Friday, August 27, 2021

UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana ya Uongozi. 2.Maana ya Kiongozi. 3.Tofauti ya kiongozi wa Kiroho na wa Ki - dunia. 4.Umuhimu wa Uongozi/Kiongozi. 5.Sura ya Uongozi/Kiongozi wa kiroho. 6.Maadili ya Kiongozi wa Kiroho. 7.Changamoto za Kiongozi/Uongozi. 8.Mafao (Thawabu), Gharama na Anasa za Uongozi. 9.Siri ya mafanikio ya Uongozi wa Kiroho. 10.Kiongozi mwenye maono na malengo na mipango. 11.Aina mbili ya Kiongozi. 12.Kiongozi anayefaa kuigwa na watu. 13.Misingi ya Kiongozi/Uongozi wa Kiroho. 14.Lugha ya Kiongozi. 15.Sifa za jumla za Kiongozi wa Kiroho. 16.Wajibu wa jumla wa Kiongozi wa Kiroho. 01. UTANGULIZI. Je, Kiongozi anahitajika? Nini umuhimu wakuwa na Kiongozi? Je, Unajua tofauti kati ya Uongozi na Utawala? Je, Wewe ni kiongozi au Mtawala? Popote unapoona kazi ya Mungu imesonga mbele na kufanya vizuri lazima kuna kiongozi aliyesimama kwenye nafasi yake vizuri. Imekuwa ni tabia ya Mungu mara zote kumchagua mtu ili kuyafanikisha malengo na mipango yake. Mfano: Mungu alimuandaa Ibrahimu na kumwita ili kuanzisha Taifa - Mwanzo 12: 1-2; Akamwandaa Yusufu ili kulihifadhi Taifa hilo - Mwanzo 45: 3 - 9, 50: 20 - 21. Akamwandaa Musa ili kulitoa Taifa hilo Utumwani - Kut.3:2-14. Akamwandaa Joshua kuliongoza Taifa hilo kuteka nyara, kupigana vita na kuliingiza Kanani - Yoshu 1: 1 - 9. Mungu alitumia wanaume na wanawake katika kufikia malengo yake kama vile Nabii Debora - Amuzi 4:4, Esta 7: 3 - 6 n.k. Pia Mungu aliwaongoza na kuwaelekeza waamuzi na wafalme katika kulisimamia kundi lake (watu) wa Mungu, pia aliwatumia Manabii ili kuwaonya na kuwasahihisha watu wa Mungu; Na hatimaye alimtuma mwanaye wa pekee mpendwa Yesu Kristo kuja kufa na kufufuka kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu kutoka katika utumwa wa dhambi - Yoh. 3:16, Math. 1:21. Yesu naye alipoondoka akamtuma Roho Mtakatifu ili atuongoze salama - Yoh. 14: 16,26, Rumi. 8:14 Jambo la pekee katika ufalme wa Mungu, mtu mmoja anaweza akaleta/akasababisha ushindi mkuu katika kanisa au Huduma. Hii ni ajabu Mungu anasema katika Ezek. 22:30 “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakaye tengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.” Kumbuka: Hitaji kubwa la nyakati zote tangu vizazi na vizazi, katika watu wa kada zote, jamaa, Taifa, Mataifa, Taasisi na Mashirika ya dini ni kupata viongozi wenye sifa na uwezo wa kuwaongoza wengine, pia wenye uwezo na hekima katika kuwaunganisha watu ili kuwafanya kuwa wamoja katika kutumia karama, vipawa, talanta, huduma na rasilimali walizonazo kwa manufaa ya maendeleo yao. Pia waweze kufikia na kukamilisha jambo/malengo na mipango yao waliyokusudia. Viongozi wanajua wanalopaswa kulifanya na wana uwezo wa kuwachukua watu mbele zaidi ya pale walipo sasa. MAANDIKO YA SOMO LA MSINGI* Marko.10:45, 1Petr.2:21, Yoh.10:10 - 11 02. MAANA YA UONGOZI. Uongozi ni hali/tendo la kuongoza. Ni hali ya kutangulia mbele, kusimamia, kulinda na kuelekeza watu njia au mwelekeo wa kuuendea au kufikia malengo Fulani. 03. MAANA YA KIONGOZI: Mark.10:45, 1Tim.4;11 - 12, 1Petr.2:21. Kiongozi ni mtu Yule ajuaye njia na yale apaswayo kupita nayo na kuzingatia katika njia hiyo. Ni mtu Yule ajuaye mwelekeo wa jambo hilo au malengo hayo na anauwezo wa kuwatangulia na kuwavutia (shawishi) wengine wamfuate. Ni mtu aliyepewa dhamana (aliyeaminiwa) na Mungu kuongoza watu wengine (kuwatumikia). Mfano: Yesu - Yoh.14:6; 10:2 - 4, Paulo - 1Kor.11:1; 4:16. Ni mtumishi (mtumwa) wa wale anaowaongoza. Mfano: Musa - Kut.10:25 - 26; 13:21 - 22, Yuda - Mw.46:28 Kumbuka: Kiongozi wa Kiroho siyo mtawala (boss) bali ni mtumishi (mtumwa). Kiongozi ni kielelezo (mfano) wa kupigiwa, kufuatwa na kuigwa na wengine - Unaosimama mbele yao kuwaongoza. Hivyo maisha ya kiongozi lazima yawe kielelezo katika maeneo matano (5) yafuatayo:- Katika Usemi: Chunga (angalia) sana matumizi ya ulimi (yale uyasemayo). Yakobo 3:1 - 12. Katika Mwenendo: (Tabia) - Maisha yako ya kila siku machoni pa watu. Math.5:16, 1Petr.2:11 - 12, Fil.2:14- 16. Katika Upendo: Kujitoa, kujali, kuhudumia na kuhurumia.Yoh.3:16,Math.9:35 - 38. Katika Imani: Maisha ya kumtegemea Mungu. Ebr.10:38; 11:1,6, Hesabu.14:11, Yer.17:5 - 8, Rumi.1:17, Gal3:11. Katika Usafi: Maisha Matakatifu - yenye ushuhuda mzuri mbele za watu.Zb.16:3, Kumb.23:14, 1Kor.3:16 - 17, 1Petr.1:16. 04. TOFAUTI YA UONGOZI/KIONGOZI WA KIROHO NA WA KIDUNIA. Uongozi wa Kiroho na ule wa kidunia unaweza ukafanana katika baadhi ya mambo Fulani tu, lakini ukatofautiana sana na kwa kiasi kikubwa katika mambo ya kimsingi.Kwa mfano katika mambo yafuatayo:- i) Hitaji na namna ya kumuandaa Kiongozi. Mungu huandaa na kumweka Kiongozi. 1Sam.16:3,7 Ezek.16:1 - 5, 1Tim.3:1,15 Yer.3:15 Math.9:38. ii) Nia ya ndani ya Kiongozi. Swali la kimsingi la kujiuliza, Kwanini wewe ni Kiongozi? au kwanini unataka kuwa Kiongozi? Zipo nia mbalimbali kama vile kutaka:- mamlaka, sifa, kuheshimiwa, utukufu, kutambulika, kiburi n.k. Hizo ni nia za Kiongozi wa Kidunia* Pia mtu anaweza kuwa kiongozi kwa nia ya kutaka kuyafanya mapenzi ya Mungu. FIlipi.2:5, 13. Kumbuka: Uongozi wa kidunia unadhihirishwa katika nia binafsi katika kupata mafao yenye kumnufaisha yeye na familia yake, kupata marupurupu mazuri, heshima; bila kujali wengine kama wanaumia au la, hivyo watu wanapigania kuwa viongozi katika kutoa rushwa kwa nia ya cheo na siyo huduma itakayotolewa au utendaji. Uongozi wa Kiroho, Mungu anasema “Msitende neno lolote kwa kushindana wala majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Fip.2:3 - 4. iii) Kutaka mapenzi ya Mungu. Rum.12:2, Efe.5:17, 1Tim.3:1 Nia yake ya moyoni ndiyo itakayobainisha kama atakuwa wa Kiroho au wa Kidunia. Kumbuka: Kiongozi wa Kiroho, yeye ni kiungo au mpatanishi kati ya Mungu na watu anaowaongoza. Mfano: Musa - Kutoka.19:9; 24:3, Yesu - Yoh.8:26 - 30, Paulo - 2Kor.5:18 - 20. 05. UMUHIMU WA UONGOZI/KIONGOZI. Tumeona uongozi ni muhimu sana mbele za Mungu na kwa watu pia. Uongozi ni kipawa (zawadi) ya Mungu kwa wanadamu ili wakae katika amani, utulivu na matumaini. Bila uongozi watu hukosa mwelekeo (dira) na amani, hivyo hufikia hatua ya kufarakana, kutawanyika, kukosa mwelekeo, kila mtu kwenda au kutenda lile analoona linamfaa yeye machoni pake. Rejea baada ya Yoshua kushindwa kuandaa kiongozi, pindi alipokufa wana wa Israel walipoteza mwelekeo kabisa, kila mwamuzi aliibuka na mfumo wake kwani hakuwepo kiongozi. Kwa sababu hiyo Mungu ameweka Uongozi ili watu wapate mwelekeo, amani na matumaini katika kuyatimiza mapenzi yake duniani. Tazama Amuzi. 21:25 watu walijiendea hovyo hovyo, Zek.13:7 - Nitampiga Mchungaji.Hesabu.27:15 - 23, Efeso. 4:11 - 13. 06. UONGOZI/KIONGOZI WA KIROHO. Yapo mambo mengi ya kuangalia au yanayotakiwa kuonekana ndani ya Uongozi wa Kiroho ila haya matatu ni ya msingi sana kutupa sura ya kiongozi wa kiroho:- i)UTUMISHI: Mark. 10:45, Lk. 22:24 - 27, Math. 20:24 - 28, Yoh. 13:1 - 17 (mst 14, 17) Je, wewe ni kiongozi wa aina gani? Mimi ni Kiongozi ninayeongoza. Mimi ni Mtumishi ninayetumika. Mimi ni Kiongozi Mtumishi. Mimi ni Mtumishi Kiongozi. Mtumishi Kiongozi: Hii ni falsafsa (msemo/imani) inayowasaidia watu kuwa na dhana ya utumishi; na baadaye kuweza kuongoza kwa nia ya kuwatumikia watu, shirika, kanisa, n.k. Mtumishi kiongozi anaweza asiwe na cheo/nafasi yoyote kanisani na bado akawa tegemeo (nguzo) kwa kanisa au watu wengi na kutoka kwake watu wanaweza kupokea hazina njema. Mchungaji wangu kiongozi siku moja alisema katika fafanuzi yake ya neno mtumishi kuwa “Kipimo cha mtumishi ni kiwango cha mtumishi (mhudumu) wa Hotelini, maarufu kama waiters hata kama akitumwa vipi hakwaziki na wala hakasiriki, akaongeza akisema mtumishi kiongozi ni Yule anayetumiwa na watu wengine kwa kadri wapendavyo wao.” Neno la Mungu linaonyesha maneno ya msingi na yenye hekima katika utumishi kama ifuatavyo:- Lk. 22:26 - 27, Math. 20:26 - 28, 1Petr. 5:2 - 3. Tabia ya Mtumishi Kiongozi. Mnyenyekevu - Math. 10:24, 2Tim. 2:25, 1Petr. 5:5 - 7. Ana bidii - Si mvivu - Math. 24:45 - 47. Ana uwezo wa kufundisha - 2Tim. 2:24. Mvumilivu - 2Tim. 4:2. Mtii - Efeso. 6:5 - 6, Tito. 2:9. Anajitoa - 2Sam. 15:21. Mwangalifu - 1Sam. 22:14. Amejaa Roho Mtakatifu - Mdo. 2:16,18. Anakubali Maonyo - Mhubiri. 4:13. II) SURA YA UCHUNGAJI: Zab. 23, Yoh.10:11; 21:15 - 17, 1Petr. 5:2 - 3. Kiini cha Uchungaji: Neno Mchungaji lilitumika sawa na mchungaji wa kondoo, ng’ombe au mifugo mingine. Yer.6:3, Math. 8:33 Mchungaji hukaa na kondoo na kazi yake muhimu ni kuwa na kondoo hizo. Kumbuka: Kondoo ndiyo wanampa kazi ya kuwa mchungaji, hivyo mchungaji ni mtumishi wa kondoo (watu). Sifa ya Mchungaji: Anawajua kondoo wake kwa majina - Yoh. 10:3, 14, 27. Sawa na Haruni juu ya wana wa Israel - Kut. 28:9, 10, 12, 29. Yuko pamoja na kondoo au anapatikana na ni rahisi kuingilika Lk. 22:27. Anatangulia mbele kuwaonyesha kondoo njia, mahali pa malisho, majani na maji..Zab.23:1 - 2. Ni jasiri na yuko tayari kujitoa kwa ajili ya kondoo. Yoh. 10: 10 - 13. Anawaongoza na kuwaelekeza kwa upole kwa fimbo ya kichungaji. Zab.23:4, Ufu. 21:15. Ili kutimiza wajibu wake kwa kondoo (washirika/kanisa): Kiongozi wa sura ya mchungaji anapaswa kujua mambo makuu matatu, nayo ni:- i) Kwamba ameitwa na Mungu - Yh. 15:16. ii) Kufahamu chanzo cha nguvu zake - Kol. 1:11, 29. Zek.4:6. iii) Kufahamu mambo aliyoitiwa kufanya, na hata jinsi ya kuyapatia vipaumbele – Yoh. 10:4. Mambo hayo humfanya mchungaji kuwa na maono, malengo na mipango mizuri katika uongozi (kazi), huduma yake. - Kol. 1:10, Efes. 4:1. Mchungaji anapaswa kuhakikisha kuwa kundi lake:- Linaongezeka kiidadi - Mdo. 2:47, 41: 6 - 7. Linakuwa kiroho - Mdo.2:42, 2Kor. 2:14, Kol. 1:10. Linamwabudu Mungu katika Roho na kweli - Yoh. 4:24, 2Kor. 4:24, 2Kor. 4:2. Linahifadhi umoja wa roho na ushirika katika mwili wa Kristo - Fil. 1:27, Efe. 4:1 - 6. Linashuhudia ulimwengu habari njema na kuwaleta watu kwa Kristo (Uinjilisti) - Mdo. 5:42; 6:7, Math. 20:18 - 20. Linapata ulinzi, usalama na amani - Mdo. 20:28 – 31 Tahadhari ya Mchungaji (kiongozi) kama kuhani wa Mungu ni kuona kuwa:- Asiwe sababisho la kundi kutawanyika katika uongozi wake. Yer.23:1 - 2, Ezek.34:2 - 5, 10. Hapotoshi mafundisho ya kweli ya Mungu; yaani hafundishi kwa nia ya kudanganya kundi kwa manufaa yake binafsi. Ezek. 22:26, 30, Tito. 2:7 - 8, Ezek. 13:1 - 7, Isa. 10:1- 3, Yer. 14:14, Isa. 30:10, Yer. 23:21 - 22, 2thes. 2:9 - 12. Anatoa malisho kwa kundi kama unavyokusudia na kwa wakati unaokubalika. Yer. 23:22, Math.24:45 - 46, 2Tim. 2:15, 2Tim.4:5. Kumbuka: Kwa kuyafanikisha haya mchungaji (kiongozi) lazima azingatie yafuatayo:- Maombi na (b).Kusoma neno la Mungu na kulitafakari kila wakati. Math. 17:20 - 21, Yoh. 15:7, Fil. 4:16, 1Thes. 5:17, Kol. 3:16, Yoh. 17:14 - 17. III. SURA YA UWAKILI. Math.25:14, 1Kor. 4:1 - 2. Wakili: Ni mtu yeyote anayepewa uwezo na mtu mwingine ili kusimamia mambo yake. Wakili: Ni mtu anyemtetea mtu mwingine mahakamani. Katika Agano jipya wakili ni mtu aliyeaminiwa na bwana wake; na hivyo alipewa mafao na mamlaka na pia alikuwa na wajibu na uwajibikaji kwa kazi yake. Lk. 12:42 - 43. Wajibu wa Wakili ulikuwa ni:- Kuangalia vipawa katika maisha ya wale anaowaongoza ili avitumie vizuri na kuzalisha. 2Tim. 1:14, 1Tim. 1:18 - 20. b) Kuhesabu rasilimali zote alizonazo, kama vile watu, fedha, vifaa na kwa neema ya Mungu kuweza kupanga na kuvitumia ipasavyo. c) Kuwa mkweli (honesty) - mwenye msimamo mwema mwadilifu (integrity) na muwazi (transparency) - Yoh. 8:12. Kuwa mwaminifu (faithful) na mwenye kupandishwa daraja kwa sababu ya uaminifu wake. - Math. 25:21, 1Kor.4:1 - 2, Math. 24:45 - 47. 07. MAADILI YA UONGOZI/KIONGOZI WA KIROHO. Maadili ni tabia njema ya mtu au mwenendo mwema (mzuri) wa mtu. Tabia - Ni mazoea ya hali Fulani au vitendo fulani. Maadili ni jambo linaloweza kutenganisha sifa za kiongozi katika mwonekano wake kati ya uongozi wa Kiroho na wale wa kidunia. Maadili yapo hasa kuonyesha msimamo katika usafi wa maisha na haki. 1Kor. 10:23, 6:12. Swali la kujiuliza; Unajisikiaje kwa yale unayoyafanya mbele za Mungu na wanadamu?. Je, ni sawa au si sawa? 1Tim. 3:2 - 12. Neno la Mungu linaeleza maadili ya msingi kwa kiongozi wa Kiroho ya kuwa anapaswa awe mtu wa:- Kutolaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, na busara, mtaratibu, mkarimu, mwenyekujua kufundisha, si mlevi, si mpiga watu, si mtu wa majadiliano, si mpenda fedha, mwenye kusimamia nyumba yake, si mchanga kiroho, mwenye ushuhuda mzuri nje, si mwenye kauli mbili, asiyetamani fedha ya aibu. Tito. 1:6 - 7. Kumbuka: Maadili yanatusaidia kuishi maisha ya mfano au kielelezo. Tazama Tito. 1:8 - 9, 2Thes.3:9, 1Tim. 4:12, 1Sam. 12: 2 - 5. Unayoyafanya yatageuza watu zaidi ya yale unayoyasema. Unavyoishi itasaidia kukazia mafundisho yako au pia kuyaondoa kabisa mioyoni mwa watu wanaokutazama. Kumbuka: Watu hujifunza zaidi kwa kuona, kisha kwa kusikia na kwa kiasi kidogo kwa yale mengineyo. Maadili bora (mema) ni uamuzi na misimamo inayoweza kumfanya mtu binafsi au jamii iweze kuishi maisha ya haki, utaratibu na usafi. Hebu tuangalie mfano wa watu (viongozi) hawa wawili:- a) Sauli: Yeye aliitwa na Mungu kuwa mfalme, alipakwa mafuta na kutumiwa na Mungu; Lakini:- 1Sam. 13:13 - 14 Alikuwa mtu wa kutenda bila kufikiri, aliweza kutoa sadaka kinyume na utaratibu wa Mungu. Alikuwa mtu wa kutumia mabavu (ubabe - nguvu), kiburi kutotii na kupenda umaarufu. 1Sam. 15:12 - 26. Na mwisho wa yote aliishia kuanguka na kukataliwa na Mungu. Tatizo lake alijiwekea maadili mabaya, ambayo hayakumpa Mungu utukufu. 