Tuesday, July 6, 2021

UONGOZI NA UTAWALA WA KANISA

 

SAUTI YA GOMBO INTERNATIONAL MINISTRIES NETWORK

                                 

         UONGOZI

               NA

UTAWALA WA KANISA.

 

UTANGULIZI

Asili yote ya Uongozi na Utawala, unatokana na Mungu mwenyewe, Mwanzo 1:26-27. Alipanga kila mwanadamu awe mtawala, ila kusudi lake liliharibiwa na dhambi, Mwanzo 3:1-10.

Dhambi ya Mwanadamu ilichelewesha Mpango wa Mungu, Kutoka 32:1-6 linganisha na Kut 19:5-6. Hivyo Mpango wa Mungu ulitimizwa kupitia kifo cha Kristo alipokuja hapa duniani 1Pet 2:5-9.

Uongozi na Utawala ni Vitu viwili tofauti ndani ya Kanisa, Makanisa mengi hayana Uongozi bali yana Utawala.

 

 

MAANA YA UONGOZI KIONGOZI

 

1) UONGOZI NI NINI?

Uongozi ni kutangulia mbele, ni kuonesha njia siyo kuswaga, ni kutenda kile ambacho unataka watu watende. Hivyo, Uongozi ni kuelekeza wengine kwa vitendo. 1Kor 11:1, Zab 23:2-3.

Uongozi ni Utumishi siyo Ubwana, bali ni kuwa kielelezo kwa kundi 1Pet 5:3  1Tim 1:16

Uongozi ni ushawishi, ni uwezo wa mtu mmoja kuwashawishi wengine waweze kufuata Uongozi wake.

Uongozi wa Kiroho unaweza kutimizwa na watu wa kiroho pekee.

Neno Uongozi linatokana na neno Kuongoza, ni ile hali ya mtu kuwatangulia wengine na kisha wengine hufuata nyuma.

 

Niccolò Machiavelli ambaye, katika kitabu chabe maarufu The Prince, aliandika kama kiongozi hawezi kuogopwa na kupendwa kwa wakati mmoja, ni afadhali aogopwe kuliko kupendwa.

Uongozi ni mamlaka au karama ya kuwaonyesha watu njia kwa vitendo.

Kipimo cha uongozi ni jinsi gani kiongozi anaweza kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.

Kiongozi bora hana muda wa kulalamika bali anatafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi au watu walio chini yake. Kiongozi wa kweli akiongea, watu husikiliza.

Uongozi ni dhanataaluma inayompa mhusika madaraka na uwezo wa kuwawezesha wale wanaongozwa naye kuunganisha nguvustadi na vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo yao. Kuongoza ni kujua lengo la wale wanaoongozwa na njia ya kufikia lengo lao.

Uongozi ni dhana, taaluma anayopewa mhusika katika kuwaongoza wale waliohitaji kusimamiwa au walioamuliwa kusimamiwa katika kufanikisha jambo fulani kwa maslahi ya wote au ya mtu mmoja mmoja.

 

AINA ZA UONGOZI

i) Kuna njia nyingi za kuainisha uongozi lakini njia ya msingi ni kuangalia jinsi kiongozi alivyoingia madarakani na utaratibu wake wa kuongoza.[1]

ii) Katika viongozi wapo

 

 Wafalme Maraisi, MawaziriWatemiMachifuWakurugenzi, Viongozi wa dini[2] n.k.

iii) Viongozi hawa wote tunaweza kuwagawa katika mafungu yafuatayo kutokana na jinsi walivyoingia madarakani na namna wanavyoongoza kama ifuatavyo:

·         i. Wale wanaopata uongozi kwa kurithi.

·         ii. Wanaopata uongozi kwa kuchaguliwa.

·         iii. Wanaojitwalia mamlaka ya kuongoza kwa nguvu.

·         iv. Wanaoteuliwa na mamlaka za juu zaidi.

iv) Kiongozi anayeingia madarakani kwa mojawapo ya njia zilizotajwa hapa juu anaweza kutumia mtindo wake wa uongozi. Ipo mitindo mbalimbali ya uongozi:

·         i. Uongozi wa kimila

·         ii. Uongozi wa kidemokrasia.

·         iii. Uongozi wa kiimla ni mtindo wa kuongoza ambao kiongozi huongoza kwa amri bila kushirikisha watu wengine katika kufanya maamuzi. Mara nyingi uongozi wa aina hii haulengi katika kukidhi maslahi ya walio wengi, bali tu ya yule anayeongoza na wale wanaomlinda.

·         iv. Uongozi wa kidemokrasia ni ule wa kushirikisha watu katika kufanya maamuzi na utekelezaji wake. Kwa kawaida viongozi wa aina hii hulenga kukidhi mahitaji ya walengwa.

Viongozi wanaochaguliwa mara nyingi huwa wanapewa muda wa kuongoza, na wale viongozi wanaojiteua hujipatia wao wenyewe muda wa kuongoza au hata hapo watakapoamua kuachia madaraka.

 

SIFA ZA KIONGOZI BORA

i.             Awe na ufahamu.

 Kiongozi ni lazima awe na ufahamu mkubwa juu ya taasisi anayoiongoza, malengo yake, mazingira na matatizo yake.

ii. Awe mwaminifu. Kila taasisi inalenga kufikia shabaha fulani. Ni wajibu wa kiongozi kuwaongoza wanataasisi ili wafikie malengo yao. Kwa hiyo kiongozi ni lazima aweze kubuni mikakati na mbinu zitakazoiwezesha taasisi anayoongoza kufikia malengo yake.

iii. Awe na maadili mema. Kiongozi ni lazima akubalike katika jamii na taasisi anayoiongoza. Ili akubalike hana budi kuzingatia maadili ya msingi ya jamii na taasisi yake. Mtu mwongo, mlevi, mvivu, asiye mwaminifu n.k. hawezi kuwa kiongozi mzuri.

iv. Amche Mungu.

v. Awe anakubalika na watu anaowaongoza.

vi. Awe anaongoza watu katika misingi bora ya uongozi bila kujali jinsiarangidini wala kabila. Awathamini watu wa makundi yote.

vii. Awe anakubali kushauriwa ua kupokea ushauri kutoka kwa wengine.

viii. Awe na uwezo wa kujifunza kutoka kwa watu wengine waliofanikiwa.

ix. Awe na mawazo ya mbele ya kuona tatizo na kuonyesha baadhi ya njia za kulitatua, pamoja na kuona fursa

 

 

Kiongozi

Kiongozi ni mtu ambaye huongoza kikundi cha watu[1]. Mara nyingi kiongozi hupewa heshima ya juu katika jamii, kikundi cha watu au katika familia ambapo huheshimiwa na watu wote katika eneo husika analolisimamia kiongozi kwa ajili ya kuwaongoza watu.

