SAUTI
YA GOMBO INTERNATIONAL MINISTRIES NETWORK
UONGOZI
NA
UTAWALA WA
KANISA.
UTANGULIZI
Asili
yote ya Uongozi na Utawala, unatokana na Mungu mwenyewe, Mwanzo 1:26-27.
Alipanga kila mwanadamu awe mtawala, ila kusudi lake liliharibiwa na dhambi,
Mwanzo 3:1-10.
Dhambi
ya Mwanadamu ilichelewesha Mpango wa Mungu, Kutoka 32:1-6 linganisha na Kut
19:5-6. Hivyo Mpango wa Mungu ulitimizwa kupitia kifo cha Kristo alipokuja hapa
duniani 1Pet 2:5-9.
Uongozi
na Utawala ni Vitu viwili tofauti ndani ya Kanisa, Makanisa mengi hayana
Uongozi bali yana Utawala.
MAANA YA UONGOZI KIONGOZI
1) UONGOZI NI NINI?
Uongozi
ni kutangulia mbele, ni kuonesha njia siyo kuswaga, ni kutenda kile ambacho
unataka watu watende. Hivyo, Uongozi ni kuelekeza wengine kwa vitendo. 1Kor
11:1, Zab 23:2-3.
Uongozi
ni Utumishi siyo Ubwana, bali ni kuwa kielelezo kwa kundi 1Pet
5:3 1Tim 1:16
Uongozi
ni ushawishi, ni uwezo wa mtu mmoja kuwashawishi wengine waweze kufuata Uongozi
wake.
Uongozi
wa Kiroho unaweza kutimizwa na watu wa kiroho pekee.
Neno
Uongozi linatokana na neno Kuongoza, ni ile hali ya mtu kuwatangulia wengine na
kisha wengine hufuata nyuma.
Niccolò Machiavelli ambaye, katika kitabu chabe maarufu The Prince, aliandika kama kiongozi hawezi kuogopwa na kupendwa kwa
wakati mmoja, ni afadhali aogopwe kuliko kupendwa.
Uongozi ni mamlaka au karama ya kuwaonyesha watu njia kwa vitendo.
Kipimo cha uongozi ni jinsi gani kiongozi anaweza
kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.
Kiongozi bora hana muda wa kulalamika bali anatafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi au watu walio chini yake.
Kiongozi wa kweli akiongea, watu husikiliza.
Uongozi
ni dhana, taaluma inayompa mhusika madaraka na uwezo wa kuwawezesha wale wanaongozwa naye
kuunganisha nguvu, stadi na vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo yao. Kuongoza ni kujua lengo la wale wanaoongozwa
na njia ya kufikia lengo lao.
Uongozi ni
dhana, taaluma anayopewa mhusika katika kuwaongoza wale waliohitaji kusimamiwa
au walioamuliwa kusimamiwa katika kufanikisha jambo fulani kwa maslahi ya wote
au ya mtu mmoja mmoja.
AINA ZA
UONGOZI
i) Kuna
njia nyingi za kuainisha uongozi lakini njia ya msingi ni kuangalia jinsi
kiongozi alivyoingia madarakani na utaratibu wake wa kuongoza.[1]
ii) Katika
viongozi wapo
Wafalme Maraisi, Mawaziri, Watemi, Machifu, Wakurugenzi, Viongozi wa dini[2] n.k.
iii)
Viongozi hawa wote tunaweza kuwagawa katika mafungu yafuatayo kutokana na jinsi walivyoingia madarakani
na namna wanavyoongoza kama ifuatavyo:
·
i. Wale
wanaopata uongozi kwa kurithi.
·
ii.
Wanaopata uongozi kwa kuchaguliwa.
·
iii.
Wanaojitwalia mamlaka ya kuongoza kwa nguvu.
·
iv.
Wanaoteuliwa na mamlaka za juu zaidi.
iv)
Kiongozi anayeingia madarakani kwa mojawapo ya njia zilizotajwa hapa juu
anaweza kutumia mtindo wake wa uongozi. Ipo mitindo mbalimbali ya uongozi:
·
i. Uongozi
wa kimila
·
ii.
Uongozi wa kidemokrasia.
·
iii.
Uongozi wa kiimla ni mtindo wa kuongoza ambao kiongozi huongoza
kwa amri bila kushirikisha watu wengine katika kufanya
maamuzi. Mara nyingi uongozi wa aina hii haulengi katika kukidhi maslahi ya walio wengi, bali tu ya yule anayeongoza na wale
wanaomlinda.
·
iv.
Uongozi wa kidemokrasia ni ule wa kushirikisha watu katika kufanya maamuzi
na utekelezaji wake. Kwa kawaida viongozi wa aina hii hulenga
kukidhi mahitaji ya walengwa.
Viongozi
wanaochaguliwa mara nyingi huwa wanapewa muda wa kuongoza, na wale viongozi
wanaojiteua hujipatia wao wenyewe muda wa kuongoza au hata hapo watakapoamua
kuachia madaraka.
SIFA ZA
KIONGOZI BORA
i.
Awe na
ufahamu.
Kiongozi ni lazima awe na ufahamu mkubwa
juu ya taasisi anayoiongoza,
malengo yake, mazingira na matatizo yake.
ii. Awe
mwaminifu. Kila taasisi inalenga kufikia shabaha fulani. Ni wajibu wa kiongozi kuwaongoza wanataasisi ili wafikie
malengo yao. Kwa hiyo kiongozi ni lazima aweze kubuni mikakati na mbinu zitakazoiwezesha
taasisi anayoongoza kufikia malengo yake.
iii. Awe
na maadili mema. Kiongozi ni lazima akubalike katika jamii na
taasisi anayoiongoza. Ili akubalike hana budi kuzingatia maadili ya msingi ya
jamii na taasisi yake. Mtu mwongo, mlevi, mvivu, asiye mwaminifu n.k. hawezi
kuwa kiongozi mzuri.
iv.
Amche Mungu.
v. Awe
anakubalika na watu anaowaongoza.
vi. Awe
anaongoza watu katika misingi bora ya uongozi bila kujali jinsia, rangi, dini wala kabila.
Awathamini watu wa makundi yote.
vii. Awe
anakubali kushauriwa ua kupokea ushauri kutoka kwa wengine.
viii. Awe
na uwezo wa kujifunza kutoka kwa watu wengine waliofanikiwa.
ix. Awe na
mawazo ya mbele ya kuona tatizo na kuonyesha baadhi ya njia za kulitatua,
pamoja na kuona fursa