Thursday, May 28, 2020

KITABU CHA UBORA WA LUGHA YA KANISA No 1

7: LUGHA INA TABIA YA UBORA. No 1

Lugha ina tabia ya ubora.Tabia hii ina maana kwamba kila lugha ni bora kwa wale wanaoitumia.Lugha zote ni bora,hakuna Lugha bora kuliko nyingine kwani kwa wale wanaoitumia inawafaa,ijapokuwa upo uwezekano wa  lugha hujitosheleza sana kwenye rejesta ambazo huzingatia mawasiliano ya kundi fulani na kuwa bora lugha badala ya lugha Bora.Kumbuka kwamba lugha tunayoizungumza katika kitabu hiki sio lugha hizi zinazotumiwa na jamii kulingana na makabila ya watu la hasha.Tunasoma au kujifunza lugha ambayo imo ndani ya lugha kwa maana nyingine tunajifunza lugha itokanayo na lugha yaani matamshi au maneno,makali, maneno laini, maneno yanayo shawishi,yanayotia moyo yanayo katisha tamaa,yanayojenga,yanayofariji,yanayo hamasisha.Maneno yanayo patanisha, maneno yanayo fungamanisha maneno yanayo tamanika   katika jamii.Fahamu ndani ya lugha mna lugha.Lugha ya kanisa la mahali ni bora au tuseme kanisa ndiyo ina lugha bora ,lakini lugha za jamii zetu au lugha za mataifa mbalimbali hazina ubora kwa maana zina mapungufu na  zina uhitaji wa maneno na misamiati.Nahilo husababisha lugha hizo kukopa au kutohoa maneno kwa lugha zingine nyingi .Kanisa lina lugha ambayo haina uhitaji wa kukopa au kutohoa maneno kutoka kwa lugha za kijamii,kwa maana lugha ya kanisa imejitosheleza kabisa.Lugha ni bora na uwezo wa kujenga, Kuimarisha kustawisha kanisa la mahali popote pale.Na lugha isiyo bora huvunja na kubomoa na kudhoofisha kanisa la mahali popote pale,kwa maana lugha hiyo ina hali ya kukatisha na kuogopesha na kudhoofisha hamasa ambayo ilikuwa ndani ya waamini.Kwa hiyo tuta jifunza lugha ya kushawishi watu kulikaribia kanisa au makanisa yetu. Vitu na watu wenye lugha Bora Biblia huwaita heri.Math 5:1-16,11:6,13:16,16:17,24:46

 Ubora Na Maana Yake.

Ubora ni sifa ya kiumbe hai au kitu chochote hasa kulingana nawengine au vingine vya aina ileile.Pengine ubora unatakiwa kulingana na kiwango au viwango vinavyotarajiwa na watumiaji na sheria za nchi.Kwa ajili hiyo Kuna taasisi maalumu zinazothibitishwa kuwa unafikia kiwango hicho.Bila uthibitisho huo bidhaa haiwezi kuuzwa.Mfano,kwenye biashara,Uhandisi,ubora unatafiriwa kisayansi kama uwezo wa kutokuwa na mapungufu ya kitu au vitu.Ubora ni dhahiri,una sifa fulani ya kujitegemea na unaweza kueleweka tofauti na watu.Watumiaji wanaweza kuangalia pia ubora wa vipimo vya bidhaa,na bora wa kufanana wa bidhaa.Wafanyakazi wa msaada wanaweza kupima ubora kwa hatua ambayo bidhaa huweza kuaminika na kudumishwa.Math 6:26,10:31,12:7,Luk 15:22,Ebr 8:6,9:23,11:4,16,35.

Kanuni Za Ushawishi Na Kushawishi.

Kanisa inapaswa kutumia lugha ishawishayo watumishi, viongozi, waamini,na waamini wapya.Lakini inahitaji makundi hayo yote katika Kanisa yafahamu na kuyaishi maisha ya ushawishi.Na katika neno hilo kuna kushawishi na hushawishika.Shawishi ni kumpa mtu maelezo ili kutaka kufanya akubali kufuata fikira au maelezo yako.Kufanya mtu avutike kutenda Jambo fulani.:Kushawishika ni kuvutiwa na kukubaliana na kile kinachoonekana au kusikika.

 Ushawishi Na Mawasiliano.