·         1Kiongozi katika jamii

·         2Kiongozi katika familia

·         3Kiongozi katika Biblia

·         4Marejeo

Kiongozi katika jamii[hariri | hariri chanzo]

Katika nchi nyingi duniani kiongozi hupatikana kwa wananchi kupiga kura ambapo watu mbalimbali wanaogombea uongozi hupigwa kura kwa ajili ya kuwa kiongozi katika jamii au kikundi cha watu hupatikana[2].

Mara nyingine kiongozi huchaguliwa kwa kuteuliwa na mtu mmoja pasipo kupigwa kura.

Pia katika jamii nyingine kiongozi hupatikana kwa kurithi, ambapo mrithi huwa kiongozi kwa kurithi uongozi kutoka kwa kiongozi aliyefariki na kuachia madaraka.

Kiongozi katika familia[hariri | hariri chanzo]

Kiongozi katika familia huwa ni mtu aliye na umri mkubwa katika familia husika, ambapo viongozi huwa ni baba na mama. Katika familia nyingi baba ndio huwa kiongozi mkubwa akifuatiwa na mama.

Pia familia huweza kuwa na kiongozi wa ukoo ambapo bibi na babu huwa viongozi wa juu katika ukoo.

Kiongozi katika Biblia[hariri | hariri chanzo]

Katika Biblia kiongozi ni mtu ambaye humwakilisha Mungu katika kuongoza watu wake hapa duniani[3]. Hivyo anapaswa kukumbuka kwamba ameshirikishwa mamlaka ya juu na kwamba atapaswa kuhukumiwa kwa namna alivyoitumia.

Yesu alisema kwa kawaida watawala hutumia mabavu na hata hivyo hupenda kuitwa wafadhili.

 

2) UTAWALA NI NINI?

Ni kule kusimamia, kumiliki, kunyenyekesha, kuamuru na kutiisha. Kwa hiyo kutawala ni kutumia Uwezo au Nguvu au daraka ulilonalo kuamuru na kutiisha.

Kupitia mambo hayo mawili Uongozi na Utawala, Matumizi yake ni sehemu mbili.

a) Ndani ya Kanisa tutumie Uongozi wa kiroho.

b) Mambo ya Kiofisi ndipo twatumia Utawala.

 

 

UKWELI HALISI.

Si vibaya mtu kutamani kuwa Kiongozi, lakini ni vibaya kutumia njia isiyo sahihi kutafuta Uongozi.

Kama mtu hana hamu ya kuwa kiongozi anakasoro katika maumbile yake. Maaana Mungu alishaweka ndani ya kila mwanadamu zile Silika 5.

1.      Silika ya kujilinda ambayo inatuonya juu ya hatari na kutuwezesha ili tujifunze wenyewe.

2.      Silika yenye nia ya kupata ambayo inatuongoza kujipatia mahitaji yatakayotusaidia.

3.      Silika ya kutaka kula, nguvu ambayo hutuongoza katika hali ya kuitosheleza njaa ya asili.

4.      Silika ya Uzazi ambayo huongoza viumbe au binadamu ili wadumishe Taifa.

5.      Silika ya kutawala au (kuongoza) ambayo humwongoza mtu au binadamu katika kujitwalia madaraka, kama vile kuitaita wengine au kutoa Amri juu ya wengine na kutaka kuwatawala.

Zaburi 8:4  Mwanzo 1:26-27

Ndani ya kila mtu mna hamu ya kuwa Kiongozi au kutawala maana kila Mwanadamu:

a)      Anapenda sifa.

b)      Anapenda cheo au Uongozi.

c)      Anapenda kuheshimika au kuheshimiwa.

d)     Anapenda kupendwa.

Kwasababu hizo hutakiwi kumkashifu Mwanadamu yoyote.

 

MAFUNDISHO YA MSINGI KUTOKA BIBLIA.

Katika Biblia Viongozi wadhihirishwa kuwa Watumishi. Musa hakuitwa “Musa kiongozi wangu” bali Mungu alimwita “Musa Mtumishi wangu”.

Hapa duniani watu wanaangalia utumishi kana kwamba ni jambo la kudharaulika, bali Yesu aliuinua Utumishi kwa nafasi ya juu kuliko vyote. Marko 10:42-43

 

MASHARTI MAKUU YA UONGOZI

Uongozi unayo Masharti makuu manne ambayo ni lazima kila kiongozi ayatimize kabla ya kuanza kazi ya Uongozi, Vinginevyo kiongozi huyo hatafaulu kuongoza.

1. Sharti la kwanza.

 

Inampasa kiongozi atayarishwe kwanza.

a) Kutayarishwa kimwili na watu.

1.      Musa alitayarishwa kielimu   Mdo 7:22

2.      Musa alitayarishwa awe Mchungaji   Kut 3:1

3.      Samwel alitayarishwa na Eli   1Samw 2:11-18

4.      Sauli alitayarishwa awe Mfalme   1Sam 9:22-27

5.      Daudi alitayarishwa awe Mchungaji   1Samw 16:11

6.      Daniel alitayarishwa kielimu   Dan 1:3-4

7.      Saul (Paulo) alitayarishwa Kielimu   Mdo 22:3, Gal 1:14

b) Kutayarishwa kiroho na Mungu (Kupakwa Mafuta)

1.      Musa alitayarishwa kwa Maono   Kut 3:2  4:1-17

2.      Sauli alitayarishwa kwa kupakwa mafuta   1Samw 10:1

3.      Daudi alitayarishwa kwa kupakwa mafuta  1Samw 16:13

4.      Elisha aliyatayarishwa kwa kupakwa mafuta  1Fal 19:15-16

5.      Daniel alitayarishwa na Mungu    Dan 1:17-21

6.      Isaya alitayarishwa na Mungu       Isaya 6:6-7

7.      Yeremia alitayarishwa na Mungu    Yer 1:9

8.      Ezekia alitayarishwa na Mungu   Ezek 3:1-4, 8

9.      Bwana Yesu alitayarishwa na Baba   Yoh. 10:36

10.  Paulo alitayarishwa na Bwana    Mdo 9:17-19

c) Kujitayarisha wewe mwenyewe.

