Friday, August 27, 2021

IFAHAMU BIBLIA AGANO LA KALE

Advertisemen Sauti Ya Gombo International Ministries Network IFAHAMU BIBLIA TAKATIFU THIOLOJIA YA BIBLIA BISHOP RHOBINSON S.BAIYE ELIMU YA BIBLIA BIBLIA NI NINI? Neno Biblia linatokana na neno la kiyunani Biblosi ambalo lina maanisha Kitabu kitabu Cha vitabu kwa sababu ndani ya Biblia kuna vitabu 66 Agano la kale 39 na Agano jipya 27.Pia Biblia ni maktaba ya Mungu kwa mwanadanmu.Mungu amefunua mawazo yake kwa mwanadamu kupitia Biblia.Hivyo tunaweza kusema kuwa Biblia ni kitabu cha mawazo ya Mungu.Ndani ya Biblia kuna mawazo ya Mungu na matendo ya Mungu. ASILI YA BIBLIA Asili ya Biblia ni Mungu mwenyewe. Mungu ndiye chimbuko la Biblia kwani ndiye aliyetoa ufunuo wa kuandika Biblia. Aliwatuma watu mbalimbali walioishi nyakati mbalimbali na historia na tamaduni tofauti tofauti kuandika Biblia. watu hao wengine hawakujuana kabisa lakini tunashangaa jinsi mawazo yao yanavyopatana katika maandiko matakatifu. “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko Upaswao kufasiriwa kama apendendavyo mtu fulani tu. Maana unabii Haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu bali wanadamu Walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho mtakatifu.2Pet 2;19 Mstari huu unathibitisha kuwa asili ya Biblia ni Mungu mwenyewe na kwamba aliwatuma wanadamu kama vyombo katika kuandika Biblia takatifu. Nigel Day Leulis anasema Biblia ni kitabu kilichoandikwa na watu waliovuviwa na Mungu chenye kumbukumbu zisizo na mapungufu au makosa, kumbukumbu zenye ufunuo wote wa mungu kwa mwanadamu na kwa hiyo Biblia inayo mamlaka ya mwisho kwetu katika mambo yote yahusuyo maisha na mafundisho. Biblia ina kila kitu tunachohitaji kujua juu ya wokovu na hakuna chochote kinachohitajika kuondolewa ndani yake au kuongezwa juu yake. BIBLIA NA MAANDISHI Mungu Roho mtakatifu aliwatumia waandishi kama 40 katika kuandika Biblia na waliandika kwa muda wa miaka kama 1600. Biblia iliandikwa na waandishi wengi kama ilivyoelezwa hapo juu baadhi yao walikuwa wafalme kama Daudi na Sulemani na wengine walikuwa waganga na wataalamu kama Isaya na Luka. Wengine walimu wa dini kama Ezra na Paulo wengine maafisa wakubwa wa Serikali kama Musa, Danieli na Nehemia, wengine wakulima na mafundi Amosi na Yohana , wengine wavuvi kama Petro , wengine watunga muziki kama Asafu na watoto wa Kora wengine manabii kama Ezekiel, Yoeli na kadharika. Wengine kati ya waandishi hawakujuana kabisa, waliishi katika nchi tofauti tofauti wengine palestina (baadhi ya manabii) wengine Babeli kama Danieli na Ezekieli na wengine wakisafiri katika Nchi za mbali Paulo na Mitume wengine na mmoja wapo aliandika akiwa kifungoni katika kisiwa cha Patmo Yohana Kwa kweli Biblia iliandikwa kwa njia ya pekee kuliko vitabu vingine vyote. Ingawa Biblia iliandikwa kwa muda wa miaka 1600 na maandishi mengi tunaiona mbele yetu kama kitu kimoja jambo hili laweza kuelezwa kwa njia moja tu. Ingawa Biblia inawaandishi wengi ni moja tu aliyeitunga nae ni Roho mtakatifu. Habari yake tunaanza kuipata katika ukurasa wa kwanza wa Biblia (Mwa: 1: 2) Nae anasema nasi mpaka ukurasa wake wa mwisho (Ufu 22:17) LUGHA ZA BIBLIA Agano la kale: liliandikwa hasa katika Kiebrania kuna sehemu ndogo zilizoandikwa katika lugha ya kiaramu jina la kiaram linaonekana katika Danieli 2:4 sehemu zilizoandikwa katika kiaramu ni hizi: Ezra 4:8 – 6:18:7:12 – 26 Danaeli 2:4 – 7:28 Yeremia 10:11. Agano Jipya: Maneno yote ya agano jipya yaliandikwa kwa kiyunani kwa kuwa ilikuwa lugha iliyojulikana kwa karibu na watu wote ingawa katika nchi hiyo ya Israel kiaramu kilikuwa ni lugha ya nyumbani zamani za Bwana Yesu kristo. UMOJA WA BIBLIA Sehemu za Biblia zinaonesha tofauti lakini ni tofauti zenye maana kwa kuwa sehemu zote zinapatana na kuwa na umoja. Nikama sehemu za nyumba jinsi zinavyopata mlango haufanani na paa ila vinapatana katika nyumba moja. Dirisha halilingani na mlango bali vinapatana vivyohivyo na sehemu zote za vitabu vyote vya Biblia ndivyo zinavyopatana katika maneno yafuatayo Tabia ya mungu Hali ya mwanadamu Ukombozi Kuja kwa masihi mara ya pili. UJUMBE WA BIBLIA Ujumbe wa Biblia nzima ni Ukombozi tangu mwanzo hadi Ufunuo yote inahusu ukombozi. Agano la kale linaonyesha watu kuwa wanaugonjwa usio kuwa na tiba wala nafuu isipokuwa Mungu alikuwa akiwaambia kuwa kuokoka kutaonekana kwa njia ya ukombozi tu. Aliwafundisha hivyo kupitia mifano na unabii dhima kuu katika unabii ni Isaya 53. Katika hii kuna mistari 12 tu.Katika Agano jipya tunaona kuwa Masihi alikuja kuwa mkombozi tunasoma maneno yake matendo yake hata kufa kwake alipojitoa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi ili achukue adhabu za wanadamu. Hivyo Biblia nzima ina ujumbe mkuyu mmoja tu nao ni ukombozi.na kiini chake ni kimoja tu nacho ni Yes u Kristo Mwokozi wa ulimwengu MUUNDO WA BIBLIA Biblia ni maktaba yenye vitabu 66 ambavyo mpangilio wake haufuati vipindi vitabu vilipoandikwa (kama ambavyo tungetarajia) lakini mara nyingine vimepangiliwa kwa kufuata mitindi ya kiuandishi. Vitabu vyenye muundo mmoja wa kiandishi vimewekwa katika fungu moja mfano vitabu vya torati, Historia, Ushahiri na unabii. MPANGILIO WA VITABU VYA AGANO LA KALE Mtindo wa kiuandishi Majina ya vitabu Jumla Sheria Mwanzo – kumbukumbu la torati 5 Historia Yoshua – Esta 12 Mashairi Ayubu Wimbo uliobora 5 Kinabii / manabii Isaya - malaki 17 Jumla ya vitabu vya agano la kale 39 Mtindo kiuandishi Majina ya vitabu Jumla Injili Mathayo – Luka 4 Historia Matendo ya Mitume Barua Warumi – Yuda Unabii Ufunuo wa Yohana Jumla ya vitabu agano jipya 27 UANDISHI WA BIBLIA YA KALE Wanadamu walianza kuandika kama mwaka 3200k.k. Kuandikwa kwa kwanza kulifanywa katika mabamba ya towe nyororo katika mawe na katika ngozi waliziunganisha ngozi na kuandika ngozi hizo ziliitwa “Parchment” kisha ngozi hizo baada ya kuziandika walizivingisha na kuitwa magombo “Scrolls’. Katika Biblia neno kuandika lilitajwa kwanza katika Kutoka 17:14 Mungu alipomwambia Musa kuandika mambo ya ushindi wa Israeli juu ya waamaleki kama mwaka 1440k.k BIBLIA NA MIAKA Zamani za kale watu hawakuandika tarehe na miaka kama tufanyavyo sasa hivi walikuwa wakitaja nyakati za wafalme wa zama zao wenyewe tu. Mfano katika Isaya 6:1 katika mwaka aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi kilicho juu sana na kuinuliwa na pindo la vazi lake vikalijaza hekalu.Luka 3:1-2 Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake kaisari Teberio Pontio Pilato alipoalipokuwa liwali wa Uyahudi na Herode Mfalme wa Galilaya na Filipo ndugu yake Mfalme wa Itulea na nchi ya Trakoniti Lisania Mfalme wa Abilene wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa.Neno la Mungu lilimjia Yohana mwana wa Zakaria jangwani.Hivi ndivyo ilivyokuwa katika nchi zote na nyakati zote za zamani hawakutaja miaka kama tunavyotaja sasa. Lakini iliandikwa hivi katika mwaka Fulani wa kutwala kwake Mfalme Sulemani. Hivyo wataalamu wa Biblia hufanya kazi ya kuchunguza na kuunganisha miaka na nyakati ya wafalme wanchi mbalimbali. Hii ni kutokana kwamba kila nchi ina hesabu yake yenyewe ya miaka. Hivyo wataalamu wa Biblia na Theologia hawakubaliani katika mambo yote kuhusu miaka, hivyo katika kutaja miaka tunatumia neno Kama kwa sababu hakuna anaejua mwaka kamili ila tunafanya makisio baada ya kufanya utafiti kwa kina. Kalenda tunayotumia sasa iligunduliwa na mtaalamu mmoja mtawa anaeitwa Dionysius Exiguus. Warumi walihesabu miaka tangu kujengwa kwa Rumi. Miaka kabla ya kuzaliwa kwa Kikristo huhesabiwa kwa kurudi nyuma toka kwa Yesu Kristo kurudi nyuma na inaitwa K.k Na B.c na baada ya kuzaliwa kwa Yesu huhesabiwa toka kwa Yesu kwenda mbele na inajulikana kama BK.AD. TAFSIRI ZA BIBLIA ZA ZAMANI SANA Kutokana na kufifia kwa lugha ya kiebrania mpaka kufikia mwaka 200 K.K na lugha hii kusahaulika na wengi na kutotumiwa na wengi ndipo ilibidi Agano la kale litafsiriwe katika lugha za mataifa mengi kama vile Kiaramu, Kisuria, Kigiriki, Kiarabu, Kimisri n.k. SEPTUAGINTI YA KIGIRIKI Mwaka 300 – 200 K.K. Agano la kale lilitafsiriwa kama lugha ya Kigiriki iliitwa Septuaginti. kwa sababu inasemekana ilitafsiriwa na watu 70. Septuagintu haiwezi kufaa kutumika kama asili ya kutafsiri Biblia tena katika lugha zingine kwa sababu tafsiri yake inajichanganya kunasehemu imetafsiriwa neno kwa neno na kupoteza mantiki{ maana} halisi na sehemu zingine hazifahaamiki vema. Ila inasaidia wataalamu wa Biblia na Theolojia kujua maana ya maneno ya kiebrania cha zamani zile. Septuaginti ilikuwa Biblia ya wakristo wa kwanza na ilisomwa siku za Bwana Yesu ilisaidia sana watu wengi kulielewa Neno la Mungu wale ambao hawakuweza kusoma kiebrania. TARGUMU ZA KIARAMU Ni Agano la kale ambalo lilitafsiriwa kwa kiaramu baada ya lugha ya kiebrania kupoteza mashiko na kufifia watu walianza kutafsiri maneno yake katika masinagogi ya wayahudi walisoma kwa kiebrania na mtumwingine alitafsiri kwa kiaramu. Baadae tafsiri hizo ndipo zilipoandikwa na kusomwa na zilipewa jina la Targumu lenye maana ya tafsiri kama Kiaramu. KISHAMU /KISURIA Ni tafsiri za Biblia ambazo zilitafsiriwa kwa lugha ya kishamu. Wakristo walipoongezeka katika nchi ya Shamu walihitaji kuwa na Biblia katika lugha yao ya kishamu na hivyo Biblia ilitafsiriwa kwa Kishamu. VULGALE ZA KITATIRI Ni Biblia iliyokuwa imetafsiriwa kwa kilatini. Mwaka 329 alizaliwa mtu mmoja aliyeitwa Jerome alikuwa ni mtaalamu alitafsiri Biblia nzima kwa lugha ya kirumi ambay o ni kilatini tafsiri hiyo iliitwa Vulgate. Vulgate ni tafsiri nzuri na imefwatwa na watu wengi katika kutafsiri maandiko. KASORO NDOGO NDOGO ZA KIUANDISHI Kabla ya kuangalia kasoro ndogo ndogo za kiuandishi zilizopo katika Biblia tuna budi kutambua namna ya uandishi uliotumika katika kuandika Biblia zamani za kale na hata vitabu vinginevyo vya kawaida. Ni vyema kutambua kwamba mashine za kuchapia vitabu hazikuwepo wakati wa kale mpaka mwaka wa 1450 BK ndipo zilipogunduliwa kwa hiyo kwa muda wa miaka 2730 watu walikuwa wakiandika kwa mkono katika mawe, ngozi, miti n.k. Hivyo kitabu kikichakaa ilipaswa kinakiliwe tena kwa herufi zote. Hivyo makosa machache yaliweza kujitokeza kutokana na zoezi la kunakiri toka kizazi hadi kizazi. Mfano no (i) 2 FAL 8:26 na 2 NYA 22:2 suruhisho 2FAL 8:17 Maandiko katika Biblia yalipangwa kwa sura kama mwaka wa 1250 BK na kardinali. Hugo na mistari iligawanywa kama 1550 BK na Sir Robert Stevens makosa hayo ni madogo na hayaleti kupingana kwa mantiki ya Maandiko Matakatifu. MAELEZO YA JUMLA YA BIBLIA Biblia ni kitabu kimoja kwanzia kitabu cha Mwanzo hadi kitabu cha Ufunuo. Ujumbe wa Biblia ni moja, yaani Kristo. Biblia yote inafundisha kuhusu jambo moja na hilo ni Kristo na kazi yake.Yaani ukombozi wa mwanadamu katika Kristo Yesu. Biblia yote ni neno la Mungu. Katika Biblia, Mungu anatufunulia kila kitu ambacho anataka tukijue kumhusu Yeye. Kwa hivyo kila neno ambalo limeandikiwa katika Biblia lafaa sana kwetu katika maagizo (Warumi 15:4). Chochote ambacho kimeandikwa katika Biblia, kimeandikwa kwa manufaa yetu, kwamba kupitia kwa Biblia ambayo ni neno la Mungu, tupate kuhimizwa katika tumaini la milele. Biblia inafundisha kwamba tangu zamani, mpango wa Mungu ni mmoja. Yaani, kusudi ni kwamba utakapowadia utimilifu wa wakati, katika Kristo atavileta pamoja vitu vyote, vile vya mbinguni na vile vya duniani. Kusudi lake katika kufanya hivyo ni kwamba, sisi tuliokuwa wa kwanza kuweka tumaini katika Kristo, tupate kuishi kwa sifa ya utukufu Wake Waefeso 1:12. Huu ni mpango ambao Mungu amekuwa nao tangu mwanza: Kumbukeni mambo yaliyopita yale ya zamani za kale Mimi ndimi Mungu wala hakuna mwingine Mimi ndimi Mungu wala hakuna mwingine aliye kaka Mimi. Ni Mimi tangazaye mwisho tangu mwanzo, naam, tangu zamani za kale, mambo ambayo hayatendeka. Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama, name nitatenda mapenzi yangu yote Isaya 46:9-10. Mpango huu ulikamilika. Tunasoma lakini ulipowadia utimilifu wa wakati Mungu alimtuma Mwanawe ambaye alizaliwa na mwanamke amezaliwa chini ya sharia kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, ili tupate kupokea zile haki kamili za kufanywa watoto wa Mungu Wagalatia 4:4-5. Kazi ya Kristo hapa ulimwenguni ndio kilele cha mpango wa Mungu katika historia yote. Msalaba wa Kristo na kusurdi kwa Kristo tena ndio mambo mawili ambayo yanakamilisha mpango huu wa Mungu. lakini kufuatana na ahadi yake, sisi tunatazamia kwa furaha mbingu mpya na dunia mpya, ambayio haki hukaa ndani yake 2 Petro 3:13. Kwa sababu mpango wa Mungu ni mmoja, Yeye alizungumza juu ya ahadi za mbeleni ambazo zilitimika katika Kuja kwa Kristo Yesu. Isaya 9:6-7 Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa. Tumepewa mtoto mwanamume nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. Kuongezeka kwa utawala wake na Amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi na juu ya ufalme wake akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu wakati huo n ahata milele. Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote atatimiza haya. Kuna hadi moja ambayo imebaki na hiyo pia itatimizwa, yaani kurudi kwa Kristo Yesu. YESU KRISTO KATIKA AGANO LA KALE Kwa sababu mpnago wa Mungu unamhusu Kristo na utukufu wake kwa sababu hii Agano la Kale lote linatuelekeza kwa Kristo. Biblia inasema kwamba kwa maana ahadi zote za Mungu zilizo katika Kristo ni ndiyo 2 Wakorintho 1:20. Yesu Kristo mwenyewe alifundisha kwamba Agano la Kale lote linafundisha kuhusu Yeye: Akawaambia,Haya ndio yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yalioandikwa kunihusu mimi katika Torati ya Musa, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.Luka 24:44. Ndipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko. Akawaambia.Haya ndio yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. Toba na msamaha wa dhambi utangazwe kutpitia kwa jina lake, kuanzia Yerusalemu. Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.Luka 24:45-48. Mungu mwenyewe aliwafungua macho ili waelewe maandiko .Luka 24:45. Agano la Kale lote linatuelekeza kwa ukamilishaji wa wokovu ambao ulifanyaka mara moja katika maisha kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo. AHADI ZA MUNGU Je, ni kwa njia gani ambapo Agano la Kale linatuelekeza kwa kristo Yesu? Kuna ahadi katika Agano la kale ambazo zinazungumzia kuja kwa Kristo Yesu akiwa Masia: Mika 5:2; Isaya 7:13-14, 9:6-7, 40:3-4, 53:1-4; Zaburi 45:6-7, 2:7, 22:1-21, 78:1-2; Yeremia 31:15; Hosea 11:2, Zakaria 9:19). Biblia yote inazungumza kumhusu tu Kristo Yesu. Agano la Kale na Agano Jipya yote yanatuelekeza kwa Kristo. VITABU VYA SHERIA KITABU CHA MWANZO UTANGULIZI Kwa miaka 2500, hadithi kumhusu Mungu zilielezwa kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine. Hii ilikuwa njia mzuri ya kutunza historia, na hadi leo kuna jamii ambazo zinatumia mtindo huu. Vitabu vitano vya kwanza vya Biblia, viliandikwa na Musa. Hivi ndivyo vitabu ambavyo vinajulikana kama vitabu vya Sheria. Kitabu cha mwanza kinazungumzia jinsi Mungu alivyoumba kila kitu na aliumba kila kitu kikiwa kizuri sana na bila dhambi yoyote. Taabu zote na shida zote katika ulimwengu huu zimetokana na dhambi ya Adamu na Hawa. Tangu dhambi ya kwanza ya Adamu na Hawa, mwanadamu ameendelea kutenda dhambi na kwa sababu hii hasira ya Mungu inawaka juu ya mwanadamu. Mungun huwa anaadhibu dhambi kwa vikali sana. Pia Biblia inafundisha kwamba baada tu ya Adamu kuanguka katika dhambi, Mungu alianza kazi ya kumwokoa Mwanadamu kutoka katika dhambi hiyo na kumrejesha katika ushirika Naye. Katika Mwanzo 12, Mungu alitangaza kwamba alikuwa anaenda kufanya kazi ya kumwokoa mwanadamu kupitia kwa uazo wa Abramu. Mwanzo 1-11, kuna mambo ambayo yalifanya katika miaka 2000 ya kwanza. 1. Kwanza, tuko na hadithi ya uumbaji wa kila kitu, Mwanzo 1:1. Katika sura ya 2, tunaelezewa umuhimu wa hadithi hii ya uumbaji wa kila kitu na Mungu. Swali ni je, kwa nini ni muhimu kuelewa hadithi hii? Ni kwa sababu ulimwengu unafundisha kwamba wanadamu tumetoka katika wanyama ambao ni Tumbili. Haya mafundisho ya ulimwengu ni ya uongo kabisa. A. Tunaposma msatari wa 1-13, tunaona kwamba Mungu aliumba kila kitu kwa urahisi sana. Hii inatusaidia kufahamu kwamba Mungu wetu ni Mungu mwenye nguvu zote. Ni lazima tumheshimu sana. Kuumba kwake kila kitu kunadhibitisha jinsi Yeye alivyo. Kwa mfano tunafahamu kwamba, Yeye anapenda vitu tofauti tofauti na pia anapenda vitu vizuri. B. Mwanzo 1:27, tunaosma kwamba mwanadamu aliumbwa katika mfano wa Mungu. Je, hii inamaanisha nini? Inamaansha kwamba tuko na uwezo kama Mungu katika mambo Fulani Fulani. Kwa mfano Mungu ametupatia akili ya kufanya mambo Fulani Fulani, tuko na hisia, tuko na mapenzi ya kufanya mambo fulani Fulani, na pia Mungu ametupatia uwezo wa kuchagua baya au zuri. Pia tuko na nafsi na mawazo ya kiroho ambayo inatuwezesha kuwa na uhusiano na Mungu. Mwanadamu si kama wanyama wengine ambao wanaongozwa na hisia tu. Mwanzo 1:26-30, inafundisha kwamba Adamu ndiye anafaa kuwa anatawala dunia yote. 1 Wakorintho 6:2-3,Je, hamjui kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Nanyi kama mtauhukumu ulimwengu, je, hamwezi kuamua mambo madogo madogo? Hamjui kwamba tutawahukumu malaika? Je, si Zaidi mambo ya maisha haya? Biblia inafundisha kwamba sisi si wanyama, sisi ni watawala kwa sababu tuko na uhusiani wa kipeke na Mungu. D. Kuna watu ambao huwa wanauliza, je, njia ya kupanga uzazi ni mbaya, kulinagana na Mwanzo 1:28? Hili swali ambalo wengi wanauliza hapa Afrika lakini katika nchi za ulaya na Marekani, hili swali halipo. Ninasema hivi kwa sababu nimesoma vitabu vingi, lakini huwa haivgusii swali hili la kujaza ulimwengu. Badala yake huwa waandishi wa vitabu hivyo wanasisitiza utawala wa mwanadamu juu ya dunia yote. Ni wao langu kwamba tunapaswa kufafanua jambo hili vyema kuanzia msatari wa 26 hadi 31. Kifungu hiki huwa kinatufundisha kwamba sisi wanadamu tumeumbwa kwa njia ya kipekee, yaani katika mfano wa Mungu. Kwa sababu ya hili, tumepewa jukumu la kutawala dunia na kuitanza. Wacha nizungumzie swala la kuujaza ulimwengu. Wakati amri hii ilitolewa, kulikuwepo na watu wawili pekee katika ulimwengu huu. Kwa sababu hii, dunia ilihitajika kujazwa na watu ili waweze kutawala dunia hii. Swali ni je, sasa kuna watu wakutosha katika dunia hii? Wacha tue wazo langu hapa. Mimi ninawaza kwamba sisi wanadamu tumetimiza amri hii ya Mungu ya kujaza dunia na kwamba kupanga uzazi si dhambi kwa sababu kuna watu wa kutosha katika ulimwengu huu. Zifuatazo ndizo sababu zangu ninasema kwamba kuna watu wa kutosha katika ulimwengu huu. 1. Idadi ya watu katika ulimwengu imeongezeka kutoka watu wawili hadi 7,000,000,000 leo. 2. Kuna watu wa kutosha leo katika dunia ambao wanapasw kutawala dunia. Tunao hili kwa sababu wanadamu ni wengi sana kuliko wanyama na sehemu nyingi za dunia zimeharibiwa na wanadamu na kwa hivyo wanyama au mimea hakuna ambacho kinaweza kuishi huko. 3. Sehemu nyingi za ulimwengu zinkumbwa na njaa na kiangazi kwa sababu kuna watu watu wengi sana leo kuliko katika sehemu hizo kuliko chakula. Ninajua si kazi yangu kusema ni watoto wangapi mtu anafaa kuwa nao, lakini nina amini kwamba Mungu anataka uwe na watoto wengi ambao utaweza kuwashughulikia katika maisha yao wote. Yaani unapaswa kuwapa chakula, mahali pa kuishi, mavazi, dawa, kuwa nao kama mzazi wao na masomo. Katika nchi za Ulaya na Amerika, familia nyingi ziko na watoto wawili kwa sababu zifuatazo. KUNA WATU WA KUTOSHA KATIKA NCHI HIZO. 1.Kuwalea watoto katika ncho hizo ni gharama kubwa ikilinganishwa na nchi zingine. Huwezi kuacha watoto wako bila kuwashughulikia. Wewe utalazimisha na serikali za huko uwashughulikia watoto wako au ufungwe. 2.Dini ukristo wa kweli inafundisha kwamba ni jukumu la wazazi kuwashughulikia watoto wao. Mpango wa uzazi ambao hauruhusu kuwepo kwa mbegu na mume na mke kukutana ili mtoto aanze kuumbwa si mbaya. Mpango wa uzazi ambao unamwua mtoto baada ya mbegu ya mke na mume kukutana ni dhambi. Mwanzo 1:31 inafundisha kwamba kiumbe kilikuwa kimekamilika kabisa. Je, ni kwa nini? Jibu ni kwamba dhambi haikuwa imeingia ulimwenguni. Mwanzo 2:1-3 Mungu aliweka siku ya Sabato kuwa siku takatifu ya kumpumzika. Hata leo tunapaswa kuzingatia siku hii na kuiheshimu. i.Tunahitaji siku moja ya kupumzika na kumwabudu Mungu. ii. Mungu alituumba na anatuptia siku moja ya kupumzika na kuwa na jamii zetu. Tutafanya kazi vyema sana ikiwa tutazingatia kupumzika siku moja katika jumaa. Mwanzo 2:4-25 Mungu anatueleza tena kuhusu kuumba kwake na wakati huu anatusisitizia umuhimu wa mwanadamu ambaye ndiye kilele cha uumbaji Wake. Mwanzo 2:15-17 tells inafundisha kwamba tunafaa kufanya kazi. Hata mbinguni tutakuwa na kazi ya kufanya. Mwanzo 2:23, inatufundisha kuhusu uhusiano wa mume na mke kupitia kwa kuumbwa kwa Hawa. Mstari wa 24, unafundisha kuhusu ndoa. Katika ndoa, mume na mke wanakuwa mwili mmoja. Kwa sababu hii, ni lazima tuheshimu wake wetu. Pia hii inatufundisha kwamba hatuwezi kamwe kutalakiana kwa sababu sisi ni mwili mmoja. Talaka ni kugawanyika. Mungu anachukia talaka Malaki 2:16. Jambo linguine la muhimu sana katika sura za kwanza za kitabu cha Mwanzo, kuanguka kwa Adamu katika dhambi. Mwanzo 3:1-7 dhambi inaingia katika ulimwengu. Adamu alikuwa na chagua la kuchagua kutii Mungu au kutomtii. Adamu alichagua kutomtii Mungu na kwa hivyo alianguka katika dhambi. Tangu wakati huo, hadi sasa mwanadamu huwa anachagua tu dhambi. Taabu zote za ulimwengu zinatokana na Adamu kukosa kumtii Mungu (Warumi 3:23; 6:23). B. Baada ya kutenda dhambi, Mungu alitangaza hapo na hapo hukumu kwa nyoka, kwa Adamu na Hawa na kwa kiumbe chote. Mwanzo 3:14-19, Warumi 8:19-23, vifungu hivi vinafundisha kwamba dhambi ni kitu kibaya na Mungu anahukumu dhambi yote. KUNA ADHAHABU MARA MBILI. 1,Kuna adhabu ya hapa ulimwenguni ambayo Mungu anayotoa kwa kila mtu awe mkristo au la. Kwa mfano, mtu anazini halfu anapata ugonjwa wa ukimwi. Mtu huyu ataumia sana na mwishowe atakufa. Kile nina maanisha hapa ni kwamba, mkristo akizini Mungu anaweza kumwadhibu kuruhusu apate ugonjwa mbaya sana kama ukimwi. Hivyo hivyo hata yule ambaye hajaokoka pia akizini, Mungu anaweza ruhusu pia apate ugonjwa huo huo. 1. Hukumu ya milele. a.Yule ambaye hajaokoa, yeye ataenda jahanum atakapokufa na atateseka milele kwa sababu ya dhambi zake. b.Yule ambaye ameokoka, dhambi zake zimelipiwa na Kristo, kwa hivyo akifa ataenda mbinguni. Yesu Kristo msalabani alikufia kila dhambi ambayo mkristo amewahi kufanya au atayaoifanya. C.Mwanzo 3:8-15 Mungu anaonyesha neema yake kwa mwanadamu kwa kutomwua hapo na hapo. Badala yake Mungu anaanza mpango wake wa kumwokoa mwanadamu. i. Katika mstari wa 8 na 9, Mungu anaanzisha kazi ya kumwokoa mwanadamu baada tu ya dhambi kuingia. Mungu anamtafuta mwanadamu ili arekebishe uhusiano wake na mwanadamu. Mstari wa 21, tunasoma kwamba Mungu aliua mnyama na akamtengeneea Adamu na Hawa nguo. Kuua ule mnyama na kuwavisha Adamu na hawa ilionyesha kwamba: a.Mwanadamu lazima avalishwa ikiwa atasimama mbele za Mungu mtakatifu. b. mwanadamu kwa nguvu zake, hawezi akajiwezesha kukubalika na Mungu. Ni Mungu mwenyewe ambaye anaweza kumfanya mwanadamu akubalike mbele zake. c. Mungu ndiye ataweza kuleta kile ambacho kinakubalika mbele zake. d. Mungu alimwua mnyama ambaye alikuwa hajafanya lolote baya, kuonyesha kwamba ni lazima kuwe na umwagaji damu, ikiwa mwanadamu atarudi paradiso. Umwagaji huu wa damu ya mnyama, ulikuwa unatuelekeza kwa kuja kwa Kristo ambaye ndiye sadaka ambayo imekamilika. Mwanzo 3:15, Mungu anaahidi kushindwa kwa shetani. Ni mstari muhimu sana kwa sababu ndani mwake Mungu anaahidi kushindwa kwa shetani na Yesu Kristo. a. Kugongwa kisigino, inamaanisha kwamba shetani angemwumiza Kristo na hili lilifanyika kwa msalaba. Msalabani, Kristo Yesu aliumizwa kwa ajili ya dhambi zote za kila mkristo. b. Kuponda kichwa inamaanisha kwamba Yesu Kristo angemwangamiza shetani na hili pia lilitimika msalabani. Msalabani, Kristo Yesu alimshinda vita shetani. D. Mwanzo 4, tunasoma kuwahusu kaini na Abeli ambao ndio walikuwa wazaliwa wa kwanza wa Adamu na Hawa. Tuansoma kuhusu kaini akimwua nduguye Abeli. Dhambi sasa inadhihirika katika maisha ya kizazi cha Adamu. Wanadamu wote waliendelea kutenda dhambi na tunaposoma biblia tunaona kwamba mwanadamu hawezi kamwe kuishi maisha yake kwa njia ambayo inamfurahisha Mungu, na kwa hivyo Mungu anamwadhibu vikali sana. 3. Tukio lingine katika sura 11 za kwanza za Mwanzo ni Garika. Mwanzo 6-9, inasimlia hadithi ya Nuhu na garika. A. Dhambi iliendelea kuenea katika ulimwengu na Mungu alikasirika na wanadamu na akasema kwamba atakiangamiza kizazi cha mwanadamu. Mwanzo 6:5-7, Mungu anazungumza kuhusu jinsi alivyohuzunishwa na uovu wa mwanadamu. B. Katika mstari wa 8, tunaona kwamba ni Nuhu pekee ambaye alipata kibali machoni pa Mungu. Kwanzia mstari wa 13-14, Mungu alizungumza na Nuhu na kumwambia kwamba ajenge safina ili kwamba yeye na jamii yake wapate kuokolewa kutoka kwa garika wakati ulimwengu wote utaangamizwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zao. C. Hadithi ya garika inatufundisha kwamba, dhambi huwa inaendelea kuzidi kila wakati ahadi Mungu atakapodhihirisha hukumu juu ya dhambi hiyo. Tunaona kwamba Mungu ni mvumilivu sana na watu lakini uvumilivu wake si wa milele kwa wale wote ambao wanakata kutubu. Yeye atawahukumu wote ambao wanakataa kutubu. i. Mwanzo 6:22, tunasoma kwamba Nuhu alitii Mungu. Waebrania 11:7, inatufundisha kwamba ni kwa Imani Nuhu aliokolewa kama tu vile wakristo wote wanavyookolewa kupitia kwa Imani. 4. Mwanadamu ameendela kuetenda dhambi. Mwanzo 11, tunasoma hadithi ya mnara wa babeli. Watu walikuja pamoja na wakapanga kutomtii Mungu. Wao waliujenga mnara kwa sababu ya kiburi chao na kukosa kumtii Mungu ambaye alikuwa amewamru kujaza dunia (Mwanzo 9:1). A. Mungu aliwapatia luga mpya wote na kwa hivyo hawakuweza kueelewa katika kazi yao ya kuujenga mnara. Kwa sababu hiyo walitanyika na kusambaa dunia yote. II. Kitabu cha Mwanzo katika sura zingine, kinatuelezea jinsi Mungu alivyowatumia watu wane; yaani Abrahamu, Isaki na Yakobo ambao wanajulika kama kina baba wa taifa la Wayahudi. 1.Kwanza alikuwa Abramu ambaye baadaye aliitwa Abrahamu. Abramu aliitwa hivi hadi kuzaliwa kwa Isaki. Yeye ndiye baba wa taifa la Wayahudi. A.Mwanzo 12:1-4, tunasoma kumhusu Abramu akiitwa na Mungu. Je, Abramu alikuwa mtu mwema ndipo Mungu akamwita? Jibu ni la. Abramu alikuwa mwenye kuabudu sanamu. Napia tunasoma kwa mara mbili alidanganya kuhusu mke wake kwa sababu aliongopa kuuliwa. Hii inatuonyesha jinsi Mungu alivyo mwenye huruma kwa wenye dhambi. Pia tunasoma kwamba, Abramu kwa Imani aliacha nyumba ya baba wake na kumfuata Mungu. Abrahamu pia anaelezwa kuwa mtu mwenye Imani (Waebrania 11:8-19). i.Mwanzo 12:1-3, Mungu aliweka agano na Abramu. Hii ni mistari mizuri ya kukumbuka. Mungu aliweka Agano hili kati yake na Abramu na kutangaza jinsi aatakavyofanya ili kumwokoa mwanadamu. Mungu anahidi kwamba atafanya kazi kupitia kwa Abramu na kizazi chake. Mungu aliwatenga Waisraeli au Wayahudi kuwa watu wake ambao agewatumia kukamilisha mpango wake. B. Mwanzo 15:1-21 Kwa damu, Mungu aliweka mhuri juu ya Agano hili na Abramu. Hii ilifanya Agano hilo liwe la hakika. Agano ni makubaliano kati ya Mungu na mwanadamu. Agano nyingi huwa ni ahadi kutoka kwa Mungu. Pia kuna Agano zingine ambazo mwanadamu huwa anahitajika kujukumika. Aina ya Agano hili ni kama Agano la Kutahiriwa katika Mwanzo 17. i. Mwanzo 15:4 Abramu aliahidiwa mtoto, lakini hata kama yeye ni mtu mwenye Imani, yeye alikuwa na shaka. Abramu aliwaza kwamba yeye ni mke wake walikuwa wamezeeka sana na kupata mtoto lilikuwa jambo gumu sana kufanyika kwao. Hapa tunajifundisha kwamba kuna walati Imani yetu inakuwa dhaifu na wakati mwingine inakuwa dhabiti. C. Mwanzo 16 tunasoma kuhusu jinsi Abramu na mke wake walipanga njia nyingine ya kupata mtoto. Abramu alipata mtoto na mfanya kazi wake Hagai. Mtoto aliitwa Ishamaeli.hata kama Waebrania 11:8 inaeleza kuhusu Abramu kwamba ni mtu wa Imani, kama mkristo yeyote, kuna wakati alikuwa na imani dhaifu. Ishamaeli alizaliwa nay eye ndiye baba wa mataifa ya Kiarabu ambayo ni maadui wakuwa wa taifa la Israeli. Kwa sababu ya kutoamini kwa Abramu, adui mkubwa wa azaliwe. D.Mwanzao 17:5, Abramu akiwa na miaka 99, jina lake lilibadilishwa na akaitwa Abrahamu kwa sababu Mungu alikuwa amemwahidi mtoto ambaye angemrithi. Mungu pia alikuwa amweahidi kwamba yeye atakuwa baba wa mataifa. Mke wake Sarai pia alibadilishwa jina na kuitwa Sarah. Jina hili lilimaanisha mama wa mataifa. Mstari wa 9-14, tunasoma kuhusu Agano la kutahiriwa, ambapo Waebrania walitengwa kutoka maitaifa yote ya ulimwengu kuwa wana wa Mungu. Kutahiriwa ilikuwa ishara kwa Mungu amewatenga Waebrania kutoka miongoni mwa watu wa mataifa mengine kama tu vile ubatizo ni ishara kwamba wakristo wamekufa kwa dhambi na sasa wako haia katika Kristo Yesu. Agani jipya linafundisha kwamba hata kama wakristo tunaishi katika ulimwengu huu, sisi si wa ulimwengu huu. Nyumbani mwetu ni mbinguni mahali ambapo Mungu yupo (Yohana 17:14-16 na 18:36). E.Mwanzo 18-19, tunasoma kuhusu miji ya Sodoma na Gomora. Hadithi hii inatufundishi juu ya uovu wa mwanadamu na jinsi hukumu ya Mungu itakavyokuwa kali sana kwa wote ambao wanakataa kutubu. i.Mwanzo 18:1-15, tunasoma kuhusu wageni ambao walimtembelea Abrahamu. Katika mstari wa 3, Abrahamu alitambua kwamba ni Mungu ambaye alikuwa anamtembelea. Abrahamu aliwashughulikia wageni wake, na pia alifahamishwa kwamba mwaka ambao ulikuwa unafuata yeye alikuwa awe baba. Sara aliposikia haya, yeye alicheka sana. Katika mstari wa 14, tunasoma, @Je, kuna jambo lo lote gumu lilowezekana kwa Bwana? Katika Luka 1:34-38, swali hili lijabiwa vyema kabisa. ii.Katika Mwanzo 18:20, Mungu alionyesha kutofurahia kwake juu ya uovu wa watu wa Sodoma na Gomora kama tu vile ilivyokuwa katika Mwanzo 6:5. Katika mstari wa 21, Mungu anaema kwamba watu hawa wanastahili kuangamizwa. Dhambi zao zilikuwa nyingi mno, lakini pia, walijihusisha na dhambi ya ushoga ambayo ilikasirisha Mungu kabisa. Dhambi hii huwa inakeuka mpango mzuri wa Mungu wa ndoa katik mume mmoja na mke mmoja. a.Mstari wa 22-33 tunasoma jinsi Abrahamu akibishana na Mungu juu ya swala Sodoma na Gomora. Tunajifundisha hapa kwamba kuna wakati ambapo tunaweza kubishana na Mungu, lakini iwe tunafanya hivyo kwa njia ya heshima kulingana na neno Lake. Hapa tunaona kwamba Abrahamu hakuwa anabishana kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe. Bali ilikuwa kwa ajili ya kuwalinda wale ambao walikuwa wenye haki katika miji ya Sodoma na Gomora. Msingi wa ubishi wa Abrahamu ulikuwa haki ya Mungu. b.Mwanzo 19, tunasoma jinsi Mungu aliingamiza miji hiyi miwili kwa sababu ya uovu wa miji hiyo. Katika miji hiii, Mungu alimwokoa tu Lutu. Tunasoma kwamba hukumu ya miji hii ilikuwa kali sana kwani Mungu aliinyeshea moto wa kiberiti.Mwanzo 19:24. c.Pia tunsoma kwamba hata jamii ya Lutu iliadhibiwa kwa sababu ya kutotii. Wao waliambiwa kwamba wasitazame nyumba, lakini mke wa Lutu alikosa kutii na kwa hivyo yeye aligeuka na kuwa nguzo la chumvi Mwanzo 19:17 na 26. d. Mwanzo 19:30-38, tunasoma kuhusu jambo la aibu sana ambalo lilifanyika kati ya Luti na wasichana wake wawili. Ni hadithi ambayo inaeleza jinsi wasichana wa Lutu hawakumwamini Mungu, na kwa hivyo walimlewesha baba yao Lutu na wakafanya mapenzi naye ili waweze kupata watoto. Wote wawili walipata watoto aambao baadaye walikuwa mataifa mawili; Moabu na Ammoni. Mataifa haya mawili yalikuwa maadui wakubwa wa Wayahudi. f. Mwanzo 20, tunasoma kuhusu umuhimu wa mamobi kwa Mungu. Tunasoma juu ya udanganyifu wa Abrahamu wakati alimpeana mke wake kwa Abimeleki. Lakini kabla ya Abimeleki kufanya mapenzi na Sarah, Mungu alimwonya na kumwambia kwamba atakufa asipomwambia Abrahamu amwombee. Mungu lihitaji Abrahamu aombe kabla ya kufanya lolote juu ya maisha ya Abimeleki. Hii ni hadithi ambayo inatuonyesha ukuu wa Mungu na nguvu na umuhimu wa maombi. g. Mwazno 21, tunasoma kwamba mwana ambaye aliahidiwa Abrahamu, yaani Isaki anazaliwa. H. Pia tunaona ni kwa nini Abrahamu anaitwa mtu wa Imani. Yeye alimtii Mungu na alikuwa tayari kumtoa mwanawe kama sadaka kwa Mungu. Pia tunaona kwamba Mungu alileta mwana-kondoo ambaye Abrahamu alimtoa kama sadaka badala ya Isaki. Hii inatuongozwa kwa Kristo Yesu ambaye Mungu alimtoa kama mwana-kondo we sadaka kwa ajili ya dhambi zetu. i. Mwazno 24, hatuambiwi lolote Zaidi kuhusu Isaki isipokuwa kwamba yeye alikuwa baba ya Yakobo. Abrahamu alimtuma mtumishi wake arudi katika taifa lao na huku akamtafutie Isaki mke ili Isaki asimwoe mwanamke kutoka katika nchi ya kigeni. Baada ye tunaona jinsi wanawake wan chi za kigeni waliwaletea watu wa Mungu taabu nyingi sana. Abrahamu alijua mapenzi ya Mungu na kwa hivyo yeye alifata mapenzi hayo. Je, tunajuaje mapenzi ya Mungu? Tunajua mapenzi ya Mungu kupitia kwa Biblia. Tuombe kwamba Mungu atatufundisha neno lake kila wakati tunapolisoma. j. Mwanzo 25 tunasoma kuhusu kifo cha Abrahamu na kuzaliwa kwa mapacha wa Isaki. Jina Yakobo linamaanisha mwogo. Yakobo ndiye alikuwa mdogo, lakini yeye alimdanganya Esau na kuchua haki yake ya kuwa mazaliwa wa kwanza na pia alimdanganya Baba yake Isaki na kuchukua Baraka zote ambazo zilikuwa za Esau. Yakobo hakuhitaji kumdanganya Esau kwa sababu tayari Mungu alikuwa amemchagua yeye na wala si Esau (Mwazno 25:23). Katika Warumi 9:10-13 tunasoma kwamba Mungu anatawala kila kitu na anamchagua yule ambaye anataka kumchagua. 