1Sam. 15:10 - 11. b) Nehemia: Katika Neh. 5:14 - 19 hapa Nehemia anaonyesha msimamo wa haki, kama maadili (tabia) yake binafsi. Alikusudia kufanya yaliyo mema na ya haki Mst.14 Alijitenga na watu walio wadhalimu (waovu) Mst.15 Alijitoa na kukaza macho yake kwenye kazi ya kuujenga ukuta - Mst.16 Nehemia alikuwa na uwezo wa kuwavuta wengine (nguvu ya ushawishi). Alitoa mali zake kusaidia wengine - Mst.17 Alitanguliza maslahi ya wengine kwanza, badala ya faida yake - Mst.17 - 18. Alionyesha kuwajibika kwa Mungu akimpa utukufu - Mst.19 Nehemia. 12:40 - 43. Kukosa maadili mema kunajidhihirisha katika mambo yafuatayo:- i) Maisha ya uasi kwa kiongozi kama vile wana wa Israel: 1Kor. 10:1 - 5. Kutamani mabaya - 1Yoh. 2:15 - 17. Kuabudu sanamu na shughuli nyingi - Mark. 4:19, Kut. 20:4 - 6. Uasherati - Gal. 5:19. Mawazo potovu. Uhusiano mbaya (ugomvi) kati ya mke na mume (wanandoa). Kukosa hekima katika kushauri/kushuriana. Kumjaribu Bwana - Lk. 4:12 Manung’uniko - Hesabu. 14:26 - 27 Kiburi - Majivuno (kujiona wewe bora kuliko wengine) - Mith. 22:10. Kumbuka: Anatazamiwa kiongozi ya kuwa:- “Alivyo kwa nje na ndivyo anavyotakiwa awe kwa ndani.” “Vile anavyokuwa madhabahuni/mbele za watu anatakiwa awe pia mbele za familia yake.” ii) Maisha mabaya katika fedha: Kupenda fedha kuliko Mungu - 1Tim6:6 - 10. Kutumia vibaya fedha za kanisa - Fil. 4:11 - 12. Udanganyifu katika matumizi - Mith. 15:27, Rumi. 13:8. Kutotoa fungu la kumi (Zaka) 10% ya mapato yako - Mal. 3:8 - 9, Ebr. 7:5 - 10, Zek.5:1- 4. Uzembe wa kutolipa madeni - Zab. 37:21, Mith.22:7 Kumbuka: Hali hii inapozoeleka kwa kiongozi inasababisha hali ya kutokuaminika na kuonewa shaka. iii) Matatizo katika ndoa: Matatizo haya yanaweza kusababishwa na:- a) Unafiki: Nje kuonekana tofauti na hali halisi ya ndani. Kuvaa sura isiyo yako. Kuficha au kufanya siri shida na matatizo ya kindoa - Math. 23:27 - 28. b) Kutokutatua matatizo madogo madogo ya ndani; na hivyo huzaa matatizo makubwa - Lk. 16:10. c) Kujilinganisha na watu wengine (ndoa nyingine): 2Kor. 10:12 Mwanandoa yeyote anayejilinganisha na mtu mwingine hana akili kabisa - zezeta. Kumbuka: Tofauti zetu zinamfurahisha Mungu, siri ya ndoa bora nimsingi wake. d) Dharau/Kiburi - 2Tim. 3:1 - 4. e) Mawasiliano mabovu - Amos. 3:3 Kumbuka: Adui hatakubali na hafurahi kuona mnaishi hivyo anachofanya ni kuwachafulia mawasiliano, msimpe nafasi. Efes. 4:27 f) Kipato/Fedha kidogo: hili nalo huweza kuleta tatizo katika ndoa nyingi, hivyo kama mwanandoa jifunze kuridhika na uwezo wa mwenzi wako huku mkiweka mipango na malengo pamoja ili kuinua kiwango cha fedha na uchumi katika familia. Fil. 4:11 - 13. g) Tabia za asili za mwenzi wako - Mith 30:11 - 14. Hivyo ni vizuri wanandoa ukamjua mwenzako vizuri hasa juu ya tabia zake za asili - ndani, wakati wa uchumba huwezi kuziona tabia za ndani bali za nje. h) Viwango vya tendo la ndoa Mith. 5:15 - 19, Wimbo. 4:12 utoshelevu. Swali la kujiuliza: Je, unaujasiri wa kuhubiri mbele ya mkeo au mumeo na pia watoto wako? Kama unakosa ujasiri mbele yao basi, kunamambo yanayohitajika kupata ufumbuzi. j) Kuacha kutunza familia kwa kisingizio cha kutingwa na huduma - Lazima kuwe na uwiano, japo ni muhimu sana kumsikiliza na Roho Mtakatifu kuliko kutii wanadamu - 1Tim. 5:8, Mdo. 5:29. iv) Kuharibu huduma yako; kwa:- Kupotosha neno la Mungu, kulighushi na bila ya kutumia kwa halali neno la kweli. 2Kor. 4:1 - 2; 2:17, 2Tim. 2:15. Kuwatumia watu kwa kujinufaisha yeye binafsi badala ya kuwajenga na kuwaimarisha katika ufalme wa Mungu. *Faida ya maisha na maadili mema ya Kiroho* Ili uwe kiongozi, lazima uwe na wafuasi. Kuwa na wafuasi lazima wakuamini. Hivyo maadili bora ni ya lazima kwani yanakuwezesha wewe kiongozi katika mambo yafuatayo:- Kurithisha (influence) tabia yako kwa wale unaowaongoza. Math.26:73, 1Tim. 4:12. Kutokuwa mtu wa kubadilika kama (kinyonga/popo). Swali la kujiuliza; Je, wewe ni yeye Yule kila wakati? Je, jambo gani unafanya ambalo hutaki watu walijue? Je, hii ndiyo tabia yako? 1Tim. 3:8. Kumbuka: Tabia yako isiyobadilika inagusa mioyo ya watu - Ebr. 13:7 Dhamiria kuwa mkweli na muwazi, usitafute kuonekana mzuri, bali uwe mzuri. Yer.7:3 - 4. Tabia huweza kujengwa na kubomolewa katika mambo madogo, hivyo dhamiria kuwa mwaminifu katika yaliyo madogo na utakuwa mwaminifu dhidi ya mambo yaliyo makubwa. Unaweza ukabadili matendo yako ili yafuatane na kanuni za maadili mema au unaweza ukabadili kanuni za maadili zifuatane na matendo yako. Uchaguzi ni wako. Dhamiria kuwa na nia ya kutumika kwa unyenyekevu, watu watakufuata wakijua nia na lengo lako ni kuwatumikia. 08. CHANGAMOTO ZA UONGOZI/KIONGOZI. Hitaji kubwa la kanisa ni kupata viongozi bora wa kiroho watakaoweza kukabiliana na changamoto zilizopo nyakati hizi za mwisho katika kumwakilisha Kristo. Je, wewe ni miongoni mwao? - 1Tim.3:1 - 7. Swali: Utafanya nini wewe binafsi ili kuboresha uongozi wako? Changamoto nyingine za kiongozi ni:- Kiwango duni (cha chini) cha elimu na ufahamu sahihi wa neno la Mungu na mambo mengine - Mith. 3:13; 4:13. Maisha yasiyo na ushuhuda mzuri. Math. 5:13 - 16 Kushindwa kufikia malengo/maono. Lk. 14:28 - 32. 09. MAFAO (FAIDA) NA THAWABU, GHARAMA NA ANASA ZA UONGOZI/KIONGOZI BORA WA KIROHO. Uongozi una mafao/thawabu, gharama na anasa zake. Anasa ni pamoja na vikwazo vilivyomo. I) {a} Mafao (Faida) & Thawabu ya Uongozi:- 1Thes. 5:12 - 13, Ebr. 13:17, 1Petr. 5:2 - 4, 1Kor. 9:10. Heshima katika jamii - (Social Status). Kutambuliwa na kueleweka - (Recognitation & Position). Mapato (Material gain). Mamlaka (Power & Authority). Kuwa na mvuto kwa watu (Influence). Mafao ya Kiroho (Spiritual Benefits). Taji ya utukufu (Glorious Crown) Dan. 12:3 na 1Kor. 15:41. Kupata kibali kwa Mungu na kwa wanadamu (God’s favour) - Mith. 3:3 - 4. {b} Kuongoza vizuri mafao/faida ya uongozi: Hesabu 27:12 - 23. Ni jambo la msingi na lakuzingatiwa sana kwa kila kiongozi aliyepata kibali cha kuongoza kuyafanya haya:- Uuone uongozi kama dhamana. Uwe na nia ya Utumishi. Jifunze kutofautisha kati ya mambo yako binafsi na cheo. Kumbuka: Panga maisha ambayo unaweza kuishi bila cheo. Wekeza kwa ajili ya siku za mbele. Uwe tayari kumpisha mwingine kuchukua cheo au nafasi yako. Kumbuka: Kuandaa Kiongozi/Viongozi (mrithi/warithi) watakaoendeleza mbio za uongozi hata wakati ambao hautakuwepo. Mfano: Eliya, kabla ya kuondoka alimwandaa Elisha. 1Falme. 19:15 - 21. Musa alimwandaa Joshua.Hesabu .27:12 - 33. Paulo alimwandaa Timotheo - 2Timotheo.2:1 - 3. Mwamini Mungu katika nafasi uliyonayo.Yosh.1:6 - 9. II) {a} Gharama za Uongozi. Math. 5:11 - 12, Yoh. 10:11, Lk. 15:4, Yoh. 15:3, 1Sam. 17:35 - 37. Kujitoa muhanga kwa ajili ya wengine (kondoo) - (Personal sacrifice). Mateso ya kibinafsi - Kutokana na hisia mbalimbali. Kukataliwa, kukatishwa tamaa, kuchekwa, kuzomewa, kulaumiwa, kudhalilishwa. Matatizo ya ndoa na familia (kutengana kimajukumu) kusingiziwa, upweke, shutuma, chuki, kusingiziwa, kusemwa, kuudhiwa. Kuingiliwa katika maisha kwa mambo binafsi. Kuwa tayari dhidi ya majaribu yatokanayo na fedha, zinaa (wanawake/wanaume) na utukufu (sifa) na matumizi mabaya ya madaraka n.k. 1Petr. 4:14; 2:20, Zab. 89:50 - 51. {b} Kukabiliana na Gharama za uongozi. Mjue sana Mungu na kumpenda - Fil. 3:8 - 10, Ayu. 22:21. Jiandae kukabiliana na gharama hizo - Fil. 1:27 - 29. Tumia muda wako vizuri kwa mambo yote, yaani uwe na kiasi. Kol.4:5, Efes. 5:15 - 16. Uwe tayari kuwajibika. Uwe mtu wa maombi, ili kumshirikisha Mungu mambo yote na kumtegemea. Zab.37:2 - 7, 23. Jaa neno la Mungu - Kol. 3:16. Jaa Roho Mtakatifu - Efes. 5:18. Inua kiwango chako cha Ibada - Yoh. 4:23 - 24. Kuishi maisha safi - Matakatifu yenye ushuhuda mzuri. Math. 5:13 - 16. III) {a} Anasa au majaribu (vikwazo) vya uongozi: Anasa ni mambo ya starehe yasiyo ya lazima. Uongozi huambatana na anasa zake ambazo ni mitego na majaribu kwa kiongozi. Baadhi ya majaribu hayo ni:- Kujiona umefika juu ya kilele (kiburi) - Isa. 14:13 - 14, Mith. 29:23. Kushindwa kuwa na maono - Mith. 29:18. Kuacha kuwa mfano wa kuigwa. Kutumia madaraka/Uongozi kwa faida binafsi. Kukataa kujipima mwenyewe - Gal. 6:4 - 5. Kuridhika na utendaji usioridhisha. Kutumia vibaya madaraka/uongozi kwa watu unaowaongoza. Zinaa/Uzinzi/Uasherati. Kujisifu na kujiinua (sifa) - Fil. 2:3, 14:16. Wivu. Kutokujali familia. Kukosa motisha na kuahirisha mambo. Kujisikia huwezi na hufai (kujidharau na kujikataa) - Hesabu. 13:32 - 33. Kupoteza dira ya uzima wa milele. Fedha - 1Tim. 6:10. na yanayofanana na hayo. {b} Namna ya kukabiliana na Anasa, mitego na majaribu ya Uongozi: Soma maandiko haya:- 2Tim. 4:15 - 16, 1Thes. 4:1; 5:17 - 18, Fil. $:6 - 7. Hivyo ni lazima:- Kukaa katika maadili mema ya Kikristo. Kudumu na kutii neno la Mungu. Kudumu katika maombi - Mith. 16:3, Lk. 18:1 - Kuhusisha mambo yako kwa walio karibu nawe, watu au timu yako ya Uongozi kwa ushauri. Mith. 20:18, Mith. 15:22. 10. SIRI YA MAFANIKIO YA UONGOZI/KIONGOZI WA KIROHO: Pamoja na kuwa na maadili bora mambo yafuatyo ni muhimu sana kwa kiongozi ili aweze kufanikiwa:- i) Kumwamini na kumpenda Mungu - Yoh. 14:1, 12, 21, 23. ii) Kufanya mapenzi ya Mungu - Math. 7:21, Efes. 5:10, Yoh. 5:24. iii) Maombi - Lk. 18:1, 1Tim. 2:1, Lk. 6:12, Mark. 1:35 - 39, Ebr5:7 - 10, Ezr. 8:21 - 23. iv) Kuwa na mipango mizuri - Lk. 14:28 - 32, 1Tim. 3:15. v) Kujali rasilimali ulizonazo pamoja na muda na watu - Kut. 10:24 - 26, 8, 9, Lk. 22:35 - 36, Efe. 5:15 - 16. vi) Mahusiano bora na wengine wanaokuzunguka - Ebr. 12:14 - 15, Yoh. 13:34 - 35.. vii) Usiridhike na ulichonacho tamani kujifunza toka kwa wengine - Mith. 2:3 - 6, Mith.12:9 - 11. KIONGOZI MWENYE MAONO NA MALENGO: Mithali 29:18. Ipo tofauti kubwa kati ya Maono na Malengo (A) MAONO NA MALENGO: MAONO: Ni ule uwezo wa kupata picha ndoto/dira/ufunuo ya mambo ya siku za mbele; ambapo MALENGO: Ni ile namna ya kuyatekeleza hayo maono uliyoyaona au uliyoyapata. Ni kufanya safari toka kwa unayoyaona sasa kwa yasiyofahamika na kuyaona kama yapo katika uhalisia. Watu wengi wanakwama kwani wanadhani kitu cha muhimu ni fedha, hapana cha kwanza ni kuwa na maono pesa ije iingie kwenye hayo maono. Pesa bila maono itapukutika yote. Rejea kwa Yusufu aliingia Misri kama mtumwa, hana kitu, lakini alikuja kuwa mtawala kwa sababu alikuwa na maono. Mfano: Nuhu aliona mapema gharika juu ya uso wa nchi akawaonya watu wake. Mwa. 6:13 - 22. Yusufu aliona miaka saba ya njaa kabla ya kutokea. Mwa.41:28 - 30. Musa aliona nchi ya ahadi - Kut.3:3 - 9. Nehemia aliona Yerusalemu mpya - Neh. 1:2 - 6, Neh. 2:3 - 5.. Paulo aliona Makedonia inahitaji injili Mdo. 16: 9 - 10. Swali: Je, wewe unaona maono gani juu ya:- {a} Kanisa? (b).Familia yako? n.k. Kumbuka: Mtu mwenye maono siku zote hufuatwa na kutafutwa na watu, bali mtu asiye na maono siku zote huwa mtu wa kufuata na kutafuta watu. Soma Mwanzo. 45: 3 - 10; 50:20 - 21. (B) BAADA YA KUONA MAONO: Ni lazima mambo yafuatayo yafanyike ili maono yawe mambo au kitu halisi na wala sio ndoto za kupita tu. Kuhamasisha watu; Ili kuyatimiza mambo uliyoyaona. Mfano, Musa alihitaji kuwaona wazee wa Israel kwanza - Mwa. 3:16 - 18, 4:29 - 31. Hivyohivyo na Nehemia pia - Neh. 2:17 - 18. Kuweka malengo: Yaani mipango ya utekelezaji ili kuyafanikisha maono lengwa/ husika. Kumbuka: Pasipo maono watu hujiendea - hupuyanga hovyohovyo na mwisho hupotea na kuangamia; Na pasipo malengo na mipango mizuri watu watashindwa kuyafikia maono, na hawawezi kuhamasika tena kuendelea mbele kuyatekeleza. Hatimaye kila mtu atafanya anavyoona inafaa machoni pake mwenyewe.Amuzi. 21:25. (C) MSINGI WA BIBLIA KUHUSU KUWEKA MALENGO: Yesu alitoa mfano wa mjenzi wa mnara na mfalme aendaye vitani. Lk. 14:28 - 32. Paulo alitoa mfano wa mwanariadha, mpiganaji ngumi, mkulima, mwanamichezo na Askari - 2Tim. 2:3 - 10, 1Kor. 9:24 - 26, Fil. 4:14, 2Tim. 4:7. Mjenzi katika kuweka malengo inamlazimu kuchora ramani, kukusanya vifaa na rasilimali zingine, kisha kuanza kujenga hatua kwa hatua. Mpiganaji kabla ya vita (pambano) hujiandaa, huandaa majeshi, vifaa, silaha na njia (mbinu) za kuendelea na hivyo hujipanga kikamilifu kabla ya yote, kwa nia ya kupigana. Kumbuka: Mpango wa Mungu wa wokovu ulikuwa na malengo na mipango yake ya utekelezaji. Hivyo Mungu aliandaa mtu mmoja ambaye ni Ibrahimu, Baba wa Imani. Kisha Taifa la Israel kuwepo. Manabii/Yesu kuzaliwa awe mkombozi wa ulimwengu. Mitume/Roho Mtakatifu/Kanisa/ Hatimaye wokovu wa milele (Uzima wa MIlele). (D) FAIDA YA KUWEKA MALENGO NA MIPANGO: i) Huwezesha kuwa na mwelekeo mzuri wa mambo au kazi katika maisha. Kumbuka: Watu wote wasio na malengo hawafiki popote. Malengo na mipango hufanya maisha yawe ya maana na huweka mwongozo wa maisha. “Kama hujui unakokwenda, njia yoyote itakufikisha huko usikokujua.” Hivyo kukosa malengo na mipango huo ni upofu, na shimoni lazima utatumbukia tu - Math. 15:14 Kumbuka: Ukilenga hewa utafanikiwa kupiga shabaha hiyo, na hakuna anayelenga hewa akaikosa.” ii) Huhamasisha mambo kufanyika: Viongozi wengi waliofaulu vizuri wanakiri kuwa walihamasika na malengo waliyokuwa nayo, na kujiona wakitembea kuelekea katika malengo hayo. Ni malengo yanayowaelekeza ni wapi wawekeze na kutoa vipaumbele katika mali na rasilimali walizonazo na pia nguvu zao. iii) Humfanya mtu kuwa na Tabia (shauku) ya kutaka kuona matokeo. Malengo na mipango humfanya kiongozi awe na hamu/ shauku ya kuona matokeo ya kazi anayoifanya na maendeleo yake yalivyo. Malengo yanamfanya mtu kuweka mkazo katika matokeo, badala ya shughuli zinazofanyika. Malengo na mipango humsaidia kiongozi Kupima utendaji na shughuli (huduma) yake. Kujua umekwenda umbali gani? (napiga hatua au hapana) Kuwajibika. Kutathimini kazi mara kwa mara na kuboresha utendaji wake. Gal 6:4 -5 Kumbuka: Viongozi waliofaulu ni watu ambao wana malengo kwa siku za mbele. Si watu wa kushughulikia matukio tu au watu na mambo yaliyopita. Huwa hawasubiri mambo yaotokee na ndipo wafanye kitu, bali ni watu wanaojitahidi kutimiza mambo, kwa sababu:- i) Wana maono yaliyo wazi. ii) Hujiwekea mipango na ratiba ya kutimiza maono hayo. iii) Wanawajibika katika kufuatilia malengo waliyojiwekea. vi) Huvumilia wakati maono, malengo na mipango inapokutana na vikwazo mbalimbali na kutotimiza malengo aliyokusudia. v) Hupata ufumbuzi na kubuni njia ya kuendelea mbele si kurudi nyuma na kukata tamaa. 