1.      Kuvaa silaha zote za Mungu     Efeso 6:11

2.      Kujitakasa na kujitenga     2Tim 2:21

3.      Kuwa na bidii katika kusoma au kujifunza   1 Tam 4:13   2Tim 3:14-15 IITim 2:2 Math 11:29

2. Sharti la pili.

Kiongozi wa kweli hukubaliwa na Mungu pamoja na Wanadamu (watu) Rum 14:18

Mifano.

1.      Samweli alipata kibali kwa Mungu na watu pia    ISam 2:26-3:20

2.      Mfalme Sauli alipata kibali kwa Mungu na kwa watu pia    ISamw 10:24

3.      Bwana Yesu alipata kibali kwa Mungu na kwa watu pia      Luk 2:52

 

A. KUKUBALIWA NA MUNGU.

Kukubaliwa ina maana ya kuchaguliwa na Mungu.

1.      Timotheo alihimizwa ajioneshe kuwa amekubaliwa na Mungu     ITim 2:15

2.      Mfalme Sauli alichaguliwa na Mungu      ISamw 9:17

3.      Mfalme Daudi alichaguliwa na Mungu     ISamw 16:12  Mdo 13:22

4.      Bwana Yesu alikubaliwa na Baba Mungu     Math 3:16 Mdo 17:31 Isay 42:1 Ebr 3:1-6

B.KUKUBALIWA NA WATU.

1.      Nabii Samweli alikubaliwa na Israel wote    ISamw 3:20

2.      Mfalme Sauli alikubaliwa na watu wote       ISamw 10:24

3.      Mfalme Daudi alikubaliwa na Israel wote    2Samw 5:1-3

4.      Bwana Yesu alikubaliwa na watu wote awe   Mfalme Yoh 6:15  Filip 2:9-11 Mark 11:8-9 Yoh 11:47-48 Math 27:54

3.Sharti la tatu.

Imempasa kiongozi ampendeze Mungu na Wanadamu pia. Rum 14:18  Luk 2:52

A.    Kumpendeza Mungu, ni kule kufanya mapenzi yake   Yoh 6:38-40   4:34  IYoh 2:17

B.     Kuwapendeza Wanadamu :-

1.      Ni kuwa mwanana kwa watu wote   2Tim 2:24

2.      Ni kuwa na huruma kwa watu wote   Math 9:36

3.      Ni kuwapendeza watu wote        Yoh 13:1  IThes 4:9

4.Sharti la Nne

Inatakiwa watu wamwamini Mungu na pia wamwamini kiongozi, Kut 14:31

a)      Watu wamwamini Mungu     Mark 11:22  Yoh 14:1

b)      Watu wanatakiwa kumwamini kiongozi     Kut. 19:9  IKor 4:1  Yoh 7:31 Luk 12:42

 

KUSUDI LA UONGOZI         Efes 3:7-14

Mungu ameweka Uongozi ndani ya kanisa kwa kusudi moja kuu, “KUWAKAMILISHA WATAKATIFU”, Baada ya Watakatifu kukamilishwa ndani ya Kanisa kutatokea mambo 6

1.      Kazi ya huduma itatendeka.    Rum 12:4-11

2.      Mwili wa Kristo utajengwa.    IPet 2:5

3.      Kufikia Umoja wa Imani.        Rum 1:17

4.      Kufahamu sana Mwana wa Mungu    Filip 3:8-10

5.      Kuwa mtu mkamilifu      Filip 3:15

6.      Kufika kwenye cheo cha kimo cha Utimilifu wa Kristo      Ef 1:22

JINSI YA KUWAKAMILISHA WATAKATIFU YAMPASAYO KIONGOZI.

1.      Kiongozi mwenyewe awe ameongoka   Luk 22:31-32

2.      Kiongozi lazima awe mkamilifu     Filp 3:15

3.      Kiongozi sharti awe kielelezo   ITim 4:11-16

4.      Kiongozi lazima awe amefuatwa na kundi     1Kor 11:1  4:6  Filp 3:17

5.      Kiongozi anapaswa kulilisha kundi    Mdo 20:20   ITim 3:2   5:17

6.      Kulionya kundi

a)      Kwa machozi    Mdo 20:31

b)      Kwa Uvumilivu wote na mafundisho   2Tim 4:2

c)      Kwa hekima yote    Kol 1:28

d)     Kwa roho ya upole    Gal 6:1

7.      Kuchunga na kutunza na kusimamia     IThes 2:6-8 IPet 5:1-4

8.      Kulihurumia kundi kwa namna mbili.

a)      Huruma kiroho – Math 9:36  Yuda 1:22-23

b)      Huruma Kimwili-Math 14:14-21 Mark 6:30-32

 

MATOKEO

 

1. KAZI YA HUDUMA ITATENDEKA

Kazi ya huduma ikitendeka italeta mfungamano wa kazi za Utumishi katika Kanisa Efes 4:1-6

a)      Kutatokea maelewano ya Watumishi na Viongozi   Gal 2:7-10   2Pet 3:15  Rum 12:16

b)      Kutakuwepo maelewano katika Utendaji wa kazi kimadaraka (kati ya zile huduma tano za kanisa)   Mdo 13:1  Filip 1:1  IIKor 11:28

c)      Maelewano yatakuwepo kati ya Wahudumu na kanisa.  IPet 4:8-11 Filip 2:1-4

d)     Kutakuwepo maelewano ya Utendaji wa Karama za Roho Mtakatifu kanisani  IKor 14:14-32, 37-39

2. MWILI WA KRISTO UTAJENGWA

Mwili wa Kristo ambao ni Kanisa kwa ujumla kutakuwa na mfungamano wa utendaji kazi ndani ya kanisa kwa pamoja Viongozi na Waamini.

