Thursday, August 26, 2021

SOMO LA UINJILISTI

Sauti Ya Gombo International Ministries Network The Voice Of The Scroll International ministries Network UINJILISTI NA MWINJILIST I YALIYOMO 1.Maswali kwa kila mmoja wetu 2.Mwinjilisti ni nani? 3.Kazi za mwinjilisti 4.Gundua mwinjilisti na wale wenye wito wa uinjilisti. 5.Kutia moyo na changamoto za mwinjilisti. 6.Saidia wachungaji kuwatambua na kuwasaidia Wainjilisti na wale wenye wito wa uinjilisti kusima Mama wenyewe. Sehemu Ya Kwanza Mwinjilisti Ni Nani? Sehemu Ya Pili Msingi Wa Uinjilisti Sehemu Ya Tatu Ujumbe Wa Mwinjilisti Sehemu Ya Nne Kazi Ya Mwinjilisti Sehemu Ya Tano Mfano Wa Mwinjilisti Filipo Sehemu Ya Sita Ishara & Miujiza Na Mwinjilisti WEWE NI MWINJILISTI? Usomapo somo hili utajiuliza wewe mwenyewe ikiwa kama wewe ni mwinjilisti. Haya ni maswali machache yakukusaidia katika sala yako ufanyayo ili kuweza kuamua kama Mungu ndiye anayekuita kuwa mwinjilisti: 1. Je, nina uhakika Bwana amesema nami kwa kuniita au katika roho yangu kwamba nina wito wa kuwa mwinjilisti? 2. Je, ninahisi uzito wa maumivu na hali ya kukuza matumaini iwapatayo watu waliotengana na Kristo? 3. Je, nina mawazo maishani mwangu kuhusu watu wanaoishi bila Kristo? 4. Je, nina mwamko wa kuwaeleza watu wengine kuhusu maisha ya Yesu Kristo, kifo chake na kufufuka kwake? 5. Je, nina njaa ya kusoma Neno la Mungu ili kupata uelewa mpana wa Injili? 6. Je, mawazo ya wanaume na wanawake wanaoishi umilele wa Jehanamu mbali na Mungu una madhara makubwa kwangu? 7. Je, ninajisikia kuona kuwa ninahitaji kuhubiri wale ambao bado hawajaokoka? 8. Je, nimekuwa na ndoto au maono ya kujikuta ninawahubiri waliopotea na kunihimiza kutaka kueneza Injili? 9. Je, ninaona maeneo yanayonihitaji mimi kutaka kusaidia wengine ili kuwaleta kwa Yesu Kristo? 10. Je, ninajisikia kubeba mzigo wowote ninapokutana na Wakristo wengine ambao hawataki kufikiri au kujali habari za kuwafikia wasiokoka na ujumbe wa Yesu? 11. Je, kuonesha wengine njia ya kwenda kwa Yesu Kristo ni kitu muhimu kwangu? 12. Je, nimeandaa mipango yoyote ya kuhubiri au kushirikiana na wengine Habari Nzuri za wokovu pekee wa Yesu Kristo? Unaweza kuwa na majibu ya “Ndiyo” katika sehemu ya maswali haya. Kama ndivyo ilivyo ni kuwa upo uwezekano halisi kuwa Mungu anakuita katika kazi ya uinjilisti. Katika somo hili utasoma kuhusu mambo yafuatayo: • Mwinjilisti ni nani? • Jadili tabia na kazi ya uinjilisti • Gundua mwinjilisti na wale wenye wito wa uinjilisti • Tia moyo, changamoto na fundisha mwinjilisti • Saidia wachungaji kuwatambua na kuwatia moyo wainjilisti, kusimama imara katika uinjilisti wao wenyewe, na pia kusaidia kanisa likue kwa kuwa na waumini wapya. • Kutoa msaada wa kimatendo kwa kusaidia uinjilisti viongozi na makanisa yao MUHIMU Somo hili litazungumzia wainjilisti wote wawili, mwanaume na mwanamke. Sasa na katika historia nzima, ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti. Yesu aliwaambia wanafunzi Wake, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” (Marko 16:15). Maandiko yanaonesha kuwa wote wanaomwamini Yesu Kristo wameitwa kushiriki Habari Zake Njema na wengine (Mathayo 28:18-20; Matendo 1:8). Hata hao ambao wameitwa na kukirimiwa kama wachungaji katika kanisa la mahali wanaangalizwa kuwa tayari kuhubiri katika nafasi mbalimbali wanazokutana nazo (2 Timotheo 4:5). Hata hivyo wapo wale ambao wameitwa kipekee na kuchaguliwa na Mungu kwa kipawa na huduma kuwa “Wainjilisti” (Waefeso 4:11). Somo hili la litasaidia kueleza wito na kazi za mwinjilisti kama Maandiko Matakatifu yasemavyo. Mafundisho haya yatakuwa ya msaada kwa kiongozi yeyote wa kanisa au waumini wa Kristo, kwani yana mikazo yenye kutia mtu nguvu, kufundisha na pia kukuwezesha wewe na wale unaowaongoza kuwapata waliopotea ili waje kwa Yesu Kristo. SEHEMU YA KWANZA:Mwinjilisti Ninani? Mwinjilisti Ni Nani? Mwinjilisti ni mwanaume au mwanamke aliyechaguliwa na Mungu kueneza Habari Njema (Injili) ya wokovu wa Yesu Kristo. Mwinjilisti ni mnenaji wa Mungu. Mwinjilisti hueleza watu habari za Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, Mkombozi. Mwinjilisti huzungumza kwa maneno habari za Kristo na shabaha ya maisha Yake, kufa Kwake, na kufufuka. Mwinjilisti, kwa maneno mengine huhubiri Injili. Hakuna ujumbe mwingine mkubwa wa kuhubiri Injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu (Warumi 1:16). Habari za Yesu Kristo zimebeba mambo yafuatayo: alivyokuja duniani; alivyoishi maisha adilifu, hakuwa na dhambi katika maisha yake; alivyokufa msalabani; alivyotoka kaburini; na pia anavyoishi milele. Shabaha ya kifo cha Kristo ilikuwa ni kuchukuwa hukumu ya Mungu kwa dhambi za watu wote, na pia kuangamiza nguvu za dhambi. Yesu alishinda mauti na pia alimshinda ibilisi na nguvu zote za uovu. Maisha ya Yesu Kristo, kufa, na kufufuka kwake kunaleta matumaini kwa watu wote na pia kuondoa woga. Kama wewe ni mwinjilisti, wewe ni mjumbe wa Mungu mwenye habari muhimu kuliko habari zote duniani! Mwinjilisti Ni Yule Ambaye Ametumwa Mwinjilisti ni mjumbe - mtu aliyetumwa kutoa tangazo. Kama Yohana Mbatizaji, mwinjilisti anamtangaza Yesu kwa watu. “Injili” ni neno lenye maana “habari njema”. Kwa hiyo mwinjilisti anabeba ujumbe wa habari njema kwa watu ambao wanataka kuusikia. Ni habari bora kwa dunia nzima zinazohusu kifo cha Yesu Msalabani na jinsi alivyojitoa kubeba ghadhabu ya Mungu kwa ajili ya dhambi zetu na kutupatia msamaha wa dhambi, na pia kutupa uzima wa milele. Yohana Mbatizaji alitumwa na Mungu Mto Yordani katika jangwa (Mathayo 3:1-12; Yohana 1:6-8,19-34). Mara nyingi mwinjilisti atatumwa kwenda mahali ambapo watu hawajui au hawajawahi kusikia habari za Yesu. Neno “mwinjilisti” linamaanisha “mtu ambaye ametumwa mwenye ujumbe”. Mungu aliwachagua wainjilisti kwenda na ujumbe wa Yesu na kuwaambia wengine. Uinjilisti ni kazi ngumu - ikiwa ni pamoja na kulisoma Neno la Mungu, kujitoa dhabihu, kufanya mipango, kujitia moyo, kusali, na kufunga. UINJILISTI NI KIPAWA Soma Waefeso 4:11-12 “Naye alitoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti; na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe”. Mistari hii inatuambia kuwa Yesu amejalia Kanisa kipawa cha wainjilisti. Zawadi maana yake ni kupokea kwa shukrani na kuikubali. Mara nyingine wainjilisti hawakubaliki na wachungaji au na kanisa. Lakini wale wanaokuja kwa Kristo kupitia katika kazi za mwinjilisti hushukuru Mungu zaidi na zaidi kwa vipawa alivyowapa - yeye aliyewaambia habari za Yesu na kuwaambia namna ya kupata wokovu na maisha mapya katika Kristo. Uinjilisti ni mojawapo ya huduma kuu tano za kiongozi-mtumishi alizotoa Kristo (Waefeso 4:11). Mwinjilisti ni kipawa kwa Kanisa maana anawaleta watu kwa Kristo. Watu waliookoka ukweli wanaenda kanisani na kujifunza namna ya kumfuata na kumtumikia Mungu. Mwinjilisti pia ni kipawa kwa watu waliopo duniani. Mwinjilisti anawaambia watu habari mpya za maajabu ya Mwokozi Yesu, yeye aliyekufa na kufufuka tena. Kwa njia ya kuhubiri Injili, watu husikia namna ya kusameheka kwa dhambi zao na kuupata uzima wa milele. Kuhubiri Injili ni kiini cha huduma ya uinjilisti Wajibu Au Ofisi Kila huduma katika Waefeso 4:11 inakamilishwa na watu ambao wameitwa kuifanya kazi ya Mungu. Mwingine ni mchungaji, mwingine ni mwinjilisti, na mwingine anaweza akawa mtume. Baadhi ya watu wanafundisha kuwa vipawa vilivyopo katika kifungu hiki (Waefeso 4:11) ni kama ofisi au nafasi za mamlaka. Wanadai eti kipawa hiki kinawapa wachungaji na wainjilisti ruhusa ya kuwaamrisha wengine katika Kanisa. Biblia haitufundishi hivyo. Uchungaji au uinjilisti siyo kuwa na mfalme juu ya watu wa Mungu. Lakini Biblia inaweka bayana kuwa mchungaji na mwinjilisti ni viongozi ambao wanafundisha wengine, kama Paulo alivyoandika, “kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe” (Waefeso 4:12). Njia ya Yesu Kristo katika huduma na pia mfano Wake kwetu sisi ni kuhudumia wengine. “Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Marko 10:45). Viongozi Ni Watumishi Yesu alikuwa na mawazo na matendo ya kiutumishi (Wafilipi 2:4-12). Kuwa kiongozi wa kimungu katika Kanisa, maana yake ni kuchukuwa njia ya Msalaba, kutokuwa na tamaa na mipango ya binafsi (soma Luka 9:23; Wagalatia 5:16-25; Wafilipi 2:3-11). Viongozi wanaofanana na Kristo huishi kama watumishi wa Mungu kuwatumikia wengine, pamoja na unyenyekevu wa kweli. Wachungaji, wainjilisti, waalimu, mitume, na manabii lazima waoneshe maisha yaliyotengwa ili kuwatumikia watu. Huduma kuu tano ni kuwa viongoziwatumishi ambao wanatumikia wengine kama Yesu alivyotumika. HUDUMA NI WITO SIO CHEO Huduma kuu tano zinazoorodheshwa katika Waefeso sura ya 4 zinabeba matendo na kazi za hao walioitwa na si vyeo. Wameitwa kuongoza na kuwafundisha wafuasi wengine wa Kristo. Kwa mfano, mchungaji atatunza waumini, kuwalisha Neno la Mungu, na pia kuwashauri. Wachungaji wanakirimiwa na kuitwa na Yesu kufanya hivyo. Mchungaji atajibu kwa Mungu jinsi alivyotunza na kufundisha ‘kondoo’ wa Mungu. Mwinjilisti naye ana kazi. Wito wake na huduma yake vilevile zinatoka kwa Yesu. Ni watu wake ambao wamechaguliwa kuhubiri habari za Yesu Kristo na Msalaba wa Yesu. Kila mtumishi-kiongozi awe wa kike au wa kiume amekirimiwa katika huduma yake kwenye eneo la huduma. Mchungaji anashughulika na matatizo na pia mahusiano katika kanisa. Ni lazima ahakikishe kuwa watu wanakua na pia wawe na afya zao za kiroho. Anaweza kuwafundisha nidhamu, kama mchunga kondoo anavyosaidia kundi lake. Hatatumia nafasi yake vibaya ili kuwa na amri juu ya watu au kufaidika nao ili atosheleze tamaa zake. Kwa kawaida wainjilisti wamekirimiwa kuwa na vipaji vya kupambanua roho na pia ujasiri wa kupingana na mapepo na roho wabaya zenye kupinga kazi ya Injili pale ambapo mwinjilisti ametumwa kuhubiri. Wana uwezo wa kuhubiri Habari Njema kwa nguvu, pamoja na ishara zitokazo mbinguni huwapa uhakika wa ujumbe wao. Siku zote wainjilisti hutarajia mafanikio pale wanapokuwa wanahubiri kwa usikivu kwa Mungu kwani wanavyofanya hivyo wanakuwa wanafanya kazi ya wito wao na pia wananena kweli ya Injili (Warumi 1:16) . UINJILISTI SIO CHEO Watu wanaopenda cheo husisitiza kuheshimika kwa vyeo vyao. Muda si mrefu wanadhani kuwa wao ni bora zaidi ya wengine. Lakini Yesu alisema, “Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 18:4). Soma zaidi kuhusu Yesu alivyosema kwa wafanyakazi na wafuasi wake kuhusu kuwa na utumishi mnyenyekevu katika Marko 9:33-35 na Yohana 13:3-15. Wengi wanadhani kwamba kupata cheo kunawastahilisha kuwaongoza wengine; lakini sivyo. Wengine wanadhani ni lazima waoneshwe heshima kubwa kama wana cheo cha “Uinjilisti”. Hata hivyo, wapo wanaume na wanawake ambao wanampenda Yesu na pia hushirikisha watu habari za Kristo katika miji na vijiji vingi. Hawana cheo au kukubalika zaidi, walakini wao ni wainjilisti wa kweli ambao wanafanya kazi iliyotakiwa. Paulo aliwaleta watu wengi Korintho kwa uwezo wa kuelewa wokovu wa Yesu. Paulo aliwaambia kuwa wao ni barua yake iliyokubalika. Kazi yake na wito wake vilioneshwa na watu wengi ambao walimwamini Yesu Kristo (soma 2 Wakorintho 2:14 - 3:3 na pia 1 Wathesalonike 2:19-20). Sehemu Ya Kwanza Mwinjilisti Ni Nani? Sehemu Ya Pili Msingi Wa Uinjilisti Sehemu Ya Tatu Ujumbe Wa Mwinjilisti Sehemu Ya Nne Kazi Ya Mwinjilisti Sehemu Ya Tano Mfano Wa Mwinjilisti Filipo Sehemu Ya Sita Ishara & Miujiza Na Mwinjilisti Sehemu Ya Saba Kuhubiri Ujumbe Ulio Wazi Wa Injili. Sehemu Ya Nane Mungu Anavyomuandaa mwinjilisti UTUMISHI Waraka wa Yakobo unatufundisha kuonesha imani yetu kwa kazi zetu, na siyo kwa maneno tu (Yakobo 2:14-20). Ni kosa kufikiri kuwa cheo pekee ndicho kinachokufanya uwe mwinjilisti. Huduma ambayo Yesu aliitoa siyo cheo. Utumishi ni huduma. Inamaanisha kufanya kazi ngumu, kuudhamini wito wako na pia kujitoa kwa Mungu. Utumishi siyo kupokea cheo ili uheshimike mbele za watu. Kazi inayofanywa na mwinjilisti ni kazi ya kumpendeza Mungu na pia inaleta heshima mbele za Mungu Mwenyewe. Biblia inafundisha, “Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe...” (Mithali 27:2). Acha watu wakubali kipawa chako kwa kazi yako na matunda yako na siyo wewe mwenyewe ujipe cheo. Yesu alisema, “Utawatambua kwa matunda yao” (Mathayo 7:16). Mchungaji anafahamika kwa utunzaji na mafundisho yake mazuri kwa kondoo wake anaongoza na kulinda watu wa Mungu. Mwinjilisti anafahamika kwa kuwaongoza watenda dhambi kuja kwa Kristo na pia kuwaleta katika Kanisa. Mojawapo Ya Karama Tano Za Uongozi Uinjilisti ni kazi kubwa na nzuri ya wito. Lakini hakuna mtu atakiwaye kujivuna kwa wito wake kwani Yesu ndiye anayetoa kipawa hiki. Uinjilisti ni mojawapo ya karama tano za uongozi iliyopewa Kanisa, zikiwa na mpango maalum wa utendaji. Wachungaji na waumini ni lazima wakubali mwinjilisti ni kama zawadi, na pia waishi naye vizuri. Wainjilisti, kama walivyo wachungaji, wapewe heshima na pia wawezeshwe kifedha (1 Wakorintho 9:14; 1 Timotheo 5:17). Kwa upande wake mwinjilisti anategemewa awe kiongozi na kutumika katika nafasi ya uinjilisti. Wakristo na viongozi ni lazima wakubali kuwa kila Mkristo ni kiungo muhimu sana katika Mwili wa Kristo (1 Wakorintho sura ya 12 & 14; Warumi 12:3-8). Kila Mkristo ni muhimu na pia ana kazi ya kumfanyia Mungu katika ulimwengu huu. Ni vizuri kufikiria huduma kuu tano katika kanisa (Waefeso 4:11-12) kama ni watu wanaofanya kazi kwa bidii kuitimiliza kazi ya Mungu na mipango yake. Wanatumika kwa kipawa maalumu maana wanamtii Yesu. Wanafikia malengo maana wamechaguliwa na Yesu. Ni vema kuwafikiria hawa viongozi, badala ya ofisi zao na vyeo vyao na mamlaka yao kueleza wengine ya kufanya. MATUNDA KATIKA UTUMISHI Wachungaji, waalimu, wainjilisti, mitume, na manabii wanaofanya kazi kwa bidii kutimiliza wito wao na pia kumfurahisha Mungu watalifanya Kanisa imara na hai. Ni vizuri kutumika kwa uadilifu na moyo zaidi badala ya kukumbatia vyeo na kuamini ubembelezaji wa watu. Yakobo 3:16 anasema, “Maana hapo palipo wivu na ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya”. Ni mpango wa Mungu kwa walio nao wito miongoni mwa huduma kuu tano wafanye kazi pamoja; kila mmoja kwa wito wake, na pia hupata matunda kwa Mungu. Tafuta kuzipata roho zinazopotea na pia fanya kazi na watu wengine, na kila mtu ataelewa kuwa wewe ni mwinjilisti wa kweli. Kazi yako itatoa ushuhuda wako. Wachungaji Na Wainjilisti Wanatakiwa Wasaidiane Wachungaji na wainjilisti wana kazi tofauti na wana wito tofauti, lakini wote ni wafanyakazi kwa pamoja hapa duniani kwa Yesu Kristo. Wachungaji na wainjilisti ni lazima wathaminiane na kuheshimiana kwa vipawa vyao na pia wito wao. Wito wa mtu mmoja siyo bora zaidi ya wito wa mwenzake; wote ni muhimu. Wachungaji na wainjilisti wana kazi tofauti. Ni lazima wajitahidi kusaidiana katika kazi ya Injili. Wengine wamesema mchungaji ni kiongozi muhimu zaidi katika Kanisa. Hii siyo kweli. Viongozi wote wa Agano Jipya ni muhimu na pia wana thamani kwa Mungu na kwa malengo Yake. Kumbuka Yesu amewaita na kuupa ulimwengu wanawake na wanaume wenye vipawa vya kiroho. Wakati Yesu akiwa hapa duniani, alitumika kama mtume, mwinjilisti, mchungaji, mwalimu, na pia nabii. Na sasa kazi hizo ameziacha kwa wengine (Waefeso 4:11-12). Mwinjilisti anamsaidia mchungaji kuwaleta Wakristo wapya katika Kanisa. Kanisa linaongezeka. Mwinjilisti anajua kuwa mchungaji atamfundisha muumini mpya na kumsaidia kuwa imara katika Kristo. Mchungaji anamsaidia mwinjilisti kwa kumwombea, kuwatia moyo watu kumsaidia mwinjilisti katika kazi yake, na kumsaidia kwa msaada wa fedha na mali. Mchungaji na mwinjilisti ni watu wanaoishi pamoja tena wanahitajiana tena wanapendana (Warumi 12:10; Waefeso 4:1-6). Hakuna anayemwambia mwenzake afanye nini; wote wapo chini ya mamlaka ya Mungu. Wengine Ni Wachungaji–Wainjilisti Maeneo mengi watu wanaokolewa kwa muda mfupi. Wanatakiwa wafundishwe na wakue katika maisha yao na Yesu. Mwinjilisti anayehubiri ujumbe wa Kristo na kuwapata waumini anatakiwa kuwatunza hawa kondoo katika kundi lake Mungu hadi mchungaji apatikane na pia awatunze hawa waumini wapya. Wapo wanaume na wanawake ambao “wana miito ya aina mbili” - kuwaongoza watenda dhambi kwa Yesu na pia kuwafundisha kama waumini wapya. Ni wito waliojitia kuwafanya watu wawe waumini wa Kristo. Unaweza ukawa wewe ni mchungaji ambaye una wito wa uinjilisti. Kama saa zote wewe unatafuta waliopotea kwa Yesu, unatunza yale mtume Paulo aliosema kwa Timotheo kama mchungaji, “Fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako” (2 Timotheo 4:5). Mungu amekuweka wewe hapo mahali ulipo ili utunze kondoo, na pia unaweza ukafanya uinjilisti hapo ulipo. Pengine Mungu anataka uanzishe kanisa lingine katika mji au jiji lingine. Karama yako ya uinjilisti itakusaidia kuwapata watu waokoke. Lakini angalia usijaribu kuwafundisha wale ambao wana wito wa wainjilisti wawe wachungaji. Mwinjilisti Ni Mtaalamu Mungu amezungumza na wanaume au wanawake maalumu kuhubiri na pia kueleza ujumbe wa wokovu. Mwinjilisti atasema “Ndio” kumtumikia Mungu katika njia hii. Kila Mkristo ameamriwa kushiriki imani yake katika Yesu Kristo na wengine (Mathayo 28:18-20; Marko 16:15; Luka 24:46-48; Matendo 1:8). Kila Mkristo anatakiwa kwa furaha aeleze Kristo ni nani na amemfanyia nini? Wakristo wote wanatakiwa wawalete wengine kwa Yesu Kristo! Lakini mwinjilisti ana wito maalumu katika kufanya hivyo. Mwinjilisti amefundishwa na kuwezeshwa kuwavuta waliopotea kuja kwa Yesu. Mwinjilisti akapewa wito wa maisha kuvua wanaume na wanawake kwa Kristo Yesu. Yesu