12. AINA YA VIONGOZI/UONGOZI. Kuna viongozi wa aina nyingi, leo tuangalie mbili ambao ni: Wale wanasababisha mambo kutokea na Wale wanaosubiri mambo yatokee. I} sifa za viongozi wanaosababisha mambo yatokee. Wana mtazamo wa mbele (wana ndoto, maono, malengo, mipango) Mith. 29:18, Mwanzo 37:5-11. Wako tayari kupanga mipango, na kuona jinsi gani watakavyoyatimiza malengo/maono hayo. Mwanzo 41:1 – 44 (Mst. 25 – 40) Wanaweka mikakati ya kuzuia matatizo yatakayoweza kutokea. Mwz 41:33 – 36. Hawakati tamaa na pia ni hodari na jasiri. Hesabu 14;6 – 9’13:30 II} sifa za viongozi wanaosubiri mambo yatokee. Hawafanyi chochote/hawajishughulishi mpaka mambo yatokee. Hutumia muda mwingi kushughulikia matukio. Hesabu 13:31 -33 Ni wazima moto na hutumia muda mwingi kuzima moto bila kujiuliza chanzo cha huo moto kutokea. Math 9:32 – 33. Kumbuka: Tofauti kubwa kati ya viongozi wa aina mbili hii ni Uwezo katika malengo na kujishughulisha na mipango pia mikakati mbalimbali katika kutimiza maono yaliyopo. Kumbuka: Maono, malengo na mipango lazima iwe Smart (safi), yaani iwe na sifa hizi:- Uongozi wa Roho Mtakatifu na yenye shabaha (yaliyo wazi – bayana). Measurable – kupimika/yenye kutathiminika. Attainable – yenye kufikika. Realistic – yawe halisi Time targeted – muda maalum Soma Lk. 4.:18 – 22, 1Tm. 4:7, 1Kor. 9:24 – 26 Maono/mipango/malengo yanaweza kushindikana kufikiwa kutokana na sababu zifuatazo:- Hayakuwa na shabaha (bayana) maalumu. Hayapimiki. Hayafikiki kirahisi. Hayako halisi kibinadamu. Hayakutengewa muda maalumu, yangekuwa na muda yangeweza kuhimizwa na kukamilishwa haraka na hivyo kufurahia matokeo yake. Kumbuka: Maono yako yafafanuliwe kwa maneno yako, maneno yako yazae matendo na tabia, malengo, mipango na mikakati. Hatimaye yataonekana matokeo kamili (halisi) kutokana na mawazo uliyonayo> bila hivyo mawazo/maono uliyonayo yatabaki kuwa ndoto tena za mchana. Hivyo kiongozi wa kiroho lazima kuwa na mtazamo wa ki Mungu, kama vile Mungu mwenye Enzi alivyo na maono thabiti tangu mwanzo hadi mwisho wa kazi yake katika ulimwengu huu na ule ujao. Mipango na mikakati yake ya wokovu imekuwa na ushirikishwaji wa mwanadamu na kwa uwazi kabisa. Rumi 8:28. Uongozi wa kiroho unabeba sura ya Mungu mwenyewe kwa wana wa Mungu wanaotegemea. Mith. 16:4, Rumi 8:14, Yhn. 15:6, Isa. 14:24, Math. 28:20 13.KIONGOZI ANAYEFAA KUIGWA NA WATU WENGINE. Zifuatazo ni baadhi ya sifa/vigezo apasavyo kiongozi kuwa navyo ili watu wengine waweze kuiga kutoka kwake. Watu huvutiwa na kumfuata kiongozi aliye na:- I} Maono. Kiongozi asiye na maono hafai kuwa kiongozi. Mungu humtumia mtu mwenye maono na mipango safi. Mfano Musa, Joshua n.k. Hivyo kiongozi lazima ujue unakwenda wapi na Mungu anataka nifanye nini? Mith. 29:18 II} Mfano/Kielelezo: 1Tim 4:11 – 12, 2Kor. 3:2 -3 Mtume Paulo hakusita kuwaeleza watu kuwa wamfuate/wamuige yeye anavyofanya. 1Kor. 11:1, Fil. 3:17, Fil. 4:9, 2Thes. 3:7, Lk. 14:25. Kumbuka: Kuacha/kushindwa kuongoza kwa mfano mwema ndio kuzaliwa hadithi za kale, utasikia mtu anasema, enzi zetu, wakati, miaka ile tulifanya hiki na kile, lakini leo hawezi, hilo tayari ni tatizo, umeshindwa kuwa kielelezo kizuri. III} Uadilifu: 1Sam 16:7 – Uadilifu ni suala linalohusika na moyo wa mtu mwenyewe (tabia) yake.1Sam. 16:7, Zab. 78:72 Kumbuka: Unapopoteza uadilifu umepoteza uthamani na ubora (kibali) cha uongozi wako. Uadilifu unajengwa kupitia; kufanya (kutenda) na kutekeleza ahadi na kujitoa kikamilifu. IV} Neno la Mungu: Ebr. 4:12, 2Tim 13:17, Mdo 6;2, Ebr 13:7, Kol. 3:16, Yh 1:1 – 14. Viongozi ni wasomi wa neno (Leaders are Readers) kwa sababu, Mtumishi wa Mungu hutegemea neno la Mungu, kumuongoza Zab. 119:105 na kumpa nguvu (chakula) Math 4:4, Ay 23:12. Je unafanya nini ili kujilisha neno? Unafanya nini katika kuhakikisha wengine wanakula (pata) neno la Mungu? V} Maombi: mdo. 6:4, Lk. 5:16. Kama kiongozi lazima ujitoe kikamilifu katika maombi na kulihudumia neno. Mara zote mwanadamu hutafuta njia zilizo bora zaidi. Mungu naye anatafuta mtu (kiongozi) bora aliyeshujaa na hodari katika maombi. Mfano Joshua akiwa vitani Kut. 17. VI} kiongozi aliyejaa roho mtakatifu: Mdo 6:3, Yhn. 15:5, 2kor. 3:5 – 6, 2kor 13:14, Kol.1:1 – 29. Sisi (viongozi) bila roho mtakatifu hutuwezi kufanya chochote. Kumbuka: Popote palipo na kiongozi aliyejaa Roho Mtakatifu elewa kuwa nyuma yake yupo Mungu 2kor 3:5 – 6. VII} Mwenye Bidii na Kazi: 1Thes. 5:12 – 13, kut. 2:15 Kiongozi bora, Mtumishi lazima awe na bidii ya kazi za mikono na huduma ili watu wamkubali. Rumi. 12:8 VIII} Mwenye Imani: Ebr 13:7, 11:1,6, Ebr. 10:38, Rumi 1:17. Mwanafalsafa mmoja alisema “Ni bora kuwa na simba mmoja anayewaongoza kondoo elfu moja, kuliko kondoo mmoja kuongoza simba elfu moja.” Kiongozi bora lazima awajibike kuwaongoza watu katika kumwamini Mungu na kumtegemea yeye (Mungu). IX} Anayekua/Ongezeka (Mwenye Kujifunza) Yh. 8:31 – 36. Kiongozi hayuko kamili ila mara zote yupo kwenye mchakato wa kujifunza mambo mapya katika maisha yake ya Imani. Kumbuka: Kiongozi aachapo kujifunza na kukua ndipo mwisho wake wa kuongoza hufika. X} Maisha Safi ya Nyumbani: 1tim. 4:12 -16. Mtu mmoja alisema, “ikiwa haifai nyumbani, usiiuze nje.” Ukishindwa kusimamia nyumba yako, yaani mke/mume na watoto tayari umeshindwa kuwa kiongozi bora wa kiroho ( ki – kristo). 14. Misingi ya Kiongozi/Uongozi wa Kiroho. Misingi ni nguzo ambazo kwazo kiongozi wamejengwa au anajengwa ili kufaa katika uongozi: a} Kujitoa kwa Kristo (Bwana – Mungu) – 2Kor 8:5 Watu – 9yhn 3:16 b} Utii: mwz. 12:1 – 4 Neno utii limeunganishwa na Bwana wa majeshi. Hii lugha ya kijeshi wajibu wa askari ni kutii kutekeleza amri kwanza na maelezo baadae Efo. 6:1- 2. c} Uaminifu: 1kor. 4:1 – 2. Kipimo cha Kiongozi ni Uaminifu Katika Maagano. Mahudhurio. Muda. Matokeo. Ibada n.k. d} Tabia za Kiroho/Nidhamu za Kiroho: Mdo 6:4 Maombi Kusoma na kutafakari neno. Ibada Matokeo Utumishi (Huduma) Kumbuka: Nguvu zetu katika huduma inategemea muda ninaokaa mbele za Mungu, kuomba na kutafakari neno lake. e} Uwajibikaji: Mark 6:7, 30 unapokuwa kiongozi kuna maneno ya:- Kuagiza. Kutumwa (kuagizwa jambo) Amri (hakuna kuhoji ni kutekeleza tu). Kumbuka: Ni lazima kutoa taarifa kwa mkuu wako ( Mchungaji) Lazima uwe mtu wa mawasiliano. f} Kuambatana: 1Sam. 18:1, 1Kor. 1:10, Math. 12:30, Ruth. 1.14 – 18. Kuambatana ni kushikana na viongozi wenzako ili kutompa nafasi ibilisi (Adui) shetani kutushinda. Efe. 4:27.Kutokuwa kigeugeu Mith 26:21. Misingi ya kuambatana: 1kor. 1:10 Kunena mamoja. Kutokuwa na faraka – matengano Kuwa na nia moja. Kuwa na shauri moja. Siri ya kufikia hatima yako njema salama katika uongozi ni lazima ujifunze kuambata na wenzako vizuri, bila hivyo hutafika mbali (itakuwa kama mbio za panya sakafuni). Nikinukuu maneno ya makamu Askofu Mkuu wa TAG Dr Magnus Mhiche alisema siku moja kuwa “ukitaka kwenda mbali nenda mwenyewe (peke yako), lakini ukitaka kwenda mbali zaidi jifunze kwenda (kuambatana) na wengine. Mfano: Gehazi alishindwa kufikia hatima yake akiwa na nabii Elisha baada ya kujitenga kushindwa kuambatana naye. 2Falme 5:20 – 27. Pia Akani aliuwawa kwa kupigwa mawe maana hakuweza kuambatana na Joshua. Yosh.7:9 – 25. Kumbuka: Ili ufike (mwisho) hatima yako lazima ujifunze kuambatana na wenzako maana wao ni walinzi wako. Dawa/tiba ya mtu asiyependa kuambatana na wenzake ni kumtupa nje kumwondoa. Mith 22:10, Yosh. 7:1 – 25 kwani bila kufanya hivyo wote mtapigwa na adui wala hamtaweza kusimama tena. g} Kupokea Maonyo: Mhubiri 4:13 Kiongozi bora wa kiroho lazima ajifunze kupokea maonyo/awe tayari kuonywa na kusahihishwa pale atakapo kengeuka/kosea. H} Kuwa Balozi Wako (Mchungaji) Jifunze kumtaja vizuri au kumnena vema kiongozi/mchungaji wako (Mkuu wa kituo) mbele ya watu pia jaribu kunukuu na kurejea mafundisho yake ukionyesha jinsi yalivyokusaidia na waimarishe watu kutokana na mafundisho yake na maono ya Kanisa hasa pale upatapo nafasi kusimama madhabahuni au katika idara yoyote na kipindi chochote Kanisani na siyo kumpinga (kumponda) na kuanzisha kitu kipya. 15. Lugha ya Kiongozi/Uongozi. Lugha ni njia ya mawasiliano. Na ili adui awaweze na kuwashinda ni lazima kwanza aharibu miundo mbinu yenu ya mawasiliano. Lugha pekee ya kiongozi ni KUAMBATANA. Tazama Ruth. 1:14 – 18, Amos. 3:3 na 1Sam 18:1. 16. Sifa za Jumla za Kiongozi/Uongozi wa Kiroho. Kiongozi wa kiroho lazima awe na:- Uwezo wa kuongoza Mcha mungu Mkweli Achukie mapato ya udhalimu (utapeli) yasiyo halali (rushwa). Mtu mwema/mwadilifu. Amaanishe anachosema na aseme anacho maanisha. Ajae roho mtakatifu. Awe mvumilivu Awe na maono (Mith. 29:78) Apende ibada Awe mtunza siri. Awe mbunifu Mw 30:25 – 43, 2:15 Awe na hekima. Awe mtu wa kujitoa Asiwe mtu wa udhuru Awe mnyenyekevu 1Pt 5:6, Math 8:21 – 22, 1Flm 19:20. Awe mcheshi Aishi maisha ya uanafunzi. Yhn. 8:31 – 36. Anayekubali changamoto na kufanya uamuzi. Awe amezaliwa mara ya pili. Yh.3:3 – 8. Awe na huruma. Lk. 7:12 – 13, Math. 9: 35 – 38. Awe mtu mzima katika imani, siyo mchanga. 1Tim.3:6 Anayekubali ushauri. Kut. 18:13 – 27. Awe na ufahamu sahihi wa neno la Mungu na mambo mengine Mith. 2:3 – 6. Soma Pia: Kut. 18:21 – 24, Mdo 6:3, Rumi 12:6, Mith 11:30, 2Nyakati 1:11 – 12, 1Tim 3:1 – 13, 1Falme 3:5 – 28. 17. Wajibu wa Jumla wa Kiongozi wa Kiroho. Mdo 20:1 – 38, Yhn 10:11 – 15. Wajibu ni majukumu (kazi) apaswayo kiongozi kuyafanya kwa nguvu zake zote ili kuyatimiza malengo yake. Baadhi ya majukumu/wajibu wake ni :- i} Kujitunza nafsi yake: 1Thes 5:23 Nafsi imebeba:- a} Akili b} Makusudi (nia) c} Hisia Mith. 4:23, 1Kor 15:33 – 34 Hivyo kama kiongozi lazima uitawale nafsi yako mbele ya hao unaowaongoza. ii} Kulitunza Kundi Ni wajibu wa kiongozi kulilinda, kulichunga na kulihakikishia usalama kundi ninaloliongoza dhidi ya:- a} Mbwamwitu wakali: Watumishi waharibifu ambao kondoo siyo wito wao. b} Imani potofu: Mafundisho ya uongo (Mashetani). Kumbuka: Hili litawezekana pale tu kiongozi atajitoa kwa kufundisha watu wake Elimu sahihi ya Imani (Neno la Mungu) – (Sound Doctrine). Tunayapinga mafundisho ya uongo kwa kufundisha kweli ya Mungu. Yuda 1:3 – 6, Yhu 8:31 – 36, Hosea 4:6, Mith. 11:9 na Mith. 21:16 Kumbuka: Kanisa linaangamizwa kwa kukosa maarifa, Elimu sahihi ya neno la Mungu. Hosea 4:6, Mith. 21:16. Hali kadhalika Kanisa linapona kwa maarifa. Mith 11:9, Yhn 8:31 – 36. Kumbuka: Kanisa linajengwa/kuimarishwa na kuponywa kwa mafundisho, mafafanuzi ya neno la Mungu. Za 119:130 na wala siyo Mahubiri, kukemea maombezi. Kumbuka: Shetani haogopi mahubiri wala maombezi au makemeo bali anaogopa ufahamu unaomjua Mungu. Ay.22:21, Lk. 4:1 – 14. Hitimisho: Mungu haangalii uliipataje nafasi hiyo ya uongozi, yeye anaangalia kusudi lake la hiyo nafasi linatimia kikamilifu. Elewa kuwa Roho Mtakatifu ndiye aliyehusika kuwatumia hao waliokuchagua au aliyekuteua katika nafasi hiyo ya uongozi uliopo. Hivyo sasa, kuwa huwajibiki kwa mtu (mwanadamu) bali kwa Mungu moja kwa moja. Mdo. 20:28. Elewa, kuwa kutokutimiza wajibu wako kama kiongozi haumkomoi mtu bali unatafuta ugomvi na Mungu aliyekuwa kuwa mwangalizi, kiongozi na msimamizi wa kundi lake. Zingatia: Itakuwa heri kwako, Bwana akikukuta ukidumu katika kuwahudumia watumwa, watu wake kwa Uadilifu na Uaminifu wote na kwa unyenyekevu kabisa; atakuweka kuwa juu ya vitu vyake vyote na usipofanya hivyo atakukatakata vipande vipande na kukutupilia mbali. Math. 24:45 – 51. SOMO LIMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA BISHOP RHOBINSON S.BAIYE MKOLANI MWANZA TANZANIA. 10/ 5/2021

MBINU ZA KUTAFAKARI NA KUTAFSIRI MAANDIKO MATAKATIFU