2. Baba wa pili wa taifa la Wayahudi.Isaka Mwanzo 26:2-4, Mungu anaahidi Isaki kile ambacho alikuwa ameahidi Abrahamu. Hili kumbusho kwamba ahadi hiyi bado Mungu alikuwa anaizingatia sana. Baba wa tatu wa taifla la Wayahudi ni Yakobo. Tunajua Yakobo ni mtu wa aina gani kulingana na jina lake. Yeye alikuwa mwongo. Yeye alikuwa na watoto 12 ambao walifanya makabila ya Israeli. Mwanzo 28 tunaosma kwamba Yakobo alikimbilia Padani Aramu kwa sababu alikuwa anmwogopa Esau kwa sababu alikuwa amechukua Baraka zake zote. Mwanzo 27:41-42, tunasoma kwamba Esau alitaka kumwua Yakobo. Yakobo alikuwa mwongo, lakini mjomba wake Labani alikuwa mwongo Zaidi. Alimdanganya Yakobo mara kadhaa. Yakobo alipokuwa anataoroka Esau, yeye alikuwa mtu ambaye aliogopa kwa sababu alikuwa anaenda kwa nchi ngeni sana kwake. Mwanzo 28:10-19, tunaosma jinsi Mungu alikuja kwake na kumfariji. Hata kama inaonekana kwamba Yakobo alikuwa peke yake huku jangwani, ukweli ni kwamba Mungu alikuwa pamoja naye. Mathayo 28:20, inatufundisha kwamba Mungu huwa pamoja na wale ambao wameokoka kila wakati. Yakobo alikuwa amekulia katika jamii tajiri, lakini sana alikuwa pakee yake na hakuwa na mali yoyote. Lakini Mungu alimfariji. Katika mistari ya 13-15, Mungu alirudia ile ahadi ambayo alikuwa amempa Abrahamu kwa Yakobo. Mungu alimwambia yakobo kwamba yeye ndiye alikuwa mrithi wa ahadi hiyo. Alimhakikisha Yakobo kwamba kila kitu kitakuwa sawa na kwamba yeye ataishi na siku moja atarudi katika nchi ambayo Mungu aliahidi Abrahamu na warithi wake. Mungu alimhakikishia Yakobo kwamba, yeye pia atakuwa na jamii. Mwanzo 29, tunasoma jinsi Yakobo alikutana na kupenda Raheli. Yakobo alikubali kumfanyia kazi mjomba wake kwa miaka saba ili ampate Raheli kama mke wake. Tunasoma jinsi Labani alivyomdanganya Yakobo na akamletea Lea badala ya Raheli. Je, jambo hili lilifanya aje? Ilimbidi Yakobo afanye kazi kwa mwaka mingine 7 ndipo ampate Raheli. Baada ye Yakobo alikuwa na taabu nyingi kwa sababu ya kuwaoa wake wawili. Mwanzo 31:1-55 tunasoma kuhusu safari ya Yakobo ya kurudi nyumba baada ya zaid miaka 25. Katika mistari ya 1-3, tunaona kwamba sasa wakati wa Yakobo kurudi nyumbani ulikuwa umefika. Jambo kuu katika safari hii, ni wakati ambapo alikutana na Mungu Mwanzo 32:22-28. Yakobo aliogopa sana alikutana na Mungu na Biblia inasema kwamba alikuwa peke yake. Mara kwa mara hadi mtu anapokuwa katika hali ya Yakobo, ndipo atahisi kwamba kweli anamhitaji Mungu. Yakobo kwa usiku wote alipigana mweleka na Mungu na baadaye Yakobo alijinyenye keza kwa Mungu. KIukutana huku na Mungu kulibadilisha maisha ya Yakobo kabisa kama vile mtu anavyokuja kwa Mungu na kuokolewa na kufanya kiumbe kipya. Tunaona jina la Yakobo likibadilishwa kutoka kwa Yakobo mwongo, kwa Israeli. Yeye alikuwa baba wa makabila 12 ya Israeli. Tunaweza kulinganisha mabadiliko haya kwa kuzaliwa mara ya pili. Yakobo amebadilishwa na kupewa jina mpya kuonyesha kwamba sasa Yakobo si yule mwongo tena. Maisha ya Yakobo ya baadaye yalifanywa magumu na watoto wake. Tunajifunza hapa kwamba Mungu huwaokoa na kuwatumia wenye dhambi wa kila aina. Mwanzo 34 tunasoma jinsi Dina binti wa Yakobo alivyonajisiwa na Shekemu. Shekemu alitaka kumwoa Dina lakini jambo hili liliktaliwa kwa sababu Waisraeli wangepolea miongoni mwa watu hawa Washekemu na ingemaanisha kwamba huu ndio ungemwisho wa Waisraeli ambao ndani mwake Mungu alikuwa amepanga kuleta wokovu katika ulimwengu. Yakobo alilipiza kisasi na kuangamiza mji wa Sechemu na watu wake wote. Mwazo 38, tunasoma kuhusu mambo mabaya kumhusu Yuda mmoja wa watoto wa yakobo na jamii yake. Yuda alikuwa mwovu sana na ni ktuoak katika kabila hili, Yesu Kristo anazaliwa. Pia hapa tunafundishwa kwamba Mungu anaweza kumwokoa na kumtumia mtu yeyote haijalishi yeye ni mwovu kiwango gani. Mwanzo 38:1-5, tunasoma kwamba Yuda alienda akawa rafiki na mwamume mkanani na akamwoa mmoja wa wanawake wakanani. Mwanzo 38:5-10 tunasoma kuhusu kifo Cha Onani ambaye mwana wa Yuda amabye alikosa kumtii Mungu na aliadhibiwa kuwa kuuliwa. Iii. Mstari wa 11-26 tunasoma kuhusu hadithi ya Huzni ya Tamari ambaye alikuwa mkwe wa Yuda. Wakati mume wake alikufa, Yuda alikuwa na jukumu la kuhakikisha kwamba anampa mume mwingine kutoka miongoni mwa watoto wake. Lakini Yuda hakufanya hivyo. Kwa hivyo Tamari alimdanya Yuda na akalala naye na kuwa mjaa mzito. Kwa hasira, Yuda alipanga kuwua Tamari hata ni yeye alikuwa wakulaumiwa. Tunajifundisha kwamba watu wanaweza kuwa waovu san ahata kama wao ni wa kizazi cha Kristo. Je, ni kwa nini Tamara awawe na si Yuda? 1. Baba wa mwisho wa Wayahudi ni Yusufu Yusufu alikuwa mtu tofauti kabisa kwa sababu katika maisha yake hutusomi kuhusu kashifa yoyote. Mwazno 37, tunasoma kuhusu hadithi ya Yusufu na jinsi Mungu alivyotengeza njia kwa watu wake kuishi Misri. Yusufiu alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Raheli ambaye alikuwa tasi kwa miaka mingi sana wakati dadake Lea alikuwa na uwezo wa kupata watot. Kumbuka kwamba Raheli ndiye alikuwa anpenddwa sana na Yakobo na Yusufu mtoto wake pia alipenda sana na Yakobo na kila mtu alifahamu jambo hili. Yusuf alikuwa na miaka 17, wakati hadithi hii inaanza. Mwanzo 37:5-11 tunasoma kuhusu Yusufu akimweleza babake ndoto mbili ambazo zilihusu watu wa jamii yake wakimwinamia na kuheshimu. Jambo hili lilikasirisha jamii yake san ahata kama baadaye jambo hili lilitimika. Jambo hili lilimfanya Yusufu achukiwe na ndugu zake. Mwanzo 37:28, tunasoma kwamba ndugu zake walimwuza kama mtumwa kwa Waishimali ambao walimpeleka Misri. Kupitia kwa haya, Mungu alikuwa anatengeneza njia ya watu wake kwenda Misri ambapo wangeishi hadi wakati walipokuwa tayari kuchua nchi ya ahadi. Mwanzo 39:1 tunasoma kwamba Mungu alimbariki Yusufu sana. Kwa sababu ya kazi ya nzuri, Yusufu aliuzwa kwa Potifa ambaye alikuwa mkuu katika serikali ya Misri. Yusufu alikuwa mwaminifu sana kwa Mungu na mUngu akambariki sana na Yusufu alifanywa mkuu katika nyumba ya Potifa. Mke wa Potifa alijaribu kumtongoza Yusufu, lakini Yusufu alikataa na kwa sababu hiyo, mke wa Potifa alimsingizia kwamba Yusufu alikuwa anamtaka. Yusufu alifungwa gerezani na pia huko Mungu alimbariki sana na akafanywa kuwa kiongozi ndani ya gerazani. Mwanzo 40 tunasoma tunaona mpango ambao Mungu alikuwa nao katika maisha ya Yusufu wakati alipomwacha afungwe kwa geraza. Huko gerezani, Yusufu alikutana na Mnyweshaji wa Farao ambaye alikuwa amfungwa kwa muda mfupi. Yusufu alitafsiri ndoto ya huyu Mnyweshaji ambaye aliregeshewa cheo chake katika nyumba ya mfalme. Baadaye katika hadithi hii tutaona jinsi Mungu alitumia njia hii kuwaleta watu wake Misri. Mwanzo 40:14 tunasoma kuhusu Yusufu akimweleza yule Mnyweshaji kwamba asimsahau wakati atakapotoka kwa gerezani. Katika mstari 23, tunaojna jinsi watu wengi huwa hawa shukurani, kwani yule mnyweshaji alimsahau Yusufu. Mwanzo 41 tunsoma kwamba baada yam waka miwili, farao alikuwa na ndoto ambayo hakuna mtu ambaye angeitafsiri. Mnyweshaji alikubuka kwmab Yusufu alikuwa na uwezo wa kutafsiri ndoto kwa hivyo alimwambia Farao ambaye alitoa gerezani ilia je kumtafsiria ndoto yake. Mwanzo 41:17-24 Farao alimweleza Yusufu ndano yake. Katika mstari wa 25-36 Mungu alitukuzwa wakati Yusufu alitafsiri ndoto na kutabiri juu ya kiangazi na kumpa farao ushauri jnis ilimpasa kufanya ili watu wake wasife kwa njaa na pia kwa njia hii Farao alikuwa atajirike sana. Mistari ya 37-41 tunasoma kuhusu Yusufu akupewa mamlaka ya juu sana. Yeye alikuwa kiongozi wa pili kutoka kwa mfalme Farao. Sasa Yusufu alikuwa na mamlaka ya kuwasaidia watu wake. Mwanzo 42 tunasoma kwamba kulikuwa na kianganza ambacho kiliwalazimisha ndugu za Yusufu kutafuta usaidizi Misri. Baadaye Yusufu alijidhihirisha kwa ndugu zake na jamii yake yote ikihamia Misri. Hii ilikuwa timizo kwa sehemu moja ya ahadi ya Mungu katika Mwanzo 15:13-14. Mwazno 50, baada ya Ykovbo kufa, ndugu za Yusufu waliogopa kwamba Yusufu angeliiza kisasi. Lakini katika msitari ya 4-21, Yusufu alidhihirisha ucha Mungu wake kwa ndugu zake na kuwahimiza kwamba yeye hakuwa na nia ya kuwaumiza. Katika mstari wa 20, Maneno ya Yusufu yanaambata nay ale ya Paulo katika Warumi 8:28. Hii ni mistari ya faraja sana kwa watu wote wa Mungu wakati tuko katika hali ngumu au wakati watu wanatuumiza. Mwanzo 50:25 Yusufu anawaeleza Ndugu zake kwamba watakapoondoka Misri, waondoke na mifupa yake na waizike katika nchi ya ahadi. Kitabu cha Mwanzo kinamalizika Israeli akiwa Misri mahali ambapo Mungu alimtaka awe kwa wakti huo. MAFUDNDISHO YA KITABU CHA MWANZO KWA UFUPI. Katika kitabu cha Mwanzo, Ulimwengu unaumbwa ukiwa katika hali ya ukamilifu. Baadaye mwanadamu atenda dhambi na dhambi inaingia katika ulimwengu. Wakati mwanadmu mmoja alipotenda dhambi, wanadamu wote wameendelea kutenda dhambi. Mara kwa mara tunaona kwamba Mungu ni Mungu ambaye anahukumu na anaadhibu dhambi. Wakati Fulani tunaona watu wakihukumiwa vibaya sana kama Onani. Wakati Nuhu tunaona kwamba ni Nuhu peke yake ambaye alihurumiwa na wengi wote walihukumiwa. Baada tu ya Adamu na Hawa kuanguka dhambi, Mungu alianzisha mpango wa wokovu kupitia kwa Kristo Yesu na tunaona mpango huu ukifunuliwa. Mungu aliwachagua waisraeli kuwa watu ambao angewatumia kuleta wokovu katika ulimwengu. Katika kitabu cha Mwanzo tunaona mpnago huu wa wokovu wa Mungu. Pia tunaona kwamba mwanadamu kwa asili yake hawezi kamwe kujiokoa. Katika Agano la Kale lote Mungu anaonyesha jinsi anavyotekeleza mpango huu kupitia watu Fulani na hali Fulani Fulani na kutayarisha kuja kwa Kristo. KITABU CHA KUTOKA Kitabu cha Kutoka kina sehemu mbili muhimu sana. Sura ya 1-18, ni hadithi kuhusu jinsi Mungu alivyowakomboa Waebrania kutoka katika utumwa huko Misri. Huu ni mfano wwa Kristo Yesu ambaye ametukomboa leo kutoka katika utumwa wa dhambi na shetani. Sehemu ya pili inahusu jinsi Mungu alianza kuwafundisha watu wake jinsi walipaswa kuishi maisha yao tofauti kabisa na watu wa mataifa mengine kwa sababu sasa wao walikuwa watu wa Mungu. Leo pia watu wa Mungu wanapaswa kuishi maisha yao tofauti kabisa, yaani maisha yao yanapaswa kuwa maisha matakatifu. Katika kitabu hiki, Mungu aliwapatia watu wake amri kumi kuwaonyesha jinsi walipaswa kumwabudu. Musa ni wapo wa Manabii katika Biblia ambao Mungu aliwatumia sana kuwaongoza watu wake. Musa aliandika vitabu vitano vya kwanza na Zaburi 90. Musa aliishi miaka 120 na kwa miaka hii yote, Mungu aliishi maisha yake kabiru sana na Mungu. Lakini pia tunapaswa kukumbuka kwamba kama mkristo yeyote, Musa hakuwa amekamilika. Yeye kwa sababu ya dhambi yake ya asira, Musa hakuingia Kanani, nchi ya ahadi. Hadithi za kitabu cha Kutoka ni za miaka 430 baada ya hadithi za kitabu cha Mwanzo. Mungu anatawala kila jambo na sasa ulikuwa umewadia wakati ambapo alikuwa amemwaahidi Abrahamu kwamba kiziza chake kitaichukua nchi ya Kanani. Ukweli ni kwamba hatujui kabisa ni kwa nini Waebrania walimaliza miaka 430 katika utumwa huko Misri. Huenda sababu moja ni kwamba walikuwa watambulike kama taifa. Sababu nyingi inaweza kuwa kwamba walikuwa kwanza waongezeka katika idadi ili wawe na uwezo na nguvu za kupigana na maitafa memngine ndipo waichukue nchi ya Kanani. Kutoka 1:1-2:10, Tunasoma kuhusu kuzaliowa na maisha ya utotoni ya Musa. Wakati Yusufu alipokuwa hai, Wayahudi walipendwa na Farao ambaye alikuwepo wakati huo, lakini baada ya kifo cha huyu Farao na Yusfu, Farao aliyefuata pamajo na viongozi wake, waliwachukia sana Waebrania na wakapanga kuwaua. Maisha ya Waebrania yalikuwa magumu sana na huu ndio wakati Mungu alikuwa amepanga kwamba waondoke humo Misri na waende waichukua nchi ya Kanani. Mistari ya\ 11-14, tunasoma jinsi wamisri walivyo wanyanyasa Waebrania. Katika mistari ya 15-22, tunasoma kuhusu Farao akiamuru kwamba watoto vijana wote ambao walizaliwa na Waebrania wawawe. Jambo hili lilitokie miaka 1500 baadaye wakati Yesu alipozaliwa. Sura ya 2:1-10, tunasoma jinsi Musa alivyokolewa kutokana na kifo na kulelewa nab inti ya Farao. Mungu alipanga kwamba hata wakati MJusa alichukuliwa na Binti ya Farao, ni mama mazazi wa Musa ambaye alichukuliwa na kumtunza Musa. Wakati alikuwa anamtunza Mungu, alikuwa analipwa kwa kazi hii Musa alilelewa na kufundishwa katika nyumba ya Farao. Mwaka 40 ya kwanza ya Musa, aliimazliza katika nyumba ya Farao akiwa katika jaii ya kifalme. Sura 2:11-15, tunasoma kuhusu jinsi Musa alivyomwua Mmsiri. Musa alifahamu kwamba yeye alikuwa Mhebrania, na kwa hivyo alikasirishwa sana na jinsi Wamisiri walivyokuwa wakiwashughulikia Waebrania. Alipoona jinsi Mmisiri mmoja alivyokuwa ana mpiga Mhebrania, alikasirika sana na alimwua yule Mmsiri. Kwa sababu hii, Musa alitorokea Midiani (sasa nchi ya Saudi Arabia) kwa sababu aliogopea maisha yake. Alipokuwa kuwa huko Midiani, Musa alimwoa Zipora ambaye alikuwa binti wa Jethro na aliishi huko kwa miaka mingi sana. Wakati huo huo, Waebrania waliendelea kuteseka katika mikono ya Wamisri. Sura ya 2:16-4:17, tunasoma kuhusu miaka 40 za Musa akiishi katika jangwa. Sura ya 3:1-6, Musa alikutana na Mungu. Mungu alikutana na Musa kwa njia ambayo ilimwezesha Musa kutambua kwamba huyu alikuwa ni Mungu. Mbeleni jambo hili liliwanyikia Abrahamu na Yakobo. Biblia inafundisha kwamba Mungu ni Roho nay eye haonekani kwa macho ya kiasili (Wakolosai 1:15). Wale ambao Mungu alikuwa amewachagua kuwatumia, Yeye alikutana nao kwa njia ambayo wanadamu wangestahimili katika hali yao ya upungufu ambayo imesababishwa na dhambi. Katika mistari ya 7-10, Mungu alimwita Musa ili awaongoze watu wake kutoka katika nchi ya Misri hadi katika ncho ya ahadu ambayo ni Kanani. Katika mstari wa 11, tunasoma kuhusu jinis Musa alivyojitetea kwa sababu hakutaka kuenda Misri. Atika Isaya 6:8, tunaosma kuhusu majibu ambayo kila mkristo anapswa kuwa nayo wakati Mungu amemwita kufanya kazi Fulani. Ktia sura 3, tunasoma kuhusu mazungumzo katika Mungu na Musa juu ya kazi ambayo Mungu alikuwa anataka Musa ifanye. Mungu alitaka Musa arudi Misri na awaongoze watu wake kutoka katika utumwa huo. Katika sura ya 3:21-22, tunasoma kuhusu Mungu akiikumbuka ahadi ambayo alikuwa nayo kati yake na Abrahamu (Mwanzo 15:14). Ahadi hii ilihusu kwamba Waebrania wangetoka Misri na utajiri mwingi sana. Katika sura ya 4, mazungumzo yaliendelea na Mungu alikasirishwa na ubishi wa Musa na kwa hivyo aliweka Aroni awe msdemaji wa Musa. Hii intuonya kwamba lazima tuwe waangalifu sana wakati tunaanza ubishi na Mungu. Katika mstari wa 18, tunasoma kuhusu Musa akirudi Misri na kuwaeleza Waebrania kwamba Mungu alikuwa anaenda kuwakomboa ktuoka katika utumwa wao. Watu walifurahia jambo hili sana (Mstari wa 31). Kutoka 4:24-26 tunapewa mfanoa wa jinsi tunapaswa kumtii Mungu. Musa hakuwa amemtii Mungu kwa sababu hakuwa amemtahiri mwanawe. Katika Kutoka 5, Musa anaenda kwa Farao na kumwuliza kwamba awapatia ruhusa Waebrania waende katika jamngwa ili wamwabudu Mungu kwa siku tatu. Farao alijibu kwa kufanya kazi ya Waebrania iwe ngumu sana kwa sababu alisema kwamba wao wanawaza hivyo kwa sababu hawakuwa na kazi ya kutosha (Mitari 6-9). Matokeo ya hili ni kwamba watu walimlaumu sana Musa kwa taabu zao nyingi na kuonyesha kwamba hawakumwamini Mungu (21-23). Hata Musa musa naye alimlalamikia Mungu. Hii intuonyesha kwamba hatufai kulalamika bali tunapasw akuendelea kumwamini Mungu, kwa sababu Mungu akisema atafanya. Kutoka 6:1-8, Mungu aliwavumilia sana watu na aliahidi kwamba atawakomboa kutoka kwa utumwa wao na kuwaleta katika nchi ya ahadi. Pia Mungu aliahadi kwamba Yeye atakuwa Mungu wao. Yeye alifanya hivi hata baada ya Musa na waebrania wote kumlalamikia na kuonyesha kutokuwa na Imani katika ahadi zake. Hii intufundisha kwamba Mungu ni Mungu wa upendo na uvumilivu mkubwa sana. Kutoka 6:28-12:30 tunasoma kuhusu mapigo 10 ambayo yalidhihirisha vita kati ya Musa na Farao. Upaosoma sura ya 8:1-15, utaona jinsi mambo yalivyofanyika kati Musa na Farao. Mungu alifanya muujiza kupitia kwa Musa. Farao naye akawaagiza waganga wake wafanye hivyo. Wakati Farao aliona kwamba hata waganga wake wamefanya hivyo. Kwa sababu hii Mungu aliufanya moyo wa farao kuwa mgumu sana. Hii pia inatufufndisha kwamba Mungu ndiye anatawala kila kitu na kila hali. Piga la miwsho ambalo tunalisoma katika sura ya 12, ndiyo lilikuwa bay asana kuliko mapigo mengi yote. Mungu aliwaua wazaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama kwa Wamisri. Hii ndio ilimfanya Farao kuwakubali Waebrania waondoke Misri. Hadithi ya Pasaka ilihusu damu ya mwana-kondoo ambayo ili nyunyiziwa milango za Waebrania kuwaokoa wale ambao waliokuwa ndani ya nyumba hizo. Kondoo wa Pasaka anatuongoza kwa Kristo Yesu ambaye baadaye angekufa na kutuletea wokovu. Ni damu ya Mwana-kondo wa Mungu ambaye ni Kristo Yesu ambyo inatukomboa kutoka kwa moto wa jahamu. Biblia inasema kwamba, bila umwagaji damu, hakuna msamaha wa dhambi (Waebrania 9:22). Kutoka 12:1-14, tunasoma kuhusu maagizo juu ya Pasaka na jinsi walipaswa kufanya na jinsi ya kuikumbuka katika maisya ya mbeleni. Kutoka 12:29, tunasoma kwamba usiku wa manane, kila mzaliwa wa kwanza wa Wamisri aliuliwa na pia ikiwa katika mlango wa mtu yeyote ahata awe Mhebrania hakukuwa na damu ya mwana-kondoo, pia humo malaika wa kifo angeingia na kumwua mzaliwa wa kwaza wa mwanadama na wa mnyama. Katika Kutoka 13:17-22, tunasoma jisni Mungu alivyowaongoza Waebrania kutoka Misri kwa nguso ya wingu mchana na nguso ya moto usiku. Katika mstari wa 19, tunasoma kwamba wao walikumbuka maneno ya Yusufu (Mwanzo 5:25) kwa hivyo walibeba mifupa yake. Katika Kutoka 14:4, tunasoma tgena kwamba Mungu aliufanya moy wa farao kuwa mgumu na Farao aliamua kufuata Waebrania ili awarudishe katika utumwa. Mstari wa 10-12, Waebrania tena walimlamikia Mungu. Kutoka 14, tunasoma kuhuus kuvuka kwa bahari ya shamu. Farao aliwaza kwamba yeye alikuwa amefaulu kwa sababu Waebrania hawakuwa na njia nyingine kwa sababu bahari ilikuwa mbele yao. Hivi ndivyo shetani anavyofanya katika maisha ya wale ambao wameokoka. Yeye anajaribu kila wakati kutujaribi ili atufudishe katika utumwa wa dhambi. Mungu alimwamuru Musa ayapige maji ya bahari kwa fimbo aliyo kuwa nayo. Musa alipofanya hivyo, maji yagawanyika na katikati ya maji njia ambayo imekauka ikajitokeza kwa Waebrania wapiti hapo hadi upande mwingine wa bahari. Farao alipoona hivyo, yeye aliamua kuwafuata na Mungu naye alifunga njia ile na kuzamisha jeshili lote la Farao katika bahari ya shamu. Mungu aliwasaidia watu wake kutoroka Farao. Hii pia inatufunza kwamba Mungu atafanya lolote kuona kwamba watu wake wanalindwa kutoka kwa adui wao ambaye ni dhambi na shetani. Mungu hataruhusu wale ambao wameokoka, kupotea tena katika dhambi au kudanganywa na shetani. Yesu alisema, @nami ninawapa uzima wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono yangu@ (Yohana 6:28). Kutoka 15:1-21, tunasoma kuhusu jinsi watu walivyofurahia sana na wakaimba wimbo wa kumsifu Mungu ambaye unajulikanja kama Wimbo wa Musa. Watu walimsifu Mungu na Musa, lakini wapokumbana na majaribu mengine, walalamika tena (msitari ya 22-24). Tunaona kwamba watu hawa hawakuwa na imani na Mungu kwa sababu kila wakati mambo yalikuwa mabaya, wao walilalamikia Mungu sana. Katika mstari wa 25, tunasoma jinsi Mungu alivyowapatia chakula na maji ya kunywa. Hii tena inatuonyesha upendo wa Mungu na uvumilivu wake kwa wenye ambao hatustahili lolote zuri. Kutoka 16 tunsoma jinsi Mungu alivyoleta chakula kwa watu wake kutoka mbinguni ambayo ilikuwa Mana na Kware. Tena katika mistari ya 1-3, tunasoma jinsi watu walivyomlalamikai Mungu kwa sababu wao walikuwa na njaa. Watu walionyesha tena ukose wa Imani kwa Mungu. Lakini hata hivyo, Mungu aliwapatia chakula. Mungu aliwapatia chakula kwa miaka 40. Wao walikula bila kukosa chakula kaw awakati wowote. Mungu aliwahimiza kwamba walipaswa kukusanya tu kile ambacho walikuwa wale kwa siku moja tu. Siku moja kbala ya Sabato, Mungu aliwakubali wachukue mara mbili ili siku ya Sabato wasitoke nje kutafuta chakula. Mungu aliwapatia chakula hiki hadi wakati walipofika nchi ya kanani. Katika Kutoka 17, Tena tunsoma kwamba watu walilalamika dhidi ya Mungu na Musa kwa sababu walitaka maji ya kunywa. Pia tunsoam wakiwa wamefika mlimani Sinai. Kutoka 19, tunaanza sehemu ya pili ya kitabu cha Kutoka. Sehemu hii inahusu jinsi Mungu alivyokuwa anwafundisha watu wake jinsi ya kuishi maisha yao na kumwabudu Yeye. Haya ni mafundisho marefu sana ambayo yanakamilika katika kitabu cha Kumbukumbuka Torati wakati watu walipoingia nchi ya ahadi. Mungu alikuwa anwafundisha jinis ya kuishi maisha yao kama watu wake, watu ambao maisha yao yanapaswa kuwa tofauti kabisa nay a mataifu mengine. Agano Jipya linafundisha kwamba wakristo wanapaswa kuishi maisha yao tofaquti kabisa nay a wale ambao hawajaokoka (Yohana 15:19). Mungu pia anawafundisha watu wake jinsi ya kumwabudu na kuishi maisha yao kwa utukufu wake. Kutoka 20-23, tunasoma kwamba Mungu altengeneza Agano na watu wake wakati alipowapatia Amri Kumi. Yeye aliwaahidi Baraka ikiwa watatii na ikiwa hawatatii, laana. Mungu alipeana Amri Kumi ambazo ni za muhimu sab ahata katika maisha yetu leo. Amri Kumi za Mungu 1.Usiwe na miungu mingine ila mimi. 2. Usijifanyie sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu cho chote kilicho mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. Usivisujudu au kuviabudu. 3. Usilitaje bure jina la BWANA Mungu wako, kwa kuwa BWANA hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure. 4. Ikumbuke siku ya Sabato, uistakase. 5. Waheshimu baba na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa BWANA Mungu wako. 6. Usiue. 7. Usizini. 8. Usiibe. 9. Usitoe ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yako. 10. Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usitamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake, wa kiume au wa kike, wala ng’ombe wake au punda wake, wala cho chote kile alicho nacho jirani yako. Katika sura ya 24, Mungu anaendelea kuwapa watu wake sharia za jinis iliwapasa kuishi. Sheria hizi zilihusu siku ya Sabato na watumwa. Kutoka 25-31, Mungu alipeana maagizo jinsi Hema la Kukutania lilipaswa kujengwa. Hema hili lilidhihirisha uwepo wa Mungu miongoni wa watu wake. Neno Hema, linamaanisha mahali pa kuishi (Kutoka 25:8). Hii ilimaanisha kwamba katika hii Hema Mungu angeishi miongoni mwa watu wake. Katika mstari wa 9, lilikuwa jambo la muhimu sana kwa Mungu kwamba Hema linajengwa kwa njia mabyo Yeye mwenyewe alikuwa ameagiza. Sura zingine za kitabu hiki zinashughulika na kutueleza jinia Mungu alaitaka Hema hili lijengwe. Tunajifundisha kutokana na haya kwamba Mungu ameweka njia ambazo tunapaswa kuja kwake na tusipotumia njia hizo, kamwe hatutamfikia Mungu. Mungu anataka aabuidwe kwa njia mzuri ambaye inamletea Yeye utukufu. Kutoka 32, tunaona jinsi mioyo ya watu ilivyokuwa. Wakati Musa alipokuwa anamaliza muda wake na Mungu, wao walikuwa wanaabudu mtoto wa ng’ombe. Katika mistari ya 1-6 , Mungu na Musa walikasirishwa sana na jambo hili. Katika mstari wa 7-14, Mungu alikuwa ametisha kuangamiza hawa watu wote. Musa alimwomba Mungu kwamba asifanye hivyo. Mstari 14, tunsoam kwamba Mungu alikubali na hakuwaangamiza wote. Katika mistari ya 19-20 tuona kwamba Musa alikuwa mtu mwenye hasira. Tunaona pia kwamba wato 3000 wale waliuliwa kwa sababu walikataa kutubu. Kutoka 33:18-23, Musa alienda kuzungumza na Mungu tena. Mungu alimpa Musa maagizo ya jinsi Waebrania walipaswa kuishi maisha yao. Lakini hata kama Musa alikuwa na kibali machoni pa Mungu, baadaye tunaona kwamba Mungu hakumkubali kuingia kanani kwa sababu Musa alitenda dhambi ya kupinga mwamba badala ya kuzungumza nao jinsi Mungu alikuwa amemwahidi. Kutoka 35, tunasoma jinsi watu walivyotoa dhambi yao, ili itumika kwa kumjegea Mungu Hema la kukutania. Hii dhambi walitoka nayo Misri jinsi Mungu alikuwa ameahidi katika Mwanzo 15:14. Maagizo ya Mungu kwa jinsi ya kuijenga Hema la kukutania ma jinsi tunapaswa kumwabudu, inatufundisha kwamba lazima tuwe waangalifu sana wakati tunakuja mbele za Mungu. Maagizo kuhusu jinsi tunapaswa kuishi maisha yetu, yanatufundisha kwamba sisi ambao tumeokoka ni watu tofauti sana na wale ambao hawajaokoka. Tumebarikiwa sana kwa sababu tunaweza kuja mbele za Mungu wakati wowote kwa sababu kupitia kwa Kristo tunekubalika mebel za Mungu. Kitabu cha Kutoka kinamalizikia katika mstari wa 34 ambao tunasoma kuhusu utukufu wa Mungu ukiwa umejaa katika Hema la kukutania. Hapa ndipo mahali ambapo Mungu tena alizungumza na watu wake (Mambo ya Walawi 1:1). KITABU CHA MAMBO YA WALAWI Mada ya Kitabu cha Walawi: Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi ni Mtakatifu (1Petro 1:16 na Mambo ya Walawi 11:44-45). Kitabu cha Walawi kinaendeleza haditi ya Kitabu cha Kutoka ya Wayahudi wakiwa mlimani Sinai. Mungu alikuwa anwafundisha Wayahudio jinsi ya kuishi maisha ambayo yanamletea utukufu, maisha ambayo yandhihirisha kwamba kweli wao ni watu Wake. Wayudi walikuwa waishi yao tofauti kabisa na watu wa mataifa mengine. Sisi ambao tumeokoka, tunapaswa kusihi maisha yetu tofauti kabisa na maisha ya wale wote ambao hawajaokoka ( Yohana 15:19. Sheria ilipeanwa kwa wayahudi ili wafahamu kiile ambacho Mungu alikuwa anataka kutoka kwao. Ikiwa wangetii kabisa sharia ya Mungu, basi wao wangepatishwa na Mungu kutipita kwa kazi zao. Lakini ukweli ni kwamba wao hawakuweza kabisa kutii. Kwa hivyo walihitaji mwokozi. Uposoma kitabu cha Walawi, linaweza kuwa jambo ambalo ni la kushoshwa. Lakini hata hivyo, kuna mafundisho mengi ambayo tunaweza kujifunza kutokana na kitabu hicho. 1. Mungu wetu ni Mungu ambaye anajihusisha katika maisha yetu kila wakati. 2. Mungu anataka tumwabudu kwa njia ambayo anataka mwenyewe. Yeye amepetaia kanisa lake njia ya jnis tunapaswa kumwabudu leo. Haya yote yanapatikana katika kitabu cha Mambo ya Walawi. 3. Tofauti ya sadaka za wat wa Mungu na wale ambao si wa Mungu. A. Watu wengine walitoa sadaka kwa sababu walikuwa wanataka kupendeza miungu wao. B. Wayahudi walitoa sadaka zao kuonyesha kwamba walihityajika kuwa watakatifu. Hii ilikuwa njia ya kuondoa dhambi ambayo ilikuwa mfano wa Kristo Yesu ambaye alikuwa awe sadaka kuu ya kuondoa dhambi. 4. Kabiala la walawi ndio walikuwa makuhani na kuhani mkuu pekee ndiye aliingia mahali patakatifu pa Patakatifu. Sasa leo tunaye Kristo Yesu ambaye ndiye Kuhani wetu Mkuu (Waebrania 5:5). Kwa sababu ya Kristo, sisi ambao tumeokoka tunakibali cha kuja mbeleza Mungu kila wakati (Waebrania 4:14-160. Mungu yuko tayari kila wakati kutana nasi kwa maombi. Wale ambao hawajaokoka hawana kibali cha kuja kwa Mungu kwa sababu wao hawajamwimini kristo Yesu (Isaya 59:2 na Yohana 9:31). Wale ambao hawajaokoka, wanaweza tu kuja kwa Mungu ikiwa watattubu dhambi zao na kumwamini Kristo Yesu. 5. Kwa hivyo leo hakuna haja ya kutoa sadaka, lakini tunapswa kusoma na kujifunza kuhusu sadaka. Kitabu cha Walawim kinatufundisha mengi kuhusu umuhimu wa kutoa damu kama njia ya kuondoa dhambi, wakati huo na wakati wa sasa (mambo ya Walawi 17:11). Agano Jipya pia linatufundisha katika Waebrania 9:22 na 1 Yohana 1:7, kwamba hakuna ondoleo la dhambi bila kumwaga damu. Mkristo amepata msamaha wa dhambi zake kwa sababu ya damu ambaye Kristo alimwaga msalabani Kalivari. Je, kwa nini tujifunze kuhusu hizi sharia? Kuna wakristo wengi ambao wanasema kwamba hatuhitaji kujifunza hizi sharia kwa sababu sasa hatuko chini yake. Wao wanasema kwamba sasa tuko chini ya neema na wala si sharia. Kwa kusema hivi, wanasema ukweli lakini huu ni nusu. Sheria hizi zimegawanywa katika vikundi vitati: sheria za kimadili; Sheria za kiraia na sheria za sherehe. Wengi wanasema kwamba tunahitaji kutii sharia za kimadili, yaani amri kumi za Mungu. Jesus alisema, sijakuja kuondoa sharia bali kuikamilsha (Mathayo 5:17). Matendo ya Mitume inamalizika na sheri ya ceremonia na ambayo inamaliza kutengeana katika ya Wayahudi na watu Mataifa. Tunahitaji kutazama nini sharia inatufundisha na kutii zile sharia ambazo bado zinafanya kazi wakati wetu sasa kama Kumbukumbu la Torati 25:4 and Kutoka 23:5 and Mambo ya Walawi 25:14 Mafundisho ya Kitabu cha Walawi: 1. Mungu ni Mtakatifu na sisi wanadamu ni wenye dhambi. Dhambi ndio shida kubwa sana ambayo tuko nayo kama wanadamu. Ujumbe wa Mambo ya walawi, ni ujmbe wa msamaha na kuoshwa kwa dhambi ndipo tuwe na uhusiano na ushirika na Mungu. 2. Mamabo ya Walawi ni kitabu ambacho kimejawa na sharia nyingi sana katika Biblia yote. Kuna sharia nyingi ambazo zimekusudiwa na Mungu kutuongoza kwa Kristo ili tuweze kufanywa wenye haki kupitia kwa Imani. Sheria ya Mungu huwa inadhihirisha uovu wa na hatia ya mwanadamu mbele za Mungu. Chati hii inaonyesha sadaka za Walawi na jinsi Agano Jipya zinakamailisha sadaka hizi. Hapa tunaona sharia kuhusu vyakula mbali mbali. Baadaye katika Matendo ya Mitume 10:10-16, tunasoma kwamba sasa Wakristo wanaweza kula vyakula vyote. 