alimwambia Petro “Njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu” (Marko 1:17). UINJILISTI NI KARAMA Mungu amewapa wainjilisti karama na vifaa vya kazi. Mwinjilisti atahubiri kwa mamlaka na nguvu kwa kuwa ni sehemu ya kipawa chao toka kwa Mungu. Miujiza hutokea wakati mwinjilisti anahudumu lakini ni Injili pekee na siyo miujiza inayookoa (Warumi 1:16; 1 Wakorintho 1:21-24). Mungu anaweza kumfundisha mwinjilisti namna ya kuhubiri ili watu waelewe Injili na kuiamini. Kama wewe ni mwinjilisti, unaweza kumuuliza Mungu akupe dhana na uelewa wa kuifanya kazi yako vizuri. MWINJILISTI NI MUHIMU Katika nchi yetu pasingekuwepo na Mkristo kama hakuna mtu aliyekuja kuhubiri Injili. Mtume Tomaso ndiye wa kwanza aliyesafiri kwenda nchi ya India kueneza Habari Njema. Towashi wa Kushi katika Matendo ya Mitume sura ya 8 alipeleka Injili Afrika. Wainjilisti waliweza wakawepo maaskari wa Kirumi na Wafanyabiashara waliopeleka habari za Yesu Ulaya. Watu waliopotea hawawezi kuokolewa pasipo kufahamu habari za Injili ya wokovu katika Yesu Kristo (Warumi 10:14-15). MWINJILISTI AWEZESHWE NA ATIWE MOYO Mwinjilisti ni mtu, mwanaume na mwanamke, aliyepewa ari ya kueneza ukweli wa wokovu kwa watu wengi inavyowezekana. Hii inaweza kuleta ugumu kwa mwinjilisti. Mara nyingi Mungu anatuma mwinjilisti maeneo ya vijijini au maeneo ambayo Injili inapingwa. Ibilisi anapingana na kazi ya mwinjilisti wa kweli. Shetani anapinga uinjilisti kwa sababu anajua nguvu kubwa ya Injili iwaokoavyo watu kutoka kuzimu, inabadilisha maisha na kuwaweka huru kutoka dhambi na nguvu za mapepo. Mwinjilisti anaombea walio wagonjwa na wale waliopagawa na pepo na kuwaweka huru. Mwinjilisti anawaita watu watubu kutoka dhambi na kumtumikia Mungu aishiye na wa kweli. Wainjilisti wanakwenda mahali na kuwaleta wengine kwa Yesu na hivyo kuwawezesha kuanzisha kanisa. Wachungaji na makanisa ni muhimu wawathamini wainjilisti na kuwawezesha kufanya kazi yao kwa maombi na kifedha. Hatutegemei watu wasiookoka wamlipe mwinjilisti kwa kuwaleta na kufahamu Habari Njema ya Yesu. Ni wajibu wa Wakristo na makanisa kuwawezesha na kuwatia moyo wainjilisti. Kanisa linahitaji wainjilisti! Hata hivyo, kila mhudumu apende kufanya kazi ili aweze kujisaidia mwenyewe. Mtume Paulo alifanya hivi kwa kutengeneza mahema (Matendo 18:1-3; 20:34; 1 Wakorintho 4:12). Paulo anaeleza kuwa ni vema kupokea msaada kutoka kwa wengine kama mhudumu (1 Wakorintho 9:1-23). Lakini Paulo anasisitiza kuwa hakutegemea hali hii, “Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bali kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili” (1 Wakorintho 9:18). Mwinjilisti, na wahudumu wote, watumie hekima na waongoze kwa Roho Mtakatifu katika mambo haya, ili wasipate malalamiko au changamoto kwa ajili yao au Injili ya Yesu Kristo. Yesu Alihubiri Injili Yesu aliposafiri kando kando ya miji ya Galilaya, watu walikuja katoka maeneo mbalimbali ili waponywe na kumsikiliza akihubiri na kufundisha. “Simoni na wenziwe wakamfuata; nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta. Akawaambia, Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea” (Marko 1:36-38). Yesu alikuwa anahubiri nini? La msingi ni Injili! Yesu alihubiri Habari Njema: “Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili” (Marko 1:14-15). Yesu alikuwa akihubiri kama mwinjilisti! Mwishoni mwa huduma ya Yesu, alikuwa akifundisha watu na kuhubiri habari kwamba watu watubu na kumwamini (Yesu) ili waokolewe Ikawa siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri habari njema, wakuu wa makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafula Kazi ya kwanza ya mwinjilisti ni kueleza watu matendo ya ajabu ya Yesu Kristo.(Luka 20:1). Mstari huu unaonesha kuwa Yesu alikuwa akihubiri kwa watu wasioamini karibu na muda wake wa kwenda Msalabani. Kwa kuwa Yesu alihubiri Injili tugundue kwamba huduma ya uinjilisti ni muhimu sana. Mitume Walihubiri Injili Yesu alituma mitume kupeleka Injili “Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri” (Marko 3:14). Baadaye Yesu aliwatuma 70 zaidi kwa kazi hii ya kuwaambia Habari Njema (Luka 10:1,9). Paulo Alihubiri Injili Safari za Mtume Paulo zilimpeleka kwa watu wengi ambao walikuwa hawajasikia habari za Yesu. Katika safari yake ya pili, Paulo na kundi lake walikwenda Makedonia kwa sababu ya ndoto aliyompa Mungu (Matendo 16:9). Katika miji hiyo, alihubiri kama mwinjilisti kwa watu wasio Wayahudi. Baadaye, waumini walikusanyika pamoja na Paulo aliwafundisha kama mchungaji. Kazi yake ya kwanza ni kuhubiri Kristo kwa wote ambao hawakumjua. Baadaye makanisa yalikua katika miji hii. Paulo alikwenda katika miji ya karibu na alihubiri tena kama mwinjilisti. Hata hivyo Paulo alimtuma Timotheo, Tito au mtu mwingine katika kundi lake kufundisha na kuwasaidia wafuasi wapya. Katika Makedonia, Paulo alikwenda Filipi, Thesalonike, Beroya, Athene na hatimaye Korintho (angalia Matendo 16:9 - 18:7). Kila mara, jambo la kwanza alihubiri kama mwinjilisti. Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaeleza kuwa Paulo alikaa Korintho kwa miezi 18 kwa amri ya Bwana. Alitenda yote mawili ya kuhubiri kama mwinjilisti na kufundisha na kuongoza watu kama mchungaji. Wanafunzi Wengi Walihubiri Injili Mariamu Magdalene alitumwa na Yesu kama mwinjilisti wa kwanza kuwaambia wanafunzi kuwa amefufuka kutoka kwa wafu (Yohana 20:17-18). Filipo aliitwa “mwinjilisti” (Matendo 21:8). Wengine walifanya kama wainjilisti kabla ya kuwa wachungaji. Petro alihubiri kama mwinjilisti siku ya Pentekoste Safari za Mtume Paulo zilimkutanisha na watu wengi ambao bado hawajamsikia Yesu. (Matendo 2:14-36). Aliwahubiria watu ambao walijua Mungu wa kweli lakini ambao walikuwa hawajamwamini Yesu. Mahubiri yake katika Matendo ya Mitume sura ya 2 yatatupa ukweli wa Yesu na maelezo ya ukweli kuwa - wakati Yesu alipokufa, ilikuwa na maana muhimu. Petro aliwaambia watu pia kuhusu mambo ya kufanya, sasa wanapojua kazi ya Mungu kwa njia ya Yesu Kristo (Matendo 2:37-39). Waandishi wanne wa Injili katika Agano Jipya wana ujumbe ulio wazi wa uinjilisti na makusudi (Mathayo 28:18-20; Marko 1:1; Luka 1:1-4; Yohana 20:31; 1 Yohana 1:1-4). Mathayo, Marko, Luka, na Yohana wanatimiza kazi ya uinjilisti kwa sababu wameandika habari za Yesu ili kila mtu apate kusoma. Wameandika vitabu vinne vya kwanza vya Agano Jipya. Wanaeleza jinsi Yesu alivyoteswa, alivyomwaga damu yake Msalabani, na kufa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu. Injili pia inauambia ulimwengu jinsi Yesu alivyofufuka kutoka kaburini na kushinda kifo. Waandishi wa nyaraka za Agano Jipya wanatimiza kazi ya uinjilisti. Paulo, Petro, Yakobo, Yohana, Yuda, na mwandishi wa Kitabu cha Waebrania wanaeleza umuhimu wa ukweli wa Injili. Kila mwinjilisti (na kila mwamini) anapaswa ajifunze nyaraka na kupata ufahamu wa kweli wa Habari Njema za wokovu katika Yesu Kristo. Maandiko yana nguvu, yasiyo na makosa na vyanzo muhimu ambavyo Mungu ametoa kwa kila mtu. SEHEMU YA PILI: MSINGI WA UINJILISTI Hii ni sehemu muhimu kwa wachungaji na wainjilisti kuisoma. Hii itawasaidia katika kufundisha uinjilisti kwa wengine. Kila nyumba inahitaji msingi imara. Kama msingi haujasimama wima, siyo imara, au umejengwa kwa vifaa vibaya, nyumba inaweza kuanguka, hasa wakati wa dhoruba (Mathayo 7:24-27). Habari za nyumba mbili, uliyoelezwa na Yesu inafanyika kwa lolote ufanyalo kwa Mungu. Huduma, familia, na maisha yako binafsi lazima ujengwe katika msingi imara ambao hautatia ufa na hautaoza. Ndiyo ilivyo kazi ya uinjilisti. Uinjilisti haufahamiki vema kwa viongozi wengi wa Kanisa. Wengine wanafikiria uinjilisti ni kuwa na mkutano ya kanisa na kutegemea wasiookoka waje kanisani na kuitikia Injili. Wengine wanafanya makosa kwa kuwaambia watu wafuate taratibu fulani za Kikristo, badala ya kuwaonesha hitaji la kumpokea na kumfuata Kristo. Kuwapata watu na kuwaingiza katika hali fulani na kuwafanya kufuata taratibu zao siyo kuwaleta kwa wokovu katika Kristo! Kuwa Mkristo maana yake ni kuwa mmoja anayepokea na kumfuata Kristo na kuwekwa katika uhusiano mzuri wa Mungu Baba. Huokolewi kwa kujiunga na kanisa au kufuata mapokeo ya kidini. Kuokolewa ni kupokea Yesu aliyefufuka, kutoa maisha yako kwa Yesu, kumtegemea Yeye na kazi Yake ya kutuokoa Msalabani, na kumfanya Yeye kuwa Bwana na Mwokozi wako. Ni lazima kuwakilisha ukweli wote wa Injili ya Yesu Kristo. Hii ndiyo sababu ni vema kujifunza yale ambayo Biblia inatufundisha kuhusu uinjilisti na ukweli wa ujumbe wa Injili. Ujumbe wa uinjilisti usifanywe kuwa ni kitu kigumu. Uwekwe wazi, uwekwe sawa na rahisi kueleweka katika kuwakilisha Ukweli wa Yesu kama Maandiko yasemavyo. Ni muhimu utolewe katika hali itakayomfanya msikilizaji aelewe. Hii ndiyo kazi ya mwinjilisti. Injili Ni Kuhusu Mtu – Yesu Paulo anatoa ujumbe kwa Injili rahisi katika 1 Wakorintho 15:1-5: Yesu Kristo alikufa kama dhabihu kwa dhambi zetu, alizikwa, na alifufuka toka kwa wafu na kutupa wokovu na kufanya tuwe na uhusiano na Mungu. Hii ndiyo Injili iokoayo. Uinjilisti Ni Kutangaza Injili Kuwashirikisha Injili maana yake kuwaambia matendo makuu Yesu aliyotenda. Yesu anawapenda watu sana hata akafa badala yao na kuchukua mwenyewe adhabu ya dhambi zao. Wakati Yesu alipofufuka toka kwa wafu, alishinda dhambi, kifo, kuzimu, na nguvu zote za uovu. Hii ni habari njema kwa kila mtu dunia yote! Mambo Yaoneshayo Uinjilisti Kuelewa na kutumia maneno haya kutakusaidia kuwakilisha Injili kwa njia iliyo wazi ili kila mtu apate kuelewa mpango wa Mungu wa wokovu. Upendo: Mungu anakupenda na alimtoa mwanaye afe na kuchukua adhabu ya dhambi yako. Upendo wa Mungu ni upendo wa milele, upendo usio na mipaka au masharti. Mungu anakupenda pamoja na kuwa una dhambi na unamchukiza. Hakuna kitu wala yeyote awezaye kubadilisha upendo wa Mungu kwa ajili yako Yohana 3:16; Warumi 5:18; 8:31-39. Kutubu: Ina maana kubadilisha mawazo, inayotokana na kubadilisha kusudi na maamuzi. Hivyo, kutubu ni kuamua kubadilisha dira/mwelekeo kugeuka kutoka ubaya na njia ya uovu na kumgeukia Mungu. Toba si kusema tu samahani; inahusisha kuungunukia dhambi na kubadili tabia Mathayo 3:8.Kutubu ni kukubali kuwa mwenye dhambi na kuchagua njia ya Mungu badala ya njia zako mwenyewe Marko 1:15; Luka 7:44-49.Matendo 26:20). Kusamehewa: Kila mtu amefanya dhambi na anahitaji kusamehewa. Kila mmoja anahitaji kujua kuwa aibu na hatia ya dhambi zinaweza kuondolewa. Msamaha wa Mungu maana yake Mungu amekuondolea mzigo wa lile baya lililokuumiza. Amechukua na amesahau dhambi zako (Warumi 4:6-8; Waefeso 1:7). Uzima Mpya (Uzima wa Milele): Yesu anatoa uhai mpya kwa wote wanaomwamini. Unakuwa kiumbe kipya (2 Wakorintho 5:17). Unapokea maisha mapya, msamaha wa dhambi zako, amani ya moyo wako, upendo wa Mungu kwa ajili yako na wengine, na kuishi maisha mapya. Pia utaishi maisha ya milele na Yesu Kristo mbinguni (Yohana 3:1-6; 10:27-29; 1 Yohana 5:11-12). Uhusiano: Uhusiano kati ya Mungu na mtu unawezekana kwa njia ya Yesu Kristo tu. Dhambi zetu zinatutenga na Mungu Mtakatifu, lakini wakati tunapokea dhabihu ya Kristo kwa ajili ya dhambi zetu na msamaha wake, Mungu hatuhesabii tena dhambi kinyume chetu (soma Warumi 4:4-8). Mungu anatuhesabia “wenye haki” kwa sababu ya kazi ya Kristo, na tunaweza kuwa na uhusiano na Mungu na kumkaribia (Warumi 3:23-24; 5:18-19; 1 Wakorintho 1:30; 2 Wakorintho 5:21). Wokovu na uhusiano wetu na Mungu hauji kwa kutunza orodha za sheria “usifanye hiki” na fanya hivi. Ni ukweli kuwa kama tutampenda Mungu, tutatimiza amri zake (Yohana 14:15). Lakini kazi zetu haziwezi kutuokoa (Waefeso 2:8-10). Yesu alimfunua Mungu kwetu sisi kama Baba yetu Mathayo 6:9; Yohana 14:7-9. Tunaweza kumfahamu Mungu na anaweza kutujua sisi (Yohana 17:3; 2 Timotheo 2:19). Ndiyo maisha ya Mkristo - siyo matambiko matupu, kuishi kwa woga au kutenda mema kiasi cha kukubaliwa na Mungu. Kuamini: “Kuamini” ni kuweka tumaini, kuwa na imani, kushawishiwa kabisa, kutegemea. Kuamini Yesu ni kuweka tumaini lote kwake na kuwa mfuasi wake. Hili si jambo la kukubali tu kiakili; ina maana kuyatoa maisha yako kabisa kwa Yesu (Yohana 1:12). Kuamini ni kushawishika kuwa utakiri kwa maneno imani yako kwa Kristo (Warumi 10:9-10). Kuzimu/Jehanum: Biblia inatoa maelezo ya ziwa la moto lililopo kwa ajili ya Shetani na malaika zake Mathayo 25:41. Yesu alisema kuwa kuzimu kuna “giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno” (Mathayo 8:12). Wote wanaomkataa Yesu Kristo na kazi zake palepale wanaamua kutenda dhambi na kufuata njia zao. Mbaya zaidi, watamfuata Shetani mpaka mahali pa adhabu ya milele, kuzimu/Jehanum. Mungu hakukusudia hili kwa watu wake na si kusudi lake yeyote aangamie na kuteseka milele (1 Timotheo 2:4; 2 Petro 3:9). Lakini kila mtu ni lazima achague Yesu kuwa mwokozi wake na kuishi na Mungu au kuteseka milele na kutengwa na Mungu huko kuzimu. Mambo Manne Ya Msingi Wa Injili Injili ina mambo makubwa manne. Wakati wowote unapohubiri ujumbe, au unapomshirikisha mwingine, kuandika barua, au kuzungumza na kundi la wanaume au wanawake, ujumbe muhimu unafanana. Mambo haya ni: Mpango wa Mungu - Kuasi kwa Mwanadamu - Kazi ya Yesu ya Kutokoa – Itikio la Mwanadamu. Jifunze Maandiko yaliyoko chini ili upate kujifunza zaidi katika kila jambo. [Wachungaji: Uwafundishe watu wa kanisa lako ili waweze kuwashirikisha wengine Injili! 1. MPANGO WA MUNGU • Mungu anakupenda (Yohana 3:16; Warumi 8:35-39) • Mungu amekusudia kukupa maisha tele ya milele na kuwa na faragha naye (Yohana 10:10; Ufunuo 3:20) • Mungu amekusudia mema kwa ajili ya maisha yako (Yeremia 29:11; Warumi 8:28) • Mungu amekusudia wewe umfahamu (Yohana 7:3) 2. Dhambi ya Mwanadamu • Dhambi ni uasi dhidi ya Mungu na njia zake (Yohana 3:19-20; Warumi 5:10) • Dhambi inatutenga na Mungu (Waefeso 2:12; 4:18) • Kila mtu ametenda dhambi, imeleta maumivu makubwa, mateso na kifo katika ulimwengu (Warumi 3:23; 5:12) • Haki ya kweli ya Mungu inaleta hukumu kwa dhambi ya Mwanadamu (Warumi 6:23) 3. Kazi ya Yesu Kristo ya Kutuokoa • Yesu alikufa Msalabani badala yetu kutulipia gharama ya dhambi zetu (Wakolosai 2:13-15; 1 Petro 2:24) • Yesu aliweka njia pekee kwa ajili yetu ili tuweze kumrudia Mungu (Yohana 14:1-6; Matendo 4:12) • Yesu alishinda dhambi na kifo na alifufuka toka kwa wafu (Warumi 1:3-4, 1 Wakorintho 15:20-23) • Yesu anatupa msamaha wa dhambi, anatupa amani, upendo, na maisha mapya (Yohana 10:10; Warumi 5:1) • Yesu anaishi leo kama Mfalme wa wafalme (Ufunuo 1:17-18; 19:16) 4. Itikio la Mwanadamu • Ni lazima niitike lile ambalo Yesu amesema na kufanya (2 Wakorintho 6:1-2) • Nikubali dhabihu ya Kristo kwa ajili yangu na dhambi yangu (Matendo 2:37-41; 16:30-34) • Nimwambie Yesu anisamehe dhambi zangu na awe Bwana na Mwokozi wangu (Yohana 3:15-16; Waefeso 1:7) • Nigeuke kutoka maisha ya dhambi na kuishi kwa Neno la Mungu na mpango wake (Warumi sura ya 6; Waefeso 4:17-32) • Nimfuate Kristo kila siku (Luka 9:23-26; 1 Yohana 1:7) • Niwashirikishe wengine imani yangu kwa Yesu (Mathayo 28:19; Marko 16:15) Kutoa ujumbe mzuri wa Injili – kwa kutumia mambo haya manne yanaweza kuwa hivi: Kuna mmoja mwenye nguvu kuliko wote, Mungu, ambaye ameumba ulimwengu wote. Yeye ni mkamilifu mtakatifu na wa haki; mkubwa kuliko chochote au yeyote. Hakuna kinachoweza kulinganishwa na ukubwa na nguvu za Mungu mwenye enzi. Mungu huyu anakupenda. Amekuumba ili uwe naye. Amekusudia kuwa na uhusiano na wewe. Lakini kuna jambo ambalo limetokea kati yetu na Mungu. Kuna jambo linakuzuia usiwe na uhusiano na Mungu na kujua upendo wake na kusudi lake kwa ajili yako katika maisha haya. Hili linaitwa dhambi. Dhambi imekuja kati yako na Mungu. Dhambi inaleta shida nyingi na matatizo katika ulimwengu. Dhambi ni kama kusema uongo, kudanganya, chuki, kuiba, mawazo mabaya, mauaji. Biblia inatuambia kuwa moyo wa kila mwanadamu umejaa dhambi Yeremia 17:9. Tangu Adamu na Hawa (Eva) (wanadamu wa kwanza) hawakumtii Mungu katika bustani ya Edeni, kila mtu amezaliwa na asili ya dhambi Zaburi 51:5. Dhambi ni kama ukuta, unaokufanya ujitenge na Mungu. Kwa sababu ya dhambi ya asili, tunataka tuishi tutakavyo kuliko kuishi katika njia ya Mungu. Watu wote wamefanya dhambi 1 Wafalme 8:46; Warumi 3:23). Haki ya Mungu iliyo timilifu inataka tuadhibiwe kwa dhambi zetu. Mungu anajua tu wafu ndani yetu kwa sababu ya dhambi zetu (Waefeso 2:1; Wakolosai 2:13). Amemtuma mwanaye, Yesu Kristo, achukue adhabu tuliyopaswa sisi kwa ajili ya dhambi zetu na afe badala yetu Msalabani. Yesu alivunja ukuta wa dhambi na kufanya njia yetu ya kumrudia Mungu. Yesu alifufuka toka wafu kuonesha kuwa Yesu ni Mungu (Warumi 1:4). Yesu Kristo anaishi milele kama Mfalme aliye Mkuu kuliko mfalme yeyote yule Unaweza kuamini kuwa hii ni kweli kwa kukubali dhabihu ya Kristo. Unaweza kukubali kuwa wewe ni mwenye dhambi, mwambie Mungu kuwa najutia makosa yangu, na kupokea msamaha wa Kristo, na kuishi kwa amani na Mungu. Uchaguzi ni wako mwenyewe: Mwamini Kristo na kupokea msamaha, au kuendelea katika dhambi zako na kuishi katika uharibifu sasa na hata milele. Je, unachagua kumwamini Yesu Kristo? Kuna njia nyingi za kuzungumza juu ya mambo haya manne. Kuelezea mambo haya manne ya Injili kutakuwa rahisi unavyojizoesha kufanya mara kwa mara. Unaweza kuanza kwa kuyasema kwa sauti mwenyewe; baadaye jizoeze na Wakristo wenzako; na hatimaye anza kuwaelezea wasioamini. Jozi Katika Kupeleka Injili Hapa kuna “jozi” ambayo inafanya kazi pamoja wakati wa kupeleka Injili. Jifunze kuitumia; itakusaidia katika kushirikisha Injili wazi na kuwaongoza watu katika kumkubali Kristo. Jozi Ya Kwanza - Habari Zako Mwenyewe & Neno La Mungu Waeleze habari zako au shuhuda au jinsi ulivyoanza kuamini Yesu inasaidia watu kumwona Mungu na kwamba anapenda kuwasaidia wao binafsi pia. Ni vema kutoa neno la shukrani na kuwaambia wengine mambo ambayo Mungu amekutendea (Luka 8:39). Wakati mwingine inasaidia unapowaambia habari za watu wengine. Ushuhuda wa mambo ayatendayo Mungu kugeuza maisha ya watu ni ushuhuda wenye nguvu kuhusu uwezo wa Kristo kubadilisha maisha ya mtu. USHUHUDA MZURI UNA MAENEO MATATU: 1) Maisha yangu yalikuwaje kabla ya mimi kukutana na Yesu? 2) Ilikuwaje nikakutana na Yesu (ni mazingira yapi yaliyonileta kwa Kristo)? 