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KUTAFAKARI NA KUTAFSIRI MAANDIKO MATAKATIFU (BIBLIA) NENO LA MUNGU ( Yosh 1:8-9 Zab 1:1-6 Md 17:11 BISHOPO RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO 1:Kutafakari Maandiko……………………………………………………… 2:Kutafsiri Maandiko………………………………………………………... 3:Mbinu Za Kutafakari Na Kutafsiri Maandiko……………………….. a.Soma maandiko matakatifu mara kwa mara……………………….. b.Fanya utafiti wa mambo…………………………………………………. c.Fanya udadisi wa mambo……………………………………………….. d,Gundua mambo muhimu yaliofichika……………………………….. e.Nidhamu katika matumizi ya sarufi………………………………….. f.Mahitaji muhimu………………………………………………………….. 1:KUTAFAKARI MAANDIKO MATAKATIFU KUTAFAKARI Kutafakari ni kitenzi kitokanacho na neno tafakuri au tafakari,likiwa na maana ya kufikiria jambo kwa makini na fikira nzito juu ya jambo fulani yaani mazingatio.Kutokana na tafsiri hiyo,inatupa picha yakwamba kutafakari na kutafakuri huleta maana ya kuchukuwa munda na kuwa makini katika jambo unalowaza na kulichunguza kwa kulizungumzia,kwa uangalifu.kwanza kwa makini na kwa undani dhaidi.kujenga picha katika fikra zako namna ambavyo jambo linaweza kuwa.Ni kujifunza kuchunguza ili ujue kusema jambo kwa sauti ya chini ambayo haisikiki vizuri kwa ajili kuwa na mawazo ya kumshirikisha mtu mwingine,hisia zako au misisimko yako bila kutamka neno na hata kulalamika. Je! Ninawezaje Kutafakari Maandiko Matakatifu? Mazoezi ya kiroho ya kutafakari sio jambo geni kwa Ukristo. Dini nyingi zisizo za Kikristo na vikundi vya kilimwengu hufanya mazoezi ya kutafakari. Walakini, wakati Biblia inazungumza juu ya kutafakari, kama vile inavyofanya mara nyingi, sio aina ya kutafakari ambayo hutafuta kujitenga, kimya, au kufunua akili, kama vile ilivyo katika aina ya dini za kutafakari mafumbo ya akili au tafalaro ua Wabudha. Maandiko yanafundisha tafakari ambayo hushughulisha sana akili kwa kusudi la kuelewa Neno la Mungu na kuliweka katika matumizi. Je! Tunawezaje kutafakari Neno la Mungu ili lizae ndani yetu maisha yenye matunda na matakatifu mbele,za,Mungu? Katika ulimwengu wa kale wa Kiebrania, kutafakari wakati mwingi kulihusisha kutumia na kushirikisha akili. Thomas Watson, mchungaji wa Wa-puritani wa karne ya kumi na saba, alitumia muda mwingi katika maisha yake kuitafakari Biblia, huku akiiweka katika mazoezi na kufundisha juu yake. Alifafanua vyema sana nidhamu hiyo katika kitabu chake Heaven Taken by Storm kama mazoezi matakatifu ya akili, ambayo kwayo tunaleta ukweli wa Mungu katika kumbukumbu, na kuyatafakari kwa uzito, na kuyatumia,sisi.wenyewe. Kwa mjibu wa ufafanuzi wa Watson, tunaweza kutafakari juu ya Neno la Mungu kwa kukumbuka ukweli Wake. Kukumbuka kunahitaji kukumbuka kwa bidii na kwa ufahamu wa kile tunachokijua juu ya Mungu kutoka kwa Neno Lake: "Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku" (Zaburi 63: 6). Kulingana na Zaburi 1: 2, mtu aliyebarikiwa, anayezaa matunda, na mwenye haki hufurahia Neno la Bwana "naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana." Tafakari hii ni ya endelefu ("mchana na usiku") na inazingatia Neno la Mungu ("sheria yake"). Tunalitafakari Neno la Mungu kwa kujaza akili zetu na Neno hilo mchana na usiku. Mungu alimwita Yoshua kutafakari kwa uhodari na kwa kuendelea: Usiache Kitabu hiki cha Sheria kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi" (Yoshua 1: 8). Hapa, kutafakari kwa kibiblia kunapanuka kutoka kufikiria tu hadi usemi ("kwenye midomo yako"). Kifungu hiki pia kinasema kusudi la tafakari, ambayo ni, kutii Neno la Mungu, ambalo huzaa mafanikio na ufanisi mbele za Mungu. Maelezo ya Watson ya kutafakari hujumuisha na kutafakari kwa uzito au kutafakari ukweli wa Mungu. Zaburi 119: 15 inasema, Nitajifunza maagizo yako na kuziangalia njia zako." Kwa hivyo tafakari ya kibiblia inajumuisha kutafakari kwa kina na kujifunza Neno la Mungu. Tunapoisoma Biblia, je, tunaisoma pole pole na kwa makusudi? Je! Tunafikiria juu ya umuhimu wa maneno na jinsi yanahusiana na maisha yetu na maisha ya wengine? Ikiwa ndivyo, basi tunatafakari juu ya Neno la Mungu. Kutafakari kunahitaji wakati na bidii. Hakuwezi kuharakiswa. Kunajumuisha kujiondoa kwenye usumbufu wa maisha haya ili tuweze kuweka mawazo yetu kwa Mungu na Neno Lake. Kwa kufunga kelele za ulimwengu huu, tunaweza kuelekeza mawazo yetu kwa Mungu na kuelewa njia zake: "Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako" (Zaburi 119: 99). Hatimaye, kama vile Watson alivyogusia, tafakari ya kibiblia inatafuta kutumia Neno la Mungu kwa maisha yetu. Zaburi 19:14 inaonyesha ukweli huu: "Maneno ya kinywa change na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu na Mkombozi wangu." Kutafakari juu ya Neno la Mungu kunapendeza machoni pa Mungu kwa sababu husababisha mabadiliko ya maisha yetu. Tunaposoma na kunena ukweli wa Mungu na kuutafakari kwa bidii, Roho Mtakatifu hutuwezesha kuutumia ukweli huo katika vitendo. Katika Wafilipi 4: 8–9, mtume Paulo anatupa taswira hii nzuri na kamili ya tafakari ya kibiblia: "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo. Mambo yote mliyojifunza au kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja,nanyi." Kutafakari ni njia ya kuzingatia Neno la Mungu kwa ndani —kuliweka ndani ya mioyo yetu — ili Roho Mtakatifu aweze kufanya kazi kupitia kwalo ili atuongoze, atufundishe, atutakase na kutubadilisha kutoka ndani. Tunaweza kuisikiliza Biblia ikisomwa, tuisome, na kukariri Maandiko ili tuingize akilini mwetu, lakini pia lazima tuitafakari kila wakati mioyoni mwetu ili tuweze kuielewa zaidi na jinsi inavyotumika katika maisha yetu. Vidokezo vya kutafakari neno la Mungu 1. Chagua wakati na mahali maalum kila siku wakati hautaweza kusumbuliwa au kuachishwa ili upate kuwa peke yako na kutafakari. 2. Anza na maombi na mwombe Mungu akusaidie katika kutafakari kwako. Unaweza kumwuliza Bwana akulete karibu naye, afungue macho yako kwa ukweli Wake, akusaidie kuuweka ukweli huo maishani mwako, na akubadilishe unapotafakari juu ya Neno la Mungu. 3. Chagua sehemu ndogo ya Maandiko. Fikiria juu ya kile kifungu hicho kinamaanisha. Jifunze kwa kina ili uweze kukielewa katika muktadha. Andika hati. Uliza maswali. Kariri kifungu hicho. Muulize Mungu anataka kusema nini nawe kupitia maandishi hayo. 4. Fikiria jinsi unaweza kutumia kifungu hicho katika maisha yako kwa njia za vitendo, na umwombe Mungu akusaidie kuifuata kwa kutii,kile,Anachokuonyesha. MAMBO YA KUTAFAKARI UNAPOTAFAKARI. 1:Maana 2:Tukio lenyewe/Matukio 3:Nyakati / Wakati/Nidhamu ya sarufi ufuatwe. 4:Msemaji au Tendaji 5:Mwandishi 6:Mlengwa/Walengwa. 7:Lugha Ya Msemaji / Mwandishi/Biblia/Mungu/ 8:Mazingira/Jografia 9:Utamaduni/Mila/Desturi. 10:Sababu/Lengo/Uhijaji/Shabaa. Utakapofanya hayo utafanikiwa kuupata ukweli na mambo halisi.Na itakupa nguvu za kujiamini kwa kutafsiri neno kwa usahihi na kuwa mtu makini asiye kurupuka madhabahuni. Matokeo Ya Kutafakari Neno La Mungu Vizuri. 1. Utapendwa na Mungu. 2. Mungu atakutumainia 3. Mungu atakutegemea 4. Mungu atakuheshimisha. 5. Mungu atakutukuza. 6. Utapendwa na watu 7. Utahitajika na watu 8. Utawaelimisha watu na kujua kweli. 9. Utakuwa mtu wa Mungu na watu. 2:KUTAFSIRI MAANDIKO MATAKATIFU TAFSIRI. Neno tafsiri lina maana mengi kama,1.Kutafsiri ni matini yaliyotolewa ni maelezo kutoka lugha moja hadi lugha nyingine.2.Kutafsiri ni Eleza maana ya maneno kutoka matini yaliyoandikwa katika lugha moja na kwenda katika lugha nyingine.3Kutafsiri maandiko ni kuweka wazi mafumbo,mithali,mifano na maneno ya wenye hekima. Mara nyingi wenye kupotosha ni kwa sababu baadhi yao hawajapitia mafunzo ya sayansi ya kutafsiri Biblia.Wengi hawajui kwamba pamoja na Biblia ni kitabu huru kusomwa na kutafsiriwa na kila mtu kwa kadiri anavyojaliwa au kufunuliwa na Roho Mtakatifu;bado ziko kanuni za kitaalamu za kutafsiri maandiko katika Biblia.Ni muhimu kujua na kufahamu na kuziishi kanuni muhimu na makini ambazo zimethibitishwa kuwa zinafaa kutafsiri Biblia ili kupata maana sahihi na makini za maandiko matakatifu. Neno mojawapo linalotumiwa na watafsiri wa maandiko linajulikana kwa kingereza kama Exegesis,ambalo tafsiri yake kwa Kiswahili ni ufafanuzi au uchambuzi.Sasa basi ufafanuzi au uchambuzi wa kibiblia unahusishwa kupima na kutambua kifungi cha andiko kwa lengo la kukitafsiri kwa usahihi.Exegesis ni sehemu ya mchakato wa hermeneutics,ambayo ndiyo sayansi ya tafsiri.2Tim 2:15) Kwa mujibu wa mstari wa andiko hilo.Tumeimizwa kulishika na kuliishi neno la Mungu kwa usahihi kwa bidii katika kujifunza.Ziko baadhi ya kanuni nzuri zinazoaminika katika uchambuzi wa maandiko ambazo baadhi yake ni kama ifuatavyo: Kanuni ya sanaa ya Lugha. Biblia iliandikwa kwa Lugha za kibinadamu na kila Lugha inamuundo na maneno na maana zake sahihi kwa ajili ya mawasiliano.Kwa hiyo tunaposaoma Biblia tukumbuke tunaisoma katika lugha za kibinadamu ambazozina ujuzi wake wa kutafsiri na zimebeba maana kamili ya ujumbe ulioandikwa humo.Uchambuzi wa kibiblia unaanza na kupata tafsiri sahihi ya misamiati ya maneno yaliyotumika kwenye maandiko.Kwa hiyo ni lazima kusoma na kutafuta kuelewa kike mwandishi alichomaanisha kwa wakati ule alipokuwa akiandika.Nilazima kujua kusudi la mwandishi kutumia misamiati ya maneno tunayosoma lilikuwa ni nini kwa wakati huo.Ili kuakikisha unapata maanasa sahihi inabidi kutafuta tafsiri rasmi za misamiati kwa kutumia kanuni za lugha za asili zilizotumika kuandika maandikohusika kama ni Kiebrania au Kiyunani. Ziko changamoto katika kutafsiri neno kutoka lugha moja kwenda katika lugha nyingine.Changamoto yenyewe ni pale ambapo neno moja linaweza kuwa na maana zaidi ya moja katika lugha ya msingi,lakini neno hilo likakosa neno sahihi kwenye lugha ya piliinayotafsiriwa.Katika mazingira haya kazi ya mtafsiri hulazimika ama kutafuta neno lenye kukabiliana na maana halisi katika lugha ya asili.Au njia nyingine ni kulikopa neno hilo kwa kulifanya neno jipya la lugha inayotafsiriwa. Kwa mantiki hii ndiyo maana haitoshi kutafsiri maandiko kutoka katika lugha zetu za asili mpaka tujiridhishe kwa kufuatilia neno hilo katika lugha ya asili ya Biblia ili kujua maana yake kwa mukhtadha wa lugha hiyo. Kanuni ya Kihistoria. NAKALA YA KWANZA YA TAFSIRI YA BIBLIA YA KIEBRANIA/TANAKH: Kwa mara ya kwanza na bila kutegemewa, Biblia ya Kiebrania, Tanakh ilitafsiriwa kwenye lugha ya KIGIRIKI/KIYUNANI kwa amri ya Mfalme Ptolemy II (285-246kk) katika ufalme wa Kiyunani uliokuwa na nguvu nchini Misri mjini Alexandria. Tafsiri hiyo ya kwanza ya Biblia Ya Kiebrania kwenda Biblia Ya Kigiriki/Kiyunani Iliitwa Septuaginta. BIBLIA YA KIYUNANI/SEPTUAGINTA. Septuaginta ni neno la Kilatini lenye maana ya “70”; kifupi LXX) ni tafsiri ya Biblia ya Kiebrania (Tanakh) kwa lugha ya Kigiriki ililofanywa mjini Aleksandria (Misri) kuanzia karne ya 3kk hadi karne ya 1kk. Inasadikika kwamba Mfalme Ptolemy II aliwaingiza wataalamu Wayahudi wapatao 72 katika vyumba 72 (kila mmoja na chumba chake) na akawapa amri ya kitafsiri vitabu vya Torati kwa Kigiriki bila kukosea ndani ya muda wa siku 72. Cha ajabu walifanikiwa kuitafsiri Torah kwa usahihi, kila mmoja akifanana na mwenzake. Idadi ya 72 ilitokana na watu sita kutoka kila moja kati ya makabila 12 ya Israeli ikafupishwa kwa kuikumbuka kirahisi kuwa “70”. Jina hilo liliendelea kutumiwa kwa tafsiri ya Kigiriki ya vitabu vyote vya Tanakh. Historia ya Septuaginta inasema, wakati wa utawala wa Ptolemi II vitabu vyote vya Torati vilitafsiriwa, ila vingine viliendelea taratibu kwa takriban miaka 200 baadaye. Kutokana na historia hiyo ndefu kuna tofauti katika lugha ya vitabu mbalimbali ndani ya Septuaginta. Septuaginta ina vitabu kadhaa visivyopatikana katika Biblia ya Kiebrania ya leo. Inaonekana vilitafsiriwa vitabu vyote vilivyotazamwa na Wayahudi wa Aleksandria kuwa Neno la Mungu katika karne ya 3kk – 1kk, vikiwa ni pamoja na vile visivyokubaliwa katika maeneo mengine. Biblia hii ya Kigiriki/ Kiyunani ilitafsiri vitabu vyote vya Tanakh. Pamoja na vitabu hivyo, Septuaginta iliongeza vitabu vingine kadhaa ambavyo navyo vilisadikiwa kufaa katika maandiko matakatifu na Wayahudi waliokuwa wanaishi Misri kipindi cha Mfalme Ptolemy II na walikuwa wanatumia Kiebrania cha kikoinia kuwa lugha yao ya mawasiliano. Vitabu hivyo vya nyongeza vinaitwa Deutrocanon yaani Kanoni ya pili. Hivi vitabu pia vimekuwa vinaitwa vitabu vya Apokrifa (Apocrypha books) kwa maana ya Vitabu vilivyofichwa (hidden books). Kwasasa vitabu hivyo ni zaidi ya 20 na vinatumika tofauti tofauti miongoni mwa madhehebu ya Kikristo. Vitabu vya nyongeza, Deutrocanon vilivyoongezwa kwenye Septuaginta ni pamoja na Tobiti, Yuditha, Hekima ya Suleiman, Hekima ya Yesu mwana wa Sirak, Baruku, Waraka wa Yeremia (Sura ya sita ya Baruku katika Vulgata), Sala ya Azaria kama nyongeza katika kitabu cha Daniel, Wimbo wa watoto watatu, Kitabu cha Suzana, Beli na dragoni, Wamakabayo 1,2,3&4, Kitabu cha Ode (Sala ya Manase), Zaburi za Suleiman na Zaburi 151. Vingi vya vitabu hivi vinaasili ya Kiyunani isipokuwa vitabu vitatu ambacho ni Siraki, Tobiti na Zaburi 151. Maridhiano kamili kati ya Wayahudi juu ya vitabu vinavyostahili kukubaliwa kama sehemu ya Biblia ulitokea mnamo mwaka 100bk, ambapo vitabu vichache vilivyotafsiriwa katika Septuaginta viliondolewa na Wayahudi wa Kifarisayo wa shule ya Yamnia walioshika uongozi wa Uyahudi na kushindana na Wakristo. 1 Timotheo 1 :3-5; “Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine; wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si madaraka ya Mungu yaliyo katika imani; basi ufanye hivyo. Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.” Azimio hilo lilisambaa polepole katika jumuiya za Wayahudi wa nchi mbalimbali. Lakini wakati huo Septuaginta ilikuwa tayari Biblia ya kawaida ya Wakristo wa kwanza, hata kabla ya kukamilika kwa kanuni ya Agano Jipya. 1 Wakorintho 1 :20-25; “Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa. Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu. Mafarakano kati ya Wakristo wa kwanza na Uyahudi yakawa yameisha tayari, hivyo Wakristo hawakuona sababu ya kubadilisha vitabu vya Agano la Kale walivyopokea katika Uyahudi. Sababu ya muhimu ilikuwa tofauti kubwa kati yao kuhusu lugha. Tito 3:9-11; “Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana. Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.” Wakristo, walioanza kama kundi la Kiyahudi, waliendelea kupokea watu wengi kutoka dini za kipagani za Dola la Roma wakatumia hasa Kigiriki kama lugha ya kimataifa ya mawasiliano. Hata Wayahudi wengi walitumia Kigiriki kwa mazungumzo kati yao lakini karne ya 1bk waliweka pia mkazo mpya kwenye matumizi ya lugha yao Kiebrania. Baada ya maangamizi ya hekalu ya Yerusalemu mwaka 70bk wakati wa vita ya Waroma dhidi ya Wayahudi, Wayahudi wengi waliona haja ya kushikamana zaidi hivyo ukawekwa mkazo zaidi kwenye utamaduni na mapokeo ya Kiebrania. Kanuni ya Andiko kutafsiri Andiko. 