Mwili wa Kristo hujengwa na:-

a)      Jiwe kuu la Msingi ambalo ni Bwana Yesu    IKor 3:10

b)      Mawe ya kuujenga Msingi ni Mitume na Manabii    Efeso 2:20-22

c)      Mawe ya kujengea jengo lote ni Waamini    IPet 2:5

d)     Wajenzi ni Watumishi na Waamini   Efes 4:16

e)      Namna ya kujenga, tunajenga kwa Upendo   Efes 4:16

 

3. KUFIKIA UMOJA WA IMANI.

Katika Warumi 1:17 inaelezea aina mbili za Imani zilizo kuu. Pamoja na hizo kuna aina zingine:-

1.      Imani ya Karama, hii ni kwa ajili ya Uwezo     IKor 12:9

2.      Imani ya Tunda la Roho     Gal 5:22

3.      Imani ya kuokoka   Rum 10:9  Efes 2:6

4.      Imani ya kuponywa    Mdo 14:8-10

5.      Imani ya kutenda    Amuz 14:5-6   ISamw 17:34

6.      Imani ya kutendewa   Dan 6:21-24  Ebr 11:30  Mdo 12:5-11  16:23-34

 

4. KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU

Inatupasa tufike mahali pa kumtambua Yesu Kristo jinsi inavyopasa.

a)      Tujue Uungu wake     Isaya 9:6  Math 16:16   IYoh 5:9-12

b)      Tujue Ubinadamu wake    Gal 4:4-5

c)      Tujue uwezo wa kufufuka kwake    Filip 3:14

d)     Tujue wema wake      Tito 3:4

 

5. KUWA MTU MKAMILIFU

Hatuwezi kuwa wakamilifu kwa nguvu zetu, bali tunakuwa wakamilifu kwa utoshelevu au kutoshelezwa na Kristo mwenyewe   2Kor 3:4-6

Tunapewa Ushindi wa Kristo  IKor 15:57. Bila yeye Yesu Kristo sisi ni wakamilifu  Filip 3:15 lakini bado tunaendelea mbele ili tufikie Ukamilifu halisi. Filip 3:12.

 

6. KUFIKA KWENYE CHEO CHA KIMO CHA UTIMILIFU WA KRISTO.

Hatua hii ndicho kilele cha mwisho kabisa katika kazi ya kuwakamilisha watakatifu Efes 5:25-27

Katika kilele hicho ndipo mahali ambapo Kristo anapotaka kuja kulichukua kanisa la Mungu na Hekima ya Mungu ni Kanisa la Kristo   Efeso 1:22-23

Kanisa hufikia hatua hiyo baada ya kupitia zile hatua kwa kupitia Mateso, Matengenezo, Kuthibitishwa na Kutiwa Nguvu  IPet 5:10. Tunalindwa ili tusijikwae. Yuda 1:24  IYoh 5:18-21  3:2-3

 

NGUZO ZA UONGOZI

Uongozi wa kiroho una nguzo 4 muhimu. Nguzo hizo ni:-

Mamlaka, Uwezo, Utendaji na Wajibu.

MAELEZO YA HAYA MAMBO MANNE.

 

1. MAMLAKA. Math 28:18  Luka 9:1 (AUTHORITY)

Kuwa na mamlaka ni kule kuwa na haki ya kutoa Amri au haki ya kutumia Uwezo.

Pasipo mamlaka hakuna haki ya kutumia Uwezo na pia pasipo Uwezo mamlaka hayana faida. Mdo 19:13-16

Katika Ukristo tumepokea mamlaka, mamlaka ni Urithi tunaoupata katika kumwamini Yesu kristo. Uwezo wetu ni Roho Mtakatifu.

 

2. UWEZO  (POWER) Mdo 1:8  EBR 1:3

Uwezo wa kanisa na viongozi wa kanisa ni Roho mtakatifu. Huu ni uwezo wa kuendesha Utawala wa kanisa. Ikiwa Kiongozi wa kanisa hana huu Uwezo, atatumia udikiteta IKor 2:1   Filp 4:3

Uwezo wetu ni kule kusema Neno tu. Luk 7:7 tunayo haki kisheria ya kutenda au Uwezo wa kutenda au kutoa nguvu.

Mf. Nguvu ya Serikali huwezeshwa na Jeshi, Mahakama na Magereza.

Mamlaka bila Uwezo ni Bunduki isiyo na Risasi

Efes 1:19  3:7,20  Ikor 2:1-4

Uwezo wetu siyo katika maneno.

 

3. UTENDAJI = ETFECTUAL WORKING (OPERATIONS)  

IKor 2:6

Utendaji ni nguvu za utekelezaji, Utendaji ni uwezo wa kuamuru ni uwezo wa utekelezaji, ni kuweka Imani katika Vitendo kwa kusema na kutenda.

Katika utendaji kiongozi anahitaji mambo manne:-

1.      Kupanga   IKor 14:40  IThes 5:14

2.      Kuandaa    Luk 14:28-32

3.      Kuelekeza   Mark 11:1-10

4.      Ufuatiliaji   Mdo 20:28

Utendaji ni kule kuwa na Uwezo wa kuamuru na kutekeleza.

Mifano hai katika maandiko.

a)      Mtume Petro aliamuru kiwete asimame   Mdo 3:6

b)      Mtume Petro aliamuru watu wa nyumbani mwa Kornelio wabatizwe     Mdo 10:48

c)      Towashi aliamuru gari lisimame  8:38

d)     Mtume Paulo aliamuru kiwete asimame  Mdo 14:10

Katika utekelezaji kuna mambo mawili muhimu.

1.      KUAMURU

Kuamuru ni kutoa Amri ya kutaka utekelezaji ufanyike   Dan 9:23   10:12  Luk 10:19

Tumepewa Amri ya kuamuru, kazi yetu ni kuamuru.