3) Maisha yangu yana tofauti gani tangu nikutane na Yesu? Kama utajibu maswali haya matatu utatoa ushuhuda mzuri unapozungumza. Usiwaambie kila kitu, lakini chagua yale mambo muhimu. Usiweke mkazo sana katika mambo mabaya uliyotenda zamani, lakini eleza uzuri wa Yesu na jinsi alivyobadilisha maisha yako. Ni vema ukaandika ushuhuda wako. Siyo lazima ushuhuda Kuhadithia au kutoa ushuhuda wako juu ya jinsi ulivyoweza kumuamini Yesu Kristo kutasaidia watu waone kuwa Mungu anajishughulisha nao pia. wako ukawa mrefu sana. Unaleta mafanikio mazuri kama utaelezwa kwa habari fupi. Neno la Biblia lina uhai na lina nguvu. Hakuna neno jingine ambalo ni muhimu zaidi. Washirikishe maneno ya Biblia, kwani Neno la Mungu lina nguvu kuokoa wenye dhambi: Kwa kuwa nimezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele…. Neno la Bwana hudumu hata milele. Na neno hili ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu”1 Petro 1:23-25; angalia pia Yakobo 1:18). Biblia ndiyo zana yetu muhimu. Shuhuda zetu pia zaweza kuwa zana muhimu. Tumia zana hizi mbili (jozi) pamoja wakati unaposhuhudia Yesu au wakati wa kuhubiri. Jozi Ya Pili – Neno & Roho Wakati unaposhuhudia au kuhubiri kwa ajili ya Kristo, tumia maneno ya Biblia. Katika baadhi ya tamaduni, wana ufahamu mdogo wa elimu. Wanaweza wakawa hawajui hata kusoma. Maneno uyatumiayo yawe na mpaka na yawe marahisi. Kama ikilazimu, kwa uangalifu, chukua neno la Mungu na kulifanya rahisi kwa wengine kulielewa. Kwa mfano, unaweza kusema, “Watu wote wamefanya mambo mabaya na kutokumtii Mungu; tunapaswa tuadhibiwe, lakini Mungu ametoa msamaha kwa njia ya Kristo. Hii ndiyo ukweli unaopatikana katika Biblia katika Warumi 3:23 na Warumi 6:23, kwamba umeweka katika maneno marahisi. Lakini uwe mwangalifu sana usibadilishe kamwe maana ya yale Biblia inasema. Roho Mtakatifu ni sehemu ya pili ya jozi hii. Yeye ameahidi kuwa atakusaidia kuelewa na kukumbuka yale ambayo alifundisha Yesu (Yohana 14:26; 15:26; 16:13). Ni Roho Mtakatifu anayemfanya mwenye dhambi kushawishika na kuongoza wengi wamwamini Yesu (Yohana 16:8). Pasipo kazi ya Roho Mtakatifu huwezi kuwaleta watu katika wokovu. Roho wa Mungu ameahidi kutupa uwezo wa kuwa mashahidi (angalizi: “Ujazwe na Roho Mtakatifu” katika Sehemu ya Saba). Ni vema umwambie Roho Mtakatifu akupe nguvu na ujasiri. Hubiri kwa kutumia Neno la Mungu na amini Roho Mtakatifu kuleta moyo wa kupokea. Ni mapenzi ya Mungu kwa watu wote waokolewe na kujua ukweli (1 Timotheo 2:4); hivyo Mungu atakusaidia! Jozi Ya Tatu – Maombi & Maandalizi Unaweza kupata mafanikio makubwa katika kuwaleta watu kwa Yesu kwa kadri utakavyokuwa unawaombea wale utakaowaendea kuwashirikisha Injili. Ni muhimu kuwaombea watu na maeneo ambayo utakwenda kuhubiri. Inawezekana Mungu atakupa mzigo katika mawazo yako kwa mtu fulani. Utapaswa kuomba mara kwa mara kwa ajili ya mtu huyu. Unapaswa pia uwe na maandalio. Maandalio ni pamoja na: • kusoma na kujifunza Neno la Mungu • andaa ujumbe (angalia Sehemu ya Saba katika gazeti hili) • jizoeze katika lile utakalosema • tumia muda mwingi na Mungu katika maombi Chukua muda na ujiulize, “Nichukue habari ipi ya kumwendea mtu huyu au kikundi?” Kariri mistari katika Biblia. Mwombe Yesu akuoneshe njia nzuri ya kuwashirikisha watu wengine. Kama utachukua tahadhari nzuri, Mungu atakusaidia ili watu wengi waje na kumfahamu Kristo. Jozi Ya Nne – Nenda Mkiwa Wawili Wawili Yesu aliona ni muhimu watumishi wake wasiende mmoja mmoja, bali “wawili wawili”. Kama unashuhudia katika maeneo ya barabarani, chukua mtu mwingine atakayekuombea kimya kimya wakati unazungumza. Hili ni jambo zuri. Kufanya wawili wawili kunatoa nafasi ya kuelimisha wengine katika Neno la Biblia ni hai na lina nguvu. kazi ya kushuhudia na uinjilisti. Mnaweza pia kutiana moyo na kusaidiana. Katika Nchi ya Afrika Kusini kuna wanaume vijana na wanawake wanaompenda Yesu Kristo na wanafanya kazi kila siku kuleta roho za watu kwa Yesu. Wengine ni wanafunzi na wengine ni wafanyakazi. Hawafanyi kazi ya uchungaji ya kanisa bali ni wavuvi wa roho za watu. Kila juma wanatoka na kwenda barabarani au katika nyumba kuwaambia wengine habari za Yesu. Wamejifunza mambo manne ya kueneza Injili na wangeelewa zana muhimu (hii jozi) za kutumia. Wanaomba na kujiandaa wenyewe ili kuwashuhudia. Mwanamke analeta watu wawili hadi wanne kila juma anapotembelea mjini wakati wa chakula cha mchana na kuongea na watu. Anawaongoza watu kwa Yesu na kuwaleta kanisani. Haya Ni Mpaenzi Ya Mungu Kwa Kila Mkristo: Uufahamu ujumbe wa Injili, ujue jinsi ya kupeleka ujumbe na jinsi ya kuzungumza pasipo woga au aibu. Kila Mkristo ni muhimu ajifunze jinsi ya kuwashirikisha wengine Injili kwa njia bora ili upate mafanikio mengi. Uwe Wazi Wakati Unapoongea Biblia inasema, “Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?” (Warumi 10:14). Watu wanawezaje kuokolewa pasipo kuelewa ujumbe wa neno? Ni muhimu kujifunza jinsi ya kupeleka Injili kwa njia iliyo rahisi na iliyo wazi ili watu waelewe uamuzi ambao wanaitwa kuufanya na wauamini katika ukweli wake. (Angalia Sehemu ya Tatu, Ujumbe Wa Mwinjilisti.) Wakati mwingine maneno ya kidini tunayotumia yanaeleweka kwetu, hata hivyo yanasikika kama lugha mpya kwa mtu asiyeelewa. Epuka kutumia maneno yasiyoeleweka kwa watu ambao hawana ufahamu wa Kikristo. Tumia maneno ya kawaida katika kueneza Injili. Kama utatumia maneno ya Kikristo uwe na uhakika wa kuyaelezea na mawazo ya Injili wasiyoyajua. Zaidi ya hayo yote, hakikisha maneno uyatumiayo yanaeleza ukweli wa Injili nzima. Mifano Vigumu Kueleweka .Ni muhimu uokolewe, jiachie kwa Yesu. .Haleluya, ndugu maisha ya milele ni kwa ajili yako. .Nimeokolewa na kukombolewa. .Nilikuwa mwenye dhambi lakini sasa nimeokolewa. .Ngoja nikuambie ushuhuda wangu. Rahisi Kueleweka .Unalo hitaji. Kristo alikufa kwa ajili yako na kuchukua dhambi zako. Mpe maisha yako. Rafiki yangu, Yesu anataka uwe na maisha - sasa na milele! Yesu amechukua dhambi zangu na kuniweka huru.” “Maisha yangu yalitawaliwa na dhambi. Baadaye nilikutana na Yesu na akanisamehe dhambi zangu. Amenipa maisha yanayonifanya nitake kuishi.” “Ngoja nikuambie habari zangu jinsi Yesu alivyoniokoa. MAMBO MUHIMU Njia nzuri ya kufuata: Weka maneno yako kuwa marahisi kueleweka bila kubadilisha ukweli wa Injili. Njia ya pili: Jaribu kuelewa mazingira ya watu unaotaka kuzungumza nao. Ukiwaelewa, itakuwa rahisi kuzungumza nao. Ni muhimu kwako – kama mchungaji, mwinjilisti, au kiongozi wa kanisa - uelewe jinsi ya kutoa ujumbe wa Injili. Ni vema ukajua jinsi ya kuwakilisha Injili kwa wazi na kwa njia ya ukamilifu. Mara unapojua njia hii, unaweza kuzungumza habari za Yesu Kristo kila mahali, na kwa kila mtu na kwa njia itakayohitajika wakati huo. Mungu anatutaka tutoe ukweli wa kazi, uhakika, na kwa uangalifu (2 Timotheo 2:15). Hii ina maana zaidi kuliko kuelezea Biblia kwa Wakristo. Hii ina maana pia tuweze kuleta Injili ya Yesu Kristo kwa wanaume na wanawake wasiookoka. Njia Za Kushirikisha Injili 1. Katika uhusiano: Mara nyingine hii inaitwa “uinjilisti kirafiki”. Kuwa rafiki na mtu fulani. Upate nafasi ya kumjua mtu huyo kabla ya kumshirikisha habari za Yesu. Jenga daraja la kuaminika na kutunzana. Mtu atakuwa tayari kufungua moyo wake kusikia habari za Kristo kwa kadri unavyopenda na kuishi maisha yako yawe mfano wa imani mbele ya wengine. Katika hali nyingine (kwa mfano, Waislamu), upate ruhusa ya kuzungumza nao. Watu wanahitaji muda wa kuona kuwa wewe ni mkweli na mwaminifu. Njia hii ya uinjilisti inachukua muda. Huu ndio mwenendo. Ina maana utahusika na maisha ya mtu huyu na uangalizi wake na furaha, mahangaiko na matumaini yake, familia na kazi yake. 2. Nafasi moja tu na kuzungumza: Njia hii ya uinjilisti ni ya haraka na yenye nguvu. Ni kile ambacho unaweza kushirikisha wakati unakaa katika gari moshi au basi karibu na mtu, au wakati umekutana na mtu kando ya barabara. Mara nyingi ni mtu mgeni ambaye hujabahatika kukutana naye. Hii ni kama kukabiliana. Waambie mambo manne ya Injili na kama pana uwezekano muulize kama unaweza kuomba naye ili ampokee Kristo. Wakati mwingine unaweza kumwachia Biblia au kipande cha maandiko au tract (vipeperushi). Unaweza kumwonesha upendo wa Mungu. Mwombe Mungu akupe ujasiri wa kumshirikisha Injili wakati ukiwa na nafasi. 3.Tendo la huduma: Hali ya upole au kujitoa kunazungumza kwa ukubwa zaidi. Kufanya jambo la kumsaidia mtu kunafungua moyo wa kusikiliza Injili ya Yesu. Omba na angalia nafasi ya kumshirikisha habari za Yesu kwa njia hii. Hili ndilo ambalo Mungu ametutendea. Alionesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Yesu kuja kwa ajili yetu (Warumi 5:8). 4.Kutamka hadharani: Aina hii ya uinjilisti ni kuzungumza katika mhadhara wa watu. Wakati mwingine unahitaji kuwakusanya watu pamoja ili uzungumze nao. Nyimbo, waimbaji, wachezaji, au tendo ambalo linaweza kuwavuta watu, na hatimaye kuwahubiria habari njema za Yesu. Huu siyo wakati wa kuhubiri mahubiri marefu. Utoe Injili kwa muda wa dakika tano au sita. Watu hawatangoja ili wakusikilize kama utahubiri muda mrefu. Kumbuka huu si mkutano wa Kanisa! Una muda mfupi tu kushirikisha habari iliyo muhimu kwa watu wanaosikiliza. Huu ni muda wa kuwaita watu waombe nawe ili kumpokea Yesu. 5. Tukio maalum: Kanisa lako na huduma inaweza kukuwezesha katika tukio au wajibu wa kukusanya watu. Makanisa mengi katika nchi mbalimbali wamefanya hivi. Wamekuwa na tamasha la muziki, au sikukuu, kualika wahubiri maalum, kutoa maigizo, kuonesha sinema ya Injili, au tamasha la kwaya. Baadhi ya makanisa wameandaa chakula na kualika wageni ambao hawajaokoka. Watu katika kanisa lako wanaweza kwenda kutoa huduma katika shule au katika hospitali. Hii inaweza kutoa nafasi ya kuwashirikisha Injili kwa kundi la watu. Unatakiwa uweze kuwafanya watu wajisikie kukaribishwa na wasifungwe katika mipaka ya desturi za kanisa fulani. Kama unataka kuwafanya wawe waumini wa kanisa lako, wataweza kuona motisha wa ubinafsi. Lakini kama unataka kuwatambulisha kwa Mwokozi Yesu, watapenda kumpokea Kristo. (na wanaweza kuja katika kanisa lako). Kuna njia nyingi za kuwafikia watu. Mungu atakupa hekima ya kujua jinsi ya kuwashirikisha wengine Injili na kuwaelimisha wengine jinsi ya kufanya hivyo. Jifunze na kumbuka mambo manne ya Injili. Hivyo utaweza kufundisha wengine jinsi ya kuwashirikisha habari za Yesu. Mungu anatutaka tutoe ukweli wa kazi, uhakika, na kwa uangalifu (2 Timotheo 2:15). Hii ina maana zaidi kuliko kuelezea Biblia kwa Wakristo. Hii ina maana pia tuweze kuleta Injili ya Yesu Kristo kwa wanaume na wanawake wasiookoka. SEHEMU YA TATU:UJUMBE WAMWINJILISTI Ujumbe Muhimu Wa Injili Kuhubiri Injili ni kueneza habari ya Yesu. Ujumbe wa mwinjilisti unahusika na maisha, kifo na kufufuka kwa Yesu. Kuwa na ufahamu wa ujumbe wa Maandiko ya Injili, inakupasa usome na ujifunze kwa uangalifu vifungu vifuatavyo vya Biblia. Yesu Kristo Alitabiriwa Mwanzo 3:15 Kumbukumbu 18:15 Zaburi 16:10; 22:1-31; 41:9 Isaya 7:14, 9:6-7; 53:1-12; sura ya 61 Zekaria 11:12-13 Kuja Kwa Yesu Kristo Na Ujumbe Wake Mathayo 1:21; 7:13-14; 18:11 Marko 1:15; 10:27,45; 16:16 Luka 2:10-11; 9:56; 19:10; 23:33 Yohana 1:12-13; 3:16; 10:10,28; 14:1-7; 20:31 Matendo 2:17-39; 3:19; 4:12 Warumi 3:9-26; 5:1-21; 6:17-23; 8:1-11,15-17 1 Wakorintho 15:1-4 2 Wakorintho 5:18-21 Wagalatia 2:16; 3:13,21-26; 4:4-7; 5:16-24 Waefeso 1:1-14; 2:1-18 Wakolosai 1:13-14 1 Timotheo 2:5-6 1 Petro 1:1-5; 3:18 2 Petro 3:9 1 Yohana 4:9-10 Kurudi Kwa Yesu Kristo Mathayo sura ya 24 Yohana 14:1-3 Matendo 1:10-11 1 Wathesalonike 4:15-18 2 Wathesalonike 2:1-2 Tito 2:13 Ufunuo wa Yohana 22:1-5,20 Kuhubiri vizuri kwa mwinjilisti ni lazima aeleze habari za Yesu, kueleza jinsi Biblia isemavyo kuhusu Yesu, na kuwaita watu ili watubu na kumwamini Yesu. Soma Matendo sura ya 2. Hapa Petro alihubiri na watu 3,000 walimwamini Yesu Kristo. Petro aliwaambia ukweli kuhusu Yesu na aliwaelezea watu. Hatimaye Petro aliwaambia makutano waliosikiliza mambo ya kufanya kwa kuwa sasa wamepata kuelewa ukweli. Aliwaambia watubu na kumrudia Mungu na kuamini Yesu na kumfuata. Hubiri Ukweli Wewe pia unaweza kuwaona watu wakija kwa Yesu Kristo; wakati unapohubiri ujumbe wa Injili ya Yesu. Kama Paulo aandikavyo katika 1 Wakorintho 15:1-4: Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiria; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri; isipokuwa mliamini bure. Kwa maana naliwatolea ninyi hapo Kwa mwinjilisti na kuwaita watu ili watubu na kumwamini Yesu... Petro aliwaambia makutano waliosikiliza mambo ya kufanya kwa kuwa sasa wamepata kuelewa ukweli. Aliwaambia watubu na kumrudia Mungu na kuamini Yesu na kumfuata. mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko”. Huu ni ujumbe rahisi: Yesu aliishi, alikufa Msalabani, alizikwa na alifufuka kwa nguvu ya Mungu (angalia Warumi 1:4). Eleza Ukweli Eleza kuwa Yesu alikuja ili kurudisha uhusiano wetu na Mungu anayetupenda (Warumi 5:1; 2 Wakorintho 5:18-20; Waefeso 2:11-18; 1 Yohana 4:9-10). Yesu alikuja ili kutusamehe dhambi zetu (Waefeso 1:7; Wakolosai 1:13-14) na kutuweka huru kutoka kongwa la dhambi (Warumi 6:17-23). Yesu Kristo alikuja kutupa maisha mapya na safi (Waefeso 1:3-4; 2:10; Tito 2:13-14). Amemtuma Roho Mtakatifu wake kutupa nguvu ya kuishi maisha ya haki na kumpendeza Mungu (Warumi 8:1-11; Wagalatia 5:16-23). Kwa sababu ya Yesu, tunawezeshwa kustahimili kama wana wa Mungu Aishiye milele, tuwe warithi pamoja na Yesu (Yohana 1:12-13; Warumi 8:15-17; Wagalatia 4:4-7). Na siku moja, wajibu wetu tuliopewa duniani utakapotimilika, tutakaa katika uwepo wa Mungu milele, kumfurahia Mungu milele (Yohana 17:3; Ufunuo wa Yohana 22:1-5). Mara Zote Uwaite Waitikie Yesu anataka wanaume na wanawake kumwitikia Yeye. Baada ya Yesu kumponya kipofu, Yesu alimtafuta na kumtaka amwamini Yeye (Yohana 9:35-38). Katika Injili ya Yohana mlango wa 4, Yesu alitumia muda kwa kuongea na mwanamke Msamaria kisimani na kumwita amwamini Yeye Mwenyewe - kama Mwana wa Mungu. Mwinjilisti anapenda kuomba itikio la watu mara upatapo nafasi (isipokuwa, labda kwa sababu maalumu wanadhani wasingeweza kufanya). Watu wanahitaji kuusikia ukweli wa Injili na hivyo wafanye jambo fulani kwa lile walilolisikia. Katika mji fulani nchini India, kikundi cha Injili walitembelea gereza kila juma na kuwashirikisha Injili ya Yesu, lakini hawakutoa nafasi kabisa ya watu kumpokea Kristo. Mwishoni mwinjilisti mgeni alikuja na kuzungumza habari za Kristo na kuwaambia watu umuhimu wa wao kumpokea Kristo. Alisema, “Ni wangapi kati yetu wanapenda kuomba nami kumpokea Yesu Kristo kama Mungu wako na Bwana wako?” Wengi wa wasikilizaji waliitikia na kumpokea Yesu. Ni muhimu wakaonesha itikio lao wakati wanaposikia Habari Njema kuhusu mambo ambayo Mungu amefanya katika Yesu Kristo. Waambie watu jinsi ya kuitikia. Ni lazima watubu dhambi zao; ni lazima wamrudie Mungu na kumwomba awasamehe. Ni lazima wapokee kazi ya kafara ya Kristo na kumkubali kuwa Bwana na Mwokozi wao. Kumtaka Yesu awe ndani ya mioyo yao, ni muhimu wakajitoa kumfuata Kristo aliye Bwana. Ujumbe Wenye Nguvu Ni muhimu kuamini kuwa Mungu ameagiza, anawapa nguvu, na kubariki mahubiri ya Neno Lake kuhusu Yesu (Isaya 55:10-11; Warumi 10:14-17; 1 Wathesalonike 2:13; 2 Timotheo 4:1-5). Amini hivi kwa sababu Yesu alisema mbegu ya Neno huzaa mavuno na watu wataokolewa (Marko 4:26-29). Mungu anaeleza jinsi ujumbe wa neno kuhusu Kristo ulivyo na nguvu: “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu, iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. Maana, mwili wote ni kama majani, na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka; bali Neno la Bwana hudumu milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu” (1 Petro 1:23-25; angalia pia Yakobo 1:18). Ujumbe wa Injili ni habari yenye nguvu kubwa katika dunia. Linaweza kubadilisha moyo wa mwanaume au mwanamke; linaweza kubadili familia, mji, au taifa. Unapohubiri na kushirikisha ujumbe wa Injili wenye nguvu, unaweza kuvuna roho nyingi kwa Mungu. Uinjilisti unafafanua kazi ya Yesu, unaelezea ni nini maana yake kwa watu leo hii. Ujumbe wa Injili ni ujumbe wenye habari nzuri duniani. SIMULIZI ZA MAMBO YA WOKOVU msalabani - na kuchukua hukumu ya Mungu kwa ajili ya dhambi zetu • Aliharibu nguvu ya dhambi • Alifufuka toka wafu kuonesha kuwa Yeye ni Mungu • Anaishi na kutawala milele kama Mfalme wa wafalme Jambo ambalo Yesu alilifanya ni kwa ajili ya wanadamu wote. Kila mtu amefanya dhambi na anahitaji kuokolewa kutoka matokeo ya dhambi zake. Hili linaweza kufanyika wakati mtu anapoamini kuwa Yesu Kristo alikuja na kufa kwa ajili yetu na akafufuka toka kwa wafu. Kila mtu ni lazima atubu dhambi zake na kukubali kafara ambayo Yesu alifanya ili kutuokoa kutoka kifo. Wanapofanya hivi, Mungu anasamehe dhambi zao na kuondoa