3. Sadaka tano ambazo zinapatika katika kitabu cha Walawi: A. Sadaka za kuteketezwa (1:3-17). Watu walijitolea kwa Mungu kutpitia kwa sadaka hizi. B. Sadaka za vyakula(2:1-16). Hizi zilikuwa za kumshukuru Mungu kwa sababu ya maisha yao na kutoa maisha yao kwa ajili ya kumtumikia Mungu. C. Sadaka za Amani (3:1-17). Hizi zilihusu kuhusika katika baraka ya kuwa na ushirika na Mungu. D. Sadaka za dhambi (4:1-5:13). Hizi zilihusu kupewa msamaha wa dhambi. E. Sadaka kwa ajili ya dhambi (5:14-6:7). Hizi zilihusu kusamehewa kwa ajili ya dhambi ambazo walikuwa wametenda. 4. Sura ambazo zinafundisha kuhusu Kuhani na kazi yake (8:10-21:22). 1. Afisi ya Kuhani katika Agano la Kale ilikuwa ya muhimu sana kwa sababu yeye alikuwa mpatanisha kati ya Mungu na watu wake. Hii ndio sababu kuna maelezo mengi sana kuhusu afisi hii katika kitabu cha walawi. Leo Kristop ndiye mpatanishi wetu na anatuleta kwa Mungu mwemyewe. 1. Kitabu cha Waebarnia kinatundisha wazi kikilinganisha kuhani wa Agano la Kale ambaye alikuwa mwanadamu mwenye dhambi na kuhani mkuu wa Agano Jipya ambaye ndiye Kuhana mkuu ambaye amekamilika, yanni Kristo Yesu. 1. Kitabu cha Walawi 7:31-36 Mungu aliweka jinsi makuhani walihitaji kupata chakula chao. Leo pia ni lazima tuufuate mfano huo na tuhakikishe kwamba wachungaji wetu wanakula. 1. Katika Sura ya 8:1-4, tunasoma kwamba Mungu aliamru Aroni na wanawe wawekwa kuwa makunani. Mungu aliwatita katika huduma kama tu jinsi leo Mungu anawaita wengi kufanya kazi ya uchungaji. Kila mchungajia napaswa kuhakikisha kwamba ameitwa na Mungu na kwamba hajajiita. E. Sura ya 10:1-2, Watoto wa Aroni waliuliwa na Mungu kwa sababu hawakumwabudu Mungu jinsi Mungu alikuwa amesema. Tunapaswa kuja mbele za Mungu kwa njia ambayo Yeye mwenyewe amesema na si jinsi tunavyotaka. Tunafaa kuja kwa heshima na kwa mioyo ambayo imetubu. Ni jambo la muhimu kuja mbele za Mungu kwa ombi la toba. 1. Siku ya Upatanisho (Walawi 16). 1. Hii ilikuwa siku ya muhimu sana katika nchi ya Israeli kwa sababu siku hii, dhambi za watu zilipata kusamehewa. Hii ndio ilikuwa siku ya pekee katika mwaka ambapo Kuhani Mkuu aliingai Patakatifu pa Patakatifu katika Hema la kukutania. Hii ndio ilikuwa siku ya pekee katika mwakla ambapo watu walihitajika kufunga. 1. Walawi 16, tunasoma jinsi mbuzi wawili walichagualiwa. Mmoja alijichinjwa na mwingine dhambi za watu ziliwekwa juu yake na alitolea nje ya kambi. Mistari ya 21-22, tunasoma kuhusu kuondolewa kwa dhambi. B. Siku ya upatanisho ili ondolewa na sadaka ya Kristo Yesu malabani kalivari kwa ajili ya ondoleo la dhambi. 5. Siku takatifu Holy 23-25 1. Mungu aliweka siku takatifu ambapo watu wangemaliza muda wakimwabudu na kuwaza juu yake. Leo pia kuna siku ambazo zitengwa kwa ajili ya kukutana pamoja kama watu wa Mungu na kumwabudu Mungu. Siku ya Jumapili, siku takatifu ambayo tunakutana pamoja na kumwabudu Mungu. Kuna mafundisho katika kitabu cha Mambo ya Walawi. Katika sura ya 20:1-5, Mungu anachukia sadaka za kutoa watoto. Mungu anadhibi hii kwa kifo. Katika mstari wa 4-5, Mungu ameahidi adhabu kali sana kwa wale wote wanafanya na pi wale ambao wanashuhudia vitendo hivi na hawafanyi lolote. KITABU CHA HESABU Hadithi za kitabu hiki zinaendelea jangwani. Mwanzoni kitabu hiki killitwa “jangwani.” Tafsiri la kwanza la Agano la Kale, lilibadilisha jina la kitabu hiki na kuitwa Hesabu. Mada ya kitabu hiki. Waisraeli walimaliza miaka 40 jangwani kwa sababu ya kutotii kwao pamoja na Musa. Kitabu hiki kinafundisha kwamba Mungu ataadhibu dhambi na kwamba wale ambao watattii watabarikiwa na Mungu kama Yoshua na Kalebu ambao Mungu aliwawezesha kuingia katika nchi ya ahadi. Watu walihesbiwa. Waisraeli walichukua miazi 3 kutoka Misri hadi mlimani Sinai. Walimaliza karibu mwaka mmoja wakiwa Sinai halafu miaka 40 kufika Moabu na kanani. Kitabu hiki kina sehemu tatu muhimu sana. I. Sehemu kwanza, wako mlimani Sinai na wanajitayarisha kuondoka. Hapa mahali ndipo wamekuwa tangu Kutoka 18. Numbers 1:1 thru 10:10 A. Hesabu 1:1-54, tunasoma kuhusu kuhesabiwa mara ya kwanza ya watu wote. B. Hesabu 2:1-4:49, tunasoma kuhusu mipangalio katika kambi. Kila kabila lilikuwa na mahali pake na baadaye kila kabila ilipewa sehemu. C. Mungu aligawanya watu; walawi ambao walikuwa makuhani na watu wengine. Mungu alipanga watu. Halfu baadaye Mungu aliwatayarisha watu wake kuondoka na kuelekea katika nchi ya ahadi. Mungu aliendelea kuwapa maagizo ya jinsi wal;ihistali kuishi. Hesabu 3:1-10, tunasoma tena kuhusu jinsi wana wa Aroni walivyouliwa kwa sababu ya kutomtii Mungu. Pia tunasoma jinsi Mungu alivyoongeza idadi ya Walawi kwa kuongoza kabila la Walawi lote. D. Sheria 5:1-8:26 E. Mambo ya mwisho mlimani Sinai 9:1-10:10 II. Sehemu ya pili ya kitabu hiki ni kitoka mlimani Sinai hadi Edomu (10:11-20:21). Wayahudi walisafari kwa majuma mawili kwa sababu ya kiburi chao kwa Mungu. A. safari ya Kadeshi 10:11-12:16 Sura ya 12 tunsoma jinsi Aroni na dadake waliasi dhidi ya Musa mtumishi wa Mungu. 1. Huko kadeshi 13:1-2, Mungu aliwatumia vijana waende na wapelelezi nchi ambayo alikuwa ameahidi kuwapataia. Mstari wa 3-16, Mungu aliwatuma waakilishi kutoka katika kila kabila kumi na mbili za Wayahudi aambo walikuwa waichukue ili nchi ya ahadi. Katika msitaru ya 25-33, tunasoma kuhusu tipoti ya wapelelezi. Kalebu na Yoshua waliripoti kwamba walipaswa kuingia mara moja na kuichukua ile nchi lakini wale wengine, walikuwa na shauka kama kweli alikuwa angekuwa mwaminifu kwa ahadi yake. Wao walisema kwamba wenyeji wan chi ile walikuwa watu wenye nguvu sana na ingekuwa vigumu sana kuwashinda. Hii ilionyesha kwamba wao hawakuwa na Imani katika Mungu. Sura ya 14, tunasomakwamba watu walimwasi Mungu na hili limkasirisha Mungu sana. Katika mistari ya 13-19, Musa aliomba kwa Mungu na Mungu alisamehe lakini pia aliahidi kuadhibu. Katika mistari ya 20-37, Mungu aliwaambia watu wazima wote kwamba hakuna hata mmoja wao ambao angeingia kanani. Wao watazunguka mika 40 katika jangwa hadi wakati ule watu wazima watakufa wote. Msitari ya 37-38, Hapo na hapo Mungu aliwaua wale wapelelezi 10 ambao hakuamwamini. 1. Tunasoma kuhusu kuasi kwa Musa. Sura 20:2-5, tunasoma jinsi watu walivyomkasirisha Musa kwa kulalamlalamikai Mungu. Mungu alimptatia Musa maagizo kwamba azungumze na mwamba kule Meriba na kwamba mwamba huo ungeleta maji. Badala ya kuzungumza, Musa aliupiga mwamba. Kwa sababu hii Mungu alimwambia Musa kwamba hataingia katika nchi ya Ahadi. III.Sehemu ya tatu inazingatia sura 2);22-36:13. Sehemu hii inatueleza kuhusu miaka ambayo walimaliza wakizunguka zunguma katika jangwa hadi wale ambao walikuwa watu wazima wakafa wote. A. Sura ya 20:22-29, tunasoma kuhusu kifo cha Aroni. B. Katika sura 21:4-9, tunasikia tena watu wakilalamika dhidi ya Mungu. Kwa sababu kulalamika kwao, Mungu aliwatumia nyoka wa sumu ambao waliwauma kwa sababu ya ukosefu wa utiifu kwa Mungu. Mungu anamamru kwamba nyoka wa shaba atengenezwe na wekwe juu ya mti na kwamba wale wote ambao watageuka na kutubu kwa kumtazama huyu nyoka, wangeishi wala hawangekufa. Wale ambao walitubu, Mungu aliwasamehe. Katika Yohana 3:14-15, nyoka huyu ni mfano wa Yesu ambaye aliangikwa juu ya msalaba na wote ambao wanamwamini wao wanasamehewa uovu wan a Mungu. C. Hesabu 27:12-23, Mungu alimweka Yoshua kuchukua nafasi ya Musa. D. Hesabu 28-30 tunasoma kuhusu maagizo mengine kuhusu kumwabudu Mungu. E. Hesabu 36 tunsoma kuhus waisraeli wakiwa wamefika mlamini Moabu ambapo palikuwa mahali pa kuingilia katika nchi ya ahadi. KUMBUKUMBU LA TORATI Kitabu hiki pia kinaweza itwa usomaji wa sharia mara ya pili au Maagizo ya mwisho ya Musa kwa Waisraeli. 1. Kumbukumbu la Torati 1-3, miaka 40 zimepita tangu waondoke Misri na sasa wa Waisraeli wako kando yam to Yorodani wakiwa tayari kuvuka. Kwa kawaida hii ingewachukua siku 11, lakini kwa sababu ya kukotii kwao, iliwachukua miaka 40. Musa aliwapatia maagizo ya mwisho kabla ya waingia kanani. Yeye anawaelezea historia yao tangu waondoke Mlaminai Horebu, yaani Sinai. Musa aliwakumbusha watu hatari ya dhambi na uasi wao. Sura 1:3, Musa anawakumbusha kwamba mamlaka yote inatoka kwa Mungu na pia anawaambia kwamba maneno yake, ni maneno ya Mungu. II. Musa aliwasomea watu sharia mabzo Mungu alikuwa amewapatia. 1. Kumbukumbu la Torati 4, Musa anawaambia watu kwamba wakimtii Mungu, watabarikiwa na ikiwa watakosa kumtiii Mungu, wataadhibiwa. 1. Kumbukumbu la Torati 5, Musa anawakumbusha watu kuhusu Amri Kumi za Mungu. 1. Kumbukumbu la Torati 6:4-10, tunafundishwa kwamba tunapaswa kumpenda Mungu kwa kila kitu ambacho tuko nacho. Katika Marko 12:, Yesu alirudia amri hii. Kuonyesha Mungu upendo ni lazima tumtii. 1. Kumbukumbu la Torati 7:6-8, tunasoma kuhusu msingi wa Agano la uhusiano wetu na Mungu. Ni kwa mapenzi na utawala wa Mungu anatuleta katika uhusiano naye (Warumi 8:29-30). 1. Kumbukumbu la Torati 14:21, tunafunzwa jinsi ya kufahamu Biblia na kuwa na msingi bora wa Imani. Wayahudi walitumia mstari huu kufundisha kwamba mtu hawezi kula nyama na wakati huo huo, anakunywa maziwa. 1. Kumbukumbu la Torati 18:15-22, Kuna maafundisho mazuri sana kuhusu manabii. Tunsoma kwamba Musa ni nanbii wa ukweli na katika mstari 15, Musa anasema kwamba miongoni mwa Waisraeli Mungu anatamleta nabii mwingine mkuu kuliko Musa mwenywe, nabii huyu ni Kristo Yesu. Katika mstari wa 22, tunasoma kwamba tutamfahamu nabii wa kweli ikiwa unabii wake utatimia. Je, ni nani ambaye alikuwa nabii wa kwanza kutajwa katika Biblia? III. Kumbukumbu la Torati 27-30. Maagizo ya mwisho ya Musa kuhusu kumtii Mungu. A. Kumbukumbu la Torati 27, tunasoma kuhusu orodha ya laani ambazo zinaambatana na kukosa kumtii Mungu. B. Kumbukumbu la Torati 28:1-14, tunasoma kuhusu ahadi za Mungu kwa wale ambao wanamtii Mungu (1-6 ) na katika mistari 15-19 tunasoma kuhusu ahadi za laana na adhabu kwa wale wote ambao watakataa kumtiii Mungu. Isaya 57, inafundisha jambo hili pia. Mara kwa mara tunaona memngi yameaandikwa kuhusu laana kuliko baraka. Hii ni kwa sababu Mungu anataka kuhakikisha kwamba tunaonywa kabisa. C. Kumbukumbu la Torati 29, tunasoma kuhusu kutangaza upya kwa Agano la Mungu ambalo alilipeana mlimani Sinai (Kutoka 20-23) wakati alipowatia Waisraeli sheria na kuwaahidi baraka ikiwa watatii. 1. Kumbukumbu la Torati 29:29 na Isaya 55:8-9, hivi vifungu vinatusaidia kuelewa kwamba hatujui kila kitu kumhusu Mungu na kwa hivyo hatuweza kueleza yale ambayo hatuyajui kwa sababu Mungu hajayaweka katika neno lake. D. Kumbukumbu la Torati 30, Mungu aliwakumbusha watu kwamba wanauhuru wa kuchagua kifo au maisha. Mstari wa 16, una ahadi baraka kwa wale ambao wanatii na mstari wa 17-19, una kifo kwa wale ambao wanakosa kutii. IV. Kumbukumbu la Torati 31-34 Yoshua anapewa uongozi. A. Kumbukumbu la Torati 31, tunasoma kuhusu kifo cha Musa alipokuwa miaka 120. Yeye alikuwa bado katika afya nzuri sana. Mungu alimpeleka Musa juu yam lima Nebo na akamkubali kuiona nchi ya ahadi, lakini Mungu hakumruhusu aingia katika nchi ya ahadi. KITABU CHA YOSHUA Kitabu hiki kinaanzisha sehemu nyingine ya Biblia. Sehemu hii inaitwa ya kihistoria kwa sababu tunasoma kuhusu Historia ya nchi ya Israeli kuanzaia kwa kuingia kwao katika nchi ya ahadi kitabu cha Esta. Kitabu hiki cha Yoshua tunasoma kuhusu waisraeli wakipigana vita na Mungu akiwapatia ushundi dhidi ya maadui wao. Lakini pia ndani mwake kuna visaq ambapo Waisraeli walishindwa. Kitabu hiki kina sehemu mbili za muhimu. I. Yoshua 1-12, tunasoma jinsi watu walivyo ichukua nchi ya ahadi. 1. Yoshua1, Mungu alimtuma Yoshua (1-9). Tunajifunza mambo kadhaa kutoka na hili. A. Mistari ya 5-7,9; Tunahitaji kuwa na ujasiri tunapomtumikia Mungu. Mungu anasema kwamba kila wakati yeye huwa pamoja nasi. B. Mistari ya 7-8, tunakumbushwa kwamba lazima kila wakati tumtii Mungu. 2. Yoshua 2-5:13-6:27, tunasoma kuhusu kuuchukua mji ya Yeriko. Yoshua 5:13-15, wengi wanaiwzia kuwa mfano wa kuja Kristo Yesu. A. Yoshua 2, tunasoma kuhusu rahabu ambaye aliwaficha wapelelezi na maisha yeke yalisazwa wakati waisraeli waliuvamia mji huo. B. Hawa wapelelezi walileta habari mzuri si kama wale wa kwanza. C. Tunasoma kuhusu kuanguka kwa Yeriko. Mungu aliamru kwamba jesji lizunguka mara moja kwa siku kwa siku sita. Siku ya saba walizunguke mji mara saba na mwisho wapige kelele na kuta za mji huo zianguke. Kila hazina mle ilikuwa ya Mungu na maisha yote ilikuwa ingamizwe katika mji yule isipokuwa familia ya rahabu. Ushindi wa huko Yeriko, ulikuwa mkubwa sana kwa watu wa Mungu. 3. Yoshua 3:1-17, Tunasoma kuhusu jinsi walivyovuka mto Yorodani kama tu jinsi walivyovuka bahari ya shamu. Mungu alitimiza ahadi yake kwa Abahamu kwamba kizazi chake kitamiliki nchi ya ahadi. 4. Yoshua 4:1-9, tunsoma jinsi watu walivyoweka kumbukumbu kwa Mungu kwa kutumia mawe. 5. Yoshua 7-8, tunasoma jinsi mji wa Ai ulipochukuliwa. Hadithi ya kukotii ilifuata na kutii na ushind mkubwa sana. A. Tunasoma kwamba Akani ambaye alikosa kumtii Mungu. Yeye alificha vitu ambavyo alipata katika hema jambo hili lilifanya Waisraeli washindwa vita walipokuwa vitani kule Ai. Akani na familia Mungu aliamua waliuliwe. 5. Yoshua 9, tunasoma jinsi Waisraeli walivyodanganywa kwa sababu hawakuuliza ushauri kutoka kwa Mungu wakati walikumbana na Wagibeoni. Hii ili maanisha kwamb Waisraeli waishi na Wagibeoni na wasiwaangamize. A. Tunajifunza hapa kwamba, tunapaswa kila wakati kutafuta ushauri kutoka kwa Mungu na wala si, kufanya mambo jinsi tunavyotaka. Mstari wa 14, tunaambiwa kwamba hawa hawakutafuta ushauri wa Mungu. B. Tunajifnza pia kwamba hata kiongozi mzuri pia kuna wakati anakosea kabisa. 6. Yoshua 10-12, tunasoma jinsi jeshi la Mungu lilivyoangamiza falme nyingi. II. Yoshua 13-24, hii ni sehemu ya pili ya kitabu hiki. Katika sehemu hii tunaelezewa jinsi nchi iligawanywa. 1. Kila kabila ilipewa sehemu ya arithi isipokuwa kabila la Walawi. Je ni kwa nini kabila hili halikupewa sehemu ya aridhi. 2. Yoshua 23, tunasoma kuhusu maneno ya Joshua ya mwisho kwa viongozi wa Israeli. A. Yoshua alizungumza kuhusu yale ambayo aliweza kutimiza na ni kwa nini yeye alikuwa mtu ambaye kweli alimpenda Mungu. Mistari ya 3 na 5, Yoshua anamtukuza Mungu kwa sababu alifahamu kwamba ni Mungu ambaye alikuwa akiwapa ushindi dhidi ya maadui wao. B. Yoshua pia aliwahimiza kwamba walipaswa kuendelea kuwa waminifu kwa Mungu haswa katika ndoa zao. Aliwaambai kwamba wasiwaoe wanawake wa kanani. Iliwaonya kwamba ikiwa watakosa kumwamini Mungu, Mungu atawaadhibu vikali sana. Huu ndio ujumbe ambao Musa pia alikuwa amewambia. 3. Yoshua 24:1-13, aliwakumbusha kuhusu uaminifu wa Mungu kwao wakati wote na jinsi alivyowapatia nchi ambayo alikuwa ameahidi wazazi wao katika Mwanzo 12:7. 4. Yoshua 24: 14-28, Yoshua alitoa hutuba yake ya mwisho kwa watu na aliwahimiza wawe waaminifu kwa Mungu na kumtumikia Mungu pekee. Katika mstari 15, Yoshua anatoa familia yake yote kwa kumtumikia Mungu. Watu wote waliahidi kumtii Mungu. Katika kitabu cha waamuzi, tutasoma jinsi wao walivyotekeleza jambo hili. 5. Yoshua alikufa akiwa na miaka 110 na alizikwa katika aridhi ambayo Mungu alikuwa amempatia. KITABU CHA WAAMUZI UTANGULIZI. Mwandishi na wakati wa kuandikwa wa kitabu hiki haujulikani. Kitabu hiki kimejumlisha zaidi ya miaka 400 ambayo inafahamika kama miaka ambayo Waisraeli kwa sababu ya kukosa kutii kwao, Mungu aliwaadhibu sana kwa kuwaweka mikono mwa adui wao ambao waliwatumikia kwa miaka mingi. Katika sura ya mwisho na mstari wa 25, tunasoma kwamba watu walitoka kwa Mungu na wakaenenda kwa njia zao mwenyewe. Jambo hili mara kwa mara linaonekana katika kitabu hiki. Yesu Kristo alizungumza kuhusu jambo hili katika Yohana 14:15, “Kama mnanipenda mtazishika amri zangu.” Hawa watu mioyo yao ilitoka kwa Mungu, yaani upendo wao kwa Mungu ulipunguka kabisa. Ahadi ambayo walikuwa wameahidi kwamba watazishika amri za Mungu waliivunja. Hawa waamuzi walikuwa kama viongozi wa kijeshi. Hadithi katiika kitabu hiki ni kwamba, watu walitenda dhambi dhidi ya Mungu. Mungu kwa kuwaadhibu aliwatumia maadui ambao waliwageuza kuwa watumwa kwa miaka kadhaa. Baadaye walimlilia Mungu, na Mungu aliwatumia Mwamuzi ambaye alikuja na kuwasaidia na kuwatoa katika utumwa wao. Ktika kitabu hili tunasoma kuhusu Waamuzi 12. II. Waamuzi 1-16, tunasoma kuhusu Waamuzi 12. 1. Waamuzi 1:1-2:5, tunasoma kuhusu shida ya kwanza baada ya Yoshua kufa. Waisraeli walishindwa kuendelea na vita ili kuwatoa kabisa maadui wa Mungu katika nchi ile. Kwa kusosa kufanya hivyo walimwasi Mungu (Kumbukumbu la Torati 20:16-18). Kwa sababu hii, wao waliendelea na maisha ya kukosa kutii neno la Mungu. Leo pia tunapatana na jambo hili. Maadui wa Mungu ambao walibaki katika nchi ya Kanani, waliwashswishi watu wa Mungu katika njia mbaya. Je, walifanyi hivi kwa njia gani? 2. Waamuzi 2:1-5, kutotii kwa Waisraeli ndio kilikuwa chanzo cha shida zao za maisha ya mebeleni. Hii ndio hadithi ya Biblia nzima. Kutotii Mungu ndio chanzo cha matatizo yote katika maisha ya mwanadamu. Dhambi ndio chanzo cha shida za mwanadamu. A. Chapter 1 Verse 1 is a theophany. (explain see also Exodus 3:2-6) 3. Waamuzi 2:6-16:31 Tunasoma kuhuus hadith za kutomtii Mungu. Kizazi cha Yoshua chote kilikuwa kimekufa na kizazi ambacho kilifuata kilikosa kumtii Mungu. A. Waamuzi 2:10, tunasoma kwamba kizazi ambacho kilikuja baada ya Yoshua hakikumjua Mungu. Hili likuwa na linaendelea kuwa shida kubwa sana katika kanisa. Katika Kumbukumbu la Torati 4:10, Mungu anatuhimiza kwamba tunapaswa kuwafundisha watoto wetu neno lake. Kila mzazi anajukumu la kuwafundisha watoto wake kumhusu Kristo. Ufuatao ndio mwenendo wa kitabu cha Waamuzi. Dhamibi = Waisraeli watenda dhambi machoni pa Mungu. Mungu aliwaadhibu = Mungu aliwaachilia katika mikono ya maadui wao kwa miaka kadhaa. Toba = Waisraeli walimlilia Mungu awakomboe kutoka katika mikono ya maadui wao. Ukombozi = Mungu aliwaletea mkombozi ambaye alikuwa Mwamuzi ambaye alikuja na kuwakomboa kutoka mikono ya maadui wao. Na nchi ilkuwa na Amani kwa muda hadi tena wakati mwingine walipoanguka katika dhambi tena. Waamuzi wengine walikuwa wazuri na wengine walikuwa wabatya. 4. Debora alikuwa mwamuzi mzuri ambaye alimletea Mungu sifa (5:1-9 na 31). 5. Yesfta (11:1-12:7) alikuwa mwamuzi mbaya (11:29-40). A. Je, nathiri yake katika mistari 30-31, ilikuwa nzuri au mbaya? Katika mistari ya 34-40, tunasoma kuhusu matokeo ya nathiri yake. Toa hoja zako. III. Kitabu cha Waamuzi kinamalizikia kwa hadith mbili mbaya sana. Katika nchi ya Waisraeli kulikuwa na tabia ya kutotii sheria na dhambi iliongezeka sana (17-21). 1. sehemu ya mwisho ni kinyume na sehemu kwanza. Shida za ndani za Isreali zilikuw kubwa sana kuliko zile kutoka kwa maadui wao. Adui mkubwa wa Israeli alikuwa yeye mwenyewe. Kama tu leo, adui mkubwa wa kanisa, ni kanisa lenyewe. Vita viko ndani ya kanisa. Hii ni shida kubwa sana ambayo tunakumbana nay oleo katika kila kanisa. 2. Waamuzi 17-18, tunasoma kuhusu hadithi ya Micah, hadith ambayo ilihusu kuabudu sanamu ambako kulihusisha mlawi na kabila la dani. 3. Waamuzi 19-21, tunasoma kuhusu hadithi mbaya ya unajisi na mauaji katika kabila moja la Israeli. Hii inadhihirisha jinsi watu wa Mungu walivyokuwa wameanguka katikla dhambi kama watu wa Sodoma na Gomora. A. Kabila la benjamini lilikuwa limeangamia sana,. Lakini tunasoma pia kwamba waliobaki, wake walipeanwa kwao. 4. Waamuzi 21:25, Tunasoma kwamba katika siku hizo, hakukuwa na mfalme na kila mtu alifanya jinsi alivyotaka. Hii inatufundisha kwamba, tunapaswa kuwa na mpangilio na sheria za kuongoza katika maisha yetu. KITABU CHA RUTHU Hiki ni mojawapo wa vitabu viwili vya Biblia ambavyo vimeandikwa kwa jina la mwanamke. Hii ni hadithi ambayo inatuonyesha jinsi Mungu aliwabariki wale ambao walikuwa waaminifu kwake. Tunaona katika sura ya kwanza kwamba hadithi hii ilifanyika wakati wa Waamuzi. Ruthu, naomi na Boazi ndio watu muhimu katika kitabu hiki. Ruthu hakuwa Mwebrania lakinia likuwa mkwe wa naomi. Ruthu alimpenda mamake mkwe na alirudi naye Israeli. Boazi alimwona Ruthu ambaye baadaye alimchukua na akawa mke wake. Walifuata sheria za wakati huo za ndoa kabla waoane. Ruthu na Boazi walikuwa mababu wa mfalme Daudi ambaye alikuwa katika koo ya Kristo Yesu. Katika koo hiyo tunamwona pia Rahabu ambaye alikuwa kahaba. Kitabu hiki tunatufundisha tofauti ya maisha ya watu watatu ambao ni waaminifu kwa Mungu na ukosefu wa uaminifu wa taifa la Israeli wakati wa Waamuzi. Ruthu ambaye alikuwa anatoka katika nchi ya Moabu aliddhihirisha kwamba Agano la Mungu si kwa Waisreali pekee bali kwa wote ambao watafurahia barakla za Mungu kwa kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu. 1. Ruthu 1, tunsoma kwamba Ruthu na mama mkwe wake wote walipoteza waume wao kwa kifo. Naomi anaamua kurudi Israeli na Ruthu pia anamua kurudi naye. 2. Ruth 2, Ruthu alikutana na Boazi ambaye alikuwa mwema kwake. 3. Ruthu 3 na 4, tunasoma kwamba Ruthu na Boazi walioana na Mungu aliwabariki na mtoto ambaye aliitwa Jessi ambaye ndiye baba wa Mfalme Daudi. Ruthu na Boazi ni mababu wa Kristo Yesu (Mathayo 1:5-6 na31). I NA II SAMWELI Samweli, sauli na Daudi ndio watu watatu ambao tunasoma sana kuwahusu katika vitabu hivi viwili vya Biblia. Samweli ndiye alikuwa kuhani. Katika maisha ya samweli, hatusikii mambo mabaya kumhusu kama yale ambayo tunayasikia katika maisha ya mfalme Daudi. 1SAMWELI 1. Katika I Samweli 1:1-8, tunsoma kuhuus Hana ambaye alikuwa mke wa Elikana. Hana alikuwa tasa na alitamani sana kuwa na mtoto. Yeye alikuwa anakeliwa na wake wenza (1:6). 2. Hana alimwomba Mungu (9-18). Alimwomba kwam,ba Mungu ampatia kijana ambaye angemtoa kumtumikia Mungu katika maisha yek yote. Katika mstari wa 18, tunasoma jinsi Hana alipata Amani baada ya kumwomba Mungu. Hana aliomba kwamba mtoto wake atakuwa mnadhiri. Je, hii ina nadhiri nzuri? Kumbuka nadhiri ya Yefta. Katika Luka 1, Roho Mtakatifu alisema kwamba Yohana Mbatizaji atakuwa Mnadhiri. Mara ya kwanza kusikia jambo hili la unadhiri ni katika Hesabu 6:2-8. Hii nadhiri ni ya kutengwa kwa ajili ya kazi ya huduma wa Mungu. 3. 1 Samweli 1:20, tunasoma kwamba Mungu alimpataia Hana mtoto nan aye akamtoa mtoto huyu jinsi alivyokuwa ameahidi Mungu. Baada ya Samweli kuachishwa maziwa ya mama na kuanza kupewa chakula cha kawaida, yeye alipelekwa katika hekalu na alianza kutumika huku akiwa na Eli kuhani. Kila wakati tukumbuke kwamba kuna gharama ya kuwa mwaminifu kwa Mungu. Gharama hii hana aliilipa kwa kupeana mtoto wake wa pekee kuwa kuhani. Huenda kuna wakati alihisi kuwa pamoja na mtoto wake, lakini hata hivyo alikubali mtoto wake amtumikie Mungu. Kutumikia Mungu kuna gharama ambaye ni lazima tuilipe. Kwa mfano, wengi ambao wanaenda kuhubiri na kufundisha neno la Mungu katika sehemu mbali mabli za ulimwengu huu, huwa inawabidi waache familia zao. Wengine wanaenda katika sehemu ambazo maisha ni magumu sana, kwa sababu hiyo wo wanagonjeka na ahat wengine wanakufa. 4. 1 samweli 2:1-11, trunasoma kuhusu wimbo wa Hana. Hana alimsifu Mungu. Wimbo huu unaweza kulinganisha na wimbo wa Maria (Luka 1:46-56) na wengine ambao walimsifu Mungu kwa sababu ya uaminifu wake. Tunafaa kuiga hawa na wakati meingine kumaliza muda katika kumsifu Mungu. 5. 1 Samweli 2-3, tunasoma kuhusu uovu wa wana wa Eli ambaye alikuwa kuhani na hukumu ya Mungu ambaye alitangaza kwao. Watoto hawa walikufa na kifo hiki kinatajwa katika 1 Wafalme 2:27). 6. 1 Samweli 3:1-10, tunasoma kuhusu kuitwa kwa samweli na jinsi Mungu alivyokuwa naye katika maisha yake. Samweli ndiye alikuwa Mwamuzi wa mwisho. Tujadili kuitwa na Mungu? 7. 1 Samweli 4:10-11, tunasoma jinsi Waisraeli walivyopoteza Sanduku la Agano. Sanduku hili lilikuwa la muhimu sana kwa sababu lilidhihirisha uwepo wa Mungu miongoni mwao. Walilipoteza kwa sababu ya kulileta katika vita kama sanamu ya kuwaletea ushindi. Jadilini sanamu kama njia ya kuleta bahati mzuri au mbaya? 8. 1 Samweli 8, tunasoma kuhusu taifa la Israeli wakitaka mfalme. Pia tunasoma kwamba wana wa samweli waliwekwa kuwa makuhani. Lakini watoto wake walikuwa watu waovu ambao walichukua rushua. Hii ilisababbisha Waisraeli kuwakataa na kutaka wapewe Mfalme. Samweli alikasirika sana, lakini katika mstari wa 7, Mungu alimwambia kwamba hawakuwa wanamkataa yeye, walikuwa wanamkataa Mungu. Katika 1:10-18, Mungu alimwambia Samweli awaonye watu juu ya tabia ya wafalme. Mungu aliwapatia watu mfalme 19-22. Tunaposoma kuhusu tabia ta wafalme kwa watu tunaona kwamba, onyo ya Mungu kwa watu juu ya walfalme ilikuwa ya kweli. Mara kwa mara watu huwafuata wafalme wao na walfalme wengi waliwaongoza watu wa Israeli katika kuabudu miungu na kukotii Mungu na hili liliwaletea taabu kubwa sana kutoka kwa Mungu. 9. 1 Samweli 9, Mungu alimweka sauli kutoka katika kabila la benjamini kuwa mfalme wa kwanza wa Israeli. Katika mstari wa 2, tunaona jinsi sauli alifafanuliwa kutokana na jinsi alivyokuwa nje. Kumbuka jambo hili wakati tunajifunza kuhusu Daudi. II. Hadith ya mfalme Sauli kabla ya Daudi kuwea mfalme. Tunasoma kuhusu sauli alikuwa mfalme wa aina gani. 1. 1 Samweli 10, tunasoma kuhusu kupakwa mafuta kwa Sauli ambaye alikuwa anatoka katika kabila benjamini. 2. 1 Samweli 12, tunasoma kuhusu hotuba ya Samweli ya kuaga watu. Katika hotuba hiyo, Samweli anawahimiza waisraeli wamtii Mungu. Mistari ya 13-25, inalinganishwa na hotuba ya mwisho ya Musa. 3. 1 Samweli 13:8-14, baada tu ya kushinda vita, tunaona moyo halisi wa Sauli jinsi ulivyo. Sauli alitoa sadaka kwa Mungu na Samweli alimkemea sana kwa kufanya kile ambacho hakuhitajika kufanya. Je, kwa nini Samweli alimkemea sana? Kwa sababu Samweli alimwambi kwamba Mungu alikuwa amemkataa na kwamba Mungu alikuwa amepeana ufalme huo kwa mtu mwingine. Mfalme huyu angekuwa mfalme ambaye moyo wake unampenda sana Mungu. 4. 1 Samweli 13-14, tunaendelea kusikia hadithi kumhusu ushindi ambao Sauli aliendelea kupata hata kama alikuwa anafanya uamuzi mbaya kama kulaani yeyote ambaye alikula kabla ya vita kuisha na adui kushindwa. 5. 1 Samweli 15, tunasoma jinsi Mungu alimkataa tena Sauli. Sauli aliagizwa kwamba aende apigane na Wameleki na awaue wote na wanyama. Sauli alikosa kutii amri ya Mungu na Mungu alimwambia Samweli kwamba alihuzunika kwa sababu ya kumfanya Sauli kuwa mfalme. Sauli alionekana kwamba anatubu lakini halikuwa jambo la ukweli. Kwanzzi hapa, Samweli alimwacha kabisa. III. I Samweli 16-31, tunasoma kuwahusu Mfalme Daudi na Sauli. Mungu alimchagua Daudi kuwa mfalme baada uya kukataa sauli. Sura ya 16:7, tunapewa tunafafanuliwa Daudi alikuwa mtu wa aina gani, haswa moyo wake ulikuwa moyo wa aina gani. Katika sura yote tunaelezewa jinsi sauli alijaribu sana kumwua Daudi, lakini hata kama Daudi alikuwa na nafasi ya kumwua sauli, Daudi hakufanya hivyo kwa sababu alimwona Sauli kuwa mtumishi wa Mungu. 1. 1 Samweli 17, tunasoma kuhusu hadithi ya Daudi na Goliathi. Hadithi hii inatuonyesha Imani kuu ambayo Daudi alikuwa nayo kwa Mungu. Daudi alishinda vita hivi. 2. 1 Samweli 18:6-16, tuansoma jinsi sauli alivyomchukia sana Daudi. Katika mstari wa 7, tunasoma kuhusu chanzo cha wivu wake dhidi ya Daudi. 3. 1 Samweli 18:10, tunasoma kwamba Sauli alikuwa mwenda wazimu. Katika sura 16:13-14, tunaona kwamba Mungu akitoa baraka zake kwa Daudi na ameziondoa kwa Sauli. 4. Mstari wa 11, tunasomakwamba hasira yake ilimzidi na alijaribu kumwua Daudi. Lakini hata kama sauli alijaribu sana kumwua Daudi, Mungu hakukubali jambo hilo lifanyike kamwe. 5. 1 Samweli 24:1-7, Daudi alikuwa na fursa ya kumwua sauli lakini hakufany hivyo. Daudi alimpenda sana Mungu na kuona kwamba mipango yake inakamilika hata kama ni Sauli kuendelea kuishi aki angaishi maisha yake Daudi. 6. Daudi alivimilia miaka mingi sana ya mateso ya sauli, lakini hakumdhuru sauli kwa njia yoyote kwa sababu alijua kwamba Sauli alikuwa mpakwa mafuta na Mungu. Katika 2 samweli 1, tunasoma kwamba Daudi aliamuru yule mtu awawe ambaye alimwua Sauli. 7. 1 Samweli 29, tunasoma kuhusu uovu wa Sauli wakatika alienda kwa mganga. II SAMWELI Katika kitabu hiki tunasoma kuhusu utawala wa mfalme Daudi. Yeye alijulikana kuwa mtwana na mtu ambaye alimpenda sana Mungu, Yeye alikuwa mwepesi wa kutubu. Daudi alijulikana na mfalme wa vita. Kila wakati alikuwa katika vita na alipanua mpaka ya nchi ya Israeli na kuichukua nchi yote ambayo Mungu alikuwa ameahidi Abrahamu Isaki na Yakobo. Daudi kwanza alikuwa ahakikishe kwamba Yuda iko salama ndipo aweze kuhakikisha usalama wa Isreali yote. Vita ambavyo ilihusika navyo vya mwisho vilikuwa kwa sababu dhambi yake na Bethsabe. Kijana wake Absolomu baadaye alijaribu kuleta mapinduzi. Sura ya 13 tunasoma kuhusu hadithi ya Absolomu. I. 2 Samweli 1-10, tunasoma kuhusu vita vya Daudi kuhakikishia ufalme usalama. 1. Daudi alikuwa mfalme kwa miaka saba na nusu wa Yuda na miaka 33 akiwa mfalme wa Israeli. 2. 2 Samweli 5, tunasoma kuhusu jeshi la Daudi lilivyouchukua mji wa Yerusalemu, ambao pia uliitwa mji wa Daudi. Huu ndio ulikuwa mji mkuu wa Israeli na mahali ambapo walikutania kuabudu. Hadi leo huu ndio mjii wa mkuu. 3. 2 samweli 6, tunasoma jinsi Sanduka la Agano lilirusihwa Yerusalemu. Mstari wa 6-7, tunakumbushwa kwamba Mungu aliwahitaji watu wa Isareli wamtii. Mistari hii inadhihirisha dhambi ya aina mbili; kwanza wao hawakusafirisha Sanduku la Agano jinsi Mungu alikuwa amewagiza (Kutoka 25:12-14). Pili ni kwamba Uzzah hakuhitajika kugusa Sanduka la Agano kwa sababu yeye hakuwa Mlawi. Hii ni hadithi ya kuofya sana. Lakini tunafundishi kwamba Mungu anataka kila wakati tufuate maagizo yake na kwamba pia anataka tumwabudu kwa njia ambayo inampendeza na wala siyo ile ambayo inatupendeza. A. 2 samweli 6:13-21, tunasoma kwamba waisraeli walifurahia sana wakati Sanduka la Agano lilipoletwa Yerusalemu. Kulikuwa na sherehe. Ni jambo jema sana kusherekea baraka na ushindi wa Mungu. B. Mstari 16 na 20-23, tunasoma jinsi Mikali alivyomdharau Daudi wakati alipomwona akirukaruka na kucheza mbele za Bwana. Huyu Mikali alikuwa binti wa mfalme Sauli. Je, unawaza nini kuhuus hili? 4. 2 Samweli 7, Daudi alikuwa na tamma ya kutaka kumjengea Mungu hekalu lakini Mungu alikataa. Baadaye katika 1 Mambo ya Nyakati 22:8, tunsoma kwamba ni mtoto wa Daudi ambaye ndiye alikuwa aijenge kwa sababu Daudi alikuwa amehusika katika vifo vya watu wengi. Lakini hata hivyo Mungu alimzawadia Daudi tamma hii na kumwambia kwamba: A. mstari 10-11, Mungu angepatia mahali pa Israeli kuishi milele. B. Mistari 12-13, Mungu angemwezesha mtoto wa Daudi kulijenga hekalu. C. Mstari 13, Mungu angeweka ufalme wa Daudi uwe wa milele. D. Mstari wa 14, Mungu angeanzisha uhusiano wa mwana na Baba na kizazi cha Daudi. Tunafurahia uhusiano huu leo kwa sababu sisi tumefanywa kuwa wana wa Mungu kupitia kwa Imani ndani ya Kristo (Yohana 1:12). E. Mistari ya 14-15, Upendo wa Mungu hangeondoka katika nasaba ya Daudi kama ulivyoondoka katika nasaba ya Sauli. Hii huwa inajulikana na Agano la Daudi ambalo linatimika katika Yesu Kristo. Mistari ya 18-19, tunasoma kuhusu maombi ya shukurani ya Daudi. 5. 2 Samweli 8-10, tunasoma kuhusu ushindi mwingine na ukarimu wa Daudi kwa mjuku wa Sauli. II. 2 Samweli 11-19:8, Tunasoma kuhusu dhambi ya Daudi na shinda nyingi ambazo zilikumba familia yake. 1. Mambo mazuri yote ya mbeleni, yalifuatwa na hadithi mbaya sana za hadithi ya Daudi kuanguka katika dhambi. Ikiwa hadithi hii hujaisema, tafadhali iseme. 2. 