo kinatakiwa kiende na lazima utafurahia maisha yako na nchi yako upewayo na Bwana Mungu wako.

Ukijipena wewe mwenyewe kuna baadhi ya vitu ambavyo vinaitajika kujifanyia mwenyewe badala ya kusubiri mtu mweingine aje akufanyie.Ukikaa na kusubiri mtu  unayempenda akufanyie, nina uhakika kabisa kuwa inawekana,ukasubiri milele na vitu hivyo visitokee.Kwa hiyo basi ukijipenda wewe mwenyewe utaweza kufanya  vitu kama unavyotaka.

Mambo Ya Kudhingatia Unapofanya Maamuzi.

Unapo jipenda mwenyewe kuna mambo ambayo unatakiwa kuyadhingatia ili maisha yako yaende sawa.

 a.Kuwa huru kufanya mambo yako mwenyewe.

 b.Jipatie vile ambavyo unavihitaji bila kusubiri kuja kupewa au kufanyiwa na mtu mwingine.

 c.Tambua udhaifu wako na nguvu zako,wakati huo huo ukitumia vizuri nguvu zako huku ukijitahidi kuweka sawa unadhifu wako.

d.Jiamini katika kufanya kazi kwa kile ambacho unakuwa unakihitaji.

 e.Jua na kufahamu kwamba wewe mwenyewe unatosha kwa jinsi ulivyo.

g.Kuwa mtu wa kujifariji na kujitia moyo pale ambapo utakuwa umekosea na kufanya mambo yako yawe rahisi.

Bila shaka hayo mambo yaliyotajwa hapo juu ya nakupa tunaini kubwa la kuweza kujipenda mwenyewe,kwani kila kitu kitaenda katika mstari wako na hiyo ni habari njema kwa kila mtu.

Kujipenda Mwenyewe Hakuna Gharama.

Kujipenda mwenyewe hakuna gharama yoyote ile zaidi ya wewe mwenyewe kujitambua na kujua ni nini ambacho unakitaka katika maisha yako.Unaweza ukajiuliza nitawezaje kujipenda Mimi mwenyewe?.Tazama hapa chini imeandaliwa njia kadhaa ambazo zitasaidia katika safari yako ya kuanza kujipenda wewe mwenyewe na utazifurahia bila shaka kwani zitakusaidia sana katika kuyaendesha maisha yako na ya wengine.Mtu asipojipenda yeye wenyewe hawazi kumpenda mtu mwingine,nikama mtu hasipo jihurumia hawezi kumuhurumia mtu mwingine.

Mambo Ya Kufanya Unapo Jipenda Mwenyewe

1:Jiongeleshe Mwenyewe Kama Vile Unaongea na Mtu Ambaye Unampenda na kumjali.

 2:Jione Mwenyewe katika Macho Ya Yule Anayekupenda.

 3:Kama kuna Kitu hukipendi Kutoka Kwako Mwanyewe basi huna budi kukibadilisha.

 4:Jihudumie vizuri mwenyewe.

 5:Jisikilize Wewe Mwenyewe

 6:Jiulize ni vitu gani unavihitaji wewe mwenyewe.

1.Ongea Wewe Mwenyewe Kama Unaongea Na Mtu.

Mara nyingi tunapoongea na watu ambao tunawapenda na kuwajali huwa tunatunia sauti tamu yenye upole ndani yake bila kusahau maneno ya busara na yaliyojaa ustaarabu ya kutosha ili tu waweze kutuelewa na waweze kutambua kuwa tunawajali na kuwapenda.Vivyo hivyo kwako mwenyewe unatakiwa uongee ndani ya kichwa chako kwa sauti tamu yenye upole huku ukiwa na maneno ya busara hakika na kwambia utajisikia vizuri sana na utaona ni jinsi gani una upendo wako mwenyewe na ujitaidi mara njingi kuonea  maneno yenye kutia moyo na faraja moyo wako.Epuka kuongea maneno mabaya ya kukukatisha tamaa na kukifanya kujiona mnyonge katika jamii.

2.Jione Mwenyewe Katika Macho Ya Yule.

Mfikirie mtu yeyote anayekupenda anaweza kuwa mtoto wako,mchumba,mama,baba,dada,mtu yeyote anayekupenda muone kama kasimama mbele yako anakuangalia,jiulize(a)anaona nini kwako.(b)Akiambiwa akuelezee wewe ni mtu wa namna gani atakuelezaje.(c)Kwa nini anakupenda?(d)Ni kitu gani anajivunia kutoka kwako?.Ukifanya zoezi litakusaidia sana kutambua ni jinsi gani unapendwa kwa kuwa maswali hayo ukijiuliza lazima majibu yake yata kuwa mazuri ambayo moja kwa moja yatakushawishi wewe mwenyewe kujipenda badala ya kujichukia.penda nafsi yako kwanza.

3:Kama Kuna Kitu Hukipendi Kutoka Kwako.