adhabu ya kifo kwa ajili yao. Kwa njia hii wanaweza kuwa na uhusiano na Mungu, aliye Baba yetu wa mbinguni, sasa na mpaka milele. Watu hawawezi kufanya mema wenyewe kiasi cha kumrudia Mungu au kupata wokovu. Hata nguvu zetu bora ni kama takataka ukilinganisha na utimilifu wa Mungu. Hakuna njia nyingine ya kumjua Mungu isipokuwa kukubali malipo ya Yesu aliyolipia madeni yetu ya dhambi. Tunapomwamini Kristo kama Mwokozi na Bwana wetu, Roho wa Mungu anakuja katika maisha yetu. Roho Mtakatifu anatusaidia ili tupate kumjua Mungu na kufikiri, kuamini na kuishi katika njia ya Mungu. Kwa kuwa Mungu anataka kila mtu aokolewe, Roho Matakatifu anatupa nguvu ili tuwe na ujasiri wa kuwashirikisha wengine Habari Njema za wokovu upatikanao katika Yesu Kristo. Mungu amejifunua Mwenyewe katika nafsi ya Yesu Kristo. Pia amejifunua Mwenyewe katika njia na mpango wa wokovu kwa ajili yetu katika Biblia. Biblia ni maneno ya Mungu ambayo Mungu aliwafunulia watu kuandika kwa kadri walivyoongozwa na Roho. Biblia inatufundisha lile lililo kweli. Tunaweza kuliamini na kulitumaini. Ni lazima tulisome na kujifunza Biblia mara nyingi kwa kadri inavyowezekana. Kila mtu atakufa kifo cha mwili. Lakini tunapoamini Yesu Kristo na wokovu wake, tutakaa katika maisha ya milele mbinguni na Mungu. Wale wote wanaokataa mwaliko wa Mungu wa msamaha watatengwa na Mungu na kuingia Kuzimuni. Mungu ni wa milele - Yeye hana mwanzo wala hana mwisho. Yeye ni Mungu Pekee wa kweli, Mwenye enzi na Ajuaye kila kitu. Anao upendo mkamilifu, ana huruma, ana samehe, mvumilivu, na mpole. Mungu ni wa rehema; tena ni Mungu wa haki. Mungu amejifunua mwenyewe kwetu kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu - ni nafsi tatu za Mungu Mmoja. Mungu aliumba mbingu na nchi. Katika mfano wake aliwaumba Adamu na Hawa (Eva). Aliwaweka ili watawale vilivyoko duniani, na kuwapa Bustani nzuri ya Edeni kuishi. Mungu aliwaambia wazae na kuongezeka. Mungu aliwapenda, aliwatembelea na kuzungumza nao. Shetani alimjia Hawa na Adamu katika mfano wa nyoka, na kuwashawishi kuwa kuna mambo mengi katika maisha kuliko yale ambayo Mungu aliwajalia. Huyu muongo, mwizi, na mharibifu alileta changamoto kwa Mungu na Neno lake, kama alivyofanya wakati alipoleta uasi mbinguni na akafukuzwa na wafuasi wake. Shetani na mapepo yake bado wanafanya kazi ya kuwajaribu watu wamwache Mungu. Adamu na Hawa wakachagua kuasi agizo la Mungu la utunzaji wake na kutokula katika mti ambao matunda yake yangeweza kuwafanya kuona uovu. Kutokutii kwao kulifanya dhambi iingie katika wanadamu. Dhambi ni mawazo, maneno, na matendo yaliyo kinyume na sheria ya Mungu na kusudi lake la upendo kwa binadamu. Dhambi inaleta uharibifu na maumivu kwa binadamu. Dhambi inatutenga na Mungu na mpango wa Mungu wa maisha yetu sasa na hata milele. Haki ya Mungu iliyo kamilifu inatutaka tufahamu matokeo ya dhambi, ambayo ni kifo – kimwili na kiroho. Lakini Mungu, katika upendo wake mkamilifu, ameweka mpango wa kumwokoa mwanadamu kutoka dhambi na mauti na kutufanya tuwe na uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu ambao dhambi iliharibu. Katika muda mwafaka katika historia ya mwanadamu, Mungu alimtuma Mwana Wake wa pekee, Yesu Kristo, kutimiliza mpango wake wa wokovu kwa mwanadamu. Yesu Kristo, alikuwa na ambaye ni Mungu: • Alizaliwa na bikira, aliishi maisha yasiyo na dhambi • Alimfunua Mungu na mpango wake wa kumwokoa mwanadamu • Alitoa maisha yake badala ya mwanadamu - akafa SEHEMU YA NNE KAZI YA MWINJILISTI Wajibu Wa Mwinjilisti 1) Kazi muhimu za mwinjilisti ni: • kueleza habari za Yesu (Yesu ni nani na Amefanya nini?) • kuwaita watu watubu dhambi zao. • kuwataka wamwamini Kristo • kuwaambia watu wampokee Kristo kwani ndiyo njia pekee ya kuwa na uhusiano na Mungu Wainjilisti wa kweli wengi wanajisikia mzigo kwa ajili ya giza la kiroho ambalo limewapofusha wanaume na wanawake wanaowazunguka, na ambao wamepotea na wanakwenda Kuzimu pasipo Kristo. Wainjilisti hawajisikii kutosheka kwa kuhudhuria kanisani. Wanafahamu kuwa Mungu huwatumia ili kuwaokoa watu kutoka giza walilo nalo sasa, na kutoka katika maisha ya kuzimu milele, ambayo yameandaliwa kwa wale waliomkataa Kristo (Wagalatia 1:4; Wakolosai 1:13; 1 Wathesalonike 1:10). Wainjilisti wanajisikia kusukumwa kuwaombea na kuwataka watu waliopotea (wanaweza kuwa wa taifa la mwinjilisti au kutoka maeneo mengine ya dunia). Tena watakuwa na hamu kubwa kuwaendea watu hawa na kuwaambia ukweli ili waokolewe. Watu wengine wanaweza kuwakatisha tamaa wasiende, kuwatia woga au changamoto nyingine. Lakini pamoja na hayo wainjilisti watakwenda, kwa sababu wanajua kuwa Mungu amezungumza nao na wanalazimika kutii. Hizi ni baadhi ya ishara za wale walio na wito wa uinjilisti. Mwinjilisti ni lazima ajifunze kuonesha matokeo ya kuita watu wampokee Yesu na kuwasaidia waweze kuweka maisha yao yote katika kumfuata Kristo. Ni lazima ajifunze jinsi ya kutoa mwaliko wa Mungu kwa watu waliopotea ili wapokee msamaha. Ni lazima waweze kuwaongoza katika maombi ya kukiri dhambi zao na kutaka Kristo awe Bwana wa maisha yao. 2) Mwinjilisti aelimishe wainjilisti wengine. Wainjilisti wengi wameonesha mafanikio makubwa katika huduma zao. Pamoja na hayo, wameshindwa kupeleka elimu, ujuzi na uzoefu wao kwa wengine. Mwinjilisti anaweza kuleta maelfu ya watu, hata makumi ya maelfu kwa Kristo. Lakini wainjilisti watakuwa hawajatimiza utume wao kama hawataweza kuelimisha wainjilisti wapya. Mpango wa Mungu mara zote kwa viongozi (ambao ni pamoja na wainjilisti, wachungaji, waalimu, na wengine) ni muhimu kuelimisha wengine na kuwainua waweze kuendeleza kazi ya Mungu (Waefeso 4:11-12; 2 Timotheo 2:2). Kwa njia hii kazi ya huduma inaongezeka kizazi hata kizazi. Kama wewe ni mwinjilisti, ni yupi unamwinua katika huduma ya uinjilisti? Ni nani atakufuata katika kazi yako? Paulo anamwandikia Timotheo, “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2 Timotheo 2:2). Kila kiongozi anawiwa kufundisha kizazi kinachofuata na kuwarithisha hekima na uzoefu wao. Hawa walioelimishwa, wanaume na wanawake, ni muhimu waelimishe wengine wawe wainjilisti pia. Uzoefu wako una thamani kwa vijana. Mwongozo Mwinjilisti anawaandaa wainjilisti wengine. ufahamu wako, na ujuzi vinasaidia kuepuka makosa na matatizo. Tumia muda wako kuelimisha wainjilisti ambao Mungu amewaleta ili uwaelimishe. Nenda nao katika huduma zako. Wape masomo ya uinjilisti. Wafundishe toka Biblia. Waelimishe jinsi ya kufanya huduma ya uinjilisti. Kwa njia hii Ufalme wa Mungu unakua. Kuna mtu huko Ulaya ambaye ni mchungaji na mwinjilisti mwenye kazi nyingi. Ana kanisa lenye waumini maelfu. Bado anatumia siku moja kila juma kuelimisha watu 12 kwa ajili ya huduma ya Injili. Anatumia masaa kuongea, kushauri, kusikia, na kuomba pamoja nao. Anawapa kazi kumsaidia na hata kutoa huduma, wakati anapowafundisha. Baada ya mwaka au miaka miwili wanakuwa tayari, anawaacha wakafanye huduma zao. Kila mmoja kati ya hawa 12 anaanza kuelimisha 12 wengine. Baada ya miaka 2 tu watakuwa wameelimishwa watu 144 ili kutumikia Mungu kama viongozi wa Kikristo. Baada ya miaka miwili mingine kutakuwa na watu 1728 ambao watakuwa wameelimishwa na kuendelea! Na inaendelea hivyo. Hii ndiyo njia ambayo Yesu aliwaelimisha wanafunzi wake. Ni lazima utumie muda kukaa na wale wanaotaka kuwa wainjilisti. Wachungaji, ni muhimu utafute mwinjilisti mwenye uzoefu ambaye ataweza kuelimisha wengine. Ni vema akawa ni mtumishi mwenzi na rafiki wako. Wainjilisti wanaweza kuwa baraka kwa kanisa lako na kwa Ufalme wa Mungu. 3) Mwinjilisti anafundisha waumini jinsi ya kueneza Injili. Kazi ya tatu ya mwinjilisti ni kuelezea yaliyoko kwa Waefeso 4:11-12: “Naye alitoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti; na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujenge. Elewa kuwa katika mistari hii viongozi wa Mungu, ni pamoja na wainjilisti, wanafundisha watu katika Mwili wa Kristo ili watende kazi ya kumtumikia Mungu katika ulimwengu. Mwinjilisti anaitwa kufundisha na kuandaa watu kwa kazi hii. Uinjilisti ni kazi ya kila Mkristo. Mungu amewaita wainjilisti watoe maisha yao ili kuwashirikisha wengine Injili. Lakini kila muumini ajitahidi kuwaambia wengine habari za Kristo na mambo aliowatendea. Ni jambo linalohitajika kuwa kila Mkristo aelimishwe kushirikisha imani yake kwa wengine. Mwinjilisti anawafundisha wengine jinsi ya kuwaleta watu kwa Yesu na jinsi ya kuwashirikisha wengine imani ili watu wengi waje katika mpango wa wokovu wa Yesu Kristo. Hii ni kazi muhimu kwa mwinjilisti. Mwinjilisti analeta mwamko wa imani na kuwafanya wengine wapate hamu kutangaza habari za Kristo. Kuwafundisha wengine jinsi ya kushirikisha imani ya Kristo inasaidia wengi kukua na kuimarika. Imani katika Kristo ni kuwashirikisha wengine. Ni lazima uchukue muda na wale ambao wanataka kujifunza kuwa wainjilisti. Hayo ndiyo Yesu aliyofanya. SEHEMU YA TANO:MFANO WA MWINJILISTI FILIPO Chukua dakika chache na usome mlango wa 8 wa Kitabu cha Matendo ya Mitume. Utaelewa kuwa Filipo alikuwa mtu wa Mungu na mwenye tabia njema. Ndiye peke yake katika Biblia anaitwa “mhubiri wa Injili”, yaani mwinjilisti (Matendo 21:8). Mtu Aliyewatumikia Wengine Mara ya kwanza tumesoma habari za Filipo katika Matendo sura ya 6. Ni miongoni wa wahudumu saba waliochaguliwa na kanisa la Yerusalemu kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali. Filipo alianza kumtumikia Mungu kwa kuwasaidia maskini na wajane. Alitumika kwa sababu kanisa na viongozi walimtaka afanye kazi hiyo. Filipo hakukataa kufanya huduma hii ya ushemasi kwa sababu, labda, hakujifikiria kuwa mkuu kuliko huduma ya shemasi. Alikuwa tayari kujinyenyekeza na kutumika pamoja na kujifunza. Kama unataka Mungu akubariki anzia pale Mungu alipokuweka. Biblia inaeleza kuwa Filipo alikuwa miongoni mwa wahudumu saba waliokuwa na sifa nzuri kwa ajili ya imani yao, hekima zao, na nguvu za kiroho katika Roho Mtakatifu (Matendo 6:1-6). Sifa hizo nzuri za kiroho zilimstahilisha kuwapa wajane chakula mezani Filipo alifanya kazi yake kwa bidii, akiwatimizia mahitaji yao ya kimwili na ya kiroho pia. Tafuta kufanya kazi kwa uangalifu katika kanisa au katika huduma mahali ambapo Mungu amekuweka. Uwe macho sana kuona mahitaji ya watu wanaokuzunguka. Watumikie wanawake na wanaume ambao Mungu amekuweka juu yao, kama Filipo alivyotumikia mitume, na viongozi wa kanisa la Yerusalemu. Jitahidi kujituma mwenyewe na kuwa mtumishi mwaminifu, na wakati unafanya hivi, Mungu atakuongezea na kukupeleka maeneo mengine katika wajibu mkubwa zaidi (Mathayo 25:21; Luka 16:10). Filipo: Mtu wa Maombi Katika Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaeleza kuwa Filipo alikwenda kaskazini mpaka Samaria. Kwa nini Filipo aende mji mgeni? Biblia inatueleza kuwa alikwenda kwa sababu ya mateso makubwa yaliyoanza Yerusalemu. Filipo angeweza kutumia muda wake kuomba na kumsikiliza Mungu na kumtaka Mungu amueleze mahali atakapokwenda kuhubiri. Filipo pia angeliweza kuombea waliokuwa wagonjwa kwa sababu Biblia inatuambia kuwa wengi waliponywa. Fikira Ya Kimungu Kwa Ajili Ya Waliopotea Filipo alijisikia kutumwa na Mungu kuhubiri Wasamaria. Hawa walikuwa tofauti kuliko Wayahudi ambao Filipo aliwafahamu. Filipo alikwenda kwa watu wageni, ambao waliwachukia Wayahudi, kuwaambia habari za Yesu. Filipo alikuwa na mzigo kwa Wasamaria ambao hawakumjua Yesu. Walimhitaji Kristo pia. Alikwenda kwa sababu Yesu alimtuma. Alikwenda kuwaambia wengine habari za Yesu Kristo. Alikwenda kwa sababu alijua fikira ya Mungu kwa watu waliopotea. Kile ambacho Mungu alikijali, pia Filipo alikijali. Filipo alianza kuwa na moyo uliofanana na ule wa Filipo alienda kwa watu wageni, wale waliochukua watu wake, kuwaambia habari za Yesu. Yesu, pengine kwa njia ya maombi na kumsikiliza Mungu katika maombi. Lakini Filipo hakuomba tu; bali alifanya kwa vitendo. Alikwenda kuhubiri. Ujumbe Aliohubiri Filipo Ulikuwa Mrahisi Wa Kueleweka Injili yenyewe ni wazi, ujumbe wa kueleweka. Mungu alituumba sisi na anatupenda sisi. Tumetengwa na Mungu kwa sababu ya dhambi. Yesu, Mwana wa Mungu, alikuja duniani katika hali ya mtu; alikufa Msalabani ili tusamehewe dhambi zetu na kutuwezesha kumrudia Mungu. Kristo alizikwa na alifufuka kutoka kwa wafu na kaburi. Dhambi na nguvu za Shetani ziliharibiwa. Yesu Kristo anaishi leo na ana nguvu zote. Yesu anakutaka umwamini Yeye na kumpa maisha yako. Hukumu inawangoja wale wote waliomkataa Mwana wa Mungu; baraka zisizo na mwisho zipo kwa wale waliofuata Yesu. Huu ni ujumbe wenye nguvu na ambao unafanya kazi ya kugeuza watu. Unagusa mioyo migumu na unaleta tumaini kwa wale walio gizani. Kuwaambia watu inatakiwa wawe wazuri siyo Injili. Wanaume na wanawake hawawezi kuwa wazuri wao wenyewe; wanahitaji nguvu ya Yesu katika maisha yao ili waweze kushinda uovu na kuishi katika haki. Ni muhimu kuwaambia watu kuwa Yesu anayo nguvu na anaweza kuondoa dhambi zao zote, aibu yao kwa ajili ya dhambi zao. Yesu anaweza kufanya mtu mpya kutoka mfanya dhambi (2 Wakorintho 5:17). Yeye anaweza kuleta tumaini kwa waliokata tamaa na nguvu kwa walio wadhaifu (Isaya 40:29; Warumi 15:13). Anaponya walio wagonjwa na kutupa mahitaji yetu yote tunayohitaji katika maisha yetu kwa ajili ya Mungu. Injili ni ujumbe mzuri, uliojaa matumaini na ahadi! Kama mwinjilisti mwema, Filipo alijua jinsi ya kuhubiri ujumbe mwepesi ulioleta maana kwa wasikilizaji na wengi waliokolewa. Filipo Alipewa Miujiza Miujiza, ishara, na maajabu ni sehemu ya huduma ya mwinjilisti. Biblia inatuambia kwamba miujiza mikubwa ilifanyika wakati Filipo alipohubiri (Matendo 8:6-7,13). Watu waliona miujiza na ishara zilizowafanya wavutiwe kusikia maneno ya Filipo. “Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yake yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya” (Matendo 8:6). Ishara ni matendo ambayo si ya kawaida kutoka kwa Mungu yanayomfunua kuwa wa kweli na mwenye nguvu. Ishara na miujiza imeahidiwa kwa kila amwaminiye Kristo; wainjilisti kwa upekee wa mara nyingi wana ishara na maajabu wakati wakihubiri Injili (soma Marko 16:15-18). Siku za karibuni mwinjilisti alikuwa akihubiri katika kijiji msituni. Aliwaambia watu kuwa Mungu amemtuma kwao na ujumbe. Aliwaambia jinsi Yesu alivyoteswa na kufa na kufufuka siku ya tatu; na kuwa Yesu anatoa msamaha wa dhambi. Hatimaye mwinjilisti akasema, “Ili kuwahakikishia niliyoyasema kwenu ni kweli, tutawaombea watu wote wagonjwa, na nitamwomba Yesu awaponye.” Alianza kuwaombea wagonjwa na wakapona. Mchawi alitubu na alianguka ardhini wakati mapepo yalipoamriwa kutoka katika Jina la Yesu. Watu walipoona mambo haya, walimwamini Yesu. Zaidi ya watu ishirini katika kijiji kile walimpokea Yesu Kristo siku hiyo! Ipo mifano mingi ya ishara na miujiza. Katika Afrika, katika kijiji cha Waislamu, kikundi cha wanawake walipewa ruhusa ya kuwaambia watu habari za Injili. Kulikuwa na ukame mkubwa kwa muda mrefu. Kila mara mwinjilisti alipozungumza na mvua ikaanza kunyesha! Kila mmoja katika kijiji, hata kiongozi wa kijiji, alikubali kuwa Mungu alikuwa anatuma baraka kwa sababu mvua inanyesha. Wainjilisti wanatoa ujumbe wa Injili na miujiza inatokea wakati wakiomba na kuzungumza. Yesu alisema, “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio...” (Marko 16:17). Kama mwinjilisti, unaweza kumuomba Mungu miujiza, na kuomba mpaka miujiza itokee. Ombea wagonjwa katika jina la Yesu wakati unapohubiri na amini kuwa Mungu atawaponya watu. Hivyo miujiza na ishara nyingi zilifanyika Samaria na mji mzima ukataharuki na kufahamu jambo hilo. Biblia inatuambia kuwa mji wote ukajaa furaha (Matendo 8:8). Mahali popote ambapo Injili inakwenda panakuwa na furaha na shauku njema. Injili inapohubiriwa na kuaminiwa, dhambi zinasamehewa na maisha mapya yanapatikana; na hiyo ndiyo miujiza ya Mungu ikitenda kazi! Mara nyingi, kuna mambo ya nyongeza kama magonjwa yanapona, mapepo yanatolewa, na watu wanafunguliwa na kufanywa upya. Injili ina nguvu! Siyo muda mrefu uliopita, mwinjilisti alikuwa anahubiri katika mji mmoja na mvulana mdogo ambaye alikuwa kiziwi na bubu aliponywa wakati wakimwombea. Ujumbe wa matumaini na ahadi ambao Filipo alihubiri ulikuwa wazi na mwepesi. Mungu ametuumba sisi na anatupenda sisi... Kristo alikufa kwa ajili yetu... Huu ni ujumbe mzito ambao hufanya kazi ya kubadili watu. Mama yake akaenda kwa majirani, marafiki, na familia na wote wakaona kuwa aliweza kusikia na alianza kuzungumza. Usiku uliofuata watu waliongezeka na mama alisimama mbele na kuwaambia watu jinsi mtoto wake alivyoponywa. Usiku ule watu wengi waliyatoa maisha yao kwa Yesu, pamoja na mama yake yule mwana. Baada ya ujumbe wa Injili, Bwana Mungu anatoa uponyaji wa aina nyingi. Watu wengi waliamini kwa sababu waliona jinsi motto alivyoponywa, na kundi liliendelea kuongezeka kila mara. Mamia ya watu waliokolewa kwa siku tatu. Ndivyo ilivyotokea wakati Filipo alipokwenda Samaria! Filipo Alikuwa Mwepesi Kutii Yesu anajua mahali ambapo watu wako tayari kusikia Injili. Alimtuma Filipo Samaria. Baadaye Yesu alimtuma Filipo kutoka kazi ya uinjilisti yenye mafanikio makubwa kwenda kuzungumza na mtu mmoja katikati ya jangwa. Matendo 8:26: “Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa. Mwinjilisti ni lazima atumie muda wake kuendelea kujifunza kufahamu kusudi na mapenzi ya Mungu, na kutii Mungu anapomwongoza. Mipango mizuri ingaliweza kumhimiza Filipo akae Samaria, ambapo alikuwa amepata mafanikio mazuri, na watu wengi walikuwa wakimpokea Yesu Kristo. Lakini Mungu alizungumza na