2 Samweli 12, eleza jinsi nabii nathani alivyokuja kwa Daudi na kumweleza kuhusu dhambi yake. Katika mstari wa 13, tunaona moyo wa Daudi, alipoanmbiwa kwamba ni yeye ambaye alikuwa amefanya dhambi hiyo, yeye alitubu. Katika mistari ya 15-22, tunasoma kuhusu kifo cha mtoto wao na Bethsabe. Daudi aliomba na kufunga kwamba mtoto apone, lakini mtoto alikufa na Daudi alikubali mapenzi ya Mungu. 3. 2 Samweli 13-18, tunaendelea kusoma kuhusu adhabu ya Daudi kwa sababu ya dhambi yake. Mtoto wake Amoni alimnajisi dadake Tamari na Absolomu ndugu yake alimwua. Absolomu naye alijaribu kupinduwa serikali ya Daudi. Kwa sababu hii daudi alikimbia kutoka kwa mji. Absolomu naye alilala na wajakazi wa Daudi mbele ya watu wote. Baadaye Absolomu aliuliwa na Daudi aliomboleza sana kwa ajili ya mtoto wake. Tunajifunza kwamba, mtu anaweza kutubu dhambi zake, lakini bado Mungu amwadhibu hapa duniani. III. 2 samweli 19-24, kitabu hiki kinaisha tukiendelea kuelezwa memngi kuhusu shida za Daudi. 1. 2 Samweli 20, tunasoma kuhusu Sheba amabye alitoka katika kabila la Benjamini ambaye aliongoza kupinduliwa kwa serikali ya Daudi. 2. 2 Samweli 21,tunasoma kuhusu kiangaza ambnacho Mungu alimwambia kwamba kinasababishwa na ukose wa haki ambao mfalme sauli aliwanyia Wagibeoni. Hawa watu walikubali kuwaua watoto saba wa Sauli ili jambo hili litulizwe. 3. 2 Samweli 21, tunasoma kuhusu vita vingine na wafilisti. 4. 2 Samweli 22, tuansoma kuhusu wimbo wa Daudi wa ukombozi (mistari ya 1-7). 5. 2 Samweli 24, tumalizia kitabu hiki, tena tukisoma kuhusu Dauddi akiwa kwenye shida. Pia tunasoma kuhusu kununuliwa kwa kipande cha aridhi Yerusalemu ambapo sadaka zingikuwa zinatolewa kwa Mungu. Kuna mambo mazuri na mabaya katika suta hii ya mwisho ambayo yanazungumza jinsi Daudi alivyoishi maisha yake. A. Katika mstari 1, tunasoma jinsi Mungu alikubali shetani amwongoze Daudi kuwahesabu watu jambo ambalo Mungu alikuwa amelikataa. B. Mstari wa 10, tunasoma kwamba Daudi alijua kwamba alikuwa na hatia kwa kuamuru kwamba watu wahesabiwe. Kwa sababu hii dhamira yake ilimsumbua sana na kwa hivyo alienda mbele za Mungu. C. Mistari ya 11-17, tunaswoma jinsi Mungu alivyomwadhibu Daudi. Mungu alimpatia achague katika adhabu 3. Daudi alichagua na Mungu akatuma ugonjwa ambao uliwua watu 70,000. Onya ya Saweli ilikuwa ya kweli kwamba wafalme huleta taabu kwa watu. Je ni nani am,baye anamtaka Mfalme? E. 2 Samuel 24:18-25, tunasoma jinsi Daudi alinunua aridhi ya madgabahu mahali ambapo baadaye hekalu lilijengwa. Kuna funzo kwetu katika mstari 24, tuwe tayari kulipa gharama katika kumtumikia Mungu. Leo kuan wakristo wengi ambao wanateseka na kuetswa kwa sababnu ya kumtumikia Mungu na kumwabudu. Chini hapa kuna amelezo kuhusu mateso ya wakristo huko Uganda. Kuna wakristo wengi ambao wamepata mateso mengi haswa katika sehemu ambazo kuna waislamu. Idi amini wakati alipochukua mamlaka katika mwaka wa 1971, yeye na wenzake walijaribu kufanya Uganda iwe nchi ya Kiislamu wakiwa wanafadhiliwa na nchi ya Saudi na Libya. Shida mabyo walikumbana nay o ni kwamba wengi wa watu walikuwa wakristo. Kwa sababu hii walianza kuwaua watu. Wakati alipotoka mamalakani, katika mwaka wa 1979, alikuwa amewaua 500,000 ambao 300,000 walikuwa wakristo. Wale wote ambao tumeokoka, lazima tuwe tayari kulipa gharama ya kumwabudu na kumtumikia Mungu. I NA II WAFALME Hii hadith ya Wafalme wote wa Isreali baada ya Daudi hadi kuanguka kwa mji wa Yerusalem na mwisho wa utawala wa wafalme. Hadithi hii inaanza wakati Solomoni alikuwa mfalme wa nchi ya Israeli wakati ambapo taifa hili lilipokuwa tajiri na taifa lenye nguvu na ushawishi mkubwa sana. Hadithi zake ni huzuni kwani tunaelezwa jinsi watu wa Mungu walivyokosa kumtii Mungu na kwa sababbu hii, taifa hili liliendelea kuangamia. Mfalme Solomoni alichukua mamlaka akiwa na ahadi za kuwa mfalme mazuri, lakini yeye aliwaooa wake ambao hawakuwa wayahudi na aliongozwa katika kuabudu sanama na wake hawa. Vitabu vya Mambo ya Nyakati, vinatueleza pia kuhusu hadithi ya taifa la Israeli lakini vikizingatia hadithi za makuhani. Kitabu cha 1 Wafalme kina sehemu mbili. Sehemu kwanza inaanzia 1-12. Katika sura hizi tunasoma kumhusu mfalme Solomoni na taifa la Israeli likiwa taifa ambalo limeunganika pamoja. Sehemu ya pili ya kitabu hiki, tunasoma kuhusu taifa hili la Israeli likiwa limegawanyika mara kwanza. Vitabu hiivi vya Walme ni kitabu kimoja kwa sababu 2 Wafalme wa pili, ni kuendeleza 1 Wafalme. Katika 2 walme tunaosna kuwahusu watu wa Mungu wakimwasi Mungu na kuanza kufuata miungu hata kaka Mungu alijaribu mara nyingi kuhakiksiha kwamba watu wake wnafuata njia yake. Mungu alifanya hivi kwa kuwatuma manabii. I. Mfalme Solomoni atawala taifa la Israeli wakati lilikuwa limeunganika. 1. 1 Walme 1:1-5, kabla ya Daudi kufa, kulikuwa na mafarakano ni nani ambaye alifaa kuwa mrirthi wake na awe mfalme. Adonaji ambaye alikuwa mmoja wa wana wa Daudi alijitawaza kuwa mfalme na wakati Daudi aliposikia jambo hilio, Daudi alitangaza kwamba Solomoni mwana wa Bethsaba ndiye awe mfalme. Kile kilifuata ni kutawazwa kwa Solomoni na kuuliwa kwa Adonaji. 2. 1 Walme 2:1-4, Daudi alizingumza na Solomoni mwanawe na kumwagiza kwamba awe mwaminifu kwa Mungu na Mungu atambariki. 3. 1 Wafalme 3:1-2, tunasoma kuhusu makubaliano ya Solomoni kumwoa binti wa farao na hiki ndicho kilikuwa chanzo cha kuangamiza kwa nchi ya Israeli. Katika Mistari ya 5-14, tunasoma kuhusu swali la Mungu kwa Solomoni. Badala ya Solomoni kuagiza vitu vya dunia, alimwuliza Mungu ampe maarifa ya kuweza kutawala watu wake. Jambo hili lilimfurahisha Mungu sana na katika mistari ya 12-14 tunsoamkwamba Mungu alimzidisha hata mali ya ulimwengu. Katika Mathayo 6:33 Yesu anasema, “lakini utafuteni kwanza ufalme wa Ufalme wa Mungu na haki yake na haya yote mtaongezewa.” Katika mistari ya 16-28, tunsoma kuhuus uamuzi wa Solomoni ambao ulidhirisha maafifa ambayo Mungu alikuwa amempatia. Tuna kwa kweli kwamba Solomoni alianza vyema sana katika maisha yake kama mfalme. Lakini baadaye tunaona kwamba Solomoni alibadilika na akakosa kuwa mwaminifu kwa Mungu nah ii ilimfanya akosee sana Mungu n ahata katika majukumu yake kama mfalme. Tunapaswa tuwe waangalifu sana, ni rahisi kuanza vizuri sana lakini tumalize vibaya sana ikiwa hatuendelea kumwamini Mungu. 4. 1 Wafalme 4, tunasoma jinsi ufalme wa Solomoni uliyoendelea kunawili kwa sababu ya baraka ambazo Mungu alikuwa analeta juu yake. Katika mistari ya 20-23 na 25-26, tunaona jinsi Mungu alimbariki mfalme Solomoni. 5. Tunasoma kuhuus kujengwa kwa hekalu kuanzia katika sura 5 hadi katika sura ya 8 ambapo ilitolewa kwa Mungu. Hekalu ilikuwa mahali ambapo Mungu anaishi mwingoni mwa watu wake na mahali ambapo watu walikusanyika kumwabudu Mungu. Hekalu lilikuwa mjengo wa bei sana na maridadi kabisa. Kwa mfano kulikuwa na dhahabu nyingi sana mabyo ilitumoka katika kujenga hekalu hili. Hekalu hili lilijengwa wakati Solomoni alikuwa anatawala kwa njia ambayo ilimpemdeza Mungu. Katika sura ya 8:63, tunaona gharama wakati hekalu lilikuwa linatolewa kwa Mungu. Kwa miaka mingi sana maisha ya Wayahudi yaliongozwa na hekalu hilo. Sasa Kristo ndiye hekalu ambapo kila mtu ambaye anatubu na kuwamini Kristo anakutana na Mungu. Ndano ya Kristo, Mungu yuko pamoja nasi kila wakati siku zote. 6. 1 Walfalme 9:1-9 , tunasoma kwamba baada ya ukamilishaji wa hekalu, Mungu alimjia Solomoni. Mungu alirudia tena ahadi ya baraka ikiwa watatii na adhabu kali sana kwa kutotii neno lake. Vivyo hivyo Mungu anahidi wale wote ambao wanatii neno lake kwa kuja kwa Kristo kwamba Yeye atawabariki kwa kuwaokoa na kuwapa maisha ya milele. Lakini kwa wale wote ambao wanakataa kumwamini Kristo, Mungu ameahidi kuwatupa jahanum (Yohana 3:16). Pia Mungu ameahidi baraka zake kwa watoto wake ambao wanaendelea kutii nenoa lake kwa kuishi maisha matakatifu na adhabu kali sana kwa watoto wake ambao wanaishi maisha ya dhambi (Matendo ya Mitume 5:1-11). 7. 1 Wafalme 9:10-11:13, tunasoma kuhusu miaka ya utawala mzuri wa Solomoni. Mungu alimbariki na utajiri mwingi sana. Wafalme wengine walimheshimu sana. Pia tunsoma kwamba Solomoni alikuwa na wake wa mataifa mengine 700 na Masuria 300. 1 Wafalme 11: 2-8, tunasoma jinsi Mungu alivyokuwa kasirika kwa sababu jinsi hawa wake wa Solomoni walivyomwongoza katika kuabudu sanamu badala ya kumwabudu Mungu. 8. 1 Wafalme 11:9-13, tunasoam kwa nini Mungu alikasirika na Solomoni na mpango wa Mungu wa kuwaleta amaadui dhidi ya Solomoni kama Yeoboan ambaye aliivunja nchi ya Israeli wakati wa utawala wa mwana wa Solomoni. Mungu hakutekeleza hilo hadi wakatik Solomoni alipokufa kwa sababu ya ahadi ambayo alikuwa amempa Daudi babake Solomoni. 9. Kuna mafundisho mengi ambayo tunapaswa kujifunza kutokana na maisha ya Solomoni. Solomoni alikuwa amebarikiwa na hekima na utajiri. Yeye alikuwa na kila kitu ambacho mtu yeyote angependa kwa sababu Mungu alikuwa amempa. Lakini baadaye aligeukia miungu na mwishowe aliona jinsi maisha yake yalivyokuwa bure. Unaposoma kitabu cha Mhubiri, utaona jinsi Solomoni alivyoharibu maisha yake. Kuna wengi ambao wanajuta baadaye kwamba wamefuata vitu ambavyo si vya muhimu katika maisha yao, kama pesa na anasa. Maisha ya ndiyo tuko nayo ambayo Mungu ametupatia, je, tunafaa kuyaishi kwa ajili ya tamaa zetu au kwa ajili ya Mungu. Utawala wa mfalme Solomoni ndicho kilele cha histaria ya Israeli. Tunasoma kwamba wakati huu, nchi ilikuwa imeendelea kiuchumi sana. Historia nyingine ya Israeli ni taifa ambalo liko katika shida nyingi. Katika taifa la kasikazini, uharibifu wao ulikuwa kuwa wa mara moja lakini katikam Yuda, kulikuwa na wakati mzuri na wakati mbaya sana. Taifa la kasikazini lilikuwa na wafalme ambao walikuwa waovu sana. Lakini Yuda alikuwa na wafalme ambao baadhi yao walikuwa wzuri sana ambao walifanya Mungu asileta hukumu yake kwa haraka. II. Sehemu ya pili, ya kitabu hiki inazungumza kuhusu ufalme ambao ulikuwa umegawanyika. 1. 1 Walfame 12:4-14, tunasoma kuhusu Rehoboamu ambaye alikuwa mwana wa Solomoni. Rehoboamu alikuwa mkali kwa watu na kwa sababu hii yeye alisababisha kugawanyika kwa nchi ya Israeli. Tunasoma katika mistari ya 18-19 kwamba, taifa la kasikazini liliasi na kujitenga na Yuda. Waliongozwa na Yeroboamu ambaye alianzisha taifa linguini la kasikazini au Efraimu. Makabila mawili pekee ndiyo yaliachwa: kabila la Yuda na kabila la Benjamini. 2. Wakati Reboamu aliona hivi, yeye aliamuru jeshi lake liwarejesha watu lakini Mungu alipeana maagizo tofauti kabisa na yake (12:21-24). Je ni kwa nini Mungu alipeana maagizo haya? Huenda alikuwa anataka kuhifadhi Yuda isiangamizwe. Rehoboamu akiwa na makabila mawili alitaka kupigana na makabila 10. Baadaye katika historia tunaelezwa kwamba mataifa haya mawili yalipigana. 3. 1 Wafalme 12:25-33, tunasoma kwamba Yeroboamu aliweka sehemu mbili za kuabudu. Yeye alitengeneza ndama wawili ambao walikuwa miungu na kuambia watu wawaabudu. Yeroboamu aliwaongoza watu kabisa kutoka kwa Mungu na kuwaongoza katika uabudu sanamu. Alifanya hvi ilikuwazuia watu wasirudu Yerusalemu kuabudu Mungu vile iliwapasa kwa sababu aliogopa kwamba wakirudi huko huenda watarudi kuishi katika Yuda. Yerobaoamu alikuwa mfalme mbaya sana machoni pa Mungu. Kila wakati tunaposoma kuhusu mfalme mpya katika Yuda au Isreali tunasoma kuhusu kama mfalme huyo aliongoza watu vyema katika macho ya Mungu au aliwaongoza katika kuabudu sanamu. Wafalme wote wa Isreali walikuwa wabaya sana. Wengine wa Yuda walikuwa wazuri na wengine wabaya sana. Kwa sababu ya wafalme wazuri, Yuda alikuwepo kwa miaka nyingi sana kuliko Israeli. 4. 1 Wafalme 17, tunasoma kuhusu nabii Eliya ambaye alikuwa anatoka katika Israeli. Mungu aliwatuma manabii wengi sana katika mataifa haya yote: Israeli na Yuda. Mungu alifanya hivi kwa sababu alikuwa anataka watu wake watubu dhambi zao na warudia kumwabudu Mungu na kumtumikia Mungu kama jinsi iliwapasa. A. 1 Wafalme 17:1, Elikya atabiri kwamba hakutakuwa na nvua kwa miaka mitatu na nusu na hili likafanyika. Hili ilikuwa ishara ya nabii wa kweli. B. Katika mistari ya 8-24, Eliya alienda zarefati mahali ambapo alimsadia mjane mmoja na kijana wake huko. Katika 17-23, tunasoma kwamba alimrudisha uhai kijana wa mjane huyu. Kumbu ak kwamba Eliya alifanya hii katika nchi ya kigeni. Baadaye katika Luka 4:26, Yesu alizungumza kuhusu hadithi, Yesu alisema kwamba hakutumwa tu kwa Wayahudi lakini kuwaokoa watu kutoka kila mahali kutoka katika dhambi zao.Wayahudi walikasirika sana juu ya jambo hili na walijaribu kuwua Kristo. Je, ni kwa nini Wayahudi walikuwa na wivu sana? Wivu ni dhambi mbaya sana ambayo ina madhara mabaya sana. Dhambi hii imo katika kanisa na shida kubwa sana katika migawanyika makanisani. C. 1 Wafalme 18, tunasoma kuhusu hadithi hii ambayo ilifanyika miaka mitatu baada ya Eliya kutabiri kuwepo kwa ukame. Katika mistari ta 20-39, tunasoma jinsi Eliya alivyowaisbisha manabii wa bali. Katika mstari 27, Eliya aliwakejeri manabii hawa. Katika mstari 46, tunasoma kwamba Eliya alikimbia mbio zaidi ya farasa. Je, unamaini hili kwamba wanadamu wanaweza kukimbia zaidi kuliko farasi? D. 1 Wafalme 19, tunasoma kwamba Eliya aliongopa sana na alitoroka kutoka kwa mfalme Ahabu. Mstari huu unadhihirisha kwamba kuna wakati sisi sote tunaweza kupungukiwa na Imani. Katika Mathayo 14:28-31, yesu alimsadia Petro alipokuwa anazama. Katika mstari wa 5-16, tunasoma jinsi Mungu alihudumia Eliya alipokuwa amehuzunika na jinsi Mungu alirejesha katika huduma wa kumtumikia. Mstari wa 18, unataufundisha kwamba kila wakati Mungu huwa ana watu wake ambao wamebaki wakiwa waaminifu sana kwake. E. 1 Wafalme 19:16-21, tunasoma kuhusu kuitwa kwa Elisha ambaye alikuwa nabii ambaye alichukua nafasi ya Eliya. Mungu anafundishi viongozi wa makanisa kwamba wanapaswa kuwatayarisha wengine kuenedelea huduma wakati wao waondoka. Viongozi wanapaswa kujua kwamba hudumu si wao bali ni wa Mungu na ni kazi ya Mungu. Ninaomba kwamba huduma huu ambao ninaufanya, hautakufa wakati nimekufa na kwamba utaendelea. F. 2 Wafalme 2:1-12, tunsoma jinsi Elisha alivyochukuliwa na kupelekwa mbinguni. Katika biblia tunasoma kuwahusu watu wawili ambao hawakufa: Eliya na Enosi (Mwanzo 5:24). Mungu alituma chariote ya moto ambayo ilkuja na kumchukua Eliya na kumpeleka mbinguni. Hii inatufundisha kwamba wakristo ambao watakuwa hai wakati Kristo atakaporudi, hawataonja kifo cha mwili (1 Wathesalonike 4:16-17). 5. Huduma wa Elisha ulikuwa kama wa Eliya ambao ni kuwaita watu kutoka katika dhambi na kurudi kwa Mungu ili Mungu aweze kuwabariki. A. Elisha alifanya pia miujiza. 2 Wafalme 2:18-21, tunasoma jinsi alaiyasafisha maji ya mji wa Yeriko. B. 2 Wafalme 4:1-7, tunasoma kuhusu Elisha akimsaidia mjane. Jadili juu ya upendo wa Mungu juu ya wajane na mayatima. Katika Yakobo 1:27, tunafundishwa jinsi tunapaswa kuwafanyia wajane na mayatima. Hwa watu wawili ni wa muhimu kwa Mungu. C. 2 Wafalme 4:8-36, tunasoma kuhusu muujiza wa Elisha wa kumrudisha kijana wa mjane uhai kama tu vile Eliya alivyofanya. Katika Biblia tunasoma kuhusu watu watano ambao waliwarudishia watu uhai wao. Wao ni: Eliya na Elisha katika Agano la kale; Yesu, Petro na Paulo katika agno Jipya. Hawa wote walivyohivyo kwa nguvu za Mungu na pia tunajifunza kwamba Kristo ameahidi kuwafufua wote ambao wamemwamini na kuwaleta mbingu na nchi mpya. Pia Mungu anazo nguvu za kuwafufua wafu wa kiroho na kuwa uhai wa kiroho wale wote ambao wanamwamini Kristo Yesu. D. 2 Wafalme 13, tunaosm akuhusu kifo cha Elisha. Tunajifunza hapa kwamba hata watumishi wa Mungu hufa. Kifo kinamfikia kila mtu, awe ameokoka au la; awe mtumishi wa mhubiri au hapana; awe raisi au mtu wa kawaida; tajiri au maskini; umesoma sana au hapana; wote kifo kitawafikia na kwa hivyo wote wanahitaji kujitayarisha kwa ajili kufa. Wote wanahitaji kumwamini Yesu Kristo ili maisha yao ya baada ya kifo yawe mazuri. Pia tunsoma kwamba kuna mtu ambaye alikuwa amekufa na walipokuwa wanampeleka kumzika, walipoona vikosa vya washanmbuliaji, wao walimtupa mwili katika kaburi la Elisha na mara tu mwili huo ulipogusana na mafupa ya Elisha, Biblia inasema kwamba mtu huyu alifufuka (mistari 20-21). Huu muujiza hakufanyika kwa nguvu za Elisha, kwa sababu alikuwa amekufa. Ni Mungu aliufanya. Miujiza ambaye alifanywa na watu wa Mungu, haikufanyika kwa nguvu zao, ni nguvu za Mungu miujuiza hii ilifanyika. Kwa hivyo kila wakati tunapoona mujiza, tumshukuru Mungu na wala tusimwabudu mwanadamu, kwani mwanadamu ni chombo tu ambacho Mungu anakitumia. Je, miujiza ilikuwa na kusudi gani katika Biblia? Miujiza alidhihirisha huruma wa Mungu kwa watu wake na kudhibitisha kwamba wale ambao walifanya miujiza hii walikuwa watu wa Mungu na wametumwa na Mungu. Kuhusu Kristo, tunasoma, “..Yesu wa nazareti alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa miujiza, maajabu na ishara, ambayo Mungu alitenda miongoni mwenu kwa kupitia Yeye, kama ninyi wenyewe mjuavyo” (Matendo ya Mitume 2:22). III. mafundisho juu ya Israeli katika Muhtasari 1. Israeli ilikuwa na wafalme 19 na wote hawakuwa wema mbele za Mungu. Israeli ilikuwepo kwa 208 kabla ya Ashuru kuwavamia na kuwachukua mateka. Taifa hili la kasikazini hadi leo halipo tena. Ilikuwa tabia ya nchi ambayo iliwachukua mateka maadui wake kuwachukua na kuwapeleka kwingine na kuwaondoa kabisa katika nchi hiyo. Kwa kufanya hivi, walihakikisha kwamba hawamateka hwarudi pamoja na kuanzisha uasi. Baada ya kuwaondoa watu katika nchi yao, waliwachukua mateka wengine kutoka nchi nyingine na kuwaleta katika nchi hiyo. 1. Watu wa Yuda katika siku ya za Kristo Yesu, walichukia sana Wasamaria ambao waliletwa katika nchi hiyo ya kasikazini Wao walisema kwamba hwa watu walikuwa wameichukua nchi ya mandugu wao. Katika Agano Jipya tunasoma kuhusu uadui huu. Makabila 10 ambayo yalichukuliwa na Waashuru na hadi leo hakuna mtu anayejua wako wapi. Wao wanajulikana kama “makabila ya Israeli yaliyo[potea.” Hadithi ya wafalme wa Israeli ni hadith ya huzuni kwa sababu tunsoam jinsi walivyogeuka na kumwaacha Mungu na jinsi Mungu alivyowaadhibu vikali. Wao walitoka katika baraka na kujiletea hukumu. 1. Mfale mmoja wa Israeli, Mfalme Yehoahazi ambaye alitawala Israeli katika mwaka 814 BC (2 Wafalme 13:1-9). Yeye alikuwa mtu mwovu na Mungu alikubali maadui wake wa mwadhibu. Katika mstari 4, mfalme alimwomba Mungu, na Mungu aliwakomboa na wakaishi kwa utulivu. Katika mistari ya 6-7, tunasoma kwamba watenda dhambi tena, na Mungu akawaadhibu twena. Mfalme huyu alitawala kwa miaka 17 kabla ya la jeshi la Ashuru kuja na kuangamiza jeshu la Ashuru. Je, kuna swali lolote kuhusu jambo hili, kwa nini Mungu aliadhibu hawa watu? Tunapata funzo hapa pia kwamba wafalme huwa wanawaletea watu shidi nyingi sana. IV. Tunaposoma kuhusu Yuda, tunaona kwamba wafalme wake wengine walikuwa wazuri na wengine wabaya sana. Kwa sababu ya Mungu wale wazuri huenda ndio sababu Mungu hakueleta maangimizo kwa taifa hilio kwa haraka. 1. 2 Wafalme 18:1-8, tunasoma kumhusu mfalme Hezekia ambaye alikuwa mfalme mazuri ambaye alimcha Mungu. Yeye alikuwa mfalme wakatika nchi ya kasikazini ilivamia na waashuru. Baada ya miaka michache ya kuanguka kwa nchi ya kasikazini, mfalme wa Ashuru alikuja na kuvamia Yuda. Yerusalemu pekee ndio ambaye waashuru hawakuvamia. 2. 2 Wafalme 18:19-35, tunsoma kuhusu madharau ya mkuu wa jeshi la Ashuru ambaye aliwaambia watu katika Yerusalemu kwamba wajisalimishi kwa sababu alikuwa ameuzingira mji wote. 3. 2 Wafalme 19, tunasoma jinsi mfalme Hezekia aliogopa sana. Aliingia katika hekalu na kuwmomba Mungu ili awasaidie. Nabii Isaya alikuja kwake na kumwambia kwamba Mungu alikuwa anaenda kumsaidia na kumwondoa katika mikon ya maadui. Isaya alitabiri kuangamizwa kwa jeshi la Ashuru. Katika mstari wa 35-36, tunasolma kuhusu vifo vya watu wanajeshi 185,000 wa ashuru. Hii iliwafanya waashuru wakarudi katika mji wao wakiwa wameshindwa kabisa. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa kuanguka kwa himaya ya Ashuru. Babilomi sasa ilianza kuamka na kuwa himaya yenye nguvu. Hii inatupatia himizo kwamba Mungu kila wakati anafanya kazi ya kuwalinda na kuwatettea watu wake. Wakati wa shida, Hezekia aliomba. Yeye alikuwa mfalme ambaye hakutegemea nguvu za jeshi lake. Alimwomba Mungu. Kwa hivyo hata sisi leo katika kila hali, wakati wowote tunalete mahitaji yetu kwa Mungu ambaye ni Mkuu anaweza kufanya lolote (Wafilipi 4:6-7). 4. 2 Wafalme 21:1-2, tunasoma kuhusu kifo cha Hezekia na mwanawe Manase alichukua hatamu za uongozi. Manase alikuwa mwovu. Yeye hakuishi na kutawala kama babake. Ni kwa wakati huu ambapo Mungu alitabiri kwamba, kwa sababu ya uovu wao, Mungu atakubali nchi ya Yuda ichukuliwe katika utumwa (mistari 10-15). Baadaye katika utumwa akiwa ameteswa sana na wale ambao walikuwa wamemteka mateka, Manase aliokoka na Mungu akubali ufalme wake kuendelea kwa miaka mingine 50. 3. 2 Wafalme 25, tunasoma jinsi Babiloni ilivyokuja na kuwachuka watu wa Yuda katika utumwa. Huu ulikuwa wakati mbaya sana. Wayahudi wengi walichukuliwa kama watumwa. Mara mingi Mungu huwa ni mvumilivu kwa watu lakini uvumilivu wake unapoishi, hukumu au adhabu yake huwa kali sana. I NA II MAMBO YA NYAKATI I na II Mambo ya Nyakati ni kama Wafalme, ni kitabu kimoja. Mara yangu ya kwanza kusoma Agano la kale nilijiuliza kwa nini mambo ya rudiwa tudiwa. Ukweli ni kwamba historia ya Wayahudi huwa inarudiwa sana lakini huwa imeandikwa tofauti sana ili kuwakumbsuah watu juu ya uhusiano wao a Mungu. Lengo la kuandika vitabu hivi vya I na II, ni kutueleza kuhusu Mungu. Vitabu hivi viliandikwa babaya ya uhamisho wa Yuda mwisho ya historia ya Agano la kale. Kuna mwandishi mmoja ambaye anaitwa Gleason Archer, alinadika kwamba vitabu hiiv viliandikwa na kusudi la kuwajulisha Wayahudi ambao walitoka uhamishoni kwamba wao walikuwa watu wa Mungu wa Agano. Kusudi hili likuwa la kuwaeleza kwamba utukufu wa kweli wa taifa la Wayahudi ulipatikana katika Agano lao na Mungu. Kwa hivyo Mungu aliwapatia nafasi nyingine ya kuishi. Vitabu hiiv vya Mambo ya nyakati ni onyo kwa watu kwamba wasiwahi tena kuacha kuabudu Mungu wa kweli. Wao walikuwa wameadhibiwa vikali na Mungu na sasa ni lazima wawe kwamba wamepata funzo na kwa hivyo walikuwa sasa wametii Mungu vilivyo. Lakini hata kaka wayahudi walikuwa wmerudi katika nchi yao, wao hawakuwa huru njisi walivyokuwa wakati Sauli na Daudi. Wao sasa walitawaliwa na Persia na wengine kama warumi baadaye katika siku za Kristo Yesu. Hekalu ambalo walilijenga halikuwa zuri kama lile ambalo lilijengwa na Solomoni. I. Sura za kwanza za vitabu hivi, zinazungumza juu ya ukoo wa Wayahudi hata wale ambao walitoka katika uhamisho. II. Hadithi nyingi zinahusu utawala wa Daudi na Solomoni. 1. 1 Mambo ya Nyakati 10, tunasoma kuhusu mwisho wa sauli kuwa mfalme. Katika smtari wa 13, tunasoma jinsi mfalme Sauli alivyokufa. Alikufa kwa sababui hakuwa mwaminifu kwa Mungu hata alienda kwa mganga badala ya kuenda kwa Mungu. 2. 1 Mambo ya Nyakati 11, tunasoma kuhusu jinsi Daudi akiwa mfalme na utawala wake. 3. 1 Mambo ya Nyakati 16:8-36, tunasoma kuhusu wimbo wa Daudi wa sifa na shukurani kwa Mungu wakati alipokuwa ansherekea kuletwa kwa Sanduka la Agano Yerusalemu. Himiza wanafunzi kwamba ni vizuri kuiga wimbo katika maombi yao. Wahimiza kila wakati kuomba kulingana na neno la Mungu. 4. 1 mambo ya Nyakati 17, tunasoma kuhusu ahadi ya Mungu kwa Daudi kwamba Ufalem wake utadumu milele. Je, hii inafahamika kama Agano gani? Eleza ufalme ambao Mungu anazungumzia kwamba utakuwa wa milele. 5. Mungu hakumkubali Daudi amjengee Hekalu, lakini Mungu alimkubali asaidie katika kutayarisha ujenzi wa Hekalu. 1 Mambo ya Nyakati 22,28 na 29, tunasoma kuhsu kile ambacho Daudi alifanya kuhusu kutayarisha kwa ujenzi wa Hekalu. Daudi alikusanya vifaa ambavyo vingetumika katika ujenzi wa hekalu. 1 mambo ya Nyakati tunasoma kwamba alileta hata dhahabu na fedha. 1 Mambo ya Nyakati 28, tunsoma Daudi akimwagiza Solomomoni mwanawe jinsi anapaswa kulijenga Hekalu na kumtumikia Mungu kwa uaminifu sana. Mstari 20, Solomoni anapata kuhimizwa. Hili ni himizo kwetu wote leo: tuwe hodari na wenye moyo mkuu, kufanya kazi ya Mungu. Tusiogope wala kufadhaika kwa kuwa Bwana, Mungu yuko pamoja nasi jinsi alivyokuwa pamoja na watumishi wake wote katika Biblia. 6. 1 Mambo ya nyakati 29, tunasoma kwamba Daudi alimpenda sana Mungu. Hili linadhihirika wakati alipotoa mali yake kwa sabau ya kumjengea Mungu Hekalu. Pia katika mstari wa 6-7, watu pia walitoa kwa ajili ya ujenzi wa Hekali hili na walifurahi sana kwa sababu waliweza kutoa kwa ajili ya kazi hii. Huu ni mfano mkubwa sana kwetu leo. Hali ya mioyo yetu wakati tunatoa. Biblia iansema kwamba Mungu anampenda yule ambaye anatoa kwa moyo mkunjufu (2 Wakorintho 9:7). Pia Biblia inatuhimza kwamba tumtumikia Mungu hata kwa mali zetu. 7. 1 Mambio ya Nyakati 29:10-19, tunapata mfano mzuri sana jinsi tunapaswa kuomba. 8. Tunafika mwisho wa maisha ya Daudi, lakini hatusikii kutanjwa kwa dhambi ambayo aliyoifanya na Bethsaba au uasi wa Adonija. Hadithi ya 2 Wafalme 11:9-13 hazingumziwi hapa. Kiatbu hiki kimesudiwa kuzungumza juu ya historian a wokovu. Mwandishi alitaka kusisitiza kwamba hata kama wao walikuwa wametenda dhambi nyingio sana na kuadhibiwa vikali sana na Mungu, ahadi za Agano bado zilikuwepo, Mungu bado alikuwa mwaminifu kwa ahadi zake. III. Kuna mambo machache sana ambayo tunasikia kuhusu nchi ya kasikazini katika vitabu hivi. Mafundisho ya vitabu hivi, haswa iko kwa hekalu na ufalme. Haya haswa yanahusu kuabudu Mungu. IV. hatima ya mwisho ya mji wa Yerusalemu: 2 mambo ya Nyakati 36 1. Ktika mistari ya 11-16, tunsoma kwamba mfalme wa mwisho ya Yuda alikuwa mtu mwovu sana. Pia tunasoma kwamba viongozi wote, makuhani na watu watu walikosa kuwa waaminifu kwa Mungu. Pia tunaona kwamba kwa sababu uvumilivu wa Mung, Yeye aliwatumia watu manabii ambao hawakuwasikia na kwa kufanya hivi walikosa kumsikia Mungu. 2. Mistari ya 17-20, tunsoma kuhusu adhabu kali sana ya Mungu kwa watu hawa. Wale ambao walibaki ambao wengi walikuwa maskini walipelekwa katika utumwa huko babeli (2 wafalme 25:12). 3. hata wakati Mungu alikuwa anawadhibu watu, tunaona upendo wa Mungu. Yeye alikuwa anawapatia tumaini la mbeleni. Yeremia aliahidi kwamba uhamisho utachukuwa miaka 70(Yeremia 35:11-12 na 29:10). Uhamisho huu wa Yuda hukuwa wa milele kama nchi ya kasikazini. 4. Katika mistari ya 22-23, tunasoma kumhusu Cyrus ambaye Mungu anamwita mtumishio wake ambaye angewakomboa wayahudi kutoka utmwani. Unabii huu kuhusu Cyrus ulipeanwa miaki 100 ambayo ilikuwa imepita (Isaya 44:28-45:2). KITABU CHA EZRA, NEHEMIA NA ESTA Vitabu hivi vinakamilisha historia ya Agano la Kale. Kitabu cha Esta kiliandikwa wakati wa uhamisho na Ezra na nehemia viliandikwa baada ya uhamisho jinsi watu walivyoishi wakati walirudi katika Yerusalemu. Kwa sasa tunatarajia kuwaona wayahudi wakiishi maisha yao kwa utiifu sana. Kurudi kwa watu baada ya miaka sabini, kulitimiza unabii wa Yeremia na Isaya na Danieli. KITABU CHA EZRA Kitabu cha Ezra kinahusu kurudi Yerusalemu 1. Walirudi wa kwanza waliongozwa na Zerubabeli katika mwaka wa 536 BC. Kulikuwa na manabii wawili ambao walitumwa na Mungu wakati Yuda alikuwa uhamishoni na manaii watatu baada ya uhamishoni. Mungu hatawahi kuwaacha watu wake kamwe katika kuwaongoza katika njia ya haki (Waebrania 13:5). 2. Ezra 1, tunasoma jinsi Mungu alivyomwongoza Cyrus katika kuwakubali watu warudi na pia kuwasaidia na vitu ambavyo walitaka (mistari 1-8). Cyrus hakuwa mtu mkarimu kwa kawadia kulingana na historia. Hii ilifanyika kwa sababu Mungu aliutawala moyo wake (Mithali 21:1). 3. Ezra 2, tunasoma kuhus wale ambao walirudi Zerubabeli akiwa akiwaongoza watu. Zerubabeli alikuwa anatoka katika koo ya Daudi. Ni wachache tu ambao walirudi. 4. Ezra 3, tunsoma kwamba watu walipoanza kujenga hekalu na walikumbana na upinzani na kazi hiyo ikasimama katika mwaka wa 534 BC kwa miaka 14. Wao walianza na madhabahu halafu Hekalu lenyewe. Walijenga madhabahu kwanza ili waweze kuendelea na kutoa sadaka zao. A. Sababu zingine kwa nini kazi hiyo ilisimama ni kwa sababu ya upinzani ambao walikumbana nao. Lakini pia tunaona sababu nyingine katika Hagai 1:4, watu kwanza walijishughulikia wenyewe. Ni lazima Mungu awe wa kwanza katika maisha yetu. 5. Ezra 4:1-3,Tunasoma kuhusu maadui wa Wayahudi amabo walikuja kwa Zerubabeli na kuaomba kwamba wangetaka kuwapa usaidizi katika kujenga Hekalu, lakini Wayahudi walikataa jambo hili na kutii amri ya Cyrus. Kuna mambo kadhaa mabyo tunajifunza kutokana na hili. Kila wakati kazi ya Bwana inapokuwa inaendelea vizuri, lazima upinzani utatolea kutoka kwa adui wetu. Pia tunapaswa kuhakikisha (Warumi 5:10). Kwa hivyi wale ambao walikuja kwa Zerubabeli kwamba wanataka kumsaidia hawakuwa marafikiwa kweli. Mstari wa 2 unasema kwamba wao walikuwa kama wale masameria na walikuwa watu ambao waliabudu miungu. Wao walichanga kuabudu Mungu wa kweli na miungu, na hili halikuwafanya sasa wawe watu ambao walikuwa wanamwabudu Mungu wa kweli. Mfano wa hii ni kuchanganya ukristo na uganga. Mfano mwingine kumkubali mtu ambaye hajaokoka kuhubiri katika makanisa yetu kwa sababu anajua mambo fulani fulani ya dini ya ukristo. A. Wakristo tunaishi katika ulimwengu huu na kwa njia moja au nyingine tunauhusiana na wale ambao hawajokoka. Lakini tunapaswa kujizingatia hali yetu, sisi tumetengwa na ulimwengu. 6. Hawa maadui walifaulu katika kusimamishi kazi ya ujenzi wa Hekalu ahadi mfalme mwingine alipochukua utawala katika Persia. Mfalme Darius aliamuru kwamba Hekalu lijengwe na kwamba hazina ya ufalme wake itolewa katika kusaidia katika jambo hilo. Katika Ezra 6:8, kazi ya ujenzi ilianze tena mwaka wa 520 BC na kumalizika baada ya miaka minne. Manabii wawili, Hagai na Zechariah walimwahimiza watu sana katika kazi hii. 7. Tuzungumza juu ya msaada wa wafalme wa Persia katika kuwasaidia Wayahudi kurejesha maisha yao. Hawa wafalme walikuwa watu ambao hawakuwa wameokoka na walijulikana kuwa watu ambao hawakuwa wakarimu kwa mali yao. Lakini walipeana mali yao katika ujenzi wa mji Yerusalemu na Hekalu. Ezra 7:21-24, tunaona kwamba mfalme alitoa pesa yake kwa ajili ya ujunzi huu na kwamba hata alisema kwamba makuhani walisitozwe kuoda. Hapa Mungu ambaye anaonyesha kwamba Yeye ndiye anatawala kila kitu katika ulimwengu. Yeye aliwasababisha hawa wafalme wachoyo kuwa watu wa karimu kwa kazi yake na watu wake. Leo kuna nchi nyingi ambamo makanisa hayatozwi kondi. 8. Ezra 7, tunasoma kuhusu Ezra akiwa kuhani ambaye alikuwa na juzi katika sheria na ambaye aliwaongoza watu wa Yerusalemu katika kuabudu Mungu kwa kweli. 9. Ezra 9, tunasoma kwamba watu hawakuwa wanamtii Mungu hata baada ya kupitia katika magumu. Ezra alimlilia Mungu kwa maombi. Ombi hili ni moja wapo ya maombi mazuri sana (2-15). Ezra alikiri na kutubu dhambi za watu. Pia alikubali kwamna ni viongozi ambao walikuwa wamewaongoza watu katika dhambi. Haya ni mafundisho mazuri kuhusu jinsi tunapaswa kuja mbele za Mungu tukitubu. Tusona kwamba kufunga kuliambatishwa na maombi. Dhambi kuu ambayo walikuwa wamefanya ilikuwa ni kuwaoa watu ambao hawakuwa Wayahudi. 