Kama kuna kitu ambacho hukipendi kutoka kwa mtu mwingine ambaye ni wakaribu yako bila shaka,utajitahidi kadiri ya uwezo wako ili mtu yule Kibadilishe,vivyo hivyo kama kuna kitu ambacho hukipendi kutoka kwako huna budi kukibadilisha kwani kikiendelea kuwepo kinaweza kuyaharidu maisha yako.Mara nyingi vitu vingi ambavyo huwa hatuvipendi kutoka kwetu wenyewe huwa vinatokana na malezi ambayo tumekulia kwa mnda mrufu,kwa hiyo kuna vijitabia ambavyo unakuta sio vizuri na huwa hatuvipendi.Basi ukishatambua kuwa kuna kitu ambacho hukipendi kutoka kwako hanza kukibadili kitu hicho kwa maana hakuna kitu ambacho kinashindikana chini ya jua hasa ukiwa umeamua kutoka moyoni kwamba kitu fulani lazima nikiache kwani hakifai katika maisha yangu.

Jihudumie  Vizuri Wewe Mwenewe.

Watu wengi huwa tunajua kuwapa zawadi watu tunaowajali na kuwapenda na katika orodha  ya kuwapatia zawadi huwa tunasahau kujiweka na sisi wenyewe.Tunachohitaji ni wengine kuwa na furaha huku Sisi tukiwa nyuma na wanyonge.

Yabadili maisha yako sasa kwa kuweza kujipendelea wewe mwenyewe kwenye ile orodha ya watu wanaostahili kupata zawadi kutoka kwako mwenyewe halafu ya wengine yafuate.Unapojipa zawadi mwenyewe unajipa nafasi kubwa ya kujipenda na kuona kabisa kuwa unastahili vitu vizuri katika maisha yako na usisite kujipongeza kwa zawadi uliyojipatia.

5.Jisikilize Wewe Mwenyewe.

Mara nyingi tunapenda kusikiliza mawazo ya watu wengine huku tukiwa hatujipi na fasi nzuru ya kusikiliza mawazo yetu ambayo kwa kiasi kikubwa yanaweza kutusaidia sana katika maisha yetu.Ukiwa na tabia ya kujisikiliza wewe mwenyewe,nakuakikishia kwamba kila kitu lazima kitaenda sawa.Lakini wakati ukiwa unajisikiliza wewe mwenyewe haimaanishi kuwa mawazo ya watu wengine hayana nafasi,lakini pia mawazo ya watu wengine yawe na nafasi pia.kwa hiyo jijengee mahusiano mazuri wewe mwenyewe kwa kujisikiliza  wewe mwenyewe huku ukiendelea kujipenda wewe mwenyewe.

6.Jiulize Ni Vitu Gani Unahitaji Wewe Mwenyewe.

Jiulize ni vitu gani unahitaji kwa kujiuliza mwaswali haya.

a.Je nahitaji nini kwa sasa?

b.Je nahitaji muda wa kukaa peke yangu?

c.Je nahitaji kurahisisha maisha?

d.Je nahitaji muda wa kucheza na kufurahia maisha?

e.Je nahitaji kwenda sehemu yoyote?

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo unaweza kujiuliza wewe mwenyewe katika harakati za kujipenda zaidi na zaidi wewe mwenyewe.Bila shaka au mashaka akitokea mtu akikutatulia maswali yako hayo hakuna utakachokifanya zaidi ya kumpenda sana mtu huyo.Itakuwa vyema maswali ukiyatafutia ufumbuzi wewe mwenyewe ili ujipe nafasi ya kujipenda.Kukifanikiwa kujipenda utaona maisha yako yanavyobadikika na wala hautajuta katika maamuzi yako ya kujipenda wewe mwenyewe kwanza,halafu wengine wafuate ni uamuzi mzuri utakuwa umejitendea haki.

Kuipenda Nafsi Yako Kuna Maanisha Nini?

Kumbuka kwamba tumekwisha kufahamu maana ya kupenda,mwanzoni mwakitabu hiki.Kimetuambia kwamba,watu wengi wametoa maana tofautitofauti za upendo.Sasa fahumu kwamba wanatoa maana ya upendo kutokana na aina za upendo.Jambo ambalo sio sahii.Kumbuka maana ya upendo halisi ni kumbatio,maanuzi,aminio,adhimio,kukubali,kuridhia,atamio la moyo nafsi na akili.Na ili kufahamu kuipenda nafsi yako kunamaanisha nini endelea kusoma hapo chini.

Kuipenda Nafsi Yako Kwa Afya Ya Roho.