2.      UTEKELEZAJI

Utekelezaji ni kutimiza kile kinachotakiwa kutendwa   Filip 2:13

Kazi yetu ni kuamuru na kazi ya Mungu ni kutekeleza. Mungu anataka sisi tuwe na ile hali ya kutaka na Mungu atekeleze   IKor 3:9  Filip 2:13

Sisi tutake, tuwe na nia ya kufanya ili Mungu atekeleze, kazi kuu ya kanisa ni kuamuru na Mungu ni kutekeleza. Mungu anataka sisi tuwe na hali ya kutaka na kutenda.

Mara nyingi tunakosa vitu kwasababu hatujui kuviamuru vitujie. Baraka zote ziko katika ulimwengu wa kiroho, ni juu yetu kuziamuru zije katika ulimwengu wa kimwili. Efeso 1:3 Mark 11:23

 

SABABU ZINAZOFANYA AU KUZUIA UTEKELEZAJI USIFANYIKE.

1.      Kama jambo hilo liko nje ya makusudi ya Mungu halitatekelezwa.  IYoh 5:14 Filip 2:13  Mfano ni Balaamu.

2.      Ikiwa ni jambo liko nje ya mapenzi ya Mungu  IYoh 5:14  Mdo 21:14

3.      Shetani anaweza pia kuchelewesha utekelezaji.

 

4. WAJIBU (RESPONSIBILITY)

Wajibu unaambatana na utaratibu wa shughuli za muhimu za kila siku, kila wiki, kila mwezi na kila mwaka.

Daraka ni kile kitendo utakachofanya kufuatana na daraka lako. Na katika kufanya haya lazima uwe na ramani ya kazi (Action plan).

 

Mfano huu

TAREHE

SIKU

SAA

SHUGHULI

16/04/2017

Jumapili

Saa 4-8:00

Ibada ya Pasaka

01/05/2017

Jumatatu

Saa 8 Mchana

Kukutana na Vijana

 

Pia ni vema kuwepo na mchanganuo wa madaraka na utendaji wa kazi (Scheme  of Work), maana Mungu wetu ni Mungu wa Utaratibu   IKor 14:40   Kol 2:5

 

Mtume Paulo alifanya kazi kwa utaratibu, Ona Rum 15:24-29  IKor 16:5-12   IKor 14:40. Safari za Injili zina mifumo miwili.

1.      Kutumwa na Roho Mtakatifu.

2.      Kuazimia Rohoni.

Mtu anayeweza kutimiza wajibu ni Yule aliye na Mzigo mzito moyoni. Mdo 20:22   5:29   15:36  IIKor 11:28

 

WITO WA MUNGU KATIKA UONGOZI

Mambo manne ambayo hutokea kuhusu Wito wa Mungu.

WITO,  JIBU,  UJUMBE,  UTUMWE

Mfano ni kutoka kwa wito wa Musa, Ni jinsi gani huita? Mungu hatuiti tunapookoka au baada ya kuokoka bali hutuita kabla ya kuzaliwa. Musa aliitwa, aliitika, akapewa ujumbe, Nenda Misri kuokoa Wana wa Israel. Musa aliumwa ili aende Misri.

Wito wa Mungu kwa watu wake kuwa viongozi siyo jambo la kuchukulia juu juu bali ni kitu cha nafasi ya kipekee katika maisha.

 

VIONGOZI LAZIMA WAANDALIWE.

Paulo alimwandaa Timotheo

Musa alimwandaa Yoshua.

Timotheo aliandaa Wazee kule efeso

Tito aliwaandaa Wazee kwa kanisa la Crete

Barnaba alimwandaa John Marko

Eliya alimwandaa Elisha.

Wewe kama kiongozi uliopo sehemu mwandae mtu kwa ajili ya huduma, mwinue kiongozi kabla ya kwenda kwenye huduma.

Kuza mtu kwa ajili ya Kesho.

 

MIIKO SABA YA VIONGOZI.

Kuna mambo ambayo ni mwiko kwa kiongozi yeyote kufanya na kama atafanya ni lazima asababishe migogoro na matatizo na kuharibu nidhamu kazini.

1. Kiongozi kamwe asiwe na upendeleo.

a)      Asipendelee matajiri   Yak 2:1-4

b)      Asipendelee ndugu zake  Mdo 15:36-40

c)      Asipendelee kabila lake   Mdo 6:1

2. Kiongozi kamwe asisikilize Majungu au Matetano

ITim 5:13  TITO 3:10  Mith 29:12

Kila kiongozi anatakiwa atambue kuna makundi ya aina tatu kwa wale wanaoongozwa

1.      Waliombelembele

2.      Waliokatikati

3.      Walionyuma.

3. Kiongozi kamwe asiwe na Majivuno  Yer 9:23-25   IIKor 10:12-18

a)      Kunia makuu

b)      Kushughulishwa na manyonge

c)      Kutojivunia akili.

4. Kiongozi asiwe na tabia ya Upelelezi na kufuatilia mambo madogo madogo Gal 2:4 Kol 3:13 Ef 4:32

5. Kiongozi asiwe Mgomvi  2Tim 2:24  Tito 3:2

6. Kiongozi asiwe Mnafiki  ITim 1:5  Math 23:27

7. Kiongozi asiwe kigeugeu  Yak 1:17   2Kor 1:11  Math 5:37   Mith 24:21

 

 

TABIA TATU KUU ZA KIONGOZI

1. Kuwa na Sifa ya Tabia ihusuyo mambo ya kijamii (Social Qualification)

a)      Kuwapenda watu wote

Aina 4 za Upendo

1.      Upendo wa Ndugu   Ebr 13:1   2Pet 1:7

2.      Upendo wa kumiminwa (AGAPE)  Rum 5:5

3.      Upendo wa kuambatanishwa   ISamw 18:1 Mith 18:24 Mw 44:30

4.      Upendo wa Tamaa ambao umekatazwa kanisani  2Samw 16:1-22 Phileo

b)      Kuwatembelea watu wote     Mdo 20:20

c)      Kusikiliza kwa makini matatizo ya watu.

d)     Kuwafurahia kundi lako.

e)      Kuwa na upole na utulivu mbele ya kundi.

f)       Kuwa na unyenyekevu mbele ya kundi.