10. Ezra 10, Ezra anamalizia kuandika tukisikia kwam,ba watu wanakiri na kutubu dhambi yao ya kuwaoa watu ambao hawakuwa Wayahudi na walikuwa kuwaondoa wake hawa. Hatuelezewi nini kilifanyika kwa wanawake hawa na watoto wao. KITABU CHA NEHEMIA Kitabu cha Nehemia kinaendeleza hadithi hii ya Nehemiah akiwasaidia Wayahudi kurejea katika Yuda. Nehemia ni mtu ambaye aliomba sana. Hii ni ishara mzuri ya mtumishi wa Mungu. Mfano wa Nehemia ni utaonyesha tamaa ambayo tunafaa kuwa nayo kwa ajili ya kazi ya Mungu na kwamba hajalishi gharama ni gani, lazima tuendelee kufanya kazi ya Mungu. Nehemia alikuwa na cheo kikuu katika serikali na alikuwa na uhusiano wa karibu sana na mfalme Ahusuero. Nehemia alikuwa tayari kuacha cheo chake na kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kazi ya Mungu. Je, wewe uko tayari? I. Nehemiah 1, tunasoma kwamba Nehemia alipata ripoti kutoka Yuda kwamba mambo hayakuwa mazuri hata kidogo. Ni baada ya miaka kama 90 baada ya kikundi cha kwanza kurudi kutoka uhamishoni kikiongozwa na Zerubabeli na tangu wakati huo kuta za mji wa Yerusalemu hazikuwa zimejengwa. Kumbuka kwamba siku hizo kuta ndiyo zilikuwa zikilinda mji. 2. Nehemia 1:4-11, tunsoma jinsi Nehemia alivyojibu kuhusu huu ujumbe amabo aliupata kutoka Yuda. Tunapaswa kusoma ombi la Nehemia na kuliiga na tujue kwamba kufunga ni jambo zuri la kufanya. 3. Nehemia 2, tunasoma kumhusu Nehemia akimwomba mfalme ruhusa ili arudi Yerusalemu. Akiwa Yerusalem, alikakgua kuta za Yerusalemu na kama kiongozi mzuri alipeana ushauri jinsi ya kujenga kuta hizo. Katika mstari wa 19, tunaona kazi ya adui katika maisha ya Sanbalati na Tobia. 4. Nehemia 4, tunasoam kuhusu Nehemia akiwapanga watu na kazi ya ujenzi ikaendelea. Pia katika surah ii tunasoma kuhusu upinzania ambao uliinuka na jinsi kazi hii ilivyoendelea Wayahudi wengine wakifanya kazi na wengine wakichungawale ambao walikuwa wakifanya kazi. 5. Nehemia 5, tunasoma kwamba Nehemia si tu mtu wakuongoza katika ujenzi lakini pia kiongozi wa kiroho (1-13). Kulikuwa na kiangazi na wengi waliuza mashamba yao na wengine walijiuza katika utumwa kwa wayahudi wenzao ambao walikuwa matajiri. Jambo hili lilimfanya Nehemia akakasirika sana na aliwaambia wale matajiri waache kuwanyanyasa wale ambao ni maskini na wawarudishia mashamba yao. A. Mistari 14-19, tunasoma kwamba alikataa mshahara mkubwa ambao alikuwa amepewa kama gavana wa Yuda. Yeye hakutaka kuwa mzigo kwa watu. Huu ni mfano mwema kwa viongozi wote. Tunapaswa kujitolea kwa watu na wala si kuwanyanyasa. Tuwatumikia na wala si kuwaibia. 6. Nehemia 6, tunasoma kuhusu upinzani ambao hakufaulu. Mstari wa 15 tunasoma kwamba kuta zimekalika kwa siku 52. Huu ulikuwa ushindi mkubwa sana kwa sababu sasa nji wa Yerusalemu ulikuwa unaweza kujilinda kutokana na maadui wake. 7. Nehemia 8-10,tunasoma kuhusu ufufuo katika mji wa Yerusalemu. Katika Nehemia 8:1-3 na 5-8, tunawaona watu wakikusanyika kusoma neno la Mungu. Tunasoma kwamba walisimama siku mzima wakisikiliza maandiko yakisomwa kwao. Kulikuwa na walawi ambao waliwafafanulia kile ambacho kilikuwa kinasomwa. Tunasoma jinsi Nehemia alivyoinuliwa juu alipokuwa akisoma. Hivi ndivyo tunapaswa kulizingatia neno la Mungu wakati linasomwa. Tunapaswa kuliheshimu. Mafundisho yetu na mahubiri yetu yanapaswa kuwa msingi wake ni Biblia. A. Nehemia 9:1-3, tunasoma kwamba watu walikusanyika kumwabudu Mungu. Wao walifunga na kutubu. Katika msitari ya 6-37, tunasoma kuhusu maombi marefu ya toba ya watu. Katika mistari ya 32-37, watu walitambua kwamba Mungu amewashughulikia kwa haki na kwa uaminifu. Wao walitambua kwamba walikuwa wamekosa kuwa waminifu na kwa hviyo walistahili adhabu ya Mungu ambayo walikuwa wamepata. Wao wanazungumza juu ya ukali wa adhabu yao. B. Nehemia 38:9 na Nehemiah 10: 1-39, watu walitengeze makubaliana kwamba wao watamtii Mungu. Hatua ambazo zililete ufufuo ni kufunga, kuomba na kutubu na kumwomba Mungu kwamba amalize adhabu yao kwa sababu walikuwa wameahidi kutii. Hii ndivyo tunapswa kufanya wote. Watu waligeuka na kutoka kwa sanamu na kuwaoa wake wa mataifa memngine na wakawa watu wa sheria. Katika Yesu za Yesu tunawaona Mafarisayo na Masadukayo. 8. Nehemiah 12, tunasoma kuhusu watu wakimshukuru Mungu kwa sababu ya ukuta katika Hekalu. Sasa mambo yalionekana kuwa mazuri kwa Wayahudi. 9. Nehemiah 13, tunasoma kwamba kulitokea shida wakati Nehemia alikuwa amesafiri na kurudi kwa mfalme. Ktika mistari 4-5, tunasoma kwamba Tobia ambaye alikuwa adui wa Wayahud (Nehemia 2:10 na 4:7-8), alipewa nafasi katika Hekalu kuishi humo. Hii ni kinyume kabisa na maagizo ambayo tunayasoma katika mstari 1. Baada ya Nehemia kurudi Yerusalemu, alitatua jambo hili mara moja (6-9). Tunasoma kwamba samani za Tobia zilitupwa nje ya Hekalu. A. Nehemia 13, tunsoma kwamba watu hawakutekeleza ahadi yao kwa Mungu ya kumtii. Nehemia alimaliza muda wake wote akiwasahihisha watu walipokosa kumtii Mungu. Katika mistari ya 30-31, tunasoma maneno ya mwisho ya Nehemia mtumishi wa Mungu. Funzo: Kila wakatika katika nyakati zote na katika kila ahli zote, Mungu amekuwa mwaminifu na anaendelea kuwa mwaminifu kwa ahadi zake. KITABU CHA ESTA Hii ni kitabu cha katika Biblia ambacho kimepewa jina la mwanamke. Hadithi za kitabu hiki, ni za mapema sana kuliko Nehemia. Hadithi zake zinafanyika katika Persia wakati wa uhamisho. Tunsoam jinsi Mungu alitumia Esta kuokoa watu wake kutoka katika mikono ya adui. Katika kitabu hiki hatupati Jina la Mungu, lakini hata hivyo tunawaza kwamba mkono wa Mungu uko unafanya kazi katika kila jambo ambalo linafanyika katika kitabu hiki. Kitabu hiki kinatupatia himizo kwamba Mungu hatakuwa adui awaangamize watu wake kamwe. Kanisa la Mungu litaendelea kuwepo wakati wowote kwa mapenzi ya Mungu. Hadithi za kitabu hiki ni nzuri sana kusoma na kuelewa. 1. Sehemi muhimu ya kitabu hiki ni kwamba Wayahudi walikuwa wametishwa kuuliwa wote. Hili ni jambo ambalo linafanyika katika historia yote. Mungu ataendelea kuwalinda watu wake kila wakati hadi kusudi lake katika maisha ya watu wake litimike. Kanisa liko na adui ambaye kila wakati anataka kuliangamiza kabisa. Watu waovu ambao wanatumika na shetani kila wakati wanapanga kuona kwamba kanisa linaisha. Lakini Mungu ameahidi kwamba shetani hatashinda, anaweza kutatiza, lakini hatashinda. 2. Tunasoma kwamba hatima ya Wayahudi imepangwa na Mungu na wala si mfalme wa Persia. Mungu huwa anawatumia wanawake kwa njia tofauti tofauti kuwabariki watu wake kama vile alivyomtumia Esta. Alimtumia Maria kuwaeleza mitume kwamba Kristo alikuwa amefufuka. Alimtumia Debora kuwaongoza watu wake katika vita. Biblia inaweka wazi kabisa kwamba Mungu amewapatia wanawake majukumu ya kumfanyia (Tito 2:3-5; Waefeso 5:22-24). 3. Wayahudu hadi leo huwa wanasherikia siku ya Purim. Hii ilikuwa siku ambayo walikumba kwamba ndio ilikuwa adui amue ni sku gani Wayahudi wote watauliwa. Siku wanaisherekea kwa sababu Mungu hakuruhusu wauliwe badala yake, maadui wote ndio waliouliwa. Hiki ndicho kilele cha histria ya Wayahudi katika Agano la Kale. Vitabu vingine ambavyotujifunza katikam Agano la kale vinahusu nyakati za matukio ambayo tumeyasoma hadi sasa. Kitabu cha Esta kimegawanywa katika sehemu nne. 1. Mpango wa uovu unaonekani kwa umbali 1:1-2:23. Mungu aliruhusu mambo ili Esta ambaye alikuwa Myahudi awe Malikia ambaye baadaye angewaokoa Wayahudi ili wasiuliwe. 2. Mpango wa uovu unapangwa 3:1-4:17. Mwovu Hamani anamdanganya Mfalme ili ampe mamlaka ya kuwaua Wayahudi wote. Watu walifunga na kuomba. 3. Mpango wa uovu unazimwa 5:1-9:17. Hamani ambaye alikuwa amewpanguia mabaya watu wa Mungu yeye ndiye aliyeuliwa. 4. Watu walisherekea ushindi 9:18-10:3. Hii ndio ilikuwa siku ya purim ambaye Wayahudi wanaisehrekea hadi leo. AYUBU,ZABURI MITHALI, MHUBIRI, WIMBO ULIO BORA Tumemazliza kuona vile vitabu ambavyo vinajulikana kama vitabu vya historian sasa tutatazama vile ambavyo vinajulikana kama vitabu vya mashairi. Wakati mwingine vitabu hivi binaitwa vitabu vya hekima kwa sababu ndani mwake kuna ushauri mwingine. Njia mzuri ya kujifunza Zaburi ni kusoma sura moja kila siku. KITABU CHA AYUBU Ayubu alishi Karibu na wakati Abrahamu. Hiki ni kitabu kizuri cha kujifunza ikiwa unapitia katika hali ngumu ya maisha kwa sababu kitakusaidia kufahamu baadhi ya maswali magumu ya maisha yetu. Kama: 1. Je, haki huwa inashinda? 2. Je, kweli Mungu huwa anayajali maisha ya watoto wake? 3. je, ni kwa nini watu wa Mungu huwa wanakumbana na majaribu makali sana katika maisha yao? Je, ni kwa sababu ya dhambi zao? Ukweli ni kwamba wakati mwingine ni kwa sababu ya dhambi zao na wakati mwingine hapa. Shida kubwa ni kwamba tuko katika ulimwengu wa dhambi. 4. Je, ni mambo katika maisha ambayo ni bora? 5. Je, shetani yupo? 6. Je, kuna maisha baada ya kufa? Haya ndio baadhi ya mambo ambayo tutakuwa tunayaona kwa ufupi katika kitabu hiki. 1. Ayubu 1 na 2, tunasoma kuhus majaribu ya Ayubu. Yeye alikuwa amtu ambaye alimcha Mungu na pia alikuwa tajiri alikuwa maskini sana kwa muda mfupi sana. Shetani alienda kwa Mungu na kumpa Mungu changamoto kwamba Ayubu alimpenda Mungu kwa sababu Mungu alikuwa amembariki na vitu vingi vya ulimwengu. Alimwambia Mungu kwamba ni rahisi sana mtu kumfurahia Mungu kwa sababu hapati shida katika maisha yake. Kwa sababu Mungu alimkubali shetani achukue mali ya Ayubu yote n ahata kuuvamia mwili wa Ayubu na magonjwa. Katika mistari ya 20-22, tunaona moyo wa Ayubu ulikuwa moyo wa aina gani. Kuna wengi ambao huwa wanamwambud Mungu kwa sababu maisha yao yanaendelea vyema lakini shida vinapowakumba, wao humsahau Mungu na huwaza kumwuliza maswali mengi sana kama mweli Yeye yupo. Je hii ni ukweli kwako? Ayubu 2:9-10, tunaona marafiki wa Ayubu wakimshusha moyo. Pia tunaona jinsi Ayubu alivyobaki akiwa mwaminifu hata wakati mke wake alimwambia kwamba amlaani Mungu. II. Sehemu ya pili ya kitabu hiki, 3-38, tunasoma kuhusu kushushwa moyo kwa Ayubu na marafiki wake wakimpa ushauri ambao hakuwa wa kumsaidia hata kidogo. Hawa walikuwa marafiki ambao waliketi naye kwa wiki mzima kabla ya kumwambia lolote. Mateso ya Ayubu yalikuwa makali sana kiwango kwamba katika sura 2:11, marafiki wake hawangeweza kumtambua. 1. Ayubu 3, tunasoma kumhusu Ayubu akilalamikia sana siku ambayo alizaliwa. 2. Ayubu4-27, Marafiki wa Ayubu wanazungumza na kumalaumu Ayubu kwa kujiletea shida hizi zote kwa matendo yake. Ni ukweli kwamba kuna wakati sisi wenyewe tunajiletea shida ambazo tunazipitia. Lakini hili halikuwa hivyo kwa Ayubu kwa sababu yeye hakuwa amefanya lolote baya kusa babisha haya ambayo alikuwa akiyapitia. A. Kwa mfano mtoto wako anavunjika mkono kwa sababu alikuwa anajaribu kuupanda mti. Katika hali hii, makossa ya mtoto wako. Yeye anaumia kwa sababu alikuwa anajaribu kupanda mti ambao hangeweza. B. Tunasoma kwamba mateso ya Ayubu hakusababishwa na baya ambalo Ayubu alikuwa amelifanya. C. Ayubu 28-31, Ayubu anakaana yale yote ambayo marafiki wake walikuwa wakisema na anasema kwamba anasubiri haki ya Mungu ifanyike. III. Mungu alizungumza na kurejeshia Ayubu maisha yake na mali nyingi. 1. Ayubu 38:3, Mungu alimkemea Ayubu kwa sababu ya ujinga na alimkumbusha kwamba yeye ni mwanadamu tu. 2. Ayubu alimanyamaza mbele za Mungu. 3. Mungu alimpa Ayubu changamoto ya kulinganaisha nguvu zake na za Mungu 4. Ayubu 42:2-3, Ayubu alifahamu kwamba Mungu ni muweza nay eye ni mjinga. Katika mstari wa 5-6, anatubu. 5. Ayubu 42:7-17, Mungu aliwakemea marafiki wa Ayubu kwa sababu ya maneno yao na Mungu alirejesha Ayubu katika hali nzuri zaidi kuliko ile ya kwanza. Tunajifunza kwamba ni vyema kuwafariji wale ambao wanaumia badala ya kuwalaumu, haswa ikiwa hatuna uhakika kwamba yale ambayo yamewatukia wameyasababisha wenyewe. Mafundisho kutoka kwa Ayubu: 1. Kubali mateso ambayo Mungu anayaruhusu katika maisha yako bila kulalamika (Warumi 8:28). Kwa sababu Biblia iansema kwamba kwa wale ambao wanampenda Mungu, mambo yote yanafanyika kwa uzuri, kwa wale ambao wameitwa kulingana na kusidi la Mungu. Mungu huwa anatufundisha kumwamini kwa sababu Yeye ni Mungu na si kwa sababu ya yale ambayo anatufanyia. 2. Tunaona kwamba uaminifu wa Ayubu kwa Mungu ulikuwa wa kweli naye Mungu alidhihirika kuwa Mungu mwaminifu. 3. Tunapata funzo kuhusu urahiki. Marafiki wa Ayubu walikuwa watu ambao hawakujali na hawakuelewa jinis ya kuwa marafiki wazuri. Wakati mtu anapokuwa anaumia, siyo wakati mzuri wa kuanza kumkubusha kuhusu mabaya yake. Hii haimaanisha kwamba hatufain kuwaambia watu kuhusu dhambi zao, lakini ni vyema kuzingatia jinsi tunavyosema ukweli huo. Isiwe kwa njia ambayo ni ya kuwaumiza kabisa. Tunapaswa kusema ukweli kwa njia mabyo watasaidika na kuhimizwa. 4. Tunafundisho kuhuus uchungu na mateso. A. Je, ni kwa nini watu wa Mungu huwa wanateseka na wale ambao hawajaokoka wananawili tu katika maisha yao? i. Marafiki wa Ayubu walipeana jibu baya kwa swali. Walisema kwamba mateso ni hukumu ya Mungu kwa wale ambao wanafanya dhambi. Ni kweli kwamba wale ambao hawajaokoka watateseka sana wasipotubu na kuwamini Kristo. Huko Jahanum mateso yao yatakuwa ya kila siku. Lakini humu duniani, hata wale ambao tumeokoka tutateseka, kwa sababu Mungu anatumia mateso haya kwa uzuri wetu. Mateso ya mkristo si lazima yawe yametokana na dhambi. ii. Elihu alipeana jibu sahihi. Alisema kwamba mates ohayo yalikuwa nji ya Mungu kumfundisha, kumwadhibu na kuboresha maisha ya Ayubu. iii. Jibu la kluhusu mateso ni, ni njia ya kutujaribu kama tunamwamini Mungu jinsi alivyo na si kwa sababu ya yale ambayo ametufanyia. KITABU CHA ZABURI Barua za upendo kutoka kwa Mungu kwa kanisa lake. Kuna watu kadhaa ambao wameandika kitabu hiki, Daudi akiwa mmoja wao ambaye amaeandika zaidi ya nusu ya kitabu hiki. Zaburi inajumlishi hisia nyingi za wanadamu; huzuni na furaha. Zaburi zimenukuliwa mara 166 katika Agano Jipya. Nyingi ya zaburi zinatuelekeza katika kumwabudu Mungu kwa njia ambayo inapaswa. Zaburi hizi ni tofauti: 1. Zaburi za Kufundisha=Zaburi ambazo zinafundisha jinsi ya kuishi maisha (1, 5, 7, 15, 17, 50, 73, 94, 101). 2. Zaburi za Historia= (78,105,106,13) 3. Zaburi za sifa = (106, 111-113, 115-17, 135, 146-50). 4. Zaburi za Toba = (6, 32, 38, 51, 102, 130, 143). 5. Zaburi za dua au sala au maombi = (86). 6. Zaburi za shukurani = (16, 18). 7. Zaburi kumhusu Yesu = (2, 20-24, 41, 68, 118). 8. Zaburi kuhusu asili = (8, 19, 28, 33, 65, 104). 9. Zaburi kuhusu hija. Yaani wakati ambapo watu walikuja Yerusalem kuabudu = (132-140). 10. Zaburi kuhusu laana = (35, 52, 58, 59, 69, 83, 109, 137, 140). Tuone mifano kadhaa 1. Zaburi za kufundisha (Zaburi 15). Tunasoma kuhusu ni mtu wa aina ambaye anakaribishwa na Mungu. Mistari ya 2-5, tunsoma kuhusu tabia ambayo inafaa. 2. Zaburi za sifa (Zaburi 113). Inatufunza kuhusu kumsifu Mungu. 3. Zaburi ya toba (Zaburi 32). Mistari ya 1-4 tufundishwa kwamba ni wale tu ambao wamesamahewa ndio wako na futaha ya kweli. Mistari 5-11, tunasoma kuhusu toba na mstari wa 11 tunfunzidhwa kuhudu furaha ya kweli. 4. Zaburi 86, tunfundishwa jinsi ya kumwomba Mungu jambo kwa nji ambayo ianalaswa. 5. Zaburi 16 tunafundishwa jinsi tunapaswa kumshukuru Mungu. 6. Zaburi 2, tunasoma kuhusu mfalme ambaye ni mwanadamu, lakini mfalme huu anatimilika katika Kristo Yesu. Mistari mingine inazungumzia mfalme Daudi na ingine kama wa 7, unazungumza kumhusu Yesu Kristo. Zaburi 22, ni zaburi ambayo inazungumza kumhusu Kristo. Zaburi hii inazungumza kumhusu Kristo akiwa mslabani. Mstari 1, tunasoma maneno ambayo Yesu Kristo alaiyazungumza miaka nyingi sana baadaye akiwa msalabani (Mathayo 27:46). 7.Zaburi 109, hii inazungumza kuhusu laana kwa mtu kama mganga. Msitari ya 6-11, tunsoam kwamba mwandishi anaomba kwamba Mungu amwondolee adui wake. Wakristo wengi huwa tunatatizwa na zaburi hizi. Katika mistari hii, tunaona kwamba mwandishi anaomba Mungu amhukumu adui. Tunapaswa kumwomba Mungu kila wakati kutuongoza na kutusaidia wakati tunakumbana na maadui wetu. Zaburi 23, zaburi hii, ni zaburi ya faraja sana kwetu leo. Tuisome pamoja. KITABU MITHALI Nyingi za Mithali ziliandikwa na mfalme Solomoni na zingine na mfalme Hezekia na zingine na waandishi wengine. Mithali ni inamaana kufundishi ukweli. Mithali hizi zinagumza juu ya kila jambo katika ulimwengu huu. Mitahli hizi ni mashauri mazuri, lakini siyo ahadi. Kusudi lake ni kutuhimiza tuishi maisha matakatifu mbele za Mungu. Nyingi ya mithali hizi ni rahisi kufahamu na pia kuna zingine ambazo ni ngumu kuelewa. Kuwa mwanagalifu sana jinsi unavyojifunza Mithali hizi. Hufai tu kuzisoma na kuzichukua hivi, lazima utafute maana ya mitahli ndipo utajifunza vyema na kujengwa. Mithali 22:22-25, tunajifunza kwamba ni lazima tuwe wangalifu ni nani ambaye tunafanya urafiki naye. Kuna mithali ambazo ni rahisi kuelewa kama Mithali 9:10 na 1:7 ambazo zinahusu hekima. Mithali nyingi ni ushauri kwa vijana kama (Mithali 1:8-10, 3:11, 5:20, 10:5), na nyingine nyingi. Ziko na maagizo mazuri sana juu ya jinsi vijana wanapaswa kuishi maisha yao na kuepeuka na shida nyingi za maisha. Mithali zingine zinahusu dhambi, uaminifu, watu waovu, mahusiano ya kijamii, na mambo mengine ambayo tunaweza kumbana nayo katika maisha yetu. Tutamalizia hapa masomo yetu kuhusu kitabu cha Mithali kwa sasa. Hakikisha kwamba unasoma kitabu hiki. KITABU CHA MHUBIRI Hiki ni kitabu kingine cha hekima. Haijulikani kabisa ni nani ambaye aliandika kitabu hiki isipokuwa wengi wamekihushisha na Solomoni. Aliishi maisha yake kwa njia ambayo kitabu hiki kinaeleza hisia zake wakati alipokaribia mwisho wa maisha yake. Tunasoma kumhusu mtu ambaye alishushwa moyo sana kwa jinsi alivyoishi maisha yake. Tunajua kwamba Solomoni alianza maisha yake kwa nji mzuri sana akiwa na ahadi nyingi kutoka kwa Mungu. Mungu alimpa hekima na utajiri. Solomoni hakutosheka, yeye alitafuta mali nyingine nyingi na aliabudu miungu mingine. Mwisho wa maisha yake alifahamu vyema kwamba maisha yake bila Mungu yalikuwa maisha bure. Yale ambao ni ya milele, ni yale ambayo tunafanya kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Hili ni fundisha ambalo watu wengi huwa hawajifundishi ahadi wakati wa mwisho wa maisha yao. Mambo ambayo tunajitahidi katika ya ulimwengu huu ni bure; manyumba, vyeo, utajiri, masomo na mambo mengine mengi ni bure. Je, ni nini ambacho tutatoka nacho humu duniani? 2 Timotheo 4:8, tunsoma kuhusu taji la haki ambalo Yesu atawazawdia wale wote ambao wameokoka tutakapoingia mbinguni. Taji hili litakuwa kwa sababu ya kuwa waaminifu kwake. Huku mbinguni tutakuwa na ushirika na watu ambao tuliwaambia kuhusu Yesu na wakaamini. Tutazame mafundisho ya kitabu cha Mhubiri. I. Kuna maoni ya aina mbili kuhusu maisha. Moja ya maoni hayo ni ya wanadamu ambao hawajaokoka. Maonni mengine ni ya wale ambao wameokoka. Kusudi la Mhubiri ni kutuonyesha hatari ya kufuata vitu vya ulimwengu huu. Pia kutonyesha kwamba chanzo cha furaha ya kweli ni Mungu. 1. Chochote mwanadamua anatafuta bila Mungu anamaliza wakati wake bure. 2. Ni Mungu pekee ambaye anafanya maisha na kazi za mwanadamu ziwe na umuhimu. II. Ubatili. 1. Aina ya ubatili: Hekima ya mwanadamu 2:15-16 Kazi za mwanadamu 2:19-21 Kusudi la Mwanadamu 2:26 Tamaa ya mwanadmu 6:9 Ubinafsi wa mwanadamu 4:4 Uchoyo wa mwanadamu 4:8 Tuzo za mwanadamu 8:10, 14. Umaarufu wa mwanadamu 4:16 Kutotosheka kwa mwanadamu 5:10 Ubembelezi wa mwanadamu 7:4 Mhubiri 12:9-14, kila mwanadamu anaishi na kuwepo kwa nguvu za Mungu. Mhubiri 12:13, tunasoma kwamba, “Hii ndio jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa: mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.” Hii ndiyo sababun ya kusihi kwa mwanadamu. Kumtii Mungu ni kuwa mwanadamu na kuweza kuyafikia malengo yote ambalo ndilo kusudi la kuumbwa kwetu. Kwa ufupi ni kwamba, tania yetu kama wanadamu inapaswa kuwa uhusiano na Mungu. WIMBO ULIO BORA Huu ni wimbo wa mapenzi, mstari wa kwanza utaueleza kwamba unahusu mfalme Solomoni. Kuna wale ambao wanaona wimbo kama kati ya Mungu na watu wake Israeli. Wengine mimi, tunauona kama wimbi kati ya wanaopendana ambao wameumbwa katika mfano wa Mungu. Hiki kitabu kinatuonyesha kwamba Mungu anajali jinsi tunavyoishi maisha yetu. Uhusiano kati ya mume na mke ndio uhusiano ambao unafuata ule wa kristo na kanisa lake. Ndoa takatifu huwa inamletea Mungu utukufu na ni mahali pazuri kuwalea watoto wa Mungu. Wimbo Ulio Bora 4:1-5, tunaona kwamba hivi ndivyo ilivyokuwa wakati kijana alimtamani msichana katika nyakati hizo. Kuna watu wengi ambao wako na haya ya mambo ambayo yamo katika kitabu hiki. Mungu anasema kwamba mapenzi ni kitu kizuri sana kati ya mume na mke. Mafundisho muhimu: Kizazi cha leo kinajihusisha mambao ya kufanya mapenzi wakati ambapo haifai kwao na kwa sababu hii, wengi wamejiletea shida nyingi sana. Kitabu hiki kinatuonyesha kwamba Mungu ndiye aliumba hali ya kufanya mapenzi na kwamba ni kitu kizuri Sanaa machoni pa Mungu. Mume na mke wanapofanya mapenzi huwa wanafurahia baraka ya Mungu katika ndoa yao. Kumbuka kwamba mapenzi ni kati ya mke na mume. Ndoa inafannya watu wawili mume na mke waje karibu sana (Mwanzo 2:24). Hakuna uhusiano mwingine ambao wanapaswa kuwaleta mume na mke pamoja kama ndoa. Katika uhusiano huu hakuna aibu (Mwanzo 2:25). Kitabu hiki tunatufundisha kwamba mume na mke wanatoshelezana katika uhusiano wao katika ndoa. Kitabu hiki kinatufundisha kwamna ndoa ni kitu kitakatifu na kwa hivyo wale ambao wako katika ndoa wanapaswa kufurahiana na kuja pamoja bila aibu yoyote kwa sababu Mungu amewabariki sana. Kumbuka kwamba ushoga, yaani wanaume na waume kuoan au kufanya mapenzi ni dhambi mbele za Mungu. Ndoa kati mwanamke na mwanamke au kufanya mapenzi kati ya mwanamke na mwanamke ni dhambi mbele za Mungu. Kufanya mapenzi kabla ya kuoa au kuolewanje ni dhambi mbele za Mungu. Kufanya mapenzi nje ya ndoa ni dhambi mbele za Mungu. VITABU VYA MANABII. Sehemu kubwa na muhimu ya mwisho ya Agano la Kale ni manabii. The last major section of the Old Testament is the prophets. Mpangilio wa vitabu haumaanishi hivyo ndivyo matukio yanavyofuatana lakini hata hivyo ujumbe wa vitabu hivi unaashilia kwamba Mungu anatupenda. Baada ya mwanadamu kuchagua kutenda dhambi, yeye alianza vita na Mungu na alifanyika mwana wa jahanum. Mwanadamu hakuweza kujifanyia lolote kwa hivyo Mungu alimtumia manabii kumwezesha mwanadamu atoke katika dhambi na arudi kwa Mungu. Hili halikufaulu na tumaini la mwanadamu sasa ni moja tu, Kristo Yesu. Kazi ya nabii ni zipi? 1. Wanazungumza neno la Mungu la sasa: Walimu wa Biblia wa leo, hii ndio kazi yao. Wao hawazungumzi katika maisha ya mbeleni. 2. Kutabiri: Wao walitabiri maisha ya mbeleni. Wao walitabiri kuja kwa Kristo. Kumbuka kwamba hawakuona ya mbeleni na amara mingi hawakujua kile ambacho kile ambacho walikuwa wanasema (2 Petro 1:20-21;Dan. 12:8-9). Vitabu hivi vya manabii huwa havisomwi na wengi . Wachungaji na walimu wengin wa Biblia huwa hawasomi vitabu vya manabii. Ninasema hivi kwa sababu: Sababu ya kwanza, ujumbe wa manabii ni mgumu kukubali ulikuwa umejawa na onyo kwa sababu ya dhambi. Sababu nyingine ni kwamba ujumbe wa manabii mgumu kuelewa. Ujumbe wa manabii unastahili kusomwa na kujifunza kwa sababu unamafundishio mengi sana kwetu leo. Wakati unaposoma vitabu vya manabii hakikisha kwamba unafahamu wakati ambapo manabii hawa walikuwa wakitoa unabii wao na ni wapi walikuwa wautolea na walikuwa wakiwaelezea kina nani. Wakati mwingine ninajua kwamba inaweza kuwa vingumu sana kujua wakatio na mahali. Kuna wale ambao tunawajua kama Yeremia tunajua kwamba alikuwa manabii kwa Yuda alizungumza wakati wa kabla na wakiwa uhamishoni Babeli. Mambo muhimu kuwahusu manbii 1. Kuna manabii wengi ambao hatuwajui kwa sababu hawajatajwa katika Biblia kwa majina lakini wametajwa tu katika vifungu (1 Samweli 10:5). Kuna wengui kama hawa. 2. Manabii wengine wametajwa katika vitabu tofauti vya Biblia kama: Elijah I Wafalme 17:1, Elisha Nathani na Moses. Lakini wengine wao hawajaandika kitabu chochote cha Biblia. 3. Kuna wale ambao waliandika vitabu na vitabu hivyo vinaitwa majina yao kama: Isaya, Yeremia na Amosi. 4. Kuna wale ambao wanaita manabii wakuu kwa sababu ya urefu wa vitabu vyao ambavyo wameviandika. Hawa ni kama Isaya , Yeremia,Ezekieli na Danieli. . 5. Kuan wale ambao tunawaita manabii wadogo kwa sababu ya ufupi wa maandishi yao kama Yona, Hagai, Mika na wengine. 6. Kila maandiko ya nabii ni ya muhimu sana haijalishi kwamba ni marefu an mafupi. 7. Je, unaweza kujua kama nabii ni wa ukweli au ni wauongo? A. Je, ujumbe wake unaambatan na mafundisho ya Biblia? Nabii wa ukweli hatawahi kuleta ujumbe ambao ni kinyume na neno la Mungu (Biblia). Kwa mfano nanbii wa ukweli hatawahi kusema kwamba ana ujumbe ambao ni kinyume na amri ta Mungu: “Mungu amesema umwache mume wako na uoleke kwa mwingine.” Huu ni uongo kwa sababu Mungu anasema aqnachuki talaka. B. Je, yale ambayo amesema yametimika? Kuna adhabu kali sana kwa manabii? Kumbukumbu la Torati 13:5 au 18:20). Ujumbe wa manabii kuna wakati ambapo unakuwa mgumu sana kuelewe. Wakristo wengi huwa hawasomi vitabu hivi kwa sababu mara kwa mara unahitaji kusoma kwa bidii. Bidii hii ni mzuri kwa sababu utapata kuelewa vyema ujumbe wa vitabu hivi. Ustarajie kufahamu kila kitu kwa haraka, soma pole pole na utaelewa. Mwombe Roho Mtakatifu akusaidie kukufunza neno la Mungu. Leo hatuna tena manabii ambao wanatabiri (Ufunuo 22:18-19 na Deut 4:2). Je leo Mungu anazungumza nasi kwa njia gani? Jibu ni, kupitia kwa Neno lake (biblia). Mada kuu katika vitabu vya manabii 1. Majukumu ya wana wa Agano: Mungu anatarajia utiifu kutoka kwa wale ambao ni watoto wake. Anawahimiza kwamba wakumbuke Mungu ni nani nay ale ambayo ameyafanya. Wao wanaitwa kuishi maisha matakatif ambayo yanamletyea Mungu utukufu. A. Manabii waliwahubiria watu wamrudie Mungu na neno Lake. B. Manabii waliwahubiria watu wakumbuke kwamba Mungu amewaita na kuwatenga kutoka katika dhambi na kwamba walihitaji kuishi maisha matakatifu. Wao walikuwa waishi maiasha ya kwa utukufu wa Mungu. C. watu walihitajika kuishi kwa Amani. Kanisa linafaa kuwa Amani miongoni mwa washirika wake. 2. Maada nyingine ni siku ya Bwana: Hii ni siku ambayo Mungu atahukumu ulimwengu. Hii inamaansiha mambo mawili. A. Hukumu ya Mungu wakristo. Mungu anasema kwamba wale ambao wanakataa kutubu dhambi ambayo bado imo ndani mwao, atawadhibu. B. Wokovu ni kwa watu wa Mungu ambao watatakaswa. Siku ya Bwana itakapofika, wenye dhambi watahukumiwa na wale ambao ni waaminifu watazawadiwa. 3. Mada nyingine kuja kwa Masiya ambaye ni Kristo. A.Kuna utabiri mwingi na ufafanuzi mwingi kuhusu Kristo katika vitabu vya manabii. KITABU CHA ISAYA Isaya alitabiri sana kumhusu Kristo Yesu. Pia alizungumza kuhusu hukumu ambao unakuja. Yeye alitabiri kwamba Israeli wangevamia na kuadhibiwa na maadui wao. Haya mambo yote yalifanyika hata kama yalichukua muda merefu kutimika. Kwa mfano jina la Cyrus lilitajwa miaka mingi sana kabal aya kuzaliwa kwa Cyrus mwenyewe. Wakati unasoma kuwahusu manabii, ni jambo la maana sana kuhakikisha kwamba unafahamu ni wapi walikuwa wakati walikuwa wanatabiri na ni wakati gani walitoa unabii huu. Kwa mfano Isaya alikuwa nabii kutoka Yuda ambaye alitabiri wakati wa mfalme Uzia, Yotam, Ahazi na Hezekia. Wakati wake Isaya, Yuda ilkuwa imeendelea kiuchumi sana na wazi kwamba mara kwa mara wakati watu wananedelea katika maisha yao huwa wanajaribiwa kumwaacha Mungu kwa sababu ya utajiri ambao huwa wanaufurahia sana. Kwa mfano unapotazama mataifa mengo ambayo yameendelea kiuchumi, utapata kwamba wao hazingatia kamwe njia za Mungu au Mungu mwenyewe. Wakati Isaya alipokuwa anamalizia huduma wake, nchi ya Yuda ilikuwa imeanza kufifia kiuchumi. Ni lazima wote tuwe waangalifu sana. Utajiri huwa unawatoa wengi kwa Mungu. Maisha yanapokuwa mazuri sana kwa watu, watu huaza kuishi maisha ya anasa na ya kujifurahisha tu katika vitu vya ulimwengu. Wakati wanapofanya hivi, wao huwa wanamwasi Mungu kwa kuacha njia zake na neno lake. Isaya 1-39, sura hizi, tunashughulikia dhambi ya Yerusalemu na mataifa ambayo yaliwazingiria. Katika sura hizi, ujumbe mkuu ni hukumu ya Mungu. Katika Agano la Kale, Mungu alifanya kazi na Wayahudi lakini pia alijidhihirisha kwa mataifa mengine kwamba Yeye ni Mungu ambaye anatawala ulimwengu wote. Unabii wa Isaya, ulikuwa umekusudiwa katika sura hizi kuwaonya watu. Tutazame Isaya 1 na tuone mpangilio wa ujumbe huu. 1. Isaya 1:1, tunasoma kuhusu wapi Isaya alikuwa na ni watu wa aina gani alifanya kazi nao. 2. Isaya 1:2-9, tunasoma kuhusu orodha ya dhambi ambazo watu walikuwa wamefanya na adhabu ya Mungu kwa watu hawa. Mungu aliwaeleza kwamba wao walikuwa wamefanya dhambi na dhambi yao ilkuwa kwamba walikuwa wamem,wacha Mungu. Isaya anandika akiwaonya watu kuhusu kuabudu sanamu badala yake walikuwa waabudu Mungu. Isaya aliwaambia watu kwamba Mungu alikuwa amekasirika nao. Kulingana na maandisha ya Isaya, tunaona kwamba Isaya alikuwa mtu ambaye alikuwa amesoma sana. Ktika mstari wa 3, anawaambia kwamba ng’ombe anamjua bwana wake, naye punda anajua hori la mmiliki wake, lakini isreali hajui Bwana wake. 3. Isaya 1:10-15, Mungu anasema kwamba kuabudu kwa waisraeli hakukubaliki naye kwa sababu mioyo yao ilikuwa mbali sana Naye. Katika mstari wa 15, Mungu alitisha kuwaacha kabisa. Hili lilikuwa tisho kali sana na tunafaa kuogopa sana ikiwa Mungu atasema hivi kutuhusu au kuhusu nchio yetu. Katika 2 mambo ya Nykatai 7:13-14, tunasoma kuhusu kile ambacho kunafanyika wakati Mungu ametoa baraka zake mahali na kile ambacho kinafanyika wakati watu wake wanatubu dhambi zao. 4. Isaya 1:16-19, Mungu anawaita watu watubu na kugeuka kutoka katika dhambi zao na kufuata Mungu. Kuna baraka nyingi ambazo Mungu anaahidi wale wote ambao watageuka na kutoka katika dhambi zao na kumgeukia Mungu. 5. Mistari ambayo inabaki katika surab ya 1, inaeleza kwamba Mungu atawabarikiwa tu wake. Huu ndio ujumbe wetu leo. Mungu atawabariki wote na baraka zoet za kirohoni (Waefeso 1:3-4)wale ambao wanageuka na kutoka katika dhambi zao na kumgeukia Mungu kupitia kwa Imani ndai ya Kristo Yesu. Mungu ameahidi baraka za milele kwa wale wote ambao watamwamini Kristo (Yohana 3:16). Wakati mwingine unaweza kupata ujumbe wa isaya ni mgumu kuelewa kwa sababu matokeo yake hayafuati mpangilio. Kwa mfano usiwaze kwamba kila jambo lilifuatana jinsi limfuatana katika Biblia. Katika sura ya 6, tunasoma Mungu akimwita Isaya kuwa nabii. Kwa kawaida unaweza kuwaza kwamba surah ii ndio ilifaa kuwa ya kwanza. Nimeanbiwa kwamba sababu yah ii ni kwamba , Isaya alipozungumza, maneno yake yaliandikwa na kubandikwa kwa Malanga ya mjii ili watu wasome. Baadaye maandishi haya yalikusanywa na kuwekwa katika kitabu kimoja. Kwa sababu hayakuwekwa katika mpangilio sawa sawa. Isaya 6, tunasoma kuhusu kuitwa kwa Isaya awe nanbii. Katika mstari wa 5, tunaosma kwamba Isaya alimwona Mungu. Je, unakumbuka kile ambacho tulijifunza wakati Musa alimwona Mungu? Je, hii inaitwaje? Hii inajulikana kama Mungu kujitambulisha kwa mwanadamu (Kutoka 3:2-6). Je, baada ya Isaya kuona maono kuhusu Mungu alifanyaje? Majibu ya Isaya ndio yanafaa kuwa majibu yetu leo kila waktai tunawaza juu ya Mungu na wakati tunasikia ujumbe kutoka katika neno lake. Tunafaa kujawa na heshimu na uchaji Mungu. Tunapaswa kuneynyekea na kuomba huruma kwa sababu sisi ni wenye dhambi na Mungu ni mtakatatifu. and our wretched sinfulness. 