Filipo kwenda na kuzungumza na mtu mmoja. Tunaweza kujifunza jambo muhimu sana katika habari hii. Ni lazima kumtii Mungu. Yeye anajua zaidi mipango yake. Mungu alijua kuwa mtu wa Kushi aliyekutana na Filipo angeamini na kuchukua ujumbe wa Injili katika nchi yake katika Afrika. Alikuwa mtu mashuhuri (alikuwa na mamlaka chini ya Kandake Malkia wa Kushi). Mtu huyu mmoja alikuwa muhimu kwa Mungu. Kupelekewa Injili ulikuwa ni mpango kamili. Mtu wa Kushi angeweza kuongea na taifa, na Mungu alimtuma mwinjilisti kuzungumza naye. Mwinjilisti ni lazima awe mnyenyekevu, awe tayari kuzungumza na mtu mmoja sawa na kuzungumza na kundi kubwa. Azungumze na watu waliokataliwa, ambao wanaonekana hawana umuhimu, hata kwa mtu mmoja. Mtu mmoja ambaye hathaminiwi na watu wa dunia anaweza kuwa muhimu sana mbele zake Mungu. Inawezekana Mungu anachagua kiongozi mmoja ambaye anaweza kushawishi watu wengi na Mungu anaweza kukutumia kwake. Utii amri ya Mungu akikutuma kwenda na kuhubiri hata wakati watu wanazungumza mabaya kuhusu wewe, au hata wakati wewe binafsi huelewi ni kwa nini. Mungu amejaa hekima na uwezo na anawabariki wote Wainjilisti ni lazima wawe watiifu katika wito wao ambao Mungu ameuweka maishani mwao hata wakati ambao ni mgumu au wakati mwingine watu hawaelewi. Kutii amri ya Mungu ni muhimu mno kwa mwinjilisti. Utii amri ya Mungu akikutuma kwenda na kuhubiri hata wakati watu wanazungumza mabaya kuhusu wewe, au hata wakati wewe binafsi huelewi ni kwa nini. Mungu amejaa hekima na uwezo na anawabariki wote wanaomtii. Uwe Tayari Kwenda Mwinjilisti ni lazima awe tayari kwenda mahali popote ambapo Mungu anamtuma. Mungu anaweza kumtuma mahali pageni na mahali papya. Mungu anaweza mara nyingi hututuma kwa watu ambao hawatufanani. Wasamaria walikuwa hawako sawa na Filipo. Ingewezekana kuwa ni jambo geni na mahali ambapo asingejisikia kupapenda yeye mwenyewe. Hata mtu wa Kushi hakuwa sawa na Filipo. Lakini Filipo alikuwa tayari kwenda mahali pale Mungu alipomwita. Mwinjilisti ni lazima wawe tayari kujitoa mwenyewe na kwenda mahali pale ambapo Mungu anawatuma. Mwinjilisti mmoja ameeleza jinsi alivyokwenda vijiji vingi kuhubiri Injili. Katika baadhi ya vijiji alipigwa; mahali pengine alifungiwa nje ya nyumba. Lakini hata hivyo alikwenda. Watu wengi walichagua kumwamini Yesu. Angesema nini kwa Yesu kama hakuwa amekwenda katika vijiji na watu wangekuwa hawajasikiliza ujumbe? Watu wengi katika dunia wanaangamia bila kufahamu habari za Mungu kwa sababu hakuna mtu wa kuwapelekea Habari Njema za Yesu. Mwinjilisti huyo alimsifu Bwana kwani Mungu alimkubali afikwe na mateso kwa ajili ya Yesu - na alimsifu Mungu kwani wengi watakuwa mbinguni! Mateso, kukataliwa, maisha magumu, na uovu kama itikio la watu ni sehemu ya wito wa mwinjilisti. Kila mwamini ni lazima akutane na mateso wakati anapotaka kuishi maisha ya kumpendeza Mungu ya kumtii (2 Timotheo 3:12). Lakini Mungu atakusaidia, atakulinda na kukuongoza, na kukupa utoshelevu na tuzo katikati ya mateso na maisha magumu. Filipo alikuwa na mafanikio ya kweli. Kwa sababu Filipo alimtii Mungu na alihubiri Injili kamili, watu wengi waliokolewa. Kila Mkristo ni lazima amtii Mungu. Usiangalie tu mafanikio mbele ya macho ya watu; badala yake kila mara jaribu kumfurahisha Mungu. 􀂄 SEHEMU YA SITA ISHARA MAAJABU YA MWINJILISTI Sababu Za Kumuuliza Mungu Akupe Ishara Na Miujiza 1. Yesu aliwaahidi wote wamwaminio (Marko 16:17-20; 1 Wakorintho 12:8-11; 13:2-8). 2. Yesu alisema wote wamwaminio watapewa kufanya mambo makubwa kuliko alivyofanya (Yohana 14:12-13). 3. Kristo aliondoa kazi zote za giza na mapepo katika Msalaba (Wakolosai 2:15). Aliwapa waaminio mamlaka juu ya nguvu za giza (Marko 16:17; Yohana 14:12-13). Wakati mwinjilisti anapotumia mamlaka ya Kristo kutoa mapepo, nguvu za mapepo zinazomtawala mtu zinavunjika na mtu anafunguliwa. Watu wengi wamefungwa na nguvu za mapepo na wanahitaji kuwekwa huru kwa nguvu za Yesu. Wale wote wanaojikuta katika nguvu za mapepo wanapaswa kujua kuwa kama Mkristo, hawako chini ya nguvu za giza na hawapaswi kuishi kwa hofu. 4. Ishara na miujiza inaonesha nguvu ya kweli na mamlaka ya Yesu Kristo. 5. Ishara na miujiza inasaidia kuifanya Injili iwe na nguvu pale inapohubiriwa. 6. Paulo aliona miujiza mingi wakati wa huduma yake (Warumi 15:18-19; 2 Wakorintho 12:12), kama alivyofanya Filipo. Petro naye aliona miujiza ikifanyika wakati alipokuwa anahubiri habari za Yesu. Wainjilisti wengi na wahudumu wa Neno mahali pote duniani nyakati zote hata siku hizi wanaona Mungu akitenda miujiza wakati wanapoombea watu. Kama mwanafunzi na mhudumu wa Kristo, ni vema ukafahamu na kuamini Mungu kwa ishara na miujiza kama sehemu mojawapo ya huduma. Miujiza Yaweza Kuleta Matatizo Miujiza inawafanya watu wawe na sababu ya kufurahia na kuamini Injili. Yohana 20:30-31 inaeleza, Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa; ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Lakini miujiza inayofanywa kwa jina la Yesu inaweza isilete kila mara itikio lenye mwelekeo mwema. Yesu alipingwa wakati alipokuwa akifanya miujiza (Mathayo 12:9-14). Paulo alikutana na shida nyingi wakati akihubiri Injili na miujiza ikatokea (soma Matendo 19:9-12,23-41). Shetani anapinga Injili na kila kitu ambacho kinamtukuza Yesu aliyefufuka; watu ambao hawajakombolewa hufanya hivyo pia. Omba na kutaka ulinzi wa Mungu. Mungu atakusaidia kila mara unapohubiri na kuwaombea wagonjwa na kukabiliana na mapepo. Kila mara msikilize Roho Mtakatifu na fanya kwa hakika lile ambalo Roho Mtakatifu anakueleza ufanye. Usijaribu kufanya kama watu wengine wafanyavyo au mitindo ya huduma za wengine. Wewe huna huduma zao. Wewe una huduma ambayo Mungu amekupa, na inaweza kuwa na nguvu kwa njia ya Kristo. Fanya kwa imani lile ambalo Bwana anakuonesha. Jinsi Ya Kuanza Kuona Miujiza Moja: Mtii Mungu. Hubiri Injili pale ambapo Mungu amekutuma. Waambie watu kuwa Yesu anaweza kuwaponya na wawekee mikono na kuwaombea katika jina la Yesu; wapake mafuta walio wagonjwa, kulingana na Maandiko Matakatifu (Marko 6:13; Yakobo 5:14). Kumbuka, si wewe au karama yako inayowaponesha watu. Ni nguvu ya Mungu inayoponesha wakati unatii kuongozwa na Roho Mtakatifu. Mbili: Neno la Mungu lina nguvu na li hai (Waebrania 4:12) na linabebwa na mamlaka ya Mungu. Kariri mistari au milango kadha ya Biblia mara nyingi kama sehemu ya tabia yako ya Kikristo. Hatimaye, wakati unapowaombea wengine, nukuu mistari ya Maandiko ambayo Roho Mtakatifu anaileta katika mawazo yako. Kwa mfano, kama unamwombea mtu aliye mgonjwa, unaweza kusema, “Yesu, Neno Lako linatuambia kuwa, maombi ya imani yataokoa walio wagonjwa, na Bwana utawainua wewe. Hivyo, sasa hivi, tunakubali maneno yako na tunakutaka wewe umponye na kumuinua mtu huyu!” Kuna nguvu wakati Neno la Mungu linapozungumzwa. Tatu: Uwe na imani katika Yesu Kristo kwamba Yeye ndiye ambaye Biblia inasema wazi kuwa ni Yeye Mwenye mamlaka Yote, na nguvu Zote! Wakati tunatembea katika utii wa kuongozwa na Roho Mtakatifu na Neno la Mungu, Kristo atafanya kazi kwa njia yetu katika nguvu zake za mamlaka ya kutenda mapenzi yake. (Mathayo 18:18-20; Marko16:17. Nne: Ni vema ukataka sana karama ya maarifa na ya hekima na ya utambuzi. (1 Wakorintho 12:8-11). Je mtu ni mgonjwa kwa sababu amepagawa na mapepo, magonjwa ya kimwili au yote mawili? Je, kuna dhambi katika maisha yake ambayo inasababisha magonjwa? Je, mtu huyo au familia yake imeshajihusisha na mambo ya ushirikina? Tegemea zaidi Roho Mtakatifu kukusaidia katika kutambua sababu za ugonjwa au matatizo, ili uweze kusema ukweli wa shida katika maombi. Usiwe na haraka. Katika hali nyingine, kufunga na maombi ya ziada yatahitajika (Mathayo 17:21). Tano: Katika muda wako wa maombi, umwombe Bwana upate kutiwa moyo ili uwe tayari kuona ishara na miujiza. Omba kwa lugha na jieleze mwenyewe, jenga imani yako (Yuda 20). Sita: Mwambie Roho Mtakatifu akufundishe kuhusu miujiza unaposoma Biblia. Mwambie Mungu akupe watu wengine ambao watakufundisha na kukusaidia kukua katika maeneo hayo. Wakati unapohubiri au kuwashirikisha Habari Njema wengine, uulize kama kuna mtu mgonjwa kati yao. Waulize ruhusa kama unaweza kuwaombea. Waambie kuwa Yesu anaweza kuponya walio wagonjwa. Omba na amini kuwa Mungu atafanya miujiza. Hatimaye washirikishe Injili na kuomba nao ili wampokee Kristo. Wakati unapoombea wagonjwa, uwe makini katika Roho Mtakatifu. Msikilize wakati unapohudumu. Ni jambo muhimu sana kumleta mgonjwa au waliopagawa na pepo ili waokolewe katika Kristo kwa sababu wanayo nguvu ya kupinga mipango yote ya kipepo kwa njia ya Kristo tu (Mathayo 12:43-45; Waefeso 6:10-18; Yakobo 4:7; 1 Petro 5:8-9). Ishara, Maajabu, Na Miujiza Mara Nyingi Vinatendwa Na Wainjilisti Katika masomo yaliyotangulia, tumejifunza kuwa Filipo alihubiri na aliomba kwa jina la Yesu. Maroho machafu yaliondoka; watu waliokuwa wagonjwa walipona. Haya yote ni ishara zenye nguvu zinazoonesha watu kuwa Filipo aliwaambia ukweli. Hivyo watu Omba na mwambie Mungu akupe ulinzi wake. Mungu atakusaidia kila mara unapohubiri na omba kwa ajili ya wagonjwa na pia kemea mapepo. Siku zote sikiliza Roho Mtakatifu na fanya kile ambacho Roho Mtakatifu amekuambia ufanye. walishangaa na kufurahia (Matendo 8:5-13). Soma tena Matendo 8:5-13, mwambie Bwana akufundishe. Kama wewe ni mwinjilisti ambaye anamtii Mungu na anahubiri ujumbe kamili wa Injili, amini kuwa Mungu atakupa miujiza na ishara zitafuata! Kundi la wainjilisti katika bara la Afrika waliomba na walijisikia kuongozwa na Mungu kwenda katika vijiji viwili kuhubiri Injili. Walikwenda pale na kuhubiri Injili; watu wengi wakamkubali Yesu Kristo. Wanakijiji waliwataka wainjilisti waombe mvua, kwani hapakuwepo na mvua kwa miezi mingi. Baada ya kundi hili kuondoka na kwenda kijiji kingine, mvua ilinyesha kwa masaa matatu na nusu! Wanakijiji waliwatuma watu wafuate kundi hilo na kuwaambia habari hizo. Mungu aliwapa ishara kijiji kizima kwamba nguvu za Mungu ni za kweli na kwamba yale ambayo wainjilisti waliyasema ni kweli. Miujiza ilifanyika kila mahali Yesu alipokuwa. Miujiza ilifanyika mahali wanafunzi walipokwenda. (Warumi 15:19; Matendo 6:8). Filipo alikuwa ni mwanafunzi na wewe ni mwanafunzi pia. Dunia imebadilika lakini Mungu habadiliki (Waebrania 13:8). Mwambie Mungu kwa imani akupe karama ya miujiza ili kuthibitisha nguvu za Mungu na ujumbe wa Injili. Sababu Miujiza Isiweze Kufanyika Moja: Kutokuwa na imani au unashindana na kutokuamini. Ni muhimu kuwa na imani katika Yesu na kwamba Yeye ni nani ili nguvu za miujiza ziweze kuonekana (Mathayo 17:14-20; Waebrania 11:6). Mbili: Kama huamini kuwa Mungu anafanya miujiza, au anaweza kukutumia kuwa wewe uombe kwa miujiza. Mungu hakuahidi nguvu zake kwa watu walio na elimu, matajiri, wasomi, au kwa watu wasemaji bora. Yesu aliahidi nguvu zake kwa watu wote, “hao waaminio” (Marko 16:16-17). Tatu: Kama maisha yako si safi. Hukumtii Mungu au unatenda dhambi. Au unakuwa na malengo ambayo si sawa, kutaka kufanya miujiza ya Mungu ili kujitukuza mwenyewe na siyo Yesu Kristo (Matendo 8:14-23). Ni lazima utubu nenda kwa kaka au dada na kukiri madhaifu yako na waombe kwa ajili yako na kukuombea (Yakobo 5:16; 1 Yohana 1:9). Wahudumu wote wa Injili ni lazima waishi maisha maadilifu. (1 Timotheo 3:2; Tito 1:6). Nne: Mtu fulani amekufundisha kuwa miujiza haifanyiki siku hizi. Una habari ambazo si za kweli. Amua kusoma Neno la Mungu na jifunze ukweli kuhusu mambo ambayo Yesu alifanya na alivyosema kuhusu miujiza. Inahitaji imani kuamini Mungu na Neno Lake. Kumbuka, tunamtumikia Mwokozi aliyefufuka na asiyebadilika, “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele” (Waebrania 13:8). Yesu Mwenyewe alisema, “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya” (Marko 16:17-18). Kuhusu Paulo na Barnaba, inasemekana, “Basi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa ushujaa katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao” (Matendo 14:3). Mwambie Mungu akupe hayo matendo ya nguvu kwa ajili ya huduma yako ili Mungu apate kutukuzwa na Ufalme wa Mungu upate kukua. Tano: Ingewezekana umekosa taratibu au una kiburi. Huchukui muda wa kusoma na kujifunza Biblia au kuijenga imani yako kwa Mungu. Ni mara chache unahubiri au kuwaambia wengine habari za Yesu Kristo. Unataka mialiko maalum kwa ajili ya kuhubiri. Katika mambo haya yote unatakiwa utubu! Ni lazima uamue kuwa mwanafunzi mwaminifu, kuomba na kujifunza. Ni muhimu ukawa tayari kukubali kwenda mahali ambapo Mungu anakutuma ukahubiri - na kwa yeyote ambaye hajapata kusikia Habari Njema! Wakati tunapokuwa waaminifu katika madogo au vitu dhaifu, ndipo Mungu anatoa zaidi (Mathayo 25:23). Inachukua muda kwa imani yako kukua katika hali itakayokufanya uamini Mungu kwa miujiza. Soma Biblia yako ili ujifunze vizuri ujumbe wa Injili. Soma sehemu hii ya ujumbe mara nyingi, na masomo mengine yanayoonesha miujiza. Anza kuamini Neno la Mungu na mwambie Mungu, “Ninakuamini.” Mungu anapokupa nafasi kuwashirikisha wengine Injili, omba kwa ajili ya mahitaji ya mtu au watu wale unaowashirikisha. Mwombe Mungu akuongoze na kukuelekeza na kukufundisha. Muda si mrefu utaanza kuona mambo ya miujiza yakifanyika. Uwe mtii katika yale yote Mungu anayokuonesha, na hivyo utakua katika ufahamu na Bwana Yesu atakutumia. Vifungu Vya Biblia Vioneshavyo Ishara, Maajabu, Na Miujiza Chukua muda kusoma, kujifunza, na kuomba kwa ajili ya mistari kutoka Maandiko ambayo yanakuambia kuhusu nguvu za Mungu na miujiza, ishara, na maajabu: Ayubu 5:9 Yeremia 32:21 Mika 7:15 Mathayo 12:28 Marko 16:16-17,20 Luka 5:17; 10:18-20 Yohana 4:54; 6:14; 12:9-11; 14:12 Matendo 3:16; 4:7-10,16,22; 4:29-30; 8:5-13; 10:38; 14:3; 15:12; 19:11-12 Warumi 15:19 1 Wakorintho 4:20; 12:9,10,28 2 Wakorintho 12:12 Waefeso 1:18-19 1 Wathesalonike 1:5 Waebrania 2:2-4 􀂄 SEHEMU YA SABA:KUHUBIRI UJUMBE ULIO WAZI WA INJILI Ni Mungu, kwa njia ya Roho Mtakatifu Wake, huwaita watu waje kwake Mwenyewe (Yohana 6:44). Ni lazima tuombe sana, kumwambia Mungu awalete wote katika wokovu wale ambao hawajamjua Yesu. Lakini tutakuwa tumefanya makosa kama hatutatambua ushauri mzima wa Neno la Mungu na maagizo ya Kristo: Pamoja na kuwa Mungu atawavuta watu, ni lazima sisi tumtii Mungu na kwenda kuhubiri Injili na kuwaambia watu Habari Njema! Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!” (Warumi 10:14-15). Ndiyo, Roho Mtakatifu atawavuta watu kwa wokovu. Lakini kama kifungu hiki kinavyoeleza kwa uwazi kabisa, watu ni lazima wasikie habari za Yesu kabla ya wao kumuamini. Yesu aliwaagiza wanafunzi wake, “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19-20); “Enendeni ulimwenguni mwote, mkahubiri Injili kwa kila kiumbe” (Marko 16:15). Kama jambo hili halikuwa muhimu mno kwa watu kupokea wokovu, hivyo ingekuwa ni zoezi ambalo halina maana. Ni lazima tuende; ni lazima tutangaze! Watu wanaangamia kila siku ambao hawajasikia Injili. Ni kusudi la Mungu kwamba Hata Mmoja asiangamie, lakini Wote waje na kutubu (2 Petro 3:9). Wakristo ni lazima wamtii Kristo, wafuate mfano wake waite watu wapate kutubu na kuamini, wahubiri Injili kwa kila kiumbe kama Kristo alivyotuagiza tufanye! Na wakati tunapohubiri ujumbe wa Injili, ni muhimu ukawa rahisi na kueleweka. Tena ujumbe huo ulete maana kwa wasikilizaji. Ujumbe wa Injili ni lazima ueleweke ili watu wawe na uhakika na uamuzi ambao watafanya. Ujumbe mzuri wa uinjilisti ni wa kipekee kwani ni kuhusu Yesu ni nani – na siyo jinsi ya kuomba, kusaidia wengine, au jinsi ya kufanya mambo mema (yale mafundisho siyo ujumbe wa uinjilisti). Wakati mwinjilisti anapohubiri, anawaambia watu habari za Yesu Kristo na kuwaita watu kwa Yesu Kristo kwa toba. Wahubiri wengi hawajui jinsi ya kuhubiri ujumbe wa uinjilisti. Ujumbe wa kiinjili ni lazima uwe juu ya Yesu na kwa nini watu wanahitaji kumpokea Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Chagua Somo La Biblia Lenye Umuhimu Wake Chagua somo la kuhubiri ambalo litaleta maana kwa watakaolisikia. Hapa ipo mifano michache kutoka Biblia ya kuhubiri ili kuwafanya watu wamfahamu Yesu Kristo na wokovu ambao anatoa kwa ajili yao: • Kondoo aliyepotea (Luka 15:4-7) • Shilingi iliyopotea (Luka 15:8-10) • Mtu ambaye Yesu alimfungua kutoka nguvu za mapepo (Marko 5:1-15) • Mwanamke aliyemwendea Yesu kwa hitaji lake (Luka 8:43-48) • Mwaliko uliokataliwa (Mathayo 22:1-10) • Je, jina lako liko katika Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo? (Ufunuo 20:12-15) • Yesu atakuwa Mchungaji Wako (Yohana 10:2-4,26-29) • Njia mbili za maisha (Mathayo 7:13-14) • Kumwita Yesu wakati wa shida (Warumi 10:13) Kuna vifungu vya Maandiko vingi ambavyo vitakuwa msingi jinsi ya kutoa ujumbe ulio wazi wa Injili. Mwambie Mungu akupe mwelekeo wa Biblia na maisha ya watu ili unapohubiri ueleweke. Kutoa Injili Ya Upendo Baadhi ya wainjilisti wanaanza kutoa ujumbe wao kwa kusema, “Ni lazima uokoke! Utakwenda Jehanam!” Wanarudia maneno haya tena na tena. Hali hii ya kuhubiri inawafanya watu wajione hawafai na kujenga kujihukumu. Baada ya muda, wataacha kusikiliza na wakaondoka. Maneno yako ni lazima yawavute watu. Bibliainatufundisha ni wema wa Mungu unaotuongoza tufikie toba (Warumi 2:4). Je, unaweza kuwaambia watu kwa nini ni lazima waokoke? Je, unaweza kuwaambia upendo mkubwa wa Mungu, na kafara kubwa ya Yesu aliotoa kwa ajili yao? Je, unaweza kuwaambia furaha iliyopo kwa kumjua Yesu? Waambie mambo watakayokosa kwa kumkataa Yesu. Waambie mambo ambayo watapata wakimpokea Yesu Kristo! Hapa kuna mifano michache