Ili kufamu kuipenda nadsi yako,Kumbuka kwamba ni tamko la maandiko matakatifu yaani Blblia takatifu.Kumbuka Mungu aliumba mtu akiwa  nafsi hai. Mwa 2:7. Zab 66:9. Bwana wetu Yesu Kristo alisema kwamba  Luk 17:33,Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake,ataiangamiza;na ye yote atakayeiangamiza ataiponya.Math 16:25-26, kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake,ataipoteza,na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.Kwanza atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote,na kupata hasara ya nafsi yake?Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?. Katika maandiko hayo mawili kuna mambo muhimu ya kutafakari sana.Moja kuangamiza nafsi.Mbili kuiponya natsi.Tatu kuipoteza nafsi.Nne, kuiona nafsi.Kupoteza nafsi hapa linamaanisha kwamba,kukosekana na kutojulikana na kutojali mambo ya ulimengu,kwa hiyo katika mambo ya mwili tumwe wafu.Kut 20 :13-17.Usiuwe,Usizini,Usiibe,usishudie uongo,Usitamani.Gal 5:19-21.Basi matendo ya mwili nidhahiri,ndiyo haya,uasherati,uchafu,ufisadi,ibada ya sanamu,uchawi,uadui,ugomvi,wivu,hasira,fitina,faraka,uzushi,husuda,ulevi,ulafi,na Mambo yanayofanana na hayo,katika hayo aawaambia,mapema,kama nilivyokwisha kuwaambia,ya kwamba watu watendao Mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.1Yoh 2:15-17. Msipende dunia,wala mambo yaliyomo katika dunia.Mtu akiipend dunia,kumpenda baba hakumo ndani yake.Maana kila kilichomo duniani,yaani,tamaa ya mwili,na tamaa ya macho,na kiburi cha uzima,havitokani na Baba,bali na vyatokana na dunia.Na dunia inapita,pamoja na tamaa zake,bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.Gal 5:22-24.Lakini tunda la Roho ni upendo,furaha,amani,uvumilifu,utu wema,fadhili,uaminifu,upole,kiasi,juu ya Mambo kama hayo hakuna sheria.Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake

.Ukimpenda Mungu utaipenda nafsi yako ambaye ndiye chanzo cha nafsi yako.Ukimpenda Mungu utangamiza nafsi yako,na mambo ya dunia hayatakuwa tena na mvuto kwako.Imeandikwa katika 1Yoh 2:15-17,huwezi kufurahia anasa za ulimwengu na kuwa rafiki wa Mungu.Imeandikwa katika Yak 4:4. Je ni mambogani mabaya?Imeandikwa  Gal 5:19-21.Usifuate mambo yanayopendwa na dunia yasiyo mema.Imeandikwa katika  Rum 12:2. Kumjua Yesu Kristo kunakata tamaa za ulimwengu.Imeandikwa katika Gal 6:14.Epuka elimu za dunia.Imeandikwa katika Kol 2:8.Ishi kama makao yako yako mbinguni.Imeandikwa kataka 1Pet 2:11.

Ifungue Nafsi Yako Katika Kifungo Cha Nafsi.

Mwanadamu ana sehemu kuu tatu ambazo ni,mwili,nafsi na roho.Kazi ya nafsi ni kuunganisha mwili na roho.Biblia inaongelea kuhusu uumbaji uliofanywa na Mungu kama ilivyoandikwa.Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,akampulizia puani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai.Ndiyo maana kila mwanadamu alifinyangwa kutoka kwenye mavumbi ya ardhi,na kitendo cha Mungu kumpulizia pumzi huyu mwandamu,maana yake Mungu aliweka Roho.Mtu akawa nafsi hai na hivyo Biblia haisemi kwamba mtu akawa roho hai bali nafsi hai.Maana yake kama nafsi iliwekwa ndani ya mtu vivyo hivyo nafsi yaweza kuondolewa na mtu kufa.Kuna mtu wa mbinguni na kuna  mtu wa duniani.Ndivyo ilivyoandikwa,Mtu wa kwanza,Adamu,akawa nafsi iliyo hai;Adamu wa mwisho ni Roho yenye kuhuisha. 1Kor 15:45-47.   Maana yake mbinguni hakutoki udongo,bali roho.Mtu wa kwanza udongo mtu wa pili ni roho.Zab 14:7,Uitoe nafsi yangu kifungoni.Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki wata nuzunguka.Kwa kuwa wewe unanikirimu.Nafsi inaweza kuwekwa kifungoni.Fahamu kwamba ndani ya nafsi ndiko kunakowekezwa aina zote  za elimu na imani na ujuzi.Daudi alijua kwamba nafsi yake ilikuwa salama,na kama nafsi iko salama mambo yote yatakuwa salama.Na ukimwona mtu ye yote hajisikii raha akiwa ndani ya Kristo,ujue tayari nafsi yake mtu huyo ipo kifungoni.Hesabu 30:10-13,Ayubu 33:18,22,28.Zab 35:7. Mith 3:4-5:( Zab 86:13)(Mith 23:13-14( Luk 9:23-24)Yoh 12:25,Gal 2:20,Rum 12:2(1Sam 2:30-35)Moyoni mwangu nimeliweka neno lako. Zab 119:11,Kut 15:19,123:4

 

Bishpo Rhobinson S.Baiye

rhobinsons.blogspot.com

Whatsapp:0764127531

 rhobinsonsaleh1@gmail.com

Mwanza Tanzania

 

 

 


UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...