1. Katika mstari wa 6-7, tunsoma kwamba Isaya alisafishwa modomo yake na Mungu. Hivi ndivyo Mungu huwa anatufanyia, Yeye hutusafisha dhambi zetu wakati wakati tunakuja kwake. Hakuna mwandamu ambaye anaweza kujiosha dhambi . Biblia inafundisha kwamba ni Mungu pekee kupitia kwa Kristo Yesu ambaye anaweza kutuosha. Msamaha wa dhambi unakuja kupitia kwa Kristo Yesu. 2. Baada ya Isaya kusamehewa na kuondolewa dhambi, Mungu alimwuliza swali ambalo anamwuliza kila mtu ambaye ameokoka. Nimetume nani? Isaya alimjibu, Mimi hapa. Mungu ametuokoa ili tuweze kumtumikia.njia moja ya kumtumikia Mungu ni kueneza ujumbe wa Injili kwa watu wote. Lakini his is njia ya pekee. Mungu amewaita wengi na amewapatia majukumu tofauti tofauti katika kanisa lake. Kuna wale ambao ni wahubiri, wengine ni mashamanzi, wengine wa kuhimiza wengine kusafisha na wengine usaidizi. Kila mmoja wa hawa anafanya kazi ya Mungu na kwa hivyo kila mmoja anapaswa kufurahia mwito wake. 3. Tunasoma katika sutra hii kwamba, huduma wa Isaya hakuwa huduamwa kufaulu na ulikuwa wa muda mrefu sana. Isaya alikuwa nabii kwa miaka 65. Mashahid wanasema kwamba mfalme Manase alimwua Isaya. Ujumbe wa Isaya haukupokelewa na watu, watu walikataa kumtiii Mungu. Lakini hata hivyo Isaya aliendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu. Maisha yake yanapaswa kuwa mfano kwetu leo. Kuna wakati ambapo tutafanya kazi ya Mungu lakini watu watakataa kumwamini Mungu, watakataa kuokoka. Wakati mwingine wakakosa kuwa wenye kushukuru n ahata wakati mwingine watumishi wa Mungu watauliwa. Tusishangae, mioyo ya watu ni mwiovu sana. Lakini hata hivyo tunapaswa kuendelea kuwa waminifu kwa Mungu katika mwito wetu. Isaya alifahamu kwamba Mungu ni mtakatifu naada ya kuona moano hayo. Jambo hili lilidhidhiri hata katika maandisha ya Isaya. Isaya anatumia “Mtakatifu wa Isreai zaidi ya mara 25 kufafanua Mungu. Tunapaswa hata sisi leo kuiga mfano wa Isaya wa kufahamu Mungu kama Mungu mtakatifu kwa sababu hili litaongoza jinsi tunavyoishi maisha yetu kama wakristo na jinsi tunavymtumikia Mungu. Tutazame badhi ya mifano ya ujumbewa Isaya. Isaya 5:1-7, Mungu anzungumza kuhusu shamba la mizabibu ambalo amelitunza vyema. Mstari wa 2 tunasoma kwamba aMungu alitarajia kuvuna mizabibu mizuri lakini badala yake alivuna mizabibu mibaya ambayo haistahili kuliwa. Kwa sababu hii Mungu anasema katika mstari wa 5, kwamba ataondoa ulinzi wake na katika smtari wa 6, anasema kwamba ataachilia hukumu. Katika mstari wa 7, tunasoma kwamba Mungu anungumza kuwahusu watu wake. Mistari mingine katika surah ii inazungumza kuhusu hukumu kali ya Mungu. Katika surah ii, hatusikii mwito wa kutubu na kuepwa baraka kama katika sura zingine au vifungu vingine. Mungu hakuwapatia nafasi nyingine. Hii ni onyo kali sana kwa sisi soet leo. Ikiwa Mungu anaendelea kutuita kutoka kwa dhambi kila wakati akiwatumia wahubiri wa neno lake na tunakaa kutubu, Mungu siku moja atafunga mlongo huo na milele wale ambao wamekataa watafungia nje ya Ufalme wa Mungu. Tuwe waangalifu sana wakati tunasikia ujumbe wa neno la Mungu. Tusiupuuze4 hata kidogo. Isaya 19, tunasoma kuhusu unabii juu ya Misri. Katika smtari wa 1-3 tunsoma kwamba wao walikuwa na hatia ya kuabudu sanamu na uganga. Mungu alitangaza hukumu kwa sababu ya dhambi hizi. Katika mistari ya 16, tunaona kwamba watu wa misri walimkiri Mungu (Zaburi 111:10). Katika mistari ya 18-21, tunsoma kuhusu mazungumzo kati ya watu wenyewe. Mstari wa 22 tunsoma kwamba atawaponya watu baada ya wao kufanyaika watoto wake. Katika mstari wa 25, Mungu alitangaza baraka juu ya wake wake wa misri. Kanisa la kwanza lilikuwa na nguvu sana huko misri na hadi leo kuna wati wake huko. Isaya 40, ujumbe ulibadilika kutoka kwa hukumu kwa faraja. Katika isaya 40:1, tunsoma kuhusu Isaya akzungumza na watu kutoka mbali ambao wanateseka. Jambo hili la faraja kutoka kwa Mungu linfaa kuhimiza kila mkristo. Mungu ana nguvu sana za kutufariji na anatuipenda (Yohana 3:16-17). Wale ammba tumeokoka tunasababu ya kuwa na furaha kila wakati kwa sababu tuko katika uhusoano na Mungu. Isaya pia alitabiri kuhusu siku za mwisho. Katika Isaya 65:1-7, tunsoma kuhusu akiahid hukumu kwa wale wote ambao wanakataa kumtii. 65:17-25, tunasoma kuhusu baraka za Mungu kwa wale ambao wanamtii. Isaya 57, tunsoam kuhusu hatima ya wale ambao wanamtii Mungu na wale ambao wanaklataa kumtii Mungu. Mistari ya 1-2, tunasoma kuhusu hatima ya wale ambao wanamtii Mungu. Isaya anasema kwamba kwa hawa watu, kuna Amani na kupumzika. Mistari ya 20-21, tunsoma kwamba hakutakuwa na Amani kwa wale ambao wanakataa kumtiii Mungu. Isaya 58, surah ii inahusu kuabudu. Katika mistari 1-2, tunsoma kwamba Mungu anakatalia mbali kuabudu kwa Waisraeli kwa sababu wao wanamwabudu ilhali bado wako katika dhambi zao. Mistari ya 3-6, tunafundishwa kuhusu kufunga. Katika mistari ya 8-14, Mungu anawaambia kwamba atafurahia sana nao ikiwa watamwabudu wakati huo huo wakiishi maisha matakatifu. Kuna unabii mwingi sana katika Isaya kumhusu Kristo Yesu. Katika kitabu cha Isaya, tunaona wai kabisa mateso ya Kristo ambayo yalitabiriwa miaka 700 kabla ya kuja kwa Kristo Yesu. Wayahudi walisoma kitabu hiki na kukataa mambo ambayo yalikuwa yanamhusu Kristo. Hili ni dhihdirisho kwamba wale wote ambao wanamkataa Kristo, ni watu ambao wamepofushwa sana na shetani. Yeyote ambaye anakisoma kitabu hiki, ataona wazi kabisa unabii huu ambao ulitimika katika Kristo. Yeye ataona kwamba kweli kristo ndiye Mesiya. Kwa mfano: 1. Isaya 7:14, tunsoma kuhusu bikira ambaye angemzaa mtoto na mtoto huyo angeitwa Imanueli, nyaani Mungu yuko pamoja nasi. Katika Luka 1, tunasoma kumhusu bikira huyu ambaye aliitwa Maria. Katika Biblia yote hakuna bikira mwingine ambaye tunasoma kuhusu ambaye alipata mtoto. Unabii huu ulitimia katika Kristo Yesu. 2. Isaya 9:1-7, tunasoma kuhusu utawala wa Kristo (6-7) ambao ndio utawala bora. Isaya pia alitabiri kuhusu utawala mbaya ambao Mungu angeruhusu miongoni mwa watu wake kama njia ya adhabu kwa sababu ya kutomtii. Hili halizungumzii Kristo, ni watawala wa dunia. 3. Isaya 11:1-17, tunsoma kuhusu shina la Yesse ambaye alikuwa baba wa Daudi. Shina hili ni Kristo ambaye alitoka kwa koo ya Daudi na ambaye aliitwa mwana wa Daudi. Mungu alikuwa amemwahidi Daudi kwamba mfalme wake utakuwa wa milele (2 Samweli 7:16). Ahadi hii ilizingatia Kristo na wala si Solomoni ambaye alikufa na ufalme wa Israeli haupo tena. Ni Ufalme wa Kristo ambao ni wa milele (1 Petro 1:11). 4. Isaya 42:1-7, tunsoma kifungu ambacho kinajulikana kama moja wa vifungu ambavyo vinaeleza kazi ya Kristo. Katika mstari wa 2-3, tunsoma kwamba Yeye anatakuwa mtawala mpole. Mistari ya 2-3, tunsoma kwamba Yeye atawaponya vipofu wa kiroho n ahata wa kimwili. 5. Isaya 49:1-7 na 50:4-11, pia tunsoma kumhusu Kristo ambaye angekuwa mtumishi (Marko 10:45). 6. Isaya 52:13-53:12, hivi ni vifungu wazi kabisa kuhusu kazi ya Kristo Yesu. A. Isaya 52:13, tusoma kwamba Kristo atatukuzwa na anainuliwa juu sana na atakweza wafalme wa dunia. B. Isaya 53:1-3, Kristo alikataliwa na watu na alikuwa mtu mwenye huzuni. C.Isaya 53:4-6, Kristo aliteseka kwa ajili yetu na kwamba ni Mungu ambaye alikusidia Kristo ateseke. D. Mistari ya 7-9, Kristo hakulalamika alikubali kufa kwa ajili ya dhambi zetu hata kama Yeye hakuwa amefanya dhambi yoyote. Yesu alikufa msalabai kwa sababu alitupenda sana. Yeye hakulazimishwa alikufa kwa sababu alitaka kutuokoa (Yohana 15:13). E. Mistari ya 10-12, tumsoma kwamba Mungu ambaye alimleta afe kwa ajili ya dhambi zetu, alimzawadia kwa kumfufua kutoka kwa wafu (Matendo ya Mitume 2:24) na pia amemtukuza na kumpa jina lililo kuu kuliko majina yote na amemketisha juu kwa mkono wake wa kuume (Wafilipi 2:9-11). Yesu Kristo alikuja hapa ulimwenguni akiwa mtumishi na alipata ushindi dhidi ya nguvu za dhambi na shetani kupitia kwa mateso na kwa mates ohayo, mpango wa Mungu ilikamilika. YEREMIA NA MAOMBOLEZO Yeremia alikuwa nabii ambaye alikuja baada ya miaka 16 ya kifo cha Isaya. Ujumbe wa Yeremia ulikuwa unahusu hukumu ambayo alikuja juu ya Yuda. Yeremia anajulika sana kama nabii ambaye alilia sana. Kwa sababu moyo wake uliumia sana alipokuwa anatoa unabii wa hukumu (Yeremia 9:1 na 13:15-17). Kitabu hiki kimejawa na historia nyingi kuhusu siku za mwisho mwisho za ufalme wa Yuda. Sehemu moja ya kitabu hiki inahusu maisha ya Yeremia na sehemu nyingine inahusu unabii kwa nchi ya Yuda. Kitabu hiki wengi wanaweza kukipata kikiwa kinachanganya kwa sababu matokeo yake hayapangwa yakifuatana. Ni kama kitabu cha Isaya. Ujumbe ambao umo ulipeanwa kwa wakti tofauti tofauti na kuwekwa pamoja baadaye. Yeremia aliitwa kuwa nabii na Mungu hata kabla ya kuzaliwa. Kama Musa, pia yeye hakutaka kufanya kazi ambayo Mungu alikuwa amemwita aifanye. Lakini Mungu alimhakikishia kwamba atamsaidia na kumlinda. Hata kama Yeremia alipiatia mateso kama kuwekwa gerezani, kupigwa hata karibu kuuliwa, Mungu aliyahifadhi maisha yake. Yeremia ni mfano kwetu kwamba Mungu akituita katika huduma, lazima tuitika haijalishi gharama ni gani. Gharama mara kwa mara huwa ni juu na wakati mwingine inaweza kuwa ni maisha yako. Lakini hata hivyo ni lazima tukubali kuitika. Yeremia alikuwa nabii kwa miaka zaid ya 40 wakati wa utawala wa wafalme 5. Mfalme Yosia ndiye alikuwa mcha Mungu pekee miongoni mwa hawa watano. Yeremia alikuwa nabii wakati Wababeli walikuwa wameivamia Yerusalemu. Huu ulikuwa wakati mgumu sana kwa Yerusalemu kwa sababu Wababeli walikuwa watu wabaya sana na Yeremia aliwapenda sana watu wake. Wakati huu Yuda hakuwa na huru, nchi ilikuwa inafanya mambo yake kupitia kwa Misri au babeli. Mataifa haya mawili yalikuwa yanashindana kujtawala Yuda. Israeli wakati Solomoni ilikuwa na nguvu na uchumi wake ulikuwa mzuri kwa sababu alikuwa amewabariki sana. Wakati wa Yeremia, dhambi za Yuda ailikuwa zimefanya Mungu aondoe baraka zake za ulinzi. Hii ilimaanisha kwamba Yuda alikuwa mdhaifu sana kuendeleza uhuru wake. I. Yeremia wakati wa utawala wa mfalme Yosia (640-609 BC 2 Mambo ya Nyakati 34-35:27). 1. Baada ya miak 5, Yeremia akiwa nabii, kitabu cha Sheria kilipatika katika Hekalu (2 Walame 22:8). Jambi hili lilileta Ufufuo katika nchi ya Yuda na watu walianza tena kumwabudu Mungu wakiwa wanatawaliwa na Yosia ambaye alikuwa mfalme mcha Mungu. Yeremia aliwaonya watu kwamba ufufuo ulikuwa wa kweli ikiwa watu watakuwa waaminifu katika kumwabudu Mungu (Yeremia 2:22). 2. Kitabu cha sheria hakikuwa kimepotea kabisa, bali mafundisha yake hayakuwa yanafuatwa na watu. Jambo hili ni kama kile ambacho kilefanyika wakati wa Martin Luther. Biblia ilikuwepo na ni wachache ambao walikuwa nayo, lakini wao hawakufuata mafundisho ya Biblia. Klanisa lilivumbua njia zingine zake za kuabudu. Martini Luther aliposma biblia,alianzisha kanisa la Lutheran kama njia ya kupinga kanisa la kikatoliki na mafundisho yake. Baada ya mfalme Yosia kufa, wale ambao walikuja nyuma yake walikuwa wafalme waovu sana machoni pa Mungu. Kwa sababu hii Yuda aliacha kuabudu Mungu wa kweli. Hii ilidhihirisha kwamba watu hawakumsikiliza Yeremia aliwambai kwamba walikuwa wawe waaminifu kwa kumwabudu Mungu wa kweli. Wao walimwabudu Mungu kwa nje lakini mioyo yao ilikuwa mbali sana na Mungu na ilikuwa bado katika dhambi. II. Wafalme watatu waovu waiongoza Yuda kutoka 609 BC hadi 597 BC. 1. Wa kwanza kwa hawa alikuwa Yehoahazi ambaye alitawala kwa miezi mitatu na alipelekwa katika utumwa Misri. Yeremia alizungumza juu ya mambo mabaya ya mfalme wa na watu. Kwa kawaida kuzungumza juu ya mfalme kwa njia ambayo ni ya kumkashifu huwa ni jambo la kuhatarisha maisha ya mtu. Lakini hata hivyo Yeremia alimkashifu mfalme kwa sababu ya ubaya wake. Hata nabii Ezekieli alitabiri juu kupelekwa kwa mfalme Jehoazi katika ujtumwa ( Ezekieli 19:3-4). 2. Mfalme Yehoyakimu alichukua utawala naye alikuwa mtu mwovu sana. Mfalme wa Misri alimfanya kuwa mfalme baada ya kumwondoa Yehoyazi. Wakati yehoyakimu alipokuwa mfalme, Misri na babebli walihusika katika vita na babebli ikishinda na ikiwa ndio nchi yenye nguvu katika eneo hilo. Yuda ilikuwa nchi ambayo ilikuwa dhaifu sana. Kwanza walitawaliwa na Misri halfu babeli. Babeli waliwachukua watu wengi wa Yuda na hazina nyingi na kupeleka huko babeli. Nabii Danieli alikuwa mmoja wa wale ambai walipelekwa katika utumwa na babeli. A.Yeremia aliwaonya watu kwamba dhambi zao zingewaongoza katika uangamizi. A. Kupitia kwa Yeremia, Mungu aliwaambia watu kwamba watubu dhambi zao ili aweze kuwabariki. Lakini watu hawakusikia, wao waliendelea katika dhambi (Yeremia 7:23-24). B. Mungu anachukia kuabudu sanamu na dhambi ya zina na pia alimtumia Yeremia kuwaonya walimu wa uongo na manabii wa uongo ambao waliwaongoza watu kwa kuwadanganya (Yeremia 23:1-2 na 27:1, 9-10). Viongozi na manabii hawakuufurahia ujumbe wa hukumu wa yeremia na waliagiza kwamba Yeremia awawe (Yeremia 26:8). Maisha ya Yeremia yalikuwa katika hatari sana kwani hata kulikuwa na nabii mmoja ambaye aliitwa Uria aliuliwa (Yeremia 26:20-23). C. Yeremia alitoa unabii kuhusu kifo cha Yehoyakimu (Yeremia 22:19). 3. Mfalme Yehoyakimu alichukua utawala kwa miaka 3. Yeye alikuwa mwovu sana na Yeremia alitoa unabii kwamba angepelekwa utumwani katika Babeli. Jambo lilifanyika kwani alifungwa gerezani huko babeli kwa miaka 37 (Yeremia 22:24-30 na Ezekieli 19:9). IV. Mfalme wa mwisho wa Yuda aliitwa Matania, ambaye aliitwa Zedekia na mfalme Nabukaduneza mfalme wa Babeli. Ezekieli 17:12-13, inaonyesha kwamba nchi ya Babeli ilitawala Yuda, kwa sababu tunasoma kwamba Nebukaduneza ndiye alimfanya Zedekia kuwa mfalme. 1. Kupitia kwa nabii Yeremia, Mungu aliwambia watu Yuda kwamba wamtii mfalme Nebukaduneza na utawala wake kwa miaka 70. Yeremia 29:10 na 51:59, tunasoma kwamba Zedekia alienda babeli labda kuhakikishia Nebukaduneza uaminifu wake kwake. 2. Mika 5 baadaye, Zedekia alikosa kumtii Mungu kwa kukosa kuasi dhidi ya ufalme wa babeli. Mbeleni alikuwa amemwahidi Nebukaduneza kwa kiapo kwa Mungu kwamba hataasi dhidi ya babeli (2 mambo ya Nyakati 36:13 na Ezekieli 17:13-21). 3. Kwa sababu ya uasi wake, Nebukaduneza alivamia Yuda. Mfalme Zedekia alimwuliza Yeremia kama vita hivyo atavishinda, lakini Yeremia alimwambia kwamba watu walifaa kujitoa kwa Nebukaduneza kwa sababu mfalme Zedekia alikuwa anaenda kupoteza vita hivyo. Pia alimwambia kwamba anapaswa kuomba huruma kutoka kwa nebukaduneza kwa sababu Yerusalemu ilikuwa inanenda kuangamizwa (yeremia 21:9-10). 4. Ujumbe wa Yeremia hakupendwa na kwa sababu hiyo, Yeremia alitiwa kwenye kisima (Yeremia 38:6). Katika mstari wa 13, tunasoma kwamba Yeremia aliokolewa na Ebed-Meleki Mkushi. 5. Ujumbe kuhusu hukumu ya Mungu kwa Yerusalemu, ulikuwa ujumbe wa kuhuzunisha. Hii ilikuwa iwe hukumu kali sana, lakini pia wakati huo Mungu alimpa Yeremia ujumbe wa faraja na wa kuhimiza kwamba atawakomboa. Yeremia 30:18,22 na 31:3, tumajifunza kwamba ni jambo la muhimu sana kuwadhibu wale ambao tunawapenda, lakini pia tunapaswa kuwakumbusha kwamba tunawapenda na kwamba adhabu hiyo ni kwa uzuri wao. Mungu aliwaambia watu kwamba baada ya kuwaadhibu, Yeye atawarejsha Yerusalem (Yeremia 29:10). 6. Wababeli waliuharibu mji na Hekalu. Watu wengi wa Yuda walipelekwa katika utumwa huko Babeli. Yeremia alibaki katika mji hadi alipolazimishwa kuenda Misri mahali ambapo alikufia. V. katibu kitabu hiki kuna huzuni mwingi lakini pia kuna unabii mwingi kumhusu Yesu Kristo. 1. Yeremia 3, tunasoma kumhusu Mungu akiwa amekasirika kwa sababu ya dhambi ya watu ya kuabdu sanamu. Lakini katika smtari wa 12, Mungu aliwaahidi kwamba ikiwa watatubu dhambi zao, Yeye atawahurumia. Matamshi ya kutazama kasikazini, ni njia moja Mungu anasema kwamba huruma wake ataupeana kwa watu waliobaki wa taifa la kasikazini na wale wa Yuda. A. Mistari ya 16-17, inazungumzia wakati ambapo hatutahitaji tena Sanduku la Agano kwa sababu mwokozi alikuwa anakuja na atatosheleza kila aina ya hitaji. 2. Ahadi ya Agano Jipya inatajwa hapa. Taifa la Israeli lilikuwa taifa ambalo lilikuwa katika Agano na Mungu tangu siku za Abrahamu (Mwanzo 12:1-3). Mlimani Sinai, Mungu aliwapatia waisraeli agano la sheria ambalo lilizingatia kwamba wale ambao wanakosa kutii watalaaniwa na wale ambao wanatii watabarikiwa (Kutoka 24:7). Watu hawakuweza kutii sheria hiyo kwa hivyo walihukumiwa. A. Yeremia aliwaonyesha Agano jipya ambalo lingekuwa la kutosheleza kwa ajili ya msamaha wa dhambi na wokovu (Yeremia 31:31-34). B. Agano jipya lilichukua nafasi ya Agano Kale (waebrania 8:13). Maisha na kifo cha Kristo Yesu ndio msingi wa Agano Jipya (Luka 22:20). C. Agano Jipya ni Agano la neema. Kristo amefanya kila kazi ambayo inapaswa kutuwezesha kuwa katika uhusiana na Mungu. Kwa hivyo wokovu tunapewa bure wale wote ambao tunamwamini Kristo (waefeso 2:8-9). Wokovu ni bure kwetu lakini kuna gharama ambayo ilitolewa kwa ajili ya wokovu huo na gharama hii ni kifo cha Kristo Yesu. VI. Jinsi tunapaswa kuishi kulingana na mafundisho haya. 1. Ujumbe wa Yeremia mwingi ulikuwa ujumbe wa hukumu. Kwa sababu hii Yeremia alilia sana kwa ajili ya watu wa Israeli )Yeremia 9:1 na 13:16-17). A. Miaka 700 baadaye tunaona upole wa Yeremia katika nabii mweingine ambaye ni Kristo Yesu ambaye pia alilia kwa ajili ya watu wake (Mathayo 23:37). B. Yeremia alitoa unabii ambao uliwahuzunisha wengi, lakini pia alizingumza maneno mengi ya neema ya Mungu. Haya ni maneno ya upendo na huruma kutoka kwa Mungu (Yeremia 29:11 na 31:3). 2. Kutangaza huku ya Mungu. A. Yeremia alikuwa mpole ambaye alitabiri juu ya hukumu kali ya Mungu kwa watu ambao aliwapenda sana (Yeremia 7:20,30,33-34). Moja wapo ya ishara ya kiongozi mkristo ni kwamba yeye ni mtu mwenye upendo na upole kwa watu ambao anawaongoza. Lakini pia yeye ni mtu ambaye anazingatia ndihamu ya Mungu kwa watu wake wakatika inapohotajika kutekelezwa. i. Kuna mafundisho mengi katika Biblia kuhusu hasira na gadhabu ya Mungu kuliko kuhusu upendo na upole wake (Zaburi 90:11). B. katika Agano Jipya, tunaona kwamba Yesu mwenyewe alifundsiah sana kuhusu jahanum kuliko mtu mwingine yeyote. Msalabani Kalivari, gadhabu ya Mungu ilimwagwa juu ya Kristo Yesu na akafa kwa ajili ya sisi watu wake. Tunaona hili wakati alipolia, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha (Mathayo 27:46). Dhambi ni kitu kibaya sana na jahanum pia ni mahali pabaya sana, na kwa hivyo tunapswa kuwa watu wenye shukurani sana kwa ajili ya wokovu wetu ambao tumepewa na Kristo. 3. Hali ya asili ya moyo wa mwanadamu. A. Moyo wa mwanadamu ni mwovu kwa asili (Yeremia 17:9). Yesu alifundisha kwamba ni uovu amabo unatoka ndani ya mtu ndio unamchafua mtu (Marko 7:21-23 na Mathayo 23:27). B. Kila mtu ni mwovu na anahukumiwa na dhambi zake. Dhambi zetu ndio kizuizi kwetu kuingia katika ufalme wa Mungu (Warumi 8:7-8). C. Ili tuweze kuungia ufalme wa mbinguni, ni lazima tuwe na moyo mpya (ezekieli 36:26). Yesu alisema jambo hili kwa kutuangiza kwamba ni lazima tuzaliwe mara ya pili (Yohana 3:5). 4. Onyo kwa wale ambao walikuwa wameacha kumwabudu Mungu. A. Yeremia aliwahimiza watu wa Mungu kwamba wasiache kumwabudu Mungu bali wamrudie kama wakati bado upo. i. Yeremia aliwaambia watu kwamba wao walikuwa wenye dhambi sana kuliko wataifa la kasakazini. Aliwakumbusha kwamba Mungu aliadhibu Itaifa la kasikazini kwa kuruhusu Ashuru waje na kuwaondoa katika nchi yao na kuwatawanya katika mataifa mengine (Yeremia 3:11). ii. Yeremia aliwaambia watu kwamba wamrudie Mungu na Mungu hataendelea kuwakasirikia (Yeremia 3:12-13). iii. Yeremia aliwahimiza kwamba walifaa kumrudia Mungu kwa haraka sana kwani nyungu ambayo ikon a kasoro inaweza tu kutengenezeka wakati bado ni mbichi (yeremia 18:4-6). Nyungu ikisha kauka, haiwezi tena kutengenezeka, itavunjwa tu na kuaharibiwa (yeremia 29:13-14 na Isaya 55:6-7). 5. Yeremia mara nyingi alijihisi kwamba alikuwa peke yake. A. Yeremia alihis kuwa peke yake. Ni ukweli kwamba ikiwa utahubiri ukweli wa neno la Mungu ambao wengi wanachukia, wewe utaachwa peke yako. Wengi hawatataka kuwa na uhusiano zu ushirika nawe. Yeremia alikataliwa na familia, marafiki, viongozi, manabii n ahata makuhani. Wote hawa walimkataa. Yeremia alipigwa na kutishiwa kuuliwa. Yeremia aliteseka kama watumishi wote wakristo ambaio wanateseka kama Kristo alivyoteseka. VII. Kwa kumalizia 1. Kitabu cha Yeremia kimejawa na onyo nyingi kutoka kwa Mungu kw Yuda. Mungu alikuwa mvumilivu na Yuda: alimwonya Yuda, alimtisha Yuda na aliwalilia watu waache kukosa kumtii. Mungu alifanya hivi kwa mamia ya miaka. 1. Mungu ni mvumilivu lakini kuna wakati uvumilivu wake unaisha halfu anaamua kuadhibi au kuhukumu. Mungu hajabadilika, ni yule yule Mungu wa wakati Yeremia, ndiye Mungu wa sasa. Tuwe waangalufu sana juu ya onyo ambazo anatupatia kila wakati. MAOMBOLEZO Kitabu hiki ni kitabu cha huzuni sana kwa sababu kinahusu maombolezi ya Yuda. Kitabu hiki kiko na mashairi ya wakati wa kufiwa ambazo Yeremia alitunga. Hiki ndicho kitabu ambacho kimejawa na huzni katika Biblia yote. Mungu aliwaadhibu vikali watu wake na kitabu hiki kinafafanua huzuni wa watu wa Mungu. I. Shairi la kwanza: Kuangamizwa kwa yerusalemu (Maombolezo 1:1-22). 1. Ombolezo la kwanza ni kilio juu ya kuangamizwa kwa mji wa Yerusalemu. Mji huu ulikuwa umeangamizwa kwa sababu baada ya Mungu kuonya kwa muda mrefu watu walikataa kutubu. Maangamizi ya mji yalikuwa mabaya sana kiwango kwamba mji ulikuwa hauna mtu kati yake na ulidharauliwa sana. Hii ni mfano wa mjane ambaye amempoteza mume wake na watoto wake na wakati huo hana tumaini lolote. 2. Yeremia alisema kwamba adhabu hiyo ilitoka kwa Mungu na ili sababishwa na uovu wa watu. Katika maombolezo 1:8, Yeremia anasema kwamba watu wanakubali kwamba wao wako na hatia na kwa hivyo Mungu ako na haki ya kuwaadhibu kwa ajili ya uasi ana uovu wao. 3. Yeremia anazungumza jinsi maadui wao walivyo na furaha kwa sababu yay ale ambayo yamewatokea. Yeremia anasema kwamba hata hao maadui wao walifaa kuangamizwa kwa sababu hata wao ni waovu na niwaasi dhidi ya Mungu (Maombolezo 1:21-22). II. Shairi la pili: Hasira ya haki ya Mungu (Maombolezo 2:1-22). 1. Maangamizi ya mji ya yerusalemu yalifanywa na Wababeli kwa sababu Mungu aliwatumia kama chombo cha kuadhibu watu wake. Ni Mungu ambnaye alikuwa ameruhusu kuangamizwa kwa mji huo (Maombolezo 1:1-6). Kuna wakati Mungu anawatumia wale ambao si wake kutekeleza yale ambayo anataka yafanyike, hata kuadhibu watu wake. Mwanzoni aliwatumia washuru kuadhibu taifa la kasikazini la Israeli. Isaya alitabiri kwamba Mungu angemtumia Cyrus kuwatoa watu katika utumwa na kuwarejesha Yerusalemu (isaya 44:28 na 45:1). 2. Mungu alikuwa na sababu mzuri sana kwa nini aliwadhibu watu wake. Yeremia aliwahimiza watu kwamba walifaa kutubu. Yeremia alimkumbusha Mungu kwamba hawa walikuwa watu wake bado hata kama walikuwa wametenda dhambi. Yeremia anamsihi Mungu awahurumie (Maombolezo 2:19-20). III. Shairi la tatu: Huzuni na tumaini la nabbi Yeremia na watu wote (Maombolezo 3:1-66). 1. Yeremia alikuwa mmoja na watu katika shida. Yeye alihuzunika sana kwa sababu ya taabu za watu. Hata wakati huu yeye alikuwa na tumaini na ujasiri katika Mungu (maombolezo 3:23-24). 2. Hata katika wakati huu wa huzuni mkubwa, Yeremia alikuwa na anamwamini Mungu kwa sababu Mungu alkiwa mwaminifi siku zote. Yeremia alijua kwamba Mungu hafurahia katika kuadhibu, ni jambo ambalo analifany akiwa na sababu za msingi (Maombolezo 3:33). 3. Yeremia anaendele akusema kwamba watu walistahili adhabu hiyo kwa sababu ya dhambi zao na uasi dhidi ya Mungu (Maombolezo 3:40-42). IV. Shairi la nne: Yerusalemu yavamiwa (Maombolezo 4:1-22). 1. Yeremia anaseema kwamba kuna wakati walikuwa na utukufu na utajiri. Anafanya hivi kuonyesha jinsi watu walivyoanguka katika dhambi zao (Maombolezo 4:1). 2. Yeremia alizumgumza juu ya mateso makali ya watu wakati wa uvamizi na baada ya kuanguka kwa Yerusalemu. Yeye anafananisha watu kama wafu ambao wanatembea. Yeremia anapeana mfano wa hukumu kali sana kutoka kwa Mungu. Hili ni onyo kwa mtu kwamba dhambi zake asipotubu, zintamletea hukumu kali sana kutoka kwa Mungu (Maombolezo 4:2-8). V. shairi la tano: Yeremia anamsihi Mungu alete urejesho (Maombolezo 5:1-22). 1. Watu walitubu dhambi zao na kumwomba Mungu awakomboe kutoka katika mateso yao (Maombolezo 5:1). Kitabu hiki kinaisha bila hakikisho lolote kwamba Mungu ataleta ukombozi. Lakini hata hivyo tumaini lao la pekee ni Mungu ambaye wanamwomba (maombolezo 5:21). VI. Kristo na kanisa lake 1. Yeremia akiwa mfano wa Kristo. Yeremia alilia mji wa Yerusalemu na watu wake (Maombolezo 4:11,13). Miaka 600 baadaye, Yesu aliilia mji wa Yerusalem kwa sababu hukumu ambayo inalikuwa inakuja juu yake (Luka 19:21-33). Mungu alikuwa anaenda kuadhibu Wayahudi kwa sababu ya dhambi zao ambazo walikataa kutubu (mathayo 23:37). 2. Katika kitabu cha Maombolezo hakuna unabii wa wazi kabisa kumhusu Kristo, lakini mifano kuja kwa Mesiya ambaye alikuwa ameahidiwa na Mungu. A. Maombolezo 2:15-16; Zaburi 22:13 na Mathayo 27:39-44 B. Maombolezo 3:8 na Mathayo 27:46 C. Maombolezo 3:14; Zaburi 69:12 na Mathayo 26:57-68 D. maombolezo 3:18; Zaburi 69:21 and Mathayo 27:34 E. Maombolezo 3:30; Zaburi 69:20; Isaya 50:6 na Luka 22:63-64 VII. Jinsi tunapaswa kuishi kulingana na mafundisho ya kitabu cha Maombolezo. 1. Maisha bila Mungu A. Hali ya watu kuwa bila Mungu inafafanuliwa kama kuwa bila pumziko, bila faraja na bila malisho (Maombolezo 1:3,6,9). Hivi nidvyo wale ambao hawajawamini Kristo walivyo. Maihs ayao ni maisha bila Mungu hata kama wanajiwazia kwamba wanamjua Mungu. Bila Kristo hawana Mungu na kwa hivyo hawana faraja, hawana malisho na hawana pumziko. Ni katika Kristo pekee tunapata mambo haya (Mathayo 11:28; Yohana 10:9 na Yohona 14:16-17 2. Uaminifu wa Mungu A. Hata kama watu walikuwa katika mateso makali sana, bado kulikuwa na tumaini na imani kwamba Mungu atawahurumia (Maombolezo 3:22-23). Tunapaswa kumtegemea Mungu na kuendelea kumwamini hata katika hali zetu ngumu sana (Isaya 50:10). VIII. Kwa kumalizia 1. Kitabu cha Maombolezo ni kitabu cha huzuni mwingi sana. Lakini hata katika huzuni huu, Yeremia bado anatangaza utakatifu, haki na utawala wa Mungu katika adhabu ambayo aliwadhibu nayo watu wa Yuda. 2. Hakuna mtu ambaye angemshitumu Mungu kwamba Yeye si mvumilivu. Ni baada ya miaka nyingi ya onyo, vitisho na kuwasihi watu wa Yuda, ndipo Mungu alileta adhabu kwao. 3. Hata wakati wa mateso makubwa katika maisha yao, wao bado walikuwa na tumaini kwa sababu Mungu nu mwaminifu (Maombolezo 3:23). 4. katika maneno ya mwisho ya Maombolezo, kuna tumaini la mbeleni (Maombolezo 5:21-22). 5. Hali ilikuwa mbaya sana lakini hata hivyo, Yeremia aliendelea kuamini katika ahadi za Mungu. Ahadi za Mungu kwa Abrahamu, Musa, Daudi na Yuda alijua kwamba Mungu atazitimiza. Yeremia kama Abrahamu aliamini wakati ambapo mambo yalionekana hayawezekani (Warumi 4:18). Haijalishi hali yako ni hali ya aina gani, haijalishi ugumu wa jambo, hakuna chochote katika ulimwengu ambacho kinaweza kuwafanya watoto wa Mungu wakose kuamini katika neno la Mungu. Wacha Mungu awe mwaminifu na kila mwanadamu mwongo (Warumi 3:4). KITABU CHA EZEKIELI Kitabu hiki kiliandikwa na Ezekieli ambaye alikuwa nabii na kuhani kwa Waisraeli ambao walikuwa utumwani babeli. Yeye alizaliwa yerusalme na alipelekwa katika utumwa pamoja na waisraeli na Wababeli. Yeye alifanya kazi wakati mmoja na Danieli na Yeremia. Yeremia alikuwa nabii kwa Yerusalemu wakati wa siku za mwisho kabla ya Nebukaduneza kuangamiza yerusalemu. Wakati huo huo Danieli alikuwa nabii huko Babeli katika makao ya ufalme. Ezekieli alizalwa huko Yerusalemu na alipelekwa katika utumwa na Nebukaduneza wakati wa uvamizi wa pili. Maandishi ya Ezekieli si mepesi kuelewa na kwa sababu hii wengi huwa hawasomi kitabu hiki. Hii ni kwa sababu kitabu hiki kimejawa na mifano ya picha nyingi. Mwandishi anatumia maono, unabii, ishara na mifano kueleza ujumbe wa Mungu wa kitabu hiki. Hii inafanya wengi wapate kitabu hiki kigumu kuelewa. Lakini katika kitabu hiki kuna ukweli ambao tunapaswa kuelewa wote kwa sababu ni wa muhimu sana kwetu. I. Sehemu ya kwanza ya kitabu hiki inazungumza juu ya kuitwa na kutumwa kwa Ezekieli na Mungu (Ezekieli. 1:1-3:27). 1. Mungu alimtokea Ezekieli kwa maono kama tu Isaya na kumwonyesha picha ya utukufu mkku wa manabii. Tunasoma kuhusu hali ya Ezekieli wakati aliona maono ya Mungu. Hii ni kawaida wakati mwanadamu anapokuja katika uwepo na utukufu wa Mungu. Ezekieli 1:28, tunsoma kwamba Ezekieli alianguka chini wakati alipoona utukufu wa Mungu. A. Tunafaa kuja mbele za Mungu na heshimu sana haswa wakati tunasoma neno la Mungu na wakati wa maombi (Isaya 66:5), kwa sababu Mungu ni Mungu Mtakatifu na sisi ni wenye dhambi. 2. Baada ya Ezekieli kuneyenyekezwa na Mungu, Mungu aliamua kumtuma. Ezekieli alifahamu kwamba huduma wake utakuwa mgumu sana kama tu manabi wengine. A. Ezekieli alikuwa mwana wa Buzi. Mungu alikuwa anawaadhibu watu wake, lakini hakuwa amewasahau kwa sababu hii, alimtuma Ezekieli (Ezekieli 2:3). B. Ezekieli alikuwa na mamlaka kutoka kwa Mungu (Ezekieli 3:4). C. Ezekieli alipata nguvu kutoka kwa Mungu. Tunasoma kwamba Mungu alimwinua na kusimamisha ( Ezekieli 2:2). Watumishi wa wote wa Mungu hawapaswi kufanya kazi kwa kutegema nguvu zao, bali wanapswa kumtegemea Mungu. Ezekieli alijua kwamba anaenda kufanya kazi miongoni mwa watu ambao watamsikiliza na kwa hivyo huduma wake ulikuwa mgumu sana (Ezekieli 3:7). Maneno ambayo imetumika kuel;eza ugumu wa mioyo ya watu ni kama yale ambayo yametumika kueleza jinsi moyo wa farao ulivyokuwa. Moyo wa farao ulikuwa mgumu sana dhidi ya maneno ya Musa (Ezekieli 3:8-9). D. Ezekieli alikuwa awe mwaminifu kw awatu hata kama alijua kwamba mioyo yao itakuwa migumu sana kupokea ujumbe wake (Ezekieli 3:5,11). Katika sura ya pili tunasoma kwamba watu watalikataa neno na Mungu kama tu vile walivyo wapinga manbii wengine wa Mungu. i. Tunafundishwa hapa kwamba lazima tume waaminifu kwa kuhubiri neno la Mungu hata kama watu watalikataa au kutukataa sisi. Ni lazima tuendelea kufanya kazi hii hata kama maisha yetu yatakuwa hatarini. Tunapaswa kuhubiri neno la Mungu kwa bidi sana. Mahubiri wengi wa uongo huwa wamejotolea kabisa kuhubiri uongo wao. Vivyo hivyo, sisi ambao tuko na ukweli tunapaswa kujitoa zaidi. Ni lazima tuhubiri kile tu ambacho Biblia inafundisha. E. Ni lazima tuwe watiifu kwa Mungu katika kila jambo. We must be obedient to God. See how Ezekiel obeyed God and ate the scroll when ordered to. Chapter 2:1-2 we learn what obedience is from the Bible. 3. Mwana lazima ajibike ndio ujumbe ambao Mungu alimpa Ezekieli (Ezekieli 2:18,20; 33:8). Mungu anataka kila mmoja wetu ajibiki katika jambo ambalo Mungu anataka tufanye. Kila mkristo ameitwa kuwa mwinjilisti na ni lazima tufanya kazi hii kwa uaminifu. A. Jambo la kuajibika mbele za Mungu ni jambo linafundishwa kila mahali katika Biblia. Paulo anazungumza kwamba asipo hubiri injili, maisha yake yako hatarini (1 Wakorintho 9:16). II. Sehemu ya pili ya kitabu hiki ni wakati Ezelieli atangazia Yuda hukumu kabla ya kuaguka kwa Yerusalemu (Ezekieli 4-27). Wakati huu Yeremia alikuwa bado ako Yerusalemu na Ezekieli alikuwa kasikazini mwa Babebli na wote walikuwa wanatoa unabii sawa. Unabii huu ulikuwa unahusu hukumu ya Mungu ambayo ilikuwa inakuja kwa Yuda kwa sababu ya dhambi zake. 1. Mungu aliahidi kuleta adhabu kali sana kwa watu wake kwa sababu dhambi zao zilikuwa mbaysa zaidi kuliko za mataifa yasio mcha Mungu (Ezekieli 5:7-9). 