itakayokusudia kuelewa mahubiri mazuri ya kiuinjilisti: Baadhi Wanahubiri... *Wote ni watenda dhambi na mtakufa Ni lazima uokoke *Ni lazima uwe Mkristo *Usiwe mdhambi, njoo kanisani. *Utakwenda Jehanam *Ni lazima uwe mzuri! *Ni lazima ubadilishe maisha yako *Ninajua mengi kuhusu Mungu *Sikiliza mtu mwenye nguvu za Mungu Mahubiri Mazuri *Wote tumefanya dhambi. Hukumu ya Mungu kwa dhambi ni kifo. Yesu alichukua hukumu hii Mwenyewe. Kama utampokea Kristo na dhabihu yake kwa ajili yako, Yeye atakusamehe dhambi na kukupa uzima. *Dhambi inatutenga na Mungu na upendo wake. Ndiyo sababu unamhitaji Yesu - alikufa na kulipia dhambi zako. *Unaweza kumfahamu Mungu kwa kumpokea Yesu awe Mwokozi wako. *Je, umechoka na dhambi na kutengwa na Mungu? Yesu peke yake anasamehe dhambi na kukusafisha na mambo yote yasiyo haki, na kukuponya madhara yote ya dhambi. *Wote wanaompokea Yesu Kristo watafanywa kuwa wa Mungu na kukaa naye milele. Wale wote wanaomkataa Kristo watatengwa na Mungu milele, pale Jehanam. Mungu anapenda ukae naye lakini ni uamue mwenyewe. *Wote tumefanya dhambi mbele za Mungu. Lakini Yesu alikufa Msalabani ili tupate kusamehewa dhambi. Hatuwezi kuwa wema pasipo msaada wa Kristo. *Wengi wetu tunapenda kubadilika, lakini hatuna nguvu kujibadilisha wenyewe. Yesu anatupa nguvu ya kubadilika, kushinda dhambi, kukataa ubaya na kuwapenda wengine badala ya kuwachukia. *Uwezo wa kumfahamu kiakili tu Mungu au Yesu hauwezi kutuokoa. Ni lazima upokee msamaha wa Kristo na kumkubali awe Bwana na Mwokozi. *Mimi si mzuri zaidi yako. Mimi ni mkosaji. Lakini nimempokea Yesu Kristo. Yeye amenisamehe na amenipa Uzima na Roho Wake, na sasa ninamfahamu Mungu. Niko hapa kukuwezesha nawe upate nafasi hii. Elewa Watu Ambao Unawahubiria Ni watu gani ambao unapenda kuwashirikisha Injili? Je, ni wafanyabiashara? Wanawake? Wafanyakazi? Wanafunzi? Watu muhimu? Waislamu? Wahindu? Wabudaa? Jitahidi ufahamu desturi zao, mawazo yao, na imani yao. Jitahidi kuwaelewa na kwa nini wako kama walivyo. Unaweza kufanya hivi kwa njia mbili. Moja, jifunze kila uwezalo kuhusiana na watu hawa. Wanaishije? Nini kinawaogopesha? Wanaamini nini? Wana wasiwasi na mambo gani? Wana matumaini gani? Ya pili, omba na kutaka Mungu akufunulie mahitaji yao. Mngojee Mungu naye atakuelekeza kwa njia ya maneno, mitazamo, au kwa njia ya picha katika mawazo yako. Tayari Roho Mtakatifu anajua maisha yao na atakusaidia jinsi ya kuzungumza nao. Atakusaidia. Kuhubiri mahitaji muhimu ya binadamu ni njia yenye nguvu katika mahubiri ya kiuinjilisti. Wathamini Watu Ambao Unawahubiria Mara nyingi utawahubiria wanaume, wanawake na watoto pamoja. (Hata watoto wadogo sana wanaweza kuelewa Injili na kumpokea Yesu!) Ni lazima useme kwa kuheshimu na ukweli (1 Petro 3:15). Wainjilisti hawakuitwa kuwahukumu watu (Yohana 3:17). Ni lazima kuwa wanyenyekevu na kukumbuka kuwa kila mtu (pamoja na sisi) tumefanya dhambi na tunamhitaji Yesu - kwani hakuna aliye bora zaidi ya mwingine. Wasaidie watu watambue upendo wa Mungu kwa ajili yao; waite katika tumaini lipatikanalo kwa Yesu Kristo. Kama ukiwaonesha watu upendo wa kweli na heshima, kwa vyovyote watapenda kusikiliza ujumbe ulio nao. Kuzungumza Kwa Kujiamini Wewe kama mtu binafsi huna lolote unaloweza kusema ili kubadilisha maisha. Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa ni Yesu anayekutuma. Wewe ni mtumishi wa kusema ujumbe wa Mtu Mwingine ambaye ni Mkubwa kuliko wewe mwenyewe. Wewe ni mtumishi kufanya mapenzi ya Bwana wako. Ameahidi kukusaidia. Jinsi utakavyohubiri zaidi, ndivyo utakavyojijenga katika kujiamini. Kila mwinjilisti anafanya makosa, lakini unaweza kujifunza kutokana na makosa ili kufikia mhubiri bora. Wakati ambapo hujafanya vizuri, omba na mwambie Yesu akufundishe jinsi ya kufanya vizuri. Kwa njia ya mazoezi mengi utakuwa mhubiri wa Injili vizuri. Ujazwe Na Roho Yesu alikuwa mfano wa aliyejazwa Roho, Roho alimtia nguvu (Matendo 10:38). Yesu alihubiri kwa mamlaka, akitoa pepo, akiponesha walio wagonjwa, na kuwafungua waliofungwa na kuwaacha huru (Mathayo 4:23; Luka 4:14-19). Yesu alikuwa mkamilifu, Mwana wa Mungu asiye na dhambi. Hata hivyo kuna wakati kabla ya kuanza huduma yake ambapo Roho Mtakatifu alikuja na kumjaza (Luka 4:1; Yohana 1:32-33). Yesu aliweka wazi kuwa wanafunzi wake – wale ambao walikuwa tayari wanamwamini – walihitaji pia Roho Mtakatifu kuwajaza ili waweze kuwa mashahidi wenye nguvu (Luka 24:45-49; Matendo 1:5,8). Ubatizo wa Roho Mtakatifu umetolewa na Yesu (Mathayo 3:11). Ubatizo huu wa Roho Mtakatifu unatenda mambo makuu katika mahubiri ya Petro na wanafunzi wengine. (Matendo 2:14-47; 3:11-26; 4:23-31), na utakusaidia wewe pia kuhubiri Injili kwa ujasiri zaidi. Wakati mtu anampokea Kristo, anazaliwa upya kwa kazi ya Roho Mtakatifu. (Yohana 3:5-6). Roho Mtakatifu anakuja na kuishi ndani yake (Warumi 8:9-11). Hata hivyo, Kristo anajua kuwa tunahitaji nguvu Yake ili tuweze kukamilisha mapenzi Yake katika dunia hii. Hivyo, Yesu ametuahidi kujazwa na Roho Mtakatifu na kufurika (Yohana 7:38-39) ili tuweze kupakwa mafuta katika huduma (Luka 24:49; Matendo 1:8). Ubatizo wa Roho Mtakatifu ulitokea kwa waumini wale waliokwisha kumwamini Kristo kama Mwokozi wao (Matendo 2:1-4). Haya yalitokea baadaye kwa wengine pia, ambao walimpokea Kristo na kubatizwa kwa maji, lakini walikuwa bado Roho Mtakatifu hajawajilia juu yao. “Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana; ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; kwa maana bado hajawashukia mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu” (Matendo 8:14-17). Je, Roho Mtakatifu amekushukia kwa nguvu? Je, unataka kuwa na ujasiri zaidi wakati unapohubiri na kuzungumza juu ya Yesu? Kama Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi wako, hivyo karama ya Roho Mtakatifu iko kwako (Matendo 2:37-41). Nguvu ikuwezeshayo kuwa na ushuhuda ufaao wa Yesu inakuja wakati unapokea ubatizo wa Roho. Kupokea Roho Mtakatifu Unapokeaje Roho Mtakatifu? Kwanza, hakikisha kuwa maisha yako ni safi mbele za Mungu. Kiri dhambi yoyote inayofahamika na kutubu mbele za Mungu. Mwombe Mungu akuchunguze, na kwa njia ya maombi yakiri mambo yote aliyokuonesha. Baadaye mwambie Yesu akujie kwa njia ya Roho Mtakatifu na kwa nguvu. Anza kumsifu Yesu Kristo. Biblia inatufundisha kuwa unaweza kuanza kwa kusema kwa lugha nyingine ambayo hujapata kujifunza, kama ilivyotokea kwa wanafunzi (Matendo 2:1-4; 10:44-46). Usikatishwe tamaa kama itatokea kuwa huanzi kusema mara moja. Chukua muda umwabudu Bwana Yesu na mwambie akupe Roho Wake Mtakatifu. Kama unamjua mtu ambaye ameshajazwa na Roho Mtakatifu, mwambie mtu huyu aweke mikono juu yako na kukuombea (Matendo 8:14-17). Mungu anajibu maombi! Ni Yesu alituambia kuwa tunahitaji kupewa - hivyo omba nawe utapokea kama Yeye Mwenyewe alivyoagiza. Uendelee Kujazwa Na Roho Mtakatifu Tunahitaji kujazwa Roho Mtakatifu kila mara na kwa upya. Biblia inaelekeza waumini kuwa, *bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote (Waefeso 5:18-20). Ni wazi kwamba maelekezo haya siyo jambo la wakati mmoja, lakini ni jambo la wakati wote. Ni lazima liwe linatokea mara kwa mara. Neno la asili la Kiyunani (Kigriki) la “kujazwa” limetafsiriwa “kuendelea kujazwa” - jambo linaloendelea na kufanywa upya kwa njia ya Roho Mtakatifu na Mungu. Tunahitaji Roho Mtakatifu akae ndani yetu kama Wakristo - ili atupe faraja, atuongoze, na kutufundisha. Tunahitaji pia Roho Mtakatifu atujie na kutupa nguvu katika huduma yetu. Na tunataka Roho Mtakatifu kuendelea kutujaza - ili kutupa upya na kutusaidia kuiwezesha mioyo yetu na midomo kujazwa na sifa, nyimbo, na shukrani! Kuamini Mungu – Tumia Karama Zako Mwinjilisti mzuri anategemea nguvu za Mungu na hekima zitende kazi ndani yake. Matokeo mazuri ya uinjilisti hayatokani na uwezo au kipawa chetu cha kiasili. Mungu anatumia mambo yetu ya kawaida, lakini Mungu anataka umwamini Yeye - kwani ni Roho Mtakatifu peke yake awezaye kuleta ushawishi kwa watu (Yohana 16:8). Wajibu wa mwinjilisti ni kuwa mwaminifu kuwashirikisha Injili, hivyo atalazimika kumwamini Bwana kwa matokeo yake. Mungu anatoa karama na vipawa kwa watu na wahubiri wenye hekima wanaovitumia kwa utukufu wa Mungu (1 Wakorintho 10:31). Mungu anatutazama tutumie vipawa kwa uwezo tulio nao (Mathayo 25:14-28). Mungu amefanya kila mtu na upekee wake. Analo kusudi la kutuumba sisi kwa jinsi tulivyo na hakuna anayeweza kufanya kama tufanyavyo. Siyo jambo la hekima kuiga wahubiri wengine; wanao wajibu wao wenyewe wa kutimiza. Hata hivyo, unaweza kupata mawazo kutoka kwa wahubiri wengine na kuyatumia katika ujumbe wako, utumie njia zako, unapowashirikisha ukweli wa Yesu. Hubiri Kwa Ajili Ya Toba Ni muhimu kwa mwinjilisti kuwaambia wanaume na wanawake kwamba ni lazima wabadilishe mwelekeo wa maisha yao. Wanatembea katika njia ya uharibifu; ni lazima wageuke na kumfuata Yesu (Mathayo 7:13-14). Waite watu wabadilishe mwelekeo (watubu), kutoka kufuata njia zao wenyewe na kufuata njia za Mungu. Hubiri na kuweka ujumbe wazi kwa watu kwamba ni lazima waamue ni nani wanataka wamfuate. Kuna uchaguzi wa aina mbili tu: kumpokea Yesu Kristo na kutembea katika njia zake; au kuchagua ubinafsi wao ambao utawafikisha katika uharibifu wa milele. Hubiri Ili Kugusa Mioyo Yao Maisha ni magumu, makatili kwa watu wengi. Ujumbe wa Injili una tumaini la kweli na la amani na Mungu, ana msamaha wa dhambi. Watu wanahitaji kufahamu kuwa Mungu atatembea nao katika maisha yote kama tu watamgeukia Yeye kwa wokovu. Hubiri na kutoa upendo wa Mungu, wokovu wa Kristo, na faraja ya Roho Mtakatifu. Hubiri ukiwaambia watu jinsi ya kumfuata Kristo. Watu wanahitaji kujua pia kuwa kuna hukumu na adhabu kwa ajili ya dhambi. Elezea kifo cha Yesu cha Msalaba, misumari iliyopigiliwa katika miguu na mikono yake, damu ilivyochuruzika katika mwili wake, Waambie jinsi Yesu alivyotundikwa juu ya Msalaba kwa masaa akiwa katika maumivu makali, jinsi alivyoteseka kwa ajili ya kafara ya dhambi zetu, akachukua adhabu yetu juu yake mwenyewe. Elezea matukio yote; chora picha kwa maneno yako mwenyewe. Waangalize kuwa hii siyo hadithi - ni Ukweli! Waambie Yesu alifufuka toka kwa wafu kwa nguvu ya Mungu na Yeye ni hai sasa. Watie moyo wafikie uamuzi wa kumchagua Kristo! Hubiri Kuendana Na Wasikilizaji Wako Njia nyingine ya kuhubiri ni kuwakilisha hoja yenye kufikirisha na kuitikisha hadi mwisho. Mtume Shiriki ukweli wa Yesu! Paulo alifundisha hivi wakati mwingine (Matendo sura ya 17). Unataka kuwashawishi watu waone mpango sahihi wa Kristo (2 Timotheo 4:2) na ukweli wa uamuzi wa kumfuata Kristo. Unafikiri na wao na kuwaleta kwa uamuzi ulio sahihi. Unaweza kuwaambia habari za faida za rohoni (lakini watu wasije wakaambiwa kumfuata Kristo kwa baraka zake tu). Kuna sababu nzuri ya kuogopa hukumu ya mwisho; ni uamuzi mzuri kumfuata Kristo. Mtu anaweza kumfuata Kristo ili aondolewe aibu na hatia yake kwa sababu ya dhambi zake huko nyuma na pia kuondoa dhamiri kujishtaki. Kumwamini Yesu kwa kutubu kunaondoa dhambi, na hii ndiyo sababu nzuri ya kumfuata Kristo. Kwa mfano nikijua mtu ambaye anaingia katika safari ya hatari na pengine kufa, ningependa kufikiri naye kuhusu uamuzi wake. Nitampa sababu kwa nini asiende: mvua itanyesha sana na kuosha barabara nzima; kuna wanyama wakali; kuna wezi na silaha kila mahali - kuna hatari. Nitamwambia yote ambayo yatampoteza katika safari yake; jinsi ambavyo familia yake itakavyoteseka, na mengineyo. Na huu ni ujumbe muhimu. Ni sawa na wakati ambao unahubiri habari za kumkubali Kristo. Safari ya maisha ni hatari na ina uangalifu mdogo sana. Maovu na mabaya hutokea pale ambapo mwanadamu anachagua njia ya dhambi. Mwanadamu anaweza kupoteza kitu muhimu sana katika maisha yake na tena anaweza kupoteza nafsi yake. Je? Unaona jinsi ambavyo sababu hii inasaidia mwanadamu kuweza kuona wazi maisha yake yalivyo kama jinsi ambavyo hakumfuata Mungu na njia Zake. Kwa mahubiri aina hii utakuwa umeweka wazi mawazo ya uongo yanayofanya watu wafikiri kuwa wanaweza kuishi bila Kristo. Unatakiwa ueleze usalama wa kitambo tu wa maisha yao, pengine ipo katika fedha, familia, mafanikio, au tambiko fulani katika dini. Sisitiza kuwa kila mtu ana uwezo wa kuchagua juu ya maisha yake, na pia kuwa matokeo ya milele katika chaguo afanyalo. Kama wanakataa kuchukua uamuzi ni kuwa wamekwisha kumkataa Kristo kwa kutokupokea wokovu anaoutoa. Tumia Picha Na Hadithi Katika Mahubiri Unapohubiri unaweza ukatumia picha za maneno za maisha ya kila siku zenye kuhusiana na watu unaozungumza nao. Yesu alifanya hivyo alipokua anazungumza katika mifano na mafundisho yake. Neno “mfano” maana yake ni “kulinganisha”, kuchukua kitu kimoja mbele ya kingine na kuonesha jinsi vilivyofanana. Yesu alizungumzia mashamba, wanyama, fedha, kula chakula, kazi za shambani, watoto wakicheza (Mathayo 11:16-19; 13:1-32; 20:1-16; 22:1-14; 25:14-30; Luka 15:4-7). Wakati Yesu anasema, “Mimi ndimi mlango” (Yohana 10:9), kila mmoja alimuelewa ana maana gani. Waliweza kuona mlango katika mawazo yao. Yesu alitumia vitu vinavyoeleweka kama picha kuonesha kuwa alikuwa Yeye ni njia pekee kumfikia Mungu. Kuna mifano mingi, habari, na picha katika Biblia zinaweza kuchora ujumbe kwa wasikilizaji wako, zenye kuonesha upendo wa Mungu, hali ya watu kupotea, na ukweli wa wokovu: • Shilingi iliyopotea (Luka 15:8-10) • Msamaria Mwema (Luka 10:30-37) • Nyumba mbili (Mathayo7:24-27) • Njia nyembamba na njia pana (Mathayo 7:13-14) • Mwanamke aliyefumaniwa (Yohana 8:3-11) • Mwizi aliyetubu akiwa msalabani (Luka 23:39-43) Mifano hii na mingine mingi itakusaidia kuhubiri kwa picha na hadithi. Itawasaidia wasikilizaji wako waelewe upendo wa Mungu na matumaini yake ya kuwaokoa watu. Hubiri Kwa Huruma NA Juhudi Vipo vitu vitatu ambavyo Mwinjilisti anahitaji. Kwanza, ni jambo la muhimu kutambua upendo mkubwa wa Mungu kwa watu wake. Mungu anawapenda watu unaowahubiria! Amewafanya Yeye Mwenyewe kwa ajili Yake, na kuchagua kuwapenda wote. Hapendi watu hawa waishi katika dhambi, kuishi katika maisha ya giza na maumivu, kuitumikia miungu ya uongo, na kutengwa na Yeye katika maisha haya hata milele. Siyo mapenzi Yake hata mmoja aangamie (2 Petro3:9). Upendo wa Mungu kwa wasikilizaji wako uujaze moyo wako. Mungu aliangalia umati kwa huruma kwa sababu aliona jinsi walivyopotea na hali waliyo nayo (Mathayo 9:36-38). Hii ndiyo huruma ya Mungu. Huruma ni pale mhubiri anapoguswa kwenda katika kina kumsaidia aliyepotea. Ni zaidi ya kusikia huruma. Ni hali ya kuona kuwa rehema za Mungu zinapatikana kwa ajili yetu ambao hatukustahili. Unatakiwa uwe na upendo wa namna hiyo kwa watu waliopotea na wanaoangamia. Pili, unahitaji mawazo ya Kristo (1 Wakorintho 2:11-16). Yesu anajua nini kuhusu watu hawa? Yeye anajua wanachohitaji, jinsi ya kuwasaidia ili waweze kumjua Yeye. Yesu alizungumza kuhusu mambo ya ndani kabisa moyoni mwa mwanamke kisimani. Alijieleza hali yake na akamwambia yale anayohitaji kuyasikia ili kumleta katika wokovu (Yohana 4:7-42). Yesu atakusaidia ujue unayohitaji kuyasema. Anajua mahitaji ya watu na wanachotaka, madhaifu yao na hofu zao. Muulize Mungu akupe hekima kwa sababu anatoa kwa wote wanaotaka (Yakobo 1:5). Tatu, kila mwinjilisti anahitaji nguvu na juhudi za Roho Mtakatifu (angalia “Kujazwa na Roho Mtakatifu” hapo juu). Wanahitaji nguvu na juhudi ya Mungu rohoni ili kuhubiri Habari Njema. Juhudi ni kujisikia kwa uzito, kuwa na mzigo, upendo usio na mpaka, na matakwa makali. Kuwa na juhudi kwa ajili ya mambo ya Mungu kunamfanya muumini amfuate Mungu na awe tayari kutenda makusudi ya Mungu. Hali hii ni kama moto wakati mwinjilisti anatumia muda wake kuomba na kuwa katika uwepo wa Mungu, na anapojifunza Neno la Mungu. Unapokuwa na juhudi kwa Injili, unakuwa na ujasiri wa kueneza ukweli kuhusu Yesu na mambo yaliyopo yanaouzunguka ulimwengu. Unashawishika kuwa lile ulisemalo ni kweli na muhimu. Roho Mtakatifu atakupa nguvu na uhai katika kuhubiri kwako, na kukujaza na mzigo wa huduma kwa ajili ya waliopotea. Tafuta huruma za Mungu kwa ajili ya watu na hii itakusaidia kuwa mnyenyekevu na kuwa tayari mbele za Bwana. Wakati mwingine mwinjilisti lazima aongee kwa ushujaa na bila woga kuwatangazia watu kwamba wamepotea katika dhambi. Lakini kila wakati kumbuka kwamba huruma na upendo wa Mungu umekugusa na kukuokoa wakati ulipokuwa mdhambi. Neema ni upendeleo wa Mungu ambao haupatikani au hatustahili. Tunapewa bure. Toa neema na huruma hiyo kwa wasikilizaji wengine wa Habari Njema. Uwe shujaa, bila woga katika Mungu, na mwombe Mungu akujaze huruma kwa ajili ya wanaokusikiliza. Toa Mwaliko Mwinjilisti huhubiri Injili, akiwaita watu watubu na kumfuata Yesu. Kila wakati maliza mahubiri kwa kuwatia moyo wanaokusikiliza ili wafanye uamuzi juu ya wanachosikia. Huu ni mwaliko wa wasikilizaji kuitikia katika ujumbe wa Injili. Mwitikio unaweza usiwezekane; lakini kama unaweza, uwaombe wasikilizaji kuamua kama watakaomkubali Kristo. Wakati unahubiri umati wa watu au katika chumba kilichojaa watu, mwinjilisti aweza akasema: • Ni wangapi wameelewa ujumbe wa Mungu? • Ni wangapi kati yenu wanataka kuomba Yesu msamaha wa dhambi zao? • Wapo watakaotoa maisha yao kwa Yesu na kuishi naye? • Nani atatubu dhambi na kumkubali Yesu Kristo? • Nani anataka kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wake? • Ni nani atachagua kumfuata Yesu? Waweza kuwaambia kuonesha matumaini yao kwa kunyoosha mikono, kusimama, kuja mbele, au kutoa maamuzi yao kwa waliokaa karibu. Waambie wachukue hatua ya kuonesha wanajitoa