 

2. KUWA NA SIFA YA AKILI (MENTAL QUALIFICATION)

a)      Uwe na Busara na akili nyingi   Math 10:16

b)      Uwe na Hekima na maarifa    Yak 3:7

c)      Uwe na ujuzi wa Neno la Mungu     KOL 3:16

d)     Uwe na Hekima ya kuamua mambo   IKor 4:5

 

3. KUWA NA SIFA YA TABIA YA UPEVU

a)      Uwe na uvumilivu kwa kila jambo

b)      Uwe mstahimilivu wa kulaumiwa

c)      Uwe mjasiri kwa kila jambo

d)     Uwe na uwezo mkubwa wa kutunza siri.

 

KIONGOZI NA MAJARIBU

1. AINA TATU ZA MAJARIBU KWA KIONGOZI

a)      Kujaribiwa na Mungu (To prove)  Yak 1:12

b)      Kujaribiwa na Shetani (To tempt)  Math 4:1

c)      Kujaribiwa na Kanisa   ITim 3:10

2. WAPINZANI WA KILA KIONGOZI

a)      Ndugu zake  Hes 12:1  Math 10:21,34

b)      Watumishi wenzake  2Kor 11:25  Gal 2:4-9

c)      Washiriki   Yoh 6:66, 70

 

3. MAADUI WA VIONGOZI

 

A. MAADUI WA NDANI   Yak 4:1

1.      Kiburi, Sifa, Utukufu  Yer 45:5  Zab 12:3  Rum 12:3  Mith 13:10  16:15

2.      Wivu  Mw 4:5   Hes 11:28

3.      Kuvunjika Moyo

B. MAADUI WA NJE

1.      Shetani   Math 13:27-28  IPet 3:8

2.      Dunia     IYoh 2:15

3.      Fedha     ITim 3:3

4.      Ugumu wa Mambo  Math 19:25

 

HATARI ZA KIPEKEE KWA KIONGOZI

1.      Hatari kuu  IKor 9:27  Math 7:21  IKor 13:5

2.      Kujaribu kujiweka kimbele mbele  Rum 12:10  Filip 2:3

3.      Kutokutaka kusahihishwa  Yak 3:17

4.      Kutokuwa na Siri  Ikor 4:1

5.      Kupendwa sana  Mdo 14:11-15  28:6

6.      Kujiamini kuwa hauwezi kukosea   Mhub 7:15 Mith 16:2

7.      Kutoaminika   Ikor 4:12

8.      Kujiona au kung’ang’ania Madaraka   Filip 2:3

9.      Kujisifu   2Kor 10:12   ITim 3:6

10.  Kupenda Sifa   Mdo 12:21-23  Luk 18:9-14

 

SIRI YA MAFANIKIO YA KIONGOZI.

 

1. TAMBUA WALE ULIO NAO KANISANI

Ndani ya Kanisa mna aina tatu za watu

a)      Kuna watu ambao hawajui yale yanayotokea

Those who do not know what is happening.

b)      Kuna watu ambao ni watazamaji wa yale yanayotukia.

Those who watch happen

c)      Kuna watu ambao wao husababisha mambo yatokee

Those who make things happen

 

2. KAA PALE MUNGU ALIPOKUITIA

Siri ya kufanikiwa kwa kila kiongozi ni kukaa pale Mungu alipokuitia, pana fedha au hapana fedha. Wewe angalia pale Mungu amekuridhia ukae. Mungu atakuinua mahali popote.

 

3. WEKA WAZI MAONO YAKO NDANI YA KUNDI.

Unapoweka wazi maono yako utafahamu aina ya makundi uliyonayo Kanisani.

a)      Ndani ya Kanisa mna wabeba Maono (Vision carriers).

b)      Ndani ya kanisa mna Wauaji wa Maono (Vision killers) kazi yao kila unapotoka wao hupanda Magugu, hubaki kwa kutengeneza kata. Huu ni mfano wa wacheza Mpira.

c)      Ndani ya kundi pia kuna Wainuaji wa Maono (Promoters). Ingawa hawa ni wachache sana katika Makundi, lakini ni muhimu sana.

 

SIFA ZA WAINUA MAONO VIONGOZI

1. Huongoza kwa kanuni  Zab 119:4,  168

2. Huongoza kwa kumaanisha  kile wanachosema.

Siyo kila mara kusema jamani Samahanini, Manisha unachosema na kutunza muda ulivyosema.

3. Huongoza kwa kufanyia mazoezi Math 23:1-3

Kinachoua Maono ni Unafiki.

4. Maisha yako yawe mfano au picha ya kuangaliwa. IITim 3:10  Filip 3:17

 

GHARAMA ZA UONGOZI (KIONGOZI)

Uongozi unazo gharama zake ambazo yeyote anayeingia katika Uongozi lazima azikabili. Kukubali kuingia katika Uongozi umekubali kuingia katika mateso na matatizo mengi kwa hiyo tunahitaji uvumilivu na kuchuliana.

Gharama zenyewe ni hizi:

1. Kujikana mwenyewe, au kutoa nafsi iwe fidia ya wengine Mark 10:44-45. Ni kuhukumiwa kifo IKor 4:9

 

2. Upweke

Kiongozi kwa vyovyote ni mtu wa upweke. Kuna vipindi viwili katika maisha ya kiongozi

a)      Kipindi cha kupendwa  Yoh 2:23

b)      Kipindi cha kuchukiwa na watu  Yoh 6:66

Bwana Yesu alipendwa, lakini kuna kipindi walimwacha wakati wa kifo chake.

Mtume Paulo aliachwa na wenzake   IITim 1:15

IITim 4:10  Mdo 15:36-40

Wakati tunapobaki peke yetu ndipo tunapoimarika.

 

3. Uchovu

Upo wakati ambao kiongozi atachoka, hata Bwana Yesu alichoka Yoh 4:6. Tunaposikia Uchovu ndipo tunakuwa na nguvu za kiroho   2Kor 12:9-10    4:16

Tunapokuwa Wadhaifu ndipo Uweza wa Mungu wakamilika.

 

4. Malaumu

Hakuna kiongozi aliyesamehewa kulaumiwa na unyenyekevu wake utaonekana wakati wa kipindi hiki cha kulaumiwa kuliko sehemu nyingine yoyote    2Kor 6:8

Lakini ifahamike kuwa kuna utofauti ya lawama na kashifa. Mungu kamwe hatavumilia kuona watu wake wakikashifiwa na shetani au watu.