Mawasiliano ni mojawapo ya misingi muhimu sana kwenye maisha ayetu ya kila siku kama wanadamu.Napia ni moja ya mahitaji muhimu kama tunataka kufikia malengo au mafanikio makubwa kwenye Jambo lolote ambalo tunalifanya.Kumbuka ya kwamba chochote unachotaka kinatoka kwa watu wengine,hivyo jinsi unavyoweza kuwashawishi na kukubaliana na wewe ndivyo itakuwezesha kupata unachotaka.Na fahamu kwamba ushawishi unaanzia kwenye mbinu bora za mawasiliano na lugha ambayo mtu anaitumia.Watu wengi wamekuwa wakiwasukuma wengine ili wapate kile wanachokitaka.Na wamekuwa wakifanya hivi kwa kubishana,kutishana,kudanganyana na hata kulaghai ili wapate wanachotaka.Kwa njia hizi  inakuwa vigumu zaidi kwa watu kuwa tayari kutoa kile ambacho wengine wanakitaka.Ni kutokana na changamoto hii Daktari na mwanasaikolojia Mark Goulson,alipokuja na kitabu ambacho kina mbinu za ushawishi ambazo zinamwelekeza mtu kupata kile anachokitaka kutoka kwa mtu yeyote.Daktari Mark anatumia taaluma yake na uzoefu wake kwenye kazi ya ushauri katika kutushirikisha mambo  muhimu ya kuzingatia kwenye mawasiliano.

DAKTARI MARK GOULSTON ANASEMAHIVI:

 1:Kila Mtu Ana Mahitaji Yake.

Kila mtu ana mahitaji yake,matamanio yake na pia ajenda zake.Na tena kila mtu ana siri yake ambayo anaificha,na hataki watu wengine waijue.Na pia kila mtu anapilika zake na msongo wa mawazo,na hana muda wa kumtosha kufanya kila anachotaka kufanya.Ili kuweza kwenda na hayo yote yanayoendelea kwenye maisha yake,mtu anajitengenezea ukuta ambao bila ya kujua hayo huwezi kumshawishi kwa jambo lolote.Fahamu kwamba ukitakamtu afanye au akupe chochote unachotaka,anza kwanza kuvunja ukuta huu ambao kila mtu amejijengea.Kanisa ni lazima kuvunja ukuta ambao umejengeka na kila mshirika kama mahitaji binafsi,matamanio binafsi,siri zake binafsi,imani za kigeni,mategemeo,matumaini,mila,testuri,na lugha utamaduni,ili Kuimarisha na kustawisha kanisa. Za 11:10,14,2:9,3:7,7:2,28:5,29:5,46:9,48:7.Mith 15:4, Mik 2:13,3:3,Ombolezo 2:9,3:4 Math 5:19,6:19,12:1,20,26:61,27:40,

 2:Ushawishi Na Mzuguko Wake.

Ushawishi unaenda kwa mzunguko ambao ana hatua tano muhimu.Yaani kabla mtu hajashawishika kufanya chochote unachomwambia,anapitia hatua hizi tano ambazo unatakiwa kuzijua na kujua jinsi ya kumpitisha mtu kwenye kila hatua.

 a:Hatua Ya Kwanza.

Hatua ya kwanza ni kumtoa mtu kwenye kukataa mpaka kuwa tayari kusikiliza.Wakati wowote mtu yupo kwenye hali ya kukataa, unahitaji kuwa na mbinu ya kufanya akusikilize.Tumia Lugha ambayo mtumishi kiongozi mshirika na asiyeamini ashawishike kukusikiliza sio lugha ya kumweka mbali nawewe na kanisa.Kufanya hivyo kutaimarisha na kustawisha kanisa

UBORA WA LUGHA YA KANISA No 1.INAYOFUATA NI UBORA WA LUGHA No 2.

Bishop: Rhobinson S.baiye.

Blog; rhobinsons.blogspot.com

E-mail: rhobinsonsaleh1@gmail.com

WhatsApp: 0764127531

Mwanza Tanzania





Monday, May 25, 2020

MAMBO 10 YANAYOWEZA KUIMARISHA NA KUSTAWISHA KANISA LAKO.

Yafahamu Mambo Kumi Muhimu
1.Kanisa kudumu katika upendo wa ki-Mungu.
2.Kanisa kudumu katika umoja wa ki-Mungu.
3.Kanisa kudumu katika mshikamano wa ki-Mungu
4.Kanisa kudumu katika maombi ya ki-Mungu.
5.Kanisa kudumu katika imani thabiti.
6.Kanisa kuwa na mfumo unaofaa.
7.Kanisa kumiliki na kutawala uchumi mkubwa.
8.Kanisa kuwa na mtazamo chanya kuhusu nyakati.
9.Kanisa kuwa na maono yenye mwelekeo bora.
10.Kanisa na uwajibikaji.
11:Kanisa na Elimu
12:Manisa na Nidhamu
Nb/ haya yote tutayatafakari na kufafanua moja baada ya nyigine.Lakini unanafasi ya kupendekeza mada ambayo unayohitaji zaidi kwa muda wako.Nami nitaeleza kwa faida ya wote.Blog hii inapatikana kwa jina

Bishop:Rhobinson Saleh Baiye.
rhobinsons.blogspot.com.
Whatsapp: 0764127531
E-mail:rhobinsonsaleh1@gmail.com
Sauti Ya Gombo International Ministries
Mwanza Tanzania.


UONGOZI BORA WA KIROHO

Sauti Ya Gombo International Ministries Network KIONGOZI BORA WA KIROHO BISHOP: RHOBINSON S.BAIYE YALIYOMO: 1.Maana...