kwa Yesu. Neno huwashauri wanaoamini kutokuwa na aibu kukiri wazi na kumfuata Yesu Kristo (Mathayo 10:32-33; Warumi 10:9-13). Waume na wake lazima wajue kwamba wanafanya maamuzi; lazima wapaswa kujua wafanye nini. Uwe wazi kabisa, hivyo hawatachanganyikiwa na kufikiri kwamba labda wanajiunga tu na kanisa au wanatoa sadaka aina fulani za kidini. Elezea wazi nini maana ya kumpokea Kristo kama Mwokozi wao. Wakati Wote Omba Na Wale Wanaoitika Wakati watu wanaonesha kutamani kumpokea Yesu, kumkubali Yesu kama Mwokozi na Bwana, waombe wasali pamoja nawe. Ni vizuri wasali kwa sauti, wakirudia sala yako. Hii yaweza kuwa ngumu kwa wengine, lakini watie moyo kushiriki. Ni rahisi kwako kusali kwanza na kuwaambia warudie maneno yako. Tumia sentensi rahisi na ufanye sala zako kwa kifupi. Huu ni mfano wa sala unayoweza kusali na wale wanaoitikia ujumbe wa Injili: “Mpendwa Bwana Yesu, naamini wewe ni Mwana wa Mungu. Naamini ulikufa Msalabani kwa ajili yangu, ili uondoe dhambi zangu. Naamini ulifufuka katika wafu. Mimi ni mdhambi. Natubu dhambi zangu zote. Natubu kwa kuishi maisha yangu kwa mapenzi yangu mwenyewe. Naomba unisamehe na uondoe dhambi zangu zote. Nioshe na unitakase. Niokoe, Yesu Kristo, na unipe maisha mapya. Ingia moyoni mwangu, na unifanye niwe Wako. Asante kwa kuniokoa. Nakuchagua uwe Bwana wangu, nikufuate Wewe siku zote za maisha yangu. Nashukuru kwa uwezo wa kumjua Mungu. Asante kwa kunipa Roho Mtakatifu Yako. Niwezeshe niishi kila siku kukupendeza Wewe. Amina.” Baada Ya Watu Kumkubali Kristo Tumia muda kuwasaidia watu kuelewa walichofanya kwa kumkubali Kristo. Waambie, “Sasa mmekuwa wa Yesu. Mmekuwa sehemu ya familia ya Mungu. Yesu atawawezesha kuishi maisha hayo. Yesu yupo karibu nawe kila wakati. Unaweza kuongea naye kwa sala na maombi, kama tulivyofanya hapa. Hakikisha kwamba unapata Biblia na kuisoma kila siku. Hii itakusaidia kujifunza juu ya Mungu na jinsi ya kuishi naye.” Katika mikutano mengine au makanisa, baada ya watu kumpokea Yesu kama Mwokozi na Bwana wao, ni vizuri kuchukua muda kidogo na kuwaombea. Watubu kwa maneno yao wenyewe. Wakatae uhusiano na mambo maovu, vitendo, au watu - kama uchawi, kuabudu mashetani, au kujihusisha na dini za uongo. Kukataa maana yake ni kuacha kutii au kuacha kufuata jambo. Wakati watu wamekataa maovu katika maisha yao, unaweza kuwaombea na kuamrisha nguvu za giza kutoka, katika Jina la Yesu. Ombea ulinzi wa Mungu katika maisha yao. Mifano ya sala hizo: Muumini Mpya: “Yesu Mpendwa, nakataa dhambi ya (uchawi au dhambi zingine). Nakataa kushiriki katika nguvu za giza na nachagua kukutumikia Wewe kama Mwokozi na Bwana wangu. Tafadhali nifanye huru katika maovu sasa nikikuita. Asante Yesu.” Mwinjilisti: “Baba Mungu, natumia mamlaka yako kupitia Yesu kuamrisha kila nguvu ya kuzimu na roho wachafu kumwacha mtu huyu na nyumbani kwake, familia yake na maisha yake yote. Nasema kwamba damu ya Yesu Kristo imemfanya huru. Nakuomba uwalinde katika njia zote. Asante, Baba, katika Jina kuu la Yesu. Amina.” Baada ya watu kumpokea Yesu ni vizuri kuwaombea kujazwa na Roho Mtakatifu (angalia “Kujazwa na Roho” hapo juu). Kama tulivyojifunza, Roho Mtakatifu huja na kukaa kwa kila mmoja anayekiri Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wake. Lakini Yesu ametoa kwa kila anayeamini kipawa cha Roho Mtakatifu kuwashukia na kuwa mashahidi wake. Waombee wapokee hiki kipawa. Wanaweza wakasali katika lugha wasizozijua. Waelekeze waelewe ni vizuri kusema katika lugha mpya. Ubatizo Wa Maji Biblia inamwamuru kila muumini katika Kristo abatizwe katika maji (Mathayo 28:19; Matendo 2:38). Mtie moyo kila anayekubali kumpokea Kristo abatizwe katika maji. Hii inaweza kufanyika kanisani au mahali popote penye maji (mtoni, baharini, bwawani n.k.). Unaweza ukawabatiza au ukamtumia mchungaji au kiongozi wa kanisa unayemwamini kuwa anaweza kuwabatiza waumini wapya katika maji. Kanisa Kama Familia Mwisho, utawaongoza watu hawa katika kanisa ambalo litawafundisha na kuwatunza. Kama hakuna uwezekano unatakiwa uwafundishe hadi mchungaji au mwalimu aje. Paulo alifanya hivi katika Matendo 14:20-23. Watakuwa pia wanahitaji Biblia kusoma na kujifunza kwayo. Jitahidi uwape waumini wapya Biblia yao wenyewe, angalau Agano Jipya. Mtumaini Mungu Katika Matokeo Amini kuwa Mungu atawaleta watenda dhambi kwa Yesu. Bwana alisema kwa Paulo, “...Usiogope, bali nena, wala usinyamaze …kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu” (Matendo 18:9-10). Amini nguvu 􀂄 Chukua muda kumgojea Bwana! za Roho Mtakatifu aliyeko ndani. Uamini ukweli na uhakika wa Neno la Mungu na Injili ya Yesu Kristo. Ni neno lililo hai na lenye nguvu! Kumbuka kuwa ni Mungu pekee ndiye anayeokoa; wewe ni mhudumu unayebeba ujumbe wake katika maagizo ya Yesu Kristo. Mungu anatamani watu wote waokoke na pia wamwamini Yesu zaidi ya jinsi wewe unavyotamani (2 Petro 3:9). Kunapokuwa na matokeo kidogo unaweza kufanya mambo mawili. Kwanza kabisa, nenda kwa Mungu kwa maombi na zungumza naye kwa hali uliyonayo. Chukua muda wa kusubiri Mungu. Mwache akushtue kama kuna jambo ambalo anatamani wewe ulielewe. Pili, mwambie Mungu akufundishe, jinsi anavyopenda wewe uhubiri Injili yake. Mungu atakaponena nawe, uitikie! Mungu atakufundisha, na pia atakupa waalimu. Unapofanya mapenzi ya Mungu kwa uweza wako wote, mtumaini kwa mafanikio. Wakati mbegu zinapoingia ardhini zinazaa matunda. Unaweza au usiweze kuyaona mafanikio yake. Jambo muhimu ni kumwamini Mungu na Neno Lake. Haimaanishi matokeo uyaonayo, msifu Mungu na kumpa shukrani. Mungu anastahili sifa zetu zote na heshima yako, muda wote, kila mara. Watu wataitikia ujumbe wako, mpe Mungu sifa. Ni Mungu anawakarimu wainjilisti; ni Neno la Mungu linaloleta uzima; ni Roho wa Mungu ndiye analeta watu kutubu. Mwinjilisti ni kama mhudumu mtiifu kwa kazi hii kubwa ya Mungu! Ni heshima gani ambayo Mungu ametuitia kuihubiri Injili na kushiriki kuleta ukweli wa Yesu Kristo kwa wengine. Wale wanaojitwika utukufu (kujisifu) wao wenyewe ni wanyonge na pia ni wajinga ambao wamekumbatia dhambi ya majivuno. Ni Mungu pekee ambaye anamwokoa mwanadamu. Hivyo mpe Mungu sifa ZOTE (Zaburi 115:1)! SEHEMU YA NANE MUNGU ANAVYOMUANDAA MWINJILISTI Mungu Anataka Ujitoe Moja Kwa Moja Wakati Yesu anapokuwa Bwana wa maisha yako, anakuwa Bwana wa kila kitu. Mipango yako, vipawa vyako na ujuzi, mawazo yako, kujisikia kwako, familia yako, mwili wako, maisha yako - vyote hivi ni vya Yesu Kristo na si vyako. Kama hujampa Yeye mambo yote na kila kitu, kutoka katika moyo wako, afanye kama atakavyo, fanya hivyo leo. Mwambie Mungu kwa njia ya maombi. Hivyo kila siku omba Roho Mtakatifu akuchunguze na aletaye kukusadikisha. Mwache Mungu akuoneshe mambo unayoyahitaji kupata au kuacha ili uweze kujiachia kwa Mungu kikamilifu. Ukiri na kutubu pale unapotambua kuwa umefanya dhambi au makosa, ubinafsi au tamaa za mwili. Uwe na nidhamu na mwili wako ili uweze kuwa mwanafunzi wa Yesu mwenye nguvu. Biblia inatuambia, “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari...” (1 Petro 5:6). Mambo yafuatayo yatakusaidia kujipima katika maisha yako. Hizi si sheria au mambo ya nje ya kujihakiki. Hii ni njia ya uaminifu ya kujitathimini maisha na huduma yako kutoka katika moyo. Maswali haya yana lengo la kukusaidia ukue katika maisha yako na kuwa chombo kizuri katika mikono ya Mungu. Uwe mwaminifu mwenyewe; na zaidi sana, uwe mwaminifu kwa Mungu. Hatuwezi kumdanganya Mungu. Anajua yaliyomo moyoni na anaona kila kitu katika maisha yetu. Ni vema kila wakati kumkaribia Mungu kwa unyenyekevu, kumtaka akusaidie kwa neema ili tuweze kukua na kuwa imara na kuwa mtumishi mwaminifu Kwake. Kama baadhi ya mambo hayo si ya kweli kwako, lakini unataka yawe yako, mtake Mungu akusaidie. Na chukua hatua ya kuyatenda! Inasemekana kuwa inatupasa tutoe muda kwa mambo yenye umuhimu. Kama mambo haya ni muhimu kwako, ni lazima uanze kutoa muda kwa ajili hiyo. Mambo Yamfanyayo Mwinjilisti Kukua • Je, mnatumia muda muafaka kwa maombi na kujifunza somo la Biblia kila siku? • Je, ninachukua muda wa kumsikiliza Mungu, kungoja ili azungumze na kuyafunua mawazo yake na mpango kwa ajili yangu? • Je, ninamwomba Roho Mtakatifu achunguze maisha yangu? Je, ninakiri dhambi zangu kila mara? • Je, ninajifunza Biblia na kupanga vizuri hubiri ambalo nitalifanya? • Je, ninajaribu kusahihisha mazungumzo, muonekano, elimu ya Biblia, na ujuzi wangu? • Je, nitakapokwenda kuhubiri, nina waumini wengine pamoja nami? • Je, nimemwomba Mungu aongeze huduma aliyonipa kwa upako na nguvu? • Je, nimejazwa na uwezo wa Roho Mtakatifu kama ilivyo katika Matendo ya Mitume sura ya 2? • Je, ninao watu wanaoniombea kila siku katika huduma yangu na kwa ajili yangu, kipekee wakati ninapokwenda kuhubiri au kuwashirikisha wengine Injili? • Je, ninaomba kwa ujasiri ili kuwa mhubiri mzuri wa Kristo? • Je, mmefunga na kuomba kwa mwezi huu? • Je, ninajua Biblia isemavyo kuhusu kuomba na kumwamini Mungu kifedha, ili Mungu aweze kutoa mahitaji kwa familia yangu NA huduma yangu? • Je, ninaye mshauri kunisaidia? Je, nimemwambia Mungu anipe mtu wa kunifundisha? • Je, kuna mwanaume au mwanamke ambaye naweza kumwomba anisaidie kwa muda wake na kunisaidia katika huduma yangu? • Je, nimeomba na kumwambia Mungu anioneshe mwanaume au mwanamke ambaye naweza kumuandaa na kumsaidia katika uinjilisti? Kama ndivyo, ilivyo je, ninafanya nini katika hilo? • Je, nina nidhamu nzuri katika njia zangu au mimi ni mvivu? • Je, ninatumia muda wangu vizuri na mwenzi wangu na watoto? • Je, ninachelewesha kuanza kazi au ninafanya kazi kwa bidii, kutunza wito wangu na kuheshimu neno langu? • Je, mawazo yangu ni mazuri? Je, mawazo yangu yapo kwa Mungu? • Je, ninasoma Biblia na vitabu vingine vya Kikristo kunisaidia mimi kukua? • Je, ninafanya kazi na wachungaji, kuwasaidia kulijaza kanisa au kuanzisha kanisa lingine? • Je, nimesoma na kuelewa - na pia ninafuata - yasemayo Maandiko kuhusu wale walioitwa katika uongozi katika kanisa la Kikristo (1 Timotheo 3:1-13; Tito 1:5-9)? Tumia mistari hii kujisaidia wewe - na wainjilisti wengine - jikumbushe na pia kutia moyo. Dhamani Ya Kuwa Mwinjilisti Mzuri Siyo rahisi kuwa katika huduma, bali zawadi ya utii wa wito wa Yesu Kristo ina thamani kuliko dhiki. Kuwaona watu wanakuja kwa Kristo ni zawadi kubwa tunayoweza kuwa nayo duniani. Biblia inatufundisha kuwa “mwenye hekima huvuta roho za watu” (Mithali 11:30). Zipo zawadi za kipekee za milele zinazowasubiri walio watiifu na wenye imani katika Kristo. Kwa wale wanaowashawishi wengine kwa ajili ya haki, Daniel 12:3 anasema, “Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.” Tunda la Injili na kuwaambia wengine habari za Kristo ni tunda la milele ambalo litadumu milele. Mungu siku zote atawafariji na kuwazawadia wale wanaomtumikia na imani na utiifu wa moyo. Yesu anaelewa vizuri, na zaidi ya wengine wote, majaribu na vikwazo ambavyo tunakutana navyo katika maisha tukiwa wafuasi Wake. Lakini tuna mfano Wake mzuri na tutashinda, “tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu” (Waebrania 12:2). Furaha ya Kristo inajumuisha uelewa kuwa kifo chake kitaturudisha katika uhusiano wa Mungu, aliye Baba – Baba yetu wa mbinguni! Sisi waumini ni furaha kwa Kristo, ni Bibi Arusi mtarajiwa kwa hamu kubwa (Waefeso 5:25-27; Ufunuo 19:7-9). Kuwaleta wengine kwa Yesu ili waokoke kupitia Yesu Kristo kutuletee furaha pia. Kukamilisha wito wa Mungu maishani mwako kutakugharimu sana. Kila muumini ana gharama zake: kuacha utajiri, uchoyo, na matendo ya mwili - na kubadilishwa tufanane na Yesu. Unapotoa maisha yako kuishi maisha ya sadaka kwa ajili ya Kristo, utafanya zaidi ya yale ambayo Baba anafanya. Utaona nguvu zaidi za Mungu na uwepo wake kwako. Unapoendelea kuwa mwenye nidhamu na mwenye imani, utakuwa mwenye ujuzi wa kuziokoa roho zinazopotea na kuwa mvuvi wa watu (Mathayo 4:19). Utakua katika hekima, na kuwa tajiri katika mambo ya Mungu. Kumtumikia Mungu kwa maisha yako kuna thamani kuliko gharama yoyote (1 Wakorintho 9:19-22 Maisha Ya Binafsi Ya Mwinjilisti Mwinjilisti – kama muumini yeyote, anajitahidi kuishi maisha safi na yenye mwelekeo mbele zake Mungu. Ni lazima awe na uhusiano mwema na familia yake na jamii yake. Matunda ya mwili kama hasira au kuhukumu, itaonesha vibaya wakati unapohubiri. Kumtendea mkeo au watoto mambo yasiyo mema halimfurahishi Mungu, na linaathiri ushuhuda wako kwa wengine. Kudanganya mtu kunatoa jina mbaya kwa ajili ya Kristo, ambaye unamwakilisha. Kusema nitafanya jambo fulani na hatimaye usifanye si jambo la uaminifu na si la Kimungu. Tabia yako ya kutenda dhambi ni lazima ishughulikiwe ili uweze kumwakilisha Kristo kama alivyo na mambo yatendwayo na nguvu yake ya kukomboa! Mwinjilisti apende Biblia na aisome na kujifunza. Atafute nafasi itakayomwezesha kuwashirikisha ukweli wa Bwana, lakini asiache wajibu wake wa kutunza familia au kazi yake ya asili. Mwinjilisti anaomba sana - katika basi, anapotembea, akiwa katika jumuia ya watu, au akiwa peke yake, daima ni vema kuomba na kumsikiliza Mungu. Moyo wa mwinjilisti ni lazima uwe laini na wa kufundishika. Wakati unapomngojea Mungu, atakusaidia umfahamu zaidi. Wakati unapokua katika kumjua zaidi, utakuwa mwinjilisti mzuri kwa sababu unamfahamu Baba yako. Yesu alifanya tu yale aliyofanya Baba; alisema tu yale Baba aliyosema (Yohana 5:19; 8:26). Shabaha yetu kama wahudumu ni kumjua Mungu kwa karibu ili tuweze kuongozwa kwa sauti yake na kujua mapenzi yake. Kama umeolewa ni lazima umwangalie mwenzi wako kama ambavyo Yesu angemwangalia, na kuwapenda kama alivyolipenda Kanisa (Waefeso 5:25). Mtunze mkeo kwa upole na kwa ufahamu (1 Petro 3:7) Mjali mumeo kwa heshima na utii (Waefeso 5:33). Kama hujaolewa lazima uwe na mawazo mazuri na mwili safi (1 Wathesalonike 4:3-5). Bwana anajua yote uyatendayo kwa siri zaidi ya masikio na macho ya watu wengine. Mhudumu ambaye hajaoa au kuolewa anapaswa kuwa na mawazo na matendo maadilifu. Ni lazima wakiri makosa yao na kujiweka mbali na vifungo vya tabia ya dhambi. Katika mahusiano ya kibiashara, kifamilia, kikanisa, au kirafiki ni lazima yasiwe na lawama ili kazi ya Yesu isiwe na kipingamizi au isemwe vibaya. Wengi wetu tumesikia watu wakipinga wokovu wa Yesu kwa sababu ya muumini wanayemfahamu hakuwa mpole, haaminiki, au si mwaminifu. Wamekuwa “kikwazo” kwa sababu ya matendo ya dhambi ya waumini (1 Wakorintho 10:32-33 Kama mhudumu unamwakilisha Mfalme wa wafalme. Maneno yako lazima yawe kweli; ni lazima utende yale yote uliyoyaahidi. Kama huwezi kwa maneno yako, na badala yake unatoa udhuru, inaweza kuwa kikwazo kwa wengine, na kuwafanya wampinge Kristo. Mnawakilisha Yesu kila dakika katika kila siku, siyo tu wakati unahubiri, lakini katika kila tendo. Maneno yako yawe ya kutia moyo, na siyo yaliyojaa lawama (Waefeso 4:15,29; Wakolosai 4:6). Mungu anatamani tuwe vyombo vya heshima (2 Timotheo 2:21). Huwezi kuwaandalia wageni wako katika vyombo vichafu. Ungependa uwape chakula katika vyombo safi. Mungu anapokea heshima wakati wewe ni msafi kiroho na kuwa tayari kuwa chombo chake. Kama dhambi, kusema mabaya, au tabia mbaya ya maisha yako hautakuwa unafaa kwa kazi ya Mungu. Chukua muda sasa wa kumtaka Roho Mtakatifu achunguze moyo wako. Wakati anapozungumza nawe, ukiri, utubu kwa njia ya maombi, na umruhusu Yesu aondoe mambo yote machafu. Utakuwa huru na utatumika kwa Bwana wako. Tubu mbele za Mungu mara kwa mara. Chukua hali ya chini ili Mungu apate kukuinua na kukuweka katika makusudi makubwa. Katika maombi yako, toba na kukiri iwe sehemu ya kila siku: Mtake Mungu akuchunguze; mwombe akusamehe, mwombe Mungu akupe uzima. Ni Lazima Ujifunze Neno La Mungu, Yaani, Biblia Biblia ni chanzo chako cha Ukweli. Ni lazima uisome kila siku, jifunze na kukariri mistari ili uweze kukua na kukomaa na ufundishe na kuhubiri vizuri. Usihubiri jambo lolote ambalo haliwezeshwi na Maandiko yote. Mafundisho ya uongo yamekuwepo sana siku hizi. Biblia inatuonya juu ya waalimu wa uongo na mafundisho ya uongo yatatokea siku za mwisho na wengi watapotoka. Wakati unapojifunza, chunguza Maandiko kila siku ili kuhakikisha kuwa lile unalolisikia ni kutoka kwa Neno la Mungu (Matendo 17:11). Mtu ambaye hajui maneno ya Mungu hawezi kutoa ushauri mzima wa Kimungu kwa watu. Bwana anaelekeza, “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” (2 Timotheo 2:15). Chukua muda sasa hivi kumwomba Roho Mtakatifu kuupeleleza moyo wako. Wakati anapozungumza na wewe, ungama, tubu katika sala, na mruhusu Yesu aondoe uchafu wote. Utakuwa huru na pia utatumika zaidi kwa Bwana wako. Kuna mwinjilisti nchini India alikuwa anakariri mistari ya Biblia kila juma. Watoto wake nao pia walikariri mistari kila juma. Alikariri maelfu ya mistari. Alipohitajiwa kuhubiri au kushauri au alipohitaji hekima, alikuwa ameweka maneno ya Mungu katika moyo wake. Mtu huyu aliye na nguvu ya Neno la Mungu ambalo laweza kugeuza watu na kumlinda mwenyewe kutoka nguvu za uovu (Zaburi 119:11). Ni Lazima Uwe Ni Mtu Wa Maombi Maombi katika maisha ya mhudumu au mwanafunzi wa Yesu hayana uchaguzi - ni agizo la msingi, na linapatikana katika Maandiko yote! Uwe ni mtu wa maombi. Anzisha tabia nzuri ya maombi. Omba katika muda uliojipangia kila siku. Omba wakati unapotembea au unapokaa. Omba kila wakati wa usiku na mchana (1 Wathesalonike 5:17). Omba kwa roho na ufahamu (1 Wakorintho 14:15). Kufunga na kuomba kunavunja vifungo vyote walivyofungwa navyo watu na maeneo. Mwinjilisti mmoja katika Afrika aliyataka makanisa mbalimbali kufunga na