1.      Musa alipokashifiwa Mungu aliingilia kati   Hesabu 12:1

2.      Yoshua alipokashifiwa na Shetani, Mungu aliingilia kati.   Zekaria 3:1 Rum 14:4

 

5. KUKATALIWA

Kiongozi anaweza kukataliwa kabisa na kundi na kudharauliwa   Isaya 53:3

Ni bora kukataliwa na watu kuliko kukataliwa na Mungu.

 

6. SHIDA NA FADHAA

Watu wengi hudhani kuwa kutembea na Mungu muda mrefu au miaka mingi huwafanya wapate Ushindi nyakati za fadhaa na shida.

Lakini sivyo, Mungu humwangalia kiongozi kama mtu aliyekomaa na hivyo humwachia uamuzi wa kiroho kama vile Ayubu.

Mungu wakati kama huu hutuachilia tujisimamie sisi wenyewe. Soma mifano hai, Mtume Paulo Mdo 20:22 na Yohana Mbatizaji   Luk 7:19

 

7. GHARAMA KWA WENGINE

Uwe na Mzigo kwa watu wengine Mdo 19:29  16:19   20:4  Kol 4:10. Tuwe kama Musa Ebr 11:24-25

 

HATUA TANO ANAZOPITIA KIONGOZI WA KIROHO 1PET 5:10

Uongozi wa kiroho unazo hatua zake muhimu unapoajiliwa Serikalini kuna hatua unazopitia, ambazo ni:-

1.      Kufanyiwa majaribio/mtihani au kazi kwa muda

2.      Kuajiliwa

3.      Kuchunguzwa

4.      Kuthibitishwa

Ndani ya Kanisa pia Bwana anazo hatua zake

Wito,  Mateso,  Matengenezo,  Kuthibitishwa na kutiwa nguvu.

 

I. WITO WA MUNGU KATIKA UONGOZI

Mungu hatuiti baada ya kuokoka bali alituita kabla ya kuzaliwa Rum 11:29 

Unapoitwa lazima utoe jibu kisha aliyekuita atakupa Ujumbe na kisha atakutuma.

Mfano ni Musa.

a)      Aliitwa – Musa

b)      Aliitika – Niko hapa

c)      Nenda Misri – Alipewa Ujumbe.

d)     Alitumwa.

Walioitwa:

1.      Wanamfahamu Mungu wao   Ef 4:4-6 Wafil 1:12  Dan 11:32

2.      Wanafahamu mkono wa Mungu uko juu yao   Rum 8:28 Ithes 5:23-24

3.      Wale ambao amewaita Mungu hawakati tama  Rum 11:29

Mungu atakutumia kama ulivyo, usiombe akutumie kama mtu mwingine tumika kwa kile Mungu alichokupa.

4.      Hujiangalia kama Mungu alivyowaita   Rum 9:20-21  ISam 16:7

5.      Kila kiongozi aliyeitwa Mungu humwangalia kupitia Yesu Kristo.  Kol 3:3 Efes 2:6

6.      Wanyo asili au Mwanzo wao ndani ya Mungu vile alivyokuwa Yesu Kristo. Yoh 4:34

 

II. MATESO       IIKOR 1:5-7

Kila kiongozi aliyeingia katika huduma anapitia eneo hili. Huu ni Ubatizo mojawapo kati ya zile nne.

1.      Kubatizwa katika Mwili wa Kristo  IKor 12:13

2.      Ubatizo wa maji mengi  Mark 16:16

3.      Ubatizo wa Roho Mtakatifu    Mdo 1:5,8

4.      Ubatizo wa Mateso  Mark 10:38-39    2Kor 1:5-7

Kila mwamini au kiongozi sharti apitie Ubatizo huu  2Kor 4:8-10, 17 Kumb 8:2-3 Mdo 14:22

III.KUTENGENEZWA – MATENGENEZO

Mungu aliyetuumba anajua siri ya maisha yetu. Mtu anapookoka hawi mkamilifu mara moja, lakini yeye ni chombo cha Mungu chenye heshima.

Katika maisha ya waamini kuna tabia zinazomng’ang’ania na kumsumbua baadhi yake ni kiburi, majivuno, kujiona, uzinzi, dhambi zote za Siri katika maisha ya kiongozi Mungu anazishughulikia kwa kumpitisha mhusika kwenye matengenezo. Isaya 4:4  Yoel 3:21

Ukisoma Zab 51:3-4, 8,12 tunaona Mungu hutakasa damu kwa Mapatilizo  Waeb 12:5-6  IISamw 7:14   12:4   IKor 11:30-32

Tunayo mifano katika maandiko ya watu wa Mungu walioshughulikiwa – Daudi, Yakobo, Paul na wengine wengi hadi wakati wetu.

 

IV.KUTHIBITISHWA     GAL 4:19

Katika mapitio hayo ya matengenezo Kristo hufanya hali mpya katika maisha ya mtu huyo.

Hali hii inamfanya na kumthibitishia mwamini, kiongozi ukaaji mpya na dalili maishani mwake. Mawazo yake na nia yake anazama kiroho, anautafuta uso wa Mungu, ujazo wa Roho Mtakatifu.

Hali hii inampeleka kwenye hatua ya tano.

 

V.KUTIWA NGUVU.

Mtumishi anatiwa nguvu baada ya kuonekana ni mwaminifu Mdo 1:8  Filip 4:13  Kol 1:29 Efes 3:20

Hali mpya huja Ay 4:12-13  IFal 19:12-13

Nguvu za Roho Mt. humtawala mhusika masikio, Macho, Fahamu na kila eneo.

 

UHUSIANO WA KIONGOZI NA KUNDI

Katika uhusiano na uwiano wa kiongozi na kundi, kiongozi anayo madaraka pamoja na Wajibu kwa wale anaowaongoza. Ni makosa kwa kiongozi kufikiria kuwa yeye anayo madaraka tu bila wajibu kwa kundi. Madaraka na Wajibu vinaenda sambamba katika uongozi, kwasababu hakuna Uongozi bila Wajibu.