3.MBINU ZA KUTAFAKARI NA KUTAFSIRI MAANDIKO MATAKATIFU MBINU Njia zenye hila na ujanja za kufanyia jambo au kutengenezea jambo,kwa makini na kwa utaffiti,udadisi,na kuleta ugunduzi wa ukweli na uhalisia wa mambo.Mbini ni hatua zinazofuatwa ili kufanya hadi kukamilisha kazi,jukumu au tendo fulani.Ni ubunifu yaani uwezo wa kubuni uliostawi sana katika Binadamu na kufanya asichoke kutafuta majibu mapya kwa maswali yanayomkera,na njia mpya kutatua matatizo yake. NIFANYE NINI ILI NITAFAKARI NA KUTAFSIRI MAANDIKO MATAKATIFU KWA USAHII? Kuna mambo ya kufanya ili kukupa njia na uwezo wa kutafakari na kutafsiri maandiko matakatifu kwa kuonyesha na kuweka wazi ukweli uliopo na yafuatayo.Kwanza soma maandiko matakatifu mara kwa mara.Pili fanya Utafiti.Tatu Fanya Udadisi.Nne Fanya Ugunduzi.Ili kufanikisha mambo hayo makubwa na muhimu,nilazima uyaishi haya.1.Unahitaji kuwa na nidhamu.2.Unahitaji kutenga muda.3.Unahitaji utulivu wa hali ya juu.4.Unahitaji kuwa na mahali pako pa siri.Maneno hayo ambayo yamekolezwa wino,tuta yatayaona kwa undani zaidi ili kupata mbinu za kuyatafakari na kuyatafsiri vizuri na kuweka wazi ukweli kuhu,maandiko matakatifu.Kwa maana hii ndio njia na mbinu za kutafakari na kutafsiri vyema maandiko matakatifu. 1:SOMA MAANDIKO MATAKATIFU (BIBLIA) MARA KWA MARA 2Tim 3:16-17 Tunapo soma maandiko matakafifu ( Biblia) Maranyi tutajua ukweli wa neno la Mungu.na katika kuso huko tutapata kukutana na changamoto ya baadhi ya Matukio,Maneno,Hadidhi na Mithali Mafumbo na Maneno ya wenyehekima ambayo hatuwezi kuyafahamu kwa haraka.Na kufuatana na hayo itatubidi kuyatafakari ili kuyaweka katika hali ya ukweli na uwazi.Na kuna faida nyingi katika kusoma maandiko matakatifu mara kwa mara.Unaweza kujiuliza kwamba kwanini kuisoma biblia Neno la Mungu? Soma yafuatayo,na kwa undani zaidi soma somo liitwalo THEOLOJIA YA BIBLIA. Neno la Mungu ni ramani ya mkristo. Napenda kusema ni ramani kwasababu vyote nilivyovielezea hapo juu na zaidi vinapatikana kwenye Neno la Mungu. Biblia ni rmani kwa mkristo inaelezea dunia imeanzia wapi Kitabu cha Mwanzo mpaka dunia itaishia wapi (kitabu cha Kitabu cha Ufunuo wa Yesu Kwa Yohana,ni ramani inayotuonyesha jinsi tunavyotakiwa kuishi na vitu tunavyotakiwa kufanya, jinsi ya kumpendeza Mungu lakini pia jinsi wenzetu walivyomtafuta Mungu kabla ya kizazi chetu. Neno la Mungu linatupa nguvu na kutuondolea woga, tukumbuke kama Mungu alitamka tu Neno lake na dunia ikawa, si zaidi hili tunalolisoma kubadilisha maisha yetu kabisa?Kwa maana neno la Mungu ni hai tena lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili, linachoma kabisa na kutenganisha nafsi na roho, viungo vya mwili na mafuta yaliyomo ndani yake; na kutambua nia na mawazo ya mioyo ya watu- Waebrania 4:12). Neno la Mungu linatueleza Mungu ni nani, na tunapata kumjua kwa ukaribu sisi wenyewe kupitia maandiko, tena neno la Mungu linatutofautishia ukweli na uongo. Wakristo tusome neno la Mungu, linatusaidia sana katika dunia hii ya sasa ambapo vitu vingi vinatuchanganya sana. Kipindi cha Yesu wakati anajaribiwa na shetani, Yeye mwenyewe mwalimu wa kweli alituonyesha ni jinsi gani ya kumshinda shetani, ni kujawa neno la Mungu ndani yetu Luka 4:1-12, kwa namna hii alimshinda shetani kwa kumwambia imeandikwa- yaani imeandikwa katika Neno la Mungu. Mabinti wazuri wa Kristo tusome neno litubadilishe tabia,mienendo na kutufanya tumjue Mungu zaidi. Lakini pia Daudi katika Zaburi anasema “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi – Zaburi 119:11”. Vijana tujawe neno tushinde tamaa za ulimwengu ili tuwe chumvi na nuru katika huu ulimwengu, Vijana tujawe neno tutofautishwe kwalo ndani ya dunia hii na mahali popote Mungu allipotuweka. Biblia sio kitabu cha stori ni kitabu chenye maneno yenye nguvu ya kubadilisha fikra, uelewa, mwenendo lakini pia maisha yetu kwa ujumla. Vijana tusome Biblia tuijue kwa undani imani tunayoiamini ili tuweze kuielezea kwa wale walio karibu yetu na kujibu maswali ya imani tuliyonayo (1 Petro 3:15-Lakini mtukuzeni Kristo kama Bwana mioyoni mwenu. Muwe tayari kumjibu yeyote atakayewaulizeni juu ya matumaini yaliyo ndani yenu), napenda tuisome Biblia ili tuijue imani tuliyonayo na huyu Yesu lakini pia Nguvu zake kwa undani, tusiamini kwa sababu wazazi wanaamini, bali tuamini kwa ajili yetu na kwasababu tumesoma na kumjua Mungu kwa undani. Tunalo neno la Mungu kwasababu hii basi, tuyachunguze maandiko. Tujiangalie sana tusije tukawa tunajua maneno ya watumishi sana kuliko Neno la Mungu. Kwasababu naamini Mungu analiangalia Neno lake ili alitimize na si ya watu, sasa kama tumeshika maneno ya watu sana kuliko Neno lake hatupo sehemu nzuri kiroho. Kwa ufupi nielezee faida za kusoma neno la Mungu, Maisha yetu yanategemea neno la Mungu- Mathayo 4:4 “Lakini Yesu akamjibu, “Imeandikwa, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno analotamka Mungu”. Yesu alimjibu shetani hivi baada ya kujaribiwa kula mkate.Hii ni kweli kwasababu Neno la Mungu ndio inatupa maelekezo katika maisha, ndio linatupa kusudi katika maisha yetu, kwahiyo tusije tukadhani kuwa maisha yetu ni vyakula, la hasha maisha yetu ni Neno la Mungu ambalo linaimarisha hata kiRoho chetu. Mtu ni Roho, Nafsi na mwili, tusijetukaujenga mwili kwa mkate na kusahau kujenga Roho kwa Neno la Mungu na hivyo kushindwa kuishi kama Yesu alivyosema katika mstari huu. Kujua maisha ya Kristo na jinsi ya kuishi maisha yetu katika kumpendeza yeye: katika vitabu vya Mathayo,Marko,Luka naYohana tunaona jinsi gani Yesu aliishi maisha yake akiwa hapa duniani. Ili tuishi maisha ambayo yanampendeza Mungu ni vyema tukajua maisha ambayo Yesu aliishi lakini pia tukajua misingi ambayo aliisema kwa ajili ya wale wanaomfuata, tukajifunza mafundisho aliyoyatoa alipokuwa duniani ili kuyafanya hayo, Neno la Mungu limeelezea vizuri maisha ya Yesu lakini pia maisha ya mitume waliomfuata baada ya Yeye kumaliza kazi. Kupata tumaini la maisha: Neno la Mungu linatupa tumaini katika njia mbili Tunaposoma habari za watu waliotembea na Mungu na kuona jinsi Mungu alivyowashindia tunajifunza, tunakua katika imani lakini pia tunapata tumaini kwa yale tunayoyapita, tunaposoma habari ya Daniel katika tundu la simba na jinsi Mungu alivyomtunza akatoka mzima, tunapata tumaini katika jaribu au tatizo lolote tunalolipia kwa maana tunaamini kama alifanya kipindi kile hata sasa anaweza kufanya- Waebrania 13:8-“Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele”. Kwahiyo kama alifanya kipindi kile,atafanya na sasa kwa maana ni Yeye yule. Na hili linatupa tumaini ya maisha yetu hapa duniani. Tunapata tumaini ya mambo yajayo, tunaishi tukijua kwamba mwishoni tunashinda, tunajua kuhusu Mbingu mpya, tunaishi tukijua duniani sio kwetu, makazi yetu ya kudumu yapo kwa Baba, na anatuandalia makao, tukishashinda yote ya dunia tutaenda kuishi naye milele. Na shauri sana mabinti wenzangu tusome ufunuo ili tujue tunapoelekea baada ya mwisho wetu wa maisha ya hapa duniani kwani tuklijua hilo tutaish maisha haya kama maandalizi ya maisha yajayo, hatutaishi kama tumefika duniani ila tutaishi kama tunapita duniani. Kujua wapi tunaelekea na matukio ya siku za mwisho, nilikutana na mtu mmoja nilipokuwa sekondari ambapo tulikuwa tunaongelea kuhusu mambo ya kifo na imani. Aliniuliza nikifa naenda wapi na matukio ya siku za mwisho, nilipo muuliza yeye hili swali alinijibu akifa anabadilika na kuwa gesi na nyota kisha atakaa kwenye mawingu na kuangaza usiku kama nyota zinavyofanya kila siku. Nilishtuka sana kwasababu sijawahi jua kuwa kuna watu hawajui matukio ya siku za mwisho, lakini pia nilishtuka sana kwamba anadhani atakuwa nyota, Neno la Mungu linaelezea matukio ya siku za mwisho, mabinti tulisome tujue tunaelekea wapi. (kujua kuhusu siku za mwisho unaweza ukasoma kitabu cha Ufunuo kinaelezea mengi). Kujitambua sisi ni nani, kuna siku nilikuwa darasani na wanafunzi wenzangu na katika maongezi yetu tukawa tunaongelea Neno la Mungu, na ndipo nilipomwambia rafiki yangu ,”hivi unajua Mungu anampango na maisha yako”,nilimwambia maneno hayo wakati tunaongelea mipango ya maisha yetu kama vijana ambapo yeye aliongelea mengi sana aliyotaka kujifanyia kuhus maisha yake. Ndipo rafiki yangu alipopigwa na butwaa na kushangaa kwani maisha yake yotehakuwahi kujua Mungu anakusudi na maisha yake, na kwamba Mungu anamjua kwa jina lake. Mabinti wenzangu katika karne hii ambapo watu wamechanganyikiwa hadi kuhusu jinsia za walizozaliwa nazo, napenda tujitambue kupitia Neno la Mungu, napenda tujue sisi ni nani kwa Mungu. 1.Lakini ninyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani akawaingizeni katika mwanga wake mkuu”- 1 Petro 2:9 2.Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika” – Mathayo 5:14 3.Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, wale ambao wameitwa kufuatana na mapenzi yake. Mungu hufanya hivyo kwa faida yao. Wale ambao Mungu alikwisha kuwachagua tangu mwanzo, pia aliwateua wafanane na Mwanae, ili Mwana awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale ambao Mungu aliwateua tangu awali pia ali waita; na wale aliowaita pia aliwahesabia haki; na wale aliowahesabia haki aliwapa utukufu wake- Warumi 8:28-30 4.Basi, kwa vile sisi ni watoto wa Mungu, tutapokea baraka zote Mungu alizowawekea watu wake, na tutashiriki urithi huo pamoja na Kristo; maana, tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake.”- Warumi 8:17 5.Lakini katika mambo yote haya sisi ni washindi, naam, na zaidi ya washindi, tukiwa ndani yake yeye aliyetu penda”- Warumi 8:37. Na haya ni machache amabyo Neno la Mungu linatuambia kuhusu sisi, naomba usome zaidi ili ujitambue ndani ya Kristo wewe ni nani. Tukijitambua sisi ni nani, na ni wa thamani kiasi gani kwa Mungu hatutohangaika kama mabinti kutafuta thamani au kutaka kujijua sisi ni nani kwa wanaume, mavazi au vitu tulivyonavyo. Neno la Mungu linatuambia thamani yetu tuliyonayo kwa Kristo zaidi ya wanaume au hata vitu tunavyomiliki. Kuujua uongo wa dunia hii ila pia kuangalia kila kitu kupitia misingi ya Mungu, unajua dunia inapoelekea kuna vitu vingi vinapotoshwa na jinsi Mungu alivyoviumba. Yatupasa kusoma Neno la Mungu ili kuutenga ukweli na uongo kupitia Neno la Mungu ili tuishi kwa kumpendeza Mungu na sio kufuata mienendo inayoletwa na dunia. Biblia ina kila jibu la maswali yetu, Neno linasema hakuna jipya chini ya jua, kwa hivyo haya yote yalikuwepo na Neno la Mungu limegusia kila ishu na mambo yanayotokea duniani kwa mtazamo wa kiMungu. Tusome Neno tuujue mtazamo wake ili tumpendeze yeye katika maisha yetu. Kutambua chakula kipi cha kiroho kukila na kipi kukiacha, hapa sanasana naongelea walimu na manabii wa uongo, Neno linasema siku za mwisho hawa watakuwa wengi. Je kama mkikristo unauwezo wa kutofautisha mafundisho ya ukweli na ya uongo ukiyasikia? Je utajuaje haya ni ya uongo? Utayajua haya ni ya uongo kwa kuwa umejawa na Neno la kweli la Mungu ndipo utakapogundua kuwa Neno limepindishwa kwa ajili ya matumizi binafsi.Biblia inasema siku za mwisho watu watatumia Neno la Mungu kwa manufaa yao, utajuaje kama hapa limetumika tofauti na makusudi ya Mungu kama haujasoma Neno mwenyewe? Matendo ya Mitume 17:11-12 Watu wa Beroya walikuwa waungwana zaidi kuliko watu wa Thesalonike. Walisikiliza neno la Mungu kwa hamu wakachambua Maandiko kila siku ili waone kama waliyokuwa wakiam biwa na Paulo ni kweli. Wengi wao waliamini, ikiwa ni pamoja na wanawake maarufu wa Kigiriki na wanaume wengi” Tunaona watu waberoya wanasifiwa kwa kuyachunguza mafundisho, sio kwa kuwasikia wahubiri tu, la hasha bali kuwasikia na kwenda kuangalia kama waliyoambiwa yanafanana na kile Neno kinasema. Mabinti napenda tujue neno mpaka tufike kiwango cha kuchagua ya kuyasikia na yapi sio ya kuyasikia kuna walimu na manabii wauongo, tumejiandaaje katika kupambanua wa ukweli na wauongo? Lakini pia kulijua ili kuwahubiria mabinti wengine wanaotuzunguka na kuwatia moyo kupitia Neno la Mungu. Kupata majibu ya maswali yanayotuzunguka, mfano mzuri ni mimi na maisha yangu. Kuna mambo mengi ambayo yanatokea katika maisha na mazingira ambayo huwa nipo kwa hivyo huwa najiuliza mbele za Mungu kitu fulani anakichukuliaje, lakini nimekuja kujua kuwa hakuna kitu kipya chini ya jua hivyo majibu yote yapo kwenye Biblia, tukitaka kujua kuhusu swala fulani katika dunia tusome Neno linasemaje kuhusu hilo swala ili tumpendeze Mungu. Tungekuwa tunasoma neno kuna mambo mengi ambayo hayakutakiwa kuwa tunabishania makanisani au hata kwenye maisha kwasababu Neno liko wazi kuhusu hayo mambo. Kuna faida nyingi za kusoma Neno ambazo nitaziongezea kwenye sehemu ya pili, lakini kwa leo inatosha. Tusome neno, kwasababu ni njia moja wapo ambayo Mungu anaitumia kuzungumza nasisi. Tunataka kupata hekima ya kiMungu katika mambo na maisha yetu lakini pia hata maamuzi,Mungu yu tayari kuzungumza nasi kupitia Neno lake.Lakini pia ukiwa unaanza kusoma Neno la Mungu usisahau kusali na kumuomba Roho Mtakatifu akufundishe na kukuelekeza yale unayoyasoma. 2:FANYA UTAFITI WA MAMBO. UTAFITI. Kama somo letu lisemavyo likiwa na nia na lengo la kutupatia mbinu za kufanikisha kutafakari na kutafsiri kwa usahihi maandiko matakatifu ya Mungu.Ni vema kufanya utafiti kwa mambo yafuatayo.1.Mwandishi.2.Lugha 3.Lugha ya mafumbo na mithali,Mifano,Vitend Awili.4.Mazingira ya uandishi.5.Lini.6.Kwa nini.7,Kwa nani.8.Jinsi gani.Tuyafanyapo hayo tusomapo maandiko matakatifu,tutaijua kweli na iyokweli itatuweka huru wa kutafsiri maandiko kwa usahihi pasipo kuongeza wala kupunguza cho chote na lo lote.Kwa msaada zaidi kuhusu utafiti soma hapo chini.Usitafsiri cho chote na lo lote bila kulifanyia utafiti wa kutasha na wa kuruzisha na uluo sahihi.Mith 1:1-6, 2Tim 4:3. Utafiti kutoka kitenzi "kutafiti") hujumuisha kazi ya ubunifu ambayo hufanywa kwa misingi ya utaratibu ili kuongeza maarifa ya elimu, ikiwa ni pamoja na ujuzi wa wanadamu, utamaduni na jamii, na matumizi ya hisa hii ya ujuzi wa kuunda maombi mapya. Inatumika kuanzisha au kuthibitisha ukweli, kuthibitisha matokeo ya kazi ya awali, kutatua matatizo mapya au yaliyopo, msaada wa nadharia, au kuendeleza nadharia mpya. Mradi wa utafiti unaweza pia kuwa upanuzi wa kazi ya zamani katika shamba. Miradi ya utafiti inaweza kutumika kwa kuendeleza ujuzi zaidi juu ya mada, au kwa mfano wa mradi wa utafiti wa shule, inaweza kutumika kwa kuendelea utafiti wa mwanafunzi wa uwezo wa kuwaandaa kwa ajira au ripoti za baadaye. Ili kuthibitisha uhalali wa vyombo, taratibu, au majaribio, utafiti unaweza kuiga vipengele vya miradi ya awali au mradi kwa ujumla. Madhumuni ya msingi ya utafiti wa msingi (kinyume na utafiti uliotumika) ni nyaraka, ugunduzi, ufafanuzi, au utafiti na maendeleo (R & D) ya njia na mifumo ya maendeleo ya ujuzi wa binadamu. Mbinu za utafiti hutegemea epistemologies, ambazo hutofautiana sana ndani na kati ya wanadamu na sayansi. Kuna aina kadhaa za utafiti: kisayansi, wanadamu, kisanii, kiuchumi, kijamii, biashara, masoko, utafiti wa wataalamu, maisha, teknolojia n.k. Ufafanuzi[hariri | hariri chanzo] Utafiti umeelezwa kwa njia mbalimbali. Ufafanuzi mpana wa utafiti unatolewa na Godwin Colibao: "Katika maana pana zaidi ya neno, ufafanuzi wa utafiti unahusisha kukusanya mambo yoyote ya data, habari, na ukweli kwa ajili ya kuendeleza ujuzi."