2. Katika maono, Ezekieli aliona baadhi ya dhambi za Yuda kama kuabudu jua na wanyama kama Wamisri walivyokuwa wakifanya (Ezekieli 8:10,14,16). A. Ezekieli aliona maono ya utukufu wa Mungu ukiondoka katika hekalu na katika mji. i. Ezekieli aliona magurudumu kwa Sanduka la Agano ili lianze kuondoka. ii. Ezekieli aliona utukufu wa Mungu ukiondoka ukielelkea kwenye kizingiti cha Hekalu (Ezekieli 10:4). Halfu ulielekea kwenye lango la mashariki (Ezekieli 10:19), halfu nje ya mji na ukatua juu ya mlimani ulio mashariki mwa mji (Ezekieli 11:23). iv. Utukufu wa Mungu uliondoka miongoni mwa Wayahudi hadi katika sura ya 43. Tunapozungumza kuhuus utukufu wa Mungu, tunamaanisha wakati watu wamemkaribia Mungu na Mungu pia amewakaribia. Yaani baraka za Mungu kwa watu wake; kama neno lake kuwa miongoni mwetu, wahubiri wa kweli ambao Mungu hutuletea, Amani ili tuweze kuhubiri injili, kuishi maisha matakatifu. Mojawapo ya adhabu ambayo watu walipata kutoka kwa Mungu ni wakati Mungu aliondoa baraka zake na uwepo wake kwa watu wake. B. Ezekieli alizungumza kwa mdomo wake, kwa ishara na kwa mifano (Ezekieli 12:6). Ezekieli alikubali kujitoa kwa Mungu na kuacha starehe zake na mapenzi yake. Ezekieli aliendelea kumtumikia Mungu hata baada ya mke wake kufa (ezekieli 24:15-18). i. Ezekieli anaonyesha uvumizi wa Yerusalemu kama kwamba alikuwa mwenyewe (Ezekieli 4:1-17). ii. Ezekilei 5, tunasoma kuhusu Ezekieli akitabiri hatima ya wale wanaoishi Yerusalemu. iii. Ezekilei alipanga vita vyake na kuchimba katika ukuta kuonyesha utumwa ambao Wayahudi walikuwa wame ndani (Ezekieli 12:1-20). C. Huko Yerusalemu, mfalme Zedekia anawaza kwamba yeye yuko salama kwa sababu aliwaza kwamba unabii wa Yeremia na Ezekieli ulikuwa auambatani. Yeremia alisema kwamba mfalme angepelekwa babeli katika utumwa (Yeremia 21:7). Ezekieli alisema kwamba mfalme hataona mji wa babeli (Ezekieli 12:13). Huu unabii wote ni wa kweli kwa sababu kabla ya Zedekia kupeleka babeli, macho yake yalitolewa. Kwa hivyo alipelekwa lakini hakuwa na macho ya kuona jinsi mji ulivyo (2 Wafalme 25:7). 3. Mfalme Zedekia alifanywa mfalme na Nebukaduneza ambaye alifanya agano naye kwamba hatawahi kumwasi. Hili lilikuwa agano ambalo Zedekia alilifanya (Ezekieli 17:13-15). Uasi wa Zedekia ulikuwa dhambi nah ii ilimkasirisha Mungu kwa sababu nebukaduneza alikuwa amemwambia Zedekia aape kwa jina la Mungu (2 Mambo ya Nyakati 36:13). 4. katika Ezekieli tunasoma kwamba Mungu alikuwa amekasirika na Israeli kwa sababu walipokuwa Misro waliabudu miungu. Sababu moja ni kwa nini Mungu hakuwa ameangmiza Israeli ni kwa sababu ya utukufu wake (Ezekieli 20:1-9). A. Mungu ataadfhibu dhambi kwa wakti wake, Yeye huwa hasahau. B. Mungu hutuokoa kwa sababu ya utukufu wake na si kwa sababu sifa zetu, hata kama huwa tunfaidika sana (Isaya 43:7, 46:13). 5. Mke wa ezekieli alikufa wakati wa kwanza wa uvamizi wa Yerusalemu (Ezekieli 24:2-18). Kifo hiki ni ishara kwamba yerusalemu ilikuwa ishindwe katika vita hivi (Ezekieli 24:16-24). III. Hukumu kwa mataifa ambayo yalizingira Israeli (Ezekieli 25:1-32:32). 1. Mungu alitangaza hukumu kwa mataifa ambayo yalikuwa yamezingira Israeli kwa sababu walikuwa wanaabudu sanamu na walifurahia kuanguka kwa watu wake. Wao pia walisaidia katika kuangamiza Yerusalemu. 2. Misri ndio nchi ambayo Mungu aliadhibu sana. Hii ni kwa sababu kwa miaka 400, nchi iliwatatiza sana watu wa Mungu. Mungu aliamua kwamba nchi ya Misri itaendelea kuwepo, lakini sin a nguvu za utawala ambazo walikuwa nazo (Ezekieli 29:15). Historia imepatikana kuwa ya kweli kwa sababu mataifa mengi yameivamia Misri na kuitawala na leo sin chi yenye umarufu duniani. IV. Unabii kuhusu kurudi na kurejeshwa kwa Yuda (Ezekieli 33:1-48:35). 1. Yerusalemu na Hekalu ziliharibiwa katika mwaka wa 538 BC, na watu waliadhibiwa vibaya sana. Watu walikataa kusikiliza onyo ambazo Mungu alikuwa amewaonya kupitia kwa manabii fulani fulani. Wao waliwaza kwamba kwa sababu walikuwa watu wa Agano wa Mungu, Mungu hangeweza kuwaadhibu vikali sana. Katika sura ya 24:25-27, tunsoma kuhusu ujumbe wa Ezekieli wa mwisho akiwaonya kuhusu adhabu kali ya Mungu ambayo ilikuwa inakuja. Baada ya hapa, Ezekieli alinyamaza kwa miaka 3 na hakuzungumza kuhusu kuangamizwa kwa Yerusalemu. 2. Baada ya mji kuanguka na watu kufahamu kwamba hata kama wao ni watu wa Agano la Mungu walistahili kutii na kwa sababu ya kutotii kwao, Mungu anawadhibu, Mungu ndipo aliwatumia ujumbe wa kuwahimiza kwamba kutakuwa na urejesho (Ezekieli 33-48). 3. Kuna jumbe nyingi sana jinsi utukufu wa watu utakavyorejeshwa. A. Kwanza, walifaa kuwasikiliza viongozi wa kiroho na kutubu (Ezekieli 33). Leo tunafaa kuwasikiliza wahubiri wa neno la Mungu ambao ni waaminifu kwa neno lake, yaani Biblia. B. Pili, walifaa kuacha kufuata walimu wa uongo na kuanza kumfuata Mchungaji mkuu wa Kondoo, yaani Kristo Yesu (Ezekieli 34). Leo tunafaa kutumia neno la Mungu kuwafahamu wale ambao ni wauongo na kuwasikiliza wale tu ambao wanafundisha kumhusu Kristo Yesu kutoka katika Biblia. C. Tatu, walifaa kuongozwa na Roho Mtakatifu (Ezekieli 37). D. Nne, Kwa kuwaondoa maadui wa Israeli (Ezekieli 38-39). E. Tano, kwa kurejesha Israeli katika nchi yake (Ezekieli 48). V. Kristo na kanisa lake. 1. Unabii kuhusu kuja kwa Mchungaji mkuu ambaye ni Kristo. A. Mungu anajitambulisha kama Mchungaji mkuu ambaye atawakomboa watu wake na kwa upendo kuwashughulikia (Ezekieli 34:11-16). Kuna mifano kumhusu huyu Mchungaji mwema ambaye atawashughulikia watu wake. Katika Agano jipya Kristo anajiita Mchunagaji Mwema (Yohana 10:11-16). 2. Ezekieli anatoa mfano wa hekalu mpya (Ezekieli 40 na 47). Ni ukweli kwamba Hekalu ya Yerusalemu alijengwa tena wakati Wayahudi walirudi kutoka utumwani. Lakini Hekalu ambalo Ezekieli anazungumza juu yake ni zuri na inautukufu mkubwa sana kuliko ambayo Wayahudi walijenga waliporudi. A. Hakelu la Ezekieli ni mfano mkuu wa Kristo Yesu. Ni mfano wa wakati Kristio atakapoishi miongoni mwa watu wake. i. Kristo ndiye Hekalu la kweli ambalo linaishi (Yohana 2:19-22). ii. Kristo anawaleta watu wake pamoja kama mawe yalio hai, yamejengwa kuwa nyumba ya Roho (1 Petro 2:5). iii. Ndani ya Kristo, jingo lote limeshikamanishwa pamoja na kusimamishwa ili kuwa Hekalu takatifu katika Bwana (Waefeso 2:21). 3. Tunasoma kuhusu mto wa uhai katika sura 47 ambao unatiririka kutoka katika Hekalu. Huu si mto wa maji ya kawaida, lakini mfano wa baraka za kiroho ambazo huleta uhai mahali ambapo hakukuwa na uhai. Huu ni mfano wa Kristo ambaye ndiye chemichemi ya baraka zote za kirohoni (Yohana 4:10 na Waefeso 1:3-4). 4. Agano Jipya A. Mungu alikuwa ananenda kutengeneza Agano la milele na Wayahudi wakati watakaporudi yerusalemu kutoka kwa utumwa (Ezekieli 37:26-28). B. Tunaona hali ya ufufuo wa kiroho wakati Mungu atakapomimina Roho wake kwa wale ambao wamekufa kiroho (Ezekieli 37:1-14). C. Mungu anaeleza jinsi watu watakavyobadilishwa wanapopewa moyo mpya wa nyama na kusafishwa (Ezekieli 36:25-27). D. Kule Yerusalemu, nabii Yeremia alikuwa anatoa ujumbe huo huo kama wa Ezekieli (yeremia 31:33-34). E. Mungu anaahidi kwamba Roho Mtakatifu ataishi ndani ya wale wote ambao wanaamini. Jambo hili ndipo lifanyike, lilihitaji kazi kuu ya Kristo Yesu ambayo aliifanya msalabani kalivari na kutukuzwa kwake. F. Baraka za Agano Jipya ni: i. Kuondolewa kabisa kwa dhambi kupitia kwa damu ya Kristo Yesu ambayo ndio damu ya Agano Jipya la milele (Ezekieli 36:25; Yeremia 31:34; Luka 22:20; Waebrania 13:20). ii. Sheria ya Mungu angeandikwa kwa mioyo yao, mioyo ya nyama ambaye imeweka nadala ya mawe(Ezekieli 36:26; Yeremia 31:33; 2 Wakorintho 3:3, 4:17). iii. Roho Mtakatifu ataishi ndani mwa wale wote ambao wameokoka (Warumi 8:9; 1 Wakorintho 3:16). VI. Jinsi ya kuishi maisha yetu kulingana na mafundisho haya. 1. Ezekieli anafundisha kwamba kila mtu anapaswa kuajibika kwa ajili ya matendo yake. Kwa kawaida, watu huwa wanalaumiana wakati dhambi imefanywa kama Adamu na Hawa. Biblia inafundisha kwamba ni lazima tukubali makossa dhambi zetu na hatufai kumlaumu yeyote. A. Adamu alimlau Hawa kwa sababu ya dhambi yake. Hawa naye alilaumu nyoka kwa sababu ya dhambi yake (Mwanzo 3:12-13). B. Jambo hili la kuajibika kila mtu kivyake tunalisoma katika Ezekieli 18:4,20). Kila mtu anapaswa kuajibika kwa sababu ya dhambi zake. 2. Moyo mpya A. Kwa sababu ya unajisi na uovu wa Isreali, Mungu alikasirika nao (Ezekieli 36:16-20). Israeli hawakufany lolote zuri ili Mungu awapende. B. Kile ambacho Mungu aliahidi kufanya ni kwa sababu hakutaka Jina la likashifiwe na wala si kwa sababu watu walifanya lolote zuri ili wapate baraka za Mungu (Ezekieli 22-23). C. Mungu aliahidi kuwapa watu wake moyo mpya. Moyo huu ulikuwa umejazwa na uoendo wa Mungu na roho wa utiifu (Ezekieli 36:25-27 na 11:19-20). D. Ahadi hii ilitimika katika injili ya Bwana wetu Yesu Kristo (Tito 3:3-6). 3. Kuzaliwa na Roho. Mara 29, Ezekiali anazungumza kuhusu Roho wa Mungu (Ezekieli 2:2 na 3:12). Katika Ezekieli tunaona kwamba ni Roho Mtakatifu ambaye anawazaa watu mara ya pili. A. Maono ya mifupa ambayo imekauka inatuonyesha kazi ya kuu ya Roho Mtakatifu (Ezekieli 37:1-14). Hadithi hii inatuonyesha hali ya kiroho ya Israeli wakati walikuwa chini ya adhabu ya Mungu na kuzaliwa kiroho ambako roho Mtakatifu anawafanyia wakati Mungu atakapowarejesha. Maono haya yanadhihirsha hali ya kiroho wakati Wayahudi walipikuwa utumwani. Ni kudhirisha hali yao ya huzuni kwa sababu ya kukosa uhai wa kiroho. i. Mifupi ilikuwa imekauka kabisa. Dhihirisho la hali ya watu chini ya adhabu ya Mungu. Uovu watu ulikuwa uasi wao dhidi ya Mungu na neno lake, utawala wa dhambi na kuanguka kabisa katika maisha ya kutojali Mungu. ii. Mungu alimwamuru Ezekieli ahubiri na aombe (Ezekieli 37:4-5). Alikuwa amwaombee wale ambao walikuwa wamekufa kiroho (Yohana 5:25) na kuita Roho wa Mungu afanye kazi ya kuwapa uhai wa kiroho (Tito 3:5). a. Maono ya mifupa ambayo imekauka, inatufundisha kwamba ni kazi ya Roho Mtakatifu kutuza mara ya pili, yaani kutupatia uhai wa kiroho. 4. Viongozi wa makanisa wanashutumiwa kwa kuendeleza tamaa zao wenyewe na kukosa kuajibika katika kazi zao (Ezekieli 13:1-23). Viongozi waliwakosea watu kwa kukosa kuongoza jinsi ilipaswa kwa sababu hii watu waligawanyishwa kwa sababu ya kukosa mchungaji (Ezekieli 43:4-5). A. Ezekielia anatufundisha kwamba viongozi walikuwa na jukumu la kuwafundisha watu kumhusu Mungu na kuwaonya watu dhidi ya dhambi. Walikuwa na uajibu wa kuwashughulikia wale ambao walikuwa wagonjwa, wajane na mayatima kama tu kondoo wao. B. Uongozi katika kanisa la Kristo, ni jambo la muhimu sana. Viongozi wanapaswa kuhubiri Injili na pia kuwashughulikia watu kwa upendo (Matendo ya Mitume 20:28; Wakolosai 4:17; 1 Timotheo 4:16; 1 Petro 5:2-4; Yakobo 3:1). Waza juu ya onyo ambazo zinapeanwa kwa viongozi wa makanisa. C. kazi ya uchungaji haiwezi kufanywa vyema bila mtu kuwa na moyo wa kuchunga. Ni lazima uitwe na Mungu kuwa mchungaji. VII. Kwa kumalizia 1. Mungu alimpataia Ezekieli kazi ya kuwaambia watu kwamba wakati wao katika utumwa ulikuwa uwe mrefa na wa maisha magumusana. Sehemu ya kwanza ya ujumbe wake ilihusu hukumu au adhabu. Baada yah ii, kulikuwa kuwe na kurejeshwa kwao Yerusalemu na kupata kibali cha Mungu ikiwa wangetubu. 2. Mara kwa mara Ezekieli alinukuu Agano Jipya kwani nukuu 69 na 48 zimo katika kitabu cha Ufunuo. Hili ni dhihirisho la kweli kwamba Mungu ataleta urejesho kwa watu wake ambao sasa ni wale wote ambao wanamwamini Kristo. 3. Ezekieli alifundisha kuhusu kurudi kwa bwana and kuishi miongoni mwa watu wake (Ezekieli 48:35). 4. Biblia inafundisha kwamba huwa kunakuwa na huzuni kubwa sana wakati Mungu anawaacha watu wake (Hosea 9:12). 5. Ni uwepo wa Mungu ambao unafanya mbinguni kunakuwa mahali pazuri sana. Ni uwepo wa Mungu katika kanisa ambao unafanya kanisa na maisha yetu kuwa mazuri. 6. Ufunuo 7:15-17, tunasoma kuhusu jinsi mbinguni kulivyo, hiyo yote ni kwa sababu Mungu yumo humo. KITABU CHA DANIELI Danilei ndio wa mwisho kwa manabii ambao vitabu vyao ni vikubwa kwa maandishi. Danieli alifanya kazi wakati wa Ezekieli na Yeremia. Aliishi wakati Yerusalemu ilivamiwa na kuangamizwa na mfalme Nebukaduneza wa Babeli. Wakati Israeli ilipelekwa katika utumwa, Danieli alikuwa kijana mdogo na huko Babeli ndipo aliishi maisha yake yote. Danieli alikuwa amesoma kwa sababu tunsoma kwamba alifanya kazi katika nyumba ya mfalme. Danieli aliishi wakati wote wa utumwa wa Isreali na pia alishuhudia kurudi kwa Israeli Yerusalemu lakini yeye hakurudi. Alikuwa mtu mcha Mungu ambaye aliishi maisha matakatifu. Alikuwa kama Yusufu. Yeye na marafiki wake walionyesha kwamba inawezekana kuihsi katika nchi ambayo inamchukia Mungu na wakati huo huo uendelea kuwa mwamainifu kwa Mungu. Katika Biblia tunasoma kuwahusu watu fulani ambao walijipata katika matatizo makubwa sana; Abrahamu, Nuhu, Daudi na Musa. Lakini wote walionyesha ukakamavu wao kwa kuendelea kumtumainia na kumwamini Mungu pekee. Je, ilikuwaje kwamba Danieli alikuwa na ushuhuda mzuri sana kumhusu Mungu ilhali aliishi miongoni mwa watu waovu? Aliweza kwa sababu alisoma neno la Mungu na pia aliomba Mungu kila wakati. Yeye aliomba kabla ya kueleza maana ya ndoto ambazo aliota. Katika Danieli 9, kuna ombi ambalo tunafaa kusoma na kujifunza kwa sababu tutaona pia sisi jinis tunapaswa kuomba itupasavyo. Katika kitabu cha Danieli tunapata hadithi nyingi za kuhimiza na aqmbazo zinfahgamika sana na wengi. Kwa mfano wengi duniani wanafahamu kwamba Danieli alitupwa katika shimo la simba. Pia kitabu hiki cha Danilei kina mojawapo wa unabii ambao wengi hawaueleiwi. Danilei mwenyewe pia hakufahamu unabii wake mwingi n ahata baadhi ya unabii wake, bado hatuuelewi. I. Utangulizi wa kitabu cha Danieli (Danieli 1:1-21). 1. Ilikuwa tabia ya mfalme Nebukaduneza kuwachukua baadhi ya wale ambao walikuwa katika utumwa na kuwafanya wa viongozi katika nyumba ya mfalme na walifundishwa kufanya kazi ya serikali. A. Danieli na marafiki wake watatu, walitawazwa kufanya kazi katika nyumba ya mfalme. Wababeli walitaka kuwageuza hawa vijana kuacha kuwa Wayahudim na wawe Wababeli. Jabo la kwanza walifanya ni kuwapataia vijana hawa majina mapya. i. Danieli 1:6-7, miongoni mwa hawa vijana kulikuwa na Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria kutoka katika kabila Yuda. Mkuu wa mafisa alibadilisha majina yao: Danieli aliitwa Belteshaza, Hanania akamwita Shadraki, Mishaeli akamwita Meshaki na Azaria akamwita Abednego. ii. Wababeli walikuwa wamejotlea kabisa kuwabadilisha wale vijana wa miaka 14, kuwa Wababeli ambao wanaabudu miungu yao. Majina yao halisi yalimtukuza Mungu lakini majina yao maya yalitukuza miungu ya Wababeli. B. Danieli na wenzake mara kwa mara walichukua hatua za imani ili waendelee kuwa waaminifu kwa Mungu. Wao walijaribiwa sana na jaribu la kwanza lilihusu chakula ambacho walipewa. Danieli alijitolea kutii sheria yua vyakula ambayo Mungu alikuwa amewapa. Kwa sababu hii aliwaeleza wale wakuu wa maafisa kile chakula ambacho alikitaka. Danieli aliwaambia kwamba hataka kulazimishwa kula kile chakula ambacho si kisafi (Danieli 2:5-16). i. Danieli kwa heshimu aliwaambia wale ambao walikuwa wamewekwa kuwashughulikia kwamba kwa siku 10 wawapatie chakula ambacho Mungu alikuwa amewaambai wale Wayahudi. Mungu alihakikisha kwamba Danieli na wenzake walieendelea vyema kiafya kwa hizo siku 10 zaidi kuliko wale wengine. 2. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa mafundisho ya miaka 3. Baada ya miaka 3, mafundisho yaliisha na Danieli na wenzake waliletwa mbele ya mfalme (Danieli 1:19-20). Hawa wane ndio walipatikana kuwa wanafunzi bora ambao walikubalika na mfalme. 3. Wao walipewa vyeo vya juu na baada ya miaka 70, Danieli bado alikuwa akifanya kazi humo. Danieli aliendelea kuwa mamlakani hata wakati Babeli alivamia na wafalme wengine (Danieli 1:21). 4. Hawa vijana waliendelea vyema sana kwa sababu walimtukuza Mungu kwanza na walimwamini Mungu pekee. Kitabu cha 1 Samweli 2:30, tunasoma kwamba wale ambao wanamtukuza Mungu, Mungu atawaheshimu. II. Matokeo katika maisha ya Danieli (Danieli 2:1-6:28) 1. Danieli 2, tunsoma kuhusu matokeo ya hatari sana katika maisha ya danieli na wenzake. Nebukanuneza alikuwa na ndoto ambayo ilimwogopesha sana na alitaka kujua maana ya ndoto hiyo. Wale waganga wake hawakuweza kueleza maana ya ndoto hiyo kwa sababu hiyo, mfalme alitisha kuwaua. Danieli na wenzake waliingilia kati na wakaomba na Mungu akawaeleza maana ya ndoto hiyo. A. Danieli 2:28-30, Danieli anamsifu Mungu ambaye alimwezesha kueleza maana ya ndoto hizo. Hili ni funzo kubwa sana kwetu, ni Mungu ambaye anamwezesha mhubiri kuhubiri vizuri. Ni nguvu za Mungu ambazo huwa zinwaponya wengi na wala si nguvu zetu. Yunapaswa kuwa wanyenyekevu na kujua kwamba kila kitu ambacho tunakifanya, tunakifanya kwa nguvu za Mungu na wala si kwa nguvu zetu. B. Ndoto ya mfalme ilihusu kuja kwa mafalme nyingi katika ulimwengu. Falme nne zimekuja na zimeondoka. Ufalme wa Warumi ndio ulikuwa wa mwisho. i. Danieli 2:44-45, Ufalme wa mwisho ni Ufalme wa Kristo Yesu ambao ni wa milele. Huu ni mfano mkubwa ambao unaelezwa hapa. Zaburi 118:22 tunaona ufalme huu ukielezwa. Mwamba unadhihirisha kuwepo milele. C. Mfalme nebukanuneza alifurahia sana na akampa Danieli cheo cha juu. Katika mstari wa 47, mfalme Nebukaduneza anatambua kwamba Mungu wa Danieli ni Mungu wa miungu na Mfalme wa wafalme. Lakini hata kama alisema haya, Nebukaduneza hakuwa ameokoka. Yeye alikuwa mwabudu sanamu na wala si mwabudu Mungu wa kweli. Kumjua tu Mungu haitoshi, tunapaswa kuacha miungu yetu na kuweka imani yetu ndani ya Kristo Yesu pekee kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu. 2. katika Danieli 3, tunaona kwamba Nebukaduneza bado yeye alikuwa mwabudu sanamu kwa sababu alitengeneza sanamu kubwa na akawamuru watu wote waiabudu. Danieli na wenzake walikataa kuiabudu na kwa sababu walitupwa katika tanuri la moto wafe. Lakini Mungu alihifadhi maisha yao. Mfalme alipoangalia katika tanuri aliwaona watu wane badala ta watatu. Huyu alikuwa Bwana Yesu Kristo ambaye alikuwa amekuja kuwa na watu wake wakati wa majaribu makali sana. Isaya 43:2, tunahimizwa kwamba Bwana wetu Yesu kristo kila wakati ako pamoja nasi hata wakati wa shida na majaribu makali sana. A. Nebukaduneza alifurahishwa na Mungu lakini hata wakati huu, yeye hakuokoka alibaki akiwa mtu mwenye kiburi na majivuno. 3. Danieli 4, tunasoma kuhusu maono mengine, tena ni Danieli pekee ambaye anaweza kueleza maana yake. Nebukaduneza ndiye alikuwa kiongozi mkuu katika ulimwengu na kwa hiovyo alikuwa amejawa na kiburi kwa sababu yay ale ambayo alikuwa ameyafanya. Kwa sababu hii Mungu aliamua kuwadhibu. A. Mungu alimfanya ale nyasi kwa miaka 7. Hali ya aina hii ipo hata leo kuna watu ambao wanawaza kwamba wao ni wanyama na wanaishi kama wanyama. Ugonjwa huu unajulikana kama Lycanthropy kwa kingereza. B. Funzo kwetu hapa ni kwamba Nebukaduneza alikuwa mtu mwenye kiburi ambaye alijisifu sana badala ya kumsifu Mungu ambaye alimwezesha kutekeleza yale yote ambayo aliyatekeleza. Kwa sababu hii, Mungu aliwadhibu kwa kufanya aishi kama mnyama na kula nyasi kwa miaka 7. Kusudii la hii ilikuwa kwamba Nebukaduneza anyenyekezwe. C. katika mistary ya 33-37, tunasoma kwamba baada ya miaka 7, Nebukaduneza alimsifu Mungu. Mungu huwa anamkweza mtu ili aweze kumwokoa. 4. Miaka 20 baadaye tunasoma sura ya 5 ambapo tunasoma kuhusu utawala wa mfalme wa mwisho wa babeli ambaye aliitwa Belshaza. Mkono uliandika kwenye ukuta na tena Danieli aliitwa kuja ili aeleze maana ya maneo ambayo yalikuwa yameandikwa. Alieleza kwamba Ufalme wa Belshaza ulikuwa umefika mwiosho wake. Siku hiyo hiyo, usiku Wamedi na Waajemi walikuja na kuvamia Babeli. 5. Danieli 6, tunsoma kuhusu Danieli akiwa katika tundu la simba. Sasa Darias ndiye alikuwa mfalme wa Wamedi na Waajemi. Hadithi ni rahisi kusoma kwa hivyo tutazungumza machache. Kuna mambo ambayo yanafanana na hadithi ya kitabu cha Esta. Watu hawa waili walipendwa na wafalme na wote walikuwa na maadui ambao walitaka kuwaua. Kulikuwa na sheria katika ufalme wa Wamedi kwamba mfalme anapotoa agizo haliwezi kubadilishwa. Katika hali zote mbili, yaani ya Danieli na Esta, mfalm,e alifanya uamuzi ambao baadaye alijuta kwa sababu hakujua kwamba uamuzi wake ungesababisha vifo vingi sana. Esta na danieli wote walimwamini Mungu kuwaokoa na waliendelea kuwa waaminifu kwake. Katika matokeo yote, Mungu aliwaokoa na kuangamiza maadui wao. Leo tunapaswa kumwamini Mungu atukomboa kutoka kwa mikono ya maadui wetu. Hata kama kwa wakati mwingine hata tukomboa kutoka kwa kifo cha mwili, Yeye atatukomboa kutoka kwa kifo cha kiroho. A. Kwa sababu yah ii, Danieli alipendwa sana na mfalme na aliwekwa katika cheo ambacho angekitumia kuwasaidia Wayahudi. III. Sehemu nyingine ya kitabu ya Danieli inahusu unabii tofauti tofauti ambao unadhihirisha utawala wa Mungu juu ya mataifa yote ya ulimwenguni. 1. Maandishi ya sura 6 za Danieli, zinahusu mambo ya mebeleni. Ni sura ambazo zinahusu ziku za mwisho. Mambo haya yanapatikana katika vitabu kadhaa za Biblia kama Isaya, Yoeli, Zekaria, Danieli na Ufunuo. Maandishi haya yamejawa na ishara, ndoto na maono. Mambo haya yanafanya maandiko haya wengi wayapate yakiwa magumu kwao kufahamu. 2. Danieli 7, tunasoma kuhusu maono juu ya falme 4. Kuna mambo ambayo yanafanana kama yale ya sura ya 2. Unaposoma kuhusu falme hivi, utaona kwamba kila moja ikon a nguvu na inaofya sana kuliko ili ambayo iliitangulia. Wakati huu tunaona hukumu itangazwa. Vita za enzi vikawe kwa, naye Mzee wa Siku akaketi kuhukumu. Falme hizi zote zimepita na falme ya Warumi ndio ilikuwa ya mwisho. A. Mstari 8, tunsoma kuhusu pembe ndogo ambayo wengi wanawazia kuwa moinga Kristo au yule mtu wa kuasi (2 Thesalonika 2). B. Kuna pingamizi nyingi kuhusu utafsiri wa kifungu hiki, lakini hata hivyo kuna mambo mengi ambayo yako wazi kuelewa. Danieli aliinua macho yake huko mbinguni akaona falme zikiondoka na zingine zikija na kuendelea hadi mwisho wa nyakati. C. Danieli anapoangalia juu katika mistari ya 9-10, aliona Kristo akiwa katika utukufu wake. Alimwona Mungu mkuu ambaye ana nguvu za kuwakweza wale wote ambao wanampinga. Muingu ndiye anaye hukumu. D. Katika mstari wa 13, tunaona kwamba maono hayo yanaendelea. Tunamwona Kristo ambaye anaonekana kama mwanadamu. Imeandikwa hivi kwa sababu Kristo alikuwa hajakuja humu duniani. Tuanona katika mstari 14, kwamba yesu kristo amepewa nguvu juu ya ufalme wa milele. E. Tunaona katika mistari ya 24-27, tunaona kwamba pembe ili ndogo au mpinga Kristo atafkuja baada ya zile falme na kutawala ulimwengu. Histroia yote inatuongoza kwa wakati ambapo mpinga Kristo atakuja akiwa na nguvu na kuwatesa wakristo. Mpinga Kristoa ataongoza hadi wakati ule nguvu za mbinguni zitamwondoa na wakristo watakuwa washindi dhiai ya uovu (mstari wa 26). Mstari wa 28, tunasoma jinsi Danieli alisumbuka kwa sababu ya kile ambacho alikiona. Lakini tunaosma kwamba hakumwambia mtu yeyote. F. Maono katika sura ya 7, yanahusu yale yatakayofanyika katika ulimwengu. Uovu utaonekana kuwa unashinda kwa muda, n ahata kuonekana kwamba umekuwa na nguvu nyingi kushinda zile za Mungu. Wakristo watateseka na kanisa litajifucha. Wakati uovu utakuwa umekuwa na nguvu sana, hapo ndipo Bwana yesu Kristo atarudi kwa ushindi mkubwa sana dhidi ya uovu. 3. Katika sura ya 8, tuna maono mengine. Mstari wa 2, unaeleza kwamba Danieli alichukuliwa katika Roho na kupelekwa katika mji mkuu wa wamedi. Maono yatueleza kuhusu falme ambazo zilionekana kuwa za mbeleni kwa danieli lakini leo kwetu ni zimeshapita. A. katika mstari wa 9, hata kama danieli alikuwa anaona pembe 4, yeye alishughulika na moja tu ambayo ilikuwa ndogo. Pembe hiyo ndogo, inadhihirisha kwamba kutakuwa na kiongozi mmoja ambaye atachukua hatama za uongozi juu ya watu ambao wanaitwa Seleucids ambaye angetawala Wayahudi kwa miaka 400 kati ya Agano la kale na Jipya. Katika mistari ya 10-12, tunsoma kuhusu wakati mbayas ambapo huyu kiongozi atawaua Wayahudi. Huyu kiongozi amlikuwa mbaya sana kwa wayahudi, hata aliwakataza kutoo sadaka kwa Mungu na kuabudu Mungu. Kiongozi wao mmoja maybe aliitwa Antiochus Epiphanes alileta uabudu sanamu katika Hekalu. Huu ulikuwa wakati mgumu sana katika maisha ya wayahudi. B. Danieli aliambiwa katika mistari 13-14, kwamba wakati huu wa mateso makali sana utakuwepo kwa miaka 6 na miazi 4 halafu Hekalu itasafishwa na wayahudi waweze kuabudu Mungu tena iwapasavyo. Hili lilifanyika. C. Je, maana ya haya yote kwa Wayahudi ilikuwa gani? Mstari wa 16, tunsoma kwamba sauti ilimwamuru malaika amwelezee Danieli haya mambo yote. Hii sauti ilikuwa ya Yesu Kristo kwa sababu ni Mungu pekee ambaye kumwamuru malaika. i. Unabii huu ulileta faraja kubwa sana kwa wayahudi ambao waliteswa sana wakati wa Antiochus. Hii ni kwa sababu katika mstari wa 25, Wayahudi waliambiwa kwamba mateso yataisha. Waliambiwa kwamba kwa wakti mzuri, Mungu angemwondoa yule ambaye alikuwa anawatesa. 4. Danieli 9:1-2, tunaona kwamba Danieli alikuwa anasoma maandiko na aliona kwamba mwisho wa wa miaka 70 ya mateso ya Wayahudi ulikuwa umefika na kwamba Mungu alikuwa anaenda kuwarejesha. Hapa Danieli alikuwa na miaka 84, naye alikuwa bado anasoma Neno la Mungu. A. Danieli aliomba. Katika msitari ya 3-19, tunsoma kuhusu ombi la Danieli. Ombi hili ni zuri sana na tunapaswa kujifunza sana kutokana nalo. Tutazame yale ambayo tunajifunza kutokana ombi hili. i. Danieli alikuwa mtu wa maombi. ii. Danieli alikuwa karibu sana na Mungu lakini hata hivyo alikuja mbele za Mungu kwa heshima. 1. Katika maombi yake anakiri kwamba yeye na watu walikuwa wametenda dhambi na kwamba ni dhambi zao ambazo zilisababbisha Mungu awadhibu (mstari wa 11,14). iv. Danieli alikuja kwa Mungu akiamini katika huruma wa Mungu (mstari wa 4). v. Danieli alikuja kwa Mungu na hitaji. Yeye alimwambia Mungu kile ambacho alikuwa anataka. vi. Danieli aliomba akiwa pekee yake. B. katika mstari wa 20-27, tunsoma kwamba ombi hili lilisikika mbinguni wakati alipokuwa anaomba. Malaika Gabrieli alikuja kwake na majibu ya maombi yake. Kuna mawazo kadhaa kwa kadhaa kuhusu maneno ya maliaka Gabrieli. Wacha tuone wazo moja. i. Mstari wa 25, unahusu ujenzi wa Yerusalemu wakati wa Ezra na Nehemia. ii. Pia tunsoma kuhusu kutabiri kumhusu Mesiya (mstari wa 25). 5. Danieli 10-12, ni sehemu moja ambayo ikon a maono mrefu sana. A. Danieli 10, tunsoma kuhusu Danieli akiomboleza juu ya shida ambazo watu wake walikuwa wanaenda kukumbana nazo. i. Pia tunaona kwamba kuna vita vya kiroho ambavyo vinanendelea. Katika biblia tunaelezwa kidogo kuhusu ulimwengu wa kiroho ambao unajumlisha nguvu ambazo ni mzuri na zile ambazo zinampinga Mungu. Shetani ndiye kiongozi wa zile nguvu ambazo ziko kinyume na Mungu. B. Danieli 11:12:1-4, tunasoma kuhusu maono ambayo yako na sehemu tatau. Kuna mawzo tofauto tofauti kuhusu unabii huu. Maono hayo yanaonyesha historia ya wakati wa Danieli hadi wakati wagiriki walitawala Israeli kati ya Agano la kale na Jipya. Maono hayo yanaonyesha siku za mwisho ambazo zitakuwa siku za mateso makali sana. i. Sehemu ya kwanza inapatikana katika mistari ya 1-19. Danieli alikuwa anatabiri matokeo ya mbeleni ya taifa la Israeli, lakini kwetu leo, matokeo haya ni historia. Matokeo haya yalitokeo wakati wa miaka 400 kati ya Agano la kale na Jipya. Unaposoma kuhusu historia ya 400 hii utaona kwamba utabiri wa Danieli ulitimika. ii. Sehemu ya pili ya unabii huu inapatikana katika mistari ya 20-35. Inahusu Antiochus Epiphanes ambaye alikuwa mwovu sana ambaye alitawala 400 katika Agano la Kale na Jipya. Yeye alitajwa katika sura ya 8 kama pembe nyingine. Ni yeye ambaye alileta uabudu sanamu katika hekalu. Historia iansema mengi kuhusu kiongozi huyu na kuonyesha kwamba yale ambayo danieli alisema yalitimika. 1. Sehemu ya mwisho ya unabii huu inapatikana katika Danieli 11:36-12:4. Kuna kutokubaliana kuhusu maana ya unabii huu. Je, tunafaa kuuchukua kama ulivyo au ni mfano? Je, ni historia au yanahusu yale ambayo yatafanyika wakati wetu? Mimi ninadhani kwamba unabii huu unahusu maisha yetu ya mbeleni kwa sababu hatuoni historia yoyote na pia mstari wa 40, unazungumza kuhusu vita wakati wa siku za mwisho. Huu ndio wakati Yesu atakaporudi na tuko na vita vya mwisho wakati shetani atashindwa kabisa na yesu atatwala milele. iv. ujumbe ni kwamba watu wa Mungu watakumbwa na majaribu na mateso mengi sana. Je, tunapaswa kufanya nini wakati huu wa mateso makali sana? Daniali 12:11, tunaosma kwamba wale ambao tumeokoka, tunavumilia katika mateso. C. Danieli 12:5-14, ndio mwisho wa kitabu cha Danieli. Maswali yanaulizwa na hakuna majibu. Tunaona kwamba kuna mambo ambayo Danieli haelewi na hata sisi hatuyaelewi. Wakati na jinsi mambo yatakavyofanyika siku ya mwisho hatujui kabisa. D. Mafundisho matatu kutoka katika danieli 12. i. Sehemu ya mwisho ya mstari wa 4, tunasoma kwamba watu watajifunza mengi lakini hawakuwa na kufahamu. Leo katika ulimwengu tunaona wengi wakisoma katika Nyanja tofauti tofauti kama sayansi, lakini ukweli ni kwamba hawana ufahamu. Hawa watu ambao wanadai kusoma sana, wamemkataa Mungu. Mithali 9:10 tunasoma kwamba hekima hutoka kwa Mungu. ii. Tunaona pia kwamba uovu utaendelea kuzidi (Danieli 12:7 na 10-11). Leo tunaona uovu ukiendelea kuzidi miongoni mwetu leo. 1.jambo la mwisho tunaona ni njia ya wenye haki. Sura ya 12, inatuhimiza sisi watu wa Mungu kwamba tutashinda katika mateso makali sana. Tunashinda kwa imani na tunaona hili katika mstari wa 9 kwa sababu Mungu hatatueleza kila kitu. Ni lazima tumwamini Mungu katika kila kitu hata katika yale ambayo hatuyaelewi. iv. katika mstari wa 10, tunaona kwamba mateso yanakuja na kwamba mwishowe wale ambao tumeokoka tunadumu na wala si wale ambao hawajaokoka. Hatuelewi mstari 11, lakini wa 12, tunsoam kwamba kwa wakati ambao Mungu anapenda, wale ambao tumeokoka tutapewa ufahamu na tutafurahia kwamba tulimwamini Mungu. Mstari wa 13, tunaosma kwamba wale tutakuwa waaminifu hadi mwisho, tutazawadiwa. MAFUNDISHO YA JUMLA YA MANABII AMBAO KURASA ZA MAANDISHO YAO FUPI Kuna vita 12 katika Biblia ambavyo ni vitabu vya manabii lakini kurasa zake ni fupi. Tutazama vitatu pekee kwa sababu ya wakati. Kama vitabu vingine vya manabii, huwa havifundishwi katika makanisa. Sababu kuu ni kwamba huwa havieleweka kwa rahisi. Sababu nyingine ni kwamba ujumbe wake ni hukumu, ujumbe amabo wengi hawapendi kuusikia. Hii ni mbaya kwa sababu vita hivi vina mengi ya kutufundisha. KITABU CHA HOSEA Hiki ndicho kitabu cha kwanza kati yah iv 12. Vitabu hivi vinapatikana katika sehemu ya mwisho ya Agano la Kale. Njia bora ya kusoma vitabu hivi, ni kusoma ukiwa na kitabu ambacho kina historia ya nabii ambaye unasoma. Hosea alikuwa nabii katika taifa la kasikazini wakati wa 2 Wafalme 14-17. Huu ndio ulikuwa wakati wa mwisho wa taifa hili la kasikazini wakati Washuru walilivamia taifa hili na kuliangamiza. Ujumbe wa Hosea ni ujumbe mgumu sana. Mungu alikuwa amekasirika na watu wake kwa sababu walikuwa wameasi kwa kuabudu miungu. Mungu alimwamuru Hosea kumwoa kahaba kama njia ya kuwaonyesha Waisraeli kile ambacho walikuwa wamemfanyia. Israeli walikuwa wamefanya ukahaba kwa kumwacha Mungu wa kweli ambaye alikuwa amewashughulikia siku hizi zote na kuenda kwa miungu. Israeli walikuwa wamemwacha Mungu ambaye alikuwa amewapatia chochote ambacho walikihitaji. Jambo hili lilidhihirika kwa jinsi Gomeri alivyoishi maisha yake na Hosea. Hosea alikuwa na maisha magumu sana. Yeye alikuwa amemwoa mwanamke ambaye alimshughulikia, lakini Gomeri alimsliti kama tu vile Israeli alikuwa imemsaliti Mungu. Mungu aliwapenda watu wa Waisraeli na hata aliwatumia manabii. Watu walihitaji ktubu dhambi zao ili Mungu asileta ghadhabu yake kwao. Kuwepo kwa taifa la Kasikazini ni ishara ya uasi wa Israeli dhidi ya Mungu. Taifa hili lilikuwepo kwa sababu ya uasi. I. Hosea 1-3, ni sehemu ya kwanza ya kitabu inafundisha kuhusu ndoa ya Hosea na Gomeri ambayo ilikuwa kama ishara ya uhusiano wa Mungu na Israeli 1.Tunasoma kuhusu hadithi ya Gomeri na Hosea ambayo ilikuwa ishara ya uhusiano wa Israeli na Mungu. Mungu alipenda Israeli na aliwashughulikia kama tu vile Hosea alimpenda Gomeri na kumshughulikia. Isreali walianza kuabudu miungu kama tu vile Gomeri alifanya ukahaba na wanaume wengine. Kila mara Hosea alimchukua na kumrudisha na vivyo hivyo Mungu kila mara Mungu alikuwa akiwakomboa watu wake kutoka katika shida zao mara kwa mara. II. Hukumu ili tangazwa dhidi ya Israeli. Sehemu ya Hosea 1-3, ni muhtasari wa miaka 40 ya mafundisha ya Hosea kuhusu dhambi za Isareli na hukumu ambayo ilikuwa inakuja. Hosea aliwahubiria watu kwamba walifaa kumrudia Mungu. III.Hosea 11:12-13:16, Hosea anasema kwamba adhabu ambayo Waisraeli walikuwa wapate walifaa kuipata kwa saba ya tabia yao ya kumwacha Mungu kila mara. Mungu aliwaonya mara kwa mara lakini wao hawkusikia waliendelea tu katika dhambi zao. Kwa sababu hii Mungu aliwadhibu watu. Hata katika hasira, bado Mungu hakuwaadhibu wote. IV. Hosea 14, tunasoma kuhusu kurejeshwa kwa Isreali. Neema ya Mungu inadhihirika wakati Mungu anasema kwamba atawarejesha watu wake na hawatawahi kuabubu miungu. Mioyo yao itabadilishwa. Hapa pia tunafananisha sehemu hii na uhusiano wa kristo na kanisa lake. 1. Vile tu Hosea alikuwa amemwoa Gomeri, vivyo hivyo Mungu ndiye alikuwa Mume wa Israeli. 