 

1. MADARAKA YA KIONGOZI.

a)      Kuonya kundi    2Tim 4:2

b)      Kukemea kundi   ITim 5:5-20

c)      Kukaripia kundi  2Tim 4:2

d)     Kuadhibu kundi kwa Upendo  IKor 5:13

e)      Kutawala na kusimamia  ITim 5:17  IPet 5:2

 

2. WAJIBU WA KIONGOZI

a)      Kulisha kundi (Kanisa)   Mdo 20:28

b)      Kuhurumia kundi     Yoh 6:5-13

c)      Kutunza kundi   Mdo 20:28

d)     Kufundisha kundi   ITim 5:17

e)      Kuonya kundi kwa machozi   Mdo 20:31  Filp 3:18

f)       Kulichunga kundi    IPet 5:2

3. WAJIBU WA KUNDI KWA KIONGOZI WAO.

a)      Kumheshimu kiongozi wao  ITim 5:17  Wafil 2:29

b)      Kumlisha kiongozi   IKor 9:7-14

c)      Kumtii kiongozi wao  Ebr 13:17 IKor 16:17

d)     Kumsitahi kiongozi wao  ITim 5:12

e)      Kumtambua kiongozi wao  ITim 5:12

f)       Kumnyenyekea kiongozi wao  Ebr 13:17  Ikor 16:17

g)      Kutokukemea kiongozi wao  ITim 5:1

h)      Kutomdharau kiongozi wao   IKor 16:11

 

4. KIONGOZI NA MAZINGIRA

a)      Kiongozi na wakati Efes 5:15-16 Mh 3:1-7 Mwanadamu hajali wakati lakini Mungu anajali wakati.

b)      Kiongozi na maombi (Prayers)  Dan 6:10

c)      Kiongozi na kusoma (Studying)  ITim 4:13

d)     Kiongozi na Siasa - (Politics) ujiepushe.

e)      Kiongozi na Utawala (Government)  Rum 13:1

f)       Kiongozi na Elimu (Education) ujifunze  IITim 3:14-16 Mdo 18:25-26

g)      Kiongozi na maendeleo naya jamii (Social Development) Uwe na Elimu juu ya jambo hili.

 

SEHEMU YA PILI YA MAFUNZO

 

UTAWALA WA KANISA EFESO 3:9-10  IKOR 12:28

 

AINA NNE ZA UTAWALA WA KANISA

 

1. UTAWALA WA MAASKOFU – EPISCOPAL ITim 3:1

Huu ni utawala wa kanisa unaoamuliwa na Maaskofu, Makasisi na Mashemasi.

Filip 1:1  Rum 15:16  ITim 3:1,8  Ufun 1:6. 5:10  Mdo 6:3

Kupitia Yesu Kristo Waamini wote ni Makuhani IPet 2:5

Kuna aina mbili za Makuhani (Watumishi)

a)      Makuhani wa watu.

b)      Makuhani wa kumhudumia Mungu  Ezek 44:10-16

Viongozi wa Kanisa wamegawanyika katika sehemu mbili kuu

1.      Vipawa vya Mungu kwa kanisa  Ef.4:8-11

Vipawa vya Mungu ni wale waliochaguliwa na Mungu mwenyewe.

2.      Mashemasi – ni Watumishi wanaochaguliwa na kanisa ili wamtumikie Mungu  Mdo 6:3

Katika utawala huu kuna aina tatu au madaraja matatu

1.      Maaskofu  ITim 3:1  Filip 1:1

2.      Makasisi   Rum 15:16 Ufun 1:6  

3.      Mashemasi ITim 3:8 Filip 1:1 Mdo  6:3

 

2. UTAWALA WA PAPA (PAPAL) BABA

Katika utawala huu ni kutokea kwa Papa, kanisa linatawaliwa na Makadirinari, Maaskofu wakuu, Maaskofu, Mapadri. Hawa Maaskofu wakuu ni wale wote kuanzia lile Baraza la Rumi hadi chini.

Katika utawala wa kipapa mshiriki wa kanisa au kanisa la mahali hawana haki yoyote ya utawala.

a)      Wanaamini Papa hawezi kukosea hata jambo moja anapofanya maamuzi ya kikanisa.

b)      Papa ni mwakilishi wa Mungu duniani.

c)      Ni Makamu wa Yesu, ana uwezo wa kumfikisha mtu mbinguni au kutomfikisha Mbinguni.

d)     Anaweza kufanya yale Mungu anayafanya hapa Duniani.

 

3. UTAWALA WA KANISA MOJA MOJA (INDEPENDENT)

Huu ni namna ya Utawala wa kanisa unaokubaliana kuwa mamlaka ya kanisa yamo mikononi mwa Washirika peke yao.

Makanisa yenye mfumo huu yana uwezo wa kuamua mambo katika uongozi wao.

 

4. UTAWALA WA WAJUMBE (REPRESENTATIVE)

Huu ni namna ya Utawala wa kanisa unaokubaliana kwamba mamlaka yamo mikononi mwa Washiriki wa kanisa – wao hufanya baraza la kuchagua Viongozi wa kuongoza na kulisimamia kanisa. Katika utawala huu Wachungaji huwekwa mikono mara moja. Wengine huondolewa kwa kupoteza nafasi zao Huu utawala hapa duniani karibu wote wanao Uongozi una aina mbili kuu.

 

1.      COLLECTIVE LEADERSHIP – UONGOZI WA PAMOJA

2.      UNITARIAN LEADERSHIP   – UONGOZI WA MMOJA MMOJA

Hizi ni aina 4 za tawala zote zinafanya huduma katika dunia yetu ndani ya kanisa la Kikristo. Ingawa zingine zimeleta shida katika kuongoza Waamini kufikia lengo la Mungu lililokusudiwa. Mungu alisaidie kanisa lake kufuata aina nzuri ya Uongozi ili kufikia kwenye lengo kuu alilolikusudia Mungu.

 

Kimeandaliwa nakuandikwa na Bishop

Rhobinson S.Baiye

Mkolani Mwanza Tanzania

30/3/2021

rhobinsonsaleh1@gmail.com

 

KunihusuKK

 

No comments:

Post a Comment

UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...