[1] Ufafanuzi mwingine wa utafiti unatolewa na John W. Creswell, ambaye anasema "ni mchakato wa hatua za kukusanya na kuchambua habari ili kuongeza uelewa wetu wa mada au suala". Inajumuisha hatua tatu: kuuliza swali, kukusanya data ili kujibu swali, na kutoa jibu la swali. wa Merriam-Webster Online unafafanua utafiti kwa undani zaidi kama " Utafsiri uchunguzi wa uchunguzi au uchunguzi, hasa uchunguzi au majaribio yenye lengo la ugunduzi na ufafanuzi wa ukweli, marekebisho ya nadharia zilizokubaliwa au sheria kulingana na ukweli mpya, au matumizi ya nadharia mpya au marekebisho mapya". Katika vyuo, wanafunzi wanafaa waandike tafiti kuhusu mada teule. Karatasi zao inafaa ziandikwe kwa kufuata kanuni za utafiti kama: kuanzia na mada nzuri, tumia teknolojia za kisasa, kufumbua na kutoa matokeo kwa njia sahihi. Aina za Utafiti Utafiti wa awali ni utafiti ambao si pekee unaozingatia muhtasari, mapitio au usanifu wa machapisho mapema kuhusu somo la utafiti. Nyenzo hii ni ya tabia ya msingi ya chanzo. Madhumuni ya utafiti wa mwanzo ni kuzalisha ujuzi mpya, badala ya kuwasilisha ujuzi uliopo katika fomu mpya (k.m., muhtasari au kutambulishwa). Utafiti wa awali unaweza kuchukua aina kadhaa, kulingana na fani inayohusika. Katika kazi ya majaribio, kwa kawaida inahusisha uchunguzi wa moja kwa moja wa somo la tafiti, kwa mfano, katika maabara au kwenye shamba, nyaraka njia, matokeo, na mahitimisho ya jaribio au seti ya majaribio, au hutoa tafsiri ya riwaya ya matokeo ya awali. Katika kazi ya uchunguzi, kuna kawaida baadhi ya mapya (kwa mfano) matokeo ya yaliyotolewa, au njia mpya ya kukabiliana na tatizo lililopo. Katika baadhi ya masomo ambayo hayafanyi majaribio au uchambuzi wa aina hii, uhalisi ni kwa namna fulani ya ufahamu uliopo tayari umebadilishwa au kutafsiriwa kulingana na matokeo ya kazi ya mtafiti. Kiwango cha asili ya utafiti ni kati ya vigezo muhimu vya makala zinazochapishwa katika majarida ya kitaaluma na kwa kawaida imara kwa njia ya mapitio ya rika. Wanafunzi wa masomo wanahitajika kufanya utafiti wa awali kama sehemu ya kutafakari Utafiti wa kisayansi. Ni njia ya utaratibu wa kukusanya data na kuunganisha udadisi. Utafiti huu hutoa maelezo ya kisayansi na nadharia kwa ufafanuzi wa asili na mali za dunia. Inafanya maombi ya vitendo iwezekanavyo. Utafiti wa kisayansi unafadhiliwa na mamlaka ya umma, na mashirika ya usaidizi na kwa makundi binafsi, ikiwa ni pamoja na makampuni mengi. Utafiti wa kisayansi unaweza kugawanywa katika ugawaji tofauti kulingana na taaluma zao za kitaaluma na maombi. Utafiti wa kisayansi ni kigezo kinachotumiwa sana kwa kuzingatia hali ya taasisi ya kitaaluma, lakini wengine wanasema kwamba vile ni tathmini isiyo sahihi ya taasisi, kwa sababu ubora wa utafiti hauelezei ubora wa mafundisho. Utafiti wanadamu unahusisha mbinu tofauti kama vile hermeneutics na semiotics. Wasomi wa wanadamu kwa kawaida hawataki jibu la mwisho kabisa kwa swali, lakini badala yake, tazama masuala na maelezo yaliyozunguka. Muda daima ni muhimu, na mazingira yanaweza kuwa ya kijamii, kihistoria, kisiasa, kitamaduni, au kikabila. Mfano wa utafiti katika wanadamu ni utafiti wa kihistoria, ambao unahusishwa na njia ya kihistoria. Wanahistoria hutumia vyanzo vya msingi na ushahidi mwingine ili kuchunguza kwa mada mada, na kisha kuandika historia kwa namna ya akaunti za zamani. Masomo mengine yanalenga kuchunguza tukio la tabia katika jamii na jamii, bila kuangalia kwa sababu au motisha za kuelezea haya. Masomo haya yanaweza kuwa ya ubora au kiasi, na inaweza kutumia mbinu mbalimbali, kama nadharia ya dhana au nadharia ya kike Utafiti wa kitaaluma, pia unaonekana kama 'utafiti wa msingi wa mazoezi', unaweza kuchukua fomu wakati kazi za ubunifu zinachukuliwa utafiti wote na kitu cha utafiti yenyewe. Ni mwili unaofaa wa mawazo ambayo hutoa njia mbadala ya kisayansi katika utafiti katika utafutaji wake wa ujuzi na ukweli. 3:FANYA UDADISI WA MAMBO Lengo la somo letu ni kutupa mbinu za kutafsiri vyema maandiko matakatifu.Hatuwezi kutafsiri vyema maandiko matakatifu tusipofanya tafakuri au kutafakari vyema maandiko matakatifu.Inahitaji mambo muhimu ya kuyaishi,ikiwemo kufanya udadisi wa mambo yenyewe.Kabla ya kuzama katika hili tuone maana ya udadisi kwa lugha nyepesi na kwa lugha ngumu yaani kwa undani zaidi. Dadisi ni neno litokanalo na kitenzi kudadisi likiwa na maana ya tendo la kupeleleza kwa kuuliza uliza na hata kwa njia nyingine. Tunapo hitaji kutafsiri maandiko matakatifu inatubidi kutafakari na kwa kufanya udadisi wa mambo kama,1.Nani mwandishi na mnenaji.2.Lugha yakuandilia.3.Lugha,iliyofichika,Mifano,MithaliVitendawili,Na Maneno ya wenyehekima ambayo hatuwezi kuyatolea tafsiri bila ya kuyafanyia Udadisi.4.Mazingira ya uandishi,Tamaduni,Mila na Desturi.5.Lini?.6.Kwa nani?7.Kwa nini?8.Jinsi.9.nidhamu ya matumizi ya sarufi ifuatwe.Nilikuwa,Nimekuwa,Nitakuwa nimekwishakuwa Nk. Gani. Udadisi kutoka neno la Kilatini curiositas yaani umakini ni tabia ya kuchunguza kitu au jambo kwa kina. Mara nyingi wanasayansi ndio wadadisi wazuri kwa maana wao huchunguza kwa kina na umakini, wakifuata kanuni na kutafuta ushahidi. Kwa njia yao udadisi umestawisha maisha ya binadamu Katika udadisi kuna ule wa kawaida na mwingine usio wa kawaida. Kwa udadisi wa kawaida mtu hudadisi kwa njia rahisi, tofauti na ule usio wa kawaida ambapo mtu asipokuwa makini anaweza hata kufa. Udadisi huu unahitaji kuwa makini sana. Udadisi unajitokeza mapema katika mtoto lakini unapozidi na kuelekea mambo yasiyo na maana kwa mfano umbeya unamzuia mtu asijue mambo ya maana; hapo ni kilema cha akili. Uchovu huponywa kwa udadisi. Udadisi hautaponya chochote. Udadisi ni hitaji la maarifa, inahusiana na seti nzuri ya mhemko, hisia na motisha, ambazo zinahusiana na kitambulisho na kutafuta uzoefu mpyas. Kupitia udadisi, uzoefu wa uzoefu mpya ambao unaleta changamoto unakuzwa. Udadisi wa tabia ni juu ya mwenendo wa jumla, udadisi wa serikali unahusiana na wakati fulani wa karibu. Katika moja utafiti wa Chuo Kikuu cha George Mason, kilichoendeshwa na Todd Kashdan na washirika wake, washiriki 90 (wanaume 45 na wanawake 45) waliulizwa ikiwa wanakubaliana na misemo kama "Kuwa na hamu ya kitu fulani, sio ngumu kwangu kukatiza. Pamoja na utafiti huu, ilihitimishwa kuwa watu wadadisi walikuwa na viwango vya juu vya kuridhika katika maisha yao, ili watu wenye viwango vya juu vya udadisi waonekane wanapata maana zaidi katika maisha yao na kwa hivyo wawe kamili zaidi, na pia wahusiane vizuri na watu. Kwa upande mwingine, wale walio na kiwango cha chini cha udadisi walipata kuridhika kutoka kwa raha za muda mfupi na shughuli walizofanya. Watu wenye hamu mara nyingi huzungukwa na shughuli mpya na vichocheo, ambavyo hulipwa kwa muda mrefu, kama wanashangaa kila wakati kwa kile kipya na hii inaleta kuridhika sana. Udadisi unajulikana kuathiri afya pia. Mnamo 1996, a kujifunza katika jarida la Saikolojia na kuzeeka, ambapo zaidi ya watu wazima 1,000 walishiriki, ambao walikuwa chini ya miaka 5 ya uchunguzi, Ilibainika kuwa wadadisi zaidi walikuwa na urefu wa wastani wa maisha, watu hawa walikuwa wakipenda kuishi kwa muda mrefu kuliko watu wasio na hamu sana. Katika uwanja wa mahusiano ya kijamii, watu walio na viwango vya juu vya udadisi kwa ujumla wana mafanikio makubwa, kwani wanaonyesha kupenda zaidi na uwazi katika kukutana na watu wapya na kujua jinsi ya kudumisha shauku hii kwa watu ambao tayari wanajulikana ambao wanataka kuendelea kukutana nao. zaidi. Pia ni rahisi kuhusishwa na watu wadadisi sana, kwani wanauliza maswali na wanavutiwa na mwingiliano na wengine. Faida nyingine ya kuwa na utu wa kudadisi ni maisha kamili na yenye furaha, wanafurahia uzoefu zaidi, wana uwezo mkubwa wa kufungua kwao na kushangaa kila wakati, pia wanahusiana vizuri na watu na hii inafanya iwe rahisi kwao kuwa na uhusiano wa karibu na kukutana na watu wapya. Yote hii inaimarisha ushawishi mzuri wa udadisi katika maisha yetu, kwani inakuza furaha. Udadisi unahusiana sana na mafanikio ya kitaaluma, ukielewa kama kiu cha kujifunza na maarifa mapya, udadisi unatuhamasisha kuongeza utamaduni wetu Kupitia data mpya, inasaidia kuongeza mafanikio ya kitaaluma. Watu wengine huwa na hamu ya udadisi kuliko wengine pia wanaielezea kwa njia tofauti. Udadisi ni kitu ambacho kinaweza kukuzwa, ambayo ni kwamba, hisia zetu za asili za udadisi zinaweza kutekelezwa. Kuongeza udadisi kunategemea motisha yetu, Ni muhimu kutafuta zaidi juu ya mada ambazo zinaamsha shauku yetu na kukuza sisi wenyewe, ili kuongeza athari kwa changamoto mpya na uzoefu ambao hututajirisha zaidi. Ili kuongeza udadisi wetu, ni muhimu kupoteza hofu ya kutokuwa na uhakika na isiyojulikana. Itakuwa busara kujaribu kujifunza kufurahiya kutokuwa na uhakika, Inaonekana kuwa ngumu, kwa sababu inazalisha kiasilia wasiwasi na ukweli unatufanya tuhisi kuwa tutakuwa salama zaidi na raha. Tunaweza kujizoeza kupoteza hofu yetu ya kutokuwa na uhakika ikiwa kila wakati tutajiweka wazi kwa shughuli mpya ambazo zinaleta changamoto kidogo kwetu pia.kuhisi mshangao na msisimko kutatufanya tujisikie kutuzwa na kugundua kuwa hakuna cha kuogopa kwa haijulikani. Hatupaswi kuruhusu ubaguzi wetu kutuzuia, shughuli nyingine ya kupendeza ili kukuza udadisi, ni kupata haijulikani katika inayojulikana, kwa kuwa inafanya kazi kusahau juu ya matarajio, hukumu, dhana na maoni ya kujiruhusu tushangae tena. Kumbuka kwamba wakati tulikuwa watoto, maumbile yetu yalituhimiza tuwe na hamu ya kuuliza, kuuliza maswali ya kila aina, kutaka kunusa, kugusa, kusikia na kuona kila kitu, tulitaka akili zetu zichunguze mazingira yetu, kiu yetu ya kujifunza ilionekana kutoshiba . Tunapokua tunapoteza udadisi huu pole pole, kwa sababu tunazoea vitu vingi ndivyo tunavyovipata zaidi, lakini itakuwa ya kupendeza ikiwa tunajaribu kurudisha uwezo wetu wa kushangaza, bila kuruhusu maisha ya kawaida ya watu wazima na ya kawaida kuangamiza uwezo wetu wa kushangaa na kuwa mdadisi, Yaliyomo kwenye kifungu hicho yanazingatia kanuni zetu za maadili ya uhariri. Kuripoti kosa bonyeza hapa. Njia kamili ya kifungu: Rasilimali za kujisaidia » Rasilimali » Uzoefu » Udadisi ni nini, jinsi ya kuiongeza na faida zake ni nini? 4:GUNDUA MAMBO. Hatua hii ya mtu kifikia kiwango cha kugundua mambo mapya na ambaya hayakujulikana wa kufahamika,ni hatua nzuri na muhumi sana kuonyesha kwamba wewe ni Mtu wa kutafakari na mtafiti na mdadisi wa mambo,na msomaji mzuri wa maandiko matakatifu.Kwa kuwa hauwezi kugundua mambo madogo na makubwa yaliofichika yasiofahamika wala kujulikana pasipokuwa na ufatiliaji wa kanuni za mbinu za kutafakari na kutafsiri maandiko matakatifu. Utakapokuwa unasoma maandiko matakatifu mara kwa mara lazima utakutana na changamoto ya kutukuelewa na kufahamu na kujua baadhi ya mambo na matukio na maneno,muhimu na yanayofaa kuyafahamu.Kwa sababu ya wasomi wa mambo ya Biblia waliyokuwa kabla yetu,waligundua mambo mengi na yanatusaidia kuielewa biblia kwa kizazi chetu.Ikiwemo 1.Elimu kuu za Biblia.2.Hadidhi za Biblia.Na kuweka vitabu vya Biblia katika makundi yenye majina kwa kutupatia wepesi wa kuisoma na kuielewa biblia kwa njia rahisi. Unaposoma Biblia kabla ya kutafsiri cho chote unachohitaji kufahamu,nivizuri kugundua vitu kama 1.Mwandishi na msemaji.2.Lugha ya asili 3.Lugha iliyofichika kama Mifano,Mithali,Viten dawili,na Mafumbo ya maneno ya wenye hekima.Mith 1:5-6/4.Mazingira 6 Lini.Kwa nani 7.Kwa nini.8.Jinsigani. Pamoja na hayo nivema kuwa makini kwa kuheshimu Lugha ya Sarufi,kama,1.Nilikuwa 2.Nimekuwa.3.Nitakuwa.3.Nilikuwa nimekwashakuwa,4.Nimekwishakuwa.Nitakuwa nimekwishakuwa.Nk.Hayo yote yatatufanya kuwa watumishi wanao tafsiri maandika matakatifu kwa usahihi.Ona baadhi ya mambo yaliogunduliwa kuhusu mambo ya kale. Form Je, Elimu ya Vitu vya Kale Inaunga Mkono Biblia? ELIMU ya vitu vya kale ni muhimu kwa wanafunzi wa Biblia kwani vitu hivyo vinavyochimbuliwa huunga mkono ujuzi wao kuhusu hali za maisha, utamaduni, na lugha za nyakati za Biblia. Pia vitu hivyo vya kale hutoa habari muhimu kuhusu utimizo wa unabii wa Biblia kama ule uliotabiri kuhusu kuanguka kwa Babiloni, Ninawi, na Tiro. (Yeremia 51:37; Ezekieli 26:4, 12; Sefania 2:13-15) Hata hivyo, elimu hiyo inapungukiwa kwa njia fulani. Vitu vilivyochimbuliwa ni lazima vifafanuliwe, na nyakati nyingine ufafanuzi huo huwa na kasoro au hupotoshwa. Imani ya Kikristo haitegemei vigae, matofali ya zamani, au kuta zilizoanguka, lakini inategemea ukweli wote wa kiroho unaopatikana katika Biblia. (2 Wakorintho 5:7; Waebrania 11:1) Kwa hakika, upatano wa Biblia, unyoofu wa waandikaji, unabii uliotimizwa, na mambo mengine mengi hutoa uthibitisho wenye kusadikisha kwamba “Andiko lote limeongozwa na roho ya Mungu.” (2 Timotheo 3:16) Fikiria ugunduzi fulani wenye kupendeza ambao unaunga mkono masimulizi ya Biblia. Kikundi cha wataalamu wa vitu vya kale kilipokuwa kikichimba huko Yerusalemu mnamo 1970, kilipata magofu ya nyumba iliyoteketea. Nahman Avigad, kiongozi wa kikundi hicho aliandika hivi: “Kwa mtu mwenye uzoefu jambo hilo lilikuwa wazi. Jengo hilo liliharibiwa kwa moto na kuta na dari zikaporomoka.” Katika chumba kimoja kulikuwa na mifupa [1] ya mkono, vidole vyake vikiwa vimenyooshwa vikijaribu kufikia ngazi. Kwenye sakafu kulikuwa na sarafu [2] zilizotapakaa, ya karibuni zaidi ikiwa ya mwaka wa nne wa maasi ya Wayahudi dhidi ya Roma, yaani, mwaka wa 69 W.K. Vitu vilikuwa vimeanguka kabla ya jengo hilo kuporomoka. Avigad anasema: “Tulipoona hilo tulikumbuka ufafanuzi wa Yosefo kuhusu askari Waroma ambao walipora nyumba baada ya jiji hilo kushindwa.” Wanahistoria wanasema kwamba uharibifu na uporaji wa Waroma ulitukia mnamo 70 W.K. Uchunguzi ulionyesha kwamba mifupa hiyo ilikuwa ya mwanamke mwenye umri wa miaka 20 hivi. Gazeti Biblical Archaeology Review linasema: “Mwanamke ambaye alikuwa jikoni katika Nyumba Iliyoteketea alianguka chini na kufa alipokuwa akijaribu kufikia ngazi karibu na mlango. Moto ulienea haraka sana . . . hivi kwamba hangeweza kuponyoka na akazikwa na mabaki ya nyumba hiyo yaliyokuwa yakiporomoka.” Mandhari hiyo inatukumbusha unabii wa Yesu kuhusu Yerusalemu uliokuwa umetolewa miaka 40 hivi mapema: “Adui zako . . . watakuangusha chini wewe na watoto wako walio ndani yako, nao hawataacha jiwe juu ya jiwe ndani yako.”