kuomba pamoja. Mikutano hii iliwasaidia kuunganisha makanisa kwa kusudi maalum na kuzidisha matokeo ya kiroho. Kazi ya ibilisi imezuiliwa wakati watu wanapokutana pamoja. Makanisa yamebadilika na watu wengi wamekuja kwa Kristo kwa sababu makanisa na wainjilisti wameomba na kufanya kazi pamoja. Huwezi kuwa mhudumu au mwinjilisti ambaye Mungu amekusudia pasipo kuwa ni mtu wa maombi. Katika maombi unapata uhuru, msamaha, nguvu, na mwongozo unaoutaka. Chukua muda wako wa kuomba na timu yako au na kiongozi mwingine. Tafuta mwombezi na kuwataka wakuombee kila siku. Chukua muda uombe kila siku na wenzako na pia omba peke yako, ombea nchi na watu ambao utawahubiria. Endelea Kuwa Mwanafunzi Inaweza kutokea kuwa hakuna uwezekano wa kujiunga na Chuo cha Biblia au Seminari. Tafuta mapenzi ya Mungu katika jambo hilo na kulifuata kwa imani. Kama pana uwezekanao, hudhuria mafundisho yatolewayo katika semina au masomo ya Biblia katika eneo lako. Chukua nafasi uongee na wahudumu wengine na wainjilisti. Jifunze kutoka kwao, na jitolee utumike nao. Wako tayari, kutenga muda wa kuwauliza maswali. Nenda uwasikie wakihubiri. Wasikilize, watathimini, na jifunze. Baadhi ya wanaume na wanawake waliofanikiwa hawakupata elimu ya masomo ya Biblia, hata hivyo walifanya mambo makubwa kwa Mungu. Wahudumu wazuri sana ni wale wanaojifunza Biblia kwa uaminifu na kuendelea kujifunza kwa kadri iwezekanavyo, na kuyaweka kwa vitendo yale waliyojifunza. Kujifunza ni zaidi ya kuingia darasani. Kujifunza ni jambo ambalo linafanyika kwa maisha yote. Tafuta Mshauri Katika Kristo; Uwe Mshauri Kwa Wengine Omba na kumtaka Mungu akupe mwalimu, mshauri katika Bwana. Huyu ni mtu ambaye amekomaa katika Mungu, atakayekusaidia kukua. Mshauri anatoa ushauri wakati anakuangalia katika maisha yako. Katika nchi nyingi, mtu ambaye ni mchanga kiimani anamtaka mtu aliyekomaa awe “baba wa kiroho” wake. Hii inafanyika pia kwa wanawake wanaohitaji mama wa kiroho. Wajibu wa mtu aliyekomaa ni kumwongoza na kumfundisha yule aliye mchanga kiimani, awe ni msaidizi atakayempa hekima. Paulo alikuwa na uhusiano na Timotheo (1 Timotheo 1; 2 Timotheo 1:2). Ni jambo la uhakika kuwa Paulo alimpenda Timotheo na alimtaka Timotheo mzuri. Paulo alikuwa tayari kujitoa na kuchukua muda kumsaidia na kumfundisha Timotheo. Walio wachanga kiimani ni lazima waheshimu wazima na uzoefu wa wale waliokomaa kiimani. Ni kwa njia hii hawa wachanga wanapata ujuzi muhimu kwa njia ya uzoefu na hekima ambayo wengine wamejifunza kwa miaka mingi. Ni njia ya Mungu kuelimisha viongozi wa vizazi vijavyo. Ni lazima uanze kuangalia mtu au watu wawili wa kuelimisha, ambao watapata faida kutokana na uzoefu na mafunzo yako (2 Timotheo 2:2). Omba na Mungu atakuonesha ni nani umwelimishe na kumshauri. Kukataliwa Na Kujaribiwa Kazi ya mwinjilisti inamweka katika hali ya kukutana na watu ambao watakubali au watamkataa Kristo. Wale watakaomkataa Kristo watamkataa mwinjilisti pia. Siyo kila mtu alimkubali Yesu na ujumbe Wake wakati alipohubiri. Baadhi ya watu watakuwa na hasira nawe na kukuchukia kwa sababu unaleta Habari Njema. Baadhi ya wainjilisti watapigwa na kutishiwa maisha yao kwa kumhubiri Kristo. Hata baadhi ya wanafamilia wanaweza kuwa kinyume nawe. Yesu alituambia tutateswa kwa sababu Yake (Mathayo 10:16-20). Watu watazungumza yasiyofaa na pia kutoa hukumu za uongo. Ni muhimu usifanye moyo wako kujishitaki au kukua katika uchungu, kwani utajichafua wewe na wengine (Zaburi 37:38; Waebrania 12:15). Usije ukawalaumu watu wengine wanapokushitaki. Usije ukapenda kulipiza kisasi. Huu siyo mpango wa Mungu wa kushughulika na majeruhi ya rohoni (Warumi 12:17-21). Hasira ya mwanadamu siku zote haitengenezi haki ya Mungu (Yakobo 1:20). Ni lazima kusamehe wale ambao wamekukosea na kukuudhi (Mathayo 18:21-35). Njoo kwa Mungu kama ungemjia Baba mpendwa ambaye anakujali na kukukubali (Warumi 15:7; Waefeso 1:6). Unaweza kuyatoa majeruhi yako kwa Mungu na pia kumwambia akuponye (Zaburi 42:4; 62:8). Acha Baba yako wa mbinguni akufariji, akutengeneze na pia kukujenga katika majaribu. Kama hupendi Mungu ayachukue majeraha yako ya kukataliwa, ibilisi atayatumia majeraha yako kukuumiza wakati unahubiri Injili. Utajaribiwa kubadili ujumbe wako ili upate kushawishi watu wakunje mkono. Biblia inaita mtego huu kuwa ni “kuwaogopa wanadamu” (Mithali 29:25). Kuwa makini pia na mtego wa mafanikio. Mafanikio katika uinjilisti yatakufanya uanze kujihesabia ushindi na kuanza kujitwalia utukufu. Unaweza ukaanguka katika dhambi ya kujivuna na kuanza kuhudumu kimwili. Angalia sana majivuno (Mithali 11:2; 16:18; 1 Petro 5:5-9). Lazima tuwe wapole kwa Mungu pamoja na majeraha tuliyonayo, tubu kwa uchoyo na kiburi, samehe waliokukosea na umwombe Mungu kwa uponyaji katika maisha yetu. Unapomruhusu Mungu akuponye utakuwa na uhakika wa Mungu zaidi na upendo. Utagundua kuwa anakupenda na pia wewe ni muhimu Kwake. Baadaye utakuwa na uwezo wa kuwapenda wanaokukataa na kuchukia, katika nafasi uliyonayo katika Kristo - ambapo ni mahali pa nguvu ya kushinda na kukubaliwa bila sharti lolote. Kuwa Na Mpangilio Na Huduma 1) Maono (Dira) Kwa Ajili Ya Huduma Je, unajua huduma yako inaenda wapi? Je, unayo dira kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kazi yako maishani? Kama huna, unaweza kumwambia Mungu akupe dira na mwelekeo katika maisha yako. Kama amekuita na kukupa kazi ya huduma yake, anapenda kukuonesha ufanye nini ili kufanikisha hilo! Katika maono ya pekee, Isaya aliyaona maono ya Bwana (Isaya sura ya 6). Isaya alikubali hali yake ya dhambi na alitubu na alibadilishwa. Mungu alimwita kuwa nabii na kufunua njia na shabaha katika maisha ya Isaya. Maono kama hayo siyo ya kawaida, na yametokea kwa watu maalum katika Maandiko ambao Mungu aliwapa mwito wa pekee (kama Isaya; na Sauli [Paulo] katika Matendo 9:1-19). Lakini Mungu amekuita katika huduma yako. Ana mpango maalum kwako ili uutimilize. Kama unavyomtafuta kwa bidii na kutumia muda katika sala, Mungu atakusaidia uweze kuona mapenzi yake katika maisha yako. Atakupa ndoto au maono. Tena atazionesha njia zako unavyomtegemea na kumkubali siku hadi siku (Mithali 3:5-6; Mathayo 6:33). Yesu alifanya tu yale ambayo Mungu alimfunulia. Alisema, “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo anamwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile” (Yohana 5:19-20). Yesu alifanya yaliyo mapenzi ya Baba. Hakufanya wala kusema kila kitu isipokuwa lile ambalo Baba alimfunulia. Yesu amekuwa ndiye ametuonesha mfano wa kumtegemea Baba kabisa. Mungu amejifunua Mwenyewe na makusudi yake katika Biblia nzima. Njia mojawapo nzuri sana ya kumtambua Mungu na makusudi Yake, ni kusoma Neno la Mungu mara nyingi uwezavyo. Biblia ni “mwanga wa njia yangu” (Zaburi 119:105). Mwanga unatuangaza njia zetu, unatusaidia kuona jinsi ya kutembea. Mruhusu Mungu akuoneshe kwa upya ukweli mtimilifu wa Maandiko ili akuongoze katika njia zake. Mungu aweza pia kukupa mwelekeo maalum, kuhusu majukumu ya huduma. Je, unataka kuufikia mji fulani ili watu wapate kumjua Kristo? Je, umeomba na kumtaka Mungu akupe mpango wake? Je, umetaka Mungu kama anayo njia ambayo ingewezesha uinjilisti kufanyika? Au jinsi ya kuanzisha kanisa? Wakati mwingine Mungu anakupa hatua za wazi kabisa za kufuata ili kuyafanya mapenzi yake. Mruhusu Roho Mtakatifu azungumze nawe na kukuongoza katika kufanya maamuzi – kama ni mahali gani pa kuhubiri, ni jambo gani la kusema, ni nani atafanya kazi nawe? Usiwe na hamu ya kujenga yafuatayo au kuwa na sifa uwe mkuu. Usiwe na hamu ya kujenga huduma yako au kuwa na mafanikio. Tunafanya kazi kwa matunda ya milele (Yohana 15:16), si ili tupate thawabu hapa duniani (Mathayo 6:1-4). Uwe na utayari wa kwenda na kufanya kazi - wakati na mahali pale Roho akuelekeza, kwa utukufu wa Mungu. Kila mji au jinsi ni tofauti; hivyo njia ya kufikia mahali au kundi la watu inaweza kutofautiana. Mtume Paulo alipewa jinsi ya kufikisha utume wake. Aliwahubiri Wayahudi kwanza; ndipo akaenda kwa wasio Wayahudi. Katika safari yake ya pili ya misheni, alitaka kwenda kaskazini na mashariki; lakini Mungu akamkataza. Alipata ndoto ambayo mtu kutoka Makedonia (Ulaya) alikuwa anamwita aende na Je unajua mtazamo wa huduma yako? kuwasaidia (Matendo 16:9-10). Paulo alikuwa anataka kuyafanya mapenzi ya Mungu, lakini alikuwa karibu na kwenda mwelekeo mbaya. Mungu alitaka Paulo na timu yake kwenda magharibi, Ulaya na kuipeleka Injili. Paulo, alipofika Makedonia, alimkuta Lidia ambaye ndiye wa kwanza kuongoka Ulaya (Matendo 16:12-15). Lidia alikuwa mfanyabiashara, alimpa Paulo nyumba yake aitumie kwa kazi yake, na kuwa ndilo kanisa la kwanza Ulaya. Nyumba hii ikawa pia msingi wa uinjilisti maeneo ya Ulaya. Lidia na wenzake walimsaidia Paulo katika kueneza Injili. Mungu alikuwa na mpangilio ulio wazi, lakini Paulo alihitaji kufahamu mpangilio utakaomsaidia kutimiza kusudi la Mungu. Mngoje Bwana, mwombe na kujitoa mbele Zake. Mwimbie Yesu; msifu; mwaga moyo wako wote Kwake; na hatimaye ngoja umsikie Yeye. Mungu ataachilia kusudi lake kwako. Mungu anaweza kukupa maono maalum au mpangilio, au kuyafunua mapenzi yake katika picha za kiakili au kwa maneno na kuziweka katika mawazo yako. Yaandike yote, pamoja na tarehe, Mungu aliyokuambia na kukuonesha. Yaombee haya yote na yaweke yote mbele ya watu wa kiroho ambao unawaamini. Anza sasa kuchukua hatua ya imani kufanya yale ambayo Mungu amekuonesha uyafanye! 2) Maelezo Ya Taswira Mara unapoanza kuona mwelekeo na dira, inasaidia, ukiandika maelezo ya taswira. Maelezo ya taswira yanakueleza kwa kifupi lile ambalo umeitwa kwalo. Maelezo haya yanasaidia sana kama yatatolewa kwa ujumla kuliko kuwa na mambo madogo madogo. Kwa mfano, badala ya kuandika “Tutaanzisha makanisa matano na nyumba za yatima mbili na kuwa na mikutano mwaka huu”, ingekuwa vizuri kama ungeandika, “Tutaeneza Injili kwa kuanzisha makanisa na kufanya kazi za kijamii kama Mungu atakavyotuelekeza, ili Yesu atukuzwe. Tenganisha maeneo ya kazi na kuyawekea malengo maalum na yaandike yote. Kwa mfano, kama Mungu amekupa wito wa kuanza shule, iweke kwenye maelezo yako pia. 3) Malengo Baada ya kuandika maelezo kwa njia ya maombi, elezea kimaandishi jinsi ya kufikia dira na taswira ili zifanyike. Je, una mpango wa kuifanya? Andika malengo yote ambayo unakusudia kukamilisha. Huo ndiyo wakati wa kuwa na mambo madogo madogo zaidi. Kwa mfano: “Baada ya muda wa miaka miwili tutaelimisha wachungaji wawili na kuanzisha makanisa mawili katika eneo hili; baada ya miaka mitano tutakuwa na makanisa matano zaidi.” Au, “Kundi letu litahubiri Injili kwa kila kijiji katika eneo hili - katika kijiji kimoja kwa mwezi, kwa miaka mitatu inayofuata.” Au, “Tutasambaza vipeperushi 10,000 katika miji kwa miezi sita ifuatayo. Pia tutakuwa na mikutano ya uinjilisti katika maeneo yote manne ya mji kila juma.” Kuwa na utaratibu mzuri unasaidia kuwezesha kazi kufanyika kwa vizuri. Kwa njia ya maombi na kumsikiliza Bwana, utajua mpango wake kwa ajili yako. Mungu atakupa njia ya kusaidia makanisa waweze kufanya kazi ya uinjilisti kwa pamoja. Maelezo ya taswira yako na malengo yako ni muhimu yaeleweke kwako, katika mawazo yako, na uwe tayari kumwambia mtu yeyote atakayekuuliza. Ni muhimu kuombea maandiko haya mara kwa mara na kuwa na nia ya kubadilisha au kurekebisha ifanyike hivyo kama ni lazima. Kumsikia Mungu na kufanya mambo yote kwa imani itakufanya uwe na mafanikio katika kukamilisha kusudi la Mungu kwako. Wengine wataona ni rahisi kuelewa na kukuwezesha na kazi yako. Kujenga Timu Ya Uinjilisti Yesu alijenga kundi la watu kumi na wawili. Yesu aliwatuma watende kazi yake wawili wawili nao; walikuja tena kutaka maelekezo na mahusiano, na kwenda tena. Mtume Paulo alijenga pia timu zake. Wakati mwingine alikwenda mwenyewe, lakini alipendelea kufanya kazi kwa timu. Kila mtu katika timu yake atakuwa na karama tofauti na wewe. Hii itaongeza mafanikio zaidi katika huduma. Mwinjilisti mmoja alikuwa na mwanamke katika timu yake aliyekuwa na karama ya kuponya. Mtu huyu mara nyingi aliona nguvu ya Yesu na kutenda miujiza ya kuponya katika mikutano yao. Watu wengi wanafunguliwa katika Injili wakati wanapomuona Yesu akiponya watu kwa njia ya huduma ya mwanamke huyu. Mwanamume mwingine katika timu alikuwa na uwezo wa kuandaa mikutano mikubwa ya kiroho katika miji. Mwinjilisti huyu aliwaelimisha wainjilisti wengine katika timu yake. Kulikuwa na wainjilisti watatu katika timu hii ambao walikuwa wakihubiri katika magulio, wanaotembelea wafungwa vifungoni au hospitali, au walifanya mambo ambayo yalihitajika katika kuwashirikisha wengine ujumbe wa wokovu. Kuwainua na kuwatia moyo wafanyakazi inasaidia kuiwezesha Injili kufikia wengi na kuwa na mafanikio makubwa. Timu inakuwa kama familia ambako mahitaji yote yatumike na malengo ya taswira yanatimilizwa. Kuwa Mtumishi Wa Ufalme Mungu hamuiti mtu yeyote awaye yote kujenga huduma yake mwenyewe. Mungu amekuita kwa makusudi yake, na amekuruhusu wewe kuwa mbia wake kama Yesu anavyojenga Ufalme wa Mungu! Viongozi wengi wa kanisa wanataka kumtumikia Mungu, lakini wanataka watengeneze jina kubwa kwa wao wenyewe. Wanadharau na kukatisha tamaa viongozi wengine na wahudumu. Ni wachoyo na hawataki kuwatumikia wahudumu wengine kama mbia. Wanafikiri utumishi wao ni mzuri zaidi, na kazi yao ndiyo kazi pekee muhimu. Na hii ni chukizo kwa dunia na Kanisa! Kiongozi wa namna hii hulenga zaidi maslahi yake mwenyewe na siyo mahitaji ya wengine, na pia siyo kwa Ufalme wa kweli wa Mungu. Hii siyo Roho ya Kristo. Kushiriki na watu wengine na wahudumu wengine kunaleta utukufu mkubwa kwa Mungu na ufanisi mzuri zaidi katika kazi. Kutia moyo na kuwasaidia wahudumu wengine kunaleta baraka kubwa za Mungu katika utumishi wako. Unapotoa, unapokea (Luka 6:38). Wakati unapopoteza maisha yako (na matakwa yako) kwa ajili ya Kristo, utapata maisha ya kweli (Mathayo 16:25). Wakati unapochukua “nafasi ndogo” ya kutumikia wahudumu wengine na huduma zingine, Mungu atakupandisha cheo (Luka 14:10-11). Maono yako yanatakiwa yawe na uwezo wa kufanya kazi na makundi mengine, makanisa, na huduma mbalimbali. Hii ni kujenga Ufalme mkubwa wa Mungu na siyo kanisa moja, dhehebu au huduma moja. Wakati wahudumu wanapofanya kazi pamoja, watu wanaona umoja wa Mwili wa Kristo na baraka za Mungu zinakuja (Zaburi 133:1-3). Wainjilisti wanajikusanya pamoja na kufanya kazi katika makanisa yaliyo mengi katika miji na kuleta baraka nyingi katika mji huo. Tenga Muda Kupumzika Wafanyakazi wengi wamechoka kama ukuni katika moto maana hawakuchukua muda wa kupumzika. Miili yao huugua; mawazo yao huchoka; roho zao hufifia; na pia kushindwa kuhimili majaribu. Mungu ameamuru kuwa tupumzike siku moja kwa juma. Sote tunahitaji mapumziko. Kila muhudumu - na kila mtu - anahitaji mapumziko angalao mara moja kwa juma kujirudisha upya kwa Mungu na kupumzisha mwili wake, mawazo yake na roho yake. Kuna wakati ratiba yako inahitajika sana zaidi ya kawaida. Utumike lakini ni lazima utenge muda wa kupumzika na utafute matendo ambayo yanaburudisha mwili wako. Wakati Yesu na wanafunzi wake walipohudumu, watu wengi walikuwa wanaingia na kutoka hata wakati mwingine Yesu na wanafunzi wake hawakuwa na muda wa kula. Yesu aliwambia, “Njooni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokua na watu, mkapumzike kidogo” (Marko 6:31). Mara kwa mara Yesu alikuwa na muda wa 􀂄 Shirikiana na watu pia wahudumu wengine kuleta utukufu mkubwa kwa Mungu na ufanisi mzuri wa kazi. kupumzika na pia kufanya sala. Yeye ni mfano kwetu kuwa hakuna asiyeruhusiwa na Mungu kupumzika. Chombo Cha Heshima Kumbuka kuwa watu watapokea zaidi uyasemayo endapo watakuheshimu wewe kama ulivyo na unavyoishi katika maisha yako. Kujiweka chini ya maongozi ya Ufalme wa Mungu ni jambo la muda mrefu. Unatakiwa siku zote ukue, ujifunze, na pia ujitoe kwa kazi ya Mungu inayolenga kwako. Mwinjilisti, Mungu amekuita kuubeba ujumbe Wake wa ukombozi kwa watu wengine. Unaweza ukawa mfano hai wa mabadiliko mazuri ambayo ujumbe wa Mungu unaweza kufanya katika maisha ya mtu. Chunga sana maisha yako yawe safi na pia angalia mwelekeo na tabia yako. Mungu anajishughulisha na mabadiliko ya maisha yako kwa jinsi ambavyo wewe unajishughulisha na kutafuta msaada Wake. Atakupenda na kukuwezesha wewe na kazi yako kwa kukubadilisha wewe kutoka ndani. Ni lazima utii na kulifuata Neno Lake. Jipe muda wa kutosha kujichunguza mbele za Mungu na kuitikia maneno Yake na kuyaacha yafanye kazi katika maisha yako na familia yako. Kwa kufanya hivyo utakuwa mwinjilisti na mhudumu mzuri wa Injili aliye chombo cha heshima na amfaaye Bwana wake! Mambo Yaliyo Muhimu Zaidi Tabia yako – itakavyokuwa ni kitu muhimu sana mbele za Mungu zaidi ya kitu chochote ungefanya kwa ajili yake. Mungu anajali zaidi jinsi ulivyobadilishwa kufanana na Yesu zaidi, kuliko kiasi cha kazi unachoweza kumfanyia. Utii na kujitoa kwako kwa Mungu ni kitu muhimu sana kwake zaidi ya mikutano mingi yenye mafanikio na wingi wa watu. Mwamko wa kumwonesha Yesu katika utukufu wake, nguvu, uweza wake ni muhimu kuliko kujitengenezea sifa. Yaweke mawazo hayo akilini mwako kila siku katika huduma yako. Miongozo hii na mafundisho haya yanalenga kukusaidia wewe uwe mtu mwenye uwezo kwa Kristo Yesu Bwana wetu. KIMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA BISHOP RHOBINSON S. BAIYE Texas Mwanza Tanzania rhobinsonsaleh1@gmail.com 255762 50 62 32 11/ 8 /2021

No comments:

Post a Comment

UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...