2. Kama vile Gomeri alivyokosa kuwa mwaminifu kwa Hosea, vivyo hivyo Isreali hawakuwa waaminifu kwa Mungu. 3. Kama tu Gomeri alikuwa amefanywa mtumwa na wapenzi wake, vivyo Israeli alikuwa amefanywa mtumwa na mataifa mengine ambayo waliyaamini. 4. Kama vile Hosea alivyomrejesha Gomeri, Mungu angewarejesha watu wake ambao walikuwa waaminifu kwake. 5. Kama tu vile Hosea alimkomboa mke wake kwa fedha na mtama, Kristo naye angewakomboa wake yaani kani sa lake kwa damu yake. Unabii katika Hosea 1. Hosea 11:1, tunaosma Mungu akisema kwamba wakati Israeli alipokuwa mwanawe, alimpenda na kumwita kutoka Misri. Unabii pia unahusu Kristo akilegea kutoka Misri ambapo alikuwa amepelekwa na wazazi wake wakimkimbia Herode ambaye alitaka kumwua (Mathayo 2:14-15). Misri ni mfano wa utumwa wa kiroho. Yesu Kristo amekomboa wake kutoka katika utumwa wa dhambi. 2. Hosea alitabiri kukataliwa kwa Wayahudi ambako kulifanyika wakati Yerusalemu aliangamizwa katika mwaka wa 70 AD. Katika warumi 9:22-26, Pauli ananukuu Hosea 2:23 na Hosea 1:10 kueleza kwamba Wayahudi na watu mataifa wote watahurumiwa na Mungu kupitia kwa Kristo Yesu. 3. Kufufuka kwa Kristo na Kanisa lake. A. Hosea 6:2 ni unabii kuhusu kufufuka kwa wafu. B. Hosea 13:14 ni unabii ambao unalinganisha kufufuka kwa Kristo na kule kufufuka kwa wafu. Kufufuka kwa Kristo ni hdihirisho kwamba hata sisi tutafufuka kutoka kwa wafu His (1 Wakorintho 15:20). Jinsi tunaopaswa kuishi maisha yetu kulingana na mafundishio haya. 1. Kuchaguliwa kwa neema. Kama tu vile Hosea alimchangua Gomeri na udhaifu wake wote, vivyo hivyo, Mungun hutuchagua tukiwa hatuna lolote zuri la kutamaniwa katika maisha yetu. Mungu bado hufanya jinsi Hosea 11:4 inavyofundisha: “Niliwaongoza kwa Kamba za huruma ya kibinadamu, kwa vifungo vya upendo; niliondoa nira shingoni mwao name nikainama kuwalisha.” 2. Mungu hahitaji sadaka, bali anataka kurumia. Hosea anafundisha kwamba bila huruma, sadaka zetu ni bure (Hosea 4:1-2). Kwanza lazima Mungu atuhurumie ikiwa kweli tutao sadaka ambazo zinampendeza. 3. Uongozi ni jambo la muhimu sana kwa Mungu. Hosea anakemea uongozi mbaya wa wakati wakati. Viongozi wabaya huwaongoza watu kwa njia mbaya sana (Hosea 4:5; 4:6; 5:1; 6:9; 10:5; 5:10; 7:3-7; 9:15). Kwa kumalizia Kitabu hiki kinauhusu uhusiano wa mwanadamu kama mfano wa ule wa Mungu na Israeli. Kuna vitisho vya hukumu kwa kukosa kutii na ahadi za baraka kwa wale ambao wanamtii Mungu. Tunasoma kuhusu ahadi kuhusu siku nzuri za mbeleni na Amani ya milele. Kwa nguvu zake Mungu na neema Yake, Mungu atawakomboa watu wake kutokana na kifo na jahanum. KITABU CHA AMOSI Kutoka na Amosi 1:1, tunasoma kwamba Amosi alikuwa mchungaji wa mifugo. Hii kazi ya mtu wa kawaida tu. Yeye hakuwa kama Isaya ambaye alikuwa amesoma sana. Amosi hakuwa tajiri. Yeye aliishi Yuda na katika Amosi 7:15, tunasoma kwamba alitumwa kuwa nabii katika taifa la kasikazini la Israeli. Katika mstari wa 1, tunasoma kuwahusu wafalme wa Israeli na Yuda. Kutokana na hili tunajua kwamba Amosi aliishi wakati maisha hayakuwa mabaysa sana wakati wa miaka 30 kabla ya wa Ashuru kuvamia taifa la kasikazini. Wakati watu walikuwa matajiri nan chi ilinawili vizuri, watu walimsahau Mungu. Tutazame mafundisho ya kitabu cha Amosi 1. Amosi 1-2, tunaona Amosi katika Israeli akihubiri kwamba Mungu alikuwa anaenda kuleta hukumu kwa mataifa ambayo yalikuwa yamewazingira kwa sababu dhambi zao. Amosi 1:3, kwa sababu ya dhambi tatu au nne Mungu hatakosa kuleta hukumu. Hii ni dhihirisho kwamba watu walikuwa wanaendelea kufanya dhambi mara kwa mara. A. Amosi chapter 1:3-10, hukumu kwa mataifa mengine ilikuwa imekusudiwa kuwaonya waisraeli. Miji ambayo ilikuwa ihukumiwa ni Damasku na Filistia na Tire. B. Miji mingine ambayo ilikuwa ihukumiwa ilikuwa inahusiano na Isreali. Kwa sababu hii walistahili hukumu yao. Amosi 1:11-2:3, tunapewa orodha ya miji hiyo: Edomu, Amani na Moabu ambao walikuwa na uhusiano na Israeli. C. Amosi 2:4-5, tunsoma kwamba mji ambao ulikuwa uhumumiwa pia ni Yuda. Ujumbe huu haukupendwa sana kwa sababu hukumu ambayo ilikuwa inakuja ilikuwa inakuja kwa qwayahudi. Wao walikuwa wamwasi Mungu kiroho. D. Amosi 2:6-16, Amosi anaonyesha kwamba yeye ni mtu mwenye ujasiri kwa sababu alitangaza adhabu kwa Israeli akiwa Israeli. Wakati alipokuwa anazungumza kuwahusu mataifa wengine, haikumsumbu sana. Lakini alipozungumza kuhusu taifa lake la Israeli, ujumbe wake ulikataliwa. Tunafundishwa hapa kwamba ni lazima tuwe waaminifu kwa Mungu hata kama mazingira ambayo tunahubiri neno la Mungu ni mabaya sana. Tunafaa kujitahidi kumfurahisha Mungu na wala si mwanadamu yeyote hata kama maisha yetu yatakuwa hatarini. Leo kuna wachungaji wengi wanahubiri mahubiri ambayo ni ya kuwafurahisha watu wengi. Mahubiri yetu hayafai kuwa ya kuwafanya watu furahie, bali tunapaswa kuwahubiria neno la Mungu hata kama inaonekana kwamba hawalitaki. E. Shida ambayo Amosi alikuwa anazungumzia hapa ni moja wapo wa shida ambazo zinapatikana miongoni mwa watu wa Mungu hata katika Agano Jipya. Wayahudi waliwaza kwamba kwa sababu wao walikuwa watu wa Mungu ambao walikuwa wamechaguliwa, Mungu hangeweza kuwaadhibu vikali sana. Mungu alimtuma Amosi kwao kuwaeleza kwamba wao walikuwa wamejidanganya. Watu wote watahukumiwa na Mungu kulingana na matendo yao na si uhusiano wao. Kuwa mshirika wa kanisa haitakuokoa kutoka kwa hukumu au adhabu ya Mungu ikiwa unakataa kutubu dhambi zako. Kuwa mhubiri wa neno la Mungu haitakuokoa ikiwa unataka kutubu dhambi zako. Je, nini ambacho kitakuokoa? Tubu dhambi zako na uishi maisha yako kulingana na neno la Mungu. 2. Amosi 3-6:15, tunsoma kuhusu orodha ya dhambi ambayo Isreali walikuwa wametenda. Tabia ya watu wa taifa la kasikazini ilikuwa mbaya sana kuliko ya mataifa ambayo yalikuwa yamewazingira. Kanisa la Kristo linapaswa kuwa na tabia ambayo si kama ya wale ambao hawajaokoka. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba wakati mwingine tabia ya kanisa nay ale wale hawajaokoka huwa si tofauti. Kwa mfano katika kanisa leo tunawasikia wengi wanapeana talaka kama tu wale ambao hawajaokoka. A. Amosi alizungumza juu ya dhambi mbili. Amosi 5:10, anakema dhambi ya wale ambao wako katika uongozini kwa kuwa na mahakama ya ufisadi. Pia anazungumza juu ya dhambi za matajiri (Amosi 5:11-12 & 8:4-6). Anasema kwamba wengi wamekuwa matajiri kwa kuwadanganya wale ambao ni maskini. Hili jambo la kweli hata leo katika nchi yetu. We ngin ambao ni matajiri, utajiri wao umetokana na kuwaibia maskini na kuwatumia vibaya maskini. Pia leo katika nchi yetu kuna udanganyifu mwingi katika mahakama. Kuna ukosefu wa kutekeleza haki. Amosi 4:1, Amosi aliwashitumu bila kuwaongopa matajiri wote. Mungu huwa hawafichi watu kuhusu uovu wao, Yeye huwaambia wazi wazi. 3. Amosi 5:21-24, Mungu ansema kwamba anachukia kuabud kwa Waisraeli kwa sababu hakuana maana yoyote. Katika mstari wa 24, anasema kwamba anataka wamwabudu kwa mioyo safi. Tunapaswa kukumbuka kwamba tunapaswa kumwabudu Mungu kwa mioyo ambayo imetubu na kama sivyo tuache kumwabudu kwa sababu kuabudu kwetu hakutakubalika machoni pake. 4. Amosi 7-8:10, tunasoma kuhusu maono ya mambo mabaya ambayo yalikuwa yamefanyikie Israeli. Kwa sababu ya haya, watu walimkasirikia Amosi na kumshitumu kwamba amesaliti nchi yake. Kwa sababu hii walimweleza kwamba anapaswa kurudi Yuda (Amosi 7:9-17). Huwa hatutaki kusikia maneno kama haya, lakini tunapswa kuwa waangalifu sana na makini sana na kubadili mwenendo wa maisha yetu. Baada ya miaka 30 baadaye, Israeli alishindwa na Ashuru na sasa Israeli haipo tena. 5. Amosi 9:1-4, tunsoma kuhusu Mungu ambaye yuko kila mahali. Hakuna mahali ambapo unaweza kutorokea kutoka kwa Mungu. 6. Kitabu hiki kinamalizkia kwa ujumbe wa tumaini (Amosi 11-15). Hata kama tunaona kwamba Israeli walikuwa wenye dhambi sana, Mungu bado alikuwa bado anawapenda na kwamba siku moja kupitia kwa ukoo wa mfalme Daudi, Isreali na mataifa mengine watafurahia baraka za Mungu. KITABU CHA MIKA 1. Mika na Isaya walikuwa manabii wakati moja na wakati mwingine ujumbe wao ulikuwa sawa. Kwa mfano soma Mika 4:1 na Isaya 2:3. Mika alikuwa nabii ambaye aliishi Yuda. Tutatazama baadhi ya mafundisho ya Mika yakilinganishwa na mafundisho ya manabii wengine. 2. Ujumbe wa Mika ni kwamba Mungu anawapenda watu wake, lakini pia Mungu anachUkia dhambi. Mika alichukia sana jinsi matajIri walivyokuwa wanawaibia maskini (Mika 3:1-3). Je, Mungu anawaza nini kuhusu mataifa ya Afrika? Mika 7:3, anataja dhambi ya kutoa na kula rushwa. Ujumbe wa Mika ni kwamba watu wanatenda dhambi, na dhambi hiyo imetanjwa na watu waliahidiwa adhabu ikiwa hawatatubu dhambi zao. Ujumbe huu unamalizikia na ahadi ya wokovu ambao Mungu ataleta. 3. Isaya na Mika wao ni kama Mungu, wao waliwapenda watu wao na pia walichukia dhambi za watu wao. Tunaona pia Mtume Paulo alikuwa na upendo huu katika Warumi 9:3. Paulo aliwaelezea watu ukweli kutoka kwa neno la Mungu hata kama watu hawapendio ukweli huo. Paulo pia aliwalilia sana watu wake. 4. Kuna mistari miwili muhimi katika hiki ambayo inapaswa kuzingatiwa sana. Mika 6:8, “Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu. Bwana anataka nini kwako? Ila kutenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.” Katika mstari huu tunasoma kile ambacho Mungu anataka kutoka kwa kila mtu. Mika 7:18, “Ni nani Mungu kama wewe, ambaye anaachilia dhambi na kusamehe makossa ya mabaki ya uriti wake? Wewe huwi na hasira milele, bali unafurahia kuonyesha rehema.” Tunasoma kwamba Mungu ni Mungu wa kusamehe dhambi zetu. 1. Mika 5:2-4, tunsoma kuhusu kuja kwa Mesiya na kwamba atazaliwa katika mji wa Bethlehemu Efrathi. Hili lilifanyika kwa sababu Kristo alizaliwa humu. KITABU CHA YONA Yona alitumwa kuenda kuwahubiria watu wa Ninawi mji katika Ahuri. Hadithi hii ni dhahiri kwamba Mungu anawajali watu wote si wayahudi tu. Hadithi ya nabii huyo inajulikana na wakristo wengi nahata watoto. Ni rahisi sana kusoma hadith hii. Yona alikuwa mtu mgumu sana. Kitabu hiki kina sura nne tu. Tunaposoma kitabu hiki tunaona kwamba Yona hakumtii Mungu na wakati Mungu alikosa kuwaangamiza watu wa Ninawi, Yona alikasirika sana. Yona aliamurishwa na Mungu anede Ninawi awahubirie watu waweze kutubu na wasiangamizwe. Yona alikataa kumtii Mungu badala yake, alipanda mashua na kuelekea mahali kwingine na si Ninawi. Mungu alituma upenpo mkali kwa bahari na mashua ambayo Yona alikuwa ndani yake ilianza kuzama. Kutuliza upepo huo, Yona alitupwa katika bahari na mara moja upepo ukatulia. Mungu alimtuma samaki mkubwa ambaye alimmeza Yona. Yona akiwa katika samaki huyo kwa siku tatu, Yona alitubu dhambi zake na akakubali kuelekea Ninawi. Yona alienda Ninawi na akahubiri huko akiwahimiza watu watubu dhambi zao. Yona akiwa mtu mwenye huzuni sana kwa sababu Mungu aliwasamehe watu wa Ninawi. Tutazame mafundisho katika kitabu hiki cha Yona 1. Mungu anatufundisha sisi watu wake kwamba tunawajibu wa kuhakikisha kwamba tunahubiri ujumbe wa wokovu kwa watu wote. Hili ni jambo ambalo wayahudi walikataa kufanyakatika siku za Kristo (Luka 4:26-29). Wakati Yesu alisema kwamba baraka za Mungu kuelekea kwa watu wengine, Wayahudi walikasirika sana. Mungu hupokea toba ya kweli ya wenye dhambi. Mngawanyo wa kitabu cha Yona Kitabu cha Yona kimegawanyishwa katika sehemu nne. 1. Yona 1:1-16, tunasoma kwamba Mungu alimwamuru Yona aende Nianwi na kuwahubiria watu huko. Badala ya Yona kuenda huko, Yona alielekea njia nyingine. Mungu alimshugulikia Yona kwa kutuma upepo mkali sana kwa na Yona alitumpwa aharini. 2. Yona 1:17-2:10, tunasoma kwamba Mungu alimhurumia Yona ana akatuma samaki mkubw amabye alimmeza Yona. Mungu aliyahifadhi maisha ya Yona akiwa tumboni mwa samaki ili Yona aweze kuenda Ninawi na kuhubiri huko. Yona aliomba na Mungu akaiamuru samaki na ikamtapika kando ya bahari. Kumtii Mungu ndio jambo ambalo tunapswa kufanya bila kulazimishwa. Yohana 1:17 na Mathayo 12:40, Yesu analinganisha kuwa kwa Yona katika samaki kwa siku tatu na kuwa kwake katika kaburi siku tatu. 3.Yona 3:1-10, tunsoma kuhusu ujumbe wa Yona ambao ulikuwa mfupi na ulieleza ukweli. Alisema, “Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.” Yona alishangaa wakati watu na mfalme wao waliamini ujumbe wa Yona na wakatubu na Mungu akawasamehe. Tunajifunza hapa kwamba, si idadi ya maneno ambayo tunayosema inafanya watu waamini, bali ni nguvu za Mungu ambazo zinaambatana Na maneno ambayo tunayosema. 4.Yona 4:1-11, Yona alikasirika sana kwa sababu ya Mungu kuwasamehe watu wa Ninawi. Alikasirika kiwango kwamba alitamani kufa. Katika mstari wa 10 na 11, Mungu alimkemea kuhusu tabia yake ya kuujali mti sana na wala si watu ambao Mungu aliwasamehe. Tunajifunza hapa kwamba Mungu ni Mungu wa huruma kwa wale wote ambao wanatubu na kumwamini pamoja na kutii. Mungu pia alitumia Yona kuonyesha kwamba Mungu huwa hatumii watu wazuri pekee kufanya kazi yake ya kuhubiri. Paulo anasema kwamba, “Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa mlipoitwa. Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi mlikuwa na nguvu, si wengi mliozaliwa katika jamaa zenye vyeo. Laini Mungu alivichagua vitu vipunbavu vya uliwengu ili aviaibishe vyenye hekima, Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili aviaibishe vyenye nguvu. Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu abavyo haviko, ili avibatishe vile vilivyoko. Ili mtu yeyote asijisifu mbele za Mungu.1Wakorintho 1:26-29 BIBLIA NA AGANO JIPYA UTANGULIZI WA AGANO JIPYA. Utangulizi Biblia Takatifu ni maandishi ya msingi kwa Wakristo wote, lakini watu wachache huelewa mengi ya muundo wake, zaidi ya ukweli kwamba kuna Agano la Kale na Agano Jipya. Vijana, hususan, kama wanavyoendelea kuendeleza imani yao huenda wasio wazi juu ya jinsi Biblia imefungwa au jinsi na kwa nini imewekwa pamoja jinsi ilivyo. Kuendeleza ufahamu huu utawasaidia vijana - na Wakristo wote, kwa sababu hiyo - wana ufahamu zaidi wa imani yao. Kuendeleza ufahamu wa muundo wa Agano Jipya, hasa, ni muhimu kwa Wakristo wote, kwani ni Agano Jipya ambayo ndiyo msingi wa mafundisho katika Kanisa la Kikristo. Wakati Agano la Kale linategemea Biblia ya Kiebrania, Agano Jipya linajitolea kwenye maisha na mafundisho ya Yesu Kristo. Hasa matatizo kwa watu wengine ni kuunganisha imani muhimu kwamba Biblia ni Neno la Mungu na ukweli kwamba, kwa kihistoria, vitabu vya Biblia vimechaguliwa na wanadamu baada ya mjadala mkubwa juu ya nini kinachopaswa kuingizwa na kile kilichochapishwa. Inakuja kama mshangao kwa watu wengi kujifunza, kwa mfano, kwamba kuna kikundi kikubwa cha fasihi za kidini, ikiwa ni pamoja na baadhi ya injili, ambazo zilikuwa zimeondolewa kwenye Biblia baada ya majadiliano makubwa, na mara nyingi yenye uchungu, na baba za kanisa. Biblia, wasomi hivi karibuni huja kuelewa, inaweza kuonekana kama neno la Mungu, lakini pia inaweza kuonekana kama waraka uliokusanyika kupitia mjadala mkubwa. Hebu tuanze na ukweli fulani wa msingi kuhusu Agano Jipya.  Idadi ya Vitabu katika Agano Jipya :: 27  Aina ya Vitabu katika Agano Jipya: Kuna aina tatu za vitabu katika Agano Jipya. Ni Vitabu vya Kihistoria, Maandishi ya Paulo, na Maandiko Matakatifu. Vitabu vya Historia Vitabu vya Historia ya Agano Jipya ni Maandiko manne - Injili kama ilivyoandikwa na Mathayo Injili Kama ilivyoandikwa na Marko, Injili Kama ilivyoandikwa na Luka, Injili Kuma ilivyoandikwa na Yohana - na Kitabu cha Matendo. Sura hizi pamoja zinasema hadithi ya Yesu na Kanisa Lake. Wanatoa mfumo ambao unaweza kuelewa yote ya Agano Jipya, kwa sababu vitabu hivi vinatoa msingi wa huduma ya Yesu. BARUA ZA PAULO Barua zinamaanisha sehemu nzuri ya Agano Jipya ina barua 13 muhimu zilizoandikwa na Mtume Paulo, walidhani kuwa zimeandikwa katika miaka 30 hadi 50 WK. Baadhi ya barua hizi ziliandikwa kwa makundi mbalimbali ya makanisa ya Kikristo, wakati wengine Ziliandikwa kwa watu binafsi, na pamoja na hayo huunda misingi wa kihistoria ya kanuni Ya Kikristo juu ya dini nzima ya Kikristo imeanzishwa. Waraka wa Paulo kwa Makanisa ni pamoja na:  Warumi  1 Wakorintho  2 Wakorintho  Wagalatia  Waefeso  Wafilipi  Wakolosai  1 Wathesalonike  2 Wathesalonike Nyaraka wa Paulo kwa watu binafsi ni pamoja na:  1 Timotheo  2 Timotheo  Tito  Filemoni Majarida Mkuu Barua hizi zilikuwa barua zilizoandikwa kwa watu mbalimbali na makanisa na waandishi mbalimbali tofauti. Wao ni kama barua za Paulo kwa kuwa walitoa maelekezo kwa watu hao, na wanaendelea kutoa maelekezo kwa Wakristo leo. Hivi ni vitabu katika kikundi cha Majarida Mkuu: Nyaraka za Mitume wengine.  Waebrania  James  1 Petro  2 Petro  1 Yohana  2 Yohana  3 Yohana  Yuda  Ufunuo Nyaraka za Wokovu .Warumi .1Kor .2Kor .Wagalatia Nyaraka za kichungaji .1Timotheo .2Timotheo .Tito .Filemoni Agano Jipya lilikusanyikaje? Kama kutazamwa na wasomi, Agano Jipya ni mkusanyiko wa matendo ya kidini yaliyoandikwa awali kwa Kigiriki na wanachama wa mwanzo wa Kanisa la Kikristo - lakini sio kwa waandishi ambao wanasemekana. Ushauri wa jumla ni kwamba vitabu vingi vya 27 vya Agano Jipya viliandikwa katika karne ya kwanza WK, ingawa baadhi yao yaliandikwa mwishoni mwa mwaka wa 150 WK. Inadhaniwa kuwa Injili, kwa mfano, haijaandikwa na wanafunzi halisi lakini kwa watu binafsi ambao walikuwa wakiandika akaunti za mashahidi wa awali walipitia kwa njia ya maneno. Wasomi wanaamini kwamba Injili ziliandikwa angalau miaka 35 hadi 65 baada ya kifo cha Yesu, ambayo inafanya uwezekano kwamba wanafunzi wenyewe waliandika Maandiko. Badala yake, labda waliandikwa na wanachama wasiojulikana wa Kanisa la kwanza. Agano Jipya lilibadilika katika fomu yake ya sasa kwa muda, kama makusanyo mbalimbali ya maandishi yaliongezwa kwenye kanuni za kisheria kwa makubaliano ya kikundi wakati wa karne nne za kwanza za Kanisa la Kikristo - ingawa sio makubaliano ya pamoja. Injili nne tunayopata sasa katika Agano Jipya ni nne tu kati ya injili nyingi zilizopo, ambazo baadhi yao zimeachwa kwa makusudi. Wengi maarufu miongoni mwa Injili hazijumuishwa katika Agano Jipya ni Injili ya Tomasi, ambayo hutoa mtazamo tofauti wa Yesu, na moja ambayo hupingana na Injili nyingine. Injili ya Thomas imeelewa sana katika miaka ya hivi karibuni. Hata Waraka wa Paulo walikuwa wakiwa na shaka, na barua nyingine ziliondolewa na waanzilishi wa kanisa la mwanzo, na mjadala mkubwa juu ya ukweli wao. Hata leo, kuna migogoro juu ya kama Paulo alikuwa kweli mwandishi wa baadhi ya barua zilizojumuishwa katika Agano Jipya la leo. Hatimaye, Kitabu cha Ufunuo kilikuwa kinyume cha mgogoro kwa miaka mingi. Haikuwa mpaka karibu mwaka wa 400 KK ambayo Kanisa lilifikia makubaliano juu ya Agano Jipya ambayo ina vitabu 27 sawa tunavyokubali sasa. KITABU CHA MIKA Neno Mika katika lugha ya Kiebrania ni kifupisho cha jina Mikaya maana yake ni nani aliye kama BWANA?Mika aliyetoa ujumbe wa kitabu hiki ni mtu tofauti na nabii aliye na jina linalofanana na hilo, yaani Mikaya 1 Fal 26:18, Mik 1:1, 14. Mika alikuwa mkulima na mfugaji. Alitoa ujumbe nyakati zile zile za nabii Isaya katikati ya karne ya nane Kabla ya Kristo Kuzaliwa kwa wakazi wa Ufalme wa Kusini uitwao Yuda tazama Isa 1:1. Kwa kuwa ujumbe wa Mika sehemu nyingi unashabihiana na ujumbe wa Isaya, wataalamu wa mambo ya Biblia wanahisi kwamba huenda Mika alikuwa mwanafunzi mmojawapo wa Isaya Isa 8:16. Katikati ya karne ya nane Kabla ya Kristo ukulima na biashara vilistawi katika Israeli na Yuda. Hata hivyo maovu nayo yalishamiri pia tazama tangulizi za Isaya,Hosea na Amosi. Viongozi wa dini walihubiri maneno ya kuunga mkono dhuluma na udhalimu ili wapate riziki yao hata kumlaumu nabii Mika kuhusiana na ujumbe alioutoa.2:6,11 na 3:5. Mika kama manabii wengine wa BWANA wa wakati huo alikemea hali hiyo. Ujumbe uliotolewa na Mika ni jumlisho la unabii wa manabii wote wa nyakati hizo. Mungu anataka watu wake wageuze nia na matendo yao, watende yote kwa haki, wapende kuwa na huruma na kuishi kwa unyenyekevu mbele za Mungu wao (6:8). Mika anawaonya watu kuwa wasipotubu miji yao mikuu itabomolewa na falme zao zitaangamizwa. Mika alitabiri hali mpya ya wokovu. Watu watakaobaki wataokoka na mfalme wa amani atazaliwa huko Bethlehemu Efrata ambaye atatunza kundi kufuata mapenzi ya Bwana 2:12-13; 4:1-4; 5:2, 4) na aibu yao itabadilishwa kuwa utukufu (5:1). YALIYOMO: 1.Hukumu ya Mungu dhidi ya Israeli na Yuda, Sura 1–3 2.Ahadi ya Mungu ya kuhusu utawala wa Masihi, Sura 4–5 3.Kesi mpya ya Israeli, Sura 6:1–7:7 4.Toba na matumaini, Sura 7:8-20 KITABU CHA NAHUMU Nahumu mkazi wa mji wa Elkoshi, alitoa ujumbe wa hukumu kwa mji wa Ninawi, makao makuu ya Ashuru. Kama maana ya jina, yaani faraja au mfariji lilivyo ndivyo amekuwa mtoa ujumbe wa faraja nyingi kwa watu wa Yuda. Karne ya nane Kabla ya Kristo kuzaliwa, taifa la Ashuru lilipata nguvu nyingi, lilipanua himaya yake kwa kuteka mataifa madogo ya Palestina. Yuda walitozwa ushuru na kodi kubwa. Baada ya miaka kama mia moja Ashuru lilipungua nguvu, Babeli iliinuka kijeshi na kimamlaka. Adui wa Ashuru walifurahi. Yuda alitegemea hukumu ya Mungu kutolewa kwa taifa jeuri na katili 3:19. Ujumbe wa Nahumu umewekwa kwa njia ya mashairi kwamba Mungu wa haki ataadhibu wenye ukatili na udhalimu na wote wapingao matakwa yake 1:11-15; 2:1. Wenye maisha yasiyo adili nao wataadhibiwa. Ninawi utaadhibiwa kwa kuwa umedhulumu Yuda 1:12-13 na mataifa mengine 3:1-7. Yuda itaokolewa 1:2. Unabii wa Nahumu ulitimia mwaka 612 Kabla ya Kristo Kuzaliwa, Ninawi ulipotekwa na Wababeli. YALIYOMO: 1. Mamlaka ya Mungu, Sura 1 2. Maangamizi kwa Ninawi, Sura 2 3. Dhambi ya Ninawi, Sura 3 KITABU CHA HABAKUKI Kitabu hiki kinazungumzia suala la mateso, dhambi na haki ya Mungu kama ilivyo kwa Ayubu na Zaburi ya 73. Habakuki anaanza kwa kumlalamikia Mungu kuwa Yuda hakutekeleza ujumbe aliopewa. Anauliza, hadi lini Yuda waendelee katika uovu bila kuadhibiwa. Mungu anajibu kuwa anaandaa adhabu itakayotolewa kwa kutumia Wakaldayo Wababeli.Habakuki anabisha mpango huo akisema: kama Mungu ni Mtakatifu na wa haki, na Wayahudi ni watu wake itawezekanaje Wakaldayo wenye maovu mengi kuliko Wayuda watumiwe na Mungu? Jibu la Mungu ni kuwa kila dhambi huleta hukumu. Hivyo wote watapata adhabu ya uovu wao. Habakuki ambaye maana yake ni kumbatia au mshindani mweleka haelezi maisha yake binafsi na hataji kwa uwazi mwaka alipotoa ujumbe. Ujumbe wenyewe unaelekeza kuwa ni wakati Wakaldayo Wababeli walipokuwa wakitawala Ashuru, Misri na Yuda lakini kabla ya kubomoa Yerusalemu. Ujumbe wa Habakuki ni Bwana Mungu sio Mungu wa Israeli na Yuda tu, yeye ni Mungu wa ulimwengu wote. Yuda na Kaldayo Babeli wataadhibiwa kwa kufuata maovu yao. Vile vile amtegemeaye Mungu akawa mwadilifu hana haja ya kuogopa hukumu maana Mwenye haki ataishi kwa Imani.Mungu atampa ushindi 2:4. Yaliyomo: 1. Malalamiko ya Habakuki na Jibu la Mungu, Sura 1:1—2:5 2. Uovu wa Wababeli, Sura 2:6-20 3. Sala ya Habakuki, Sura 3 KITABU CHA SEFANIA Maana ya Sefania ni Aliyefichwa na Yehova.Alikuwa wa ukoo wa Hezekia mfalme wa Yuda. Nabii Sefania alihudumu wakati wa utawala wa Mfalme Yosia. Sefania alionya kwamba siku ya Bwana ingeleta hukumu kwa Yuda pamoja na Yerusalemu, hivyo akawashauri Wayahudi kumrudia Mungu. Uvamizi wa kuteka Yuda ulikuwa unakuja kutoka kaskazini, nao ungekumba pia mataifa yaliyowazunguka. Ingawa hukumu ya Yuda imeainishwa, ahadi ya kufanywa upya ni yakini. Mataifa yatahukumiwa na kutiishwa na mfalme wa Israeli atakayetawala kutoka Sayuni. Mwandishi Sefania. Kusudi Kuwaonya watu wa Yuda waepukane na kuabudu sanamu na wamrudie Mungu wao. Mahali Yerusalemu. Tarehe Kati ya 640–621 K.k. Wahusika Wakuu Sefania, na watu wa Yuda. Wazo Kuu Sefania aliwapa watu matumaini kwamba Mungu angewarudisha watu wake nyumbani. Mambo Muhimu Hukumu juu ya Yuda na mataifa ya Wafilisti, Amoni na Moabu. Yerusalemu pia inatajwa kwa siku zijazo. Mgawanyo 1:Siku ya Bwana iliyo ya hukumu sura1 2:Uhakika wa hukumu sura 2 3:Hukumu dhidi ya Yerusalemu surs 3:1-7 4:Ahadi ya wokovu kwa watubuo surs 3:8-20 KITABU CHA AGAI Kitabu hiki kinaitwa cha Hagai, mmojawapo wa manabii wa kwanza kabisa kutoa unabii Yerusalemu baada ya Wayahudi kutoka uhamishoni Babeli. Nabii Hagai alifanya kazi na Nabii Zekaria karibu mwaka 520 Kabla ya Kristo Kuzaliwa. Maana ya jina Hagai ni Furaha. Wayahudi walipotoka uhamishoni wakiongozwa na Zerubabeli mjukuu wa mfalme Yehoyakini na kuhani mkuu Yoshua walikuwa na hamasa kidini na kisiasa. Madhabahu ilijengwa kwa muda mfupi sana na msingi wa hekalu ukawekwa. Hata hivyo, walikatishwa tamaa na watu fulani waliopinga ujenzi huo. Kwa muda wa miaka kumi na sita kazi ya ujenzi wa hekalu ilikuwa imesitishwa. Mungu alimtuma Hagai kutoa ujumbe kwa Wayahudi. Mara nne alitoa ujumbe kwa kuonya, kuhamisha na kutia moyo ujenzi wa hekalu (1:1-15; 2:1-23). Jambo kuu la ujumbe huu sio kujenga hekalu bali Mungu kuwa na umuhimu wa kwanza katika maisha yao na kwa kuwa na uhusiano mwema naye. Wayahudi walitumia visingizio vya waliowapinga, hali mbaya ya uchumi, na ugumu wa maisha kuwa udhuru wa kutotoa muhimu wa kwanza kwa Mungu na kutoendelea na ujenzi wa hekalu. Lakini wakati huo huo walijishughulisha na ujenzi wa nyumba zao, na kufanya sherehe mbalimbali. Kwa kuwa walijiweka mbele walitumia vifaa vya ujenzi vyenye thamani kubwa kujenga nyumba zao wenyewe badala ya Nyumba ya Mungu. Hagai anaonya kwa kusema kuwa hawana budi kujisahihisha kwa kuacha ubinafsi na unajisi. Uasi na unajisi huleta hukumu. Utii, kujitoa na kumtegemea Mungu huwa na baraka. Watu waliitikia kwa toba. Baada ya majuma matatu walianza kazi ya ujenzi wa hekalu. Hagai alisema kwamba kazi yao inaweka msingi wa taifa ambalo baadaye litaongozwa na Masihi. Hagai alimtia moyo Zerubabeli kuwa ni mjumbe mteule wa Mungu, na katika yeye ahadi za Mungu kwa nyumba ya Daudi zitatimizwa. YALIYOMO: 1. Agizo na utekelezaji wa kujenga upya hekalu, Sura 1:1-15 2. Utukufu wa hekalu litakalojengwa, Sura 2:1-9 3. Unajisi na ahadi za baraka, Sura 2:10-19 4. Ahadi ya Mungu kwa Zerubabeli, Sura 2:20-23 KITABU CHA ZEKARIA Katika Biblia kuna watu wapatao thelathini waitwao Zekaria. Wengi wa hao ni viongozi 2 Fal 15:8-11.14:29.makuhani 2 Nya 24:20-26 na manabii. Kati ya manabii hao, ajulikanaye sana ni Zekaria wa kitabu hiki 1-8. Maana ya jina Zekaria ni aliyekumbukwa na Bwana Zekaria mwandishi wa kitabu hiki ni wa ukoo wa makuhani Neh 12:4,16 aliishi Yerusalemu baada ya Wayahudi kutoka uhamishoni. Alianza kutoa ujumbe akiwa bado kijana 2:4 karibu miezi miwili baada ya ujumbe wa Hagai. Zekaria na Hagai walikuwa manabii wenza waliohimiza ujenzi wa hekalu la Yerusalemu Ezra 4:1-5, 24; 5:1-2; 6:14-15 tazama pia Utangulizi wa Hagai. Ujumbe wa Zekaria ni faraja kwa watu waliotoka utumwani Babeli. Vile vile anahimiza uamsho wa kiroho ili wajenge hekalu upya, na kutoa unabii wa matumaini juu ya maisha. Huyu Masihi wa Bwana ataingia Yerusalemu 9:9 atauzwa kwa fedha 11:12-13, 12:10 atakufa kama mchungaji baada ya kupigwa 13:7.atarudi tena kwenye mlima wa Mizeituni 14:4 na atatawala miaka elfu akiwa mfalme na kuhani mkuu 14:9. Yaliyomo: 1. Wito wa kumrudia Mungu, Sura 1:1-6 2. Maono manane ya Zekaria, Sura 1:7—6:8 3. Kutangazwa kwa Yoshua, Sura 6:9-15 4. Suala la kufunga, Sura 7—8 5. Hukumu na ukombozi, Sura 9—13 6. Unabii juu ya Masihi, Sura 14 KITABU CHA MALAKI Jina la kitabu hiki Malaki maana yake ni Mjumbe wangu au Aliyetumwa na Inawezekana likawa ndilo jina la unabii au kitambulisho maalumu kuwa mwandishi ni mjumbe halisi atokaye kwa Mungu (2:7; 3:1). Malaki hataji wakati wa kutoa ujumbe wake. Inaelekea ujumbe huu ulitolewa wakati fulani wa matengenezo ya Ezra na Nehemia, kwa sababu hali na matendo ambayo yanazungumzwa yafanana na ya nyakati hizo. Wayahudi waliporudi kutoka utumwani Babeli wakiongozwa na Zerubabeli na Yoshua walikuwa na hamasa ya kutengeneza upya na kutegemeza taifa lao kidini na kisiasa. Lakini muda mfupi walilegea tazama Utangulizi wa Hagai. Kizazi kilichofuata hakikuwa na uongozi wenye kuenzi kazi nzuri ya viongozi waliowatangulia. Watu wakarudi nyuma kiroho, hata wakatafsiri vibaya ahadi za Mungu. Kurudi tena nchini mwao na kujenga hekalu upya walikutafsiri kuwa ni nyenzo ya kupata enzi za Masihi. Kwa kuwa waliyojiwekea wenyewe hayakutokea wakawa na mashaka juu ya ahadi za Mungu kwao, waliacha ibada, ndoa za mseto kidini na talaka zikahalalika 2:10-12.Walipopata matatizo walilalamika kuwa Mungu hakubali ibada zao 2:13-16 waliona kuwa Mungu hawatendei haki 2:17. Malaki anaweka mambo sawa kwamba Mungu ni mwaminifu kwa agano lake na hivyo basi hawana budi kujilaumu wao wenyewe. Hii ni kwa sababu dhambi zao zimekuwa kizuizi cha upendo na baraka za Mungu. Malaki ametabiri Siku ya Bwana ambapo waovu watahukumiwa; kwa wanyenyekevu haki itatawala na wanaomcha Mungu watabarikiwa. YALIYOMO: Upendo wa Mungu kwa Israeli, Sura 1:1-5 2. Uovu wa viongozi wa taifa, Sura 1:6—2:17 3. Mjumbe wa Bwana, Sura 3 4. Siku ya Bwana, Sura 4 KiMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA BISHOP RHOBINSON S.BAIYE TEXAS MWANZA TANZANIA. +255762506232 16 / 8 / 2021 rhobinsonsaleh1@gmaili com Advertisements Advertisements

No comments:

Post a Comment

UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...