—Luka 19:43, 44. Ugunduzi wa vitu vya kale unaounga mkono Biblia pia unatia ndani majina ya watu wanaotajwa katika Maandiko. Baadhi ya ugunduzi huo ulimaliza madai ya mapema ya wachambuzi kwamba waandishi wa Biblia walibuni watu fulani au walitilia chumvi umaarufu wao. Maandishi Yenye Majina ya Biblia Kuna wakati ambapo wasomi maarufu walifikiri kwamba Mfalme Sargoni wa Pili wa Ashuru, ambaye jina lake linapatikana katika Biblia kwenye Isaya 20:1, hakuwahi kuishi. Hata hivyo, mnamo 1843 karibu na mji wa leo wa Khorsabad, Iraki, kwenye kijito cha Mto Tigri, jumba la Mfalme Sargoni [3] liligunduliwa. Lilijengwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 25. Sasa, Sargoni wa Pili ni kati ya wafalme wa Ashuru wanaojulikana zaidi. Katika maandishi [4] yake, anadai kwamba aliteka jiji la Samaria. Kulingana na Biblia, Waashuru walilishinda jiji la Samaria mnamo 740 K.W.K. Sargoni pia alirekodi kwamba alishinda Ashdodi, na hivyo kuunga mkono Isaya 20:1. Walipokuwa wakichimbua magofu ya jiji la kale la Babiloni, katika Iraki ya leo, wataalamu wa vitu vya kale waligundua mabamba 300 hivi karibu na Lango la Ishtar. Yakiwa yanahusianishwa na kipindi cha mtawala wa Babiloni, Mfalme Nebukadneza, maandishi hayo yanatia ndani orodha ya majina. Miongoni mwa majina hayo kuna jina “Yaukini, mfalme wa nchi ya Yahud.” Jina hilo linamrejelea Mfalme Yehoyakini wa Yuda aliyetekwa kutoka Babiloni wakati Nebukadneza aliposhinda Yerusalemu mara ya kwanza mnamo 617 K.W.K. (2 Wafalme 24:11-15) Wana watano wa Yehoyakini pia wanatajwa katika maandishi hayo.—1 Nyakati 3:17, 18. Mnamo 2005, wataalamu wa vitu vya kale walipokuwa wakichimbua eneo ambapo walitarajia kupata jumba la Mfalme Daudi, walipata jengo kubwa la mawe ambalo walifikiri liliharibiwa Wababiloni walipoteketeza Yerusalemu zaidi ya miaka 2,600 iliyopita, katika siku za nabii wa Mungu Yeremia. Hakuna uhakika kwamba jengo hilo ni mabaki ya jumba la Mfalme Daudi. Hata hivyo, mtaalamu wa vitu vya kale Eliat Mazar aligundua kitu kimoja chenye kupendeza chenye upana wa sentimita 1, yaani, muhuri wa udongo [5] wenye maandishi yaliyosema: “Wa Yehukali mwana wa Shelemiyahu mwana wa Shovi.” Yaonekana hayo ni maandishi ya muhuri wa Yehukali (pia Yukali), ofisa Myahudi anayetajwa katika Biblia ambaye alikuwa mpinzani wa Yeremia.—Yeremia 37:3; 38:1-6. Mazar anasema kwamba Yehukali ndiye “waziri wa pili wa mfalme,” baada ya Gemaria, mwana wa Shafani, ambaye jina lake liko kwenye muhuri uliopatikana katika Jiji la Daudi. Biblia inamtambulisha Yehukali, mwana wa Shelemia (Shelemiyahu), kuwa mkuu wa Yuda. Kabla ya ugunduzi huo, hakutajwa mahali pengine popote nje ya Maandiko. Je, Waliweza Kusoma na Kuandika? Biblia inaonyesha kwamba Waisraeli wa kale walijua kusoma na kuandika. (Hesabu 5:23; Yoshua 24:26; Isaya 10:19) Wachambuzi hawakukubali jambo hilo, wakisema kwamba historia ya Biblia hasa ilipitishwa kwa mdomo kwa njia isiyoweza kutegemeka. Lakini mnamo 2005, wataalamu wa vitu vya kale waliofanya kazi Tel Zayit, eneo lililo kati ya Yerusalemu na Mediterania, walipata herufi za Kiebrania [6] za zamani zaidi kuwahi kugunduliwa, herufi hizo zilikuwa zimeandikwa kwa kuchongwa kwenye mwamba wa chokaa. Wasomi fulani wanasema kwamba mwamba huo, unaosemekana kuwa wa karne ya kumi K.W.K., unadokeza “mafunzo ya uandishi,” “utamaduni wa hali ya juu,” na “usimamizi wa Kiisraeli uliokuwa ukisitawi huko Yerusalemu.” Tofauti kabisa na madai ya wachambuzi, inaonekana kwamba kufikia angalau mapema katika karne ya kumi K.W.K., Waisraeli waliweza kusoma na kuandika na hivyo wangeweza kurekodi historia yao. Rekodi za Waashuru Zinatoa Uthibitisho Zaidi Ashuru, ambayo wakati fulani ilikuwa milki yenye nguvu, hutajwa mara nyingi katika Biblia, na ugunduzi mwingi wa vitu vya kale katika eneo hilo hutoa ushuhuda kuhusu usahihi wa Maandiko. Kwa mfano, uchimbuzi katika eneo ambalo Ninawi, jiji kuu la Ashuru, lilikuwa ulifunua jiwe lililochongwa [7] katika jumba la Mfalme Senakeribu, lililoonyesha askari Waashuru wakiwapeleka mateka Wayahudi uhamishoni baada ya kuanguka kwa jiji la Lakishi mnamo 732 K.W.K. Unaweza kusoma simulizi hilo la Biblia kwenye 2 Wafalme 18:13-15. Maandishi ya kihistoria ya Senakeribu [8], yaliyopatikana huko Ninawi, yanafafanua kampeni yake ya kijeshi wakati wa utawala wa Mfalme Hezekia wa Yuda, ambaye maandishi hayo yanamtaja kwa jina. Rekodi zinazopatikana katika mabamba ya wafalme wengine zinawataja Wafalme Ahazi na Manase wa Yuda, na pia Wafalme Omri, Yehu, Yehoashi, Menahemu, na Hoshea wa Israeli. Katika masimulizi yake, Senakeribu anajisifu kuhusu mafanikio yake ya kijeshi lakini jambo la kutokeza ni kwamba hataji kwamba alishinda Yerusalemu. Kukosa kutaja jambo hilo kunathibitisha ukweli wa rekodi ya Biblia, ambayo husema kwamba mfalme huyo hakuwahi kuzingira Yerusalemu lakini alishindwa na Mungu mwenyewe. Baada ya hapo, Senakeribu aliyeaibishwa alirudi Ninawi, ambako aliuawa na wanawe. (Isaya 37:33-38) Kwa kupendeza, rekodi mbili za maandishi ya Waashuru zinatoa ushuhuda wa kuuawa kwake. Kwa sababu ya uovu wa watu wa Ninawi, manabii wa Yehova, Nahumu na Sefania, walitabiri kuharibiwa kabisa kwa jiji hilo. (Nahumu 1:1; 2:8–3:19; Sefania 2:13-15) Unabii wao ulitimizwa wakati ambapo majeshi yaliyoungana ya Nabopolasa, mfalme wa Babiloni, na ya Siaksaresi Mmedi yalizingira na kuteka Ninawi mnamo 632 K.W.K. Ugunduzi na uchimbuzi wa magofu yake unathibitisha tena ukweli wa masimulizi ya Biblia. Kati ya mwaka wa 1925 na 1931, vitu vingi vya kale, kutia ndani mabamba ya udongo 20,000 hivi, vilichimbuliwa huko Nuzi, jiji la kale lililo upande wa mashariki wa Mto Tigri na kusini-mashariki ya Ninawi. Mabamba hayo ambayo yaliandikwa kwa lugha ya Kibabiloni, yana mambo mengi sana yanayohusu desturi za kisheria zinazofanana na zile za nyakati za mababu wa ukoo wa kale zinazofafanuliwa katika kitabu cha Mwanzo. Kwa mfano, maandishi yanaonyesha kwamba miungu ya familia, ambayo mara nyingi ilikuwa sanamu ndogo za udongo, ilionekana kuwa kama hati ya kumiliki ardhi, na mwenye sanamu hizo angeweza kudai urithi. Huenda desturi hiyo ikaeleza kwa nini Raheli mke wa Yakobo alichukua miungu ya familia, au “terafimu,” zilizokuwa za baba yake, Labani, wakati familia ya Yakobo ilipohama. Inaeleweka kwa nini basi Labani alijitahidi sana kupata terafimu zake tena.—Mwanzo 31:14-16, 19, 25-35. Unabii wa Isaya na Maandishi ya Koreshi Maandishi ya kale yaliyo katika bamba la udongo lililoonyeshwa hapa yanaunga mkono simulizi lingine la Biblia. Maandishi hayo yanayoitwa Cyrus Cylinder [9], yalipatikana katika eneo la Sipari ya kale kwenye Mto Efrati, kilomita 32 kutoka Baghdad. Yanataja jinsi Koreshi Mkuu, mwanzilishi wa Milki ya Uajemi, alivyoshinda Babiloni. Kwa kupendeza, miaka 200 hivi mapema, Yehova alikuwa amesema hivi kupitia nabii Isaya kuhusu mtawala wa Umedi na Uajemi ambaye angeitwa Koreshi: “‘Yeye ni mchungaji wangu, naye atatenda kikamilifu mapendezi yangu yote’; neno langu kuhusu Yerusalemu, ‘Atajengwa upya.’”—Isaya 13:1, 17-19; 44:26–45:3. Jambo lenye kutokeza ni kwamba maandishi hayo yanataja sera ya Koreshi, iliyotofautiana na ile ya washindi wengi wa kale. Koreshi aliwaruhusu watu waliokuwa wametekwa na utawala uliomtangulia warudi kwao. Historia inayopatikana katika Biblia na kutoka katika vyanzo vingine inathibitisha kwamba Koreshi aliwaruhusu Wayahudi warudi kwao, nao wakajenga upya Yerusalemu.—2 Mambo ya Nyakati 36:23; Ezra 1:1-4. Ingawa elimu ya vitu vya kale vinavyohusiana na Biblia ni ya karibuni sana, imeibuka kuwa nyanja kubwa ya uchunguzi ambayo imetokeza habari muhimu. Na kama tulivyoona, ugunduzi mwingi unathibitisha usahihi wa Biblia, nyakati nyingine hata katika mambo madogo sana. Sargoni wa Pili, Mfalme wa Ashuru anayetajwa katika Isaya 20:1 Makala iliyochapishwa katika gazeti la Biblical Archaeology Review, ilisema kwamba kuwapo kwa watu “50 hivi” wanaotajwa katika Maandiko ya Kiebrania, kunaweza sasa kuthibitishwa na ugunduzi uliofanywa na wachimbuzi wa vitu vya kale. Watu hao hutia ndani wafalme 14 wa Yuda na Israeli kama Daudi na Hezekia, na wengine wasiojulikana sana kama vile Menahemu na Peka. Orodha hiyo inataja pia Mafarao 5 na wafalme 19 wa Ashuru, Babilonia, Moabu, Uajemi, na Siria. Hata hivyo, si watawala tu wanaotajwa katika Biblia na maandishi ya wachimbuzi wa vitu vya kale. Wengine wanaotajwa wanatia ndani watu waliokuwa na vyeo vya kadiri kama vile makuhani wakuu, mwandishi, na maofisa kadhaa. Makala hiyo inasema kwamba “kuna uthibitisho mkubwa unaokubaliwa na wasomi” unaotambulisha waziwazi watu hao waliotajwa. Ni kweli kwamba Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo yanarejelea watu wengi wanaotajwa katika historia, na uthibitisho wa wachimbuzi wa vitu vya kale unaounga mkono kuwapo kwa baadhi yao kama vile Herode, Pontio Pilato, Tiberio, Kayafa, na Sergio Paulo. Simba walioishi katika nchi zinazotajwa katika Biblia walianza kutoweka pindi gani? Michoro iliyokuwa katika kuta za matofali yenye kung’aa katika Babiloni la kale Ingawa hakuna simba katika maeneo yenye msitu ya Nchi Takatifu leo, maandiko yanarejelea mnyama huyo mara 150 hivi, kuonyesha kwamba waandishi wa Biblia walimjua mnyama huyo. Marejeo mengi yanatumia lugha ya mfano, hata hivyo baadhi ya masimulizi yanataja kuhusu mapambano pamoja na simba. Kwa mfano, Samsoni, Daudi, na Benaya wanasifiwa kwa sababu ya kuua simba. (Waamuzi 14:5, 6; 1 Samweli 17:34, 35; 2 Samweli 23:20) Watu wengine wanatajwa kwamba waliuawa na simba.—1 Wafalme 13:24; 2 Wafalme 17:25. Katika nyakati za kale, simba wa Asia (Panthera leo persica) walipatikana Asia Ndogo na Ugiriki mpaka Palestina, Siria, Mesopotamia, na kaskazini-magharibi mwa India. Wanyama hao waliheshimiwa na kuogopwa sana, na mara nyingi walionekana katika michoro ya sanaa za kale za Mashariki. Michongo ya picha za simba iliyokuwa katika kuta za matofali yenye kung’aa ilipamba Njia ya Maandamano ya Babiloni la kale. Kufikia mwishoni mwa karne ya 12 W.K., inasemekana kwamba wapiganaji wa vita vitakatifu waliendelea kuwinda simba huko Palestina. Inaonekana kwamba simba walianza kutoweka katika eneo hilo muda mfupi baada ya mwaka wa 1300. Hata hivyo, inasemekana kwamba baadhi ya simba walipatikana Mesopotamia na Siria kufikia karne ya 19, pia Iran na Iraki kufikia katikati ya karne ya 20. ILIKUFANIKISHA MAMBO HAYO NNE MUHIMU,ZINGATIA HAYA. 1.UNAHITAJI NIDHAMU Maana Ya Nidhamu Nidhamu ina maana ya utaratibu nzuri wa kuendesha jambo,Adabu adabu ni tabia njema ni ndhamu Heshima,Staha.Staha ni heshima inayoambatana na haya au aibu ya kutenda jambo lisilo zuri mbele ya watu wengine. Staha ni Hadhi.Hadhi ni cheo ni daraja ni dhima na ni utukufu. Kinachotofautisha mtu huyu na Yule ni nidhamu yao katika kuishi kwao. Nidhamu ni ile hali ya mtu kuwa makini katika kufuata uongozi sahihi au kanuni sahihi ili kufikia malengo yaliyotarajiwa. Na nidhamu ya ndani ni ile nguvu ya ndani ya mtu ambayo imejengeka, imeimarika kiasi cha kufanya mambo katika ufanisi na ujuzi wa hali ya juu yaani kufanya kitu sahihi, wakati sahihi na mahali sahihi ili kufikia kusudi sahihi. Ni wazi ya kwamba watu tumekuwa tukitafuta matokeo mazuri kiafya, kimasomo, kikazi, kifamilia, kibiashara, kijamii yaani kimaisha kwa ujumla lakini imekuwa ni kazi nzito, ngumu, kufikia malengo hayo. Jiulize je, ninafuata kanuni sahihi na kwa umakini? kwani mipango tu na juhudi nyingi hazitoshi kuleta matokeo mazuri. Kunahitajika kitu cha muhimu kinachofuatwa mara kwa mara ili kurahisisha ufikiaji wa lengo hilo, kitu hicho ni nidhamu. Pia nidhamu tunaweza kulinganisha na egemeo katika kurahisisha utendaji wa kazi yaani katika nyenzo. Udhihirisho Wa Nidhamu. Udhihirisho ni kuwa neno litokanalo na tondo la kufanya jambo kufahamika kwa kila mtu au kwa kila mahali.Ni kufanya jambo kujulikana ni kubainisha.Na kinacho dhihirisha kwamba Mcha Mungu,Mkristo,Mtumishi,Kiongozi ananidhamu ni Utii.Kuwa mti au mtiifu ni kuishi kwa kufanya sahihi na kwa wakati yaliyoamriwa.Utii ndio uweka wazi utii wandani 2.UNAHITAJI MUDA Maana Ya Muda. Muda ni kipindi maalumu baina ya saa,siku,miaka..nk.Wakati ni Muda Majira. Nidhamu Ya Muda Katika Utumishi Wa Kiroho Huyu kwa kweli ndiye adui mkubwa ambaye anazuia mafanikio makubwa ya watu wengi, kwani ana uwezo wa kupoteza, kuharibu na hata kufanya mipango ya mtu isitimie. Kusipokuwa na umakini katika kutumia muda, yaani kuwa mahali sahihi, ukifanya kitu sahihi kwa wakati sahihi lazima kunakuwa na upungufu katika kupata matokeo yaliyokusudiwa. Kama maandiko matakatifu yanavyo sema katika kitabu cha Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.” Kwa hiyo tangu mbingu na nchi ziumbwe, mwanadamu aliumbwa ili afanye mambo yake yote kwa kufuata utaratibu. Mtume Paulo aliwaonya waefeso kuhusu kuutunza muda alisema “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; Mkiukomboa wakati kwa maana nyakati hizi ni za uovu” Waefeso 5:15-16 Na pia kuna usemi wa kiingereza usemao “you can choose to be the manager of time or the servant of time” it is your choice, ikimaanisha ya kwamba ni wewe tu mwenye maamuzi ya kutumia muda kwa kuuongoza (ukawa meneja) au ukaongozwa na muda (ukawa mtumwa). Hivyo ni vema kupata moyo wa hekima katika kuyafanyia kazi mafundisho haya nawe utakuwa mwenye hekima. Weka nidhamu ya hali ya juu katika kutumia muda wako. Maisha ya ulimwengu hayawezi kutengwa na wakati.Wakati mi sehemu ya utaratibu wa uumbaji wa Mngu.Mwanzo 1:14,Ebr 1:2,Kinyume chake Mungu yeye ni wamilele na muumbaji wa vitu vyote wala hana kikomo cho chote kuhusu wakati.Maana yake ni kwamba Yeye anaona wakati kwa namna tofauti kuliko wanadamu.Isaya 57:15,1Tim 1:17,6:16.2Petr 3:8 Jinsi Ya Kupangilia Na Kutumia Muda Wako Vizuri: Mambo 7 Muhimu Ya Kuzingatia.. Bila shaka umeshawahi kusikia msemo wa wenzetu wa magharibi usemao “Time is Money”. Yawezekana kwamba msemo huo,kwa tafsiri ya moja kwa moja, unamaanisha kwamba muda ni pesa. Lakini ninavyoelewa mimi msemo huo unaongelea au unajaribu tu kuonyesha jinsi gani muda ni kitu cha thamani! Jinsi unavyoutumia muda wako hivi leo ni ishara tosha ya jinsi kesho yako itakavyokuwa.a Kwa upande mwingine umeshawahi kusikia mtu au watu fulani fulani wakilalamika kwamba “hawana muda” wa kufanya kitu fulani. Sababu itolewayo mara nyingi ni kwamba wapo “bize”. Wapo ‘bize” na ndio maana hawana muda wa kujitolea katika shughuli mbalimbali za kijamii.Ndio maana hawana muda wa kikao cha harusi cha rafiki,ndugu au jamaa.Hawana muda wa kuhudhuria msiba wa mtu. Wapo “bize” na ndio maana hawakuweza kukupigia simu nk. Sasa inakuwaje mtu mmoja awe na muda na wakati huo huo mtu mwingine asiwe kabisa na muda wakati sote tunaishi kwenye dunia moja na siku ina masaa yale yale 24? Sababu zinaweza kuwa nyingi. Zingine zinaweza kuwa ni za visingizio tu.Zingine zinaweza kuwa za kweli na za uhakika. Pamoja na hayo, jinsi unavyotumia muda wako, jinsi unavyopangilia mambo yako, ratiba zako nk, ni sababu ya kutosha kama una muda wa ziada wa kufanya mambo mengine mengi uyapendayo ikiwemo mapumziko, muda wa kukaa na wanafamilia yako, kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni na lolote lile ambalo unapenda kulifanya lakini umekuwa hulifanyi kwa sababu au kisingizio cha ukosefu wa muda. Leo tutaangalia baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyafanya ili kuokoa muda ili kujipatia muda unaohitaji kwa sababu ambazo nimezitaja hapo juu; 1. Anza siku yako mapema: Hili ni la msingi sana.Amka mapema. Ukiianza siku yako mapema, sio tu kwamba kuna faida za kiafya kama ambavyo tutakuja kuziongelea katika siku za mbeleni, bali unakuwa na muda wa ziada wa kuiandaa ratiba kamili ya siku yako. Kwa ujumla binadamu anatakiwa kulala kwa muda wa masaa nane. Siri ya kuamka mapema inaanza na kwenda kulala katika muda unaofaa ili upate hayo masaa manane. Kumbuka siku njema huonekana asubuhi.Ipe siku yako mwanzo mzuri.Lala kwa mnda ufaao ili kuandaa siku yako anayofuata kuwa siku njema.Mwanzo 1:3-5 2. Orodhesha mambo unayotaka kufanya: Ushasikia msemo usemao; Mali bila daftari hupotea bila kujua. Hali ni hiyo hiyo hata katika suala zima la muda. Unapoianza siku hakikisha umeorodhesha mahali kwenye kikaratasi au kidaftari chako cha kumbukumbu mambo yote ambayo umedhamiria kuyafanya katika siku inayokukabili.Katika zama hizi za sayansi na tekinolojia,simu nyingi za viganjani zina huduma ya kalenda ambayo unaweza kuitumia kuorodhesha mambo unayotaka kufanya kesho,mwezi ujao au hata mwakani.Zitumie.Andika pia na muda ambao ni lazima utimize mambo hayo. Faida za kuorodhesha mambo unayotaka kufanya ni kwamba kwanza orodha hiyo itakuwa inakusuta. Itakuwa inakuuliza,ulisema leo utafanya hivi imekuwaje? Pili orodha hiyo hiyo itakupa pia nguvu au ari ya kutimiza malengo yako. Tatu na muhimu zaidi kama mada yetu ya leo inavyodai, utaokoa muda. Utafanya kila jambo kutokana na muda uliojipangia kwani orodha itakuwa inakuonyesha kwamba siku bado haijaisha na mengine yanakungoja. Pia wakati unaandika orodha yako, kumbuka kuweka pamoja mambo ambayo yanaweza kufanyika kwa pamoja au katika muda huo huo.Kwa mfano, leo umepanga kwenda katika benki fulani kuomba mkopo wa biashara.Wakati huo huo umepanga kwenda kwa chakula cha mchana na rafiki yako anayefanya kazi katika benki hiyo hiyo. Hayo unaweza kuyatimiza kwa pamoja. Unaweza kumuona meneja wa mikopo wa benki na kisha baada ya kumaliza ukaenda na rafiki yako kupata chakula. Hakikisha tu kwamba rafiki yako sio huyo huyo tena ndio meneja wa mikopo.Hapo kutakuwa na harufu ya ufisadi.Unajua tena jinsi mambo yalivyo nchini mwetu hivi sasa.Kuwa makini.Mwanzo 1:1-30 3.Weka kipaumbele: Hili linaendana moja kwa moja na hilo hapo juu. Unapoandika orodha yako, weka kipaumbele katika mambo ambayo ni muhimu zaidi.Hayo yaweke juu kabisa katika orodha yako Kipaumbele kinaweza kutokana na umuhimu wako binafsi kwa jambo fulani, muda nk,Mwanzo 1:1-25. 4. Jifunze kutoahirisha mambo: Mara nyingi huwa tunakamatwa na uvivu na kusema hili nitalifanya kesho au keshokutwa.Tunasema linaweza kusubiri. Ukweli ni kwamba ni kweli jambo hilo litasubiri. Cha msingi kukumbuka ni kwamba jambo hilo litaendelea kukusubiri mpaka hapo utakapoamua kulifanya! Haliendi popote.Ushauri wangu ni kwamba ule ambao hata wazee wetu walipenda kutukumbusha,Linalowezekana Leo Lisingoje Kesho.Unapoahirisha kutimiza jambo fulani kumbuka kwamba unazidi tu kuongeza mambo katika orodha yako ya kesho au keshokutwa. Huo ndio mwanzo wa kuchanganyikiwa, kukosa kabisa muda wa kufanya yale uyapendayo zaidi maishani zaidi ya kazi na kutafuta hela.Mith 19-11 5.Muda,Na,Marafiki Kama nilivyosema hapo mwanzoni, mada ya leo ni kujaribu kuona jinsi gani mtu anaweza akaokoa muda ili apate muda wa kuwa karibu zaidi na ndugu,jamaa na marafiki katika mambo ya kijamii nk. Lakini utashangaa nikikuambia kwamba marafiki pia wanaweza kuwa chanzo kizuri cha matumizi mabaya ya muda wako?Liangalie hili kwa makini kwani inategemea sana na aina ya marafiki na jinsi mnavyoamua kutumia muda wenu. Kwa mfano kama una rafiki ambaye hazingatii muda,hana miadi ya uhakika huyo anaweza kuwa mzigo katika suala zima la matumizi ya muda. Angalia kwa makini urafiki wenu. Jaribu kumuelekeza mwenzako kuhusu umuhimu wa muda katika ratiba na mipangilio yenu.Naamini ataelewa. Pia jaribu kuangalia,mnapokutana kama marafiki,mnatumiaje muda wenu? Je mnatumia muda huo kupanga mikakati ya maana ya maisha au mnaishia tu kusengenya watu na kupiga umbea? Sihitaji kukuambia kitu zaidi.Unajua cha kufanya. Maombolezo 1:2,Ayubu 16:20,19:21,( Ayu 32:3. 6. Fanya jambo zaidi ya moja kwa wakati mmoja: Kwa kiingereza hili linaitwa “Multi-tasking”. Yapo mambo ambayo unaweza kuyafanya kwa wakati mmoja. Mifano ipo mingi. Kata kucha zako ukiwa unaangalia televisheni, sikiliza taarifa ya habari huku ukiandaa nguo zako za kuvaa kesho kazini. Unaweza pia kujibu barua pepe zako wakati unapata kifungua kinywa.Mifano ipo mingi. Cha msingi ni kuhakikisha kwamba hayo mambo mawili unayojaribu kuyafanya yanawezekana kufanyika kwa wakati mmoja na pia ni salama kufanya hivyo.Kwa mfano sikushauri uongee kwenye simu ya mkononi wakati unaendesha gari.Sikushauri utumie chombo chochote cha umeme wakati ukifanya shughuli zingine.Angalia usije kuwa kama yule jamaa ambaye alikuwa anapiga pasi,simu ikaita.Badala ya kupokea simu,akapokea pasi! Ni hatari. Math 14:21 7. Jipange, pangilia ratiba: Ukipenda unaweza kusema hili la kujipanga na kupangilia ratiba ni mkusanyiko wa yote niliyotaja hapo juu. Muda mwingi sana huwa tunaupoteza kutokana na kutopangilia vizuri mambo yetu,ratiba zetu za kila siku. Upo umuhimu kwa mfano wa kupangilia shughuli zetu kutokana na sehemu za kijiografia.Kwa mfano kama una shughuli ambazo zinahitajika kufanyika mjini(siku hizi huwa Napata tabu kubainisha wapi ni mjini), hakikisha kwamba unapokwenda mjini unazikamilisha zote kwa wakati mmoja. Haingii akili kwanini mtu aende mjini zaidi ya mara tatu kwa siku.Kwanini alipoenda mjini asubuhi asingefanya yote aliyotakiwa kuyafanya? Hali ni hiyo hiyo hata majumbani mwetu. Utakuta mtu amefanya safari zaidi ya mia mbili kutoka chumbani kwenda jikoni. Kwanini? Jibu rahisi ni ukosefu wa mpangilio. Mbinu za kuokoa muda ni nyingi zaidi ya hizi chache ambazo nimeziorodhesha. Unaweza kuongezea katika orodha hii.Jambo muhimu la kukumbuka ni kwamba yawezekana kabisa kupata muda wa ziada wa kufanya mambo uyapendayo maishani. La msingi ni kuwa na mpangilio wa muda.Tumia mbinu hizi na zinginezo ili kufanikiwa katika suala la muda.Usilale zaidi ya masaa manane kwa siku. Muda ni zawadi kutoka kwa muumba.Utumie vizuri. Mhubiri 3:1-8 3.UTULIVU. Wakati unapotafakari kwa lengo la kutafsiri maandiko matakatifu lazima uwe mwenye utulivu.Nikimaanisha kwamba uwe na mahali ambapo ni mbali na makelele ya wanafamilia na watu wengine,mbali na kelele za mitaani,mbali na simu,mbali na Tv.Je hapana mahili pa namna hiyo karibu na nawe?Je hali ya utulivu ikoje saa kumi na moja alfajiri?Hapo inawezekana hapo kuwa mahali pako pa sili ya kuteka utlivu.Fahamu kwamba Mungu huongea katika utulivu na ukumya imeandikwa.1Fal 19:11-13’ MAANDIKO,MATAKATIFU Maandiko Matakatifu Ni Nini? Maandiko Matakatifu ni Neno la Mungu lililotolewa kwa ufunuo wa Mungu kupitia kwa watu watakatifu wa Mungu ambao walinena na kuandika kama walivyoongozwa na Roho Mtakatifu. Maandiko haya yamegawanywa katika sehemu mbili kulingana na wakati/ kipindi cha uandishi wake, yaani agano la kale na agano jipya. Maandiko haya ndiyo yanayoitwa Biblia Takatifu I. Uandishi wa Biblia Maandiko Matakatifu yaliandikwa na waandishi 40 kwa kipindi cha miaka 1500: Agano la Kale (vitabu 39): 1400 – 400 K.K Agano Jipya (vitabu 27): 48 – 65 B.K II. Mambo Muhimu 4 ya Kuzingatia Juu ya Maandiko Matakatifu 1.Maandiko Matakatifu hayakuletwa kwa mapenzi ya mwanadamu. Maandiko yanashuhudia kuwa waandishi wote hawakuandika mawazo au hisia zao bali walipewa Neno toka kwa Mungu nao wakaandika wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Neno la Mungu liliandikwa ili wanadamu wote wapate kujua yale ambayo Mungu anawataka wafanye ili waishi maisha yanayomtukuza yeye. Hii ni sawa na kusema Tunapaswa kufuata maandiko ya Mungu na siyo mawazo na mitazamo yetu sisi wenyewe . 2Petro 1:21 “Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu”. Yeremia1:9 “Ndipo Bwana akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako”. 2 Samweli 23:2 “Roho ya Bwana ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa ulimini mwangu. 2. Maandiko hayawezi kutanguka Yohana 10:35 Maandiko hayawezi kubadilika na hakuna mtu awaye yote au mamlaka yoyote mwenye ruhusa ya kuyatangua. Hakuna Ufunuo 22:18-19 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, …” Methali 30:5-6* “Kila neno la Mungu limehakikishwa, Yeye ni ngao yao wamwaminio, Usipunguze neno katika maneno yake asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo”. Kulingana na Biblia watu wakifundisha jambo lolote tofauti na maelekezo ya Maandiko wanahesabiwa kuwa waongo. 3. Ndiyo yenye Mamlaka ya juu ya mwisho katika mambo yote yahusuyo imani. 2Timotheo 3:16-17 “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” Walengwa wa Maandiko ni watu wote, ni mimi na wewe. Ndani yake Mungu amemkabidhi mwanadamu elimu iliyo ya lazima kwa ajili wokovu. Maandiko ndiyo ufunuo wa mapenzi ya Mungu, ufunuo thabiti wenye mamlaka wa mafundisho ya imani. Kwa hiyo kila fundisho la kidini (imani) lazima lisikinzane na Maandiko na lazima lithibitishwe pia na Maandiko Matakatifu. 4. Mada Kuu katika Maandiko ni Wokovu wa Wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo. Katika Maandiko Mungu ametufunulia mwanzo wa kila kitu, mwanzo wa dhambi, matokeo yake na mpango wa ukombozi. Vitabu Vyote vinaongelea Mada Kuu Moja: WOKOVU. Yesu mwenyewe anasema katika Yohana 5:39 “Mwayachungunza maandiko, kwa sababu … mna uzima wa milele ndani yake na hayo ndiyo yanayonishuhudia”. Kuanzia kitabu cha kwanza (Mwanzo) hadi cha mwisho (Ufunuo) tunapata mwongozo wa jinsi mwanadamu anavyopaswa kuishi na kurudisha mahusiano yake na muumba wake na mpango mzima wa WOKOVU. Luka 24:44 “… akawaambia, … ilikuwa lazima kukamilisha yote yaliyoandikwa juu yangu katika torati ya Musa na katika vitabu vya manabii na Zaburi.“ Yohana 1:45 “Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu ..” Katika Luka 24:27 tunasoma “akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe” III. mafundisho yote ya imani na ni mwongozo thabiti wa tabia adilifu mbele za Mungu. SOMO LIMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA BISHOP RHOBINSON SALEHE BAIYE. MKOLANI NYAMAGANA MWANZA TANZANIA (10/7/2021)

UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...